Riwaya: Upepo wa usiku-1

Riwaya: Upepo wa usiku-1

UPEPO WA USIKU-7
BONIFACE BIRAGE

“Nimetoka nje ya ndoa si mara moja.”kwa kumfichia mumewe kwamba hawana ushirikiano mzuri wa kifaragha hakumsema mbele za watu.Ni jambo lao labda watu wahisi tu nasio kuwa na ushahidi kutoka kwake.Ingebaki siri yake daima!Mengine yabaki siri za sisimizi.
“Nimekuwa nikishiriki kimapenzi ya siri na Masua!”Pigo kali kama ngumi ya za wanamsumbwi!Kwa kweli hungelikabili kama una moyo wa nyama.Lilikuwa pigo la uhakika.Ni kama alimdunga sindano hasa akiwa sio mtu aliyependa kutobolewa na kifaa hicho.Hali ilianza kubadilika.Hiz karata anazocheza alitakiwa kuzipanga kwa umakini kuliko jambo lolote lile.
Bario alitizama chini kwa hasira halafu akauleta uso kwa Masua!Masua aliangalia pembeni kwa aibu!Chakula kikawa kizito kuchota nakutafuna pia!Ilikuwa mtu kati kawekwa!Yaani umenibamba viutamu!Dj Afro angekwambia bumper to bumper…Heri ushikwe kwa namna nyingine lakini si kwa uwazi kiasi hiki huku ni kumvua mtu nguo mbele ya kadamnasi
“Mke wangu kwani unasema nini?”ilibidi amuulize maana bado hakuwa ameshika maelezo ya bibi huyu.
“Ni kweli nimekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Masua kwa muda mrefu sasa.”alisema nakumwangalia mumewe kumpima kama bado ana shari zozote.Halafu mtu mwenyewe yupo mezani mwake.Anakula hapohapo?Jamaa alichanganyikiwa kwa sekunde kadhaa.
“Kwani mmefanya nini na nini?”hata hakupanga kuuliza swali kama hilo japo ilikuja tu akajikuta kauliza bila kutegemea.
“Yote ambayo umekuwa huyafanyi!”ilikuwa aibu ya mwaka.Bario alikwepesha macho nakutizama chini.Dah!Wanawake wanajua kuzicheza kete zao.Hili lilikuwa jipya nakumpiga kunako maeneo husika ya shutuma.Yaani alimtandika kwa neno zito hata wote waliokuwa mezani walijikuta wakishikwa na mshtuko uliowakaba kooni.
“Hata juzi nilipotoweka usiku nilikuwa kwake.”Laredo aliendelea kupasua mwamba bila ajizi yeyote ile.
Alitamani kujua nyendo za mkewe lakini hakuwa na wazo kama zingefikia hatua hii.Ilikuwa kali ya mwaka!Pengine hakutwakiwa kujua lolote si chochote.Hii ilikuwa kali ya mwaka!
“Unaweza kunilaumu lakini bado.Safari ni ndefu.Tumekuwa tukifanya mapenzi mara nyingi na yeye.”kwa jinsi alivyoropoka uchafu wake hata usingeamini!Halikuwa jambo la kuzungumzwa mbele ya wanaume hawa.Ni aibu ya mwaka!Pengine hata angemwita mume wake chemba walizungumze jambo hilo labda uwezekano wa suluhu ungefanyika kimyakimya.Aliumwaga mpunga katikati ya kuku wengi tena wakienyeji!Kusema habari kama hii ilihitaji ujasiri wa msemaji na hadhira anayoihutubia.Kwa kawaida hakuna ambaye angevumilia jambo hili nasiajabu zingelika ngumi hapahapo!Lakini Laredo alishawajua waume zake na namna ya kuwadhibiti.Alijua leo kapiga hatua kubwa sana kusema kitu hicho nasio kwamba kingekubaliwa.Alijaribu kete hiyo!
Bario hakuvumilia aliamka nakwenda chumbani.Laredo kidogo alie,akajikaza.Alijua anavunja ndoa japo kichwani alikuwa namahesabu kwamba ni muhimu akilipua jipu palepale kuliko kuja kugundulika baadaye.Akainuka nakumfuata mume wake hadi chumbani.Alimkuta amekaa kitandani kainamisha kichwa chini.Mwingi wa mawazo.Bora aseme jambo kuliko ukimya wa namna ile wa ghafla.Mshtuko upo ila sio kwa kiwango kile.
Alienda nakuketi ubavuni mwake.Ukimya ukapita kati yao!Ukimya uliobeba mengi na siri za utata.
“Nini kilifanyika hapa nilipokuwa hospitali.”alianza Bario akipandisha ujasiri wa mbwa wa kiume asiye na meno!
“Nililala na Masua.”kwanini afiche bora aseme ukweli.Kiwango alichofikia ilibidi aongee tu.Ukimywa wa kula gizani ulishaisha muda.Usaliti wake ulikuwa umepevuka kwa sasa.
“Wapi?”
“Kwenye hiki kitanda.”akaonesha kwa kidole.
Bario akameza mate ambapo sasa mdomo ulianza kuwa mchungu!Ukawa umekauka!Nguvu ni kama zilimwishia!Aliona kama kizunguzungu kilitaka kuja kikapotea!Alihisi mkojo umembana lakini hakuwa na haja ya kwenda chooni!Ndoa zina mambo wakati mwingine siyo zote bali baadhi tu!
“Kwanini ulifanya hivi?”
Laredo alitegemea kuulizwa vile.Akajikohoza kukusanya ujasiri.Hakuwa na sababu kwamba ni jambo gani alitakiwa kulisema ilikumuweka mumewe kwa wazo alilotaka!Wazo la kuwa na mabwana watatu!
“Hata nikwambie hutanielewa,kifupi nilikusaliti na stahili kuachwa.’’ Ni kama alijipa talaka.Alijuafika Bario asingempa talaka bali angemwacha atimbwe na ulimwengu.Ilikuwa kama dhihaka usoni mwa Bario.Tena dharau zenye chembe ya wizi wa makinikia.
“Not well at all.”alisema kwa huzuni.
“Na sio Masua tu.Nina uhusiano na Hamza pia.Nawapenda wote nipo tayari kuishi na nyie wote.Kilichobaki ni ndoa nikiwaongeza Masua na Hamza.Tutaishi mkijua kwamba mimi ni mke wenu.Mambo ya wivu hayatakuwepo.Tutakuwa na raha tukifanya mambo kwa pamoja.Ni wazo zuri mume wangu.Kuliko niendelee kuwasaliti bora wote mnioe tuishi wote hapa.Watu wa nje hawatajua kwamba nyie ni wanaume wangu wote.Watajua kwamba wewe ndo mume hao wengine ni ndugu tu.”
Bario alitumbua macho,’’Hivi unajua unachosema?”
“Nakijua.”alisisitiza binti huyu kwa ustaadi wa hali ya juu.Kama ni kilevi basi alikuwa amevuta au kunywa kile chenyewe.Lakini hakuwa amevuta wala kulewa.Ilikuwa akili tu kama mtu yeyote.Kilicho kichwani mwake nikuingiza utamaduni alioubeba kutoka maeneo ya huko ng’ambo.Vile aliona hajapigwa kofi wala kufokewa alijua fika ana hoja ya kujibu.Ni vile aliukuta moyo wa Bario ni nyama.
“Ni sehemu chache sana wanazo fanya mambo haya.”alisema Bario akimwambia mkewe.Kitu hiki kilisharipotiwa nchi za ng’ambo.Kwa mujibu wa Bario alishasoma utamaduni huo ambao ni wa watu wan je.Hakuwa wakitanzania.Huku usingekubaliwa kabisa.Ni kwamba mwanamke huyu aolewe na hawa watu watatu waishi pamoja wakishiriki mambo yote.

