RIWAYA: Sitaisahau Facebook

RIWAYA: Sitaisahau Facebook

Nilisubiri sana. Hadi pale ilipokuja taarifa kuwa baba amekutwa mtaroni. Hana jedraha lakini haijafahamika bado kama anapumua ama amekufa!!
Hii ilikuwa ni habari ya kushtua sana.
Mimi na mama tukakimbia kuelekea hospitali ambayo tulielezwa kuwa amelazwa.
Bahati mbaya zilikuwa mbio za kuwahi upepo.
Baba yangu hatukuwa naye tena!! Kifo cha utata. Hakuwa amelewa. Alikutwa na ile pesa niliyompa.


Hakika mimi sio Isabela, na kuna siri mzee wangu amekufa nayo!! Nilizungumza na nafsi yangu.
Jina langu ni nani sasa? Na kwa nini waliniita Isabela?



****



Ulikuwa msiba wa mtumaskini hata utata ungegubika vipi bado angezikwa na kusahaulika.Ndivyo ilivyokuwa kwa baba yangu.
Licha ya kifo chakekuwa na utata hapakuwa na la ziada alitakiwa kuzikwa.
Msiba huu ulivutawatu wengi kiasi kutokana na jina la mwalimu Nchimbi ambaye ni mamayangu. Mwalimu!! Hivyo wanafunzi walijaa sana.
Historia fupi yamarehemu ilisomwa.
"….marehemuameacha mjane na watoto wanne..mmoja wa kiume na watatu wakike….Sebastian John, Suzan John, na Helena John." Alimalizakutaja majina ya watoto wa marehemu.
Sauti za kugunazikatawala ghafla, watu wakawa wanaulizana hao watoto wanne mbonahawajatimia? Kina mama wakashindwa kumezea wakauliza palepale.
Ujumbe ukamfikiamsomaji baada ya kijana mmoja kuagizwa.
Msomaji akaanzakupekua hapa na pale. Kimya kikatanda!!!
"Anaitwa IsabelaJohn huyu hapa." Shangazi yangu alipaza sauti akanitambulisha ilikuondoa ile sintofahamu. Nikanyoosha mkono juu. Watu wakageuka nakunitambua.
Tendo lile la watukugeuka kuniangalia likanifanya nipatwe na aibu kidogo. Inakuwajemimi jina langu linasahaulika?
Sikuuliza!!!Nikauchuna.
"Kwa hiyo mtotowa nne ni Isabela John….samahani sana kwa mkanganyiko huu."Aliomba radhi yule msomaji. Waungwana hawakulalamika.
Alipotaka kuendeleakusoma yanayoendelea katika risala hiyo akawa anatawaliwa nakigugumizi. Hali hii sasa ikaanza kuwakera watu. Lakini kabla hilihalijapita akaanza kupiga chafya.
"Samahani!"akaomba radhi tena.
Haikukoma,ikaongezeka chafya ya pili, mara ya tatu ya nne, chjafya mfululizo.Akaachia lile karatasi lililoandikwa risala. Hali ikaonekana dhahirikuwa si nzuri!!
Akajikunja kunjahuku akionekana kuzitafuta pumzi zake. Mwili ukakosa muhimiliakaanguka chini.
Wale waliokuwa naghadhabu sasa ikawalazimu wakimbilie kutoa msaada. Msoma risalaakatulia akiwa amejishika kifuani. Akafanana na ile maiti ya babailiyopo katika jeneza.
Baadhi ya wanaumewakamchukua garini.
Tuliosaliatukaendelea na taratibu nyingine, hatimaye tukazika. Watu walikuwawanajiuliza kimemsibu nini yule bwana. Hakuna hata mmoja aliyewezakutoa majibu hata mimi pia nilikuwa katika sintofahamu.
Siku iliyofuataasubuhi na mapema la mgambo likalia. Msoma risala alikuwa amepotezamaisha!!!


