RIWAYA: Sitaisahau Facebook

RIWAYA: Sitaisahau Facebook

SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John P.




SEHEMU YA KUMI NA SITA


Ule ujumbe ulioonekana katika akaunti yangu, ulinishtua sana. Sasa sikuwa na ujanja tena nikafikia hatua ya kukubali kuwa yamenishinda na ninatakiwa kumshirikisha mtu mzigo huu.
Kitu cha kwanza niliiondoa akaunti yangu ya facebook katika matumizi ‘deactivation'. Sikuhitaji tena kuwa katika mtandao huo. Baada ya hatua hiyo nikaandika barua ya kuomba ruhusa ya kutofanya mitihani hiyo iliyokuwa mbele yangu pale chuoni.
Kwa kuwa nilikuwa nafahamika sikupata usumbufu nikapewa ruhusa hiyo upesi. Nikaamua kufunga safari kuelekea nyumbani. Lengo kuu likiwa kumueleza mama kila kitu kilichonitokea na kutishia uhai wangu. Sikuwa na ujanja mwingine.
Usiku nilikuwa nimetingwa katika kujiandaa. Ni Maria pekee ambaye nilimueleza kuwa nitasafiri, na wakati huo alikuwa akinisaidia kufungasha mabegi yangu. Tayari kwa siku inayofuata.
Ilikuwa saa sita kasoro dakika kadhaa. Nilitulia nikamtazama Maria na yeye akanitazama mimi. Kisha kila mmoja akageuka na kutilia maanani kile kinachosikika. Mlango ulikuwa unagongwa.
Hakika ni palepale katika nyumba yangu niliyokuwa naishi.
Nani huyu muda huu? Nilimuuliza Maria kana kwamba yeye alikuwa anamfahamu aliyepo mlangoni.
Maria hakuwa na cha kunijibu.


Nikiwa nimemshika mkono Maria tuliufikia malango, tukaulizia ni nani? Hakujibu. Tukauliza tena!! Kimyaa!!
Kila mmoja akamshikia mwenzake kwa nguvu sana!!
Ghafla mlango ukabamizwa kwa nguvu sana.
Mungu wangu!! Watakuwa majambazi! Nilihisi.
Kabla sijajua nini cha kufanya, mlango ulisukumwa bila kutoa kelele ukafunguka.
Waaa!!
Ghafla pakawa giza. Nikasukumwa kando na mikono ya baridi sana. Nikajaribu kupiga kelele sauti haikutoka. Nikajaribu tena sikuweza kabisa. Kisha nikasikia mlio mkubwa. Kisha kama gunia la mahindi kitu kikatua chini huku kikipiga kelele. Ilikuwa sauti ya Maria.
Kama vile haitoshi nikashikwa tena na yule mtu mwenye mikono ya baridi. Akaanza kuniburuza. Moja kwa moja hadi chumbani kwangu.
Akaninyanyua akanitupa kitandani.
Nikajaribu tena kupiga kelele sauti haikutoka.
Mara taa ikawashwa!! Chumba kikang'ara.
Ana kwa ana na mtu ninayemfahamu!!
Ni yule niliyemuandikia barua ya kuomba kuacha kazi!!
Dokta Davis mbele yangu!!
Alikuwa amevalia suti nyeupe. Na hakuwa akitabasamu!!
Nikajaribu kuzungumza, sikuweza!! Akacheka, nikamsikia.


