Riwaya: Najisikia kuua tena

Riwaya: Najisikia kuua tena

m2n

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2013
Posts
411
Reaction score
63
Riwaya: Najisikia kuua tena
mwandishi: Ben r. Mtobwa
 
mwenye riwaya ya simu ya kifo aiweke pia hapa jukwaani m2n
 
Last edited by a moderator:
mkuu endelea basi mbona mnatukata stimu sio fresh hivyo
 
At last naona mambo yanazidi kunoga hili jukwaa. Tuko pamoja mkuu
 
mode naomba muanzishe jukwaa la riwaya kwan ni miongon mwa vitu vyenyw wapenzi wa kutosha. Ben mtobwa ni miongon mwa wandishi wanaonivutia sana. asante sana kwa kuileta jf
 
Salute mkuu m2n Joram Kiango kanikosha na 'biti' zake
 
Last edited by a moderator:
Wapi Willy Gamba 1 unamfikia Joram kwa mbinu za kijasusi?
Njoo uone mwenzio huku yupo mzigoni. Njoo umsaidie hahaaa hahaaaa
 
Last edited by a moderator:
sijawahi kusoma za JK lkn sizioni ktk ubora walau nusu ya Willy Gamba. ngoja nione
 
Joram hakumjibu, aliondoka zake
polepole lakini kwa hadhari zaidi.
Dakika kadhaa baadaye, hakuwa Joram Kiango yuleyule tena. Alikuwa
mtu mwingine aliyebadilika kimavazi kiasi cha kuweza kumchanganya
mtu yeyote. Sasa alivaa suti yake nyeusi, tai nyeusi, shati jeusi na
kofia nyeusi. Kitu pekee cheupe mwilini mwake kilikuwa ni kitambaa
cheupe alichofunga shingoni.
Kitambaa ambacho kukiondoa hapo kungemfanya aonekane kivuli au
sehemu ya kiza ambacho kilitanda kwa silaha zake ambazo ni pamoja
na bastola, visu, nyembe, tochi yenye ukubwa wa kalamu na dawa
ambazo humsaidia katika shughuli zake.
Akiwa karidhika na hali yake, aliyaacha makazi yake, sehemu za Ilala
na kukiendea kituo cha basi ambapo alijiunga na watu waliokuwa
wakisubiri usafiri wa kwenda mjini kufunga siku kwa starehe za dansi,
sinema na vinywaji.
Hayo yalikuwa yakitokea dakika arobaini na tano tu baada ya Joram
kumwacha mahututi yule jambazi aliyekuwa akimnyemelea katika
vichochoro vya Mtaa wa Jamhuri. Alikuwa amesafiri harakaharaka,
akisaidiwa na usiku ambao ulianza kutawala na kumficha asionwe na
gaidi mwingine na kuweza kusumbuliwa pindi akienda kwake.
Alipofika nyumbani alipiga simu ya haraka kwa katibu wake
kumjulisha hali ilivyo, kisha hima akaanza kubadili mavazi na baadaye
kujitokeza mitaani akiwa kama alivyo. Sura ikionyesha utulivu, mavazi
yakitangaza starehe hali rohoni kabeba furushi la mashaka na taharuki
kwa kufikiria jukumu lililokuwa mbele yake.
Hofu yake haikuwa juu ya maisha yake, ingawa kwa mujibu wa taarifa
ya yule jambazi aliyepambana naye dakika chache zilizopita,
alifahamu kuwa anaelekea eneo la hatari sana. Hasa, hofu yake
ilikuwa juu ya maisha au usalama wa mtu aliyekuwa akimfuata;
Dismas Komba. Aliamini kwamba yupo mashakani. Moyo
ulimshawishi kufanya haraka sana ili kujaribu kumtoa katika hatari
hiyo.
Lilitokea basi lielekealo Posta, Joram alikuwa mtu wa kwanza
kulidandia. Na lilipowasili aliwatangulia wote kuteremka. Akafanya
haraka kuchukua teksi ambayo ilimfikisha Ferry ambako alijiunga na
wavuvi pamoja na watu wengine waliokuwa wakinunua samaki. Alijitia
mteja wa kawaida lakini macho yake yalikuwa kazini yakisoma sura za
watu kuangalia kama alikuwepo yeyote kati ya maadui ambao
walipewa jukumu la kutokumruhusu kufika Kigamboni. Aliporidhika na
nyuso hizo alimshawishi mvuvi mmoja, kijana ambaye alikubali
kumvusha hadi upande wa pili kwa shilingi hamsini akitumia ngalawa
yake.
Joram alimsaidia kijana huyo kwa kupiga kasia kwa namna ambayo
ilimchekesha sana kijana huyo kwa jinsi asivyofahamu kazi hiyo.
“Acha tu mzee,” alisema kijana huyo. Kisha alibadili sauti katika