*****


Suala la babakuondoka na siri kubwa aliyotakiwa kunieleza lilikuwa ni jambolililoutafuna sana mwili wangu. Nilikuwa najiuliza bila kufikiamuafaka.
Maisha yaliendelea.Chuo kilikuwa kimefungwa jijini mwanza na nilikuwa nina kumbukumbukuwa niliomba ruhusa maalumu kabla ya mitihani haijaanza. Hivyonilitakiwa sasa kufuatilia iwapo mtihani umekaribia ama la.
Nilitafakari nani wakumuuliza. Nikamkumbuka Maria. Nilijilazimisha kuamini kuwa yale yamimi kumuona katika pori nchini Zambia zilikuwa ni ndoto tu.
Nikajaribu kuvutakumbukumbu za wapi nimewahi kuhifadhi namba yake sikupata jawabu.Hilo nalo likawa tatizo.
Nikafikia uamuzi wakwenda katika huduma za internetcafé siombali sana kutoka nyumbani kwetu. Wakati huo sikuwa na nywelekichwani hivyo nilikuwa nimejitanda ushungi.
Nilifika kwa wakatimuafaka nikapata nafasi, nikatazama yaliyonipeleka kisha nikalipiahuduma ile.
Wakati nasimamaniweze kutoka nikagonganisha macho yangu na mtu ambaye niliamini kuwahaikuwa mara yetu ya kwanza kuonana. Alikuwa ni msichana mnene.Nikavuta kumbukumbu lakini sikulipata jina lake.
"Mambo…"nilimsalimia, akatabasamu kisha akanijibu.
"Ujue nilidhaninakufananisha. Nilikuangalia wakati unaingia ujue nikahisinimekufananisha."
"Na mimi hivyohivyo!!" nilimuunga mkono.
Tukasogea nje nakupiga stori za hapa na pale.
Wakati wa kuaganandipo tukakumbuka kuulizana majina.
"Naitwa Isabela."
"Mh!! Isabela!!Ulibadilisha jina ama..maana nakumbuka walikuwa wanakuita nanivilee." Alijaribu kuvuta kumbukumbu. Mimi nikawa namtazama tu!Nilibadilishaje jina sasa mimi.
"Hata sijabadilimbona." Nilimwelewesha. Akazidi kupinga.
Hatukufikiamakubaliano, akapigiwa simu akaniaga huku akisisitiza kuwanimemdanganya jina. Mimi sio Isabela.
Nilimsindikiza kwamacho hadi akatokomea. Nilijitazama iwapo nilifanana na mmoja kati yandugu zangu lakini hakuna niliyefanana naye ambaye ningeweza kumtupialawama kuwa watu wananifananisha naye.


*****

[FONT=Times New Roman, serif]Kile kitendo cha yule dada kuonekana kana kwamba amenifananisha kisha akakataa kuwa jina la Isabela si la kwangu nilikipuuzia na kumchukulia yule dada kuwa amepoteza kumbukumbu zake kwa kuwa miaka imepita mingi sana.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nilivyotoka pale moja kwa moja nikaenda nyumbani kwa dada Suzi kwani tangu nirejee Makambako sikuwa nimeenda kumsalimia mume wake na familia kwa ujumla zaidi ya kukutana msibani.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nilimkuta yupo nyumbani akiwa na familia yake jikoni wakiandaa chakula.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Alinipokea vyema tukasalimiana kisha nikataka kumsaidia kupika.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kuliko kunisaidia kupika ni heri unisaidie kumbeba huyu mwanao." Alizungumza huku akijitoa mtoto aliyekuwa amembeba mgongoni. Nikampokea na kumbeba.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Ghafla mtoto akaanza kulia taratibu kisha anaongeza kilio.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]He! Haka nako lini tena kameanza kuchagua watu?" Nilimuuliza dada. Hakunijibu zaidi ya kuguna akimaanisha kuwa huenda ni jambo la kawaida.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]We dogo wewe..mama yako mdogo huyo." Alisema akimaanisha kumweleza yule mtoto mdogo wa mwaka mmoja. Japo hakumuelewa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Mtoto akazidi kutoa kilio.[/FONT]