"Isabela……" aliponiita, nikajaribu kuitika sauti ikatoka.
Maajabu haya!!
"Milioni thelathini, mama yako mzazi, ama wewe!" alinieleza kwa utaratibu.
Sikumuelewa. Nadhani hata yeye aliitambua hali hiyo.
"Ni hivi..hadi sasa umetumia shilingi hizo…sasa unatakiwa kabla sikjaweka saini yangu katika barua yako kuhalalisha wewe kuacha kazi nahitaji ufanye maamuzi. Nakupa wiki moja tu!! Uwe umerejesha pesa hizo, ama mama yako akae mbali nawe maisha yako yote na mwisho ni uchaguzi ujitoe wewe kwa usiku mmoja!!"
"Usiku mmoja?" nilijiuliza. Ikawa tena kama ananisikia.
"Usiku mmoja wewe na mimi na kisha nitakuacha huru na uamuzi wako wa kuamua kuacha kazi. Ole wako umueleze mtu…nitachukua maamuzi ambayo hautaamini"
Sikuamini kama maneno hayo yanatoka kinywani mwa mtu huyu. Na ameweza vipi kufika Tanzania bila kunieleza. Mbaya zaidi amekuja nyumbani kwangu usiku mnene.
Kabla sijamjibu lolote. Alizima taa. Kisha nikasikia mlango unafungwa. Nikaendelea kutulia kama nilivyo huku naogopa.
Nilidhani yupo jirani na eneo lile. Sikuthubutu kusimama. Baada ya dakika kadhaa nikasikia hatua zikijongea kuja katika mlango wa chumba changu.
Anarudi! Niliwaza nikaendelea kutulia. Jasho likilowanisha shuka zangu.
Taa ikawashwa. Kwa ncha za macho nikamtazama aliyepo mbele yangu. Alikuwa ni Maria. Uso wake ukiwa umevimba.
"Bela…nimeanguka mwenzako." Alianza kunieleza. Nikageuka kumtazama huku nikipatwa na hisia za kumwoga.
"Mh!! Mbona hivyo Bela. Kimekusibu nini?" aliniuliza.
Sikuwa na cha kumjibu. Nilibaki kushangaa. Maana niliamini na yeye amemuona dokta Davis lakini hakuonekana kujua lolote.
Nilitamani sana kumueleza lakini hofu ya onyo la Dokta ilinitawala. Maria akanisogelea akanikumbatia. Nikahesabu alama kadhaa za vidole katika shavu lake. Huenda kabla ya kuanguka alipigwa kofi.


Siku iliyofuata nilitakiwa kusafiri. Maria aliwahi sana kuniamsha lakini sikuwa na uwezo tena wa kusafiri. Onyo la Davis kuwa iwapo nitamwambia mtu yeyote atafanya anachojua.
Niliunda sababu kadhaa nikafanikiwa kumshawishi Maria kuachana na safari hiyo. Alishangaa lakini hakuwa na jinsi maana msafiri nilikuwa ni mimi.
Siku ya pili hiyo zikasalia siku tano Dokta afanye yake aliyoyaahidi.
Bado sikuwa nimepata jibu sahihi la kumpa. Milioni alizonitajia kwa kweli sikuwa nazo hata nusu yake. Kumuondoa mama yangu katika uso wa dunia ni jambo ambalo sikutaka kulisikia.
Kulala na mimi usiku mzima. Lilikuwa ni sawa na tukio la kubakwa kwa hiari. Udhalilishaji!!
Nikajilaani kumuamini sana Davis. Majuto yakaninyanyasa.


Bila kumuaga Maria, niliamua kutoweka pale nyumbani kwangu na kwenda kupanga katika nyumba ya kulala wageni. Maeneo ya Igoma.
Nilizima simu yangu! Siku zikazidi kukatika na sasa ilikuwa imesalia siku moja ya mimi kutamka jibu langu.


Nikaiwasha simu yangu!! Nikaitafuta namba ya Davis. Nikafungua sehemu ya ujumbe nikamtumia.
USIKU MMOJA MIMI NA WEWE. Nitakueleza wapi nipo uje!!


Ujumbe ukapokelewa! Lakini haukujibiwa!!


****


Siku ya tukio ikafika!! Nilikuwa najaribu kumpigia simu Dokta huyu wa maajabu nimuelekeze wapi nipo lakini simu yake haikuwa inapatikana. Nilijaribu tena na tena bado hali ilikuwa ileile.
Hofu ikanitawala! Huenda Davis ameamua kufanya anachojua yeye. Vipi kama ameamua kumtokomeza mama yangu!! Nilianza kulia baada ya kufikiria hayo.
Nikiwa katika kulia simu ya chumbani ilianza kuita.
Nikaitazama kisha nikaipokea.
"Kuna mgeni wako.."
"Mgeni?"
"Anaitwa Davis." Sauti ya muhudumu ilinijibu.