kicheko chake na kukifanya kiwe cha kitu kama dharau ama
mshangao. Kicheko hicho kilifuatwa na swali lililodai, “Yaonyesha u
tajiri sana mzee?”
“Kwa nini? Alihoji Joram.
“Watu wenye fedha ndogo kama mimi si rahisi kukodi mtumbwi.
Pantoni iko pale na inachukua watu bure kwa haraka na usalama
zaidi.”
Ikawa zamu ya Joram kucheka. Kijana huyu hakujua kuwa alikuwa
ameepuka pantoni hiyo kwa hadhari akijua kuwa kama kuna ulinzi
wowote dhidi yake, haikuwepo sehemu nzuri zaidi ya hapo kivukoni.
Hivyo, alikuwa akiepuka kuonekana na jicho ambalo halikustahili
kumwona hasa kwa wakati huo. Lakini alimjibu kijana huyo kwa
kumlaghai, “Siku nyingi mno sijasafiri katika chombo kidogo kama
hiki. Hizo shilingi hamsini nilizokupa ni kati ya mia nilizozipata katika
bahati nasibu. Hazikuwa katika bajeti.”
“Kwa nini basi usingekuja mchana? Saa mbili u nusu za usiku! Utafaidi
nini?”
“Safari ya usiku naipenda zaidi.”
Walipowasili upande wa pili nje kabisa na kituo cha kawaida, Joram
alimshukuru kijana huyu na kisha kuanza safari ya kuingia Kigamboni.
Akiyafuata maelekezo ya yule mtumishi wa Kamata alifikia nyumba
ambayo alidhani ingekuwa ya Komba. Lakini mara baada ya kuuliza
kwa mtoto aliyeketi nje ya nyumba hiyo aligundua kwamba aliikosea.
“Ni ile pale. Si yule Komba wa Kamata?”
“Ndiye.”
“Ile pale.”
Joram alipoanza kuondoka ili aiendee, mtoto huyo alimzuia kwa
kusema, “Unakwenda pale mzee? Hapafikiki siku hizi. Hasa usiku kama
huu!”
“Kwa nini?”
“Pana miujiza sana. Mambo ya ajabu yanatokea katika nyumba ile.
Nadhani kuna jinsi au majini.”
“Kwani vipi bwana mdogo?”
“Mengi yanatukia pale. Wapangaji wote wamehama. Amebaki Dismas
peke yake. Inasemekana kwamba anajifungi achumbani usiku na
mchana. Bila shaka kati ya kesho na keshokutwa atakuwa chizi.”
Joram akajikuta akizidiwa na hamu ya kuyaelewa maongezi hayo.
“Kijana, nieleze vizuri nikuelewe. Unataka kusema kwamba kuna
mambo ya ajabu ajabu yanatokea katika nyumba ile? Kama yapi?
Nieleze hatua kwa hatua.”
“Ni habari ngumu kueleweka. Watu wanadai kuwa kabeba jini kutoka
Unguja alikokwenda hivi karibuni. Tangu alipotoka huko mambo yake
hayaeleweki. Siku ya kwanza aliporudi, alikuwa katika hali ya kawaida.
Usiku huo alisikika akilia na kunyamaza ghafla. Jirani aliyeamka na
kumwendea alirudi mbio akilia ati kapigwa kama jiwe tumboni na mtu
asiyeonekana. Asubuhi waliomwona Dismas walidai kuwa alikuwa
kachubuka usoni na damu ikiwa imekaukia puani. Yasemekana alitoka
ili aende mjini, akaingia katika pantoni na kuvuka ng’ambo, lakini
aliporudi alirudi nalo huku akitetemeka.
“Ni hapo alipoanza tabia ya kujifungia ndani. Yasemekana pia kuwa
wapangaji hao waliohama walikuwa wamelala ndani lakini
walipoamka alfajiri walijikuta wamelala nje, uchi wa mnyama, hali vitu
vyao humo ndani vikiwa vimetapanywa ovyo ovyo. Hata sisi watoto
ambao tumekuwa tukicheza mbele ya nyumba hiyo tumeacha baada
ya mwenzetu mmoja usiku wa juzi kutoweka ghafla na kuokotwa
baada ya muda mrefu kalala ufukoni. Alipoulizwa kilichomfanya alale
huko na vipi alienda huko hakuwa na jibu zaidi ya kushangaa tu.”
“Ni hadithi nzuri,” Joram alimjibu akitabasamu.
“Siyo hadithi. Yametokea na yanaendelea kutokea…”
Joram hakuwa na nafasi ya kumsikiliza zaidi. Mawazo yake tayari
yalikuwa kazini yakiifikiria taarifa hiyo. Macho yake pia yalikuwa
yakipambana na kiza kujaribu kutazama eneo la nyumba hiyo ambayo
kiasi ilijitenga na nyumba nyingine kutokana na utaratibu usioridhisha
wa mjenzi au mpimaji. Nyumba hiyo ilizungukwa na kichaka kikubwa
cha miti au maua yasiyo katika utaratibu mzuri.