"[FONT=Times New Roman, serif]Hebu mchukue mwanao nadhani ana kisilani cha usingizi."[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nilimkabidhi dada Suzi mtoto wake, cha ajabu hakunyamaza zaidi ya kuongeza kulia. Sasa Suzi akashtuka na kulichukulia uzito hili suala ambalo mwanzo ulikuwa kama mzaha fulani hivi. Alimkagua mwanae kama amechubuka mahali. Hakuna kitu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Huenda basi ameumwa na mdudu, hata hilo pia halikuwepo!!![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Mapishi yakakoma kwa muda. Mtoto analia kwa sauti ya juu sana. Machozi yanamtoka kwa wingi mno. Hatari!![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Ilianza dakika moja na sasa zilikuwa zinatimia sitini, yaani saa zima bila kilio kukoma. Mtoto alikuwa analia sana.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Majirani wakakisikia kilio hicho kikuu wakajongea pale nyumbani kwa Suzi. Na wao pia wakashangaa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Suzi akajaribu kumpa titi mtoto aweze kunyonya, akalikataa. Kila mmoja alijaribu kumbeba bila mafanikio.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kimbilio lililofuata likawa hospitali. [/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Huko napo hapakuwa na nafuu yoyote. Madaktari walimfanyia uchunguzi na kurejea na majibu yasiyoridhisha hata kidogo. Walisema kuwa mtoto hakuwa na ugonjwa wowote ule. Hivyo hawakuwa na msaada wowote ule.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tulirejea nyumbani. Tulipofika huku kila aliyetazama tukio hili akiwa katika mfadhaiko wa hali ya juu na kuegemeza imani zao katika mambo ya kishirikina. Ni hapa na mimi nilijishtukia na kuanza kuamini kuna jambo. Na jambo lenyewe ni mimi!! [/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Niliamini kuwa ni mimi baada ya kuyakumbuka maneno ya yule mzee kule Iringa. Aliyeniambia nisipofuatilia jina langu basi nitasababisha majanga mengi sana popote nitakapokuwa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Usiku mzima mtoto alikuwa analia. Na kama hiyo haitoshi mara mkono wake wa kushoto ukaanza kujikunja. Suzi naye akawa analia sasa maana hakuwa na njia nyingine. [/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Baba wa mtoto alipigiwa simu akiwa safarini kuelekea Songea akalazimika kuhairisha safari, mama yetu alikuwa hapo nyumbani pia.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Suzi alikuwa amelia sana na alikuwa amewaacha walokole wenzake wakimwombea kwa namna zote mtoto yule. Lakini hali iliendelea kuwa tete.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Mtoto huyu akifa itakuwa juu yangu!! Niliwaza na kufikia maamuzi.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Dada Suzi alikuwa mtu pekee ambaye angeweza kunisaidia katika hili. Maana tayari tulikuwa tunamtambua kuwa alikuwa mwanamke wa kipekee aliyeweza kuhifadhi siri nzito nzito.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Huenda hata siri aliyokufa nayo baba nayo angeweza kuwa nayo!! Nikarusha karata yangu.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nikamfuata dada Suzi nje alipokuwa amekaa chini ya mti akilia kwa juhudi zote.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Da Suzi." Nilimuita, akageuka akanitazama na macho yake mekundu yaliyovimba kutokana na kulia kwa muda mrefu.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Nahitaji kuzungumza nawe dada."[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Alinitazama tena bila kusema lolote.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kuna jambo nahisi…."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Nini?"[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Naweza kuwa najua chanzo cha tatizo hili."[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Suzi akageuka mzima mzima akanitazama kwa umakini kabisa akisubiri niseme neno.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Sikuwa na haja ya kumueleza kuwa ile ninayotaka kumwambia ni siri, nilikuwa namuamini sana.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Suzi…" nilianza kumuelezea kwa kirefu na mapana juu ya maisha niliyopitia, nikamueleza juu ya ile mimba ya maajabu ambayo mwisho wake ulikuja baada ya kukatwa ile alama ya 666 katika makalio yangu, nilimueleza pia juu ya Dokta Davis na pesa zake haramu, ndoto za maajabu zote pia nilimsimulia.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Dada Suzi alinisikiliza vyema sana nilipokuwa namueleza juu ya makaburi ya Kiyeyeu huko Iringa na jinsi nilivyokutana na babu nisiyemfahamu aliyenieleza kuwa jina la Isabela sio jina langu. Natakiwa kulitafuta jina langu.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Alishangazwa na kukwama kwa basi letu hadi pale niliposhuka mimi, kifo cha mwanaume aliyekuwa anasoma risala ya marehemu baba pia alishangaa nilivyomweleza kuwa yawezekana ni moja ya majanga niliyoyasababisha.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Hata baba alikuwa ameniahidi kunieleza jambo fulani lakini ajabu kabla hajaweza kunieleza ametutoka. Nahisi ni yaleyale. Najua dada yangu hauamini mambo haya lakini niamini mdogo wako."[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nilimsisitizia na ili kumfanya aamini tuliingia ndani nikamfunulia kovu langu. Hapo sasa aliweza kuniamini.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kwa hiyo mwanangu anaweza kufa pia." Aliniuliza kwa wasiwasi.