Kulisikia jina hilo tu. Nikakurupuka kutoka kitan]dani bila kujua ni wapi ninakimbilia. Nilikuwa naogopa sana jambo ambalo lilikuwa linakuja mbele yangu. Kufanya mapenzi bila hiari na kiumbe cha ajabu sana.
Haya yote niliyataka mwenyewe!! Sasa nikaanza kuhisi kuwa Davis hakuwa mtu mzuri kwangu!!
Davis ni MCHAWI!!!
Naenda kufanya mapenzi na mchawi!!
Ghafla nikaijiwa na kumbukumbuku za chapa ya shetani 666, niulipokumbuka hili nikakumbuka na mshahara wangu ulikuwa una hizi namba, hata simu ya Osmani nayo ina 666, Davis aliwahi kunitumia nauli nayo ilikuwa na 666 na sasa nipo katika chumba namba 66 namsubiri huyu mfalme wa 666
Hapana! Hapana! Niliipinga nafsi yangu. Na sasa nilikuwa nimeamua kumkimbia mchawi huyu. Kuikimbia chapa ya shetani!!!
Nikiwa najiandaa kukimbia
.Mlango ukafunguliwa!!!


NANI AMEUFUNGUA MLANGO!!!
JE ISABELA ATAIKIMBIA CHAPA HII 666.
Kama akiikimbia, je ndo anaruhusu MAMA YAKE afe!! NANI KAMA MAMA???


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei
 
Kuna jamaa kutoka Dar es Salaam alikwenda kwenye kijiji kimoja huko mkoa wa mbali. Alipofika huko, akamuona binti mzuri mno, akamsimamisha na kuanza kumpiga sound. Washikaji wa kijiji kile walipomuona, wakamfuata na kumtahadharisha kwamba msichana yule alikuwa binti wa mzee mchawi kuliko wachawi wote katika vijiji vya hapo karibuni hivyo angerogwa kama watu wengine.

Jamaa aliogopa lakini kwa jinsi demu yule alivyokuwa mkali, akasema bora arogwe kuliko kumuacha. Kweli bwana, baada ya saa chache, akamuona yule demu, akamfuata na kama kawaida akaanza kumpiga sound.

Huku akiendelea, baba wa yule binti akatokea, jamaa akaanza kutetemeka lakini akaamua kujikaza kisabuni. Yule mzee akamsogelea, akamkoromea sana na kumpa vitisho vingi vya kichawi.

"Nitakugeuza kuku, nasema nitakugeuza kuku mwanaharamu wewe," alisema yule mzee kwa hasira mpaka mate yalikuwa yakimtoka.
Msela, mjanja wa town naye hakutaka kukaa kimya kwani kila alipokuwa akiangalia huku na kule, watu wa kijijini pale walikuwa wakimwangalia kwa masikitiko kwa kuona kwamba sasa mshikaji aliingia choo cha kike.

"Unajifanya unaweza kuroga watueeeee, sasa na wewe subiri," kijana yule alisema kwa kujiamini, watu wote wakaguna ‘Mmmmmmmh!" mzee akazidi kupandwa na hasira, akamsogelea yule kijana zaidi na kuendelea kumpiga mkwara.

"Nitakuua, yaani ukifika kesho mchana ukiwa mzima labda mimi sio mzee Kuambilinyi," alisema yule mzee, alionekana kuchukia mno.
Japokuwa mjanja wa town aliogopa, naye akaanza kumpiga mkwara mzee.

"Na wewe kama utafika kesho saa nne asubuhi, mimi sio Kunjukuruwete," alisema kijana yule, hata jina hilo alikuwa amejibatiza, jina lake halisi lilikuwa James.
Yule mzee akaondoka, watu wakataka kujua ni nani alikuwa juu zaidi ya mwenzake. James alikuwa na woga, hakujua afanye nini na wakati hakuwa mchawi na wala hakuwa mganga. Alipoona kwamba hana la kufanya, akaulizia kazi alizokuwa akizifanya mzee yule, akaambiwa kwamba alikuwa mvuvi na muindaji kwa kutumia mitego.

