RIWAYA: Sitaisahau Facebook

RIWAYA: Sitaisahau Facebook

Kaka nina kama siku mbili sjaingia humu c unajua tunatafuta ugari du noma saluti mkuu
 
SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John P




SEHEMU YA KUMI NA SABA


Haya yote niliyataka mwenyewe!! Sasa nikaanza kuhisi kuwa Davis hakuwa mtu mzuri kwangu!!
Davis ni MCHAWI!!!
Naenda kufanya mapenzi na mchawi!!
Ghafla nikaijiwa na kumbukumbuku za chapa ya shetani 666, niulipokumbuka hili nikakumbuka na mshahara wangu ulikuwa una hizi namba, hata simu ya Osmani nayo ina 666, Davis aliwahi kunitumia nauli nayo ilikuwa na 666 na sasa nipo katika chumba namba 66 namsubiri huyu mfalme wa 666
Hapana! Hapana! Niliipinga nafsi yangu. Na sasa nilikuwa nimeamua kumkimbia mchawi huyu. Kuikimbia chapa ya shetani!!!
Nikiwa najiandaa kukimbia
.Mlango ukafunguliwa!!!


NANI AMEUFUNGUA MLANGO!!!
JE ISABELA ATAIKIMBIA CHAPA HII 666.
Kama akiikimbia je ndo anaruhusu MAMA YAKE afe!! NANI KAMA MAMA???


