Riwaya: Msamaha kwa mama

Riwaya: Msamaha kwa mama

seidss98

Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
17
Reaction score
7
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM.

Mwanzo
Kumbu kumbu.....

"Mama!, Kila siku nakuuliza kuhusu baba yangu yuko wapi hunijibu na kunambia utanambia utanambia utanambia, nna miaka tisa sasa hivi simjui baba yangu. kwa nini lakini mama!, kuna kitu gani hasa kikubwa kinakufanya usinambie ukweli kuhusu baba, naomba uniambie tafadhali mama. nakuomba usinifiche, shule tunasoma kila siku mficha maradhi kifo umuumbua, na bora aibu kuliko fedheha, au unahisi mimi nakuwa katika hali nzuri nnapowaona marafiki zangu wapo na wazazi wao wote wawili?.

Hiyo ilikuwa kumbu kumbu ya maneno nliyoyakumbuka kipindi nimelala chali katika kitanda ambacho huwa analala mama yangu na mimi kulala chini kutokana na hali duni ya maisha tuliyonayo.
swali hilo lilinifanya nikumbuke mengi sana yaliyotokea nyuma kipindi nna miaka tisa, nkamkumbuka sana mama yangu ambae wakati huo alikuwa ameenda kumtembelea bibi shamba.

Swali nlilomuuliza mama miaka 11 nyuma usiku mmoja wa saa mbili tuliokuwa tumekaa chini chumbani baada ya kumaliza shuguli zote za hapa na pale, lilimfanya mamaangu kipenzi aanze kuonesha dalili ya machozi machoni mwake. alitingisha kichwa. nlipomuangalia nkajua anaashiria kunisikitikia sana. aliinuka chini tulipokuwa tumekaa akashusha pazia ambayo huwa tunaitenganisha kati kwa kati chumbani, akapita upande wa pili ambao kulikuwa na kitanda chake, alilala huku machozi yakianza kumlenga akifikiria swali nlilomuuliza.

Nlimuita mara kadhaa lakini hakuitika, nkajua nimemkosea sana mama angu nkamuambia anisamehe kama nimemkosea, kwani sikuitaji hata siku moja akose furaha kwa ajili yangu.
nliinuka kwenye kigoda nlichokuwa nimekaa na kuingia kwenye neti iliyokuwa imeegeshwa kwenye mkeka nliokuwa naulalia chini siku zote nkalala.

nlikuwa mtoto lakini akili zangu zilikuwa za kiutu uzima, nlizima kibatali na kulala huku nkiwa na mawazo ya kuhisi kumkosea mama yangu kwa kumuuliza kuhusu baba japo ni wajabu wangu kuuliza swali hilo kwake, kwa sababu sikuwai kumuona tokea kuzaliwa kwangu. Tokea nlipojitambua naangaza macho na kumuona mama akiangaika peke yake juu yangu bila kujua baba yuko wapi. Kitu kilichokuwa kinanipa wakati mgumu hata nlipokuwa shule..

Wakati tayari nimelala na kuweka neti vizuri nkiichomeka chini ya mkeka. kwa mbali nlisikia kilio cha chini kwa chini nkageuza uso wangu ili kusikiliza vizuri kilio kinatokea wapi, bado sikufanikiwa licha ya kugeuza uso ikabidi niinue shingo yangu nkitega masikio yote mawili. ndo nligundua anaelia chini kwa chini ni mama yangu. Nlitamani nifunue pazia nimfate na kumuuliza kitu gani kinamliza au ni kwa sababu ya swali langu nlilomuuliza, lakini nkashindwa kwa sababu sikujua yuko katika hali gani, nliofia kufunua pazia nkiogopa kumkuta yuko uchi au katika mavazi ya kuonesha maungo yake.

Ilinibidi Nimuite na nlimuita zaidi ya mara tatu bila kuitika, hasira zilinishika nkageuka upande wa pili nkajikunja huku nkivuta shuka langu la kujifunika, nkajifunika na kuweka vidole masikion ili nsisikie kilio cha mama yangu kipenzi ambae nlimfanya wa pili kwa umuhimu baada ya Mungu alie juu.

namshukuru Mungu kutokana na uchovu nliokuwa nao wa shule pamoja shambani hazikupita dk tatu nlipitiwa na usingizi ulionipeleka mpaka saa kumi na mbili na dk 5 asubuhi nkaamka na kujiandaa kwa ajili ya kuwahi namba shuleni. Nlinawa uso nkavaa nguo na kupaka mafuta mgando ambayo nlikuwa nahakikisha yamerundikana usoni.
Nlipomaliza kuvaa kila kitu nlichukua mkoba wangu uliokuwa tayari umechanika chanika baadhi ya sehemu nkauweka mkono upande kisha nkamuita mama ili anipe chochote kitu kama kipo cha kutumia shuleni.

"Mama naenda shule. nlimuambia mama baada ya kumuita na kuitika, ikiwa kama style ya kumsikilizia atasemaje kama mzazi.

"Ok mwanangu nakutakia masomo mema, kuna shiling mia hapo juu ya mfuniko wa ndoo, ichukue ikifika saa nne utanunua hata bagia ule saa nane ukirudi utakuta chakula tayari. Hali yetu ni masikini mwanangu usije kuona wivu kwa kuwaona wenzio huko shule wanakula vitu vya bei, ni kwa sababu wazee wao wana pesa.

Hayo ndo yalikuwa maneno ya mama akiongea kwa hali ya usingizi.

nliitikia "Haya" nkaangalia juu ya mfuniko na kukuta shiling mia tu, nliichukua na kuiweka mfukon nkamuaga mama mara ya mwisho, nlifungua na kufunga mlango nkatembea haraka haraka kuwahi Namba na kwaride la shule lililokuwa linaanza saa moja na nusu.

" Ah mtoto wa mama huyooooooo!!!

Kama kawaida ya tabia ya watoto wa shule ilivyo, kipindi natembea nlikutana na kundi la wanafunzi waliokuwa wanasoma darasa la nne wakati mi niko la tatu.
ilikuwa si mara yao ya kwanza kunambia maneno hayo kila waliponiona, ni maneno ambayo nlishayazoea kutoka kwao kutokana kuniona kila siku nkiishi na mama yangu bila baba, kibaya zaid nkilala nae chumba kimoja kila siku.

Ni maneno ambayo yalikuwa yakinikera sana kiukweli moyoni japo nlikuwa mtoto, na hasira zote nlizokuwa natoka nazo hapo zilikuwa zikiishia kwa mama kumuuliza swali lililokuwa ni gumu sana kulijibu siku zote nlizokuwa nkimuuliza.

Waliendelea kuniteta kwa kusema maneno yaliyokuwa yakizidi kuniumiza moyoni mwangu kwakweli.

"Mtoto wa mama mbona hutujibu wewe?. " Muacheni bhana amezoea kudeka kwa mama yake huyoo......

Ila sikujali maneno yao kwa sababu nlishayazoea na huwa yanantia hasira sana, na tayari nlikuwa nawahi shuleni sikuitaji hata siku moja kupata adhabu toka kwa walimu au viranja kwa sababu ya kuchelewa mstarini au kwa ajili ya utovu wa nidhamu.

Nlifanikiwa kuwahi mstarini nyimbo ya taifa ilianza kuimbwa, baadae tukaesabu namba na kuingia darasani. Upo muda ambao nlipokuwa darasan nliishia kushika tama kutokana na mawazo mazito ya kuitaji kujua aliko baba yangu, na kujiuliza kwa nini mama nkimuuliza swali kuhusu baba huwa anakasirika, na bora angekuwa anakasirika alafu ananijibu lakini huchukua maamuzi ya kutoka sehemu tunayokuwa tumekaa kabisa machozi yakiwa nje nje...

Saa nane ilipofika nliwahi nyumbani haraka kutokana na njaa iliyokuwa imenikamata, Namshukuru Mungu siku hiyo nlikuta viazi vinne kwenye sufuria baada ya kufika. kwani siku nyingine huwa sikuti kitu kabisa. Nlinawa na kuanza kula pembeni nkiwa na kombe la maji, nlipomaliza nliingia shambani kumuangalia mama.

nlifanikiwa kumuona akiwa anapariria viazi vitamu vilivyokuwa vimezungukwa na magugu, nlitingisha kichwa kwa kumuonea huruma mama, Jua la saa nane lote lilikuwa likimuingia mwilini. nlimfata na kumuamkia

"Mama shkamoo

Aligeuka akaniangalia huku akiitikia shikamoo yangu.
"Maraabaa mwanangu umerudi baba.
"ndio mama nimerudi.
"mmesoma shule.
"ndio tumesoma kiswaili na haiba ya michezo.
"Ok mwanangu umepata vizuri?.
" ndio nimepata mamaa
"aya mwanangu soma uje unisaidie mama yako si unaona nnavyoangaika hapa.

Sikumjibu swali hilo pembeni kulikuwa na dumu la maji pamoja na kikombe, nliyafata nkamimina na kunywa, nlipomaliza aliniuliza.

"Ushakula?

"ndio nimekula. Nlimjibu huku nkimezea maji ya mwisho.
"aya itabidi ujiandae sasa uje hapa unisaidie.

Nlijisikia vibaya baada ya kunambia hivyo, nlijikuta namuambia nkiwa natamani kulia

"Bhana mamaa!!,Ah, nimechoka mimi!

"Mwanangu najua umechoka Ila chakula chetu ndo hiki hiki tutafanyaje?, hata mimi nimechoka lakini najikaza mwanangu.

"Dah! Sawa.
nlitoka pale nkiwa nimevimbisha uso wangu, nliingia ndani na kubadilisha nguo nkarudi shambani kwa ajili ya kumsaidia mama.

Jua la mchana lote lilituishia mwilini, mpaka saa kumi na mbili ndo tulitoka shambani tukiwa na viazi vitano kwa ajili ya kupika usiku.

Nlipofika nje ya nyumba nlitua mzigo mdogo wa kuni nliokuwa nao begani, nkachukua vidumu viwili vya maji kwa ajili ya kwenda kuchukua maji kisimani...

Uchovu mkubwa nlikuwa nao wakati huo ila nlijua kuchota maji ni wajibu wangu, na ndani kulikuwa hakuna maji hata kidogo na mama anatakiwa kuoga. Ilinilazimu kwakweli nsingekubali kumuona mama anabebana na vidumu kwenda kuchota maji wakati mimi nipo. hata niwe nimechokaje. Nlipofika bombani nlishangaa kuwaona watoto ambao nao wana kawaida ya kunitania. nlitamani kurudi nyuma lakini tayari walishaniona, nlisogea hadi kisimani nkiwa nimekunja uso wangu, walinangalia bila kunimaliza mi nkiwa nimeshikilia kifaa cha kuingiza kisimani kuteka maji na kuingiza kwenye vidumu nlivyokuwa navyo.
ukimya ulitanda muda nliofika na kuanza kuteka maji, nlijaza vidumu vyangu vyote viwili, vilipojaa nkabeba kwa ajili ya kuondoka.

"Hahahaaaaaa Mtoto wa mama huyooo lione Sura nyeusi kama usiku. Alisema mtoto mmoja kati yao alieitwa mudy nlipokuwa tayari nimewapa mgongo, ni kama walikuwa wananiteta mioyoni mwao..
" Muacheni huyo amezoea kunyonya maziwa ya mama, jitu zima bado linalala na mama yake iloooooooo lione.
" Kwani hana baba yule? Aliuliza mmoja.
"mamaake alikuwa malaya huyo anatembea na wanaume tofauti akapigwa mimba ndo akapatikana huyu mjinga, muone vile.

Ni maneno ambayo yaliniuma sana walipoyaongea baada ya kuwapa mgongo, nliweka vidumu chini mbele yangu nkayaona mawe matatu, nliyaokota na kuwarushia moja baada ya lengine kwa hasira nlizokuwa nazo, Moja ya watoto hao waliokuwa watano jiwe lilimpata na kumjeruhi vikali karibu na jicho lake la kulia, wote waliingiwa na mshangao wa "Haaaaa" huku huyo aliejeruiliwa akiinama chini na kuanza kulia.

Nlipoona hivyo nlikimbia na kuviacha vidumu, walimuacha mwenzao wakanifukuza lakini hawakunipata kutokana na uwepesi wa mwili wangu nliokuwa nao pamoja na mbio.
Nlifika nyumbani na kuingia ndani moja kwa moja, mama alikuwa jikoni akashangaa kuona natoka huko nkiwa mbio.
waliokuwa wananifukuza walifika na kumwambia mama anitoe ndani huku wakiwa wanahema.

"Mama Seid mtoe mwanao ndani haraka na sisi tumfanyie kile alichomfanyia mwenzetu.
"Kuna nini kwani jamani nyie watoto?. mama aliuliza kwa mshangao.