Alichokifanya kesho asubuhi sana akaenda mtoni kulipokuwa na nyavu za kuvulia samaki za yule mzee, alikuta samaki wengi, alichokifanya, akawachukua wote na kuondoka nao. Safari yake ilikuwa ni kwenda porini, alipofika kule, akaanza kutafuta mitego ya yule mzee, alipoiona mitego kadhaa, ni mtego mmoja tu ndiyo ulikuwa umenasa swala, alichokifanya, akamtoa yule swala, akawaweka wale samaki, akaanza kurudi harakahara kule mtoni huku akiwa na swala mkononi, alipofika kule, akamuweka yule swala katika nyavu zile za samaki na kisha kurudi.

Baadaye yule mzee akaelekea katika sehemu zake za mitego.Sehemu ya kwanza kabisa kwenda ilikuwa ni mtoni kwenye nyavu zake, alipofika kule, akapigwa na mshangao baada ya kumuona swala akiwa amenaswa katika nyavu zile, mzee akachanganyikiwa. Kwa harakaharaka akaanza kuelekea kule porini, alipofika, akaangalia mtego wake, akakuta samaki, moja kwa moja akajua kwamba James alikuwa ameanza kumchezea mchezo, akaanza kuingiwa na hofu kwa kuona kwamba kijana yule alikuwa nuksi.

Akakumbuka kwamba siku hiyo saa nne James alisema kwamba angemuua, kwa zile action alizoziona, zilimfanya kugundua kwamba James alikuwa nuksi zaidi yake, mzee akaanza kulia huku akirudi kijijini.

Kila mtu akapigwa na butwaa, mzee akaelekea mpaka katika nyumba aliyokuwa akiishi James huku akilia, akapiga hodi, akaanza kumuomba James msamaha asimuue kwani bado alitamani kuendelea kuishi. Aliomba sana msamaha lakini James akakataa kumsamehe.
"Mimi sikusamehi, lazima nikuue," alisema James huku akijifanya kuwa na hasira.
"Nisamehe kijana wangu, nisamehe sitorudiaaaa," alisema mzee yule huku akilia.
James hakutaka kumsamehe, aliendelea kusisitiza kwamba ilikuwa ni lazima kumuua. Mzee yule akaenda mpaka kwa mwenyekiti wa kijiji na kuomba kumsaidia kumuombea msamaha kwa James, hakuridhika, akaelekea mpaka kwa viongozi wa kijiji, wote wakamfuata James na kuanza kumuombea msamaha.
"Una bahati, ulibakiza saa moja tu la kuvuta pumzi ya dunia hii. Nimekusamehe ila usirudie tena, ningekupoteza na kukufanya mkulima shambani kwangu," alisema James. Mzee yule akashukuru sana.
James hakutaka kuendelea kukaa kijijini hapo, siku hiyo jioni akaondoka kurudi Dar kwani aliogopa kwa kuhisi kwamba mzee yule angeweza kumtest.

Umejifunza nini?

Leo kutokana na tatizo ambalo nilishalieleza Sitaisahau FB itaendelea kesho, lakini tutaanza na utangulizi wa nyingine.



RIWAYA: SIKU YA GRADUATION
MTUNZI: MAUNDU MWINGIZI


SEHEMU YA KWANZA

"Yaani kweli RAMLA Umeamua kunitenda kiasi hiki!!, pamoja na mapenzi yote niliyokupa lakini umeamua kunisaliti!, nimepoteza pesa zangu nyingi kukusomesha chuo nikiamini we ndo utakua mama wa Wanangu Leo wema wangu umegeuka mkuki wa sumu moyoni mwangu, Ramla Why? Why?!!" Niliendelea kulalama peke yangu huku nikilia kwa uchungu, shuka yote ikiwa imeloana jasho na machozi pale katika kitanda changu..
"Kitendo ulichonifanyia Ramla kinaniua ndani kwa ndani, huu ni zaidi ya ukatili yaani umesahau ahadi zetu zote tulizowekeana!!!.. aaaah" niliendelea kujisemea peke yangu kama Mwehu..


TUKO WANGAPI?, bonyeza like baada ya muda tuanze...


culbby mlyn Analyse princetx slim5 MUSSOLIN ram Angelicious showtie Ngoami amina mabata Moderator binti kiziwi Nicas Mtei korino Sukula aniceth mzahula Khantwe
 
Last edited by a moderator:
mkuu@Casuist hilo somo zur sana,tunachojifunz hapo tusivamie miji ya watu bila wenyeji.
 
Back
Top Bottom