ilikuwa lazima ashtuke kwa matokeo mabaya ila kwa umri wa miaka 17 sio mdogo kiasi kwamba hajui ni risk kufanya alichofanya. Ni urafiki wao tu wa kufa na kuzikana ndo ulikuwa unamcontrol kwa wakati ule
ilikuwa lazima ashtuke kwa matokeo mabaya ila kwa umri wa miaka 17 sio mdogo kiasi kwamba hajui ni risk kufanya alichofanya. Ni urafiki wao tu wa kufa na kuzikana ndo ulikuwa unamcontrol kwa wakati ule
Unataka kuniambia kama angekuwa anajua mwalimu ni mwathirika bado angelala nae for the sake of joy's happiness? Alikuwa tayari kutumia mwili wake (kwa siku moja) kwaajili ya rafiki yake na sio kwamba alijitoa kufa....hayo ya kufa yametokea tu
Joy nae bwana sa kuna ugumu gani hapo? Mbona simpo tu amwambie tu Betty 'pale kwa mtoto wa mbunge ndipo ilipo roho yangu. Ukimuua umeniua..' kwa jinsi Betty anavyompenda atamuelewa tu....mmmmhh nimesau hii ni hadithi lol
Unataka kuniambia kama angekuwa anajua mwalimu ni mwathirika bado angelala nae for the sake of joy's happiness? Alikuwa tayari kutumia mwili wake (kwa siku moja) kwaajili ya rafiki yake na sio kwamba alijitoa kufa....hayo ya kufa yametokea tu
Jamani mapenzi yanauma ingawa hayana meno. Joyce funguka dear, mi mwenyewe leo sina hata raha my wangu amenipa cm yake nimuelekeze kitu nilipofungua sup nimekutana na jina wife yani nimeshindwa hata kumwelekeza
Macho yalikuwa mekundu sana, akasingizia kuwa anaumwa kichwa, Betty akamtafutia dawa na kumpatia anywe, Joy akazipokea na kuzimeza. Kisha akakirukia kitandani, kizunguzungu kikiwa kimemwandama. Kitanda kikaonekana kama kinazunguka kwa kasi katika namna yua kukera, joto likaizidi maarifa feni iliyokuwa inapuliza pale ndani, Joy akaondoa nguo zake na kujifunika na kanga pekee. Akajilazimisha kulia machozi hayakutoka lakini kuna donge lilikuwa limemkaba kooni. Ama kwa hakika Joyce alikuwa amefikwa. Uzito wa roho kadhaa mkononi mapema kabisa ulionekana kumzidia. Ili apate ahueni alitakiwa kuchagua nini cha kutupa na kipi cha kubaki nacho. Joyce alitakiwa kufanya maamuzi ya kuokoa roho mojawapo. Ili asishindane na ule usemi ambao mchumia janga hula na wakwao. Joy akabaki kuwa mfa maji asiyeisha kutapatapa….
USINGIZI ukiwa umegoma kabisa kumtembelea Joy na kumtenganisha na dunia kwa muda na kuyasimamisha mawazo. Mara alisikia mivumo ya sauti ikinena lugha ambayo hakutaka kuisikia kabisa, lugha ya kumzungumzia Isaya. Na mnenaji alikuwa ni Betty. "Yaani huyo ameingia pabaya lakini ujue nini, mimi shida yangu ni huyo baba yake anayejiita mbunge. Nikimpata huyo sikosi milioni kama thelathini hapa. Wanajua kuhonga hao wajinga. Sasa milioni thelathini hapa hatujarekebisha walau ki'zahanati chetu cha Ukala, hatujaweka madawati kadhaa katika ile shule tuliyosoma pale Ukala. Ujue nilikuwa nachukia kukaa chini yaani we acha tu, nd'o maana nakwambia Joy mi sitaki kuondoka hivi hivi acha tu nizichume dhambi lakini hata Mungu anajua kuwa sizichumi kwa sababu ya starehe Joy wangu. Ingekuwa ni kwa ajili ya starehe nadhani hata hapa kwako ningekuwa n'shahama…mi nataka pesa kwa ajili ya maendeleo. Sijui mtoto wa mbunge sijui mtoto wa diwani mimi sijali cha msingi ni mwanaume mwenye tamaa basi ile OLE inamuhusu….." mara Betty akasita kisha akasema kwa sauti ya chini kidogo, "Sijui Joy mwenyewe keshalala najipigisha makelele peke yangu!!" kisha akaanza kujiimbia nyimbo alizokuwa amezikariri.
