RIWAYA: Sitaisahau Facebook

RIWAYA: Sitaisahau Facebook

Au Ndio gari ililipuka na Isabella kafa? Mana kimya kingi
 
SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John




SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA


Mayowe yakatawala, akinamama wakiwa wamesahau watoto wao na wanaume nao wakiwasahau wake zao sasa kila mmoja alikuwa akiipigania nafsi yake. Sikuwa katika umoja na akina Jesca tena! Hapa sasa kila mwenye macho hakungoja kuambiwa tazama!!
Makaburi yale mawili yaliendelea kufuka ule moshi wa rangi ya dhahabu.
Wenyeji wa kijiji kile walikuwa katika taharuki kubwa sana huku wakizungumzia juu ya kukasirika kwa mizimu.
Nani sasa aliyeikasirisha? Walijiuliza.
Vilio vilisikika tena kutokea gizani. Watu wakakimbilia huko. Waliporejea ilikuwa taarifa ya mama mmoja aliyekuwa anakimbia ameshambuliwa na kitu kisichofahamika na hatamaniki tena. Amekufa!!
Hali ikatulia kwa muda. Akajitokeza mzee mmoja wa makamo akitembea kwa kutumia mkongojo.
Huyu hakuogopeshwa hata kidogo na hali iliyokuwa inaendelea. Alisimama mbele ya kunndi na kuanza kusema anachokifahamu, alielezea historia fupi ya makaburi ya Kiyeyeu na majanga yanayotokea iwapo wazee wale waliolala katika makaburi yale wakikerwa na jambo. Hapa sasa akafikia kusema kuwa kuna mtu mmoja katika msafara alikuwa ameikasilisha mizimu!!
Ni lazima abaki ili kuwanusuru wenzake. Kama akiendelea mbele basi litatokea balaa kubwa zaidi ya hili. Alizungumza kwa sauti ya juu na kila mmoja aliweza kusikia. Sauti yake na umri wake vilikuwa vitu viwili tofauti!!
"Hivyo kama unajua una lolote la kuikera mizimu hii ni heri ubaki nyuma kuwanusuru wenzako." Alizungumza kisha akatuachia mtihani wa kuamua aidha kujitokeza ama la!
Maneno yake niliamini kabisa yalikuwa yanamlenga John. Nilijisikia uchungu sana, John alitakiwa kubaki nyuma. Yaani harakati zangu zote hizo zinaishia hapa!! Niliumia sana.
Niliangaza huku na huko. Sikumuona John!! Nilitaka kumuita lakini niliamini kuwa hawezi kunisikia.
Kimya kilitawala akisubiriwa mtu huyo ambaye ameikera mizimu aweze kujitoa kundini. Hakuna aliyejitokeza.
Mzee akaendelea kusubiri!! Bado hakujitokeza mtu yeyote.
Kimya kilikatishwa na sauti ya mwanaume akipiga mayowe. Tukageuka nyuma kumtazama. Alikuwa amejishika shingo yake huku akipiga kelele. Mara damu zikaanza kumtoka puani, masikioni na mdomoni. Badala ya kumsaidia kila mtu akawa anamuogopa!!
Hatimaye akaanguka na kutulia tuli! Alikuwa amekata roho!!


Kina mama wakapiga kelele sana, wanaume wakabaki kushangaa.
Yule mzee wa kimila akaipaza tena sauti yake, "Kama asipojitokeza mtu huyu majanga yataongezeka. Mizimu inakasirika."
Sasa watu wakaanza kusemezana huku wakisisitizana kuwa mtu huyu ajitokeze ili mizimu itulie. Bado hakuweza kujitokeza mtu yeyote.
Zikaanza kutolewa hirizi miilini mwa watu, lakini yule mzee wa kimila akapinga kuwa hizo ndio tatizo.
Waliokuwa na dawa za kienyeji wakatoa. Bado haikuwa tiba.
Kiza kinene kikatanda kama dalili ya mvua. Mwanga mkali ukamulika bila kutoa kelele. Watu watatu wakasalimia na ardhi.
Ilikuwa radi!! Na walikuwa maiti tayari.
Roho ikaniuma sana, nikajiona mimi ndiye muhusika. Nikatamani John atokezee nimtangaze kuwa ndiye chanzo. Lakini John hakuwepo tena!!


