UPEPO WA USIKU-4
BONIFACE BIRAGE
Alipokamilisha kuoga alirudi akielekea chumbani nakubadili kwa kujitanda khanga tu bila kuvalia chochote ndani.Alielekea sebuleni ambapo mumewe alikuwa anangoja chai.Alienda akamtengea chai kisha akaketi naye kumdadisi anavyokula kwa apetaiti.Alijua hadi vipimo vya sukari kumwekea kwenye chai.
“Vipi mipango ya leo mume wangu unajua nimechukua likizo nando naanza leo.Ungependa nikuandalie nini?”ilikuwa ni mazoea yake kumpa hamasa mumewe yakurudi nyumbani maapema.
“Chochote baby.”
“Jamani habi niambie ungependelea nini?”alimdekeadekea mumewe.Hiyo ndo nyuso ya mwanamke aliyoitumia kumnasia mumewe.Alikuwa na nyuso tofauti za kumdaka bakunja.Na kila nyuso ilikuwa na tafsiri husika.Wala usingejua matendo yake ya usiku wenye upepo.Kweli upepo hubeba mambo mengi nakuyapeleka inapotaka kwa manufaa yake wenyewe.
“Haya basi,niandalie ndizi mchemsho.Nadhani itafaa kwa mlo wa jioni.”alikamilisha ombi la mkewe.Kumridhisha.Sasa walibadilika na kuwa mtazamo tofauti ya usiku yalikuwa usiku na kuzama na siri za usiku wa kiza.
Alimaliza chai,ni kwamba aliona amechelewa yeye hutoka saa kumi na mbili kamili kuwahi kazini ndo utaratibu wake.Siku imeanza anatakiwa kuipokea kwa wepesi na haraka.
“Umeshiba?”Laredo alimswali mume wake.
“Nimeshiba.”
Kuhakikisha kama kweli mumewe ameshiba alimbinyabinya tumbo lake kulipima hivyo ndo humkagua.Hayo ndo maisha yao yalivyo.Tukio la jana likabaki kama historia!Kana kwamba hakuna kilichojiri.
Mumewe aliinuka nakutaka kutoka,”Ngoja mme wangu?”alimzuia.Akaenda akamshika mikono nakuanza kupiga sala kabla mumewe hajaondoka.Sala yenyewe iliendeshwa na Laredo mwenyewe.Kisha Bario aliondoka zake.Alimwangalia anavyoondoka akarudi hadi kwenye kochi nakujitupa.
“Mmmh!Mapenzi haya yana mambo yake.”aljisemea nusu kusikitika nusu kufurahi.Wala usingejua ni yeye katoka kumuombea mumewe muda huu.Alikuwa na tabia za ajabu.Kumdhulumu kimapenzi lilikuwa jambo la kawaida kwake na wala hakuona taabu yeyote.Na sasa anamuombea heri mume huyuhuyu aliyemsaliti usiku uliopita.
***
Bario alipita njia za mkato kufika anapofanyia kazi kwenye duka lake la dawa maeneo ya hapa Arusha mjini kaloleni ndanindani.Huwahi asubuhi akiwa na maana yake.Duka lake lilikuwa sambamba na baa kadhaa zilizofunguliwa eneo hilo.Pia kulikuwa na gesti za kumwaga.Hapa palisifika kwa biashara iliyodumu kwa miaka mingi sana.Biashara ambayo hakuna nchi au taifa lisiloifanya.Biashara ya ukahaba.Aliijua ndani nje maana makahaba hao walikuwa wateja wake wakuu.Hasa wakihitaji bidhaa kama kondomu na vidonge vya uzazi wa mpango!