Joy hakuwa amelala alisikia kila kitu, maumivu makali kabisa yakapenya katika moyo wake, akajikaza asisike kama analia lakini machozi yalimwagika kwa wingi. Akiwa hapo kitandani akakumbwa na wazo la kutatua tatizo hili, akafikiria kumweleza Isaya kuwa anampenda sana na yupo tayari kuwa katika mahusiano naye. Lakini akakumbuka mambo mawili makuu, jibu la mwisho alilowahi kumpa Isaya, "SIJAWAHI KUKUPENDA ISAYA"….hili lilimuumiza hata yeye maana lilikuwa jibu kavu linalochoma kwelikweli. Kisha akakumbuka na ujumbe alioupokea kutoka kwa Isaya siku moja iliyopita, "SITAKI MAZOEA YA KARIBU NA WEWE."
Joy alipoukumbuka ujumbe huu akazidi kutiririkwa machozi na kuona kuwa hakutendewa haki hata kidogo kupewa jibu lile. Ama hakika mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Kwa majibu haya mawili katika siku tofauti Joyce aliuona utata waziwazi, Isaya asingekuwa mwanaume mjinga akubali kirahisi kuwa katika mahusiano na mtu ambaye alimtamkia kuwa hana hisia naye. Hapa sasa Joy akaamini kumwendea Isaya na kumweleza kuna uwezekano wa kukutana na mambo mengine yenye utata zaidi, ama kupuuzwa na kutukanwa hadharani kuwa anamtaka Isaya kwa ajili ya pesa zake, ama la kuwa katika mapenzi ya foleni. Jambo ambalo binti huyu hakuwa tayari. Mawazo haya yakazidi kumpasua kichwa Joy.
Mara akafikiria pakipambazuka amweke Betty kitako na kumweleza kila kitu kilivyo juu ya huyo Isaya ambaye anajiita Joram. Wazo hili akaliona ni jema sana, lakini ghafla akakumbuka kitu. Ni kwamba Betty atamkubalia hoja yake mara moja na ataachana na Isaya. Ehe! Baada ya hapo!! Hakuna jipya jingine Isaya ataendelea na maisha yake na atakuwa na msichana mwingine ambaye Joy hana mazoea wala ukaribu naye, hivyo Joy atazidi kuumia akimuona Isaya na msichana mwingine. Joy akatambua kuwa alichokitaka yeye ni kuwa katika mahusiano na Isaya na wala si kwamba Isaya asiwe katika mahusiano na Betty.
Silaha kubwa na pekee ambayo ingeweza kuirejesha imani ya Isaya kwa Joy ni kiasi cha Joy kumtafuta na kumweka kitako kisha kumweleza kuwa msichana ambaye wapo naye katika mahusino ni mwathirika. Hivyo amemweleza hayo kwa sababu anampenda sana. Kwa kauli hiyo mwanaume yeyote duniani hawezi kuchomoka tena, na hatahitaji uthibitisho mwingine kujiaminisha kuwa anapendwa. Lakini kumweleza Isaya hayo ni sawasawa na kumsaliti, tena usaliti mkubwa kwa Betty. Kizungumkuti kikuu!!! Joy akakosa maamuzi.
****
ISAYA AKUNAAY. Mtoto wa mbunge wa Geita mjini, alikuwa ameamua kumuumiza Joyce haswaa kwa akitendo chake cha kuingia katika mahusiano mengine na msichana mwingine ambaye ni mtu wa karibu wa Joyce. Alijua kuwa taarifa zimemfikia tayari, lakini hiyo ilikuwa haitoshi bado alihitaji kufanya jambo kwa ajili ya kupigilia msumari wa mwisho. Pesa huzungumza, hii ni kweli. Akiwa kitandani kwake akapata wazo la kumtambulisha Betty kwa marafiki zake na wanachuo wengine. Hakuwa na wasiwasi katika hili kwa sababu kwa kitendo chake cha kubadilika ili ampate Joyce hakuwa na wasichana wengine tena, hivyo hakutegemea mtafaruku wa aina yoyote ile. Na isitoshe alikuwa amepigiwa chapuo agombee nafasi ya uraisi wa chuo basi alihitaji kuwa mfano kwa wanafunzi wengine. Mfano katika namna ya kuishi na pia uwazi katika mahusiano. "Yes! Ndege wawili kwa jiwe moja tu. Hapa namkomoa Kidoti na upande huu najijengea mazingira mazuri ya kuuchukua uraisi wa chuo." Alishangilia Isaya huku akijirusha rusha kitandani kwake. Wazo hilo halikuhitaji mshauri bali lilihitaji utekelezaji. Siku iliyofuata akiwa na Betty ufukweni na wapambe lukuki kama kawaida alimweleza nia yake ya kufanya ‘engagement' na kumvika pete rasmi kabla ya uchumba.