“Hii siyo open relationship yaani nikuruhusu uende na yeyote unayejisikia kwenda naye ilhali tupo pamoja.Hii ni serious ujue?”alisema Bario akikuna kichwa.Papi za midomo yake ilikauka kaukau.
“Sisi tutakuwa sehemu moja ya hiyo.Polyandry sio mbaya bali ni uhakika kwa mwanamke kuwa na waume watatu.Sina haja nakuwa na open relationship?Kuwa nayo open realationship ni hainipi uhakika mimi.Kwanza nitakuwa muhuni zaidi.Bora tufanye polyandry mwanamke mmoja anakuwa na mabwana wa halali zaidi ya mmoja.Mimi nimewachagua nyie watatu.Bario,Masua na Hamza.”alijitetea mwanamke Yule.
“Laredo umechanganyikiwa kwa kweli?How can you manage three husbands?”
“I can kwa sababu siku zote nimekuwa nikiweza.Haina haja yakuleta bifu.Tumalize kiistaarabu jambo hili.Mbona nyie wanaume mnaoa wanawake wawili hadi watano kwani mwanamke hana ujasiri huo.”

Kichwa kikacheza kwa mshangao kwa upande wa Bario.Mapya.Huu utamaduni wa ng’ambo una mashaka yake.

“Tatizo waafrika tunambana sana mwanamke hatumpi fursa ya kuridhika kwa kile anachotaka.Binadamu aliumbwa kufurahia maisha.Nikitoka na mwanamke mwanaume mwingine mnasema mimi mzinzi sasa nadai ishu ndogo tu niolewe na nyie watatu.Msiwe na wivu wowote!”
Bario aliinuka nakuja hadi ukumbini.Hamza alitaka kukimbia,”Usikimbie Hamza.We baki.Najua kinachoendelea hadi sasa.Nahitaji ushauri wenu.”
Hamza alirudi nakuketi.Alivuta pumzi ndefu nakuwaza aseme nini kwakuwa alishajua Laredo amemwleza mumewe jambo hilo,”Laredo mimi nakupenda kwa dhati nipo tayari kushare na wenzangu.”
“Hata mimi nashauri jambo hilo.”akaitikia Masua kwa haraka.Hawa walishapangwa tangu kitambo wala hakuna aliye na pingamizi.Ashukuru Mungu hawa walimwelewa lakini wangekuwa wengine ngumi zingelika kwa hatari ya kifo!
“Bario unaona wenzako wanaakili.Utakuwa muunganiko mzuri usio na vikwazo.Hamtakuwa na hofu ya kushare mke kwamba yupo na nani?Tutaishi nyumba moja kwa upendo wa ajabu na tutakuwa na familia moja iliyo na nguvu.”
“Unadhani jamii itatuonaje?”Bario akajikuta akiuliza.Kuambiwa hao wanaakili alihisi kutukanwa.
“Jamii haitajua hii ni siri yetu sisi tu.”
Bario alitulia kwanza akafikiri huku akijiambia haya ni majaribu au ndoto ya kutisha!Kuliko kupinga sana bora kieleweke mara ileile,”Sawa.”aliunga mkono huku akijiambia anataka kuona safari hiyo itaishia wapi.Japo alimpenda mkewe lakini kuna wakati alichoka nakusubiri aone mwishio wake ni nini?Pia alijiuliza ni kweli anampenda mkewe?Au mwanamke huyu ameshachuja.Jambo hilo lilikuwa gumu na hata kubali yake hakuijua imetoka wapi?Wengine wangesema kapuliziwa!
“Kwaanzia leo jueni nyie ni waume zangu na mimi ni mke wenu.”alijikaza nakuwatamkia.Wanaum wote wakatizamana kisha kwa shingo upande wakapeana mikono.Hata hakujua ilikuwaje ikawa rahisi kwa wanaume hao kukubali jambo hilo.Msafara wa ndoa baina ya mwanamke mmoja na wanume watatu ukaanza.

“Tukitaka kuwa na watoto?’’Bario akauliza.

“Hilo nachagua mimi nizae na nani?Lakini kaeni mkijua wote mtahitajika kuwa responsible kwa watoto wetu.Hakuna huyu ni wafulani.Wote ni baba kwa watoto wote sawa!’’maelezo ya Laredo yaliwashtua sana.Yalikuwa mapya kwa muafrika!
“Leo na lala na mume wangu mkubwa nyie hamtaruhusiwa kunigusa hadi tutakapofunga ndoa za kisheria.Hakuna wakutoa ushahidi kwamba nimeolewa nataka wote mnimiliki kisiri.Au sio wapenzi wangu?”
Bario alikuwa namahesabu yake.Alitaka kuona mbio za Laredo zinishia wapi?

USIKOSE TOLEO LIJALO STORY NDO KWANZA INAANZA!
Hatakama ni story.. Ila mimi siwezi kukubali