"Unajifanya hujui?, mwanao si ndo unavyomfundisha hivyo awapige watu mawe.
"Mnasemaje nyie watoto!!, (mama aliongea akionekana kuchukia kwa alichoambiwa) yani hamna adabu kiasi hicho kumbe e.
"Adabu tayari tulishawapatia wazazi wetu tukupe adabu wee nani kwani? mtoe mwanao ndani tumpige jiwe kama alivyomfanyia mwenzetu.

Watoto waliongea kijeuri, ni kama walikuwa wanamfokea mama yangu wakati hawampati hata kwa robo kiumri.
nliumia sana kusikia wanavyomjibu mama, nkatoka ndani na panga kwa hasira, waliponiona walikimbia na mimi nkawafata kwa nyuma, sikuweza kuwapata lakini kama ningewapata nadhani ningeua kutokana na kile ambacho tayari kilikuwa moyoni.

Nlirudi na kuliweka panga chini huku nkiwa nimevimbisha mdomo, Mama alishika kiuno na kuachia mguno wa "hhhmmm" akishusha pumzi zake.

"Seid umeanza utundu na wewe wa kupigana na wenzio si ndio.
nlishindwa kujibu swali lake, akaniuliza tena akionekana kukasirika na kile nlichokifanya.

"Mama kila siku nakuuliza kuhusu baba hunijibu, kila nkikuuliza hunijibu, kila nkikuuliza hutaki kunijibu kwa nini lakini mama?, mimi sio mtoto kama unavyofikiria, sawa mimi ni mdogo nna miaka tisa tu lakini nna akili za kufikiria mbali, pia nna wajibu wa kuwaona wazazi wangu wote wawili, baba yuko wapi?, Nambie ukweli mama, kama alishafariki sema? haiwezeani mi naenda bombani naambiwa mama yangu ulikuwa Ma, ma (nlishindwa kuongea hilo neno malaya, japo tayari nlishakasirika lakini ufahamu wa kujua alioko mbele yangu ni mama yangu mzazi uliniingia),
kiukweli nliongea kwa hasira sana mama akiwa amesimama na kunangalia, alinambia nimalizie kile nlichokikatisha ndo nkamwambia "naambiwa kuwa ulikuwa unawabadilisha wanaume kila siku ndo maana umenipata mimi na ulipata ujauzito bila kutegemea ndo maana hujui baba yangu aliko, japo siamini hayo maneno kwa sababu wale walionambia ni wadogo hawakuwepo wakati huo lakini baba yangu yuko wapi? nijibu mama usiishie kulia tu kila nkikuuliza..
Machozi yalishaanza kunitoka, mama nae tayari alikuwa anabubujikwa na machozi kwa nilichomuambia.

Itaendelea Sehemu ya Pili kesho asubuhi ya saa tano..
Naitwa Seid Bin Salim,, mtunzi/mwandishi wa riwaya Tanzania,, pia mdau mpya wa Jamii forums..

NAWATAKIA USIKU MWEMA..
 
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA ( sehemu ya pili )
Mwandishi: Seid Bin Salim

Sehemu ya Pili.

Machozi yalishaanza kunitoka, mama nae tayari alikuwa anabubujikwa na machozi kwa nilichomuambia.

" mamaangu mimi nateseka sana mwanao, naomba unambie kuhusu baba niteseke kwa kuchekwa kuishi na mama yangu lakini nkiwa tayari nimeujua ukweli wote, nkienda shule mimi natukanwa mama, mara naambiwa hivi mara vile unasikia raha gani hasa mwanao nnavyofanyiwa vitendo kama hivyo? najisikia vibaya mamaagu nambie ukweli niujue, kikubwa kipi hasa unanificha?

nliongea nkiwa nabubujikwa machozi. Sikuamini juu ya sauti ya huruma nliyoitumia kuongea. kama mama bado angeshindwa kunambia ukweli hatimae kutoka alikokuwa amesimama na kuingia ndani..

kiukweli nliumia sana kwa kitendo cha mama, nlimgeukia akiwa tayari amenipa mgongo nkajaribu kumuita bila kuitika, alipoingia ndani maneno ya hasira nlijikuta yakinitoka bila kujali kama ananisikia au laa.

"Najua unafurahi sana nnavyoteseka, hunipendi mama Hunipendi, unanifanya niishi kama mnyama wakati ni binadam kama wengine kwa nini lakini? au na wewe sio mama yangu uliniokota?

Nlikunja miguu yangu na kuiweka mikono juu nkainamisha uso na kuendelea kulia.

Mama baada ya kuingia ndani alipanda moja kwa moja hadi kitandani, aliendelea kulia kwa uchungu kutokana na kitu nnachomuuliza kila siku kumuuma, sikufahamu kwa nini haitaji kunambia ukweli, nlikuwa mtu wa kulalamika kila leo ili aniambie, nlijaribu kumkomfyuzi kwa kutumia akili zangu za utoto japo anambie tu baba yangu yuko wapi lakini bado sikufanikiwa.
alikuwa mtu mwenye huruma sana, Kwa nlivyomzoea sikuitaji kuamini kama ni roho ya mama yangu huyu huyu anaekubali mwanae nilie kila siku kisa baba, alinijengea mazingira ya kuamini uenda kuna siri nzito sana anaificha nsiifahamu, ila nlijipa moyo wa kuamini ipo siku ntaujua ukweli hata kama ntachelewa, na kilichokuwa kinanipa imani ni methali tunazosoma kila siku shule, huku Nkiapa kwa mungu kama nkiujua ukweli na ukawa uko tofauti ntatokea kumchukia sana mama yangu japo namuona kila siku kuangaika peke yake juu yangu.

Baada ya kulia kwa muda mrefu nliingia ndani nkamkuta mama yupo kitandani akiwa bado ana uwekundu wa macho, nlijua moja kwa moja amelia sana ilibidi nimsogelee na kumuomba anisamehe, nlimpenda sana lakini ni hasira tu ambazo zilikuwa zikinipelekea nimuulize kuhusu baba kila leo japo nlikuwa najua kabisa nkimuambia suala hilo anachukia hata kama alikuwa anacheka.

"Nisamehe sana mama ni hasira tu ambazo huwa zinaniingia mpaka kukuuliza jambo hilo ambalo najua linakukera kila leo. Nlisema kwa upole.
alinishika kichwani huku machozi yakimtoka upya.

"Nimekusamehe mwanangu.

tabasam la machozi liliingia usoni mwangu, nlimuangalia mama nkamshika machoni kumfuta machozi yaliyokuwa yanamtoka. Aliniangalia kwa huzuni machozi yakiwa bado yanamlenga, nlipogonganisha macho yangu na yake nkajua kuna kitu atakuwa ananisikitikia na kunionea huruma sana.

"ngoja niende jikoni nikuandalie chakula si unaona usiku huu unaingia? ,, aliongea akiwa anainuka kitandani mama.
"ndio mama.
"sawa, basi mi naingia jikoni chukua vitabu usome usome hapa, giza likiingia utawasha kibatali nkimaliza kupika ule ulale kesho uwahi shule sawa baba!.
"kesho jumaa mosi.
"Eh nlisahau kabisaaa! kumbe kesho uko nyumbani.
"ndio
"bado si mbaya, mtoto kulala mapema ni wajibu wake, nkimaliza kupika utakula ulale kesho tuamkie shambani sawa baba.
"Sawa mama.

Aliinuka na kusogea sehemu vilipokuwa vyombo, alichukua sufuria mbili, kiberiti pamoja na mfuniko kuelekea nje kulikokuwa na jiko.
Kipindi anataka kutoka nlimuita.
"Mama naomba unirushia huo mkoba wangu wa shule.
aliangalia sehemu ulipo mkoba, akanirushia na kwenda nje kwa ajili ya kupika.
*********

Mama huyu aliejulikana kwa jina la Bi najma baada ya kuingia jikoni na kuanza kupika, Dimbwi zito la mawazo lilimshika ghafla kipindi amekaa pembeni ya mafiga, alishika tama na kujiuliza vitu ambavyo majibu yake yalikuwa ni magumu sana kwa wakati ule lakini pia ni mepesi kwake kuyajibu, Kijana Seid aliendelea kujisomea ndani akisubiri chakula kiive, japo alikuwa mdogo lakini aliamini Elim ndo msingi wa maisha na ndo kitu pekee cha kumuondoa kwenye umasikini walionao yeye na mama yake Najma.

"Sijui mwanangu anafikiria nini mpaka kuniuliza kuhusu baba yake kila siku, laiti kama angekuwa anajua yaliyonikuta na uchungu nnaousikia, asingeniuliza kuhusu huyu mwanaume,
Uhmm ila ipo siku ntamwambia ukweli kwa sababu ni haki yake, Eh mungu nisaidie, sina nia ya kumficha mwanangu namuonea huruma tu mtoto mdogo anataka kujua mambo makubwa na mazito. Alisema peke yake maneno ya kiutu uzima najma.
aliendelea kuwa na mawazo mpaka chakula kilipoiva, alikitoa jikoni akazima jiko na kuingia ndani akiwa na sufuria mikononi.
**********

Nligeuka nkaangalia mlangoni baada ya kusikia mlango ukifunguliwa.

"bado unasoma mwanangu?, aliniuliza akiwa anaweka sufuria chini.

"ndio mama, ushamaliza?. Nlimjibu na kumtupia swali.
"bado kula tu hapa, nakuwekea chakula kwenye sahani kipoe mi naenda kuoga, endelea kusoma nkirudi kitakuwa kishapoa ule utandike ulale sawa!?
"Sawa nimekuelewa.

” au unataka nikutandikie?,, aliniuliza swali lililonifanya nitabasam.
“ hapana mama ntatandika tu mwenyewe. Lakini mama maji hamna unaenda kuoga nini?
nlimuuliza nlipokumbuka vidumu nimeviacha bombani.
"Itabidi nioge haya haya ya kunywa ntafanyaje sasa, wee si umeacha vidumu bombani?

Nlikaa kimya sikuwa na la kuongezea, alimimina maji yaliyokuwa kwenye ndoo ya maji ya kunywa na kwenda kwenye bafu lililopo hatua 20 mpaka 30 kutoka kwenye nyumba yetu kwa ajili ya kuoga.
Giza tayari lilishaingia, nlishusha kanga iliyokuwa kwenye dirisha kama pazia ambayo ipo mpaka leo kuzuia mbuu wasiingie ndani, nlichukua kibatali nkawasha, nlikisogeza karibu na daftari langu nlilokuwa nasoma, nkaendelea kupitia baadhi ya maswali na majibu kujijenga vizuri kiakili.

Somo nlilokuwa nkipenda tokea niko darasa la kwanza ni Hisabati, nlikuwa tayari kufeli masomo mengine lakini si somo hili, nlihakikisha napata mia chini ya mia kila mtihani unaokuja mbele yangu wa hesabu, hata walimu waliokuwa wakinifundisha hesabu walifahamu wazi kuwa nalipenda na kufanya juu chini wakinikazania kuhakikisha sifeli. maks zangu kubwa zilikuwa ni tisini mpaka mia. Walimu wote shuleni walinipenda kutokana na adabu, heshima na mwenendo mzuri wa masomo yangu darasani.

Namshukuru sana Mungu wangu na mama yangu pia aliekuwa kipau mbele kuhakikisha nakuwa vizuri masomoni, alikuwa yuko tayari kufanya lolote kuhakikisha pesa yoyote iliyotakiwa shuleni inapatikana, akili nlizokuwa nazionesha pamoja na jitihada aliamini ntafika ngazi za juu katika masomo.

nlikuwa darasa la tatu tu lakini walimu wote walinipenda kuanzia usafi na kwa mengine mengi nliyokuwa nayo ambayo mwalimu kama mwalimu anapenda kuona kwa mwanafunzi.

Mama alitoka bafuni na kunikuta nkiwa bado najisomea, alisogea pembeni yangu akanangalia nami nliinua uso wangu nkaachia tabasam baada ya kumkuta mama amenitazama.

"Mbona unaniangalia mama?, nlimuuliza
"Hapana mwanangu, nioneshe mlipo soma leo.

nlifunua madaftari tuliosoma siku hiyo nkamuomesha, alifurahi sana alipokuta good good masomo yote matatu, alipomaliza kukagua alianza kunifundisha hesabu za mbele kama ilivyokuwa kawaida yake,,
Pesa za kunipeleka tution hakuwa nazo, hivyo yeye aliamua kuwa mwalimu wangu wa nyumbani hasa katika masomo mawili hesabu na kiswahili, kupitia yeye nlipata mwangaza mkubwa sana darasan na kuonekana bora kila mara kutokana na kukifanyia mazoezi kitu cha mbele kupitia mama.

Ilipofika saa mbili kamili, mama aliniomba nifunike madaftari nkale kisha nlale, nlifanya hivyo madaftari yangu yote nkayaweka kwenye mkoba, nliinuka na kwenda kutundika mkoba wangu kwenye kimsumari kilichokuwa mlangoni, nkachukua chakula kilichokuwa juu ya ndoo na kuanza kula.

"Mama wewe huli? nlimuuliza baada ya kumuangalia na kumuona hana mpango wa kula.
"Nakula mwanangu, we kula ulale sawa baba.