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Sijui nisemeje lakini kiukweli naogopa sana…" nilimjibu.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Sasa Bela mimi nafanyaje hapa katika hili."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Dada kama unaweza kujua lolote lile kuhusiana na mimi tafadhali nieleze tumuokoe mtoto. Hana makosa hata kidogo." Nilimsihi Suzi. Kilio cha mtoto kilikuwa juu kama kilivyoanza na alikuwa anazidi kujikunja mkono.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Suzi alinitazama usoni kama anayesoma kitu fulani kwangu.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Bela…yapo baadhi ninayoyajua….nitakueleza, sio kwa imani za kishirikina hapana!! Nakueleza kwa kuwa ni lazima uyajue. Kama mwenyezi Mungu amenipa pigo hili ili nikueleze siri hii basi nakueleza. Lakini jitahidi kuwa na moyo mgumu." Nilianza kutetemeka kwa maneno hayo ya dada, hakika nilikuwa namuheshimu kwa kuwa na siri nzito nzito.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kabla ya kunieleza aliniongoza katika sala. Nikamfuatisha hadi alipomaliza.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Sasa uwanja ukawa wake nami nikawa katika zamu ya kusikiliza.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Siri hii hata aliyenieleza hajui kama alinieleza."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kivipi?"[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Mzee alikuwa amelewa siku hiyo. Na pesa ya kulewa nilimpa mimi. Baada ya kulewa akawa anasemezana nami kwa njia kama ya kupitiwa ama hajui anazungumza na nani."[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nikakubali kwa njia ya kichwa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Suzi alinielezea juu ya upendo wa baba kwa mama yangu ulivyomlazimisha kufanya jambo hili la ajabu. Tendo la kuiba mtoto na kumpatia mama bila yeye kujua.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Aliiba mtoto…kivipi?"[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Baada ya mimi kuzaliwa mama alizaa mtoto mwingine, akafariki dunia akiwa tumboni. Siku chache kabla ya kuzaliwa. Baada ya hapo akashika mimba nyingine tena. Alipojifungua tu mtoto akafariki tena." Alinieleza dada Suzi, taarifa ile ya pili ikanisisimua kuliko ile ya kwanza, maana nilikuwa naifahamu hiyo kuwa iliwahi kutokea. Hii ya pili sikuwa naifahamu.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Baba akazungumza na manesi, akawapatia pesa nyingi ambazo ziliwafanya wasahau wajibu wao. Wakakiuka maadili wakaiba mtoto na kumpelekea mama halafu yule mtoto aliyekufa akapelekwa wanapojua wao."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kwa hiyo mama alipozinduka?"[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Akajikuta ana mtoto wa kike….akaamini ni mtoto wake wa kumzaa."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kwa hiyo mama anajua kuwa hayo yalitokea?" niliuliza kwa hamaki.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Si yeye wala ndugu mwingine anayefahamu jambo hili. Kama nilivyokwambia hata mimi baba alinieleza akiwa amelewa."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Sasa huyo mtoto mwingine yupo wapi sasa hivi? Na anaitwa nani jamani"[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Ndiye huyu mbele yangu, anaitwa Isabela." [/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Nilipiga yowe la mshtuko!! Suzi akawahi kuniziba mdogo na kunikanya kuwa niwe mtulivu kama kweli nimeamua kuichukua siri hiyo. Nikajilazimisha kutulia.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Isabela…wewe sio mtoto wa familia hii ya mwalimu Nchimbi, mimi sio dada yako wa damu, mwalimu sio mama yako na hata marehemu pia hakuwa baba yako." Alisema Suzi huku akiwa amenitazama usoni moja kwa moja. Nikashtushwa na kauli hiyo. Nilitegemea kuwa Suzi atabadili kauli hiyo huenda amesema kimakosa, lakini hakubadili.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Mapigo ya moyo yakaenda kasi sana!! Nikatamani ile iwe filamu na itamalizika baada ya muda fulani. Lakini hali ikaendelea kuwa kama ilivyo.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Dada Suzi, kwahiyo mimi…eeh!" nilikuwa nimepagawa.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Hiyo ndiyo siri Isabela. Haya! Je, inahusika kwa namna yoyote na tatizo la mwanangu???"[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Dada yawezekana kweli yahusika sana. Kwa maana hiyo mimi sio Isabela. Hili jina alinipa nani sasa?"[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Baba na mama….namaanisha mwalimu Nchimbi na marehemu mume wake."[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Basi mimi sio Isabela. Mama yangu na baba yangu watakuwa wapi Mungu wangu!!" nilijiuliza huku nikijikuna kichwa changu pasipo kuwashwa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Wakati najikuna kichwani zikarejea zile kumbukumbu za kudekezwa sana na mwanamke huyu ambaye sasa naambiwa kuwa sio mama yangu. Upendo wa dhati alionionyesha tangu nikiwa mdogo ulizidi kunifanya kimya kimya nipingane na kauli za dada yangu. Lakini ule uwezo wa dada kutunza siri ulinirejesha kuamini kuwa ule ni ukweli.[/FONT]
"[FONT=Times New Roman, serif]Kwa hiyo inakuwaje?" Alinishtua Suzi na kunifanya nikumbuke kuwa tulikuwa na tatizo.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Natakiwa kulipata jina langu na ukoo wangu!! Nilimwambia Suzi.