Tears of the sun
 
UPEPO WA USIKU-9
BONIFACE BIRAGE
Alizitamani nyota zile nakujiambia zipo mbali na upeo wa macho yake.Alijiambia penzi lake kwa Laredo ni refu umbali wa nyota zile na ardhi ya dunia.IlikuwA burudani tosha kwake kuzitazama nakufurahia uumbaji wa Mungu ambao ni pekee kwake.
Akiwa amezama kwenye mawazo alishtuka kufunikwa na mikono ya moto kwenye mboni za mach yake.Akahisi harufu ya Laredo nyuma yake.Busu mwanana likapita kwenye shavu lake.
“Hujalala mpenzi?”ilikuwa sauti ya Laredo.
Hamza hakujibu kitu.Alibaki kimya ni kama amechukia kitu Fulani.Laredo ni kama alitambua hilo.Akamkumbatia kwa nguvu kurudisha mudi ya furaha.Binadamu hutumia hisia kumuongoza mwenzake.Hamza alikuwa na hasiira Fulani kwenye kichwa chake.Hasira zilizoambatana na wivu.
“Unanini mpenzi wangu?”
“Hamna kitu.”
“Jamani Hamza wangu,mpenzi niiambie baba?”kama ilivyo desturi yake Laredo bingwa wa kubembeleza wanaume.
“Kila siku ni mimi wa kuona wenzako wakifurahi lakini mimi tu?”alilalamika.Hilo lilitambulika kwa Laredo.Na alijua ipo siku lingetokea na laijianda kukabiliana na tatizo kama hilo.
“Baby usikasirike mpenzi wangu.Kwani ulizuiwa kufurahi na mimi mpenzi wako.Mimi nipo kwaajili yako.Nipo tayari kukupa penzi tamu kushinda wote.Usisononeke.”
“Lakini nahitaji kukuita mke wangu?”
Laredo alimshika mkono nakumvuta hadi kando kwenye kibaraza akamfungua zipu nakukamata maiki akaanza kuimba nyimbo za tamtam!Kuchukuchu ikafuatia kwa mistari mizito yenye kibwagizo cha maziwa mazito.Uchu ni kama kilevi cha hisia za binadamu.Kwa dakika kama kumi Hamza alikuwa dunia nyingine hadi alipoharibu kinywani mwa Laredo ambaye alikuwa soloist wa nyimbo hiyo.Jasho likiwa linamtoka alikuwa karidhika kwa kiasi kikubwa.
“Kuna lazaidi mpenzi wangu?”alisema Laredo akijifuta unyevu uliotapakaa kwenye kinywa chake.
‘Nahitaji ndoa.”
“Ulitaka iweje?”
“Tutafunga ya kidini kwa Shekhe wangu.”
“Fanya huo mpango kesho kutwa ndoa ifanyike haraka ili ule vyako na roho yako iridhike.”
Alimuunga mkono Laredo.
“Sasa tunaenda chumbani kwangu?”Laredo aliongeza.
“Hapana Hamza anahitaji uwepo wako zaid.”
“Achana naye Yule mchana wote nilimfuruga,kachoka kama nini.Minaona twende tukalale wote.Unajua Hamza hujawahi kuniingilia kimwili?”
Hamza alivuta puumzi ndefu nakuzishusha.Akacheka kidigo akitafuta namna ya kumtuliza Laredo,”Ni kweli lakini na subiri siku ya ndoa yetu kesho kutwa si mbali.”
“Nimesha onja ya Bario na Masua bado wewe.”
“Lakini si hapa umeonja tayari?”
‘Raha ya kiuno si ya mdomoni.”
Wakajikuta wakicheka wote.Walishikana mikono,Hamza alimbeba Laredo nakwenda naye ndani.Laredo alidhani usiku huo ungekuwa wake na Hamza.Mikiki ya wanaume hawa wawili ilimchanganya na kuzidisha hawaa za mwili wake.Alitaka kufurahia na Hamza.Lakini tofauti na wazo lake Hamza hakumpeleka chumbani kwake bali alimpeleka kwa Masua nakumuweka kitandani.Tayari Masua alishapitiwa na usingizi mzito.Laredo alitabasamu tu lakini hakuridhika na hatua hiyo.Aliapa kama akipata fursa basi angemchakaza Hamza ili siku nyingine asithubutu kumkwepa.
***
Kiujumla watu hawa waliishi maisha yao kivyao.Hakuna aliyejua siri zao.Wote walijipanga kivyao.Watu wengi walijua Laredo ni mke wa Bario,hawakujua kama Hamza na yeye yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Laredo,vilevile Masua alikuwa mume wa Laredo.Watu walijua kama ndugu wanaishi nyumaba moja.Maisha yalikuwa mepesi kwa Laredo hasa akiwa hudumia wanaume wote watatu kwa mpigo.Jambo ni kwamba hawakupenda kuzungumzia maisha yao ya kingono kwa pamoja.Mambo mengine yakimaisha walipanga pamoja huku Laredo akiwa ndo msemaji mkuu wa familia.Kila mwanaume alitoa fedha za matumizi kwa Laredo ambaye alipanga namna fedha hizo zingetumika.Alipanga pia na maendeleo mengine yakifamilia kwakununua kiwanja nakujenga nyuma kupitia fedha za waume zake.Aliweka jina lake katika umiliki wa nyumba hiyo.Vitu vingine kama gari aliandika jina lake.Hiyvo akawa yeye ndo kiongozi na mpangaji wa mambo ya familia.
Usiku wa ndoa yake na Hamza ulikuwa muhimu sana kwa Hamza.Ilifanyika ndoa ya kidini,ambapo hakukuwa na sherehe bali ndoa ilifungishwa ofini kwa shekhe na wao wakapewa hati yao nakutia sahihi.Kama ilivyo kwa wengine hakusema kama ameolewa na hata aliyewafungisha ndoa hakujua lolote.
Ilikuwa raha kwake na kwa kwa familia nzima.Usiku huo ilikuwa mara ya kwanza kukutana kimwili na Hamza.Ambaye alifundisha mengi na Laredo kuhusiana na mapenzi jinsi ya kufanya.Na kwa mara ya kwanza akaingia kiotani ,walipoingia Bario na Masua.Mapenzi yakazidi na wao wakajisahau.
Kiujumla walikuwa na amani.Kwa Laredo ilikuwa ukamilifu wakuridhishwa kimapenzi na wanaume wote.Kuna wakati alifanya na Bario kisha akiamua,hutoka na kwenda kwa Hamza na kumalizia kwa Masua ndani ya usiku mmoja.Siku nyingine hulala na mwanaume mmoja tu.Au kuna wakati akichoka sana basi hubaki chumbani kwake nakupumzika.Huo ndo ulikuwa utaratibu wao.Wakati mwingine alichora kabisa ratiba kwamba leo kwa huyu kesho kwa mwingine.Vilevile alivunja ratiba wakati mwingine.Hakutoa siri za mwanaume huyu kwa mwingine bali alibaki nazo peke yake.
Kiuchunguzi aligundua mazuri na madgaifu ya wanaume wale,Bario alipenda ubize sana kiasi haki ya ndoa ilikuwa mara mojamoja.Kwa upande wa Masua alikuwa mvivu kitandani,Hamza yeye alikuwa mkali kitandani na mkali wa romance lakini mchungu wa utoaji wa matumizi.Halafu anawivu wa kijinga.Alijua tabia zao nakujua namna ya kuwatuliza mara kwa mara.
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 87
UPEPO WA USIKU-10
BONIFACE BIRAGE
Siku zote chokochoko mchokoe pweza binadamu atakuweza.Hustahimilivu wa mtu hupingwa na hujuma za majaribu.Jinsi maendeleo yalivyokuwa kwa Laredo alitaka kuwa mtawala kwa wanaume wale.Hamza hakuridhika kabisa na hali hiyo yakushare mke na wenzake.Allihisi kama wenzako wanachukua mali zisizowahusu.Kila walipokuwa faragha na Laredo alipewa sifa nyingi na mke huyokwamba aliweza mambo nakumfurahisha kwa kiasi kikubwa.Alijipa sifa na kuwa na kakiburi.Aliapa kwamba angewashikisha wenzake adabu kwa kuanza kuwapangua mmoja baaada ya mwingine.
