Riwaya: Msamaha kwa mama

Riwaya: Msamaha kwa mama

Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM.

SEHEMU YA 07

Lilikuwa swali zito sana kwake kulijibu, machozi yalimtiririka kama baadhi ya wanafunzi ambao walikuta matokeo ya siamini wakashindwa kujizuia na kuangua kilio.

Hakuweza kuamini alichokiona Seid, maswali mengi yaliingia kichwani mwake, akawa na msongo wa mawazo, alihisi presha kupanda na kushuka ghafla, taratibu alianza kuanguka chini na kupoteza fahamu, wenzake waliokuwa karibu walimdaka wakampeleka chini pole pole akiwemo kijana mmoja aliekuwa swahiba wake wa karibu aitwae Hamad...

Songa nayo......

"Subirini kwanza muacheni apate hewa, au tafuteni kitu mumpepee!. Nini kimetokea?.

Yalikuwa maneno ya Ticha ambae ndie aliempatia majibu ya mapema seid. baada ya kuingia eneo hilo. Aliuliza kimetokea nini?. Wanafunzi walimjibu kwa kumuambia kafika hapa akiwa anasema nimeshinda nimeshinda, anaangalia matokeo tunaona mtu anaanguka chini.

Ticha hakujibu kitu chochote, alisogea mpaka kwenye ubao yalipokuwa yamebandikwa matokeo, namba ya seid alikuwa anaijua vizuri sana, alivaa miwani akaanza kusoma namba moja baada ya nyingine mpaka alipoipata namba ya Seid. Nae pia hakuamini alichokiona, jasho lembamba lilianza kumtoka, alitikisa kichwa akaachia msonyo wa kushangaa, wanafunzi wakauliza vipi ticha?.
Ticha aliwaangalia wote waliokuwa wamesimama mbele yake.

"kwa hiki nlichokiona ana haki ya kuzimia, na kwa namna hii hakika Tanzania haitoendelea maisha yote. Alisema.
"Unatufumba mwalimu wangu una maana gani?. Aliuliza Hamad ambae alikuwa ni rafiki wa karibu mno na seid, alikuwa na furaha zake za kufaulu, alikuwa moja ya vijana wa watu wakubwa ndani ya nchi ya Zanzibar.
"Nna asilimia mia matokeo ya seid yameuzwa. Ticha maneno yalimtoka kwa hasira.
"Unamaanisha nini mwalimu.
aliuliza tena kijana huyo hamad. Aliekuwa mfupi mwenye asili ya kiarabu na upara wa dizani aliokuwa akipenda kuupaka mafuta.

"Inauma sana lakini haina haja ya kujua kwa sababu hata mkijua hamtosaidia chochote, Mungu atasaidia tu nshallah. Ticha aliongea kwa uchungu.
"Mwalimu ukifanya hivyo Wallah utakuwa umetuacha njia panda, tena utakuwa unatukosea sana, we ndo ulikuwa ukitupitisha mambo ya misemo kila siku na kutupa habari za ushujaa wa william mwandishi mkongwe kutoka Uingereza. Nakumbuka uliwahi kutuambia maneno haya ambayo nayakumbuka sana yanauozungumzia ushujaa wake.

** Wanadam wako wa aina nne tofauti katika hii dunia, ukiwajua hakika utaishi vizuri, aina ya kwanza watu ambao wanafurahi kuona maendeleo ya wenzao yanarudi nyuma hasa wanyonge, na dawa ya mtu ambaye unahisi anaitaji kurudisha maendeleo ya mtu nyuma, ni kuongea mabaya yake aliyoyatenda.
Mwalimu ulizungumza maneno haya ila baadhi ya wanafunzi watakuwa wameyasahau kwa sababu ulitumia kifaransa, mimi niliyashika ili badae yaje yanisaidie, nilivyoiangalia hii picha naona kabisa Seid atakuwa amekosewa, ukiwa kama msemaji mkuu wa wiliam inakuwaje unashindwa kuzungumza ukweli!?. Ticha wewe ni mwalim mkubwa hapa chuo, wanafunzi wengi wanakufahamu na wana kukubali kutokana na kazi yako nzuri ya ufundishaji, vipi unaonekana kuwa mnyonge baada ya kuwatetea wanyonge?.