[/FONT]



I T A E N D E L E A




culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korinoSukula aniceth mzahula Khantwe kelcie Meljons
 
Ukiwa unatucheleweshea itabd utoe fain kwa kutuwekea mbili casuist umeskia?
 
Iko poa, ngoja tusubiri kujua jina halisi la Isabela, a.k.a bella
 
*****


Kama ilivyokuwa kwangu ndivyo ilivyomuwia mwalimu Nchimbi ugumu sana kuweza kuamini alichokuwa anaelezwa na dada Suzi. Almanusura azimie kama zisingekuwa jitihada za dada Suzi kulegeza maneno makali na kuyafanya laini.
Hatimaye mama aliyekuwa mbishi kipindi chote cha mazungumzo alikubali kwa shingo upande kuwa mimi sio mwanaye.
Kwa kuokoa maisha ya mtoto wa dada Suzi ambaye alikuwa analia mfululizo tuliamua kwa pamoja kushirikiana kulitatua tatizo hili.
Hospitali!! Hapa ndio tulianzia kumtafuta mama yangu. Ilikuwa hospitali ya serikali nani miaka mingi sana ilikuwa imepita. Kila kitu kilikuwa kimebadilika, hakuwepo wa kuweza kutusikiliza na kutusaidia.
Mtoto akiwa amebaki nyumbani, sisi tukiwa katika hekaheka hizi ndipo mama alipokuja nawazo la kumwendea mkunga ambaye alimzalisha. Mama alikiri kumkumbuka mama huyo ambaye ni mstaafu tayari.
Hakuna aliyelalamika kuhusu kuchoka. Tulitembea kwa miguu. Tulipofika maeneo ambayo mama alihisi kuwa ndipo anaishi yule mkunga tulianza kuulizia. Ilituchukua muda mfupi tu kuweza kuyapata makazi yake.
"Ameenda sokoni lakini atarudi muda si mrefu." Msichana tuliyemkuta pale nyumbani alitujibu.
Tukajiweka katika mkeka tulioukuta pale nje na kumsubiri.
Kama tulivyoelezwa mama huyo mkongwe kiasi alifika, kwa kumtazama alionyesha kuwa ujanani alikuwa mrembo sana lakini mwenye maringo.
Licha ya uzee huo bado alikuwa na maringo kiasi katika sauti yake.
Alitukaribisha huku akiwa amesimama kwa namna ya kutusikiliza shida yetu ni ipi.
Kila mmoja akamwachia mama jukumu la kuzungumza.
"Naitwa mama Isabela au …" kabla hajamaliza kujitambulisha ilisikika sauti kutokea dirishani, "Shikamoo mwalimu!!"
"He! We ni nani tena unanisalimia umejificha…?" alisema mama kwa kitetemeshi cha ualimu.
Yule mkunga akasaidiana nasi kutazama mlangoni. Akatoka msichana kwa makisio ni umri wa miaka kumi na moja.
Akamsalimia mama kwakupiga magoti.
Kabla ya kujibu mama akaanza kuvuta kumbukumbu.
"Eliza….nimekosea!!!"alimkumbuk a jina lake kwa usahihi.
"Mjukuu wangu huyu, kumbe ni mwanafunzi wako." Yule mkunga aliyekuwa amesimama akasema huku sasa akikaa. Mwanafunzi yule akawa ameujenga urafiki kati yetu.
Tukakaribishwa ndani!!!
Baada ya utambulisho mama alianza kujielezea juu ya jambo lililotuleta. Alianzia mbali sana hadi akalifikia lengo letu.