Vile vifo vya radi ya ghafla vilimshtua kidogo yule mzee.
Mara akabadilika sura na kuwa kama aliyekasirika!!
Akatoa amri ya watu kujipanga msitari. Amri ikasikilizwa. Wanaume na wanawake mstari mmoja, mistari ilipopangwa ndipo nilimuona John. Na yeye alikuwa amepanga mstari. Akaanza kupita na kufanya kile anachokijua mwenyewe. Alimfikia John, na yeye akamuona akamshika mkono. Ina maana John anaonekana? Nilijiuliza.
Nikiwa katika hali ya mashaka ya kila kinachoendelea. Mara yule mzee mkongwe alinifikia, alikuwa anatabasamu, mgongo wake uliopinda ulimfanya awe ameinama na kuwa mfupi sana!!
"Shkamoo babu." Nilimsalimia.
"Marahaba mjukuu wangu." Alinijibu kwa ukarimu sana.
Kisha akanishika mkono.
Alipofanya hivyo kwa wasafiri wengine hakutumia muda mrefu, lakini kwangu ni kama alitumia sekunde nyingi.
"Unaitwa nani binti."
"Isabela!!"
"Nani alikwambia unaitwa Isabela." Aliniuliza huku akinitazama usoni.
"Naitwa Isabela mzee." Nilitaharuki kutokana na maswali ya mzee huyu.
"Hilo sio jina lako binti."
"Sio jina langu?"
"Na litakugharimu sana na kuwaumikza wengine katika maisha yako." Kauli nzito za mzee huyu zilinishangaza.
Isabela sio jina langu? Ni miaka zaidi ya ishirini tangu nipewe jina hilo. Sasa leo ananiambia kuwa hilo sio jina langu? Maajabu haya.
"Hautaendelea na safari hii…kuwaepusha wenzako na mabalaa yasiyowahusu." Alininong'oneza. Nikahisi ubaridi ukinipenya mwilini, mapigo ya moyo yakapungua kasi. Nikakata tamaa.
Mimi tena? Sio John!! Maajabu haya.
"Kama unao upendo waruhusu wenzako waende zao. Janga lako haliwahusu hata kidogo." Alinisihi. Nikatikisa kichwa kukubali. Huku nikiamini kwa asilimia kadhaa kuwa tatizo ni John na yule mzee hajui kitu.
Mzee akawatangazia watu kuwa tatizo limekwisha. Na kweli nilipokubali tu waondoke zao. Nilipogeuka makaburini. Ule ukungu haukuwepo tena.
Abiria wakaingia katika basi lile la ziada lililokuja kutuchukua.
Tofauti na mawazo yangu. Kuwa John atazuia basi lisiondoke baada ya yeye pia kuwa mmoja kati ya abiria. Haikuwa hivyo. Basi liliwaka vyema. Na kutoweka!!
Ilikuwa usiku mnene lakini kinyume na taratibu za usafiri Tanzania, basi lile lilisafiri usiku. Hayakusikika malalamiko ya kubanana tena. Kila mmoja alitaka kutoweka eneo lile. Hata madereva na makondakta wote walikuwa waoga.
Nilibaki na yule babu!!! Akina Samson, Jesca, na Jenipher walitaka kubaki na mimi lakini kwa maneno ya yule babu kuwa mzigo wangu hauwahusu. Niliwaruhusu waende zao huku nikiwapatia pesa nyingine ya ziada.
"Nendeni mkautangaze ushuhuda huu popote pale. Msifiche hata moja lililotokea. Hata kama sitafika huko mtakapokuwa. Naamini sisi ni washindi." Niliwaeleza. Wakalia kwa uchungu. Samson akagoma kabisa kuondoka lakini hatimaye alikubali kuondoka.


Nilibaki na mzee yule tukizungumza. Alinieleza juu ya jina langu. Akadai kuwa hakuwa akijua nilikuwa naitwa nani lakini Isabela halikuwa jina langu.
"Rejea nyumbani ukalitafute jina lako. Jina lako limepotea ama limefichwa. Na ukiendelea kuamini kuwa wewe ni Isabela basi maisha yako yatakuwa ya tabu sana. Utawatesa wenzako nawe utateseka sana." Alinieleza yule babu.
"Unaweza kwenda kupumzika nyumbani kwangu. Kesho upatafute nyumbani kwenu. Ukalitafute jina lako."
Tuliongozana na yule mzee hadi nyumbani kwake. Hapo tulipokelewa na mbwa wengi sana waliomlaki bwana huyu kwa furaha.
Wahehe na mbwa!! Niliwaza.