Kwa mtu kama Joram ilikuwa ni rahisi kuhisi kichaka hicho kingeweza
kuwa hifadhi nzuri ya mtu au watu waliodhamiria kumtendea Dismas
Komba jambo fulani, si kama walivyodhani watu wengine kuwa ni
majini yaliyofanya yote hayo. Joram alimshuku pia kuwa kile kitendo
cha watoto na majirani kilidhamiriwa kuwaweka watu wote mbali ya
eneo hilo ili wapate nafasi nzuri ya kuendelea na harakati zao.
Harakati ambazo zilikusudiwa kupoteza maisha ya Komba. Kwa nini?
Hakuwa na nafasi ya kujijibu maswali hayo. Damu ilikuwa ikimchemka
na moyo kumwenda mbio huku nafsi ikimshawishi kufanya haraka
kabla halijatukia lolote baya zaidi kwa Komba.
Hata hivyo, baada ya kumshukuru mtoto huyo kwa sauti ambayo
haikuonyesha kuwa kaamini lolote kati ya hayo, aliondoka zake
polepole akielekea upande mwingine. Mikono yake ilikuwa shingoni
kuondoa kile kitambaa cheupe. Mara akawa kama kivuli. Ili kupima
kama alikuwa katika hali ya kuridhisha alipiga hatua mbili nje ya
barabara na kusimama.
Watu wengi walipita bila ya kumwona. Mara alitokea mzee, kafutana
na binti mwenye umri wa mjukuu wake. Walikuwa wakizungumza
mambo ambayo yalimshangaza Joram kupita kiasi. Walipomkaribia
zaidi walisimama na kuendelea na maongezi yao.
Nusura atokwe na kicheko kwa kusikiliza utongozaji huo wa kizamani
mno. Lakini alijikuta akishindwa kustahimili kuondoka pindi maongezi
hayo yalipopamba moto na kubadilika kuwa mahaba kwa mtindo
ambao Joram hakutarajia kuwa binti mdogo kama huyo angediriki
kumtendea babu wa kiasi hicho.
Aliondoka kwa kunyata akiifuata nyumba ya Dismas Komba.
Alipoikaribia alitafuta nafasi nzuri katika kichaka cha maua na kuketi
chini akisubiri.
Alisubiri sana. Kusubiri ikiwa miongoni mwa shughuli zake hakukinai
kuketi hapo, akivumilia mirija ya mbu huku macho yake ambayo
yalikwishazoea giza yakiwa wazi kutazama lolote. Nia yake ilikuwa
ifike saa saba au nane ya usiku ndipo aendelee na safari yake hadi
katika nyumba ambamo alikusudia kuonana na Komba. Kwenda
papara baada ya kusikia ‘hadithi’ ya yule kijana juu ya nyumba hiyo
isingetofautiana na nondo aendavyo katika moto kwa tamaa ya
mwanga.
Joram alipoitazama tena saa yake na kuona ikikaribia saa sita za
usiku, alianza kujiandaa kuisogelea nyumba hiyo. Nia yake ikiwa
ashughulikie dirisha moja au mlango na kuingia ndani ambako
angehitaji kupata hakika kama sehemu ya kiza ikichezacheza hatua
kadhaa mbele yake. Baada ya kutazama kwa makini aliona dalili za
kiumbe hai, kikitembea polepole kuiendea nyumba hiyohiyo. Alikuwa
mtu! Kavaa mavazi mieusi kama yake. Macho ya Joram yaliongeza
juhudi kutazama kama mtu huyo alikuwa peke yake. Hakuona dalili ya
mtu mwingine. Ndipo Joram alipouinua mguu mmoja baada ya
mwingine kwa hadhari na utulivu kama kivuli akimfuata.
Mtu huyo alipoufikia mlango hakuchelewa sana kuushughulikia,
ukafunguka polepole naye akaingia huku akiufunga. Joram alimpa
dakika mbili, tatu kisha akausogelea mlango na kuujaribu. Haukuwa
umefungwa. Akaufungua na kunyata ndani huku masikio yake yakiwa
wazi, mkono wake ukiipapasa bastola yake.
Humo ndani kulikuwa na kiza ambacho kilitisha mno. Nuru hafifu sana
ilionekana kwa shida kutoka chumba kimoja. Joram alikifuata chumba
hicho na kutega sikio lake katika tundu la ufunguo akisikiliza.
Haikuwepo haja ya kusikiliza kwa makini kiasi hicho.
Sauti ya mtu au watu wanaogombana kidhaifu ilimfikia kwa urahisi.
Mmoja alikuwa akisema, “Wapi? Usiposema nitakuua…” Mwingine
alilalamika tu.
“Nitakuua kweli,” ilidai tena sauti hiyo nzito zaidi. Ikafuatwa na
malalamiko ya maumivu makali.
Joram hakustahimili zaidi. Akaufungua mlango kimyakimya kwa
haraka zaidi na kujitoma ndani. Aliingia wakati mzuri sana wa kuwa
shahidi aliyeshuhudia jisu kali na refu likiingia katika kifua cha mtu
aliyelala juu ya sakafu.
Pigo la pili Joram alilizuia kwa kumpiga muuaji huyo judo ya shingo.
 