Hamad aliongea maneno yaliyoonekana kumgusa Ticha, ticha moyo wake ulifunguka na kuitaji kuwaambia ukweli, kabla ya kuanza Seid aliamka akiwa kama mtu aliechanganyikiwa, walijaribu kumtuliza lakini hakutulia, alimuangalia Ticha na kumuuliza.
"Nakumbuka ulinipigia cm mbele ya mama yangu na kuniambia nimefaulu, inakuwaje hata matokeo ya chet sipati? ulikuwa unantania?

Alivyozungumza tu kila mtu alijua kabisa mshkaji kadata, ticha alikaa kimya akashindwa la kuongea, kijana Hamad ambaye alimkumbusha maneno ya wiliam mwandishi wa misemo maarufu nchini uingereza, alimuangalia Ticha wake akavua miwani na kumuomba ajibu swali la Seid.
Seid alimtolea ticha macho, tayari akili zake hazikuwa sawa, Ticha aliwangalia wanafunzi kijasho chembamba kikiwa kinamvuja.

" Seid ni mwanafunzi mwenzenu na ni mwanafunzi ambaye wengi wakisikia kafeli watashangaa sana, Ila hayo ndo matokeo yaliyopo kwenye ubao na ndio maana nimesema kwa namna hii Tanzania hatutoendelea kwa sababu, kabla ya hapo niliyaona matokeo ya Seid na alikuwa amepata matokeo ya juu sana, kwa hiyo sielewi imekuwaje. Alisema.
" Una maanisha matokeo ya Seid yameuzwa?. Hamad alimuuliza Ticha.
"Yeah.
"Waaoo!. Seid my friend, Hamad alimgeukia seid akamshika begani huku akimuita, wewe ni mnyonge. Yeah wewe ni mnyonge rafiki yangu.
kuna walimu wako ngazi za juu wanaujua unyonge wako hapa shule, na wameamua kucheza huu mchezo ila usijali, nakuahidi kabla ya mipango ya kuingia chuo haijaanza, matokeo yako yatarudi. Naomba nikuahidi hilo. Alisema kwa kujiamini.
"Hamad. Wewe ni rafiki yangu sawa. Na umenisaidia vingi sana sikatai, unadhani utanisaidiaje juu ya hili.?.
Seid aliuliza huku machozi yakimlenga lenga.
" Babaangu ni mtu mkubwa sana serikalini, na anapenda sana kutetea haki za wanyonge, nimesoma na wewe miaka mitatu, naijua hali yako ilivyo mbaya na unategemea kitabu kikusaidie katika maisha. Haina haja ya kuchanganyikiwa, wewe ni rafiki yangu nitakusaidia na matokeo yako utayapata tu, I Promise you.. alisema hamad.

Seid alishusha pumzi kidogo akili zake zikakaa sawa. Hamad alikuwa akimpenda sana mshikaji, ukoo wake wote ulikuwa ukoo wa wasomi, kuanzia mababu zake mpaka ndugu zake wote wana elimu zao za kutosha. Hali ngumu ya maisha aliyokuwa nayo Seid aliifahamu vizuri kwa sababu seid hakujificha shuleni maisha yake halisi, alimweleza kila mmoja kuwa yeye ni masikini na anategemea kitabu kuja kumtoa. Hali ilipelekea kupata baadhi ya misaada japo wapo waliomcheka, lakini hamad alimueshim sana na kumchukulia kama moja ya ndugu zake wakubwa na anaowaeshim.

Alipomaliza kumpa moyo seid alimgeukia mwalimu na kumuomba wasogee yeye na seid pembeni waongee private ( secret conversation). mwalimu alikubaliana kila kitu na hamad kwa sababu nae alikuwa na mawasiliano ya karibu sana na Seid. Walienda wakakaa chini ya mti wa pambo la shule na kuongea zaid ya nusu saa, mwisho hamad aliwaomba wote wawili waingie kwenye gari lake waende kiwengwa shamba alikokuwa akiishi seid kwa ajili ya kumpeleka, kwani alijua kabisa rafiki yake hayuko sawa wakimuachia aende peke yake na usafiri wa dala dala anaweza asifike.