Alinunua sumu maalum ilianze na kisanga chake.Sumu hiyo alipanga kuitumia kwa kuitia kwenye chakula siku ambayo aliipanga mwenywe.Aliongoja kwa hamu na ghamu siku hiyo ifike.Japo alitaka kumshirikisha na Laredo lakini wazo hilo lilikuwa la kuogopa maana alihofia kusalitiwa na binti huyo.
Maisha yakiwa sawa kati ya familia,nyongo ilitumbukia kwa mmoja wao!Hamza jioni hiyo akiwa amewahi kurudi nyumbani alimkuta Laredo anapika jikoni alimsalimia..
“Za kushinda mke wangu?”
“Oh hubaa huyoo.Karibu mwandani wangu.”
“Nimekaribia bibie.”
“Asante na wewe.”
“Haya nipo ndani.”alienda ndani akiwa mwingi wa mawazo maana alitaka usiku huo uwe wa pekee.Lakini hakutaka atende mwenyewe dhambi hiyo alichofanya alioga.
Muda kidogo Laredo aliandaa meza tayari kwa familia kula.Kila siku wao huwa ni mipango ya kukaa.
Alipofika mezani alikuta sahani zote zimesha pakuliwa tayari kwa ungalifu akajua mahali anapokaa Masua.Akamtengea sumu kwa kuinyunyiza kwenye chakula.Hiyo ingekuwa pigo tosha.AkasubiriWatu wote waliketi mezani akiwa tayari kasha tegesha sumu kwenye chakula.
“Nyie wanaume leo mmeniletea zawadi zangu?”alianza Laredo utani wake kama ilivyo desturi yake.Wanaume wote wakaangaliana kwamba walitakiwa kukumbushana.Lakini mtazamo wao ilikuwa nani hajaleta waanze kuchekana.Kumbe kila mmoja alileta wakaenda kuleta.Wakati wanaenda kuleta Laredo aliangalia jinsi alivyopakua akagundua hakuweka usawa hivyo akachukua sahani zote nakuzichanganya kwenye bakuli kubwa alilowekea mwanzo hivyo kukichanganya chakula chote.Kiisha akapakua kwa kuwakea wanaume wote.Siku hiyo asingekula kutookana na kwamba alikuwa hasikii njaa.
Wanaume zake wakarudi na zawadi zao ambapo kila mmoja alikuja na pipi aina ya lolpop.Akapewa pipi tatu na yeye kwenda kuketi kwenye kochi akianza kuzinyonya huku akiwatizama kwa ushaufu akiendelea na unyonyaji wa pipi.
Kwakuwa vyakula vilichanganywa hakuna aloyejua achilia mbali Hamza mwenyewe.Baada ya kula wanaume wote walienda kulala ambapo siku hiyo Laredo hakulala na yeyote alibaki mwenyewe kwenye chumba chake.Hadi kuna kucha hakuna jipya lililojiri zaidi ya Laredo kuamka nakuanza shughuli zake,aliamua aoge kwanza ndipo atoke maana alitakiwa kuwahi sehemu.Alienda maliwatoni kisha akaoga.Wakati huo hakuwa amefika sebuleni.Aliporudi akiwa na khanga tu aliamua kupitia sebuleni nakukuta kilichomshtua!Wanaume wote walikuwa wamelala wakitokea korido za vyumba vyao.Hawakujijua.Laredo alijua wanamtania.Alisogea hadi walipo nakuwageuza.AKashtuka!Walijaa mapovu mdomoni!Mwili wake ukasisimka!
AKawsogelea nakuanza kkuhisi mapigo yao ya moyo aakakuta sifuri!Hii ilitokana na hofu aliyokuwa nayo!Akasogea tena hadi jikoni nakukuta panya watatu wamekufa kando ya lile bakuli alilowekea chakula.Kwa kweli hakuwa ameweka sumu ya panya useme panya hawa walikula sumu?
Akili ilizunguka na kumfanya achukue lile bakuli akatooka nalo.Alimwitta mbwa wake nakumpa chakula kilichobaki.Mbwa alikifakamia.Wakati huo Laredo alikuwa na presha kilo mia.Hazikumalizika dakika ishirini mbwa alianza kutapatapa nakuanguka chini!
“Nimepika mimi hiki chakula nakweli sikukionja hii si kesi.’alirudi ndani akiwa hajielewi aanzie wapi alitaka kukimbia akashindwa.Aliziangalia maiti za waume zake nakuishiwa nguvu.Akaangua kilio maana ndo kitu pekee angefanya.Kwa muda akili ilikuwa kama imezima.Hivi sasa nitafanyaje?Pale anamwona Bario,Masua na Hamza wamelala chini bila fahamu zozote.Akatoka nje nakuangalia,uzuri kulikuwa hakuna mtu.Ni nyumbani kwake.
Aliwaza kuwapeleka hospitali lakini akaona kama angejiiingiza kwenye matatizo maana yeye ndo mpishi na yeye ndo aliwapakulia!Wanaishi wote na hivi walikuwa waume zake itamlazimu atoboe siri hiyo.Bila shaka siri hiyo ikitoka watasema alitaka kuwauwa wote maana haikuwa kawaida kwa mwanamke mmoja kuolewa na wanaume watatu.Mawazo yalimweka kwenye wakati mgumu sana.Akainuka akifuta machozi nakwenda chumbani kwake akabadili mavazi.Hakupata muda wakuchanganua mawazo yake akachukua kadi ya benki pamoja na vitambulisho vyake.Kama mwizi alitoka na funguo za gari nakuamua kutoweka kwenye uso wa wanaume wale.Alibeba na bastola ya Bario kwaaajili ya ulinzi wake.Ile anataka kutoka alihisi vishindo vya miguu ya mtu!Wasiwasi ukamjia?Inamaana wamevamiwa?Polisi wamekuja?Au ni mtu kaja kumfumania na maiti za waume zake?Akaweka bastola tayari kwaajili ya lolote.Alisogea kwa kunyata hadi sebuleni.
Alipofika tu akasikia kishindo tena kikikimbilia nyuma ya sofa!Akajua kuna mtu!Bila hata kuwaza aakaelekeza bastola upande huo nakufyetua paa!Paaa!Kimya kikafuata na yeye kusogea!Hakuamini alipomkuta mtoto wake akiwa ameanguka chini hana fahamu kichwa kikiwa kimepasuliwa kwa risasi!Ndo kwanza akakumbuka kwamba walikuwa wamefunga shule na siku hiyo ndo akarejea!
Laredo hakupenda ilitokea bahati mbaya alikusudia dhana nyingine na sio hiyo?Alijilaumu sana kwa jambo hilo!Mikono ikamtetemeka na yeye kuachia ile bastola chini!Akasogelea maiti ya mwanaye.
“Mwananguuu?AAAAA!”aliangua kilio kikubwa.
“Mwangu mama yupo hapa?Mama yupooo?Mwanangu nisameheee?”alilia sana bila hata kujua afanye nini?Mambo yalichafuka kwa siku hiyo nakuanza sekeseke zima la mauaji!Bila shaka roho ya mauti iliingia kwenye boma hilo.Alijipata aakikaa chini nakuugua maumivu ya moyo!Hiki ni kitu gani jamani kina tokea kwake?
Hakuelewa hata kidogo!Ni kama mkosi uliingia kwenye maisha.Akiangalia sakafu anahesabu miili iliyolala chini dahh!Alichanganyikiwa kwa kweli.Mambo yalizidi kuwa magumu sekunde hata sekunde!
Hatari hii ilithibitisha kwamba kuna safari mpya inaanza kwenye maisha yake.Safari kwamba yeye anakuwa mwathiriwa wa matukio hayo ya kuogofya akiwa kama mhusika mkuu!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 76
UPEPO WA USIKU-11
BONIFACE BIRAGE