******


Nililala katika mkeka. Ni kama nililala kwa sekunde kadhaa hatimaye pakapambazuka.
Mzee akaniamsha, akanisihi sana nihakikishe Napata jina langu halisi na hapo nitaendelea na maisha yangu vizuri.
"Jina langu ni nani?" nilijiuliza kwa sauti akanisikia.
"|Hata mimi silijui lakini ni lazima ulipate ili kuzikwepa laana za ukoo wako. Fuatilia historia yako vyema mwanzo hadi mwisho. Historia ya kweli ipo kwa mama…kamuulize mama yako. Wewe ni nani? Lakini nakukumbusha kuwa wewe sio Isabela"
Mzee alinisindikiza hadi njia ya mabasi.
"Usizungumze na mtu yeyote, kwa usalama wako na abiria wenzako." Alifanya kunisemesha kwa sauti hafifu. Nikamsikia na kumwelewa.


Basi likapita. Nikapanda!! Mzee alinilipia nauli huku akichukua fursa ya kuzungumza na kondakta.
Safari ya kurejea Makambako. Safari ya kwenda kulitafuta jina langu. Jina lililopotea.
Kaka aliyekuwa pembeni yangu alikuwa anaongea maneno mengi sana. Lakini sikuwa namjibu chochote.
Hatimaye tukaifikia Makambako!! Nikashuka garini nikaikanyaga ardhi ya Makambako kwa huzuni sana!! Hatua kwa hatua nikaanza kuelekea nyumbani.


*****
Mwanamke wa makamo ambaye sasa mvi zilikikaribia kichwa chake chote alikuwa anafagia uwanja. Alikuwa akiimba nyimbo anazozijua yeye huku akionekana kuzifurahia. Nilimtazama kwa makini. Nikatamani ningekuwa nimekuja kwa mazuri huenda ningemshtua kisha tukacheka wote. Lakini nilikuwa nimekuja kwa mengine magumu sana.
Huyu alikuwa ni mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi.


Nikanyemelea. Akashtuka akageuka.
"Belaaa….Belaaa mwanangu." Akautupa ufagio, akanikimbilia, akanikumbatia kwa nguvu. Joto lake likaupenya mwili wangu ulio dfhaifu. Nikaamini kuwa nilikuwa nimemkumbuka sana. Chozi likanitoka. Nikamkumbatia kwa nguvu zaidi.


"Karibu mwanangu…mbaya wewe..yaani kimya kimya au uliongea na Suzi..wabaya sana nyie." Alilalamika nikajilazimisha kutabasamu.
Tuliingia ndani. Tukafanya mazungumzo ya hapa na pale. Hadi tulipokatishwa na nyimbo nyingine kutoka kwa mlevi. Huyu alikuwa baba yangu mzazi. Asubuhi sana alikuwa anatokea kilabuni.
Sijui alilala huko? Nilimuuliza mama./
"Hamna sema ameamkia huko."
"We Helena wewe…Aaah!! Suzy..inaq maana haunioni uje kunipokea…si ku hizi hamsalimii watu!!" alizungumza kilevi. Macho yake hayakumwezesha kujua iwapo mimi ni Isabela.
Akapita akiacha nyuma harufu ya pombe kali. Akaingia chumbani.
Baada ya kelele za hapa na pale akasikika akikoroma!!!


Nilijikaza sana na sasa nikaamua kumueleza mama kilichonileta pale nyumbani.
"Mama hivi hili jina la Isabela ni nani alinitungia."
"Mbona wauliza hivyo mwanangu."
"Nipe jibu mama..ama ukoo wangu ni upi."
"We mtoto umekuwaje lakini."
"Nijibu mama."
"Mbona kila kitu kipo wazi..ukoo wako ni huu wa baba yako, na jina hilo ni mimi na baba yako tulikupatia." Alinijibu.
Niliondoka sebuleni nikaenda chumba cha wasichana nikajinyoosha. Nikapitiwa na na usingizi.


Nilikuja kushtuka nikiwa na njaa kali.
Nikaliendea jiko.
Nikajihudumia vilivyokuwepo, kisha nikareje chumbani.
Majibu ya mama yalikuwa hayajaniridhisha hata kidogo.
Nitamuuliza baba pia!! Huenda kuna kitu anajua.
Kwa nini aliniita Isabela.
Nikasinzia huku nikiwa nimejiahidi hivyo kichwani mwangu.