Na vilevile pia alifanya nao biashara hiyo ya nipe nikupe.Kuwahi asubuhi ndo starehe yake kuwaona machangudoa hao wakiwa ndo wanamalizia shift za usiku.Ungewaona walevi,wamechoka sana.Na anaowapata asubuhi ni wale ambao hawakuingiza biashara usiku au unapata kipata hakikuridhisha.Hao ndo huwapata asubuhi wakiwadaka wapita njia nakujinadi kwao.Aliweza kuwatambua wanawake Malaya kwa urahisi sana kila asubuhi.Wako aliwaona wakibebwa kwenye pikipiki ungewaona na viguo vifupi au wamejisetiri kwa mitandio.Akacheka kila alipowaona alishalala na wengi nakuwajua ndani nje ladha zao.
Aliingia dukani nakufungua.Kisha hata kabla hajalifungua lote alijiwa na moja ya popo wa usiku.Alipomtizama alimtambua ni Amina.Bila shaka upepo wa usiku ulishampiga.
“Niambie DK Bario za asubuhi?’
“Salama vipi hujaenda nyumbani?”
“Hamna dokta,nilikuwa na ngoja nikupe huduma unajua na deni lako.Nilichukua dawa za uzazi wa mpango nasijalipa.Kijiwe kilikuwa kibaya.Wacha tumalizane kiaina au vipi?”
Bario akatabasamu.Amina aliurudishia mlango akazama ndani.Walitekeleza shughuli yao palepale dukani.Hayo ndo maisha yake.Bario hakuyapenda maisha yakina dada hawa.Upepo uliowapiga haukuridhisha kabisha.Maisha yalijaa kila aina ya uchafu.Walipokamilisha Amina alivaa nguo zake.
“Halafu dokta,sina nauli naomba unikopeshe.Nikishindwa kulipa tutamalizana hivihvi au vipi?”alisema Amina mwenye wingi wa ushaufu huku akijipindapinda kama anogea maji yenye joto la kuridhisha.
“Poa.”alijibiwa purazai huku dokta Bario akitengeneza shati lake.
Bario alivaa suruale yake kisha akatoa mfukoni elfu moja na kumpa Amina.
“Asante mpenzi.Tutaonana jioni basi.”amina alichanua kwa tabasamu la shukrani kutoka moyoni.Ilikuwa pesa nzuri ambayo ingemfikisha nyumbani mwake.
“Poa.”
Amina akatoka zake.Bario akafungua duka.Mteja wa kwanza akaja.Alikuwa ni msichana hivi.Mweupe aliyetumia sana mkorogo.Bila shaka ni mafuta kama carolight.
“Karibu sana.”
“Asante.”binti alionesha kama kukichunguza chumba kile kana kwamba kuna kitu anataka.Bario alimwacha aagize anachotaka.
“Nahitaji marashi ya maiti!Pamoja na damu lita mbili!Tena damu ya binadamu.!”alisema Yule msichana nakumkata maini Bario!Akatumbua macho kwa mshangao asijue ni kitu gani huyu binti anasema!Alihitaji vitu ambavyo havikueleweka,”Halfu na chupa moja ya maji ya maiti.Yaani maji yaliyooshewa maiti.”tena alizungumza akiwa makini!Bila kupepesa macho!Bario alitumbua macho kwa mshangao na mwili wote kusisimka!
Kisha alifanya kama kufunua nguo yake akimwonesha kitu Bario.Alifungua hadi usawa wakifua.Titi la upande wa kushoto lilikuwa limeoza nakutoa harufu kali!Bario hakustahamili alitua chini kama mzoga !
UPEPO WA USIKU-5
BONIFACE BIRAGE
Laredo alienda mjini kutembea hasa kwa kipindi hiki cha likizo.Alikatiza kwenye viunga vingi vya mji huku akiwa na kesi kubwa ya kujibu baina ya wanaume wawili wanaompelekesha mpaka sasa!Ni mume wake?Au ni Masua.Wote walimuweka kati kwenye mtanange ambao kwa upande wake haukuwa na njia ya kutokea.Angefanya nini?
