hakika shukrani za kipekee zikufikie mzaramo popote ulipo.
Riwaya hii ni kama inasadiki mateso makali wanayopitia dada zetu huko mashariki ya kati siku hizi. Viongozi wakubwa kama kina Mtemvu wameanzisha taasisi eti hupeleka wasichana kwenda kufanya kazi za ndani loool wakifika huko ni mateso na udhalili mkubwa wanakutana nao. Hawana cha Inspecta Zay B, Sajenti Pilipili wala IGP Sungura wa kuwatetea wishowe kabisa hurudi nchini na madera matatu mapya na shuka mbili na kuja kuanza upya maana ujira wao wameshadhulumiwa.