Uzito wa matukio ulimpeleka kwenye kipande cha mstari mgumu kuliko yote nakujiona kama ana balaa flani.Balaa lililokuja wakati alianza kufurahia ndoa yake kuu!Nitafanya nini?Alijiuliza bila kupata jibu.Akiwa mwingi wa machozi.Aliamka kwa kujikakamua nakuanza kuokota maiti ya mwanaye aliiweka kwenye sofa.Moyo ukawa mzito nakujikamua ujasiri.Aliwaza bila kupata njia.Dakika zikapita nakukatika huku yeye mwenyewe akiwa haelewi wapi pakwenda.Japo mwanzoni alikuwa na ujasiri wa yeye kutoka pale.
Bila shaka siri ile isingekaa milele kwa kujificha.Ingejitokeza siku moja kama sio siku ile basi siku nyingine ambayo ingekuwa nzito zaidi ya zote!
“Nitafanya nini jamani?Mbona mambo yamegeuka ghafla kiasi hiki?”
Kwakweli asingepata tafsiri ya kwanini watu hawa muhimu wameondoka kwenye maisha yake.Jambo zito ni kifo cha waume wake.Wamekufa kifo ambacho hakujua tafsiri yake ni nini na kwanini kimetokea mbele za macho yake.Ni nani aliyetia sumu kwenye chakula kile?Hakujua.Aliyepika ni yeye na aliyepakua ni yeye.Tofauti ni kwamba yeye hakula mezani pamoja na waume zao hasa kipindi hiki alipokuwa na mchakato wa kupunguza unene wa mwili.Hiyo ilitosha kumwambia kwamba hana analojua kuhusu sumu iliyotiwa kwenye chakula.
Alitaka kuondoa maiti ya mumewe lakini akagoma hakuona umuhimu wa kuondoa mwili wa mtu huyo wala wa yeyote.Alibeba bastola yake nakutoka nayo nje kaenda kwenye gari.Alitaka kuingia akasita.Lakini mwisho aliingia nakuketi kwenye usukani wa gari hilo.
Dakika kama moja hivi aliitumia kufikiria akiwa ameshikilia usukani wa gari.Hata kama angetoka angeenda wapi kwa siku hiyo.Kulikuwa na dalili kwamba kesi ile inamuhusu asilimia mia moja.
Gahfla akashtushwa na mlio wa simu.Nywele zikamsimama kwa wasiwasi huku kumbimbi za ubataani zikicheza kwa kekefu za woga.Alitizama namba nakukuta ni ya mama mkwe wake!Mamake na Bario alitamani asipokee na kweli hakupokea.Aliiacha simu iite hadi ilipoisha.
Akawasha gari nakuondoka nalo kwa mwendo usio na mashaka.Lengo likiwa ni kutoka mji wa Arusha napengine kuhama kabisa Tanzania.Muda kidogo alikuwa amefika mjini.Hata ungemuuliza kilichomleta mjini asingekupa jibu lolote.Alizunguka na gari mjini na baadaye kufika hadi relini.Aliingia maeneo hayo nakuegesha gari eneo Fulani.Yeye akashuka nakwenda moja kwa moja maeneo hayo ya relini.Upepo ukiwa unapuliza alihisi utulivu uliokatika upepo huo na pumziko.Pengine upepo ungebeba mashaka yake nakumpa kitulivu cha moyo kama kinywaji baridi.Lakini ilikuwa bado katika siku ile ndefu kuliko zote.
Dakika zilikatika huku msongo wa mawazo ukimvaa.Hakika alipatikana nakuwezwa na mkumbo wa maisha.Masaa yakafutika bado yupo kwenye lindi la mawazo.Mida ya saa saba mchana alipokea tena simu.Hii ilitoka kwa jirani yake.Moyo ukapiga paa!Angesema nini?Au polisi wamekuja nini?Woga mtindo mmoja hadi akahisi chupi ikilowa wasiwasi!Nitafanya nini?Pengine wamegundua kilichopo nyumbani kwake.Hakupokea simu.Aliipuzia tena simu hiyo.Ikarudia mara ya pili na tatu bado hakuwa amepokea.Lakini hakufanikiwa kuipokea simu hiyo.Hadi inafika jioni hakuwa amepokea simu yoyote.Kulikuwa na miss call nyingi kwa utomvu wake wa kutopokea simu.Akaamua kupiga ile ya jirani yake.
Haikuchukua muda mtu huyo alipokea simu.Moyo ulimwenda mbio akijiandaa kujua kuna kitu gani ataambiwa!Hali ya hisia aliona atapokea habari mbaya kuliko zote.
“Helo?”
“Mbona napiga simu hupokei?”
“Nilikuwa kwenye mkutano nikasahau kuzima simu.”
“Dah!Yaani simu yako hupokei na hata mumeo hapokei.”
alipotajwa mumewe alihisi koo kukauka maana alijua alipomuacha ni wapi?Akatetemeka nakuhisi kama sauti ya jirani inapasua maskio yake.Alijikaza kisabuni kusugua suruale ya kitambaa kigumu!
“Amesafiri na yeye ameenda kwenye mkutano.”
“Hata ya shemeji yako haipatikani.”hapo alimaanisha Hamza na hivi ukijua kwamba Hamza alikuwa mume wa Laredo bado kulikuwa na shutuma za kumwaga baina ya watu hao!
“Hata yeye alisafiri.”
“Hamza alisafiri?”
Ikawa zamu ya jirani mama Shully kuuliza.Ndo kwanza Laredo akakumbuka kwamba Shully alifanya ofisi moja na Hamza kwa hivyo kumwambia kwamba Hamza amesafiri nikuzaa maswali bila majibu.
“Aliondoka alfajiri na mume wangu.”
“Dah!Sasa hapa una ugeni na mama mkwe wako.”
Laredo alihisi mishipa ya kichwa kutaka kumpasuka!Inamaana mama mkwe alipopiga simu alikuwa anakuja?Itakuwaje kama amefika nakukuta vya kukuta.Na kama amekuta bila shaka atakuwa ameita polisi na huo unaweza kuwa mtego.Lakini wazo hilo likafa kibudu kwa asilimia chache hasa akiwazia namna ya yeye kujijenga ujasiri na kwenda nyumbani kukabiliana na kesi kubwa kuliko zote.
Wakati mwingine hakujua kinachomkimbiza ni nini?Hakuwauwa watu wale isipokuwa mwanaye kwa kumkita risasi kimakosa tu.Polisi hawana dogo.Na kama angepata mwendesha mashtaka mjanja angembana na kumuweka katika hatia.Kwa jinsi alivyo mwepesi angesema kwamba alimpiga risasi mwaanaye kimakosa hapo ingezua kesi.Na tena yeye ndo mpishi wa chakula kile wangemhisi kama alitega kimakusudi.Na hivi mama mkwe hakumpenda bila shaka angemkandamiza kwa kumshutumu kusababisha vifo vya wanaye.
Aliishiwa nguvu.
“Kaja saa ngapi?”
“Toka saa tatu.”
Laredo akakosa pumzi akawa analazimisha hivyo kuleta msongo wa pumzi kutaka kuingia na kutoka kwenye kifua na kusababisha msongamano wa pumzi puani na kifuani.
“Yupo wapi mama mkwe wangu?”aliuliza Laredo.
Kabla hajassema simu ya Laredo ilikata chaji!Akaauma meno kwa hasira.Ilibidi aamke nakuanza safari ya kwenda nyubani kwake.Lakini anaenda nyumbani kwake kufanza kitu gani?Huko nikujipeleka kwenye kitanzi mwenyewe!Na maiti bado zipo sakafuni isipokuwa ya mwanaye ipo kwenye sofa nikiasi tu cha kuingia nakuziona!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 100
UPEPO WA USIKU-12
BONIFACE BIRAGE