ENDELEA


Nilipokishika kitasa ili kuufungua nitoke nikakumbwa na kihoro! Mlango ukafunguka kama vile ulikuwa katika kungojea amri yangu!!
Niliamini kabisa si muhudumu anayeweza kuingia katika chumba cha mteja bila ruhusa. Kwa hiyo kama sio muhudumu basi angekuwa Dokta.
Hakika. Alikuwa ni yeye! Nikatazamana naye ana kwa ana, akapiga hatua mbili akawa ameingia vyema ndani ya chumba. Akaufunga mlango.
Alitaka kuongea jambo lakini mlango ukagongwa tena, akasita kisha akaufungua! Alikuwa muhudumu.
"Barcadi, na Sprite!" aliagiza Davis bila kutoa malipo ya awali. Vinywaji alivyoagiza nilijua fika ni kwa ajili yangu na yeye!
Mlango ukafungwa tena.
Sasa aliufunga na funguo kisha akaziacha pale mlangoni zikining'inia.
Mimi nilikuwa wima mkoba begani nikitetemeka.
Davis akaliendea kochi kubwa hapo chumbani akaketi.
Kisha kwa ishara akaniita!
Naitwa na shetani! Nilihamaki. Nikasita kwenda.
"Hautaki?" aliuliza, sikumjibu!
Akaitwaa simu yake kubwa ya kisasa.
"Tabasamu kidogo nikupige picha Bela?" alinishawishi. Sikushawishika.
Alipochoka kunichekesha nisiyecheka akatoweka na kwenda bafuni. Nikabaki chumbani peke yangu! Hapo likanivamia ghafla wazo la kutoroka! Funguo zilikuwa mlangoni! Kwanini nisikimbie? Nilijiuliza. Hapo sasa ndipo nikagundua kwanini sina ubavu wa kukimbia. Huyu bwana alikuwa anahodhi maisha ya mama yangu! Mwalimu Nchimbi.
Nilipotambua hilo nikafadhaika. Nikakiendea kitanda nikajitupa, nikautupa na mkoba wangu!
Ilikuwa lazima nifanye mapenzi na Davis ili kuokoa maisha yake.
Nilifadhaika bila kujua nini la kufanya.
Mlango wa maliwatoni ukafunguliwa. Kichwa kilikuwa kizito hata kunyanyuka kushuhudia ni kimbwanga gani kipya atakizua Dokta huyu!
Akajikoholesha kama anayerekebisha koo. Nikaijua nia yake! Nikanyanyua kidogo! Macho wazi!! Yowe la uoga likanitoka kwa nilichokiona.
Hili lilikuwa kubwa kupita yote!
Kilichokuwa mbele yangu ni kiumbe kile kile kinachoitwa Davis.
Lakini sasa hakuwa na nguo. Maungo yake yote yakawa yananidhihaki, japo alikuwa mweusi tii. Lakini ule mwanga pale ndani uliniwezesha kutambua kuwa alikuwa amelowana damu katika viungo vyake vya uzazi, na hiyo damu ilikuwa mbichi na ni kama ilikuwa inaendelea kumtoka lakini ajabu haikuwa inadondoka katika marumaru!
Hapa sasa nilimsahau kwa muda mwalimu Nchimbi, nikauacha mkoba nikakimbilia mlangoni.
Ajabu! Ule funguo haukuwepo tena mahala pake!
Dokta akacheka sana huku akinifuata kwa hatua ndogo ndogo!
Nilitegemea huenda nitapoteza fahamu. Lakini hiyo haikutokea niliendelea kushuhudia kiumbe huyu akinifuata.
Nikawa narudi kinyumenyume hadi nikafika mwisho. Davis akazidi kunisogelea. Sasa alikuwa amenifikia!
Akanishika mkono! Kiganja chake kilikuwa cha baridi sana!! Akanitazama usoni, nami nikamtazama. Akaniachia kisha akasonya kwa dharau. Akakiendea kitanda akajirusha pale!
Bado mashuka hayakuchafuliwa na damu mbichi.
Hakika sikuwa tayari kufanya mapenzi na kiumbe kile cha ajabu!! Niliapa!
Muwasho ulianza kama wa kawaida tu katika chuchu yangu moja, nikajikuna, muwasho ukapita.Mara ile chuchu ya pili nayo ikawasha nikaikuna ikatulia.
Sasa zikawa zinawasha zote kwa pamoja, muwasho usiofanana na ule wa kumwagiwa -----. Huu ulikuwa wa tofauti. Nikatazama kitandani yule Dokta alikuwa amesinzia. Nikaitoa Sidiria yangu ili nijikune vizuri. Nikabaki bila nguo kwa juu. Nikafanya jitihada za kujikuna!! Ile hali ya kujikuna ikautwaa uoga wangu nikahamia katika hisia za raha! Raha ya kujipapasa! Mazito!
Ni heri ningekuwa na mikono mitatu huenda ningeweza kuipinga hali hii. Maana sasa kati kati ya mapaja muwasho ukazaliwa. Niache wapi? Nikune wapi? Nikajiuliza.
Raha ikawa karaha!
Nikaanza kulia huku nagalagala chini. Nilijikunja na kujikukunjua bila mafanikio!
Nilihitaji msaada wa hali ya juu! Msaada wa kukunwa!
Mara kama ameshtuka ndotoni yule kiumbe pale kitandani aligutuka. Akasimama akanitazama kisha akachuchumaa. Akanisogelea karibu zaidi. Sikuwa na nguvu mwilini.
Hakuwa na nguo nami sikuwa na nguo!
Kama vile alijua ninapowashwa! Akaanza kunikuna kwa namna ya kupapasa! Nikahisi raha ya kipekee ambayo sijawahi kuipata duniani. Bila kujitambua nikamkumbatia Dokta Davis.
Akaendelea kunikuna! Sasa nilikuwa hoi.
Fanya unalotaka! Ndivyo ningeweza kusema kama angeniuliza.
Lakini hakuniuliza!
Nikajikuta katika ulimwengu wa mahaba mazito!
Kama kukunwa hakika nilipata mkunaji! Muwasho ukatoweka kabisa. Jasho mwili mzima.
Nikapitiwa na usingizi kutokana na uchovu.


*****


Saa kumi na moja alfajiri hapakuwa na Dokta wala nguo zake pale ndani. Nilikuwa peke yangu.
Maumivu kifuani kama niliegemezewa gogo! Maumivu haya yakanikumbusha ndoto za kuota nazini na gogo!
Nikashtuka! Mbio mbio bafuni nikatapika!
Kumbukumbu ya kufanya mapenzi na Davis usiku uliopita ilinijia kichwani!
Yupo wapi sasa shetani yule? Nilijiuliza.
Ile hali ya maungo ya Davis kuwa na damu ilinisisimua na kujiona kuwa sina thamani tena ulimwenguni.
Kama sina thamani, bora nife! Niliamua!
Nitakufa vipi sasa? Hilo likawa swali la kujiuliza.
Nikayakumbuka maneno ya dada Suzi. Kuhusu utoaji mimba na madhara yake!
Nikafikia maamuzi ya kutoa mimba! Kisha nitajua nini cha kufanya!