Taarifa hii ni ya mwisho itakayofanyika kwa siri kubwa kiasi hiki.
Wakati wowote katika wiki mbili zijazo mambo yatapamba moto. Watu
wetu wataarifiwa kwa dharura ili kuanza mambo. Ndipo maji
yatakatwa kwa siku kadhaa kuwalegeza wananchi, vyombo vya habari
vitatoa habari za ajabuajabu zenye nia ya kuwachukiza wananchi
dhidi ya Serikali yao, kisha siku hiyo umeme utakatika ghafla na
mapambano kuanza. Itakuwa rahisi sana. Wachache watatiwa pingu,
wachache watauawa na kutakapopambazuka utawala utakuwa mpya.
Joram alimaliza kuisoma karatasi hiyo huku akitetemeka kidogo.
Haikuwa na mzaha hata chembe ingawa aliamini kuwa iliandikwa na
watu wenye wazimu na tamaa ya madaraka ya uroho wa utajiri wa
haraka haraka. Kama alivyokuwa amehisi kitambo, zilikuwepo njama
kubwa zaidi ya ile iliyofikiriwa na polisi ya mwandishi aliyechanganyik
iwa –Bazile – kupata kichaa na kuanza kuua ovyo. Mauaji hayo
yalipangwa tu, yakitumia jina la Bazile ili yaendelee kufanyika kwa siri
bila wahusika kuhisi lolote. Na kiini cha mauaji pengine kilikuwa hiki
cha kuficha siri hii ambayo kwa namna moja au nyingine iliondokea
kuifikia mikono ya watu wasiohusika.
Mara Joram akagutuka na kumsogelea yule adui aliyekuwa
akipambana naye muda mfupi uliopita. Alikuwa amekumbuka kuwa
sura yake haikuwa ngeni machoni mwake. Akainama na kummulika
usoni kwa kurunzi lake. Naam, sura ilikuwa ile ile ambayo si yeye tu
bali karibu kila mtu aliifahamu na kuiogopa. Sura ya mtu yuleyule
ambaye alikuwa akihitajiwa sana na polisi. Yule mtunzi wa vitabu vya
mauaji na ambaye aliondoka kuwa muuaji mkubwa; Bazile
Ramadhani.
Ugunduzi huu ungeweza kuwafurahisha polisi, kwani mtu hatari sana
alikuwa amenaswa. Lakini kwa Joram Kiango, kunaswa kwa Bazile
hakungeweza kumpa furaha hata chembe: Taarifa ya njama za
mapinduzi ilikuwa mfukoni ikimkodolea macho. Hakuona vipi Bazile
aliweza kuingia katika kikundi hicho na vile aliondokea kuwa hodari
kwa mauaji.
Kwa kweli alikuwa haamini kuwa muuaji ni Bazile. Na kama alikuwa
huyo, kulingana na madai au ushahidi wa polisi hasa kwa kifo cha
Kitenge yule mtoaji vitabu, basi Joram aliamini ni kifo hicho tu
ambacho angeweza kukifanya. Vifo vingine alihisi kuwa ziko njama za
mtu au watu wengine. Lakini leo kashuhudia mwenyewe, na anaye
mkononi Bazile huyohuyo, muuaji, anaweza vipi kuendelea
kukanusha? Akazidi kumtazama vizuri.
Akaingiza mikono yake mifukoni na kutoa silaha za kijasusi ambazo
hutumiwa na majasusi wa hali ya juu sana. Vitu kama vikopo vyenye
sumu za kulevya, vidonge viwezavyo kuua kwa muda mfupi sana,
bastola ndogo, kitambulisho na kadhalika. Vyote hivyo Joram alivitia
mfukoni mwake. Kisha akarudisha macho yake juu ya uso wa Bazile
kwa mshangao.
Macho yake yalikuwa wazi yakimtazama kwa ujeuri na kutokujali.
Hayakuwa macho ambayo Joram alimtegemea mwandishi huyo kuwa
nayo. Akaupeleka mkono wake kuupapasa uso huo. Mara Joram
akaangua kicheko. Alipoutoa tena mkono wake ulikuwa umeshikilia
ngozi ya uso wa Bazile ambao uling’oka kwa taabu. Uliobaki badala ya
uso huo ulikuwa uso mweupe wa mtu mwenye sura mbaya. Uso wa
jasusi lenye moyo wa mnyama ambalo bila
shaka lilikuwa limekodiwa kufanya mauaji hayo.