*****


Asubuhi na mapema nilikuwa wa kwanza kuamka. Nilihitaji kumuwahi baba akiwa katika akili zake vyema kabisa.
Kabla hajalewa!!
Niliwahi na kujifanya naosha vyombo.
Hatimaye nikasikia mlango wa chumbani unafunguliwa. Baba akatoka.
"Aaah!! Bela mwanangu…lini tena umetuvamia wewe…umemaliza mitihani lakini."
"Nimemaliza..shkamoo baba…."
`aliijibu salamu. Tukabadilishana mawazo na hatimaye kama kawaida yake akaniomba pesa.
"baba kabla ya hilo…nahitaji kukuuliza kitu."
Alinisikiliza kwa makini, nikamueleza kile nilichomueleza mama. Baba alionekana kushtushwa na habari hiyo. Alijaribu kujiweka sawa lakini nilikuwa nimemsoma.
"Fanya hivi…nipatie hiyo pesa nikirejea tutaongea ni stori ndefu kidogo..si unataka kujua maana ya Isabela na kwanini tulikuita hivyo..nifanyie kwanza nienda kupata supu kidogo." Alijaribu kukwepesha mada.
Niliheshimu maamuzi yake. Nikaingia ndani nikarejea na pesa kidogo nikampatia. Akatoweka.
Moyoni nilipata matumaini makubwa sana!! Niliyaamini yale maneno ya yule mzee.
Sasa mimi ni nani kama sio Isabela? Na kuna siri gani inazunguka hapa. Nilijiuliza. Wa kunijibu alikuwa ni baba.


Nilisubiri sana. Hadi pale ilipokuja taarifa kuwa baba amekutwa mtaroni. Hana jedraha lakini haijafahamika bado kama anapumua ama amekufa!!
Hii ilikuwa ni habari ya kushtua sana.
Mimi na mama tukakimbia kuelekea hospitali ambayo tulielezwa kuwa amelazwa.
Bahati mbaya zilikuwa mbio za kuwahi upepo.
Baba yangu hatukuwa naye tena!! Kifo cha utata. Hakuwa amelewa. Alikutwa na ile pesa niliyompa.


Hakika mimi sio Isabela, na kuna siri mzee wangu amekufa nayo!! Nilizungumza na nafsi yangu.
Jina langu ni nani sasa? Na kwa nini waliniita Isabela?




***Najua wengi watafadhaishwa na hili……lakini hakuna jinsi lazima iwe hivi.
***ISABELA katika wakati mwingine mgumu…amehakikishiwa kuwa Isabela si jina lake. Na hicho ndio chanzo ncha matatizo.
***JINA lake hasa ni nani? Na kama baba amekufa na siri hiyo atafanya nini kujikomboa na kuwakomboa wengine???
***JOHN, BASU, DAVIS, OSMAN…nini hatma yao viumbe hawa???




Huku katika kitabu ikiunganishwa na simulizi ya SIRI SIRINI


……Isabela katika harakati endelevu zilizoanzia kwa Dokta Davis, zikakitesa chuo kikuu alichokuwa anasoma, zikahamia Zambia, zikarejea Tunduma, zikakwamia Iringa, zikamrejesha Makambako.
Isabela sio Isabela….Isabela anasaka jina lake…Isabela anausaka ukoo wake. Isabela anaisana Siri ambayo ipo ndani ya siri kubwa..hii ni siri sirini.


***JE MZEE WAKE AMEONDOKA NA SIRI GANI??? Nani mwingine wa kumfungulia siri hii.
SIRI SIRINI itakufanya ujenge uhusiano wa maisha halisi kabisa ya mwanadamu, katika ndoa na maisha ya kawaida ya familia. Siri za wandani zinavyoweza kuleta migogoro ambayo inaweza kuzaa maafa makubwa.




T A M A T I


Nyrum Mwadunda Ngoami Cyduu Excel Khantwe binti kiziwi showtie korino Nicas Mtei Angeliciousmunimuni Meljons aniceth mzahula Samaya
 
PONGEZI KWA EMMY

549586_461275077239177_2131927771_n.jpg
 
Haiajisha fresh, imeisha but imetuacha na maswali
 
PONGEZI KWA EMMY

549586_461275077239177_2131927771_n.jpg
Ayayayayaaaaaaaaa, aiseee nimempenda ghafla huyu Emmy! Karembo rembo kweli na mambo yake si haba, ngoja nimchumu kwanza, mwaaaaaaaa! Usisahau kuni-PM ID yake ya JF! Samahani King'asti wangu usipite huku!
 
