tupe nyingine
Shukrani kwako ndugu sizizo na mwisho
Shukrani kwako ndugu sizizo na mwisho
Mimi! Kitenge aliropoka akiwa hajui la kufanya.
Wewe! Machozi alijibu. Sauti yake haikuwa ya kebehi tena, wala
haikujali kuweka furaha ya kinafiki. Ilikuwa wazi ikitangaza kulipiza
kisasi na uadui.
Wewe! aliongeza, Na nilichokuja kukuambia si kukuomba unioe au
unipe pesa za kutumia, la. Nimekuja kukuambia kuwa nakuchukia.
Ninakuchukia kama ninavyomchukia shetani. Sasa hivi, mimi ni kama
maiti ambaye hajaanza kunuka tu. Sina mbele wala nyuma. Lakini
kabla sijaoza nitahakikisha na wewe unalipa gharama za madhambi
yako. Lazima twende wote ahera Mungu akatuamulie nani mwenye
haki. Nitakuua Boni. Tena kwa mkono wangu huu! Aliutikisa mkono
huo huku akiinuka na kuanza kutoka.
Mlangoni aligeuka na kuanza kumtazama Kitenge. Kwa heri, alisema,
Tutakapoonana tena, ujue ndiyo mwisho wa uhai wako. Akatoka na
kutoweka.
Kitenge alibaki akiduwaa juu ya kiti chake. Aliyemzindua ni mama
mwenye nyumba, kikongwe ambaye huwa hapitwi na neno lolote
humo au nyumba za jirani. Alibisha hodi na kusimama mlangoni.
Baba, mwanamke huyo ni nani? aliuliza.
Simfahamu. Nadhani ni mwendawazimu, Kitenge alilaghai akiinuka
na kuelekea bafuni.
Anasema anakufahamu.... jihadhari baba, sauti ya Bi mkubwa huyo
ilimfuata.
Hakujishughulisha kumjibu.
Baada ya kicheko kingine Machozi aliongeza, Nimekuja mpenzi,
nimekuja kukukumbusha ahadi hiyo, kama umesahau. Nyumba yako
hii nimeitafuta mwaka mzima, leo ndiyo nimeipata. Nimefika
nyumbani, kwa hiyo wewe nenda zako kazini utanikuta mkeo
nimekuandalia kila kitu. Au ulianza kusahau mapenzi yetu hadi ukaoa
mke mwingine?
Bado Kitenge aliamini Machozi alikuwa akimkebehi, hakuwa amesema
alilokusudia. Hata hivyo tayari alianza kupandwa na hasira, huku
akiificha hasira hiyo katika sauti yake alisema, Sikia Machozi, mimi
sina muda wa kupoteza. Kama umechanganyikiwa nenda mahala
ukazungumze yote unayotaka kuzungumza. Hapa sipo kabisa. Sasa
inuka utoke zako.
Kweli mpenzi tuseme umesahau ahadi zako zote?
Toka
. umesahau barua zako tamu
uende zako haraka!
.zenye kila neno la mapenzi na ahadi za kuishi pamoja?
Nasema toka!
Pamoja na jinsi nilivyokupenda nikajitoa kwako mwili na roho?
Umesahau kweli mara hii? Siamini!
Ana wazimu mwanamke huyu? Kitenge alijiuliza. Mapenzi!
Mapenzi gani hayo ambayo hakumbuki? Kwa kadri ya kumbukumbu
zake, neno nakupenda wakati huo lilikuwa moja ya michezo ya
kawaida mongoni mwa watoto. Angeweza kumwambia yeyote wakati
wowote wewe ni wangu wa heri na shari, kadhalika angeweza
kusikiliza jibu lolote la msichana yeyote na kumwamini.
Halikuwa jambo la ajabu mtu kumwambia mtu nikila sishibi kwa ajili
yako au usiku silali. Karibu kila mvulana alikuwa na faili kubwa la
barua za mapenzi. Barua hizo zilikuwa zikiandikwa kwa ufundi au
kunakiliwa kutoka vitabuni huku zikiwa zimenakshiwa kwa maua ya
kuvutia pamoja na kupambwa kwa harufu ya poda. Machozi alikuwa
na akili gani hadi leo hii kuendelea kuamini mambo kama hayo?
Mchezo wa mapenzi, vichakani na hata nyumbani ni jambo lililokuwa
la kawaida pia. Ingawa Kitenge hakuwa mpenzi sana wa mchezo huo,
lakini Machozi alikuwa mmoja tu katika orodha ndefu ya wasichana
aliowahi kufanya nao mapenzi.