Mama yule kwanza,alishtushwa na taarifa hiyo kisha akasema kuwa hajui lolote kuhusu tukio hilo.
"Kwa hiyo una uhakika kuwa nilizaa mtoto na akawa hai?" mama alimuuliza akiwa amemkazia macho. Mkunga akawahi kukwepesha macho yake, nikamsoma nakugundua anatudanganya.
"Sikumbuki..ujue nimewazalisha akina mama wengi sana…hakika sikumbuki." Alijitetea huku akiwa na hofu.
Aliusimamia uongo wake huo hadi pale nilipoamua kuyaingilia mazungumzo haya, hasira ilikuwa imeanza kunitawala.
Nikarusha karata yangu!!!
"Mama mimi nadhani nimpigie simu yule baba aliyeshuhudia tukio hili, najua nikimpigia atakuja na yule askari. Kwa hiyo tutaufahamu ukweli."
Yule mama akatowa yowe la hofu huku akizungumza kikabila cha kwao, hakika alitaharuki kusikia polisi.
"Mwanangu…usipigesimu subiri tunayazungumza haya yanaisha."
Uwanja ukawa wake akazungumza.
Kama dada Suzi alivyosimuliwa na marehemu baba juu ya uwepo wangu katika familia ile ndivyo ilivyokuwa kwa nesi huyu ambaye mara kwa mara alitusihi tuyamalize kindugu.
"Na mama yangu ni yupi?" nilimuuliza ghafla akashangaa.
"Sikuelewi unaniuliza mimi au?"
"Ndio nakuuliza wewe…..mimi ni huyo mtoto aliyeibiwa."
Akakodoa macho yake kwa hofu. Nikaiskia hasira ikinichemka sana nikatamani kumrukia.
"Kwakweli mimi sijui labda Gloria ndio atakuwa anafahamu."
"Gloria ndionani?" mama alimuuliza.
"Tulikuwanaye..huyo ndiye aliyenishawishi.




*****

Hatukupoteza muda, tulimpa nafasi kidogo ya kujiandaa tukaondoka kuelekea kwa huyo aliyemuita Gloria. Haikuwa safari ndefu sana, tulitumia taksi.
Na yeye tulimkuta vilevile akiwa yupo katika uzee.
Baada ya salamu mbili tatu. Moja kwa moja ikawa zamu ya yule nesi kumueleza mwenzake juu ya tukio la miaka zaidi ya ishirini iliyopita.
Kama ilivyokuwa wakati tunamueleza na yeye alileta ujanja wa kutaka kumruka mwenzake lakini alipothibitishiwa kuwa akileta udanganyifu yupo shahidi na polisi pia. Naye akanywea!
"Tunachohitaji kujua ni kitu kimoja tu!! Mama aliyeibiwa mtoto ni nani." Nilikoroma kwa hasira. Suzi na mama wakawa wakimya.
"Ni Dina….Dina yule….."
"Dina ni nani na anakaa wapi."
"Dina ni kichaa…eeh! Mungu nisamehe mimi nisamehe…" alianza kulia yule mwanamke." Hakuna aliyembembeleza.
Neno lake la kuwa Dina ni kichaa liliniacha njia panda, ina maana mama yangu ni kichaa na anaitwa Dina? Hapana haiwezi kuwa!!! Nilipinga kimya kimya.


I T A E N D E L E A

culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korinoSukula aniceth mzahula Khantwe kelcie Meljons
 
Hahaha..inatia huzuni kidogo..kidogo hofu..ni hofu kutaka kujua isabelaa ni mtoto wa nan dahh
 
Back
Top Bottom