Wakati natoka pale chumbani na kupita mapokezi nilikumbana na swali, "mwenzako bado yupo? Maana tunataka kufanya usafi". Mwenzangu? Mwenzangu nani? Wanamaamisha Dokta Davis.
Sikuwajibu nikajongea na kupotea eneo lile.
Nikaamua kurejea nyumbani kwangu. Tayari nilikuwa na taarifa kuwa mama anaendelea vizuri kiafya!


Tumbo! Tumbo! Tumbo lilianza ghafla kuniuma, upande wa kushoto!! Nililalamika sana, dereva wa teksi akaegesha pembeni akaniuliza kulikoni.
"Nipeleke hopitali!! Nipeleke nitakulipa" nilimsihi huku nikizidi kuugulia.
Kama nilivyoomba akaendesha hadi hospitali iliyokuwa jirani. Alikuwa ni kati ya masalia ya watu wakarimu waliobaki hapa duniani. Aliwahi kuwaita manesi. Japo walichelewa lakini walikuwa kunibeba kutoka ndani ya gari lile.
Moja kwa moja nikakimbizwa wodi ya wanawake!!
Nikapatiwa huduma ya kwanza!!
Baada ya muda damu ikaanza kunitoka!! Nilikuwa nimeingia katika siku zangu ama? Nilijiuliza bila kupata majibu!! Mjamzito naingia katika siku zangu!!
Kadri damu ilivyokuwa inavuja ndivyo maumivu yalizidi kupungua na hatimaye kuisha kabisa.
Majibu ya daktari yalikuwa kwamba. Ni tatizo la kawaida tu kwa mwanamke kuumwa tumbo akiwa anaingia katika siku zake. Lakini mimi nilikuwa mjamzito sasa!! Au mimba imetoka.
Sikutaka kuondoka na dukuduku. Nilimvuta daktari tukazungumza kinagaubaga.
Akafikia hatua ya kunipima ujauzito!!


Hakuchukua muda mrefu akarejea.
Alikuwa hajachangamka na ni kama alikuwa na jambo anahitaji kunieleza.
"Ina miezi miwili sasa!!." Alinieleza.
"Ni maajabu wewe kuingia katika siku zako!!" aliendelea. Mimi nikiwa msikilizaji.
"Kwa hiyo ni nini Dokta."
"Rudi baada ya siku saba. Kama ikiendelea hivyo. Ama la basi utakuwa mshtuko tu." Alimaliza.
Nikaondoka zangu huku nikiitazama dunia jinsi inavyonizomea.


****


Maria hakushangazwa na hali yangu ya kuvuja damu!! Aliamini ni kawaida tu kwa msichana. Hakujua kama nina mimba!!
Siri nikabaki nayo. Mimi na daktari!!
Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu….damu zinaendelea kuvuja tena bila kukoma!!!! Kazi ikawa ipo kwangu kila mara kubadili nguo zangu.
Siku ya nne, ya tano….bado tatizo likawa lile lile. Mateso sasa!!! Mimba gani hii!!!
Sikuingoja siku ya saba ifike. Nikarejea hospitali.
Daktari alinipokea vizuri. Nikampa kwa siri kiasi fulani cha pesa ili aweze kunihudumia kwa upendeleo.
"Hadi leo bado damu inakutoka?" alishangaa daktari. Nikamthibitishia kuwa bado zinatoka tena mfululizo.
Akakuna kichwa chake chenye mvi nyingi kasha akahamia kidevuni. Na penyewe akajikuna kwa muda.
"Hebu njoo…" akanipeleka katika chumba kingine. Akanipima tena mimba.
Daktari akashtuka!!!
"Kwa mara ya kwanza katika miaka yangu 20 ya kazi!!!" alihamaki.
"Nini? Nini dokta." Niliuliza.
"Wiki iliyopita ilikuwa na miezi mingapi vile."
"Mitatu ulisema."
"Sasa imefikaje miezi sita leo???" aliniuliza. Nikahisi kuzizima. Nikakaa chini!!!
Daktari naye alikuwa ana hofu!!