Alipita mpaka casino nakupata vinywaji pamoja na makadabrasha mengine kuchangamka kwa siku kama ile.Alitumia muda mwingi kunywa ilikupoteza hofu na kiwewe cha mumewe kumkwepa kimapenzi.Alifikiria tena mzunguko wote wa ndoa yake.Ni kweli kwamba amezama kwa Masua nakutoka ni muhali mkubwa sana.
Alishajipa mawazo ya kuondoka katika mkusanyiko huo wa ndoa.Lakini haikuwa busara kuvunja ndoa.Ingekuwa vipi?Kila akikumbuka matukio ya mumewe alijipata akiugua moyo.Mpango wake ulimtuma kuwa na wanaume wawili.Liwalo liwe lakini lazima awe na wawili.Kuivunja dhamira hiyo ni vigumu.Ndiyo mapenzi ya mumewe yamepungua lakini sio hatma ya yeye kuwa bila mtu.Na kama angefanikiwa kuwachukua wote wawili angetekeleza kitu tunaita Polyandry yaani mwanamke mmoja wanaume zaidi ya wawili.
Angeandika historia ya tukio hilo na hakuna wakumuhukumu kuhusu hilo.Alirudi nyumbani akiwa amelewa sana bila kuzungumza akaingia bafuni nakuoga kisha akaenda kulala.Alishtushwa na ujio wa Masua.Bila hata haya Masua alinza purukushani za kukabiliana na Laredo,”Mwenzangu vipi kwani?”
“Nimetoroka kazini bibie yaani na usongo na wewe ile mbaya.”wakati huo alishaweka busu la mdomoni ambalo lilipwaya kutokana na kupishana kauli.
“Yaani umetoroka kazini juu yangu mwanaume hasidi wewe.”alijibu Laredo kwa maringo ya kike kuona anakubalika hadi mtu anatoroka kazini kuja kupumzika naye.
“Sasa nifanyeje Laredo mimi mwenyewe hoi juu yako.”kauli yake ilijaa hawaa.
“Jamani sasa mume wangu akija si itakuwa taabu?”
Masua alicheka.Maana alijua mume wa huyu awezi kurudi mchana hata iweje.Nyakati zake huwa ni usiku tu.Alitabasamu na kwa mtindo ule wa kutabasamu ulionesha kwamba amegundua uongo wake.Laredo bila kufikiria mara mbili alimvuta Masua kitandani.Akachojoa nguo za Masua nakuziweka kando!Laredo alitoa khanga ikawa huko!Mwili wake ukachemka kwa joto la ghafla!Dakika chache walikuwa wanafanya mapenzi kwenye kitanda cha mume wake!Msuguano mzito ulibebwa na tama zisizo na kikomo!Hawakutambua lolote kadri muda ulivyosonga!
Walikuwa mbali katika zoezi hilo!Huku wakiburuzana kwa kasi ya ajabu!Uwizi wa mapenzi!Wakati wakiwa wamezama kabisa walishtushwa na hodi iliyokuwa inabishwa!Jasho likiwa linawatoka wakajipata wakikurupuka kutoka kitandani!
“Atakuwa nani?”aliuliza Laredo wakati huo wakiwa na wasiwasi na mashaka!Mioyo yao ilienda mbio kwamba wapo mbioni kugundulika.Akili ya Laredo iliwaza mambo mengine!Mahesabu yake ni kumiliki wanaume wote wawili kwa wakati mmoja.Hilo ndo wazo lake usiku na mchana.Akiwa bado damu inachemka na wenge la kutoka kufanya mapenzi na Masua alijipata miguu ikitetemeka.
“Nikwambie kitu ingia chini ya mvungu.”
“Lakini?”alitaka kubisha kwa wasiwasi.
“Fanya hivyo Masua sina jinsi.”alitetemeka mpaka kichwa kwa hofu na mashaka!
Masua alitii amri nakuingia chini ya mvungu mara moja!Akasahau kumwambia avae nguo.Masua aliingia chini ya mvungu akiwa uchi wa mnyama!Pigo kwake tena kubwa!