Yalitokea, yakatoweka. Yeye Kitenge baada ya kufaulu darasa la saba,
akiwa mtoto pekee aliyetoka katika kijiji hicho cha Mayange, wilayani
Kasulu, alijibidiisha zaidi katika masomo yake. Kila aliporudi likizo
wasichana wote walimlaki kwa furaha na kuridhia lolote alilotaka;
Machozi akiwa mmojawao.
Alipohitimu kidato cha sita na kupata kazi hapa Dar es Salaam, alikata
mguu kijijini hapo. Hakuwa na muda wa kutosha kumfikisha huko
mara kwa mara kutokana na shida ya usafiri. Huu ulikuwa mwaka
wake wa sita tangu alipofika huko kwa mara ya mwisho. Likizo ya
mwaka huu alikuwa akijiandaa au kutarajia kuwa angeenda. Katika
mapya na mageni yote aliyotarajia kuyakuta huko nyumbani, hili
hakulitarajia kabisa.
Unatoka katika nyumba hii au hutoki? aliuliza ghafla.
Machozi hakumjibu haraka. Alitazama huku na huko kisha akasema,
Nikisema sitoki nadhani utaniitia mgambo. Vizuri sana. Sasa
nitasema dhamira ya safari yangu hii; ilikuwa ni kukupa hongera,
ndiyo, lakini si hongera ya mafanikio ya kuandika kwako vitabu. Ni
hongera kwa kufanikiwa kwako kuniharibia maisha yangu. Kwa
kunidanganya hata nikadanganyika na kuamini kuwa ulikuwa
wanipenda kumbe la. Haukuishia hapo, ukanijaza mimba na kisha
ukaikana. Hongera sana Boni.
Ndipo Kitenge alipokumbuka kuwa aliwahi kupata barua moja kutoka
kwa baba au mmoja wa wadogo zake ambaye alidai kuwa amemtia
mimba msichana mmoja. Ati aende akamuoe! Wakati huo, Kitenge
alikuwa ndiyo kwanza anaanza kazi. Wazo la kuoa, na hasa kumuoa
mtu kama huyo, lilikuwa nje ya ratiba yake a maisha. Hivyo suala hilo
alilipuuza. Hakumbuki kuwa aliwahi kujibu barua hiyo. Kumbe ilikuwa
kweli? Yaweza kuwa kweli? Alijiuliza.
Nikikuruhusu kusema utaanza kuikana mimba hiyo. Waweza hata
kudai kuwa hukuwahi kufanya nami mapenzi japo ni wewe
uliyeniharibia ubikira. Napenda kukufahamisha kuwa mwanao alikuwa
msichana. Nilimtupa katika mapipa ya takataka za hospitali ya
Maweni. Kama walimwokota akiwa hai au maiti, sijui. Sikujali. Najua
na wewe hujali wala usingejali. Machozi akanyamaza akimtazama
Kitenge kuona hadithi yake ilimwingia vyema.
Alipomwona akitoa macho ya mshangao aliongeza: Usiseme
unasikitika, najua una moyo wa jiwe kama mimi. Ingawa mimi
sikuzaliwa na moyo huo, nimeupata ukubwani kwa haki kabisa ingawa
nikiiambia hivyo jamii haitanielewa.
Akasita kidogo na kuendelea, Ninachotaka kueleza ni taabu
niliyoipitia baada ya kumtupa mtoto huyo. Njaa ilinifanya niangukie
mikononi mwa mwanamume mwingine. Huyu, tangu awali nilijua
ananilaghai, lakini sikuwa na njia ya kumzuia asinitie mimba nyingine.
Alipogundua nina mimba aliniepuka, ikabidi niteseke sana kutunza
mimba hiyo bila mafanikio. Mwisho, niliamua kumeza dawa za kuitoa.
Ilitoka kwa taabu, nami niliponea chupuchupu. Nilipopata nafuu
zawadi yangu ilikuwa kifungo cha miaka mitatu.
Majuzi tu ndiyo nimetoka jela. Maisha yangu yamekuwa mpira usio
na thamani. Unaochezwa na kila mwanaume atakaye. Nadhalilishwa,
naonewa na kufanywa kiumbe duni asiye na haki ya kuwa hai. Yote
hayo ni kwa ajili yako Boni. Ni wewe uliyenivuta katika mkondo huu
ukahakikisha siwezi kutoka.

RIWAYA: NAJISIKIA KUUA TENA
MWANDISHI: BEN R. MTOBWA
**** **** **** **** ****
SURA YA KWANZA
POLISI kikosi cha kumi na mbili Inspekta Kombora anaongea. Nani
mwenzangu?
Kwa muda kukawa kimya. Kombora alisikiliza kupumua kwa dalili ya
hofu katika chombo cha simu kutoka upande wa pili. Nani
mwenzangu? akaongeza nguvu kidogo.
Ni Kombora mwenyewe anayeongea? iliuliza sauti hiyo yenye
wasiwasi kutoka upande wa pili.