Jiografia ya pale sebuleni kwake ilikuwa rahisi sana kwa mtu yeyote kuonza miili liyokufa ikiwa sakafuni na mwili wa mtoto ukiwa kwenye sofa.Laredo alipata picha yote ya sebuleni kwake akagundua kwamba alikuwa katika wakati mgumu kuliko wote aliowahi kupitia.Mpaka sasa hajui kama mama keshaona tukio zima au la!
Lakini ufunguo hakuacha kwa mtu yeyote bila shaka mama Shully atakuwa kamhifadhi mama mkwe nyumbani kwake.Kama ikiwa hivyo atakuwa na muda muafaka way eye kucheza karta mpya za namna yakukwepa kadhia hiyo.Pengine ataondoa mashaka yote akihakikisha mama mkwe haoni mwili wowote.Alipiga picha kichwani umbali wa nyumba ya mama Shully na pale anapoishi yeye.Akaona akinyatanyata ataweza kufika nyumbani kwake kisha aingie kwa mama Shully.Na kama akifanikiwa kuingia kwake bila kuhisiwa lolote ataweza kuibadili miili yote.
Laredo alirudi kwenye gari lake nakukanyaga gia kuelekea nyumbani.Bora aende kuliko kuishi na hofu dhidi ya nyumba ile yenye maiti takribani nne!Na hata akikimbia bado mwenye nyumba atarudi tu naipo siku ataamua kufungua nyumba.
Kichwa kilikuwa kizito sana.Akili iliwasha kama pilipili ulimini!Kuwa na majibu ya uhakika kuhusiana na matukio yanayomkabili lilikuwa jambo la kushtusha.Alienda moja kwa moja hadi nyumbani kwake.Mwendo wa dakika kadhaa alikuwa amefika nyumbani kwake.Gari alilipaki kuliko na jingo la CCM.Kisha akaanza kutembea kwa miguu kuelekea kwake.Alipita njia za mkato akitafuta namna yakukwepa kupita kwa mama Shully iliaweze kufika kwake bila kuvuta ufahamu wa mtu.
Alibeba maelfu ya mawazo huku akijipa moyo kwamba njia ingepatikana.
Alikatika njia kadhaa nakufika anakopanga.Alisukuma geti nakuingia ndani.Mwili wake ulitepetevuka kwa huzuni.Aliingia akiangalia mazingira ya pale.Mlangoni aliona ukiwa umefungwa kama alivyouacha.Akausogelea mlango wake kwa haraka nakutaka kutoa funguo kwenye pochi lakini kabla hajatoa aliona kitu cha ajabu pale mlangoni.Aliona kiatu cha mtoto wake!Mwili ukafa ganzi!Akajikaza huku akitaka kulia!Kumbukumbu za kumuua mwana zilikuwa bado mbichi kwenye kichwa chake maana tukio limetokea asubuhi ya siku ile!
Ni mama!Tumbo la uzazi likamuuma!Mwanaye alikuwa maiti hapo ndani.Mwili wake ukasisimka!Wakati akiwa ameganda akimfikiria mwanaye akasikia mtu kumsimamia kwa nyuma!
“Mwenzetu vipi?”ilikuwa ni sauti aliyo tamani kuikwepa kwa namna zote lakini tayari mtu huyo alikuwa nyuma yake na bila shaka alitakiwa kuonana naye!Ilikuwa sauti ya mama mkwe!Kumbe hakuwa ameenda kwa mama Shully bali alikuwepo hapo uwani.
Laredo akageuka huku akiwa tayari kafuta machozi yake.Uso wake ulisawijika!Bilula za macho zilikuwa na unyevuunyevu uliokithiri.Bila shaka ungejua alikuwa akilia kwa shake!Mama mkwe alimuona mwali wake akiwa hayupo hivyo.Alimtambua kama mtu mcheshi.Lakini uso aliokutana nao muda huu sio ule aliouzoe kila uchao.Ulikuwa uso wenye maumivu makali!
“Mkwe kwema?”aliuliza bimkubwa huku amemkazia macho.Anga lilikuwa limenuna.Ukimya wa anga ulilipa eneo lote kuwa makazi yenye ukiwa.
Laredo aliitafuta sauti yake akaipata,”Kwema shkamoo mama.”ilimtoka salamu iliyofukizwa mawimbi ya kilio.
Ungedhani manyezi yalikuwa yakimfuatilia.Macho yalipepesa kwa kihoro.Lakini hakuwa na budi alihitajika katika maneno.Maana mgeni kaja.
“Marhabaa mwanangu.Mbona nimekuja hapa masaa mengi lakini ulikuwa haupatikani?”mama aliuliza.Laredo akaona soni hasa ukizingatia yupo likizo na kuna ugeni mkubwa sana iweje nyumba ikose mtu?Hilo lilikuwa pigo kwake.
“Nilienda kwenye mkutano mama.”
“Sasa ndo mniweke masaa yoote hayo?Mimi nimetia guu langu hapa tangu muda.Nimeka wee.Sioni mtu.Nkaenda kwa jirani yako mama Shully ndo kanisetiri.Ila nkaona nimekuja kwa wanangu yanini kuwa kwa mtu muda wote?...Bora nije hapa nikusubirieni wote hapahapa.”alieleza mama mkwe kwa hali ya kulaumu flani hivi.
“Umekuja muda mrefu sana?”
“Eeeh!...Tumepiga simu wee hakuna anayepokea na hivi mama Shully alifuata kitu hapo kwake ndo kanisaidia.Wewe hupatikani malkia wa nyumba.Mwenzio Bario hapatikani.Hamza naye haonekani!Yaani leo mliamua kunifumbia maskio na macho si bure.”aliendeleza ngonjera zake.
“Samahani mama’ngu tulikuwa mbali.Sikujua kama unakuja?”alisema Laredo akiwa anatoa funguo kwenye pochi.Alipoangalia kwenye mkoba akakuta hakuna funguo!Kaziacha kwenye gari?Alijiuliza bila kupata majibu ya swali lake.Anaenda kuzitoa tena kwenye gari?Kidogo jambo la kuwa hana funguo lilimpa afueni.Maana alijua fika lazima kama zingekuwepo angetakiwa kuufungua mlango.
“Mmmh!”
“Mbona waguna mwanangu?”
“Mama sijui nimeeacha wapi funguo za nyumba?”alijiuliza ungedhani walikuwa wote na mama mkwe.Alitamani kweli kumwambia mama mkwe kwamba ndani kuna maiti za watoto wake.Ila anaanzaje?Kwa lugha ipi?Presha mwendo kasi.
“Mtumee!Kwa hiyo tuna fanyaje.Mumeo siujaribu kumpigia?’’kauli hiyo ilikuwa msumari wa mto.
“Simu yangu imeisha chaji!Halafu wote wapo safarini tangu juzi nasijui wanarudi lini.”akatunga kauli ya haraka.Kwa wakati kama ule lolote lingefaa kutoka kinywani mwake.Bora akwepe kujua kulikoni za uwepo wa Bario.
“Hivi Bario na Hamza kwani hawakukwambia kama nakuja?”aliuliza mama mkwe kwa uhakika.Ina maana alishawasiliana nao?Laredo akatumbua macho!
“Kwani wanajua kwamba ungekuja?”akauliza.Hapo mama mkwe alimuangalia kwa udadisi Fulani kana kwamba kuna kitu kina fichwa.
“Mwanangu nimeongea na hao watu wote na makubaliano tukutane hapa kwako.Nimeongea nao jana nadhani walikuwa nyumbani.Wote wakaniambia nitawakuta.Na hata nikaambiwa unanisalimia,pia nikawaambia wakusalimie na nitakuletea ulezi.”mama mkwe akashona maneno yenye kushtua.
“Kha?”
“Yaani mwanangu ukiniambia wame safari nashangaa sana.Hata Bario akaniambia mjukuu wangu anatoka shule leo.Tena nikambebea kuku wake wawili wale pale nimewafunga.Si hata naona kiatu cha mtoto hapo mlangoni.Wewe mwenyewe unajua nikija na kuku hizo za mjukuu wangu!”
Laredo akawa na pingamizi jipya!Uongo wa kwamba Bario hayupo ukafa kibudu
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 82
UPEPO WA USIKU-13
BONIFACE BIRAGE