“Kill me” lilimwamuru Joram jitu hilo.
“Who are you?” Joram alimuuliza.
“Just kill me.”
Joram akaokota tambara chafu na kulididimiza katika domo la jitu hilo
ili lisiendelee kusema. Kisha akahakikisha kamba alizotumia kulifunga
jitu hilo zilitosha. Akaongeza nyingine na kutoa kila kifaa mwilini mwa
jitu hilo. Aliporidhika, alitoka chumbani na kuufunga mlango vizuri
akiwa na hakika kuwa jasusi huyo asingepata mwanya wowote wa
kutoroka.
Saa yake ilidai ni zaidi ya saa nane za usiku. Bado alikuwa na saa nne
ili aendelee na harakati zake za kumaliza upelelezi huo.
Akaamua kusubiri papohapo akimlinda mateka wake. Alitumia funguo
zake ‘malaya’ kuingia chumba cha pili ambako alikuta kitanda kizuri
kikimsubiri. Akajilaza. Usingizi haukumjia. Akijua kwamba chumba
cha pili kina muuaji hatari na maiti ya mtu, mawazo hayakuweza
kutulia.
Zaidi, alishindwa kulala kwa jinsi fikara zilivyokuwa zikimpita kichwani
juu ya barua hiyo ya siri aliyokuwa nayo. Alifahamu kagundua siri
kubwa. Lakini bado alifahamu kuwa hajagundua lolote dhidi ya watu
hao wanaokusudia kuichukua nchi. Ilikuwa wazo kuwa majina hayo
yalikuwa bandia tu. Hakuwa na muda wa kujisumbua kumtesa mateka
wake mzungu ili amwambie.
Kwani, kwa kadri anavyowafahamu majasusi hao, hawawezi kutamka
lolote. Hata hivyo, Joram alijua lipo ambalo angefanya kesho ili
kuweza kupata walao njia ambayo ingemwezesha kuwafahamu watu
hao waliochoshwa na amani. Kiasi pia alijiuliza juu ya Bazile. Kama
muuaji alikuwa akiutumia uso wake, yeye mwenyewe yuko wapi?
Pengine naye kauawa na kuzikwa kwa siri?
Mapambazuko! Joram aliyasubiri kwa hamu kubwa mapambazuko ili
apate majibu ya maswali hayo na mengi mengine.