***ISABELA mtoto wa masikini anateseka!! Baada ya kufanya mapenzi na Davis Sasa anavuja damu.
***Nini kinamtokea msichana huyu…..
***Sasa MIMBA ina miezi sita…ndani ya wiki kadhaa….


NI KISA JUU YA KISA



culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe kelcie
 
Last edited by a moderator:
Casuist nilisema Isabela hawezi kubaliwa kuacha kazi, ukaahidi kunipa yote kama nitapatia. Sasa nipe yangu yote nijinafasi kwa blue mon hii. Huyu Davis ndiye gogo na john alishanyonywa damu siku nyingi.
 
Last edited by a moderator:
Casuist nilisema Isabela hawezi kubaliwa kuacha kazi, ukaahidi kunipa yote kama nitapatia. Sasa nipe yangu yote nijinafasi kwa blue mon hii. Huyu Davis ndiye gogo na john alishanyonywa damu siku nyingi.

Hahahaha, sikuona maana siisomagi nowdays.
Nilisema ntakutumia hadithi inayojitegemea mwanzo mwisho na sio hii...

Angalia PM muda c mrefu mkuu..
 
Hahahaha, sikuona maana siisomagi nowdays.
Nilisema ntakutumia hadithi inayojitegemea mwanzo mwisho na sio hii...

Angalia PM muda c mrefu mkuu..

Asante sana Mkuu, naisubiri kwa hamu.
 
Duh! Binti kila ukiua zinaingia 6,666,000 alama ya mpinga kristo, umeingia freemason bila kujua maskini
 
Pole Isabella, tamaa ya maisha mazuri imekupeleka pabaya
 
Mmh,jamani tamaa ni mbaya. Heri angeridhika na maisha yake tu...ona sasa aaaagrrrh anaangamia bure.
 
SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John P.