Sikuongea tena kwa sababu kiazi kilikuwa mdomoni, sekunde kadhaa zilipita nkamuangalia tena, nlivyomuona ni kama mtu ambae alikuwa yuko mbali sana kimawazo.

"mbona unaonekana una mawazo? Ilinibidi nimuulize swali hilo, aliniangalia na kunambia sina mawazo ya aina yoyote mwanangu maliza kula ulale....
******

Najma aliendelea kumuangalia mwanae Seid, alitingisha kichwa akimsikitikia baada ya kukumbuka mengi mazito kwenye kichwa chake kuhusu mwanae.

"Masikini mwanangu anaonekana ana akili sana, Nakuomba mungu umuongoze apate kile kilichomo akilini mwake na cha ziada, nami naomba unisaidie nipate riziki zangu kwa njia nzuri nimsomeshe mwanangu uenda ndo msaada wangu mkubwa. Uhm maisha haya!!!, baba mtu yuko mjini huko anakula vyakula vizuri, analalia kitanda kizuri, mwanae analalia vyakula vigumu kama hivi kwa nini wanaume wako hivi lakini, japo angekuja basi kumchukua mwanae akaishi nae huko kwa sababu ana maisha mazuri, mimi aniache na shida zangu nlizonazo. Aliwaza kichwani mwake jicho likigonga usoni mwa seid wakati yuko bize na kula...
*****

Kutokana na mapenzi ya mama aliyonayo kwangu, alipanga zamu ya kulala kitandani kwa wiki moja moja.

** Usikose kufatilia story hii ya kusikitisha kila ikitoka ili ujue nini kimo humu ndani.. kama umeiona na kuipenda msogezee na jirani kisha achia ujumbe wako
 
Inaendelea Sehemu ya Pili... karibu kwa pamoja tuianze safari ya kuifatilia story hii iliyojaa mikasa mingi sana ya maisha yetu ya kila siku..
 
Itaendelea Sehemu ya tatu jioni ya leo.. Karibu tuwe sote kuifatilia story hii ya kuhuzunisha kufuruhisha na kufundisha pia
 
Shukran muungwana naona uelekeo sio mbaya tupo pamoja endelea kumwaga vitu ni hadithi flan ambayo ukiitizama kwa kina kuna madhira makubwa yalimpata bi najma wacha nisubiri.
 
Naenda nawe sambamba ndugu najaribu kuuona mwisho flan wa ushindi kwa kijana kupitia elimu
 
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: Seid Bin Salim

Sehemu ya 03

Ilipoishia....

Kutokana na mapenzi ya mama aliyonayo kwangu, alipanga zamu ya kulala kitandani kwa wiki moja moja.
ni maisha ambayo tulishayazoea, ilipokuwa ikifika zamu yangu mama analala chini,na ikifika zamu ya mama kama hapo, mimi nalala chini.

Songa nayo....

Namshukuru Mungu amenijalia usingizi wa haraka, huwa nkiweka ubavu sigeuki mara mbili tayari nakuwa nimesinzia, nlipoingia kwenye neti hazikupita dk tano tayari nkawa mbali sana kindoto, sikuweza kushtuka wala kuelewa chochote kilichoendelea kwa upande wa mama mpaka asubuhi ya saa moja nliposhtuka.

sikushtuka kwa uwezo wangu bali ni kwa sababu ya mlango wa kutokea nje baada ya kusikia mama anauburuta kuufungua, nliamka na kukaa kwenye neti nkipikicha pikicha macho ambayo bado yalikuwa na usingizi.

"Shkamoo mama ,,nlimsalimia huku nkiwa naona kama malue lue mbele yangu kwa sababu ya matongo tongo ya kuamka nliyokuwa nayo pembezoni mwa ncha za macho yangu.

Mama aligeuka akaniitikia shkamoo yangu.
"umeamka baba? ,, aliniuliza.
"ndio mama nimeamka.
"vizuri mwanangu, basi toa neti uingize uvunguni kama kawaida, ukimaliza upige mswaki, kuna kiazi hapa kilibakia jana unaweza kukimalizia ili utafune chochote kisha utanifata shambani sawa!?.
"Sawa mama.

nlimuitika nkiwa natoka kwenye neti, alimalizia kufungua mlango akatoka nje kwa ajili ya kwenda shambani.

Nliamka na kuchukua kisturi kilichoko pembeni ya mlango nkanyagie ili kupatia juu ilipo neti, nlipanda nkaitoa kisha nkaikunja na kuiingiza uvunguni mwa kitanda. Nlichukua mswaki wa mti ambao nautumia kila siku na maji kidogo yaliyokuwa kwenye ndoo kwa ajili ya kunawa usoni..

Nadhani watoto wengi wamepitia katika hali hii hapa nliyokuwa nayo mimi, miongoni mwa vitu nlivyokuwa sivipendi ni kuoga, kwa nnavyokumbuka mpaka siku hiyo nlikuwa na zaid ya mwezi mzima sijui maji yanawekwaje mwilini, ilifikia kipindi nkawa nagombana na mama yangu kwa sababu ya kuoga.

nlimaliza kupiga mswaki nkaingia ndani, nkafunua kwenye sufuria na kukuta viazi viwili, nlivitoa vyote nkala kwa sababu nlikuwa tayari nna njaa, nlimfata mama shambani kumsaidia kulima na kupariria baadhi ya sehemu ambazo zilipandwa viazi vitamu, mpaka ilipofika saa nne na robo tulitoka nshambani kama kawaida yetu yeye akiwa amebeba viazi mimi kuni za kupikia ambazo huwa nazitafuta humo humo shambani kwa kuangaika baadhi ya sehemu zenye miti miti.

ni kama nlivyokuwa nimezoea na kufanya siku zote, nkitua kuni nachukua vidumu naenda bombani nkirud nasoma mpaka chakula kinapoiva. na siku hiyo nlifanya hivyo hivyo kwa kuwa nlishazoea bila kukumbushwa nafanya.

Ilipofika saa saba, mama alipanda kitandani ili apumzike japo nusu saa kabla ya kurudi tena shambani, nlimfata kitandani alipokuwa amelala na kukaa pembeni yake huku nkimuita.

"Naomba niende kumsalimia bibi kisha jioni narudi. Nlisema.
"Mwanangu unataka kukimbia kazi? ,,mama aliniuliza kiunyonge akionekana kulemewa na usingizi.
"Hapana mama, nna wiki mbili sasa hivi sijamwona bibi, naenda kumsalimia tu nakurudi mamaangu, kesho ni jumaa pili ntakuwepo nyumbani na ntafanya kazi.
"Sawa mwanangu baiskel yako si ni nzima?
"ndio mama.
"sawa msalimie sana
"Ok mama asante kwa kuniruhusu.

hakujibu, aligeuza ubavu wake akageukia sehemu ya pili akitafuta usingizi.
nlitoka nkafungua mlango na kuurudishia, nkaingia kwenye chumba kilichokuwa na baiskel, nlitoka nayo nje nkapanda na kuanzisha safari ya kwenda kwa bibi moyoni nkiwa na nia ya kwenda kumbana ili anambie ukweli wowote kuhusu baba au mwanaume aliempa mama mimba mpaka nkazaliwa mimi.

Kutokana na nlivyokuwa napenda kuendesha baiskel, sikumaliza dk 28 tayari nlikuwa kwenye nyumba ya makuti ambayo alikuwa akiishi bibi peke yake maeneo ya matemwe zanzibar.
nliegesha baiskel huku nkimuita, nlimuita zaid ya mara nne bila kuitika, nkaingia ndani bila kufanikiwa kumuona, nlijua maeneo yake yote anayokuwa akipenda kuwepo kama si ndani.
Nlingiza baiskel yangu ndani na kwenda nyuma ya nyumba kulikokuwa na mti mkubwa wa mnazi, nkajua lazima atakuwa huko na kama si huko basi ni kwenye shamba la karafuu.

Nlifanikiwa kumkuta chini ya mnazi nyuma ya nyumba akiwa anasokota mkeka, pembeni yake akiwa na jagi la maji pamoja na kikombe kikubwa, miguu yake alikuwa ameinyoosha akikazana kusokota mkeka.

nlimnyatia kwa nyuma ili nimzibe macho kama kumsaprize.

"Nishakuona mjukuu wangu huna haja ya kunyata tena. Alisema bibi.

nlijikuta nasema "Duh" bibi mwanga huyu" kimoyo moyo kisha nkamuuliza" umenionaje bibi wakati sijakuona kugeuza macho kama si uchawi?

"harufu yako naijua mjukuu wangu,.
"um harufu yangu?
"ndio.
"Ah hakuna lolote ndo maana mabibi mnaambiwaga wachawi hivi hivi, sijaona ukigeuza uso, niko nyuma yako hata kama ni harufu duh, Shkamoo bibi.
"Maraaba maraaaba baba ujambo!
"sijambo bibi.
"mama yuko wapi!
"yuko nyumbani amelala kasema nimsalimie sana.
"ok sawa, niko nasuka mkeka wa harusi hapa au hutaki kunioa unaniongopea.

nliishia kucheka bila kujibu chochote, nlimuangalia bibi anavyosuka mkeka, dk kadhaa zilipita tukiongea vitu flan vya kawaida kama bibi na mjukuu wake huku tukifurahi na kucheka sana.

Nlikatisha maongezi baada ya kuona tunachokiongea kinazidi kunoga wakati point ya msingi iliyonipeleka sijaiongea, nlimuita na yeye akaniitikia kwa haraka huku akiwa analamba kidole chake kipate mate flan ya kushikiza vizuri ukilii za kusukia mkeka.

"bibi naomba nikuulize swali nisameee lakini kabla ya kukuuliza.

alinyanyua jicho lake na kunitazama akanambia Uliza kisha akaendelea kusuka mkeka.
"Bibi tokea nizaliwe sijawahi muona baba, na sijawai kuambiwa kama amefariki au laa naomba unambie bibi kama unajua chochote.

Baada ya kumuuliza nlikaa kimya nkashikilia tama nkiwa nimekunja miguu huku nkimuangalia bibi anavyokazana na mkeka. Hakujibu swali langu, alikaa kimya ndani ya dk moja, aliachia pumzi kisha akauweka pembeni mkeka.
"Kweli mjukuu wangu umekuwa mpaka unauliza kuhusu baba!, aya nambie unataka ukweli gani!?
"wowote bibi ikiwezekana unambie tu aliko baba.
"usijli mjukuu wangu, ukweli utaujua tu kwa kuwa umeuitaji, Ni Stori ndefu na inataji moyo kuisimlia, hasa mama yako ngumu sana kukwambia, anajisikia uchungu sana pale alipo ila anavumilia ili kuhakikisha anakulea vizuri na kukupatia Elim, na kwa kuwa umeuitaji ukweli mimi ntakusimlia yale nnayoyajua ujue kila kitu kwa sababu mama yako ukimuuliza chochote kuhusu baba yako anaweza kufa kutokana na yaliyomkuta. Ila Njoo kesho asubuhi ndo ntakuambia leo sikuambii!
"aaaaagh bibi kwa nini usinambie sasa hivi?, hujui kiasi gani nateseka bibi, nkishaujua ukweli hata nkiteseka poa tu, naumia kwa kuwa naona yanayonikuta kisha sijui chochote naomba unambie sasa hivi tu. Nlisema. Alinipiga jicho la sekunde kadhaa kisha kuniuliza.
"Babaako unamjua anaitwa nani?

Kiukweli Lilikuwa ni swali gumu sana kwangu kwa sababu sijawai kuambiwa baba yangu anaitwa nani, kumbu kumbu ambazo nlikuwa nazo ni kumbu kumbu za jina la Sharif ambalo nliambiwa ni la babu yangu na ndo jina nnalotumia shule.

"Bibi!, mama hajawai kunambia jina la baba yangu, tokea nlipoanza shule nliandikishwa kwa jina la Said sharif, nlipokuja kumuuliza sharif ndo jina la baba alisema la Babu.
"ni kweli mjukuu wangu, Sharif ni babu yako, Mwanangu najma hakuitaji utumie jina la baba yako kwa sababu anamchukia sana kwa vitendo alivyo mfanyia.

Bibi alitoa kikombe kilichokuwa juu ya jagi nkamsaidia kumimina maji ya kunywa. Alikunywa taratibu alipomaliza alirudishia kikombe, akasogea nyuma kidogo kwa ajili ya kuegamia kwenye mti, alitoa sauti ya "E, E, E, e akiashiria uchovu wa mgongo baada ya kuukalisha bila kuuegemesha sehemu muda mrefu, aliachia pumzi kisha akaanza kunipa ukweli kuhusu baba, huku na mimi nkikaa makini kumsikiliza.
"Mjukuu wangu, waswahili wanasema Usichokijua ni sawa na usiku wa kiza.
"Pia kilichoko nyuma ya pazia huwezi kukijua mpaka liondoshwe au uambiwe.
nlijikuta nadakia maneno yake, na kumbakiza akicheka.

"kweli umekuwa inabidi unioe tu sasa hivi, alisema kiutani akaendelea kunipa story... nakumbuka ilikuwaaaaaa! Tarehe 05/02/1990 Wazee wa baba yako ambao ni babu zako, walipiga hodi kwenye nyumba yangu hii na kuleta barua ya kumuoa mama yako, kutokana na mila za hapa kijijini kwetu nliipokea vizuri na mimi hapo nguvu bado zilikuwemo hata macho yangu yalikuwa mazima, nliisoma, nlipomaliza nkawauliza.
"Ni nani mmekuja kumtolea hii posa?
walijibu kwa kusema "mtoto wetu Suudy japo bado anasoma lakini anaitaji kuoa, na tumeona tuoe katika ukoo wako mama kwa sababu ukoo wako una heshima zote.

Mjukuu wangu mama yako ndo alikuwa amemaliza darasa la tisa, sikuweza kukataa, nliongea nao muda mrefu tukapanga mambo ya mahari, Najma mama yako nlimueleza akakubali na baada ya wiki mbili ndoa ikapita.

masoudy ambae ndo baba yako mzazi. wakati huo alikuwa amemaliza form six anasubiri majibu yake.
Waliuanza ukurasa wa ndoa baada ya ndoa kupita na walikuwa wanapendana sana sana zaidi ya sanna. kila mmoja aliiangalia ndoa yao kwa jicho la tatu kutokana na mapenzi mazito waliyokuwa wakioneshana.
wakienda shamba wanaenda wote, kisiman kuchota maji wotee, sokoni wotee, kiufupi kila sehemu.

Baba yako wapo waliomuita mume bwege kwa alivyokuwa akishugulika kumsaidia mama yako, mara anafua nguo na watu wanamuona, mi mwenyewe nliwai kumkuta anaosha vyombo nlipomuuliza akasema namsaidia mke wangu kachoka leo, siku nyingine anapika, na kufanya vingine vingi kama kumsaidia mkewe.

katika shamba lao walipanda mpunga mwingi pamoja na mahindi, wakiamini vitawasaidia sana mbele kiuchumi au hata kipesa.
Walifanya mengi ndani ya miezi michache ya ndoa yao, na kupata mafanikio mengi ambayo kila mtu wa hapa kijijini aliyatamani.

Baada ya miezi sita kupita. masody alipata furaha mpya katika maisha yake alipopata matokeo ya masomo na kukuta maks zake ni za kwendelea, wiki kadhaa zilipopita akajiunga na chuo cha Suza (univarsty of Zanzibar).

Najma alimjali kwa kila kitu mmewe,
masoudy unene ulianza kuuandama mwili wake kutokana na maanjumati aliyokuwa akiyapata kwa mkewe na kumfanya arizike. Ila Alama ya kuuliza ilianza kupita pande zote mbili yani kwangu na familia ya masoudy baada ya kuona mwaka umeisha wakiwa katika ndoa hata dalili ya najma kubeba mimba haipo, ndipo kikao cha familia zote kilifanyika ikabidi tulazimike kuwaweka chini kuwauliza, walichotujibu ilitulazimu tuwe wapole na kurizika kwa majibu yao.
"waliwajibu nini?
nliingilia tena maongezi ya bibi baada ya kuona sijaelewa vizuri.
"Swali zuri, walituambia wamepanga wasizae mpaka masody amalize chuo.
Maisha yalisonga mbele, siku na miezi ikakatika, mapenzi yao yakionekana kuwa marudufu kila siku.

Mjukuu wangu!, mwaka 1992 wakiwa tayari wana miaka miwili ndani ya ndoa yao, lilitokea Tukio ambalo sitolisahau katika maisha yangu yote ya duniani, na hicho ndo kitu ambacho nahisi najma ataendelea kulaani juu ya babaako japo yapo mengi mabaya aliyomfanyia na najma kuyavumilia, ila kwa hilo tukio!, Kama baba yako atakaa siku moja chini na kulifikiria, basi naamini siku moja atarudi kwa mama yako akiwa amepiga magoti chini akiitaji msamaha, kwani ni wanawake wachache sana wanaweza kujitolea kwa jinsi alivyojitolea mwanangu najma ili kuokoa maisha ya mmewe.

>> NINI KILIENDELEA ??.. nitaipost kesho.
 
Mwandishi: Seid Bin Salim.

Sehemu ya 04

Ilipoishia jana....

"kilitokea nini?
Ni swali nlilouliza baada ya kuona amenifumba na mimi nlitaka kwenda nae sawa.

"Swali zuri, mwaka 1992 baba yako akiwa anatoka chuo baada ya kumaliza kufanya mitihani, aligongwa na gari lililokuwa linaenda mbio, na dereva kutokomea kusiko julikana, vijana walioliona tukio hilo walijaribu kulifatilia gari lililosababisha ajali na kukimbia bila kufanikiwa, haraka walimpeleka hospital ya mnazi mmoja darajani. Najma alipopata taarifa alizimia, alipozinduka aliomba aende hospital haraka akamuone mmewe kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwake.

Alipimwa ndani ya siku mbili, ndugu wa masoud pamoja na Najma waliitwa ofisini kuelezwa kinachoendelea, ndipo waliambiwa Anaitaji kuongezewa damu na figo ili kurudisha uhai wake kwani figo moja limekufa na lililobakia halina nguvu za kujitemegea.

Mjukuu wangu! ndugu zake wote waligoma kutoa damu kwa Masoud wakidai wana damu ndogo hata figo pia kumtolea walishindwa, mwanangu akasema bora nife mimi kuliko mme wangu, akaomba apimwe damu kama magroup yanaendana atatoa, na kama mafigo yake mawili yanafanya kazi basi atatoa moja, alisema hivyo huku akiwa anabubujikwa na machozi na ishallah machozi aliyoyamwaga siku hiyo mungu atayalipa tu.

Docta alimuomba aingie kwenye chumba cha maabara, alipimwa damu na kukutwa ana group A kama masoud na mafigo yake mawili yako vizuri ndipo opration ya kutoa figo na damu ilianza.

Walifanya opraishen vizuri, baada ya siku kama tano hivi, masoud akawa mzima, alimshukuru sana mke wake, walifurahi sana siku hiyo maisha yakasonga mbele.

Baada ya miezi mitatu, matokeo ya vyuo yalitoka, masoud alipata maks nzuri, akachaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi bora wa chuo cha suza, matajiri wenye makampuni makubwa walimuita kwa ajili ya kuongea nae ili awafanyie kazi zao za kiofice, Mungu akamuwekea wepesi na kufanikiwa kujiunga na kampuni moja kubwa tu iko huko mjini.

Ilikuwa ni kama sherehe kwa najma, Hakuamini kama mme wake atapata utajiri wa mali ndani ya miaka michache kiasi hicho, aliinua mikono yake juu mwanangu na kumuombea mmewe kwa mungu ili mali zake ziwe na baraka.

Masoud baada ya kupata kazi kutoka kwenye makampuni yaliyokuwa yanaongozwa na wazungu, alikabidhiwa nyumba na gari la kutembelea, Walitakiwa wahamie mjini yeye na mke wake. ndugu wote waliitana wakaandaa kashuguli kadogo ka kumuombea dua. Alimchukua mkewe pamoja na ndugu zake wengine wakaenda mjini kupaona.

Najma hakuamini kama ipo siku moja angeishi kwenye nyumba ya kifahari haraka hivyo, siku ya kwanza alipofika alizimia zaid ya mara moja kwa sababu ya mshangao, wapo baadhi walimcheka kwa ushamba lakini haikuwa ushamba bali mazingira tu yalimchanganya, tokea kuzaliwa kwake alikuwa hajawai kukanyaga kwenye nyumba yenye mandhari nzuri..

Masiku, wiki, miezi ilikatika baada ya kuamia mjini, shida zote ziliwakimbia na utajiri kupisha hodi, unene ulianza kuiandama mili yao kutokana na kurizika na vyakula wanavyokula, namna walivyokuwa wametakata kwa pesa hukuweza kuwajua kirahisi kama ulipotezana nao miezi mitano au zaid.

Nakumbuka siku moja mwanangu alikuja kunitembea akiwa na gari dogo la kutembelea, tuliongea mengi akanipatia pesa za matumizi, ila katika maongezi yetu nkamwambia "mwanangu, mali hizo ni za mwanaume, siku yoyote anaweza kukuacha na wanaume wa siku hizi wasivyokuwa na haya, anaweza asikupe chochote japo mali mmechuma wote, hivyo basi kuna kijishamba kinauzwa hapo jirani laki tatu na nusu, inabidi ukinunue kisha uweke watu wajenge japo kijibanda, maisha yanaweza kukushinda huko utakuja uendelee na kwako.

Mwanangu hakuwa mbishi, alinisikiliza ila akanambia sasa hivi hizo pesa hana akipata tu atakuja kulinunua, sasa sijui alisahau! au vipi maana sikumuona tena.
Maisha yao yalisonga mbele, shamba kubwa la masoud lililokuwa huku kijijini, kwa kuwa walikuwa hawaishi tena, nyumba iliyokuwa imejengwa ndani ya shamba iliendelea kuwepo, waliitwa watu wakalima mpunga, na mazao mengine ambayo walihisi badae yatawaingizia faida.

Mjukuu wangu mimi niishie hapo!!, mengine itabidi ukamuulize mama yako nahisi atakuambia, mbane usimpe nafasi japo yanamuuma lakini atakuambia tu kwa kuwa ushaupata mwanzo wake, akikusimlia yeye ni vizuri zaid kwani kuna vya siri nsivyovijua na wewe kwa kuwa unaonekana kuwa tayari una akili anaweza kukuambia, cha mwisho nnachokumbuka mimi, ilikuwa ni usiku wa tareeeeeeeee! 12 mwezi wa 5 mwaka 1993 ambapo tayari alikuwa na mimba yako, alikuja hapa akiwa analia na kijibegi flan hivi kidogo, kumuuliza kulikoni akasema "mama wee acha tu, sikuamini kama masoud anaweza kunifanyia hivi mimi? nliyoyashuhudia kwake yanatosha, na alivyonitesa mimi nkavumilia vyote na mwisho kudai talaka yangu mungu atanilipia tu, kwani nimemvumilia vya kutosha, kiukweli mamaangu bado siamini kama kupata mali tu angebadilika kiasi hiki.

sikuitaji kumuuliza zaid kwa sababu wanaume mi nawajua hasa wakishapata mali, sikumshauri akadai haki yake wala nini, kwa sababu asingeweza kutokana na upole alionao mamaako, nlichomuambia akae chini amuombe mungu wake atamsaidia, wasipolipana hapa duniani basi watalipana kwa mungu.
Ila kwa alichomfanyia kama amefanyiwa kweli mambo aliyoniadisia basi naamini ipo siku moja tu mungu ameipanga kwa kuwa malipo hapa hapa duniani!!, hatta siangaiki najua ipo siku na sisi tutacheka tu kumuona masoud akidhalilika, na kiungo cha mwanangu kilichoko mwilini mwake Nshallah kitamtafuna taratibu!. Alisema bibi.

"Bibi naomba unambie tu kila kitu nadhani mama hatoweza kunambia chochote mimi!

nliongea huku machozi yakinilenga, nlijikuta nkijuta baada ya muda mrefu kumuhisi mama vibaya kumbe alitendewa unyama kwa mujibu wa maneno ya bibi, bibi nae japo macho yalikuwa yakizee lakini yalianza kuiva alipokumbuka mambo yaliyomkuta mwanae, alinigomea kabisa kunambia chochote kilichoendelea, tayari nlishakuwa na mzuka wa kujua kila kitu kilichomtokea mama, sikupoteza muda nlimuaga bibi na kumuambia ntakuja kukusalimia kesho, nlitoka mbio mpaka ndani nkachukua baiskel yangu na kuanza kurudi nyumbani haraka, njia nzima moyoni mwangu kulikuwa na maneno ya" Lazima leo mama anambie ukweli wote sikubali, kumbe baba yangu ndo mshenzi wa tabia hayawani mkubwa!!!.

kama pedeli zingekuwa zinaongea nadhani siku hiyo zingeongea kuwa zinaumia kwa jinsi nlivyo kuwa nazikandamiza. Hazikupita dk kumi tayari nlikuwa nyumbani, nlishuka kwenye baiskel nkaiegesha kwenye mti wa korosho uliokuwa mbele ya nyumba yetu, nliingia ndani kwa kasi nkiita mama, mama tayari alikuwa shambani ikabidi nimfate huko huko.

nlipoingia shambani, nlimkuta anapariria, nkamuita. aligeuka na kunangalia huku akiniitikia.

" Shkamoo
"maraaba mwanangu umerudi baba.
"Ndio nimerudi, mama kuna kitu nataka tuongee ila ndani.
"um we mtoto mbona unavisa hapa haiwezekani kwani?.
"inawezekana ila naomba twende ndani.
"hhmm sawa.

aliniskiliza akanambia nichukue baadhi ya vitu. tulipoingia ndani alikaa kitandani kisha mimi nkavuta kisturi ili kumkalia kitako.

"Mama!, Naomba unisamehe mamaangu kwanza nimekukosea sana, siku zote nlikuwa nahisi uenda ulimtendea ubaya baba ndo maana hutaki kunambia chochote kuhusu yeye, ila bibi kaniambia kila kitu kilichokukuta na kunambia mengine utanambia wewe, nakuomba mamaangu unambie kila kitu kwani kufanya hivyo mimi ntapata msukumo flan wa kunifanya niwe na hasira za kusoma kwa bidii katika masomo yangu ili siku moja niwe na maisha bora, tafadhali mama.

Nlisema. Sikuweza kumuangalia machoni mama.
macho yake yalishabadilika nlipomtamkia maneno hayo, uso wake ulishakaa kihuruma, nlikumbuka maneno ya wahenga ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni, ukimwangalia unaweza kujikuta unashindwa kumuua na kukuua wewe.
"Mwanangu, bibi yako kakuambia kitu gani.?
aliniuliza kwa mshangao, nami nkamjibu.
"amenambia baba alivyokuoa mwaka 1990, mliishi kwa raha, matatizo yalianza alipopata mali, naskia alikutesa sana ndo maana ukarud nyumbani, hakuitaji kunambia vyote kwa sababu hayo mengine kasema hayajui vizuri, naitaji kujua ukweli wote mamaa! please nambie kila kitu mama angu niwe na amani, hata nkiwa natembea niwe najua ukweli wote nnao.

Mama hakuwa na jinsi, baada ya kusikia bibi ashanambia nusu, aliona haina maana tena akaamua kunisimlia kila kitu kilivyokuwa.

" Ni kweli mwanangu, baba yako anaitwa Masoud, ila namchukia kwa yale aliyonifanyia, na sikufundishi hata siku moja umchukie babaako kama utamwona, kwani waswahili wanasema mpende aliemtendea ubaya mtu muhimu katika maisha yako.
Sikuitaji kukuambia chochote kwa sababu ni story inayoniumiza ndani ya moyo wangu kila nkiikumbuka, na najaribu kuisahau moyoni lakini huwa nashindwa.
Babaako alikuwa ni mtu mzuri sana, alikuja kubadilika ghafla baada ya mimba yangu kuanza kukua, na sitomsameehe mpaka kiama kinasimama kwa alichonifanyia....

Mama alianza kulia, huruma iliniingia lakini nlionesha ukakamavu ili niujue ukweli wote hata nsiotakiwa kuujua nliitaji kuujua.
"nadhani bibi yako amekuambia mpaka tulivyohamia mjini. Alisema.
"Ndio mama
"Ok!! ni kweli tulihamia mjini mara tu baba yako alipoajiriwa kwenye kampuni kubwa na kupatiwa nyumba kubwa ya kuishi, nlifurahi sana nkijua ndo mwisho wa matatizo yangu, nliinua mikono juu na kumshukuru Mungu kwa kuniondolea tabu zilizokuwa zimenizunguka. bila kujua mabaya zaid yanakuja mbele yangu. hapo ndipo nlijua kweli ng'ombe wa maskini hazai na watu kama sisi tumezaliwa kwa ajili ya mikosi.

Tulikaa miezi sita kwa furaha huko mjini, hali yangu ilianza kubadilika kila leo bila kujua tatizo ni nini, kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo baba yako kwangu alinipeleka hospital haraka kupima vipimo vyote ndipo nkakutwa nna mimba ya mwezi mmoja.

Mme wangu alionekana mwenye furaha, tulikumbatiana mbele ya docta alietupatia majibu hayo, lakini nilishangaa kipindi tunarud nyumbani kwenye gari hakuniongelesha chochote na kila nlipomuongelesha hakujibu.

tulipofika nyumbani ilibidi nimuuliza.
"Tatizo nini mme wangu?

Nliongea kwa huruma na sauti ya chini kwani tayari nlishahisi kuna kitu nimemkosea mme wangu na mimi nlikuwa sipendi nimkosee kwa lolote.

Nlipomuuliza hivyo aliniangalia sana kwa jicho la husda mpaka nliogopa, alionekana kuwa mtu alojawa na hasira, aligeuka akanipa mgongo kisha akanambia " SIITAJI KUZAA KWA SASA HIVI.

Itaendelea... Itapostiwa Jioni ya leo saa kumi na mbili na nusu..
Kama unaifatilia kwa makini tokea ianze kupostiwa,, Mpe ushauri mwandishi na mtunzi,, Coment chochote kuonesha uwepo wako..
 
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 005

Niliongea kwa huruma na sauti ya chini kwani tayari nilishahisi kuna kitu nimemkosea mme wangu na mimi nlikuwa sipendi nimkosee kwa lolote.

Nilipomuuliza hivyo aliniangalia sana kwa jicho la husda mpaka nliogopa, alionekana kuwa mtu aliejawa na hasira, aligeuka akanipa mgongo kisha akanambia " SIITAJI KUZAA KWA SASA HIVI..

Ni jibu ambalo lilinifanya jasho lianze kunitoka kabla hata ya kumuuliza kwa nini, nlihisi tumbo linauma, mwili wote uliishiwa nguvu, nlitoa macho na kumuuliza kwa sauti ya upole.
"Kwa nini hutaki kuzaa?.
"Siitaji maswali, bali nimekwambia sitaki kuzaa nielewe mwanamke!. alinijibu hivyo baada ya kumuuliza.

Alitoka akaingia chumbani, nlijaribu kumuita mme wangu mme wangu lakini hakuitika, nlijua labda ananitania ilibidi nimfate chumbani, nlimkuta amelala chali miguu chini akiwa hajavua viatu, ilikuwa kawaida yangu kila siku kumvua viatu kwa sababu tayari nlishakubali kuwa mjinga kwake ili kulinda ndoa yangu. Nliteremka chini nkiwa katika hali ya unyonge, nkamvua viatu vyake pamoja na soks, nlisogea na kumuuliza tena machozi yakiwa yananilenga lenga.

"Mume wangu, uko serious kwa ulichonambia au unantania!?....
"Siitaji kuongea chochote niache nipumzike. alisema kwa mkato.
"Mume wangu hali yangu si nzuri nambie ukweli basi, please ongea chochote kile chengine kizuri nionee huruma mwenzio. Nilisema kwa sauti iliyokuwa imejaa upole.
"mwanamke nielewe, siitaji kuzaa kwa sasa. Alisema.

Niliumia sana kusikia hivyo kwa mara ya pili machozi yalianza kunitoka kama mtoto, aligeuka na kulalia tumbo nkasikia akisema maneno yaliyonifanya nikate kulia.

"Tena hiyo mimba nataka uitoe haraka iwezekanavyo.
"Unasemaje masoud!!? ,, nlimuuliza kwa mshangao.

"sii matangazo ya vifo umepewa masikio ili kusikia. Alijibu kwa kunikejeli.
"Masoud unanijibu hivyo mimi leo! kwa kipi kibaya hasa nlichokufanyia?....

kwanzia siku hiyo alianza kubadilika, nyumbani alikuwa akirudi muda anaotaka, ilifika kipindi akawa analala chumba chingine nkimuuliza kwa nini anasema Toa mimba.

Toa mimba ndo ukawa wimbo ulobakia nyumbani, hakukuwa na salama tena kisa mimba, nkafika sehemu nkachoka maneno yake. nakumbuka alikuwa anajiandaa kwenda kazini nlimwambia naomba niende clinic kuandikisha.

Aligeuka na kuniangalia, akaniuliza nasemaje? nkarudia tena nlichomwambia, aliniangali bila kupwepwesa macho zaid ya sekunde nne kisha akasema.
"Nimesema!, toa, hiyo, mimba.
"Hivi masoud kwa nini unakuwa hivi mume wangu ee, kuna familia inaitaji watoto, kuna wanawake hawajapewa kizazi wanalia kila siku mtoto, leo mimi nimejaaliwa kupata mimba unasema nitoe kwa nini lakini?, tena ni ya halali mume wangu hatujazini sisi au ulinioa kwa ajili ya starehe zako binafs?.
"Yyees nlikuoa kwa ajili ya Starehe, alisema masoud kwa hasira.. na bora ningeoa gumba hazai kwa sababu siitaji kuzaa. kwa nini ung'ang'anie wakati staki lakini. siitaji kuzaa mwanamke siitaaajiii kwani lazima!? na usipoitaji kutoa hiyo mimba mtafute baba yake mimi sio.
"Masoud naomba usinifanyie hivo, kwa nini lakini unanifanyia hivyo mimi, kwani kitu gani hasa kikubwa kinakufanya hivyo ee!. Nlianguka chini nkamshika mguu.

Sikuamini kama masoud anaweza kunipiga siku moja, lakini siku hiyo kudhiirisha kuwa hayuko tayari kuzaa na anaichukia mimba yangu, alinigeukia akanisukuma kitandani na kuanza kunipiga ngumi za tumbo huku akilalamika kwa kunambia.

"kwa nini hunielewi wewe mwanamke, au mpaka nikuue ndo uamini, sitaki, Sitaki, Sitaki, sitaki mpumbavu wewe,sasa kwa kuwa hutaki kutoa ngoja niitoe mimi, alaaaa unanletea upuuzi hapa!.

kila aliposema Sitaki, alikuwa akinikandika ngumi za tumbo zilizopelekea kuzimia.
jasho lilikuwa likimtoka, aliniacha bila kujali akaenda kazini, nlipozinduka nlishangaa kuona tumbo linaniuma sana, nlitoka nkaenda hospitalini, docta alinipima akanipatia dawa na kunishauri nipumzike.
Nlirudi nyumbani nkiwa natokwa na machoz. kibaya zaid nlikuwa sijui kwa nini masoud alibadilika kiasi hicho, kiukweli nliumia sana, nlihisi dunia ni chungu ndani ya muda mfupi, nlitamani kufa kwa hali nliyokuwa nayo. Bado sikuacha kumjali mume wangu, niliamini ipo siku mungu atanisaidia na kama mali ndo zimemfanya awe hivyo basi atamkumbusha kuwa anakosea, atajirekebisha.

Mwanangu!. ulikuwa ni usiku wa tarehe mbili siku ambayo sitoisahau katika maisha yangu, alikuwa ameingia bafuni kuoga, cm yake iliita nikasogea karibu kuiangalia nkakutana na jina Yulai'na kwenye screen.

nilishtuka kidogo baada ya kuangalia saa nkakuta ni saa tano usiku, nikajiuliza ni nani huyu anaempigia mume wangu usiku wote huu. nlinyanyua nkapokea, nikaweka sikioni kisha nkakaa kimya kusikia ataongea nini.
Moyo wangu ulianza kuuma na kujuta kwa nini nimepokea nliposikia akisema "Hello Darlin how are you!!
sikuongea chochote nkijua uenda ataongea kitu zaid ya hicho, na kweli baada ya kuona nimekaa kimya akasema.
"Switty! mbona kimya! , au uko na hicho kijimwanamke chako?, ila kama nlivyokuambia naomba usifanye nacho mapenzi. siitaji masoud siitaji, ikifika asubuhi kabla ya kuingia kazini njoo upate vitu vitamu huku ambavyo hakajawai kukupatia si unanijua shuguli yangu?. habari nzuri ambayo nadhani ni kiunganishi kizuri cha mapenzi yetu nimeenda kupima leo nimeambiwa nna kabeby tumboni natamani uwepo ukashike shike katumbo kangu.

sikuweza kuvumilia, miguu ilishika ganzi nkaishiwa nguvu, nlifanikiwa cm kuiweka kwenye meza nkaanguka chini.

Alipotoka bafuni aliniita huku akinimwagia maji ya baridi, nlishtuka nkalala kitandani, aliniuliza kulikoni nkamwambia hakuna ni mshtuko tu, kabla sijamaliza kuongea cm iliingia tena, aliichukua na kutoka nayo seblen, ikabidi nami nisogee nisikie atachokiongea.

"Hello Yu beib. Alisema masoud.
"mbona cm yangu ulikata?
"acha jokez bhna mi nlikuwa naoga beib nambie.
"Sina la kukuambia zaid ya kukuambia tena kesho asubuhi pita uje ukaage katoto kako tumboni nimeenda kupima nna pregnancy.

"Weeeee Sema akyamungu!.
"Akyamungu switty nna mimba yako .
"Heheheeee We mtoto mbona unataka kunifanya nimkimbie huyu mwanamke?. sii kesho nakuja sasa hivi kukaangalia kabeby kangu, Sasa hivi nakuja sawa mamaa!
"Aya njoo switty ntakuwa na amani zaid.
"Niko kwa ajili yako mmmwwaaaa!

alikata cm na kuja haraka chumbani, mimi nlimuwai nkakaa kitandani, alianza kuvaa nkamuuliza unaenda wapi sasa hivi? ,, alinijibu kwa kunambia.

"Haikuhusu.
nlishindwa kuvumilia, nlitoka hadi mlangoni na kumwambia Masoud huendi kokote, alinangalia na kunambia mara tatu naomba unipishe nipite, akaanza kunipiga makofi ya masikio, alinisukuma nkaangukia chini akapita na kuondoka zake.

Nlianza kulia kama mtoto, siku hiyo sikujua nlilala saa ngapi, aliporudi siku ya pili tayari nlishaandaa chai. nilimkaribisha vizuri kama mtu asiejua chochote, nkamuuliza kwa kujiamini nkiwa katika hali ya kawaida.
"Mke mwenzangu hajambo?
"Nini? alishangaa sana kumuuliza hivyo.
"Marudio jumaa mosi kama hujasikia limepita karibu unywe chai.
Ilibidi nimjibu vibaya siku hiyo kutokana na hasira nlizokuwa nazo kwa sababu nlishaona tayari nnakoelekea ni kubaya, nlijutia kwa nini masoud alipata mali, kwa kuwa tayari nlishajua kuwa kuna mwanamke mwenzangu ambae sikujua kama ameoa au laa, ilibidi nipunguze wivu kibaya zaid nkajua hayuko tayari kuzaa na mimi ila yupo mwanamke mwengine ambae yuko tayari kuzaa nae.
Nlipomjibu hivyo aliniuliza.
" Naona una hamu ya kupigwa sio e.
" Nshazoea kupigwa kwa sababu umenigeuza ngoma sasa hivi, kila ukijisikia unapiga tu.
Aliniangalia kwa jicho chafu, aliachia msonyo na kuingia ndani, nami nlimuangalia kwa nyuma, nkasema.
" utasonya sana mwaka huu nshaujua ukweli wala hunibabaishi, japo naumia lakini ntafanyaje.
nliongea kwa kujipa moyo lakini maumivu bado yalikuwa yakinisumbua, machozi yalianza kunitoka upya, nlimimina chai nkajaribu kunywa lakini hakikunyweka nkasukuma kikombe huko kwa hasira...

Matukio kila siku alizidi kunifanyia mapya, nlikuwa nkienda kupima hospital kila kukicha, madocta walinipa ushauri mzuri namshukuru Mungu, kwa kuwa ndo ilikuwa mimba yangu ya kwanza nlifatilia ushauri wao mwanzo mwisho, nlienda kwa wataalam wa ushauri ili kurudisha amani ndani ya ndoa yangu lakini haikuwezekana, nlipoenda kwa wazee wake kumbe tayari alishawambia wote kuwa anataka kuoa mke mwengine ambae ndo mwema kwake na mjanja, walinishambulia kwa maneno tofauti tofauti mabaya, nkawa mtu wa kulia kila siku kila kukicha.

Mwanangu ilikuwa ni siku nyingine tena mbayo sitoisahau katika maisha yangu, nlipokuwa jikoni napika aliniita nami nkaitika, nlitoka jikoni nkaenda seblen na kukutana na sura ya mwanamke aina ya kiarabu.
nlimuangalia huku mme wangu akiwa amekaa kwenye kiti anatingisha miguu, nlimsalimia mume wangu na kumwambia huyo dada karibu. kilichonishangaza baada ya kumwambia hivyo alinisonya akanishusha na kunipandisha. mume wangu alicheka sana, moja kwa moja nkajua uenda huyo ndo Yulaina.

"Najma, aliniita masoud nami nkaitika.
"Abee. Kwa upole.
"Huyu anaitwa Yulaina mtoto mzuri kuliko wote duniani , mtoto wa kiarabu, mtoto mwenye hadhi ya kukaa kwenye nyumba nzuri kama hii. Yani alivyoingia tu na nyumba imecheka kwa sababu ameendana nayo, kama unavyomuona akikaa kwenye sofa anajaa kama jini vile Heheheee vipi tumependeza ee!!!. Alisema.

sikuweza kuvumilia, hasira ziliniingia nkamwambia basi inatosha, nlitoka pale na kuingia ndani chumbani, nkapakia nguo zangu kwenye begi machozi yakiwa yananitoka, hapo tayari nlikuwa na mimba ya miezi mitano na nusu. Nilitoka ndani hadi seblen mwili wangu ukiwa hauna nguvu, nlijaribu kufuta machozi yaliyokuwa yanatoka lakini ilishindikana, nkiwa na begi nlimuangalia masoud nkamwambia.

"Asante Sana, Nashkuru masoud, Mungu akuongoze, Nshallah atanilipia kwa yote nliyokufanyia kama mke, na hiki kiumbe kilichoko tumboni ipo siku moja utakifata tu hali ya kuwa hakikutambui, na hicho kiungo kilichoko mwilini mwako kitakutafuna tu.
Aliniangalia akiwa anacheka, kabla sijatoka nje aliniita na kunambia.
" Cha kukusaidia tu ngoja nikuandikie Talaka zako zote tatu na usahau kuhusu mimi kwa sababu hatuendani, lengine kama hutojali, najua pakuishi patakuwa tabu kidogo kwa sababu huyo mama yako ana kanyumba kana chumba kimoja tu, tena si kanyumba nimekueshim kijibanda, nakuachia shamba la huko kijijini uishi humo na ni lako hilo nimekupa, nnavyokupenda na mkataba wake huu hapa, nakupatia bure si langu mimi hilo silitambui ila tu ntakuja kuvuna kila kilichomo ili upande vya kwako, wasalimie Siwezi kuwa na mwanamke wa kiswahili mimi mshamba mshamba tu, naitaji mwanamke anaejua kutumia bhana, mtoto mzuri huyu hapa kwanza kimahabba humshiki, akiwa kitandani anashugulika kweli, sii wewe dakika mbili eti mume wangu nimechoka, mashine hii hapa toto kuanzia mwili hadi ladha ni switty, sii wewe unaniita switty huku hujui kitu.

"Nashkuru Sana Masoud.

ndo jibu nlilompa baada ya kunambia aliyonambia, nlitoka nje na kukutana na kundi la ndugu zake wote, waliniangalia na kuachia kicheko nkapishana nao wakiingia ndani, nlisikia kauli tofauti tofauti wakizisema, moja ambayo nliishika mpaka kesho.
" yamekushinda ondoka usiwabane wanao weza kuyahimili.

nlitoka na maumivu makubwa sana ambayo sitoyasahau hadi kufa kwangu, na hakuna siku ntayoumia kama siku hiyo katika maisha yangu yote.
machozi yalizidi kunitiririka wakati wote, nlipofika getini nlikutana na mlinzi wa geti, tayari nae alikuwa analia kutokana na huruma aliyokuwa ananionea, kwani nliishi nae vizuri na kumchukulia kama ndugu yangu, alinikumbatia na kuomba nimpatie namba yangu ya cm, nlimpatia akatoa kiasi cha laki moja akanipatia, nlishukuru sana kiukweli huku akinambia maneno ya mwisho.

"Sitoweza kupata bosi aliekuwa na huruma kama wewe, ntakukumbuka daima, ila konga moyo wanaume ndo tulivyo hasa tukisha pata pesa. Nilikuchukulia kama dadaangu wakati ni bossi wangu, nimeshuhudia mengi ukifanyiwa ndani lakini ulivumilia, muda wote nlikuwa nkikuonea huruma bosi unavyoteswa na mumeo, ila ya waswahili hatimae yametimia, Kiukweli nami nahisi sitoweza kuendelea na kazi hapa, bora nikose kibarua kwa ajili yako madam, naomba unisubiri hapo nje niende nimwambie nimeacha kazi ili japo tuongozane nipajue utapoishi kwa sasa, tuendeleze udugu wetu sababu umenisaidia mengi sana ambayo yalinifanya nikuone wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao bado wapo katika dunia hii ya sasa, naomba unisubiri madam niende kuaga niache kabisa hii kazi, kama kibarua nitapata kwengine tu.

TUKUTANE SEHEMU YA 06

Wasiliana na Mtunzi/ mwandishi wa Story pamoja ma nyengine nyingi kwa kupitia namba ya cm: 0774320110 whtsapp/call.
 
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM

SEHEMU YA 06

bora nikose kibarua kwa ajili yako madam, naomba unisubiri hapo nje niende nimwambie nimeacha kazi ili japo tuongozane nipajue utapoishi kwa sasa, tuendeleze udugu wetu sababu umenisaidia mengi sana ambayo yalinifanya nikuone wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao bado wapo katika dunia hii ya sasa, nisubiri madam nikaage kuacha kazi, kama kazi nitapata kwengine tu.

"Hapana naomba usifanye hivyo, usiache kazi kwa ajili yangu, utanipigia cm na ntakuelekeza siku moja utakuja, hii kazi ndo inayoingiza Riziki yako usifanye hivyo kabisa. Ni maneno nliyomuambia, nkamueleza tu aishi nae vizuri hata huyo alieingia ili kulinda kibarua chake.
Nlimuomba anifungulie mlango niondoke, nlitoka na kukodi tex nkaja hadi kwa bibi yako.

Nliishi na bibi yako kipindi chote cha mimba, bado sikukata tamaa nkijua uenda Mungu atamrudisha nyuma mume wangu akumbuke tulikotoka lakini wapi, nlikuja kuamini kuwa ndo basi tena siku moja nikiwa shambani kwenye hili shamba tunaloishi. maana alisema ameniachia shamba lote. nilikuwa nalima lima ghafla nkaona linapaki gari kubwa na dogo, dogo alikuwemo yeye na huyo mwanamke wake, kubwa walijaa vijana ambao walishuka akawapa kazi ya kuvuna kila kilichoko shambani, sikuweza kuwazuia kwa sababu mwenye mali tayari alikuja, walipo maliza kuvuna akiwa peke yake nilimuuliza.
" nimekukosea nini lakini mume wangu mpaka unafaya haya yote. hakujibu swali langu zaid ya kunisonya akaenda alikokuwa mwanamke wake, wakaingia kwenye gari na kuondoka.

Mimba tayari ilishakuwa kubwa, nliteseka sana mimi mwanangu, nlilazimika kubeba mzigo wa kuni wakati tumbo tu lilikuwa mzigo tosha kwangu, kiukweli mpaka najifungua nlipitia mengi sana, nlipojifungua ndo nkahamia hapa kwa sababu kwa bibi yako kama unavyopaona kuna chumba kimoja, nliumia sana mwananguuu miimii, baba yako alinifanyia visa vingi sana ambavyo hata vingine havielezeki, naumia miimii naumia mwananguuu nkizingatia nlimueshimu sana Masoud laki ' Laki ' Lakini..
*****

Mama hakuweza kumalizia neno lakini, alianguka kitandani akiwa tayari amepoteza fahamu, nliumia sana kupata story nzima ya baba, machozi wakati wote yalikuwa yakinitoka, nlijikuta nkijuta kuuliza maswala ambayo yalipelekea mama kupoteza fahamu. nilianza kuita Mama! , Mama!, Mama amka lakini hakuamka. ndipo nilichanganyikiwa nikihisi labda amekufa.
Nilikumbuka darasan kwenye somo la kiswahili tulifundishwa namna mtu anavyoweza kuzirai au kuzimia na kupoteza fahamu muda wa nusu saa au saa, nilijikaza kiume nikachukua mfuniko wa ndoo na kuanza kumpepea nikiwa nalia huku nkisikilizia ikifika nusu saa bila kuamka niende kuita majirani waliokuwa mbali kidogo.

Namshukuru Mungu hazikupita dakika kumi mama aliamka, nikamuomba anisamehe sana kwa kumkumbusha machungu ambayo tayari yalishaanza kufutika moyoni mwake, niliumia sana kiukweli siku hiyo, nilimlaani sana baba yangu japo mama alishanambia nsimchukie aliemfanyia ubaya mtu muhimu katika maisha yangu, lakini nlitengeneza chuki na kuwachukia wanaume wote wanaowanyanyasa wanawake.

Tokea siku hiyo nikawa nasoma kwa bidii sikuwa na mchezo kwenye masomo, rafiki asieitaji kusoma sikumuitaji, nilikuwa beneti na wale wenye akili tu pamoja na walimu. nkisoma kwa uchungu ili ikiwezekana siku moja jina langu liwe miongoni mwa majina makubwa Tanzania nimsaidie mamaangu kipenzi alopitia maisha magumu kiasi cha kuwa magumu kwa ajili yangu...
*****

Hizo zote zilikuwa kumbu kumbu za kijana aitwae Seid akikumbuka stori aliyopewa na mama yake kuhusu mambo aliyofanyiwa na baba yake. kumbu kumbu alizozikumbuka akiwa amelala chali kwenye kitanda baada ya kuwa amefanya shughuli za kutwa nzima.

Zilimfanya amkumbuke sana mama yake aliekuwa ameenda kulala kwa bibi ndani ya usiku huo, macho tayari yalishavimba kwa machozi baada ya kukumbuka kila kitu alichofanyiwa mama yake huku akijisemea moyoni.
" Mungu nisaidie matokeo yangu ya form Six yatoke yakiwa mazuri niingie chuo nije nimsaidie Mama. sijui kwa nini wanaume tunakuwa hivi, ila yote sawa tu mungu yu pamoja nae, Umenisomesha kwa tabu nyingi sana mama yangu, zidi kuniombea nifaulu nkusaidie mamaa umeteseka sana.

Seid alifuta machozi yake yaliyokuwa bado yanaendelea kutoka kutokana na mambo mazito aliyoyakumbuka yaliyotokea miaka zaidi ya 11 nyuma, aligeuka akalalia ubavu wa kulia akazima kibatali na kulala usingizi.
Asubuhi na mapema alipoamka alichukua Jembe na panga akaingia shambani kwa ajili ya kupariria baadhi ya mazao na kuchanja kuni.

Tokea azaliwe mpaka anafikisha umri wa miaka 20 hakuwai kumuona baba yake na wala haitaji kumuona kwa matendo aliyoyafanya. aliendelea kuishi na mama yake akiishi maisha ya kipekee kuliko kijana yoyote, alimpenda mama yake kuliko chochote na kumtii kwa kila kitu alichoambiwa akiamini huyo ndo Mungu wake wa pili....

Mwili wa kijana huyu ulikuwa umetanuka mfano wa miraba sita kutokana na kazi nzito alizokuwa akizifanya kuingiza japo pesa ndogo ya kupata hata mboga na chakula chengine, maisha ya tabu yote kijana huyu aliyapitia, kuna muda alihisi mungu hawaoni yeye na mama yake ndo maana wanateseka, huku akijiuliza kwa nini wengine wanajenga majumba ya kifahari wakati wao hata ya udongo hawana.
Ilipofika mida ya saa tatu Bi najma alirudi toka kwa mama yake na kumkuta kijana wake shambani, alimuita mwanae. Seid aligeuka akamuitikia na kumsalimia.

" maraaba mwanangu pole.
" nshapoa mama hawajambo huko?
" ndio mwanangu hawajambo.
" Vipi umenisalimia kwa bibi?
" ndioo!! na yeye anakusalimia.
" Aya sawa mi nipo, namshukuru Mungu umerudi mamaangu, kwa sababu dah usiku nimekuwaza sana, hivi ule unga jana uliisha?. Alisema mwisho akaulizia mambo ya msosi.
"Hapana ulibaki kidogo tu, usijali lakini kuna mchele nimekuja nao kutoka kwa bibi yako shambani.
" wao leo kumbe wali!? hadi raha ukisikia mtoto hatumwi dukani mamaangu ni hapo.
" Uhm hujaacha tu mwanangu?. alisema bi najma huku akiinama na kunyukua vigugu vilivyokuwa vimebakia sehemu aliyolima mwanae.
" Mtoto hakui kwa mama wee, hapo mboga tu ndo tatizo sasa maisha haya!. aliongea akisimama kumuangalia mama yake.
" Ah! hata tukila hivi ivi sawa tu mwanangu ndo maisha yetu tutafanyaje? ukishakuwa masikini unatakiwa ukubaliane na kila kitu, ebu lete jembe nikusaidie upumzike kwanza.
" Acha tu mama hii ni kazi yangu kama kijana vile vile kumsaidia mama. alisema akaangalia mfukon kama kuna chochote akabahatika kukuta mia tano.
" Nna mia tano hapa bora tununue dagaa tonge la mia tano tuchemshe tutolee kuliko kula hivi ivi.
"sawa si mbaya pia. Alisema bi najma.

Kabla ya kuendelea kupariria seid cm yake iliyokuwa mfukon ilianza kuita, alishtuka akapapasa mfuko haraka na kuitoa, kabla ya kuangalia nani anapiga alitikisa kichwa kisha akamuangalia mama yake, bi najma alimuuliza.

" nini?
"Ni aibu mamaangu hii, vijana wenzangu wanatumia masamsung makubwa makubwa, matarch, mimi natumia samsin jamaniii!!.
" Ebu pokea kwanza cm mwanangu hayo mengine yatafata hee!!. Seid aliangalia kwenye screen akaona jina "Ticha". alipokea huku mama akitikisa kichwa na kusema chini chini " jamani shida hizi, mpaka mtoto anajisikia vibaya!"

"Haloo Ticha Salam alaykum. Alisema seid.
"W/ssalam vipi hali bosi wangu. Alisema wa upande wa pili.
"njema tu mungu anasaidia.
"Uko wapi?
"niko shamba kwetu huku kiwengwa.
"Ok matokeo yanakaribia kutoka kijana, juzi nlienda wizara ya elim nkaona nikuibie vitu. e bhana ndugu yangu umepasua. Alisema wa upande wa pili..
"Ticha nimepasua nini tena?. aliuliza seid akiwa anaachia jembe.
"Yani matokeo yako yako vizuri vibaya mno, umewaburuza Seid form six niamini mimi.
"Eee!!!

Seid hakuweza kuongea chochote, alikata cm uso wake tayari ukiwa umepagawa, japo aliambiwa ni ya kuibia lakini alijikuta na furaha sana, machozi yalianza kumlenga lenga mama yake alisogea karibu na kumuuliza.
" mwanangu vipi! kuna nini?.
Seid hakuweza kujibu, alimuangalia mama yake kisha akaangalia pembeni, macho tayari yalishajaa machozi, mama yake alimuuliza tena.
"Nini mwanangu mbona sikuelewi?
"Mama nimefaulu, Nimefaulu mama!! Eti mimi nimefaulu mimi mama..

aliongea kama mtu asiejielewa, alikaa chini huku akisema Asante Mungu kwa sauti ya kulia, bi najma alimfata na kumwambia ni jambo jema lakini asiamini asilimia mia wakati matokeo hayajatoka, kwa sababu yeye ni maskini matokeo yanaweza kununuliwa pia anaweza kuwa anamtania.

Seid aligeuka na kumuangalia mama yake baada ya kusikia maneno yake.
"Unasemaje mama!, Matokeo yangu mimi yanunuliwe!, sina utani na ticha, ticha ni mtu wangu wa karibu sana lazima alichonambia cha kweli, Mama nshafaulu mimi shida zimeisha, najua naingia chuo mama, naingia tu chuo mimi, Eh asante Mungu.
"Mwanangu ebu punguza munkari!, subiri kwanza hadi yatoke ndo uwe na furaha ya kufaulu kiasi hicho, usiwe hivo wewe ni mtu wa chini mwanangu, mara ngapi matokeo yanachukuliwa na watoto wa wenye mali?
"Mama Mimi ataenunua matokeo yangu Akyamungu naapia mbele yako Namuua,nimekulia kwenye maisha ya shida nna dhiki mpaka nazichukia, kitabu mimi ndo kitaniokoa leo mtu anunue matokeo yangu, nafungua mashtaka au nampiga kipande mama, vyote vikishindikana mimi napelekwa jela nakuapia mamaangu, shida nlizonazo hizi watu walete habari za ujinga naua mimi naua Akyamungu!!!!.

Alijikuta anaongea vitu kwa kupanic baada ya kuambiwa habari za ununuaji wa matokeo wakati ameambiwa kabisa na ticha wake kuwa amewaburuza form six.
"Tumuombe mungu nshallah kwa uwezo wake utapita ila si kujipa uhakika kiasi hicho, kuna mengi pengine jina lako kalifananisha, usiwe na furaha ya kiasi hicho mwanangu.
"Dah mamaangu kipenzi mbona hivyo!, hakulimiki tena hapa nimefurahi na kutibuka pia tuondoke.
Aliongea huku machozi ya furaha yakiwa ndo yanaishia ishia, alinyanyuka akabeba jembe na kumuomba mama watoke shambani, alifika nje ya nyumba yao akatupa jembe chini kisha akamuaga bi najma kwenda kutafuta dagaa tonge (dagaa wadogo wadogo wabichi).

baada ya nusu saa alirudi akiwa na dagaa waliokuwa kwenye gazeti, alimkuta tayari mama yake ashapika wali, ilibidi amsaidie kupika dagaa walipomaliza waliweka msosi chini wakala mchana ukapita....
Tokea siku hiyo seid alikuwa ni kijana wa kuwaza na kuwazua juu ya matokeo aliyoambiwa na rafiki yake mwalimu wake, kila alivyojiuliza alishindwa kujijibu huku uso ukiwa na tabasam kwa kuyafahamu matokeo yake mapema.

Siku na miezi ilisogea mbele, Seid na mama yake waliendelea kuishi maisha ambayo Mungu ndo alieyajua, walipopata walikula walipokosa walilala, kutokana na nyumba yao kuwa peke yake hakuna alieweza kujua maisha yao yakoje, ilikuwa ni siri yao na Mungu wao pekee...
Miezi sita mbele ilikatika, Tarehe 15 siku ambayo ilikuwa ndo siku ya kutoka matokeo ya form six ilifika. seid hakuwa na nauli ya kwenda mjini siku hiyo ilibidi ampigie rafiki yake anaetumia vifaa vya internet na kumuomba aangalie necta ya form six lakini ilishindikana hakuwa na megabite za kuingilia internet siku hiyo, ikabidi afanye juu chini aende mjini akiwa na furaha ya hali ya juu akiamini moja kwa moja yeye mshindi.

Baada ya kufika alienda hadi sehemu yalipokuwepo makaratasi ya matokeo, alifika huku akiwambia wenzake aliowakuta
" Kabla sijaangalia matokeo yangu nimeota kuwa nimeshinda.

Kimya kimya alifika na kuangalia namba yake kwa kutumia kidole. Ghafla Macho yalimtoka baada ya kuiona, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio akawa katika hali ya siamini, baadhi ya wenzake walimuuliza.
"Bosi vipi mbona kimya!
lilikuwa swali zito sana kwake kulijibu, machozi yalimtiririka kama baadhi ya wanafunzi ambao walikuta matokeo ya siamini wakashindwa kujizuia na kuangua kilio.

Hakuweza kuamini alichokiona Seid, maswali mengi yaliingia kichwani mwake, akawa na msongo wa mawazo, alihisi presha kupanda na kushuka ghafla, taratibu alianza kuanguka chini na kupoteza fahamu, wenzake waliokuwa karibu walimdaka wakampeleka chini pole pole akiwemo kijana mmoja aliekuwa swahiba wake wa karibu aitwae Hamad...

ITAENDELEA SEHEMU YA 07 KESHO SAA SITA KAMILI MCHANA..

wasiliana na mtunzi wa story kupitia ukurasa wa whatsapp: 0774320110
 
Itaendelea kesho saa sita mchana..
 
Riwaya: FORGIVENESS OF MAMA!
Mwandishi: SEID BIN SALIM.

Mwanzo
Kumbu kumbu.....

"Mama!, Kila siku nakuuliza kuhusu baba yangu yuko wapi hunijibu na kunambia utanambia utanambia utanambia, nna miaka tisa sasa hivi simjui baba yangu. kwa nini lakini mama!, kuna kitu gani hasa kikubwa kinakufanya usinambie ukweli kuhusu baba, naomba uniambie tafadhali mama. nakuomba usinifiche, shule tunasoma kila siku mficha maradhi kifo umuumbua, na bora aibu kuliko fedheha, au unahisi mimi nakuwa katika hali nzuri nnapowaona marafiki zangu wapo na wazazi wao wote wawili?.

Hiyo ilikuwa kumbu kumbu ya maneno nliyoyakumbuka kipindi nimelala chali katika kitanda ambacho huwa analala mama yangu na mimi kulala chini kutokana na hali duni ya maisha tuliyonayo.
swali hilo lilinifanya nikumbuke mengi sana yaliyotokea nyuma kipindi nna miaka tisa, nkamkumbuka sana mama yangu ambae wakati huo alikuwa ameenda kumtembelea bibi shamba.

Swali nlilomuuliza mama miaka 11 nyuma usiku mmoja wa saa mbili tuliokuwa tumekaa chini chumbani baada ya kumaliza shuguli zote za hapa na pale, lilimfanya mamaangu kipenzi aanze kuonesha dalili ya machozi machoni mwake. alitingisha kichwa. nlipomuangalia nkajua anaashiria kunisikitikia sana. aliinuka chini tulipokuwa tumekaa akashusha pazia ambayo huwa tunaitenganisha kati kwa kati chumbani, akapita upande wa pili ambao kulikuwa na kitanda chake, alilala huku machozi yakianza kumlenga akifikiria swali nlilomuuliza.

Nlimuita mara kadhaa lakini hakuitika, nkajua nimemkosea sana mama angu nkamuambia anisamehe kama nimemkosea, kwani sikuitaji hata siku moja akose furaha kwa ajili yangu.
nliinuka kwenye kigoda nlichokuwa nimekaa na kuingia kwenye neti iliyokuwa imeegeshwa kwenye mkeka nliokuwa naulalia chini siku zote nkalala.

nlikuwa mtoto lakini akili zangu zilikuwa za kiutu uzima, nlizima kibatali na kulala huku nkiwa na mawazo ya kuhisi kumkosea mama yangu kwa kumuuliza kuhusu baba japo ni wajabu wangu kuuliza swali hilo kwake, kwa sababu sikuwai kumuona tokea kuzaliwa kwangu. Tokea nlipojitambua naangaza macho na kumuona mama akiangaika peke yake juu yangu bila kujua baba yuko wapi. Kitu kilichokuwa kinanipa wakati mgumu hata nlipokuwa shule..

Wakati tayari nimelala na kuweka neti vizuri nkiichomeka chini ya mkeka. kwa mbali nlisikia kilio cha chini kwa chini nkageuza uso wangu ili kusikiliza vizuri kilio kinatokea wapi, bado sikufanikiwa licha ya kugeuza uso ikabidi niinue shingo yangu nkitega masikio yote mawili. ndo nligundua anaelia chini kwa chini ni mama yangu. Nlitamani nifunue pazia nimfate na kumuuliza kitu gani kinamliza au ni kwa sababu ya swali langu nlilomuuliza, lakini nkashindwa kwa sababu sikujua yuko katika hali gani, nliofia kufunua pazia nkiogopa kumkuta yuko uchi au katika mavazi ya kuonesha maungo yake.

Ilinibidi Nimuite na nlimuita zaidi ya mara tatu bila kuitika, hasira zilinishika nkageuka upande wa pili nkajikunja huku nkivuta shuka langu la kujifunika, nkajifunika na kuweka vidole masikion ili nsisikie kilio cha mama yangu kipenzi ambae nlimfanya wa pili kwa umuhimu baada ya Mungu alie juu.

namshukuru Mungu kutokana na uchovu nliokuwa nao wa shule pamoja shambani hazikupita dk tatu nlipitiwa na usingizi ulionipeleka mpaka saa kumi na mbili na dk 5 asubuhi nkaamka na kujiandaa kwa ajili ya kuwahi namba shuleni. Nlinawa uso nkavaa nguo na kupaka mafuta mgando ambayo nlikuwa nahakikisha yamerundikana usoni.
Nlipomaliza kuvaa kila kitu nlichukua mkoba wangu uliokuwa tayari umechanika chanika baadhi ya sehemu nkauweka mkono upande kisha nkamuita mama ili anipe chochote kitu kama kipo cha kutumia shuleni.

"Mama naenda shule. nlimuambia mama baada ya kumuita na kuitika, ikiwa kama style ya kumsikilizia atasemaje kama mzazi.

"Ok mwanangu nakutakia masomo mema, kuna shiling mia hapo juu ya mfuniko wa ndoo, ichukue ikifika saa nne utanunua hata bagia ule saa nane ukirudi utakuta chakula tayari. Hali yetu ni masikini mwanangu usije kuona wivu kwa kuwaona wenzio huko shule wanakula vitu vya bei, ni kwa sababu wazee wao wana pesa.

Hayo ndo yalikuwa maneno ya mama akiongea kwa hali ya usingizi.

nliitikia "Haya" nkaangalia juu ya mfuniko na kukuta shiling mia tu, nliichukua na kuiweka mfukon nkamuaga mama mara ya mwisho, nlifungua na kufunga mlango nkatembea haraka haraka kuwahi Namba na kwaride la shule lililokuwa linaanza saa moja na nusu.

" Ah mtoto wa mama huyooooooo!!!

Kama kawaida ya tabia ya watoto wa shule ilivyo, kipindi natembea nlikutana na kundi la wanafunzi waliokuwa wanasoma darasa la nne wakati mi niko la tatu.
ilikuwa si mara yao ya kwanza kunambia maneno hayo kila waliponiona, ni maneno ambayo nlishayazoea kutoka kwao kutokana kuniona kila siku nkiishi na mama yangu bila baba, kibaya zaid nkilala nae chumba kimoja kila siku.

Ni maneno ambayo yalikuwa yakinikera sana kiukweli moyoni japo nlikuwa mtoto, na hasira zote nlizokuwa natoka nazo hapo zilikuwa zikiishia kwa mama kumuuliza swali lililokuwa ni gumu sana kulijibu siku zote nlizokuwa nkimuuliza.

Waliendelea kuniteta kwa kusema maneno yaliyokuwa yakizidi kuniumiza moyoni mwangu kwakweli.

"Mtoto wa mama mbona hutujibu wewe?. " Muacheni bhana amezoea kudeka kwa mama yake huyoo......

Ila sikujali maneno yao kwa sababu nlishayazoea na huwa yanantia hasira sana, na tayari nlikuwa nawahi shuleni sikuitaji hata siku moja kupata adhabu toka kwa walimu au viranja kwa sababu ya kuchelewa mstarini au kwa ajili ya utovu wa nidhamu.

Nlifanikiwa kuwahi mstarini nyimbo ya taifa ilianza kuimbwa, baadae tukaesabu namba na kuingia darasani. Upo muda ambao nlipokuwa darasan nliishia kushika tama kutokana na mawazo mazito ya kuitaji kujua aliko baba yangu, na kujiuliza kwa nini mama nkimuuliza swali kuhusu baba huwa anakasirika, na bora angekuwa anakasirika alafu ananijibu lakini huchukua maamuzi ya kutoka sehemu tunayokuwa tumekaa kabisa machozi yakiwa nje nje...

Saa nane ilipofika nliwahi nyumbani haraka kutokana na njaa iliyokuwa imenikamata, Namshukuru Mungu siku hiyo nlikuta viazi vinne kwenye sufuria baada ya kufika. kwani siku nyingine huwa sikuti kitu kabisa. Nlinawa na kuanza kula pembeni nkiwa na kombe la maji, nlipomaliza nliingia shambani kumuangalia mama.

nlifanikiwa kumuona akiwa anapariria viazi vitamu vilivyokuwa vimezungukwa na magugu, nlitingisha kichwa kwa kumuonea huruma mama, Jua la saa nane lote lilikuwa likimuingia mwilini. nlimfata na kumuamkia

"Mama shkamoo

Aligeuka akaniangalia huku akiitikia shikamoo yangu.
"Maraabaa mwanangu umerudi baba.
"ndio mama nimerudi.
"mmesoma shule.
"ndio tumesoma kiswaili na haiba ya michezo.
"Ok mwanangu umepata vizuri?.
" ndio nimepata mamaa
"aya mwanangu soma uje unisaidie mama yako si unaona nnavyoangaika hapa.

Sikumjibu swali hilo pembeni kulikuwa na dumu la maji pamoja na kikombe, nliyafata nkamimina na kunywa, nlipomaliza aliniuliza.

"Ushakula?

"ndio nimekula. Nlimjibu huku nkimezea maji ya mwisho.
"aya itabidi ujiandae sasa uje hapa unisaidie.

Nlijisikia vibaya baada ya kunambia hivyo, nlijikuta namuambia nkiwa natamani kulia

"Bhana mamaa!!,Ah, nimechoka mimi!

"Mwanangu najua umechoka Ila chakula chetu ndo hiki hiki tutafanyaje?, hata mimi nimechoka lakini najikaza mwanangu.

"Dah! Sawa.
nlitoka pale nkiwa nimevimbisha uso wangu, nliingia ndani na kubadilisha nguo nkarudi shambani kwa ajili ya kumsaidia mama.

Jua la mchana lote lilituishia mwilini, mpaka saa kumi na mbili ndo tulitoka shambani tukiwa na viazi vitano kwa ajili ya kupika usiku.

Nlipofika nje ya nyumba nlitua mzigo mdogo wa kuni nliokuwa nao begani, nkachukua vidumu viwili vya maji kwa ajili ya kwenda kuchukua maji kisimani...

Uchovu mkubwa nlikuwa nao wakati huo ila nlijua kuchota maji ni wajibu wangu, na ndani kulikuwa hakuna maji hata kidogo na mama anatakiwa kuoga. Ilinilazimu kwakweli nsingekubali kumuona mama anabebana na vidumu kwenda kuchota maji wakati mimi nipo. hata niwe nimechokaje. Nlipofika bombani nlishangaa kuwaona watoto ambao nao wana kawaida ya kunitania. nlitamani kurudi nyuma lakini tayari walishaniona, nlisogea hadi kisimani nkiwa nimekunja uso wangu, walinangalia bila kunimaliza mi nkiwa nimeshikilia kifaa cha kuingiza kisimani kuteka maji na kuingiza kwenye vidumu nlivyokuwa navyo.
ukimya ulitanda muda nliofika na kuanza kuteka maji, nlijaza vidumu vyangu vyote viwili, vilipojaa nkabeba kwa ajili ya kuondoka.

"Hahahaaaaaa Mtoto wa mama huyooo lione Sura nyeusi kama usiku. Alisema mtoto mmoja kati yao alieitwa mudy nlipokuwa tayari nimewapa mgongo, ni kama walikuwa wananiteta mioyoni mwao..
" Muacheni huyo amezoea kunyonya maziwa ya mama, jitu zima bado linalala na mama yake iloooooooo lione.
" Kwani hana baba yule? Aliuliza mmoja.
"mamaake alikuwa malaya huyo anatembea na wanaume tofauti akapigwa mimba ndo akapatikana huyu mjinga, muone vile.

Ni maneno ambayo yaliniuma sana walipoyaongea baada ya kuwapa mgongo, nliweka vidumu chini mbele yangu nkayaona mawe matatu, nliyaokota na kuwarushia moja baada ya lengine kwa hasira nlizokuwa nazo, Moja ya watoto hao waliokuwa watano jiwe lilimpata na kumjeruhi vikali karibu na jicho lake la kulia, wote waliingiwa na mshangao wa "Haaaaa" huku huyo aliejeruiliwa akiinama chini na kuanza kulia.

Nlipoona hivyo nlikimbia na kuviacha vidumu, walimuacha mwenzao wakanifukuza lakini hawakunipata kutokana na uwepesi wa mwili wangu nliokuwa nao pamoja na mbio.
Nlifika nyumbani na kuingia ndani moja kwa moja, mama alikuwa jikoni akashangaa kuona natoka huko nkiwa mbio.
waliokuwa wananifukuza walifika na kumwambia mama anitoe ndani huku wakiwa wanahema.

"Mama Seid mtoe mwanao ndani haraka na sisi tumfanyie kile alichomfanyia mwenzetu.
"Kuna nini kwani jamani nyie watoto?. mama aliuliza kwa mshangao.

"Unajifanya hujui?, mwanao si ndo unavyomfundisha hivyo awapige watu mawe.
"Mnasemaje nyie watoto!!, (mama aliongea akionekana kuchukia kwa alichoambiwa) yani hamna adabu kiasi hicho kumbe e.
"Adabu tayari tulishawapatia wazazi wetu tukupe adabu wee nani kwani? mtoe mwanao ndani tumpige jiwe kama alivyomfanyia mwenzetu.

Watoto waliongea kijeuri, ni kama walikuwa wanamfokea mama yangu wakati hawampati hata kwa robo kiumri.
nliumia sana kusikia wanavyomjibu mama, nkatoka ndani na panga kwa hasira, waliponiona walikimbia na mimi nkawafata kwa nyuma, sikuweza kuwapata lakini kama ningewapata nadhani ningeua kutokana na kile ambacho tayari kilikuwa moyoni.

Nlirudi na kuliweka panga chini huku nkiwa nimevimbisha mdomo, Mama alishika kiuno na kuachia mguno wa "hhhmmm" akishusha pumzi zake.

"Seid umeanza utundu na wewe wa kupigana na wenzio si ndio.
nlishindwa kujibu swali lake, akaniuliza tena akionekana kukasirika na kile nlichokifanya.

"Mama kila siku nakuuliza kuhusu baba hunijibu, kila nkikuuliza hunijibu, kila nkikuuliza hutaki kunijibu kwa nini lakini mama?, mimi sio mtoto kama unavyofikiria, sawa mimi ni mdogo nna miaka tisa tu lakini nna akili za kufikiria mbali, pia nna wajibu wa kuwaona wazazi wangu wote wawili, baba yuko wapi?, Nambie ukweli mama, kama alishafariki sema? haiwezeani mi naenda bombani naambiwa mama yangu ulikuwa Ma, ma (nlishindwa kuongea hilo neno malaya, japo tayari nlishakasirika lakini ufahamu wa kujua alioko mbele yangu ni mama yangu mzazi uliniingia),
kiukweli nliongea kwa hasira sana mama akiwa amesimama na kunangalia, alinambia nimalizie kile nlichokikatisha ndo nkamwambia "naambiwa kuwa ulikuwa unawabadilisha wanaume kila siku ndo maana umenipata mimi na ulipata ujauzito bila kutegemea ndo maana hujui baba yangu aliko, japo siamini hayo maneno kwa sababu wale walionambia ni wadogo hawakuwepo wakati huo lakini baba yangu yuko wapi? nijibu mama usiishie kulia tu kila nkikuuliza..
Machozi yalishaanza kunitoka, mama nae tayari alikuwa anabubujikwa na machozi kwa nilichomuambia.

ITAENDELEA KESHO SAA SITA MCHANA.
 
Itaendelea Sehemu Ya pili kesho saa sita mchana
 
Back
Top Bottom