Riwaya: UCHU

da! safi mkuu mareche kama vip episod nyingine
 
UCHU
KASHESHE
XIII
Huyu Willy Gamba lazima atakuwa
kaingia hapa, hatujui kapita njia ipi na
yuko sehemu gani?", Nkubana
alimwambia Col. Gatabazi kwa njia ya
radio.
"Haiwezekani, hakikisha kwanza", Col.
Gatabazi alijibu kwa hofu.
"Hakika ni yeye Willy Gamba, tumekuta
sehemu imechimbwa chini ya ua mita
kama tatu hivi kwenda chini, hata hatujui
imetumika nini kuchimba ardhi. Kwa
maana hiyo, tumeanzisha operesheni kali
ya kumsaka ndani na nje ya kambi,
japokuwa hatuna uhakika kama bado
yuko ndani ama ametoka. Hakika mtu
huyu ni hatari sana, itabidi kuongeza
ulinzi katika eneo hilo hususan mahali
mlipo, nitatuma askari zaidi kuimarisha
ulinzi hapo", Nkubana aliahidi.
"Kuna madhara yoyote kafanya huyo
Willy", Col. Gatabazi alihoji kwa wasiwasi.
"Mpaka sasa hakuna, tumekagua sehemu
zote ni salama isipokuwa hapa kwenye ua
palipochimbwa ardhi, ni sehemu hii tu".
"Nani kagundua eneo hilo limechimbwa
na muda gani umepita toka hali hiyo
itokee", Col. Gatabazi aliuliza tena kwa
shauku.
"Niko hapa katika eneo husika afande",
Nkubana alijibu. Baada ya ukimya wa
sekunde kadhaa akaendelea. "Askari wetu
mmoja wa doria aliyepangwa kulinda
eneo hili la ua anasema haiwezi kuwa
zaidi ya dakika kumi na tano hivi
zilizopita. Nafikiri bado hajaingia ndani,
anasubiri ama ameona ndege wakati
mnaingia, anaweza kuwa anajipanga
kujaribu kuanzisha mashambulizi. Ujue
yuko pamoja na Bibiane ambaye anaijua
sehemu hii vizuri sana".
"Bibiane anataka kulipa kisasi, kwa hiyo
lazima watakuwa wanaelekea hapa baada
ya kuona tumetua kwa ndege, ongeza
ulinzi, nafikiri umebashiri sawasawa", Col.
Gatabazi alijibu.
Baada ya kuzungumza na Nkubana kwa
radio, Col. Gatabazi aliwafahamisha
wenzake kuhusu maelezo ya Nkubana.
"Huyu mtu ni hatari sana, lazima atakuwa
anaelekea hapa, nimeagiza ulinzi
uongezwe zaidi. Nia yake ni
kutuangamiza sisi kwani Bibiane atakuwa
amemweleza yote kuhusu uongozi wetu.
Naomba wote tuwe katika hadhari, huyu
mtu ananitia wasiwasi maana
anaonekana amepania ni mjuzi na
haogopi kitu. Watu wa aina hii ni hatari
sana", Col. Gatabazi alieleza.
"Hapa hawezi kuingia, ajaribu aone moto,
hii itasaidia kumkamata kirahisi maana
nyumba hii inalindwa na mitambo
maalumu ya kisasa, kuna kamera
zimetegwa eneo hili. Na tunaweza kuona
sehemu zote zinazoizunguka nyumba hii
kwa mara moja, kwenye chumba chetu
kuna vifaa vya kuangalia usalama wa
nyumba hii, kuna televisheni nne ambazo
zinaangalia mzunguko wa eneo hili kwa
umbali wa kilomita moja. Hii ina maana
hata sehemu ya upande huu wa kambi
tunaona. Halafu pale kambini kuna
mitambo kama hii, sijui imekuwaje
hawakuweza kumuona!", Kamanda Morris
alieleza kwa mshangao.
"Hebu twende kwenye hicho chumba
chako", Jean ambaye pia alianza
kuingiwa na hofu, alieleza. Wakaelekea
kwenye chumba cha mawasiliano na
usalama wa kambi hiyo.
Walipoingia ndani ya chumba hiki
waliwakuta askari kama sita hivi
waliokuwa wakisimamia kuendesha ile
mitambo ya ulinzi mle ndani. Wakiwa
ndani waliweza kuona picha za maeneo
yote yaliyozunguka ile nyumba,
waliwaona pia askari waliokuwa wakilinda
eneo hilo. Kwa kweli, kulikuwa na askari
wengi kila mahali wakiwa tayari
kupambana na adui kwa njia yoyote.
Kupitia mitambo hiyo waliweza kuwaona
askari wengine zaidi wakiongezeka na
kujipanga kwa ulinzi zaidi.
Kwa vile kambi hii inao komandoo zaidi
ya mia tano waliofuzu vizuri mafunzo yao,
hii ilimpa jeuri Jean na Col. Gatabazi
kuwa na imani kuwa hakuna adui
anayeweza kuleta rabsha mbele ya vijana
hao ambao pia walikuwa sehemu ya ulinzi
wakati huo.
"Kukitokea kitu chochote cha hatari, sisi
tutakuwa wa kwanza kukiona hata kabla
ya askari wa hapo nje hawajakiona.
Tumeweka taa kali za ulinzi ili eneo hili
lionekane kama mchana na kamera zetu
zichukue picha kwa ufasaha zaidi",
Kamanda Morris aliwaeleza na kufanya
wageni wake waridhike na maelezo hayo
na kuamini kuwa hakuna madhara.
"Lakini ikitokea bahati njema Willy Gamba
akamatwe, huyu atakuwa mfungwa
mikononi mwangu, msimuue tafadhari,
nileteeni hapa nimle nyama taratibu.
Nasisikia kuonja nyama yake", Jean
aliagiza.
"Na Bibiane?", Col. Gatabazi aliuliza huku
akimwangalia Jean.
"Huyu nitapenda kufanya naye mapenzi
kwa mara ya mwisho kabla hajaenda
ahera", Jean alijibu huku uso wake
ukionyesha uovu wa ajabu na mate
yakimjaa mdomoni.
"Huyu mtu ni mgonjwa", Col. Gatabazi
alijisemea moyoni.
"Tunaweza kuendelea na mkutano", Jean
aliagiza baada ya kujiridhisha na hali ya
usalama wa kambi, wakarudi kwenye
chumba cha mkutano walikokuwa
Kamanda Morris, Bizimaziki na
wataalamu wengine wa kijeshi
waliokodishwa, waliendelea kuwaeleza
jinsi mipango ya mashambulizi ilivyokuwa
imepangwa.
Meza moja ilikuwa na ramani ya nchi za
Zaire, Rwanda na Burundi na baadhi ya
nchi zote za maziwa makuu zikitumiwa
kuonyesha jinsi ambavyo jeshi la Akazu
lilivyojiandaa kusonga mbele katika
kuivamia Rwanda, wakitumia askari wa
miguu, magari ya kisasa ya kivita, vifaru,
makombora ya masafa mafupi na marefu
pamoja na ndege za kivita, yote ni
kuivamia nchi hiyo kijeshi.
 
asante mareche, thank you mkuu, tumalizie baba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…