Kwanza Betty hakuamini kama Isaya alikuwa amezama kiasi kile, alidhani ni wale wanaume wa kuhitaji mapenzi tu na kisha kuendelea na mambo yao. Tangu atue jijini Dar es salaam hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanaume kumtamkia juu ya kumtambulisha kisha uchumba na ndoa. Mapigo ya moyo yakaongezeka kasi yake, hakika hili lilikuwa shambulizi la ghafla sana. Shambulizi lisilotegemewa kabisa. Betty akashikwa na kigugumizi akakosa cha kusema, wakati huo tayari Isaya alikuwa amemvuta na kumlaza kifuani mwake. Zile busara alizorithi kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia na mapenzi bwana Matanuru sasa zikaanza kufanya kazi, akamshawishi Betty kwa maneno makali ya kimapenzi, sauti maridhawa kabisa ya kiume ikapenya katika masikio ya Betty na kisha kwa mara ya kwanza ikatua katika mtima wake. Betty alikuwa amekutana na mwanaume ambaye ana hisia za hali ya juu kwake. Akajisikia vibaya kwa sababu hana msamaha kwa ajili ya mwanaume yeyote akajijutia kuupata Ukimwi akiwa bado mdogo. Laiti ningekuwa salama ningenyanyua kinywa change na kukiri kuwa hatimaye nimempata mwanaume anifaaye!! Aliwaza Betty. "Mbona kimya mamii." Sauti ya Isaya ilimrejesha tena mahali pale. "Hapana mpenzi basi tu nilikuwa nafikiria juu yako. Elewa kwamba wewe ni kila kitu kwangu, nilikueleza siku ya kwanza kuwa umenikuta mimi kama Betty na sasani Betty wa Isaya. Nakusikiliza wewe." Betty alinong'ona kimahaba. Akamkosha Isaya. Kijana akambeba na kumrusha juu juu. Kisha wakakimbilia ndani ya maji wakikimbizana huku na kule. Siku hii ikamalizika kwa furaha ya aina yake. Lile lengo la Isaya likapiga hatua moja mbele.
****
JOYCE alikuwa akingojea wakati ambao Betty atarejea aweze kuzungumza naye na kumweleza kitu ambacho kinaisumbua nafsi yake. Aliamini kuwa ni Joyce pekee awezaye kumshauri ama walau kumtia moyo juu ya kitu ambacho kinaendelea kusafiri katika moyo wake. Aliamini fika kuwa bila kulitatua tatizo hilo basi ajiandae kuanguka vibaya katika masomo yake jambo ambalo hakuwa tayari kulishuhudia kwa macho yake likitokea. Masaa yakasogea hatimaye mlango ukagongwa, alikuwa ni Betty. Betty mwenye furaha tele. Ni heri Betty angemwacha Joy azungumze kwanza, lakini ilikuwa bahati mbaya kwake maana Betty alianza kuzungumza kabla. "Mwenzangu…..kuna wanaume wanapenda jamani. Eti katangaza uchumba mwenzangu duuh. Sema ni mtanashati ila ndo hivyo mi siangalii nyuma, hiyo sherehe nahudhuria, pete navikwa halafu usiku huo wa pete nampa na zawadi yake ya tamaa za kijinga jinga. Maskini Joram wangu. Pole yake." Alizungumza Betty kwa papara huku akihesabu noti kadhaa alizopewa na Isaya aitwaye Joram kwa ajili ya kununua vazi maalum kwa sherehe ile na pia kwa ajili ya matumizi yake. He! Wamefikia mambo ya uchumba tena? Mungu wangu Isaya anakufa jamani. Isaya wangu!! Alilalamika Joyce katika nafsi yake. Lakini kufikia pale hakuwa na kauli tena dhidi ya Betty. "Sasa hapo najua atataka kunipeleka kwa mzee wake, huyo mbunge. Hapo ndo napataka sasa, si ifike hiyo siku ya kuvikwa pete mtoto wa watu mie. Duh sipati picha, shosti wewe usihudhurie maana nitaona aibu si unajua nipo kazini mimi." Alizidi kubwatuka Betty bila kumpa nafasi Joy kusema lolote. Joy alilazimisha tabasamu huku akijiona akiisindikiza safari ya Isaya kuelekea kaburini.
WAKATI Joyce akiwa aamsikiliza Betty, wafuasi wa Isaya akiwemo Matanuru ambaye alikuwa mshauri mkuu walikuwa wakipanga bajeti kuhusiana na sherehe hiyo. Ukumbi, vinywaji, muziki, mapambo na mengineyo mengi vilikuwa katika orodha kuu. Isaya alingojea tu kupewa jumla ya pesa inayohitajika. Kubwa zaidi Isaya aliwahakikishia wajumbe wake kuwa patakuwepo na wabunge wasiopungua wanne pamoja na baba yake mzazi. Ilisisimua sana kuisikiliza habari hii. Baada ya siku mbili habari hii ikatapakaa chuo kizima. Isaya anamvisha mtu pete. Kila mpenda sherehe aliingoja sherehe hii. Sherehe ya mtoto wa mbunge.
****
UKUMBI ulikuwa umetapika haswaa, wenye nazo wachache walichanga pesa, mtoto wa mbunge akajazia za kwake na baba yake. Waalikwa hawakutakiwa kuchangia chochote zaidi ya zawadi ambazo pia zilikuwa hiari. Isaya aliutazama ukumbi na kukiri kuwa hili ni pigo kwa Joyce Kidoti na pia ni nafasi ya yeye kujitangaza kisiasa hapo chuoni. Mzee wake alihimiza uhudhuriaji wa watu wengi ili kuzidi kumkita mtoto wake katika siasa ili ikiwezekana aweze kumrithi kiti chake cha ubunge wakati atakapostaafu. Sherehe ikafana haswa!! Kila jicho la mwsanaume lilimtazama Betty katika namna ya matamanio, wasichana wenye wivu walitafuta cha kukosoa wakakikosa, wakabaki kusema neno moja tu ambalo huenda lilikuwa na ukweli ndani yake. Betty alikuwa akijilazimisha kutabasamu!! Japo alipendeza lakini lile tabasamu….lile tabasamu lilikuwa na utata….. Lakini nani angejali kuhusu tabasamu wakati alikuwa ameng'ara? Akavikwa pete Betty, akakumbatiana na mbunge wa Geita, na wabunge wengine watatu wa majimbo tofauti tofauti. Picha zikapigwa kwa wingi. Wale wenye wivu nao wakajisemesha kuwa wanawatakia maisha mema wawili hao. Isaya alitabasamu kutoka moyoni, alitabasamu kwa sababu alikuwa ni mshindi katika vita mbili. Vita ya mapenzi na siasa. Lakini angetambua kuwa palikuwa na vita kubwa inamsubiri, vita yenye kuogofya na kufedhehesha basi asingeruhusu jino lake hata moja kutazamwa na watu. Ama kwa hakika liishalo ni heri kuliko lijalo. Hakulijua hili Isaya.
Majira ya saa sita usiku wale wapendanao walipanda katika gari la kifahari kuelekea katika hoteli ya kifahari katikati ya mji. Jicho kali liliitazama ile gari, mwanaume akiwa amekumbatiana na mwanamke. "Isaya….Isaya usife Isaya….nakuhitaji bado pliiz!!" mwenye lile jicho alisema kwa sauti ya juu kidogo kisha akajikurupua na kujiapiza kuwa alikuwa muuaji kuruhusu Isaya afanye zinaa na Betty muuaji wa kukusudia.
Lakini akiwa anawaza haya magari yalikuwa yametoweka tayari. Joyce akataharuki, akahaha huku na kule. Alitamani kupiga mayowe kila mtu ajue kuhusu hatari iliyopo mbele yake. Lakini mara akakumbuka kile kiapo cha kuitunza siri ya Betty, siri ya kuua maksudi kwa kuambukiza Ukimwi. Nafsi ikamsuta akajiona mjinga sana anayeenda kujichumia dhambi ambayo anaweza kuiepuka. Joy akaikumbuka ahadi ya Betty kuwa usiku huo ndio usiku wa kumpa zawadi Isaya. Zawadi ya kifo. Kauli hii ikamsisimua na kumtoa katika pumbazo Joyce. Nguvu ya mapenzi ikamtekenya, ni kweli alikuwa anampenda sana Isaya, na sasa alikuwa anabariki mauaji haya ya maksudi. Upendo gani wa kushindwa kutetea ukipendacho… UTATA…. JOYCE akaamua kufanya jambo. Jambo ambalo badala ya kuwa utatuzi wa tatizo, jambo likazua jambo. Roho mkononi zikamzidia uzito, tamaa ya kuzishikilia zote tatu kwa pamoja ikamvuruga akili.
Maskini Joy, hivi kilichokufanya usiongee na Betty tangu mwanzo kuhusu Isaya ni nini? Ona sasa unavyohangaika, haya ngoja tusubiri kuona utazua jambo gani
Malumbano yaliendelea, ilikuwa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya usichana kujikuta katika mkwaruzano na wazazi wake wote wawili,tena wote wakiwa wanayapinga maamuzi yake aliyokuwa amefikia. Ni kweli alikuwa na umri mdogo na hakudanganywa na mzigo wa matiti ulioanza kujaa kifuani pasina kumtia kero. Bado aliamini ana hadhi ya kuitwa mtoto maana aliwategemea wazazi wake kwa kila kitu. Lakini katika jambo hili aliamua kusimama kidete kujitetea. Mama alikuwa haamini anachokisikia na mzee Kisanga ndo alikuwa akihisi yu ndotoni. Mama aliita kisha akageuka na upande wa pili akiwa wima, Baba .nawaheshimu sana na hilo wote mnalijua .lakini naomba katika hili muielewe azma yangu muwe na utu katika hili baba hivi leo Betty akifikia hatua ya kuwa yatima tutakuwa na furaha gani? Ndio undugu huu tunaojisifia kila kukicha. Undugu wa kushindwa kufanya jitihada kidogo tu kuokoa uhai . Aliongea kwa huzuni kuu, sauti yake ikipambana na mikwaruzo. Mama Joyce .mwanao huyo. Mzee Kisanga alimwambia mkewe katika namna ya kushutumu. Kisha akasimama ili aweze kuondoka. Baba Joyce mume wangu, yaani leo hii amekuwa mwanangu na si mtoto wetu heee! Makubwa mbona haya. Mama Joyce aliduwaa. Mzee Kisanga hakujibu lolote, akaingia chumbani kwake. Baada ya dakika kadhaa ulisikika mchakato wa baiskeli ikiegeshwa nje ya nyumba yam zee Kisanga. Kaka yake huyo labda aongee naye vizuri, mimi sitaki kuamshwa na upuuzi wenu. Mzee Kisanga kutokea chumbani alizungumza. Joyce na mama yake wakasikia. Walikuwa wanatazamana tu kama majogoo yaliyopigana na kukosekana mshindi sasa yamekosa la kuamua mshindi. Ehee! Joy Joy mdogo wangu nini tena? Umekuwaje kwani eeh mama Shkamoo. James kwa papara na kiherehere alianza kuzungumza huku akitumia kiganja cha mkono wake kujifuta jasho. Alikuwa amevaa mavazi yaliyotangaza dhiki kuu. Joyce hakujibu kitu, mama yake akaamua kuzungumza. Amengangania sasa hatujui tumfanyeje tena. Alisema kwa upole. James akaketi jirani na Joyce ambaye ni mdogo wake toka nitoke. Joyce mimi sina elimu hakika, hata hilo darasa la saba sikumaliza mdogo wangu, lakjni hilo jambo unalotaka kufanya dadangu litakugharimu maisha Joy, hivi unataka mama na baba waanze kupalilia mashamba wenyewe ama shida yako umuue baba kwa presha. Joy kama chumvi inakosekana humu ndani, tutaitoa wapi pesa ya kukupeleka hospitali kwa ajili ya tiba. Hakuna serikali hapa Ukala nadhani unajua ni sisi kama sisi. Joy utatutia wazimu, mtoto wangu huko anaumwa nimeshindwa hata kupata shilingi ya kumnunulia Panado. Joy katazame nimenyonga baiskeli isiyokuwa na upepo ili nije huku mdogo wangu, tuhurumie basi. Eeh! Mambo mengine tumwachie Mungu .unanielewa kadadaa James alimaliza kwa kumuita jina lake la utotoni. Jina ambalo humfanya Joyce atabasamu lakini siku hiyo hakutabasamu, hakika hali ilikuwa tete. Mama! Joyce aliita. Mama yake akanyanyua kichwa na kumtazama, Joyce akawahi kukwepesha macho hakupenda kumtazama mama yake akiwa anatokwa machozi. Kisha akaendelea, Unakumbuka siku ile shambani ulipojikata na jembe tukiwa tunalima? Nakumbuka mwanangu. Mimi sikuwepo ..ni nani aliyefanikisha wewe kufika hospitali. Ni Betty lakini Hakuna lakini mama niache niendelee kuongea .. Joy aligeuka mbogo. Ni Betty na la kuongezea ni kwamb a alitumia ile pesa yake ya ada kulipia huduma hospitali. Nani anajua kama wazazi wake walimtukana, nani anajua kama pesa ile ndo ilikuwa akiba pekee ya wazazi wake? alihoji. Hakuna aliyemjibu, wote walikuwa katika hamaniko. Mtumbwi wa baba ulipovunjika ziwani, wavuvi waliozama kumtafuta ni ndugu zake ina kabla hajaendelea sauti nzito ya kukaripia kutoka chumbani ilichukua hatamu. Joyce nitakupiga bakora nitakuharibu sura yako malaya wewe nasema sitaki uniunganishe katika upumbavu wako huo..tena Joy ukome nasema Kimya kikatanda mzee Kisanga alikuwa ametetemesha. Baba Joy usimuite mtoto Malaya lakini nini baba . Na wewe kimya pumbavu kabisa wewe na mtoto wako tena unganikeni basi tuone kama mtanipunguzia chochote, kwa hiyo mnafichiana tabia zenu sivyo . Wakati mama na kaka yake Joyce wakiwa wameinama bila kujua nini cha kufanya, mzee Kisanga akiendelea kupiga makelele. Joyce alisimama kwa unyonge kama asiyekuwa na mipango yoyote kichwani, kwa kumtazama alikuwa ameathirika na kauli za baba yake. Mama yake akanyanyua kichwa akamtazama. Kilichofuata hapo hakuna ambaye alitarajia kingeweza kutokea. Ulisikika mchakato wa mara moja. Walipochelewa kwa sekunde kadhaa walikuwa wamempa nafasi Joyce. Nafasi hadimu kabisa. We Joy wewe .njoo hapa nikikukamata Joy njooo!! James, kaka yake Joyce alipiga kelele za hamaniko wakati Joy akionekana kwa mbali akiinyonga baskeli huku akiwa amesimamia. Mwendokasi alioondoka nao ni wanawake wachache wanaweza kuumudu. Nini? Amekuwaje eeh! sauti ya mzee Kisanga ikaingilia mshangao wa mama na mwana. Wakageuka na kumtazama bila kumjibu kitu chochote. Akatukana kikerewe huku akiingia ndani na laana zake zisizokuwa na mlengwa. Joyce alikuwa ametoweka. Wewe na wewe ..nawapa masaa matatu aaah manne..namtaka mwanangu hapa . Maajabu sio huyu alisema yule Malaya ni mtoto wa mama yake!! Mama Joyce na mtoto wake wa kiume wakastaajabu, lakini hawakusema lolote kwani tabia ya mzee Kisanga waliijua fika. Wakatoweka bila kuwa na uelekeo maalum. Huku kila mmoja akijitahidi kulaani kitendo hicho kuliko mwenzake.