SURA YA KUMI NA TANO

KULIPOPAMBAZUKA, Joram aliwachungulia maiti na mateka na kuona
wako katika hali ile ile ya usiku. Akawafungia tena na kuamua
kuwaacha katika hali hiyo. “Maadam nyumba inaogopwa kuwa ina
mkosi au majini, wanaweza kuendelea kukaa humu walau kwa saa sita
bila kuonekana,” alijisemea akihifadhi vizuri vifaa vyake vyote
alivyopata katika nyumba hiyo. Akakiendea kivuko ambako alikuwa
miongoni kwa abiria wa kwanza. Upande wa pili alitembea kwa mguu
hadi kituoni ambako alipanda basi lililompeleka uwanja wa ndege.
Wafanyakazi walikuwa ndio bado wanawasili na mabasi yao. Joram
alitazama hadi alipomwona yule binti aliyempa orodha ya wasafiri wa
ndege aliyoihitaji jana. Binti huyo alimtazama kwa macho ya
kufahamiana na tabasamu.
“Mbona mapema hivyo?” alihoji.
“Kuna kitu nilisahau kuuliza jana,” Joram alihoji na kuongeza,
“Tafadhali jaribu kukumbuka kama uliona tukio lolote la ajabu au
ambalo halikuwa na kawaida siku ile?”
“Ipi?”
“Ile waliposafiri watu hawa,” akamwonyesha orodha ya majina yao.
Msichana huyo alijaribu kuwaza sana. mara akakumbuka jambo.
“Nakumbuka yuko mzee mmoja kati yao ambaye alitujia katoa macho
pima na kudai kuwa begi lake limeibwa, mikononi alikuwa na begi
lingine aina ileile ya suitcase. Tulipomuuliza hiyo kapata wapi alisema
ameikuta badala yake. Tukamwelekeza kwenda chumba ambacho begi
hilo lingeweza kufunguliwa ili ijulikane nani mwenyewe. Alienda huko.
Aliporudi huko alikuwa akicheka na kutuambia kuwa begi lilikuwa lake
isipokuwa lilikwaruzwa kidogo ndipo akalisahau.”
“Unamfahamu mtu huyo?”
“Sana. huwa anasafiri mara kwa mara. Jina lake ni Kwame. Nasikia
ana kampuni yake binafsi.”
Joram hakuweza kujizuia kuonyesha furaha aliyoipata baada ya
kusikia hayo. Tayari alikuwa na shilingi mia mbili mfukoni akimpa
binti huyo huku akisema, “Umenisaidia sana mpenzi.”
“Sioni nimekusaidia vipi.”
“Utaona baadaye,” Joram alisema akiondoka kuendea teksi
zilizosimama kando yao zikiwasubiri abiria.
Hisia zake za awali juu ya kuhusika kwa Kwame kwa njia fulani katika
njama hizi sasa zilikuwa zimethibitika. Kupotelewa na mfuko, Joram
alifahamu ni jambo lililotokea. Pengine marehemu Komba aliuchukua
mfuko huo kwa kukosea, pengine alikusudia. Kwame bada ya
kugundua hayo, akijua kuwa kuna siri kubwa ambayo hakupenda
ijulikane, alichanganyikiwa na kuwapigia kelele wahudumu.
Lakini baada ya kufikiri zaidi ndipo alibuni uongo kwa kudai kuwa
mfuko ni wake kwa matumaini ya kumfahamu mwenye mfuko huo kwa
kusoma hati ambazo zingekuwepo ndani ya mfuko huo.
Ni njia hiyo iliyomwezesha kumpata marehemu Komba. Pengine, hata
kuchelewa kumuua kulitokana na hofu yao ya kutojua iliko barua ile ya
siri. Naye Komba yaelekea alikuwa mgumu wa kuitoa kwa kufahamu
kuwa mara waipatapo, wasingesita kummaliza.
Wakati wakiwaza hayo, Joram alikuwa ndani ya gari akielekea mjini.
Teksi ilimfikisha nyumbani kwake ambako alioga vizuri, akavaa
mavazi yaliyomstahili na kuweka mifukoni vitu alivyovihitaji, kisha
alitoka kwenda ofisini.
Neema alimlaki na maswali mengi. Joram alijibu machache tu
akimwahidi kuwa baada ya saa chache atajibu yote. Kisha, aliandika
kadi moja ya ‘express’ na kumwomba Neema aipeleke Posta.
Aliporudi, Joram alimpa maelekezo mengine ambayo yalimfanya
Neema atoe macho kwa shauku na tamaa akijua kuwa mambo
yameanza.
Joram aliitazama saa yake, kisha akajistarehesha juu ya meza
akisoma gazeti la Daily News ambalo lilikuwa na habari za kuchekesha
chini ya kichwa cha habari: BAZILE MUUAJI HATARI YU HAI BADO
Joram aliisoma habari iliyofuata kama hadithi kisha akalitupa juu ya
meza na kuendelea kusubiri, sigara zikiungua mdomoni mwake moja
baada ya nyingine.
 
Back
Top Bottom