Last edited by a moderator:
Lete lete hiyo sehemu ya mwisho, though nina swali moja sijui utaweza kunijibu coz wewe sio mtunzi. Mara ya mwisho Isabella alikuwa kwa Dr kwa ajili ya kutoa mimba, akakabidhiwa kwa mtu anaitwa RIP, RIP akamtembeza kwenye chumba cha maiti huku wakiwa wanaangalia maiti tofauti tofauti, hapo ndio napata shida kujua isabella alitoka vipi chumba cha maiti na hadi kujikuta yuko katika vita porini na hatimae walikuja kugundua wako Ndolla Zambia! Casuist!

Haiajisha fresh, imeisha but imetuacha na maswali

Anaweza akakujibu mwenyewe baadae/ siku nyingine...
 
Lete lete hiyo sehemu ya mwisho, though nina swali moja sijui utaweza kunijibu coz wewe sio mtunzi. Mara ya mwisho Isabella alikuwa kwa Dr kwa ajili ya kutoa mimba, akakabidhiwa kwa mtu anaitwa RIP, RIP akamtembeza kwenye chumba cha maiti huku wakiwa wanaangalia maiti tofauti tofauti, hapo ndio napata shida kujua isabella alitoka vipi chumba cha maiti na hadi kujikuta yuko katika vita porini na hatimae walikuja kugundua wako Ndolla Zambia! Casuist!

Sijui nimeelewa swali lako ila nnachokumbua Bela na RIP walipanga kwamba usiku waanze safari ya kwenda huko msituni
 
Last edited by a moderator:
SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John P.




SEHEMU YA KUMI NA TISA


R.I.P hakujali kama nilikuwa nimeshtuka ama la! Aliendelea kuongeaongea huku akiwatukana matusi mazito ya nguoni wale maiti kama vile wanamsikia. Hakika alifanana na mtu aliyerukwa akili. Kuishi na maiti napo kazi sana huenda ndo maana amechanganyikiwa.
“Ulisema unaitwa nani vile.”
“Naitwa Isabela.”
“He!! Unaitwa Isabela, yupo mwenzako humu hebu njoo umuone.” Akanivuta kwa kutumia nguvu sana hadi mkono ukashtuka. Yeye hakujali hayo. Akanivuta vuta hadi tukafikia kabati jingine. Nikajiandaa kushuhudia maluweluwe mengine.
“Hili nalo lilikuwa linakula nini sijui likanenepa hivi. Majitu mengine mapumbavu sana ujue. Heri yako wewe haujanenepa sana.” Alizungumza peke yake.
Akatumia mikono miwili akavuta. Likatoka bonge la mwanamke. R.I.P akaanza kucheka, kicheko kikubwa hadi akatoa machozi.
“Anaitwa Isabela huyu, mpumbavu sana huyu alienda kunenepeana huko. Amewasumbua sana siku ya kumleta humu ndani. Kuna vindugu vyake, vyembamba hivyo basi likawa linawaponyoka. Linaanguka puu!!” alisimulia huku anacheka. Mimi sikuwa namuelewa.
Kisha tukarejea tena mahali tulipokuwa nikalazimika kukaa juu ya lile jokofu la kuhifadhia maiti.
“Au nimlete Isabela make nae, Isabela bonge.” Aliniuliza. Mimi nikawa namshangaa. Yaani alikuwa kamna mpumbavu fulani.
“Isabela….umewahi kufa wewe?” aliniuliza.
Swali gani sasa hili la kijinga!! Nikawaza.
“Bado”
“Mwenzako niliwahi kufa. Na wewe una hamu ya kufa.”
He!! Umewahi kufa….kivipi.”
“Kwani mtu akifa anakuwaje?” aliniuliza, sikujibu.
Akaendelea, “hebu tuachane na hayo..msichana mdogo kama wewe ukifa sio vizuri ujue.”
“Kama ukiwa makini hautakufa. Tena wewe hautakufa, nitakusaidia usife sawa!!”
“Sawa!!” nilijibu kwa nidhamu kubwa.