Hamadi alikuwa anapenda kuongea English na kifaransa kuliko lugha yoyote ile ulimwenguni, upo muda kiswahili kilikuwa kinampiga chenga kwa alivyozoea kingereza na kifaransa, alikuwa na upendo kwa kila mmoja lakini kwa Seid ulipitiliza, alimkubali sana seid kwa sababu alikuwa ni kijana mwenzake anaependa kitabu, pia amezungukwa na shida ambazo huwa hazifichi kwa kila mtu, huku akibukua darasani ili siku moja aweze kuokoka kimasikini kutokana na kitabu.

Alihakikisha anakuwa nae makini kwa karibu sana ili apate vitu zaid kutoka kwake kuhusu Kitabu, Pia Hamad ni mtu aliependa sana kufatilia maisha ya mashujaa wa hapa duniani, watunga mashairi pamoja na misemo, ziliiva sana na seid pamoja na mwalimu waliezoea kumuita Ticha kwa sababu na wao pia kuwa watu wanao penda sana mambo hayo.

Kutokana na bara bara za Zanzibar hasa ziendazo shamba kukosa magari ya kusababisha foleni, walitumia dakika 30 pekee kufika kiwengwa, walipaki gari mbele ya nyumba aliyokuwa akiishi seid, Bi najma aliposikia sauti ya gari ilibidi atoke ndani, kufika mlangoni akaona sura ngeni zimeongozana na mtoto wake, hakushtuka kwa sababu aliona ni vijana wenzake pia wanaonekana wanatoka mjini.
Seid aliwakaribisha sana sehemu anayoishi na mama yake, walikaribia kwa kuingia ndani huku wakimsalimia bi najma.

"Jamani karibuni sana.
Bi najma aliongea akivuta kisturi na kukaa mbele ya Ticha na Hamad waliokuwa wamekaa kwenye mkeka.
"Tushakaribia mamaangu, tushakaribia sana wala usijali. Alisema Hamad.
"E bhana karibuni ndugu zangu hapa ndo nyumbani, hamad kila nlipokuwa nakwambia twende nyumbani hukuitaji ila leo umefika. Alisema Seid.
"Heheheeee usijali rafiki yangu uenda Mungu bado alikuwa ajapanga.
"Au na wewe ulitaka kuwa kama Deniss Rwadsh alivyofanya kwa mbwa wake?. Aliuliza seid.
"Hahahahaaaaa Seid umeanza mambo yako, wewe mtu una matatizo sana Akyamungu mimi unifananishe na Deniss?, yule alikuwa kiumbe chengine myahudi yule. Alisema wakacheka. Ila kabla hatujaendelea ebu kwanza tuongee na mama, mama! vipi hali,alimgeukia Bi najma akamuangalia na kumuuliza hali yake.

"Salama babaangu, hawajambo huko?. Aliuliza bi najma.
"Mama!. Seid alimuita mama yake kabla hamad hajajibu.
"Abee mwanangu
"Huyu anaitwa hamad mwanafunzi mwenzangu, na huyu ni Mwalimu wetu tunapenda kumuita professa, kichwa kizima kimejaa Elimu hiki kione hivyo hivyo kilivyo..

Mwalimu aliachia tabasam baada ya kuitwa professa, akashika kichwani huku akisema "Hamna bhana wako maprofessa sio mimi.
" karibuni sana. aliongea bi najma akiwakaribisha kwa mara ya pili.

"asante mama tushakaribia. Alisema hamad.
" Nimefurahi sana kuwafahamu, ila naomba mnisamehe maana hapa ndo hakunaga hata kinywaji chochote zaid ya maji tu.
" Mama usijali sisi tuko sawa, tuko sawa kabisaaa yani usijali kabisa mamaangu.

"Nadhani nilikuaga naenda mjini asubuhi kuangalia matokeo. Seid aliiingilia kati.
"ndio mwanangu vipi?
" Ah mamaangu acha tu nilichokikuta huko ndio kimefanya marafiki zangu hawa wafike hapa.

Alimuambia kila kitu kilichotokea mjini, mwalimu na hamad nao walichangia kumuelewesha mama ili asiwe na presha juu ya mwanae, walimuahidi lazima sheria ichukue mkondo wake na lazima matokeo ya seid yarudi hayawezi kwenda kirahisi rahisi tu kama inavyokuwa inatokea kwa wengine.
Walizidi kuongea mengine mengi ambayo yaliwafanya wacheke sana na kufurahi, walipoona muda unaenda ilibidi waage kwa ajili ya kuondoka, Hamad alitoa wallet yake akatoa elfu 30 na kumpatia Bi najma.

"Mama angu hizi hapa zitasaidia japo sabuni.
"Eh! asante babaangu, asante sana! mungu akubariki uwe na roho iyo iyo baba!. Alisema kwa furaha bi najma.
"Usijali mama haya ndo maisha yakitanzania japo wengi wanasahau hili, ila mshairi mmoja wa kifaransa anasema hivi:. kwa nini msahau asili yenu wakati mkiiendeleza mtaishi kwa furaha kuliko mkiiga ya wageni?, mimi ni mfaransa, hata nitajirike vipi bado nitaikumbuka ufaransa, najua kuna mataifa yameendelea na wanaiona ufaransa ni nchi masikini, ila siwezi kuisahau hata nitajirike vipi kwa sababu na mimi nimezaliwa kwenye umasikini. unajua alimanisha nini hapo huyu jamaa mamaangu?. Alisema kisha kumuuliza swali bi najma.

"sijui! mambo ya wasomi hayo.

"Heheheee, wewe ni mamaangu kwa sababu unaweza kunizaa na umenizalia rafiki yangu kipenzi.
Huyu jamaa alivyomanisha mfano wake ni hivi, maisha ya kitanzania ni maisha ya kimaskini, Mtanzania ataekuambia mimi natokea kwenye ukoo wa matajiri huyo muongo, Akyamungu huyo muongo mama!, kama wewe ni tajiri basi jua kuna vibabu vyako huko nyuma vimeishi kwenye nyumba za makuti. Mamaangu mimi hapa naishi kwenye familia ya wasomi, Yeah naweza kusema hivyo kwa sababu familia yangu yote ni ya wasomi na baadhi ya ndugu zangu wana hela nyingi sana, Je! hali hii inipelekee mimi kusahau asili yangu ya kitanzania Kisa nimezaliwa kwenye Pesa nisahau kuwa asili yangu ni ya kimasikini?. Aliuliza.
"Hapana, Bi najma alijibu.

"Basi mi ngoja nikuage mama tuondoke kama jibu unalo.
Aliinuka akiwaacha wote wako kwenye kicheko cha machozi kutokana na maongezi yake, Bi najma nae alisimama akamshukuru sana kwa msaada wake na kumshukuru pia kwa kumuahidi kufatilia zoezi la mwanae, waliinuka wote wakatoka mpaka nje huku bi najma akisema karibuni sana jamanii, na wao waliitikia kwa kusema asante, wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kwenda mjini.

Seid na mama yake walisimama nje mpaka gari lilipoishiliza, Bi najma alinyoosha mikono juu kumshukuru Mungu.
"mama vipi? Aliuliza seid.
" Mwanangu elfu 30 kubwa sana kwangu mungu ambariki huyu kijana mashallah.
" Mama!, Hamad ni rafiki yangu mkubwa na amenisaidia sana kiukweli huko shule. Alisema seid. Waliingia ndani wakiwa bado wanaendelea kuongea.

Wakati wao wanaingia ndani upande wa pili Hamad na Ticha wakiwa njiani wanarudi mjini ghafla walikutana na gari nyeusi imezuia bara bara mbele yao, walipata mshangao sana wakapunguza mwendo kisha wakasimama, upande alikokuwa amekaa Ticha alitokea mtu amevaa nguo ya kumfunika uso wake kama gaidi akamtandika Risasi Ticha na kutoeka. Alikimbia fasta mpaka kwenye gari hilo leusi lililokuwa limezuia bara bara kwa mbele akaingia ndani na kukanyaga mafuta, tairi zilizungushwa, rami ikasuguliwa vizuri jamaa akatoeka kimuundo huo akimuacha ticha katika wakati mgumu wa jeraha, risasi ikimpatia maumivu makali mno ya kushindwa kustahimilia na kupoteza fahamu.

** Tukutane sehemu ya 08
** Wasiliana na Mtunzi wa story ili upate story nyingi zaidi >> 0774320110 whtsapp/call
 
** wasiliana na mtunzi wa story hii ili upate kusoma story nyingi kutoka kwake. 0774320110 whtsapp/call
** facebook page >> HADITHI ZA SEID
 
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM.

SEHEMU YA 08

Wakati wao wanaingia ndani upande wa pili Hamad na Ticha wakiwa njiani wanarudi mjini ghafla walikutana na gari nyeusi imezuia bara bara mbele yao, walipata mshangao sana wakapunguza mwendo kisha wakasimama, upande alikokuwa amekaa Ticha alitokea mtu amevaa nguo ya kumfunika uso wake kama gaidi akamtandika Risasi Ticha na kutoeka. Alikimbia fasta mpaka kwenye gari hilo leusi lililokuwa limezuia bara bara kwa mbele akaingia ndani na kukanyaga mafuta, tairi zilizungushwa, rami ikasuguliwa vizuri jamaa akatoeka kimuundo huo akimuacha ticha katika wakati mgumu wa jeraha, risasi ikimpatia maumivu makali mno ya kushindwa kustahimilia na kupoteza fahamu.
*****

Seid na mama yake waliingia ndani wakiwa na furaha ya kutembelewa na wageni na kuachiwa chochote kitu, walijua siku hiyo uhakika wa kula vizuri upo.

"Mama leo nadhani tunakula nyama. Alisema Seid akiwa amekaa chini amejiegamiza ukutani na mguu mmoja kuusimamisha, alimuangalia mama yake aliekuwa anajifuta futa jasho usoni kwa kutumia khanga yake aliyokuwa amejifunga.
"Heee mwanangu unawaza kula tu wewe baba.
"Sasa tufanyie nini hiyo fedha uliyopatiwa?. elfu 20 chukua kumi lete tule vizuri leo.
" Ila kweli mwanangu, basi hapa itabidi uchukue baiskel yako uende sokoni uchukue japo nyama na viungo viungo hivi, Mungu ametuonamo, tunavyoishi yeye ndiye anaejua, ipo siku moja atatuokoa tu na hizi shida tulionazo. Tusiache kumuomba.
" Hilo ndilo la msingi mama yangu, dua kwa sana ndio kinachotakiwa, na hasa kuhusu masomo yangu Mungu aweze kuweka uwepesi matokeo yangu yarudi, naamini ipo siku mama tutafanikiwa tu nshallah. Alisema seid. Alimaliza na neno nshallah akanyanyuka chini na kusimama.
" Sasa nipe hiyo pesa niende huko sokoni.

Bi najma aliposikia mwanae amesema hivyo aliziangalia pesa alizopewa ziko wapi na kutoa elfu kumi kumpatia, aliichukua seid na kuangalia kwa kuigeuza geuza akaachia tabasam.
"Tena hiki chakula nataka nikipike mimi mwenyewe uone nilivyo vizuri kwenye kupika mama.
"Ebu nitokee huko unajua kupika wewe!.
"Sasa mama hutaki au.
"Una miaka 20 mwanangu, mama yako nazeeka tena utoto upunguzege Eh!.
"mtoto hakui kwa mama, ila si tutampelekea na bibi?.
"hayo meno anayo?.
"We unayo? ,, seid alimtupia swali mama yake kama utani baada ya kumuuliza kama bibi yake ana meno
"Ebu nenda huko nna miaka 40 tu sijazeeka kiivyo mwanangu ila bibi yako anaenda kwenye tisini yule sasa hivi.

Seid alitoka na kumuacha mama yake anacheka, akachukua baiskel na kwenda kwenye soko la kiwengwa lililoko pwani mchangani kwa ajili ya kuchukua mazaga zaga ya mapishi ili wale vizuri siku hiyo bila kujua kilichomkuta hamad na ticha kipindi wanaondoka.

Alijikokota na baiskeli akijaribu kuzinyonga pedeli kwa nguvu ili afike haraka sokoni, uso wake ulionekana kuwa wa furaha kutokana na kujua mapema kuwa angekula chakula kizuri siku hiyo tofauti na masiku mengine yote.
Uso kwake ukiwa na furaha za kumwaga, upande wa pili kwa Hamad sura yote ilikuwa imeharibika kwa kuchanganyikiwa baada ya ticha kupigwa risasi, ubongo uliripuka na kushindwa afanye nini kwa haraka, jasho liliuzunguka uso wake huku na mwili wote ukihisi muwasho.
Hakujua afanye nini licha ya kuweza kutulia sehemu moja na kukosa papara za kuushughulisha moyo, alituliza akili, akijua endapo atakuwa na itikadi za kudata tu kutokana na kile kilichoko mbele ya macho yake hatofanya chochote. Alikuwa akipenda sana kumfatilia Wiliam shujaa alieishi miaka zaidi ya 100 duniani na kufanya mengi ikiwemo kuwakomboa watu zaid ya mia nne waliokuwa wametekwa katika meli ya uharamia somaria na kuwarudisha nchini Uingereza bila kukwama katika harakati za uandishi wake. Mawazo ya kuukumbuka ushujaa wa huyu jamaa yalimuingia, alitulia akashusha pumzi japo tayari na machozi ya presha yalishaanza kumlenga lenga, alitoa cm na kubonyeza namba za emergency call, police station akapiga, Cm haikuita sana ikapokelewa.

" Mahonda police station tukusaidie tafadhali. Ilisema sauti ya upande wa pili iliyosikika kuwa nzito kwenye cm.
" Hal,,loo haloo! Naomba mnisaidie haraka iwezekanavyo, tumevamiwa na mtu tusiomfahamu kipindi tunatoka kiwengwa, mwenzangu amepigwa risasi mimi ni mtoto wa mzee shaibu. Alisema hamad.
" Umesema uko wapi? Aliuliza kamanda, alipoambiwa mtoto wa mzee shaibu tu hakuitaji maelezo mengi zaidi.
" kiwengwa.
" Naomba nipate maelezo yote na aina ya gari iliyowavamia.
" Ilikuwa ny'e ny'eusi. Alisema pumzi zikikatika na kushindwa kabisa kuongea sentensi ndefu.
" Namba za gari?.
" ZNZ 654 AD.

Aliweza kujieleza vizuri hamad japo alishaelemewa na mzigo uliokuwa mbele yake, kamanda wa police alimuomba apunguze presha aendeshe gari kwa makini kupitia njia ya mahonda iendayo mjini atakutana na gari ya wagonjwa na watampeleka Ticha hospital haraka iwezekanavyo, huku yeye akifanya juu chini kuhakikisha anateua vijana wa kuifanya kazi ya kulitafuta gari lililowafanyia uhalifu.

Cm ilikatika hamad akafanya vile alivyoambiwa, mikono ilikuwa inatetemeka na kuwa na misisimko isiyoisha, alishika usukani wa gari akakanyaga mafuta na kuanza kulitoa gari taratibu, Huku kamanda wa police mahonda aliejulikana kwa jina la saleh, aliepokea taarifa za kuvamiwa kwa hamad aliteuwa vikosi makini kutoka katika idara yake, vijana wanne wanne magari manne tofauti waende haraka kufatilia uhalifu huo uliotokea ikiwezekana kulipata hilo gari.
Bila kupoteza muda vijana hao waliochaguliwa. Waliokuwa wakifanya kazi katika kituo cha police cha mahonda waliingia kwenye magari na kuanza safari.

Gari moja lilipita njia inayoelekea Donge na matatu kupita njia iendayo kinyasini, yalipofika kinyasini moja lilikata njia ya kiwengwa, mawili kusonga mbele.
Na yenyewe yalipofika mbele yaligawanya moja likaelekea njia ya matemwe lengine likanyoosha kuelekea nungwi wakiamini kufanya hivyo lazima gari lipatikane labda tayari liwe limeingia mafichoni.

Taarifa zilizidi kusambaa ndani ya mda mfupi, Kamanda Saleh alizisambaza haraka baada ya kujua aliempatia habari ni mtoto wa mtu mkubwa Serikalini ndani ya Zanzibar. Aliwasiliana na makamanda wenzake mjini ili nao waweze kujiweka sawa kuingia bara barani kulisaka hilo gari.

Vituo vingi vya idara ya police vilipata kufahamu nini kinaendelea na kuwa tayari kusimama imara ili mtu aliefanya huo uhalifu akamatwe, walimwagika mabara barani na silaha nzito nzito wengine wakipakizana kwenye magari kwa ajili ya kufanya doria. Bara bara ya mfenensini ilifungwa kwa muda pamoja na round ya baut ya mjini inayokutanisha magari yatokayo bububu na kwengine kwenda bandarini na stend kuu ya darajani, walihakikisha wanafanya kazi kwa makini zaid, tayari walishajua kama watafanikiwa kwa hilo watatengeneza majina na kupata kuonekana katika vyombo vya habari kutokana na Tukio lenyewe japo limetokea ghafla.

Hamad alijitahidi kuendesha gari mpaka kufika mahonda, miwani ilishajaa mvuke wa joto ilibidi aivue, Ticha alikuwa pembeni yake akiwa hoi hajitambui. Walipofika na gari ya wagonjwa ndio ilikuwa inafika eneo hilo, walifungua milango haraka wakamtoa, walimuingiza katika amburance na kuanza safari ya kumpeleka haraka mjini hospital ya serikali m/mmoja.

Hamad alichukuliwa mpaka ndani ya kituo, Askar watatu walimzunguka wakiwa tayari kuandika ripoti za kile atachowaambia.
Kabla ya kuanza kumhoji, cm ya mezani ilianza kuita, kamanda alichomoa na kuweka sikioni.
" Police station mjini no 886, Tunaomba mtoto wa mheshimiwa afike kituo kikubwa kwa ajili ya kuandika ripoti haraka. Alisema wa upande wa pili ambaye alikuwa police pia anaefanya kazi mjini.
" Sawa mkuu.

Alitoa cm sikioni na kuirudisha kwenye meza, aliwaangalia vijana wake huku akisema.
" Inabidi akaandike Ripoti mjini haraka iwezekanavyo, chukueni gari lililobaki mwende nae mjini, kijana ingia ndani ya gari lako uongozane na vijana hawa ukaojiwe juu ya lililokukuta, ulinzi uko salama, nawaamini sana vijana wangu.

Hamad hakujibu chochote, aliinuka kwenye kiti alichokuwa amekaa, akatoka nje huku vijana watatu wakiingia katika difenda nyeusi. Alifika kwenye gari akafungua na kuingia ndani, aliwasha safari ya kwenda mjini ikaanza akiwa hana amani kabisa moyoni mwake.
Gari lake lilitangulia nyuma ikafata ya mapolice. Bado tafuta tafuta ya sehemu mbali mbali iliendelea kulitafuta gari lenye usajili wa namba ZNZ 654 AD. huku kukiwepo mawasiliano ya karibu ili kujuzana kuhusu taarifa za kila kinachoendelea kona zote.

Wananchi waliokuwa sehemu mbali mbali za bara bara walikuwa wanashangaa mapolice wanavyopiga doria jioni hiyo, kitendo kilichosababisha wengi wawe na maswali tofauti tofauti.
"Amy vipi leo kuna nini mbona doria!?.
mpemba mmoja aliekuwa anachoma maindi alisikika akimuuliza amy yake aliekuwa pembeni.
" Itakuwa kuna uhalifu ushafanyika tayari na hivi Zanzibar ilivyoharibika sasa hivi sijui!.
" Au washaiba wanyamwezi maana haweshi siku hizi kuvamia mabenk yetu, juzi tu hapo Piople's bank of Zanzibar wamevamia wakaondoka na mamilioni.

kabla hawajaendelea gafla waliona linatokea gari jeusi likiwa linatimka mbio nyingi sana bara barani. watu wote waliokuwepo sehemu hiyo iliwabidi watoke mbio mbio kwa uoga, walijua tayari pashakucha, hawakukaa sawa wakaziona difenda mbili zikiwa mwendo kasi, risasi nne kwa mkupuo zililia juu kwa juu, baadhi ya wakina mama walianguka chini kwa presha huku wengine wakikimbia mbio, mtu mmoja alisikika anasema akikimbia
" Jamani hivi hii zanzibar yetu ishakuwaje sasa hivi?, kila siku vita! Kila siku vita hatupumui jamani tushachoka sieee tushachoka Wallah Ah!.

Difenda mbili zilizofanikiwa kuliona gari hilo maeneo ya bumbwini likijaribu kutafuta upenyo wa panya ili kuingia vijijini na kuanza kutimuana nalo mbio, askar wa difenda hizo walipeleka mawasiliano kwa vituo vyote vya police vilivyo karibu na bara bara, ili vijaribu kuzuia bara bara zote hasa bara bara inayochomoza bumbwini kwenda mjini au kitope, kwani ndio sehemu walioko wakilifukuza kwa karibu.

Seke seke hizo zikiwa zinaendelea Baba yake hamad mzee Shaibu habari zilimfikia, Alichanganyikiwa ghafla kutokana na kumpenda sana mwanae, alipiga cm haraka kwa maofisa usalama kuuliza usalama wa mtoto wake kwanza .

" Ndugu zangu mimi ni Mzee shaibu, nimepata habari za Ticha mtu aliekuwa ameongozana na kijana wangu kupigwa risasi na kuambiwa kuna kash kash zinaendelea huko vipi mwanangu yuko salama?. Aliuliza.
"Mzee wangu mwanao yuko salama kabisa, tunaomba usiwe na wasi wasi jeshi la police linafanya kazi yake.
" Na imetokana na nini hiyo hali.
"hatujaweza kujua chochote kwa sababu anaejua kila kitu ni Hamad mwanao na bado hajaojiwa.
"vipi kuhusu Ticha.

kabla ya kumaliza kuongea cm ilikata, alitikisa kichwa.
"Jamani ni nini hiki kinatukuta zanzibar, mbona amani inatoeka kila siku? tunaishi roho juu juu juu ya familia zetu wallah kwa nini!

Hali ilikuwa bado si shwari maeneo tofauti tofauti, watu walilaani ovyo ovyo juu ya tendo wanaloliona, wengine walipata presha na kuzimia hapo hapo. Kwa bahati nzuri hakukuwa na magari mengi katika bara bara za shamba, maskari walishawasiliana kila sehemu kuhakikisha wanaliwinda gari hilo lililoonekana kuwa imara, Risasi kadhaa zilipigwa juu kuangalia kama litasimama lakini wapi, Difenda zilizokuwa zinalifukuza zilishakuwa nne.

Baada ya kuchukua muda mrefu wakipiga risasi juu bila kusimama, askar mmoja aliekuwa na cheo kuliko wengine alisikika akisema "Lengeni gari asituzingue mpumbavu huyo.

Askar walianza kulenga gari, Risasi moja ilifanikiwa kulenga tairi, tairi liliachia pumzi na kuliacha gari likianza kukosa mwelekeo. Risasi nyingine ilipiga tairi la pili kwa nyuma, ndipo gari lilianza kufuja na kushindwa kutembea tena baada ya kuvamia nguzo ya umeme.

Difenda zililizunguka gari hilo maaskari wakikaa makini kwa ajili ya kushambulia endapo kitatokea kitu tofauti, walishuka na kuanza kutembea taratibu. Moja ya maskar aliushika mlango wa gari lililofanya uhalifu na kuufungua haraka, ndipo alitoka jamaa yule yule aliemtandika risasi Ticha akiwa ameshikilia bastola mkononi.
" Tulia hivyo hivyo kama unataka salama ya kuishi, na wambie wenzako waweke vikaragosi vyao chini!. Alisema mhalifu akinyoosha bastola yake kumnyooshea askari aliefungua mlango wa gari, lakini kitendo chake cha kuongea japo alikuwa amejifunga kitambaa usoni, baadhi ya maaskari waliosikia sauti walihisi sauti hiyo kuifahamu, haikuwa ngeni masikioni mwao.

Askari huyo hakuwa na silaha alinyoosha mikono juu, askar mwengine aliekuwa nyuma akasikika akisema
"Mjinga mkubwa shusha Silaha yako haraka kabla sijamwaga ubongo wako, huna mtu wa kumtisha hapa, uko peke yako tuko zaid ya kumi teremsha bastola yako kwa usalama.
" Mnaweza kuwa zaid ya kumi na bado mkawa mabwana wadogo tu kwangu,endapo utathubutu kushut na mimi naondoka na huyu mwenzenu kwa sababu sishindwi kumshut kabla yenu hamjanishut. Alisema.

Tukutane Sehemu ya 09
** Wasiliana na mtunzi whtsapp kwa no: 0774320110
** page ya story zangu facebook: hadithi za seid
 
** Wasiliana na mtunzi kupitia ukurasa wa whtsapp: 0774320110
** page ya story zangu facebook: Hadithi za seid
 
Back
Top Bottom