****
Uguma wa maisha katika kisiwa cha Ukala wilaya ukerewe haikuwa simulizi mpya. Sema ilikuwa haizoeleki, si kwa wageni wala wazawa. Wapiga kura walitegemea kushibisha matumbo yao kwa uvuvi mdogomdogo ambao viongozi waliuita haramu, kilimo nacho hakikuwa uti wa mgongo wa maendeleo na badala yake mavuno yaliyopatikana yalitumika kama chakula tu baada ya mahindi kusagwa na jiwe la mkono na kuwa unga wa kupikia ugali na uji kwa watoto wadogo. Huduma za kiafya zilikuwa mbali sana huku wakazi wengi wa kisiwa hicho wakitegemea hospitali ya Murutunguru ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya wanachuo na wanafunzi wa shule za sekondari Murutunguru. Licha ya huduma hizi mbovu ambazo zilionekana ubovu wake katika kipindi cha kampeni na mikutano ya kisiasa, bado wananchi walitembelewa na wageni waliojiita wataalamu na kuwahusia kuhusu kutoa damu kwa lengo la kusaidia ndugu zao na pia kwa akiba ya siku za usoni iwapo watakumbwa na jambo lolote litakalohitaji damu. Changia damu sasa kwa uhai wako na wa jamaa zako hiyo ilikuwa kauli mbiu iliyokaririwa hassahasa na watoto wa shule za msingi ambao viatu kwao vilikuwa anasa. Wazawawakajipanga foleni na kutolewa damu hasahasa baada ya kupimwa uzito. Betty na Joyce walikuwa kati ya wasichana wachache waliohamasika na tungo hizo za kuburudisha kutoka kwa wataalamu. Walihamasika kwa sababu walikuwa na kumbukumbu ya baba yake Betty kupoteza uhai kwa kupungukiwa damu mwili, ikakosekana damu ya ziada ya kuongezewa. Baba yake Betty akaaga dunia huku akilalamika kuwa anakufa kwa sababu ya umaskini. Laiti angekuwa na pesa angekimbizwa mkoani Mwanza, huko angepata tiba madhubuti na hakika asingepoteza uhai. Kwa hiari yao huku wakitabasamu wakajitolea damu kwa ajili yao na ndugu zao. Lile tabasamu likatoweka zilipoanza kusikika tetesi kuwa wagonjwa wanauziwa damu kila wanapohitaji huduma hii. Ina maana hawa si ndugu zetu!! Betty na Joyce walijiuliza. Nani angewajibu Lisilokufika huwezi kulijua uchungu wake hadi likukumbe moja kwa moja. Zile tetesi kuwa damu ianuzwa tena kwa bei ghali; hazikuwa tetesi tena, mama yake Betty alikuwa matatani. Upungufu wa damu ulikuwa umemuweka katika kitanda cha zahanati ya kijiji. Lilikuwa tukio la kushangaza ambalo lilianzia shambani mfanowe tamthilia ya kufikirika.