Hatari ilikuwa dhahiri kwenye kumbi za macho na masikio yake.Yaani aliisikia nakuiona pia kwa mkupuo.Maelezo ya mama mkwe ni msumeno.Anzeje kumdanganya kwa lipi?Huu ulikuwa mtego mzuri hasa kwa wasumbufu kama yeye.Bila shaka dalili za yeye kushtukia zingejitokeza muda simrefu.Kina Bario walijua fika kuwa mama anakuja lakini hawakumwambia lolote.Hilo lilitosha kupigilia bumbuwazi usoni mwake.

Uongo wake aliona kama utaonekana mbaya zaidi ya vile alivyotazamia.

“Hao vijana wananchezea!”mama mkwe alikata kauli kwa ukali.

“Mmmh.”akajikuta anatoa mguno huku akijiuliza ni kauli gani atumie kumficha mama mkwe.

“Mwanangu mimi naona mmeamua kunifukuza kwako.Nilikuja hapa kuwaoneni hasa na hao vijana niwape taarifa kuhusu mambo yanayoendelea huko nyumbani.Sasa mkiniambia wananidanganya nashtuka!Ujio wangu hapa si wasiku nyingi nitaondoka baada ya muda mfupi.Kuna mambo yakifamilia yana subiri kauli za vijana wangu.”

“Lakini hawapo.”alijitetea Laredo.

“Unanifukuza?”aliuliza mama mkwe.

“Sikufukuzi mama.”

“Sasa mbona unsisitiza hawapo na mimi niliongea nao wote kuwa wapo hapa.”

Laredo akameza mate machungu!Bimkubwa angepanda hewani ndani ya muda mfupi.Munkari wake unaowaka kama moto wa nyasi kavu nyikani anaujua Laredo.

“Kwanza mjukuu wangu anafika saa ngapi?”akauliza mama mkwe swali lililo gumu kuliko yote.Fundo la huzuni likachipuka kwenye mifereji ya nafsi yake!Ilikuwa ghafla sana bila kutegemea alijua alitakiwa kujibu maswali hayo.Aliwaza sana wapi pakumpeleka mama mkwe hadi atakapotoa maiti na kisha yeye kumuingiza ndani.Alikosa jibu akajiuliza.Na anapouliza kuhusu mtoto yatatakiwa majibu.Akisema haja itamlazimu kuulizia shuleni iweje mtoto awe hajafika na lazima atoe majibu hayo la sivyo kitanuka!Haitakiwi kuipa shule maswali maana kwa haraka sana wangeuliza mtoto alikuja nyumbani.Na hivyo kumlazimu kuhitimisha kwamba mtoto hajulikani alipo ni kuwapeleka polisi kutoa taarifa!Hilo lingezua mengine.Ukweli hakuwa tayari kuwashusisha polisi kwamba ni yeye anajua vyanzo vya mauaji hayo.Bila shaka nikujiingiza kwenye mzingo wa kesi!

Akataka kusema mjukuu kaenda kwao.Lakini wazo hilo likafa pia.Asingesema yupo kwao huko nikuwaingiza kwenye mzozo mpuya.Ukweli familia yake wamekufa watu wane.Ndani ya nyumba yake na yeye pekee ndo mzima.Alikuwepo hapo kalala nakuamkia hapo.Kwa vyovyote anajua bila hiyana kwamba watu hawa walipatwa na nini mpaka mauti yalipowakuta.Hilo lilitosha kumzuzua kichwa.

“Mjukuu?”

“Eenn.Mjukuu wangu yupo wapi?”

Laredo akashika kichwa akiwa kama hajielewi.Akajihangaisha huku na kule huku akichelewaa kujibu swali la bimkubwa ambaye alionesha kushangazwa na butwaa la mkwe we.

“Hivi wewe upo sawa?”alimuuliza huku akizidi kumkazia macho.Tayari jibu la yu wapi mjukuu lilichelewa.Na kweli hajui aseme nini wala kipi?

“Nashindwa kujua ufunguo upo wapi?”alijisemea kupotezea.Mama mkwe alibaki kumshangaa binti huyu.Lakini aliamua kutumia busara akitegea kwamba kuna kitu basi ataelewa.Maana alianza kuhisi kama huyu binti hayupo sawa.

“Sasa siuende kwenye gari ukaucheki?”

Laredo akazinduliwa na kauli ya mama.Lakini akajiambia kwenda kwa gari ni mzizi mpya wa kuutengenezea uwongo mpya.Akajikuta akitaka kupiga hatua lakini akasimamishwa na mama mkwe.

“Hivi mwanangu upo sawa kweli?”

“Mimi?”alijishika kifua.

“Ndiyo wewe nakuuliza upo sawa?”mama akarudia swali lake.Msichana hakuwa wakawaida tena alimezwa na wasiwasi wake.

Laredo akajikuta akipiga hatua mama mkwe akamfuata nyuma sako kwa bako.Walienda hadi kwenye gari ambapo Laredo alifungua wakaingia ndani.

“Mama naomba ubaki kwenye gari naenda kushughulikia mlango.”alisema Laredo.Kidogo mama alinunua kauli hiyo na akawa amemwelewa kishingo upande japo si kwa asilimia mia moja.Laredo alitoka pale nakurudi kwake.Tayari alipoingia kwenye gari aliuona ufunguo akauchukua bila mama kujua kuwa tayari ameshapata ufunguo.

Mwendo wa kurudi kwake aliukimbiza kwa haraka.Alipofika alifungua mlango.Akaingia nakukutana na nyumba nzito!Ilikuwa yakutisha.Halafu yenye hewa nzito.Pengine ni kwasababu alipafunga toka asubuhi bila kufanya usafi.Nyumba ilizidi kuwa nzito pengine nikutokana na matukio yenyewe tangu asubuhi hiyo iliyojizalia maiti nne.

Akasogea nakuona mwili wa mwanaye kwenye sofa.Akasisimka.Machozi yakatoka huku akihofu.Ilibidi afuate mwili ule.Akaugua moyoni mwake.Ilibidi aubebe nakutoka nao hadi chumbani mwake pengine akiuweka chini ya uvungu.Aliendelea kububujikwa na machozi huku akirudi ukumbini.Alitakiwa kufanya jitihada zote kabla ya mama mkwe kumfikia.Japo alihisi anaweza asitoke kwenye gari hadi aje lakini hilo siyo uhakika kwamba angebaki huko.Ilibidi auburuze mwili wa Bario hadi chumbani mwake.Mwili ulikuwa mzito sana na ulikaribia kumshinda lakini alijaribu kwa nguvu zote.Hata hakujua aliificha kwa madhumuni gani maana akili haikufanya kazi kwa viwango vyake.

Akarudi tena nakuukokota mwili wa Masua hadi chumbani mwake.Jasho lilikuwa likimtoka na njaa ilimuuma sana.Kiwango cha nguvu zake kilikuwa kidogo sana.Akafanya mambo hayo kwa kujikaza akikimbizana na muda.

“Jamani mababy wangu kufaa uwii…Hamza wangu umeniacha na ukiwa nani aliyewaua Mungu wangu nisaidie.”alilia kwa shake huku akiikokota mwili wa Hamza akirudi nao chumbani mwake akiwa anakaribia kuuzamisha ndani akahisi hatua za watu!Mwili wote ukazidi kutetemeka!Hatua hizo zilikuwa pale sebuleni mwake halafua akasikia hatua hizo za vishindo vikija upande wa chumbani!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 76
UPEPO WA USIKU-14
BONIFACE BIRAGE
Mwili wake ulizizima mtetemeko kama mtu mwenye arosto ya muda mrefu.Akajiandaa kukabiliana na yeyote atakaye ingia humo ndani iwe kwa kheri au shari lakini siri ya kuficha maiti zile tatu ilitakiwa itunzwe.Vishindo vikafika chumbani mwake hapo mlangoni.