Ni mimi, nani mwenzangu?
Ndiye! Mkuu wa kituo hicho sio?
Ndiye, tu
Sikiliza Inspekta, sauti ilidakia na kunongona harakaharaka, Nina
tatizo zito sana. Sijui kama utaweza kunisaidia.
Nadhani tunaweza. Tutajie tatizo lako na jina lako ili tujadiliane.
Jina sitaji, iliongeza sauti hiyo, Na tatizo lenyewe ni zito sana, siyo
mzaha. Najisikia kuua mtu Inspekta. Najisikia kuua. Na ni lazima niue.
Waweza kunisaidia Inspekta?
Kuua! Kombora aliropoka. Katika matatizo yote, hilo kamwe
hakulitegemea. Ni rahisi mtu kupiga simu polisi na kusema mtu
anataka kuniua. Ni rahisi pia mtu kudai nilimwona fulani akiua
lakini nataka kuua lilikuwa jipya kwa Inspekta Kombora.
Angeweza kulichukulia suala hilo kwa mzaha; kwamba ni chizi au
mlevi mmoja ambaye ameamua kuwasisimua polisi lakini uchizi au
ulevi haukuwemo kabisa katika sauti hiyo. Ilikuwa sauti dhaifu iliyojua
kipi inasema. Kwa muda Kombora aliduwaa akiwa hajua lipi amjibu
mtu huyo.
Upo Inspekta? ilihoji sauti.
Nipo ndugu yangu, Kombora alijibu kwa unyonge.
Mbona kimya? Huna msaada wowote?
Ninao. Sikia rafiki yangu, njoo zako hapa mara moja ili tukae na
kulijadili tatizo. Naamini tutakusaidia.
Hilo sifanyi Inspekta. Nikija huna uwezalo kufanya zaidi ya kunitia
ndani, na mimi nauhitaji uhuru wangu. Kama huna msaada
mwingine
Ninao. Ni hivi, u nani jina lako?...Uko wapi?...Na unayetaka kumuua
ni nani Kwa nini?...Haloo!...Haloo!...
Haikumchukua muda Kombora kungamua kuwa alikuwa
akizungumza katika simu iliyokatwa. Kwa muda aliendel;ea kuduwaa,
simu mkononi, macho kayakodoa kutazama ukuta uliokuwa mbele
yake, akiwaza mengi. Kisha alitua simu na kuinuka. Mara
akakumbuka kuwa hakujua anakotaka kwenda. Akaketi na kutikisa
kichwa kwa wingi wa mawazo mazito yaliyomjaa ghafla.
********
KITENGE alizinduka kutoka usingizini kwa kugutuka kidogo. Hakujua
kilichomwamsha ghafla hivyo. Akatazama huku na huko kama
anayejaribu kutafuta kitu hicho kilichomfanya auache usingizi wake
ambao haukuwa na ndoto yoyote.
Mara mlango ukagongwa tena, ndipo alipokumbuka kuwa
kilichomwamsha ni mlio wa mlngo huo. Kwa dalili za uchovu aliinuka
kutoka kitandani na kuvuta taulo iliyokuwa juu ya kiti, akaitanda
kiunoni, kisha aliuendea mlango na kuufungua.
Mlango huu ulimfikisha ukumbini ambapo alipita kuuendea mlango
mkubwa, macho yake yakiipitia saa ya ukutani ambayo ilidai kuwa ni
saa kumi na mbili kasoro dakika nne, jambo ambalo lilimshangaza
mno, kuona ugeni wa alfajiri kama hiyo.
Alifungua mlango; aliyesimama hapo nje alikuwa ni mwanamke
ambaye Kitenge, baada ya kumtazama kwa muda, alimkumbuka.
Alikuwa ni Machozi Rashidi. Mwanamke ambaye alipokuwa msichana
waliishi jirani na Kitenge wakihusiana kwa njia mbalimbali katika
harakati za maisha baina ya wasichana na wavulana.
Kitenge hakujua kama ilimpasa kumkaribisha au la. Kwa kila hali huyu
hakuwa yule Machozi ambaye Kitenge alimfahamu wakati ule. Huyu,
wakati ulikuwa umemwathiri sana na kumtenga mno na Kitenge kiasi
cha kumfanya aionee aibu kila dakika ambayo aliendelea kusimama
naye hapo mlangoni.
Hakuwa mwanamke wa haja hata kidogo. Kama aliwahi kuwa mzuri,
Kitenge hakuiona dalili yoyote ya uzuri iliyosalia katika sura hiyo.