"Uuuuuuwiii" kilio kikali kilisikika kutokea shambani walipokuwa wanalima ilikuwa sauti ya mamake Betty akitoa kilio cha uchungu tena uchungu mkali.. "Mamaaaa weeeee nakufaaaa" alipiga kelele huku akiliachia jembe lake, Betty alisikia kilio kile cha mtu mzima mbio mbio kuelekea alipokuwa mama yake huku Joyce naye akifuatilia nyuma kwa kasi lakini ajabu yeye (Joyce) ndiye aliyewahi kufika kabla ya Betty. Mama Betty alikuwa chini akilia kwa maumivu makali, damu ilikuwa inaruka juu kama mkojo wa mtoto mdogo aliyekuwa amebanwa muda mrefu na sasa uvumilivu umemshinda akawa ameuachia, jembe lilikuwa limejeruhi mguu wa mama Betty, bila kupoteza muda huku Betty akishangaa Joyce alivua blauzi yake ambayo zamani lilikuwa jeupe kwa ajili ya shule lakini sasa lilikuwa na rangi ya vumbi kutokana na shughuli za kilimo huku likiwa limechanika makwapani, alipolivua akabakiwa na sidiria ya njano iliyofubaa aakaizungusha kwenye mguu wa mama Betty kwa ustadi mkubwa kisha akashauri wajikongoje kwenda nyumbani kwa msaada zaidi. "Hapana Joyce, najiskia vizuri naweza kuendelea kulima." mama Betty alisema kwa sauti ya chini huku akiukunja uso wake kukabiliana na maumivu ya jeraha lile. "Hapana mama hapana hiyo damu haijakatika hata kidogo inaendelea kuvuja, twende walau tukaweke chumvi kidogo itasaidia japo kukausha" Joyce alipinga vikali akisaidiwa na Betty, wote hawa walitumia taaluma yao ndogo waliyopata katika somo la sayansi walipokuwa shuleni, mama hakuwa na la kupinga walielekea nyumbani huku ile shati aliyofungwa mama Betty ikizidi kuwa nyekundu. Wekundu wa damu!! Walipokelewa na wazazi wa Joyce kwa huzuni huku kila dakika mama Betty akitoa shukrani kwa Joyce kwa ukarimu na huruma aliyoonyesha kwake. Mguu wa mama Betty ulipofunguliwa hali haikuwa shwari bado damu ilikuwa inavuja kudhihirisha jembe lilikata mshipa mkubwa wa damu, hata chumvi aliyowekewa haikusaidia kitu zaidi ya kupotelea kwenye dimbwi la damu kimaajabu. Ilistaajabisha hakika!! "Nahisi nachoka na ninaishiwa nguvu .nahisi kizunguzungu jamani" alitoa kauli hiyo ya kushtua mama Betty ambaye alikuwa amejikaza kwa muda mrefu, hali iliyozusha hofu kwa kila mtu. Ilikuwa lazima wahofie kwa sababu vifo mfululizo vilitokea katika namna hiyo ya kustaajabisha. Bila kuaga Joyce alichomoka mbio na kurejea baada ya dakika 20 akiwa na baskeli, alikuwa anahema juu juu, jasho likiwa linamtiririka. "Twende hospitali" aliomba Joyce na wote wakatii amri mama Betty akapandishwa kwenye baskeli "Sidhani kama nitafika" alianza kulalamika jambo ambalo lilimrejesha Betty kwenye kumbukumbu ya kifo baba yake alijisikia upweke sana kwa mara nyingine alikuwa anataka kukubali mama yake afe kizembe, Joyce hakuacha kumfariji na kumtia moyo. **** Ilikuwa kama bahati usafiri wa mtumbwi kuvuka visiwa vya Ukara kuelekea Ukerewe ambao zamani ulikuwa wa tabu sana kutokana na wavuvi kuwa bize na zoezi la kuvua samaki na dagaa muda wote lakini tangu serikali ipandikize kampuni ya kigeni ya "Fisheries" kutoka Uswisi ambayo ilitawala maeneo yote yaliyosifika kwa kuwa na wingi wa samaki wavuvi wazaliwa wa hapo hawakuwa na shughuli za kufanya tena, hali ilikuwa ngumu sana. Hivyo mitumbwi yao wakaigeuza matumizi na kuwa ya kuvushia maskini wenzao. Kisiwa kimoja kwenda kingine. Ujio wa akina Betty na mgonjwa wao ilikuwa kama bahati ya mtende walipokelewa kama wafalme na kugombaniwa kama mpira wa kona tena katika dakika za majeruhi, gharama za mtumbwi uendao kasi kwa sababu ya kuwa na injini, shilingi 5000 iliwashnda hivyo iliwalazimu kuchukua mtumbwi wa kawaida wa makasia ambao kulingana na hali ya mama Betty ilikuwa ni kama kucheza bahati nasibu. Bahati na sibu na roho ya mwanadamu!! "Mungu atakuwa nasi" baba Joyce aliwaambia wenzake wakati wakiijiandaa kupanda ndani ya usafiri huo.
"Mama Joyce wewe rejea nyumbani ukatazame watoto na mji mimi na Joyce tutaongozana na Betty huko Hospital. Alianza kupakiwa mgonjwa, baadaye baiskel na kisha wakapanda watatu hawa kwenye mtumbwi ambapo wapiga makasia wawili walikuwa wametangulia. Mtumbwi wa kubeba watu wanne ulikuwa na idadi ya watu sita sasa. Utata!! "Ee Mungu weka mkono wako katika safari hii" Lilikuwa ombi la Joyce wakati mtumbwi ukiachia nanga yake.na makasia kuanza kupigwa kwa kasi sana. Alijua kuwa walikuwa katika hali ya hatari lakini wangefanya nini kama serikali haikuwa ikijali lolote kuhusu wao.
* * * *
Baba yake Joyce alinyonga baiskeli kwa kasi, mgonjwa akiwa ameshikilia kiti cha mbele kwa nguvu sana. Joyce na Betty walifuata kwa nyuma mbiombio kwa miguu huku wakiwa peku wote hawa dhumuni lao kufika mapema katika kituo cha afya cha Murutunguru. Pancha katika matairi yote haikuzuia safari kuendelea. Ilikuwa ni bora kuacha kuziba pancha lakini wawahi kufika hospitali. Nguvu zilikuwa zinazidi kumwishia Mama Betty japo damu zilikuwa zimekatika sasa kama ni kweli zilikuwa zimekatika. Huenda zilikuwa hazijakatika bali zilikuwa zinaelekea kuisha mwilini. Saa tisa alasiri walikuwa tayari chumba cha daktari, Joyce na Betty wakiwa hoi kwa kukimbia mwendo mrefu sana bila kupumzika wakati mama Betty alikuwa amepewa dawa aina ya PPF kwa ajili ya kukausha damu na Panadol kwa ajili ya kupunguza maumivu, hizo ndio dawa zilizopatikana hapo pamoja na Asprin, pilton na dawa mseto za malaria kwa uchache. Kwa waliotoka mjini wangejiuliza kama eneo hilo lina mwakilishi bungeni. "Mgonjwa wenu anaupungufu mkubwa wa damu na ni hatari kwa maisha yake" aliongea daktari huyu ambae vazi lake jeupe lilikuwa limechakaa sana huku likiwa na matundumatundu kama limeliwa na Panya. "Na kituo chetu hakina akiba ya damu mpaka Bugando Mwanza" "Kwa hyo tunatakiwa kufanya nini?" alihoji. "Kama hamwezi kwenda Mwanza kuchukua au kama yupo wa kujitolea atoe kuokoa maisha yake" "Nitajitolea mimi" alijibu haraka Baba Joyce. "Damu yako ni kundi gani??" aliuliza daktari. "Mh! sifahamu kwa kweli" alijibu
"Haya nifate huku ukapime kwanza" palepale alisimama daktari akifuatiwa kwa nyuma na Baba. Joyce hadi chumba chakavu kilichoandikwa kwa kutumia mkaa "MAABARA"
"Mgonjwa wenu kundi 'O' na wewe ni kundi 'B' haiwezekani hata siku moja" alitoa majibu daktari baada ya kuipima damu ya mgonjwa na baba Joyce. "Tunafanya nini sasa tena Daktari?" alirudia kuuliza lile swali tena baba Joyce "Ni kama nilivyokwambia agiza kutoka Mwanza" alijibu kwa ukali wakati huu. Kijasho chembamba kikamtiririka babake Joyce, wakati huo Betty na Joyce walikuwa mlangoni wakisikia maongezi yanavyoendelea. "Sasa....aah! Mwanza mh!" "Ndio ni shilingi elfu thelathini tu chupa moja ." daktari alimwambia huku akikunakuna kichwa chake chenye mvi. Kisha akamalizia, Nadhani hiyo itamwongezea siku za kuishi.
"Kama shilingi 5000 ya imetushnda itakuwa 30000?" alijiuliza baba Joyce huku akisimama na kutoka nje ambapo aliwakuta Betty na Joyce. Hakuwa hata na la kusema zaidi ya kuwakodolea macho yaliyokata tamaa kabisa. "Basi mimi nina dadu ya kundi 'O' niruhusu nitoe" alisema Joyce kwaq kiherehere akikumbuka majibu aliyopewa juu ya kundi la damu yake siku alipojitolea damu, jambo ambalo mzazi wake alipinga vikali kwa kuhofia usalama wa mwanae huyo mkubwa kutokana na umri wake kuwa mdogo.. Mgogoro ukaanzia hapa na kusafiri hadi nyumbani, wazazi wakipingana na Joyce. Joyce akisimamia msimamo kuwa anaweza kutoa damu na kumwokoa mama yake Betty . Huu ukawa utata ulioishia katika mtafaruku, Joyce akakimbia na baiskeli akiwaacha mama na kaka yake wakitukanwa Akakimbilia alikotambua yeye na akili yake
*****
***JE? Baada ya mgogoro na wazazi wake JOYCE amekimbilia wapi na ile baiskeli?? Na anataka kufanya nini ambacho wazazi wake wanampinga???
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.