Laredo alichukua upande wa khanga.Hofu yakuhisiwa janaba alijiadhari kwa kukaaa mbali na huyo atakayekutana naye.Alienda moja kwa moja hadi sebuleni.Tayari mgongaji alikuwa ameshaingia ndani.Tena alikuwa kwenye kochi akiwa amemweka mtu huku akimpepea!
Aliwatambua watu wale kwa haraka sana!
“Jamani shemeji imekuwaje?”aliuliza Laredo.
“Nilipitia dukani kwake namkuta kaanguka chini!”Watu wawili walikuwa wameingia ndani mwake.Huyu ni Bario pamoja na mdogo wake,Hamza.
“Shem ningoje kidogo naenda msalani.’hata hakusubiri jibu,Laredo alikimbilia bafuni kurekebisha mwili wake!”alioga fastafasta nakubadili mavazi kusudi janaba isisikike.Masua alikuwa bado chini ya mvungu!
Akarudi hadi ukumbini nakuanza shughuli ya mume wake kumhudumia arudi sawa.
Alimkagua,”Mume wangu?Mume wangu?Umepatwa na nini babaa?”
aliona mumewe akiwa kimya.Hali yake ilikuwa mbaya kiasi.Haongei wala hasemi lolote lile la kuridhisha.
“Mmmh?Shem naona aende hospitali.”Hamza alitoa ushauri huo.Hakukuwa na pingamizi zaidi ya kumbeba nakumpeleka hospitali.Walitoka hadi nje.Laredo alimwita dreva tax aliyehifadhi namba zake za simu.Muda mfupi mbele walikuwa mbioni kuelekea hospitali.Huku nyuma Masua alichomoka uvunguni akarudi chumbani kwake.Nyumba ile walikuwepo wapangaji wawili tu yaani Laredo na mumewe halafu Masua wapili.Vyumba vingine vilikuwa bado havija pata wapangaji.
***
Jioni Laredo alikuwa amerudi kutoka hospitalini akimwacha Masua amelazwa baada ya kupatwa na mshtuko.Angetakiwa kuwa mapumzikoni kwa muda kidogo ilikujipa nafasi ya kupata matibabu na hali yake ingerejea vizuri.Haikujulikana mshtuko ulisababishwa na nini?Japo alitoka akiwa sawa.Laredo asingesema mengine ya familia yake maana ni siri.Japo alijua vyema mumewe hajui karata anazozicheza.Angeupelekesha mchezo wak siri.Dhana ya kwamba mshtuko wa mumewe umeletwa na vituko vyake ilikufa kibudu!Ilibidi Hamza amrudishe jioni hiyo.Hamza alirudi kwa kutumia gari lake la kazini.Akiwa amemfikisha getini kwake yapata saa saba usiku gari likasimama.
“Asante shem wangu.”
“Haina taabu shem.”alijibu Hamza.
“Tuombe Mungu my husband is strong.Najua kesho atakuwa salama.Mpaka amepatwa na mshtuko labda ni jambo kazini.”alisema Laredo.
“Nyumbani hakuna habari ambayo ingepelekea awe na mshtuko huo.”shemeji mtu aliongeza.
“Ndiyo.”alijibu kwa uchovu ni kama lepe la usingizi lilikuwa mbioni kumkabili.
Ukimya ukapita wa muda.Ukimya huu ulikuwa wa shari.Kibaridi cha usiku kikifuka moshi!Ghafla Hamza alimvuta Laredo nakuanza kumbusu!Laredo akaitikia!Busu la shemeji yake lilimvumbua nakuukimbiza usingizi huku neva za mwili zikipitisha ukakamavu uliondoa uchovu ulioandamana kwenye mishipa ya fahamu.
Hakuwa na pingamizi!Alirudisha busu kwa shemeji mtu!
SURE NAMM NDO NAZITAFUTA LKN SIJAZUPATA ....