SEHEMU YA KUMI NA NANE


Ni kama daktari alikuwa haamini ambacho amekiona, katika mwili wangu na alichokuwa akifanya pale ni kunitoa tu katika hofu. Mabadiliko ya mimba yangu yalimfanya achanganyikiwe.
Tulirejea katika chumba chake cha ofisi. Mazungumzo yaliyokuwepo ni juu ya kuitoa mimba ile.
Daktari alikataa kata kata akidai kuwa mimba ikifikisha miezi sita na msichana akijaribu kuitoa basi lazima atapatwa na matatizo na kuna uwezekano wa kufa.
Maelekezo ya daktari yaliyoambatanishwa na neno KUFA yalinipa ahueni ya nafsi kwa sababu nilikuwa nataka kufa. Sikuwa na ujasiri wa kujiua na hakika nilikuwa naogopa kufa. Lakini kufa kwa namna anayoitaja daktari hata hakunipa hofu badala yake nikavutika na kumsihi anisaidie kuitoa ile mimba.
Mazungumzo yalikosa kabisa muafaka. Daktari yule alikuwa mbishi sana hakutaka kushiriki katika utoaji mimba huu. Nilipoona daktari huyu amekuwa na msimamo sana niliamua kutumia njia fulani ambayo hugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Nikaangusha mezani shilingi laki mbili. Akazikataa, nikaaga nikatoka. Niliporejea niliziongeza zikafika laki nne. Daktari akazikodolea macho, kisha akatazama kushoto na kulia.
"Umekuja na nani?" akaniuliza.
"Mwenyewe!" nikamjibu. Akatazama tena kushoto na kulia kisha akazikwapua zile pesa akazizamisha katika sehemu zake za siri. Nikakwepesha macho.
Akanifanyia ishara ya mkono. Nikamfuata hadi katika chumba kilichokuwa na harufu kali ya madawa. Akakifunga na funguo tukabaki wawili tu! Kimya.
Daktari alikuwa na hofu. Nililitambua hilo. Sikutaka kuuliza chochote.
"Toa nguo zote." Aliniamuru. Kauli yake ikanikumbusha kauli ya yule Mnaijeria aliyetaka kunibaka kwa kujifanya ananifanyia tiba ya asili. Huyu sasa alikuwa daktari, nikaamua kucheza pata potea. Kwanza nilikuwa natokwa damu. Sidhani kama angeweza kujaribu kunibaka.
Nikaziondoa zote, wakati huo yeye alikuwa amejikita katika kuchanganya madawa yake ambayo sikuelewa kazi yake ni ipi. Nikabaki kumsubiri.
Njoo hapa!! Aliniamuru huku akinielekezea kitandani.
Geuka hivi!! Nataka kukuchochoma sindano. Nikageuka huku nikiwa katika uoga. Kifo! Nilikuwa naogopa kufa.
Nikahisi kitu cha baridi kikinipapasa. Nikauma meno yangu kungoja uchungu wa sindano. Nilingoja huo uchungu lakini hamna nilichohisi.
"Acha kujikaza wewe sindano itakatikia ndani." Alinigombeza daktari. Nikashangaa hizo lawama zinatoka wapi wakati mimi hata sijajibana. Alipoona simjibu kitu akanichapa kibao. Nikashtuka.
"Mkubwa hivyo unaogopa sindano alaa!!" alinigombeza. Sikumjibu!!
Nikatega tena aweze kunichoma!! Hali ikawa vile vile.
"Sasa mimi nakuchoma hivyo hivyo." Alichukua maamuzi yake binafsi.
Nikageuka. Nikayasubiri maumivu!!
Badala ya maumivu nikakumbana nay owe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.
"Daktari!!." Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.
Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.
"Vaa nguo!" aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.
Kisha nikamfuata hadi ofisini!
"Chukua pesa zako!!" alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!
Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.
Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666'.
Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!
"Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako."
"Wenzangu? Wapi"
"Mnaomtumikia"
"Nani?" nilihoji kwa hofu.
"Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia." Alinihoji kwa utulivu mkubwa.
Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.
"Daktari sijui lolote mbona."
"Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa." Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!
"Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu." Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.
"Ndio maana nimejishangaa sana, iweje leo nikubali kuchukua rushwa, nikubali kutoa mimba msichana. Ama kweli kila mwenye alama hii hatakataliwa na dunia kwa lolote." Daktari alinong'ona kama anasema mwenyewe vile. Nilisikia kila kitu.
Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa!
"Nitakusaidia." Alinyanyua uso daktari akanieleza huku akinitazama vyema usoni.
Nilifarijika sana kusikia maneno yale. Kisha akaendelea, "Lakini uwe mkweli kwa kila kitu. Ukijaribu tu kuficha lolote lile. Nasema ukijaribu kuficha lolote lile. Wewe, marafiki na ukoo wako wote utatokomea. Mimi nakueleza haya kama mzee wako, katika kipindi changu cha miaka ishirini ya udaktari nakutana na matukio mengi. Lakini hili ni la tatu katika maisha yangu. Wenzako wawili, mmoja miaka saba imepita na mwingine mwaka juzi, nilitaka kuwasaidia lakini wakaleta ujanja ujan ja. Tuliwazika!! Aah!! Hatukuwazika insearch labda niseme tuliyafukia mabaki yao." Alimaliza kunielezea kisha akashusha pumzi kali sana.
Macho yangu nilihisi kama yanajilazimisha kutazama mbele. Machozi yalikuwa yamezidi. Mapigo ya moyo yalikuwa juu, sasa nikaanza kuamini niliyokuwa nayatazama katika filamu za kinaijeria. Kumbe uchawi upo? Hakika uchawi upo!!
"Kesho njoo!!" alinipa ahadi hiyo.
"Kwa hiyo sitatokwa damu tena?" niliuliza swali la kijinga.
"Kwani mimi ndiye niliyekuwekea" Daktari naye akanipa jibu la kijinga kama nilivyotegemea.
"Usimwambie mtu yeyote kuhusu maongezi haya." alinionya
Nikaaga! Kiguu na njia hadi nikaipata taksi.