“We mwanangu mbona umefungua mlango?”aliuliza mama mkwe akiwa hapo nje.

Laredo akajikusanya akiwa hajui aanzie wapi wala aseme nini.

“Nimeuvunja.”alijibu bila kujua anamaanisha nini?Akauzamisha mwili ndani kwa haraka kisha akarudi hadi mlango wa chumbani akatoka nje nakumkuta mama mkwe pamoja na mama Shully wakiwa hapo mlangoni.Alianza kuwaongoza kurudi sebuleni.Walipofika alishangaa mama mkwe kuendelea kumdadisi kana kwamba kuna kitu anakagua kwa uangalifu.Kitu ambacho hata yeye mwenyewe hakukijua.Japo kwa muda kama ule alitegemea kushukiwa kila hila.

“Umevunja mlango?”mama mkwe akarudia.

“Ndiyo mama.”

“Mlango wako wa nondo sasa umevunjaje we mwanamke?”

Laredo akashtuka tena.

“Huu mlango hauna dalili zozote za kuvunjwa.”

“Nilivunja.Kuna namna nilifanya.Lakini haikuwa kazi ngumu kiasi hicho inishinde.”

“Na hilo jasho unalovuja ni la nini?Utadhani ulikuwa unabeba gunia!”ilikuwa kauli tu lakini yenye uzito mkuu.

“Hamna mama nilikuwa na…na…na..”akapatwa na kigugumizi kumbuka kekefu za kilio alizotoa muda mfupi uliopita.Sura yake ilikuwa na maumivu makali.

“Laredo kwanini unakigugumizi?”akauliza mama mkwe.

“Kwani shoo mbona macho mekundu au ulikuwa unalia?”mama shully akaingiza gia nyingine ambayo ilizidi kuyumbisha mwendo wa maongezi haya.

“Hapana ni…nii”asikudanganye mtu kilio cha msiba kama ule ni kigumu sana.Laredo alijikuta akishindwa kujizuia nakuangua kilio kingine chenye uzito.Kilitoka kwenye chemchem za kilio cha moyo wake nakupasuka kama mwamba!Alilia!Hali hiyo iliwapa mushkeli mama mkwe pamoja na mama Shully wakishindwa kuunganisha nukta za fumbo hilo la kilio.Walibaki kumtumbulia macho.Kilikuwa kilio cha kushtukiza.

Ilimchukua dakika kama mbili hivi kurudi katika kumbukumbu zake akajua alikuwa anafanya makosa makubwa sana kulia mbele za watu hawa na bila shaka kaleta maswali mengi dhidi ya kilio chake kisicho na majibu.Ilibidi ajitathmini kwa haraka kwamba angefanza nini?

“Mbona unalia kama umefiwa?”mama mkwe akaendelea kumdadisi.

“Eti bimkubwa una nini.Unaonekana una huzuni sana.Kilio cha mtu mzima sio cha mzaha.Hebu tuambie kuna nini?”ilikuwa zamu ya mama Shully kuingilia kati.

“Hakuna kitu.”alijibu kwa sauti yenye mawimbi.Ulikuwa upumbavu maana jibu hilo halikuwa pumbaza wadadisi wake.

“Unajua maana ya kulia hivyo?Kilio chako si cha kawaida lazima kinitatulie fumbo langu.”

Akawaza kwa haraka lakini bado akili yake ilikuwa taratibu kwa viwango vikubwa sana.Alikuwa hajielewi.

“Ni kichwa kinaniuma sana.”ilimtoka.

“Unajua wewe ni mwongo.Utaumwaje na kichwa halafu ulie hivyo na mumeo ni tabibu wa madawa.”mam mkwe alikuwa kama anampasha kwa upendo.

“Nadhani nahitaji miwani yaani kinauma kwenye paji halafu kuzunguka hapa.Huwa kina jirudia mara kwa mara.”akajitetea.

“Sasa kwanini usiende hospitali muda wote huo?”

“Mama nilikuwa kwenye mkutano.”

“Ingepaswa uende uache kiburi na afya yako!Oh hooo!”alisema mama mkwe akijikaribisha kwenye kiti.Laredo hakuwa anajiamini.

Wakati wanabishana pale mama mkwe aliona kitu karibu na mlango.Akaguna.

“Shoo inabidi tu uende hospitali upewe kama ni miwani.”

“Nitaenda wala usijali.”
“Halafu nimepigiwa simu na bosi wangu wanamuulizia Hamza kuna file anatakiwa kulikabidhi.”

“Hivi bado wanamtafuata?”Laredo akauliza kama vile hajui kitu.

“Ndiyo anasakwa sana hilo file ni muhimu simu zake zilipigwa lakini hazijibiwi na yeye mwenyewe hajapiga kutoa mrejesho.”

Mama mkwe aliwaangalia tu akijiuliza hivi hapa kuna nini kinaendelea.

“Kwani ni tangu lini Hamza hajaja ofisini?”mama mkwe akauliza swali ambalo Laredo hakulitaka.

“Ni leo tu ndo hajafika kazini.”mama Shully alijibu.Ikawa zam,u ya mama mkwe kuzubaa.Hivi Laredo aliniambia nini?Mama akauma meno akijua anadanganywa mchana kweupe.Wakati wanajiuliza hayo.Simu ya mama Shully iliita akaipokea alikuwa anahitajika nyumbani kwake mara moja.Ilibidi aondoke.Muda ule mama mkwe aliinuka akijinyoosha.

“Mama ngoja nikafunge gari.’’alisema Laredo.

“Kwani hulileti nyumbani?”
“Hapana nitalilalaza kule ccm.” Alisema akiwa kainuka anaelekea nje.Alienda moja kwa moja.Wakati haya yakijiri mama mkwe alirudi pale alipoona kitu halafu akaguna.Alienda nakuona damu ikiwa imetota kwenye zulia pale ukumbini!Akaiangalia vizuri damu yenyewe ilikuwa ya masaa bado kuna kaubichi Fulani!Halafu kando kulikuwa na soksi za mtoto za shule!Pembeni tena kulikuwa na begi la mgongoni la mwanafunzi!Vyote hivyo vilimpa udadisi.Akalifuata nakulifungua,akasoma jina la daftari moja!Lilikuwa jina la mjukuu wake.Kumbe mjukuu wake!

“Kumbe mjukuu wangu karudi?”mama mkwe akajishauri apeleke begi ndani.Akaona liende chumbani kwa Laredo.Akaelekea huko ndani.Aliufungua mlango!Chumba kilitisha sana!Alipoingia ndani alipiga hatua kama tatu nakuweka begi kitandani lakini akahisi amekanyaga kitu cha unyevuunyevu!

Akahisi ni maji akarudi hadi ukumbini ila akapatwa na mshawasha wa kujua amekanyaga nini?Alipoutupia mguu wake macho akashtuka kuona damu!Nywele zikamsimama!Pale ukumbini aliona damu halafu tena hapa kaikuta!Akastaajabu sana!Hii damu kaikanyagia kule chumbani!Akainuka kwa haraka kurudu kule chumbani!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 74

Similar Discussions

Back
Top Bottom