“Njoo huku…”
Nikamfuata hadi mahali patulivu kabisa. Sasa hii ilikuwa ofisi kweli. R.I.P akanipokea. Akaniacha ofisini kwa muda, kisha akaingia tena baada ya dakika kadhaa.
Hakuwa yule tahira, hakuwa mchafumchafu kama nilivyokueleza mwanzoni. Huyu alikuwa na hadhi ya yule mvulana ninayemuhitaji. Alikuwa mtanashati.
Hakuwa akicheka hovyo! Alikuwa makini na mtaratibu.
Roho Iliyo Potea (R.I.P). Alianza kwa kujitambulisha jina lake halisi. Kisha akaniupongeza sana kwa ujasiri wangu hadi kufika hapo.
Akajieleza kwa ufupi maisha yake ya utafutaji huku na kule hadi alipojikuta akitafuta kwa njia za mashetani. Ni katika maelezo haya alinieleza juu ya namba 666. Nilishangazwa sana na maelezo yake lakini nilipiga moyo konde nikiamini tiba ipo.
Baadaye akanieleza jinsi alivyojitoa katika harakati hizo za kumtumikia shetani. Haikuwa njia rahisi. Aliwapoteza ndugu zake kadhaa lakini mwisho akawa amejikomboa.


"Hiyo chapa uliyopigwa lazima ifutwe! Ni njia hiyo tu ya kukukomboa kutoka ufalme huo. Wewe unamilikiwa na mtu kuna mtu wewe ni mtu wake..anakutumia anavyotaka" alinieleza kwa sauti iliyomaanisha msisitizo
Nilikuwa makini nikimsikiliza.!


USIKU MNENE


Safari ya kuelekea kuitoa ilea lama ilikuwa imewadia. Pesa taslimu milioni moja ilikuwa imenitoka tayari ili kufanikisha jambo hili.
Tulitumia usafiri wa gari binafsi. Tulikuwa watatu. Mimi, RIP na mwenzake ambaye sikuwa namjua jina. Yeye alikuwa anaendesha gari.


Sasa gari ilisimama. Tukashuka garini. Nilikuwa nimevaa upande wa kanga kama RIP alivyoniagiza. Tulitembea kwa muda hadi tukakifikia kichaka. Hapakuwa na vibuyu wala dawa za kienyeji lakini tulikuwa mbele ta kaburi, hilo kaburi lilikuwa likimsubiri mtu limmeza. Yaani lilikuwa wazi.
Mara akachomoa kisu, akachomoa na kisahani.
Nikaamuriwa kuvua nguo!! Nikavua. Nikawa uchi mbele ya wanaume hawa wawili. Sikuwa na aibu!!
R.I.P akatoa sindano akavuta dawa. Akanigeuza, nikageuka.
Akanidunga sindano. Hii ya sasa ilipenya. Nikaisikilizia maumivu yake kisha taratibu nikasikia mguu wangu wa kulia unakufa ganzi.
Kisu kikatwaliwa upesi. Ilikuwa saa sita kasoro dakika sita. Hii ni kwa mujibu wa RIP.
Sikujua kinachoendelea lakini nilipotazama chini niliona kitu kama maji vile. Ghafla ikasikika sauti. Sauti ya kike ikiniita kwa mbali. Sauti ile ilikuwa inanisihi sana nikimbie.
Nikimbie kwenda wapi sasa.
RIP na mwenzake walikuwa wameshikilia kile kisahani. Sasa niliweza kuona kipande cha nyama. 666 zilionekana zikiwa katika mng’aro wa dhahabu.
Nikiwa sijajua lolote linaloendelea. Mara ghafla ile sauti sasa iliweza kusogea zaidi na zaidi.
Hatimaye aliyekuwa anaita kwa juhudi zile nikamuona. Alikuwa ni Maria, yule rafiki yangu tunayeishi naye. Alikuwa yu uchi wa mnyama. Alikuwa akikimbia kwa juhudi zote lakini hakuwa akikimbia bure kuna kitu ama mtu alikuwa anamfukuza.
Nikajaribu kupiga kelele. RIP na mwenzake hawakunisikia.
Maria alikuwa anakimbizwa na nyoka. Nyoka mkubwa alikuwa anang’ara sana. Nashangaa wenzangu hakumuona.
Nikajikuta natimua mbio uchi. Na nilikuwa kitendo cha sekunde chache yule nyoka akavamia eneo lile. Sikushuhudia sana kilichowatokea wenzangu. Sasa nikaanza kuhangaika huku na huko katika pori hilo ambalo sikuwa nalifahamu.
Mguu mmoja ukiwa umekufa ganzi. Ningeweza vipi kukimbia mbio ndefu. Isabela mimi nikaanguka chini. Sasa nikawa najivuta kama nyoka. Nalia kama mtoto. Sikuwa na uelewa bado kwa nini mguu wangu ulikufa ganzi. Lakini kumbukumbu za kuchomwa sindano ile kali zilikuwa kichwani mwangu.
Nikiwa bado sijapata jibu sahihi. Lile joka la maajabu sasa likatokeza mbele yangu. Mdomoni likiwa na kipande cha nyama. Nyama ile yenye namba 666.
Nikajiinamia kwa uchungu. Nikafanya dua fupi. Nikajilaani kwqa kila hatua ya maisha yangu niliyopitia. Nikatamani ningekuwa na nguvu niweze kutimua mbio. Lakini tayari nilikuwa nimelegea. Macho yakazidi kuhesabu hatua za yule nyoka kunifikia. Sijawahi kuona nyoka mkubwqa kama huyu!!! Nakufa kwa kumezwa na nyoka. Inauma sana!!
Joka likazidi kusogea!! Joka kuu likawa linatambaa!!!