Njia nzima nilikuwa nawaza na kuwazua. Zile ndoto zangu za kumjengea mama nyumba nzuri, wadogo zangu kusoma shule za kimataifa, mimi kuwa maarufu zaidi chuoni, ndoto za kwamba nataka kuwa mtakatifu! Zote zilikuwa zimekufa. Sasa nilikuwa nahangahika huku na huko huku nikisurubika na mateso ya nafsi.
Swali likajengeka katika kichwa changu. Dokta Davius linizuia nisimueleze mtu kuhusu mambo haya. Sasa daktari ananisihi nisifiche kitu. Hapa sasa nimuamini nani? Nilijiuliza.
"Kata kushoto!!" nilimuelekeza dereva.
Mawazo yangu yakawa yameishia hapo.
Maria aliniona kuanzia mbali. Akanikimbilia, akafika akanikumbatia.
"Da Bela jamani. Mbona mnyonge hivyo!."
"Nimemkumbuka sana John." Nilidanganya, huku siri kubwa nikiwa nayo mwenyewe.
Maria akaniongoza hadi ndani. Nikajibweteka kwenye sofa sebuleni. Maria akaniletea maji ya matunda niliyokuwa nayapenda, nikayagida kwa fujo kisha nikagundua kuwa nilikuwa na njaa. Chakula kilikuwa tayari!! Maria akanihudumia. Sasa niliweza kupumzika!! Sikutaka kwenda chumbani. Nililala sebuleni.
Kila baada ya masaa kadhaa nilikuwa naamka na kubadilisha pedi na nguo ya ndani kisha kuoga. Hali hii japo ilikuwa haijatimiza hata mwezi kwangu ilikuwa mateso makubwa. Sasa sikuweza kwenda kwa marafiki wala nisingeweza kwenda. Nilijihisi ninanuka, japo Maria hakuwa ameniambia hata siku moja lakini nilijijua mwenyewew kuwa sikuwa kawaida hata kidogo.


Siku hii ikamaliza bila tatizo!!
Asubuhi ya siku iliyofuata niliwahi sana kuamka. Badala ya kumuomba Mungu anijalie uzima na aniepushe na matatizo haya mimi niliwekeza imani yangu yote iliyosalia kwa daktari yule ambaye hadi sasa sikuwa namfahamu jina lake.
Saa nne kamili asubuhi. Nilikuwa katika mlango wa kuingia ofisini kwake. Japo kulikuwa na watu kadhaa waliohitaji kuonana naye. Mimi nilipewa kipaumbele, nikawapita nikaingia ndani.
Ahaaa!! Binti! Vipi kwema? Alinichangamkia sana.
Nikamjibu salamu yake. Nikakaa kitako kumsikiliza.


"Ngoja niwaondoe hawa watu hapo nje. Wewe nitakupigia simu uje mahali." Alininong'oneza. Nikamuelewa nikampatia namba yangu ya simu kisha nikaaga.
****


Sikuchoka kusubiria. Japo alichukua muda sana. Baada ya masaa mawili na nusu. Aliniita odisini kwake. Nikaenda upesi nikamkuta akiwa pamoja na mwanaume ambaye laiti kama ningekutana naye wakati ule ambao nilikuwa na jeuri ya pesa sidhani kama alikuwa na hadhi ya kupokea salamu yangu. Nilimsalimia kwa kuwa tu alikuwa pamoja na daktari.
Nilipomsalimia badala ya kunijibu, akanikonyeza!! Nikataka kusonya nikasita.
Kwa ncha za macho yangu nikamtazama mwanaume huyu, kuanzia mavazi yalivyochoka, amechakaa nywele zake na hata ngozi ilikuwa imepauka. Nikaamini hata akili yake haiku sawa. Nilipokumbuka jambo hili la akili kutokuwa sawasawa nikaamini atakuwa ni mgonjwa wa akili. Na daktari huyu alikuwa katika kumpa tiba. Kimoyomoyo nikamsamehe kwa kosa la jinai alilofanya la kunikonyeza.
"Binti..kama nilivyokueleza jana!! Usisite kuusema ukweli wote. Ukificha haitakusaidia kitu zaidi ya kuuangamiza ukoo wako wote." Alinieleza kwa utulivu. Yule tahira akacheka.
"Sawa daktari." Nilimjibu. Tahira akacheka tena!! Akaanza kunikera.
"R.I.P mtu wako niliyekwambia ndio huyu." Sasa daktari hakuwa akizungumza na mimi, bali alikuwa akisemezana na yule tahira. Nikashtushwa na hali ile, ina maana ananikabidhi mimi kwa yule chizi au alikuwa anamtania. Niliomba iwe hivyo lakini haikuwa. Alimaanisha.
Sasa tahira akanivagaa akanishika mikono. Nikajitoa mikononi mwake akacheka!!
"Nenda naye ofisini kwake huyo akakupe maelekezo. Anaitwa R.I.P"
"Na yeye anaitwa nani." Yule mtu niliyedhani ni tahira sasa aliuliza.
"Jitambulishe binti." Tahira alinieleza huku akinishika makalio. Kidogo nimtukane. Nikasita baada ya kuona daktari hakushtushwa na jambo hilo.


Nitafanya nini sasa!! Nikaanza kufuata uelekeo alionipeleka. Mara kwa mara alikuwa anacheka. Tulipishana na watu wengi lakini hakuna aliyemshangaa. Huyu sio tahira!! Nililazimika kuamini


Mlango ukafunguliwa nikaingia ndani!! Ofisi yake ilikuwa na hewa nzito sana ya madawa lakini yeye aliifurahia.
Karibu ukae…aaah!! Usikae kwanza hebu njoo huku." Akanivuta kwa nguvu, nikamfuata. Akafungua kabati moja kwa fujo.
Mungu wangu!! Maiti!! Nikaruka pembeni, akacheka!!
"Binti hawa nao walikuwa wajing wajinga tazama….njoo..njoo" akaniita. Nikasogea. Akavuta kabati jingine likafunguka.
Maiti ya mwanamke. Akamgeuza. Alikuwa na alama ya 666 katika makalio yake. Maiti huyu nilikiri kuwa kabla ya kuwa hivi alikuwa mrembo sana.
Sijui nini kilimuua maskini!!
Akanipeleka katika kabati jingine akavuta tena. Akatoka motto mdogo. Hana kichwa nay eye ana alama ya 666..R.I.P kazi yake ilikuwa kucheka tu kama tahira. Wakati mimi nilikuwa katika hofu kuu.
Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa. Maiti karibia tano zilikuwa pamoja nasi, waziwazi. Amani ikatoweka moyoni.
"Na wewe ukificha neno lolote tu!! Utakufa na vizazi vyote vitakavyofuata." Aliongea bila kucheka sasa.
Nilikuwa natetemeka.
"Hata huyo uliyemkalia na yeye nadhani ni walewale..hebu funua."
"Wapi?" nilimuuliza, likiwa neno langu la kwanza hapo ndani.
Akanionyesha kwa kidole. Ni pale nilipokuwa nimekaa. Nikafunua nikiwa natetemeka.
"Mamaaa!!" nikapiga kelele. Kumbe nilikuwa nimekaa juu ya maiti. R.I.P akacheka sana!!
Zile dharau zangu zikawa zimeishia hapa!! Nikamuheshimu!!!


*** ISABELA ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti…je kuna msaada gani hapa!!!


***Nini hatma ya mimba yake!!!!



culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe kelcie Meljons
 
Last edited by a moderator:
Sijapita mtaa huu kwa siku tatu, lakini daaaah Nimeogopa, Nimeona huruma, Nimefadhaika, Nimehuzunika, Nimecheka! Aiseee hii ni Kali. Shukrani mkuu CASUIST.
 
Unazingua Bos, gani Vitu nusu nusu, mzuka unapanda mzuka unashuka, hongera Kazi nzuri
 
Back
Top Bottom