Sasa ilikuwa sura kavu, yenye mikwaruzo mingi, macho mekundu kwa
athari ya kitu kama gongo au bangi, nywele nyekundu, kavu zenye
dalili zote za kutoonja aina yoyote ya mafuta. na mwili mzima ulikuwa
na mikwaruzo juu ya ngozi hiyo kavu na ilikuwa dhahiri kuwa
mwanamke huyu aliishi kwenye mazingira yasiyofaa. Ngozi hiyo
ilifunikwa na mavazi hafifu ambayo pamoja na kuwa dhaifu yalikuwa
yamechanika hapa na pale.
Haunikaribishi Boni? aliuliza mwanamke huyo. Sauti yake pia
ilikuwa tishio jingine, haikuwa ya mwanamke hata kidogo, wala
haikumfaa mwanamume. Boni lilikuwa jina la utotoni la Kitenge
ambalo sasa lilikuwa limetoweka kabisa baada ya majina mengine
kuibuka, majina ambayo yalifungamana na hadhi yake mpya. Kwani
sasa Boni alikuwa mwandishi maarufu wa vitabu.
Ghafla jina hilo likamkumbusha uhusiano wa kimapenzi aliokuwanao
awali na kiumbe huyu.
Ingia, alimwambia.
Mwanamke huyo aliingia ndani na kufuata moja ya makochi sita
yaliyopangwa kistaarabu katika ukumbi huo. Alitazama kila upande
akihusudu hiki na kuvutiwa na kile. Kisha akamtupia Kitenge macho
yake mabaya. Hongera, akakoroma kwa sauti hiyo ya kuchukiza.
Kwa?
Vitabu vyako. Hukujua kuwa hata sisi washamba ambao hatukusoma
tungeweza kuviona? Ulidhani kuwa tusingeona hata picha nyuma ya
vitabu hivyo? Ama hujui kuwa hata redioni vinaongelewa? Pamoja na
hayo, ningependa kukujulisha kuwa ingawa sikusoma sana, naweza
kuelewa waandishi wanasema nini katika magazeti yao. Karibu wote
wanakusifu. Hongera tena Boni.
Kitenge hakujua kwamba ilimpasa kufurahi au kuchukia kwa sifa hizo.
Kusifiwa halikuwa jambo geni kwake. Tangu alipotoa kitabu chake cha
kwanza, MACHOZI YA DAMU, kupata sifa lilikuwa jambo la kawaida.
Kitabu cha pili, KIFO USONI, kilimzidishia sifa kemkem, cha tatu na
ambacho ni kama cha mwisho katika vitabu vilivyokwishatolewa;
ALIKUFA ANACHEKA, kilifanya sifa zitapakae pembe zote kiasi cha
kumtia katika mashaka ya kukosa nafasi ya kufikiria vitabu vingine.
Kila alikopita aliandamwa na hongera, yeyote aliyemfahamu
alimtupia tabasamu. Waandishi wa habari walimtaka picha na
mahojiano mara kwa mara. Katika baa moja aliwahi kuona maandishi
yanayosema Kondokondo Kitenge zaidi na kadhalika. Hata katika
basi ilikuwa ni jambo la kawaida kukuta kikundi cha watu kikizijadili
sifa zake.
Naam, kusifiwa kwake sasa lilikuwa jambo la kawaida. Lakini sifa hizi
za alfajiri, kutoka kwa mama huyu aliyechoka kwa sauti yake
ambayo licha ya kuchakaa, ilidhihirisha kitu kama kebehi, unafiki au
uadui katika sifa hizo, zilimfanya ghafla ahisi jambo lisilo la kawaida
katika nafsi yake. Wasiwasi ukamwingia rohoni. Wasiwasi ambao nafsi
yake ilipokonywa na hasira, akajikaza kisabuni kumtazama mama
huyo huku akisema, Nadhani hukuja asubuhi yote hii kwa ajili ya
kunisifu. Niwie radhi, kama huna zaidi, nenda zako ili nijiandae
kwenda zangu kazini.
Machozi akacheka. Kicheko chake kilikuwa kitu kingine cha kutisha,
na kilikuwa mbali kabisa na kicheko cha mwanamke, na karibu zaidi na
kile cha shetani.
Nilitegemea hutasema hayo, alisema. Najua umekuwa mtu mkubwa
na tajiri sasa. Umetoa nakala elfu ngapi hadi sasa? Haikosi una akiba
ya milioni benki. Mungu akujalie, akacheka tena. Bila kusubiri jibu la
Kitenge, aliongeza, Ndiyo nimekuja kukusifu, kwani hukumbuki kuwa
mimi ni mpenzi wako? Hukumbuki kuwa uliniahidi kuwa bila mimi
usingeishi? Kwamba lazima tungeoana tu. Hukumbuki?
Kitenge aliduwaa, hakujua mwanamke huyu anaelekea wapi katika
maongezi hayo. Hivyo akaamua kunyamaza akimtazama.