Kabla joka halijanifikia. Lilibadilisha uelekeo. Ni kama kuna kitu lilikuwa limehisi. Likaanza kutambaa kuelekea upande mwingine.
Joka linatoka mara sasa namuona John. John yule mpenzi wangu ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha pale chuoni.
“John…John!!” nilianza kumuita. Sauti ilikuwa imekauka. Haikutoka.
Joooooh!!! Nikajaribu tena, nikawa kama ninafanya mnong’ono. John akawa anaenda zake. Nikalia sana kuikosa nafasi hii hadimu ya kusikiwa na John!! Huenda angeweza kuwa msaada mkubwa kwangu.


Ubaridi ulipenya katika mwili wangu. Mwanzoni niliuhisi kuwa wa kawaida lakini baadaye nikahisi kama maumivu hivi. Nikajipapasa. Nilipoutazama mkono wangu ulikuwa na damu. Nikageuka kujitazama sehemu zangu za nyuma.
Maajabu!! Nilikuwa na kovu kubwa sana!! Na palikuwa pamechimbika. He! Ina maana nilikatwa nyama yangu ya…..!! niliduwaa.
Maumivu yakazidi. Na sasa giza likazidi kuchukua nafasi yake baada ya mbalamwezi kutoweka. Giza nene!! Hapo bado nilikuwa sijaweza kunyanyuka imara. Nikajaribu kujikunjua nisimame. Maumivu makali katika makalio. Nikaanguka kama mzigo. Nilipoanguka palikuwa na kisu kipya, kikiwa na damu.
Nikaendelea kulia. Sauti haitoki.!! Nilikuwa katika jaribio kuu maishani.


Ikiwa bado sijaweza kusimama. Lile joka lililopotea njia sasa lilionekana tena. Safari hii lilikuwa linakuja kwangu tena.
Bora nife!! Nilijiapiza. Sasa nikaanza kutambaa kumfuata huyo nyoka. Mkononi nikiwa na kisu ambacho nilikiokota, bila shaka ni kile kilichotumika kunikata nyama.
Nikawa natambaa kama joka lile linavyotambaa. Sikuwa naijua nia yangu. Lakini nilihisi ni vyema kufa kuliko mateso haya.


***ISABELA katika msitu asioujua. Kisu mkononi anataka kukabiliana na JOKA KUU la rangi ya dhahabu.
***RIP na mwezake wako wapi. Maria naye vipi huko msituni amefikaje?...JOHN? vipi naye kumbe hakufa ama!!


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe kelcie Meljons
ram kama nimekuelewa jibu la swali lako liko hapa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: ram
Sasa wapendwa wangu ram na Khantwe, ikiisha freshi mtanunuaje kitabu cha SIRI SIRINI?

I can't wait the final, Caustic unajua mkuu.

Loh!!! Jamani sasa mbona haijaisha vizuri?


Emmy kanipa softcopy ya kumalizia so inaisha yote na habari ya hardcopy alishaifanya kitambo na hamna tena,

Kesho tutaanza kumalizia...


Likes at least nijue kama bado tupo..

culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korinoSukula aniceth mzahula Khantwe kelcie Meljons
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom