RIWAYA: Mifupa 206

4

ANGALAU NIMEPUNGUZA HISIA ZANGU” Koplo Tsega alijisemea
moyoni baada ya mjadala mkubwa kumalizika nafsini mwake. Matukio ya jana
usiku yalikuwa yamemuacha hoi kwa uchovu baada ya kugaragazwa na kupindwa
katika kila namna ya mkao na mwanaume shababi mfanyakazi wa hoteli ile aliyelala
naye usiku kucha.
Tangu aliposalitiwa na mpenzi wake Koplo Tsega alikuwa ameapa kutojihusisha
tena na mapenzi katika maisha yake lakini hilo lilikuwa gumu kutekelezeka. Hisia
zikakataa kabisa kukubaliana na akili yake hivyo mapenzi akayageuza na kuyafanya
kama starehe nyingine ambapo angeyatafuta na kuyafanya na mwanaume yeyote yule
ambaye angekuwa na vigezo vyake na baada ya hapo kila mtu angeshika hamsini zake.
Usiku wa jana aliporudi kwenye hoteli ile aliyofikia iliyopo nyuma ya stendi kuu ya
mabasi yaendayo kasi eneo la Ubungo Koplo Tsega aliingia kwenye eneo la mgahawa
wa hoteli na kujipatia mlo wa nguvu kisha akashushia na kinywaji baridi huku akili
yake ikitafakari matukio yaliyopita.
Akiwa kwenye mgahawa ule akajikuta akikumbuka zile kukurukakara zilizotokea
kule nyumbani kwa Guzibert Kojo huku akijaribu kuwaza ni kwa namna gani polisi
na vyombo vya habari vitakavyolichukulia tukio lile. Akiwa katikati ya tafakari ile mara
akajikuta akimkumbuka yule mtu aliyekuwa akimfuatilia usiku wa jana tangu alipotoka
kule Vampire Casino huku akijiuliza kuwa mtu yule alikuwa nani na alikuwa akihitaji
nini kutoka kwake.
Halafu mawazo yake yakatoweshwa na taswira ya kijana mzuri handsome mhudumu
wa hotelini pale. Kijana mrefu na mweusi mwenye sura nzuri,kifua kipana kiasi chenye
misuli imara na macho ya huruma huku akiwa katika sare zake za kazi akiwahudumia
wateja.
Kijana yule alipokuwa akiinama ili aondoe vyombo na kusafisha meza aliyoketi Koplo Tsega. Koplo Tsega akabahatika kukiona kifua imara cha kijana yule
kilichohifadhiwa vyema ndani ya singlet yake nyeupe. Kukiona kifua cha kijana yule
hisia za mapenzi zikaanza kuitongoza nafsi yake na kujikuta akianza kumtamani
huku manukato yenye harufu nzuri ya kijana yule yakiziteka kabisa hisia zake. Kiu ya
mapenzi ikiwa imemnasa vilivyo Koplo Tsega akaamua kuvunja ukimya.
“Pole na kazi” Koplo Tsega akamwongelesha yule kijana wakati alipokuwa
akimalizia kufuta ile meza.
“Ahsante! dada yangu” kijana yule akaitikia kwa bashasha zote za kirafiki huku
akifikiria Tip ya mteja.
“Hivi wifi yangu akikuona unafanya kazi hizi si atakasirika?” Koplo Tsega
akachombeza utani.
“Ah! wapi mwanamke gani wa nyakati hizi utakayempata kwa mshahara wa
hotelini” yule kijana akaangua kicheko hafifu huku akiendelea kufuta ile meza aliyoketi
Koplo Tsega kwenye mgahawa ule.
“Kwa hiyo hujaoa wewe?” Koplo Tsega akauliza kwa sauti ya kubembeleza.
“Hao wasichana wenyewe wa kuoa wako wapi dada yangu. Sasa hivi kila msichana
unayemgusa hapa mjini anataka maisha mazuri utasema sisi wanaume hatuyataki hayo
maisha mazuri” yule kijana akaongea huku akionekana kufurahishwa na maongezi
yale. Ukimya kidogo ukapita kisha Koplo Tsega akavunja ukimya akimuuliza yule
kijana
“Unaitwa nani?”
“Mimi?” yule kijana akauliza kwa haya huku akijua fika kuwa ni yeye ndiye
aliyekuwa akiongeleshwa halafu walipotazamana akaachia tabasamu maridhawa
lililozidi kumchanganya vibaya Koplo Tsega.
“Naitwa Sikawa”
“Mh! jina lako tamu kama asali” Koplo Tsega akaongea huku akijitahidi kuilegeza
sauti yake ya kiafande.
“Acha utani dada yangu tangu lini jina la mtu likawa tamu kama asali” Sikawa
akaongea huku akiangua kicheko chake hafifu lakini kilichopeleka ujumbe kwa Koplo
Tsega kuwa yupo tayari kwa hatua inayofuata.
“Au hupendi nikusifie kuwa wewe ni mzuri?”
“Mh! hata sijui nisemeje dada yangu” Sikawa akaongea katika mazingira ya
kuruhusu urafiki kisha kitambo kifupi cha ukimya kikapita kabla ya Koplo Tsega
kuvunja tena ukimya.
“Utatoka kazini saa ngapi?”
“Saa nne usiku baada ya mwenzangu anayenipokea zamu kufika” Sikawa akaongea
kwa utulivu.
“Unaishi wapi hapa Dar es Salaam?”
“Nimepanga chumba mtaa wa mama Ngoma eneo la Mwenge” Sikawa akaongea
kwa utulivu huku akishindwa kuelewa muelekeo wa maongezi yale.
“Unaishi na nani?” Koplo Tsega akazidi kumdadisi Sikawa.
“Naishi peke yangu” Sikawa akaongea kwa utulivu huku akiutathmini uzuri wa
Koplo Tsega mbele yake.
“Usijali siku moja utampata mwenza wako. Mimi nipo chumba namba 18
ghorofa ya pili. Utakapotoka kazini kama hutojali unaweza kuja chumbani kwangu
tukabadilishana mawazo” Koplo Tsega akaongea kwa sauti ya kubembeleza kiasi cha
kuzivuruga hisia za Sikawa na kumfanya atabasamu.
“Sawa nitajitahidi” hatimaye Sikawa akaukubali mwaliko wa Koplo Tsega huku
akimaliza kufanya usafi juu ya ile meza na kuondoa vyombo kisha akaondoka na
kuelekea dirisha la jikoni.
Koplo Tsega akamsindikiza Sikawa kwa macho hadi pale alipotoweka mbele
yake huku wazimu wa mapenzi ukizitaabisha vibaya hisia zake. Kisha akasimama na
kuanza kuzitupa hatua zake za shibe kivivuvivu kuelekea chumbani kwake ghorofa
ya pili ya hoteli ile.
Tangu tukio la kifo cha Guzbert Kojo,Koplo Tsega alikuwa ameamua kutojitokeza
mitaani kwa muda wa siku mbili au zaidi huku akisubiri mambo yatulie kwanza.
_____
SAA TATU NA NUSU USIKU ILIPOTIMIA Koplo Tsega aliamka kutoka
kitandani alipokuwa amelala kwa muda wa masaa kadhaa akiupunguza uchovu.
Mawazo yake yalipotulia akamkumbuka Sikawa na hapo akageuka kuitazama saa
iliyokuwa imetundikwa ukutani mle chumbani. Muda mfupi baadaye alitarajia kuusikia
mlango wa chumba chake ukigongwa na Sikawa kuingia mle ndani. Hivyo akaamka
na kutandika kitanda chake vizuri kisha akawasha runinga iliyokuwa mle chumbani
juu ya meza fupi iliyokuwa kwenye kona na kuweka stesheni yenye muziki laini wa
kubembeleza.
Alipomaliza akapiga simu eneo la mapokezi na kuagizia mzinga mmoja wa
kinywaji kikali ambao wangeutumia kwa pamoja kusindikiza maongezi yao. Mzinga
huo wa pombe kali ulipoletwa na mmoja wa wahudumu wa hoteli ile Koplo Tsega
akaupokea na kuuweka juu ya meza fupi ya kioo iliyokuwa pembeni ya kochi moja la
sofa lililokuwa mle ndani pamoja na bilauri mbili kisha akaelekea bafuni kuoga.
Sikawa alikuwa ni kijana aliyekuwa akipapatikiwa sana na wanawake kutokana na
sura nzuri aliyokuwa nayo,umbo lake refu lenye kifua kipana kiasi,utanashati na tabia
yake ya ucheshi. Kwa vigezo hivyo wasichana warembo walimpenda na ama kwa
hakika alijua kucheza vizuri na hisia zao. Hivyo kwa haraka sana alikuwa ameitambua
shida ya Koplo Tsega na kwa kweli hakutaka bahati ile impite hivi hivi.
Uzuri wa Koplo Tsega ulikuwa umezikoroga vibaya hisia zake za mapenzi kiasi
kwamba kila wakati alijihisi ni kama alikuwa akimuona Koplo Tsega mbele yake. Kwa
tathmini yake ni kuwa wasichana wazuri na warembo wa sampuli ya Koplo Tsega
walikuwa wachache sana jijini Dar es Salaam na wengi wao walikuwa wakiwapenda
wanaume wenye pesa. Hivyo Sikawa akajiona ni kijana mwenye bahati sana kwa
kualikwa chumbani kwa Koplo Tsega. Akaendelea kufanya kazi zake kwa furaha huku mara kwa mara akipiga mruzi mwepesi mdomoni bila wafanyakazi wenzake
kufahamu kitu kilichokuwa kikiendelea wakati huo akiomba masaa yasogee mbele.
Ilipofika saa nne usiku Sikawa alikuwa nje ya mlango wa chumba namba 18 cha
hoteli ile ghorofa ya pili akigonga mlango.
“Karibu” sauti myepesi ya Koplo Tsega kutoka ndani ya chumba kile ikamfanya
Sikawa ajitengeneze vizuri. Wakati huu alikuwa amevaa nguo zake za uraiani;fulana
nyeupe,suruali nyeusi ya jeans na raba nyepesi miguuni.
Mlango wa chumba ulipofunguliwa Sikawa akajikuta akitazamana na macho laini
ya Koplo Tsega akiwa amejifunga kanga laini kifuani iliyolishika vema umbo lake
katika baadhi ya maeneo kutokana na ubichi wa mwili wake kwani ndiyo alikuwa
anatoka kuoga.
“Karibu ndani Sikawa,utanisamehe kidogo kwani ndiyo nilikuwa natoka kuoga”
Koplo Tsega akaongea kwa sauti laini ya kubembeleza huku tabasamu lake maridhawa
likielea usoni mwake.
“Oh! samahani kwa usumbufu bila shaka nimewahi sana” Sikawa akajibaraguza
huku akiingia mle ndani na wakati akifanya hivyo harufu nzuri ya sabuni ya kuogea ya
Koplo Tsega ikapenya puani mwake na kuamsha hisia mpya za mapenzi.
“Wala usijali kwani ungechelewa zaidi ya hapa ningekulaumu Sikawa” Koplo
Tsega akaongea huku akiangua kicheko hafifu na kuufunga ule mlango wa chumba.
“Ndiyo maana sikutaka kuchelewa” Sikawa akaangua kicheko chepesi cha
kistaarabu huku akielekea kuketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa mle ndani.
Koplo Tsega akiwa unaufahamu vizuri udhaifu wa wanaume mara baada ya kuufunga
mlango wa kile chumba akatembea taratibu kukizunguka kitanda cha mle ndani na
hatimaye kuketi kihasara kwenye pembe ya kile kitanda huku akiwa na hakika kuwa
macho ya Sikawa yalikuwa yakimsindikiza nyuma yake. Kisha akageuka ghafla na
kukutana na macho ya Sikawa yakimtazama. Sikawa kuona vile akashikwa na haya
huku akiyakwepesha macho yake haraka kutazama muziki uliokuwa ukirushwa
kwenye ile runinga ya mle chumbani ujasiri ukiwa umeanza kupungua.
Koplo Tsega alikuwa fundi mzuri wa kuanzisha maongezi hivyo akajikuta
akianzisha mada moja na kurukia nyingine huku macho yake mara kwa mara yakitua
juu ya kifua cha Sikawa. Sikawa naye hakuwa nyuma alimpatiliza vizuri Koplo Tsega
na pale alipohisi kuwa alikuwa mbioni kuishiwa hoja akazuga kwa kuinyanyua bilauri
ya kinywaji na kugida mafunda kadhaa huku macho yake mara kwa mara yakiutazama
mlima wa matiti ya wastani yaliyokuwa kifuani mwa Koplo Tsega.
Maongezi yao hayakuwa na hoja za maana lakini yaliendelea na kila mara Sikawa
alipojaribu kumdadisi Koplo Tsega kiundani zaidi alijikuta akiambulia patupu kama
siyo kudanganywa. Maongezi yalipoonekana kufifia muziki uliokuwa ukirushwa na
runinga ya mle chumbani ukarudisha uhai wa mandhari yale.
Hatimaye mshale wa saa ya ukutani mle chumbani ukasoma saa nane na robo usiku
na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha nje ikatengeneza kizingiti kingine kwa Sikawa
huku Koplo Tsega akionekana kufurahishwa na hali ile. Kile kilevi walichokuwa wakikitumia kikaanza taratibu kuwaondoa nishai kadiri muda ulivyokuwa ukisogea
mbele.
Hatimaye uvumilivu ukaondoka na kuwapelekea washindwe kuzidhibiti vyema
hisia zao. Sikawa akahamia pale kitandani huku akijidai anataka kuugemeza mgongo
wake baada ya kuchoka kukaa muda mrefu kwenye lile kochi la sofa mle chumbani.
Koplo Tsega naye akajifungua kanga yake kwa hila na kugeukia upande wa pili wa
kitanda huku akimpa mgongo Sikawa.
Nadharia ya somo la fizikia ya unlike charges attract each other hatimaye ikachukua
nafasi yake huku kila mmoja akiacha kuigiza. Muda mfupi uliyofuata shughuli ikaanza
pale kitandani kila mmoja akijitahidi kuonesha ufundi wa mapenzi kwa mwenzake.
Sikawa alikuwa fundi mzuri wa mapenzi aliyejua vizuri kumridhisha mwanamke
mwenye kiu ya mapenzi. Alimgeuza Koplo Tsega upande ule kisha akamkunja upande
huu halafu akamuinua hapa na kumkandamiza pale huku ndimi zao zikitekenyana
mdomoni na kutengeneza kiwango cha mwisho cha hisia za mapenzi kwenye miili
yao.
Mara ya kwanza,mara ya pili,mara ya tatu na walipofika mara ya nne walikuwa hoi
taaban hawajitambui kwa uchovu. Usingizi ukaja na kuwachukua huku kila mmoja
akiwa amelala kwa namna yake. Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha jijini Dar
es Salaam.
_____
Koplo Tsega ALIKUWA wa kwanza kuamka kutoka usingizini. Kitendo
cha kuuona mkono wa kiume juu ya titi lake kifuani kukamfanya amkumbuke
Sikawa,mhudumu wa hoteli ile aliyelala naye jana usiku.
Sikawa alikuwa hajitambui kwa uchovu na alikuwa akiachia sauti ya mkoromo
hafifu kinywani mwake huku miguu na mikono yake ameisambaza ovyo pale
kitandani.
Koplo Tsega akageuka na kumtazama Sikawa kwa makini pale kitandani huku
nafsi yake ikimsuta kwa kitendo cha kujirahisisha na hatimaye kugawa penzi lake
kwa kijana yule mhudumu wa hoteli. Hata hivyo kwa upande mwingine hakutaka
kujilaumu sana. Penzi zito la Sikawa lilikuwa limefanikiwa kukata kiu yake ya mapenzi
ya muda mrefu tangu alipoachana na mpenzi wake mara ya mwisho.
Koplo Tsega aliendelea kumtazama Sikawa pale kitandani huku uso wake
ukiumba tabasamu laini la shukrani. Mikiki mikiki ya usiku pale kitandani ilikuwa
imemuacha na uchovu wa aina yake. Kila kiungo cha mwilini alipojaribu kukisogeza
kilikuwa kikilalamika. Sikawa alikuwa ameitosheleza vizuri haja yake katika kila eneo
la mapenzi. Hata hivyo hisia mpya zilipomjia juu ya sababu iliyomrudisha jijini Dar
es Salaam zikamfanya aanze kuyapuuza matukio yote waliyoyafanya usiku yeye na
Sikawa.
Koplo Tsega akatupa shuka pembeni na kushuka kitandani. Kioo kikubwa
cha kabati lililokuwa mle ndani ukutani kikamfanya asimame kidogo na kuanzakujitathmini.
Macho yake makubwa bado yalikuwa legevu kwa uchovu,matiti yake madogo ya
wastani yalisimama wima kifuani pamoja na misukosuko ya Sikawa iliyoyapitia wakati
wa usiku. Kiuno chake chembamba kilichofuatiwa na mzigo wa wastani wa makalio
yake imara yaliyoshikiliwa na mihimili thabiti ya misuli ya mapaja yake yaliyonona
vikamfanya ajizungushe mbele ya kioo cha lile kabati huku akijitazama.
Matokeo ya tathmini yake kupitia taswira iliyojengeka kwenye kioo kile cha kabati
yakampelekea Koplo Tsega ajiridhishe kuwa bado alikuwa kwenye soko la uzuri kama
walivyokuwa wasichana wengine wa mijini.
Hatimaye Koplo Tsega akavinyoosha viungo vyake mwilini kwa mazoezi mepesi
kisha akaelekea maliwatoni huko ambako alimaliza haja zake zote pamoja na kuoga.
Koplo Tsega aliporudi kutoka maliwatoni akavaa bukta yake nyepesi na blauzi
yake mchinjo kisha akaelekea pale kitandani na kumwamsha Sikawa.
Sikawa alishtuka kutoka usingizini huku akiwa mwingi wa uchovu. Haraka
akayapeleka macho yake kuitazama saa ya ukutani iliyokuwa mle chumbani. Ilikuwa
ikielekea kutimia saa mbili asubuhi lakini alipokumbuka kuwa alikuwa na zamu
ya usiku ya kuingia kazini hakujipa haraka na badala yake akageuka pembeni yake
na kumtazama Koplo Tsega kwa macho yenye haya kidogo lakini yasiyojali kitu
chochote huku akitabasamu. Sikawa alitamani sana kuwa wangeendelea kulala mle
chumbani na kuendeleza starehe hata hivyo macho ya Koplo Tsega yalimuonya kuwa
hilo lisingewezekana tena kwa wakati ule.
“Umeamka saa ngapi?” Sikawa akavunja ukimya huku akitabasamu.
“Muda siyo mrefu”
“Mh! usingizi wa leo ulikuwa mzito kama wa Pono!” Sikawa akaongea huku
akivinyoosha viungo vyake mwilini na kuzipa uhai fikra zake pale kitandani.
“Mimi ndiyo hata sikumbuki kuwa ni wakati gani nilipitiwa na usingizi mpenzi”
Koplo Tsega akaongea kwa sauti nyepesi kisha walipotazamana usoni kila mmoja
akatabasamu kabla ya Koplo Tsega kuvunja ukimya.
“Amka ukaoge kumeshapambazuka”
“Asubuhi yote hii kwani tunakimbilia wapi?” Sikawa akauliza kichovuchovu.
“Huingii kazini leo?” Koplo Tsega akamuuliza Sikawa akiutazama mchoro wa
umbo la Sikawa ndani ya lile shuka la kitandani.
“Leo nina zamu ya usiku” Sikawa akajitetea.
“Hata hivyo kumeshapambazuka”
“Lakini mimi sina haraka!”
“Mimi nina haraka” Koplo Tsega akaongea kwa msisitizo huku hisia za mapenzi
zikiwa mbali naye.
“Sasa nani kakuzuia?’’ Sikawa akaongea kwa jazba akichukia kushurutishwa.
“Umeshasahau kuwa hapa siyo kwako!” Koplo Tsega akafoka.
“Lakini si ni wewe mwenyewe ndiye uliyeniita humu ndani?” Sikawa akauliza kwa
mshangao.
“Ndiyo! lakini ilikuwa jana siyo leo”
“Kwa hiyo haja yako ilikuwa ni ngono tu?”
“Pigia mstari” Koplo Tsega akaongea kwa jazba huku akihisi kuanza kukereka.
“Sasa kwanini hukuniambia mapema ili nijue?”
“Hata kama ungejua kwani ungekataa?”
“Sikiliza wewe dada…” Sikawa akaanza kujitetea hata hivyo alikatishwa.
“Nashukuru sana kwa penzi lako lakini muda wa starehe umeisha. Inuka
ukajiandae uondoke” Koplo Tsega akaongea huku haraka akiliondoa shuka mwilini
kwa Sikawa na hapo Sikawa akabaki akimshangaa kwa hasira.
“Sasa kama hutaki wanaume ilikuwaje ukajitongozesha kwangu?” Sikawa
akaongea kwa jazba.
“Nilikujua kuwa wewe ni malaya mwenzangu” Koplo Tsega akaongea kwa
msisitizo.
“Malaya ni wewe au mimi?” Sikawa akauliza kwa mshangao
“Simama ujiandae uende mpenzi malumbano hayatakusaidia kitu” Koplo
Tsega akaongea katika namna ya kupuuza hoja za Sikawa kwani alikuwa ameanza
kuwachukia tena wanaume baada ya kumkumbuka Kiango. Kiango alikuwa mpenzi
wake wa muda mrefu na mwanaume aliyemkabidhi moyo wake wote lakini siku moja
akaambulia kumfumania bila kificho akiivuruga amri ya sita na rafiki yake wa karibu.
“Hivi wewe malaya una wazimu?” Sikawa akauliza kwa hasira lakini kabla
hajamalizia kuongea ngumi mbili za korodani pale kitandani zikamfanya atulie kwa
sekunde kadhaa huku ameachama mdomo wake kama anayeimba wimbo wa taifa.
“Tafadhali! usiniite malaya wewe mpuuzi” Koplo Tsega akamuonya Sikawa huku
Sikawa akiendelea kugugumia kwa maumivu makali pale kitandani. Sikawa alipotaka
kufurukuta akatulizwa pale kitandani kama mtoto mdogo huku akishindwa kuamini
ubabe na nguvu za ajabu za msichana yule mbele yake. Hatimaye Sikawa akaacha
upinzani hivyo akaamka pale kitandani na kuelekea maliwatoni ambapo alimaliza haja
zake na kuoga ndani ya muda mfupi.
Aliporudi mle chumbani akamkuta Koplo Tsega akiwa amerejewa na utulivu
na bashasha zote za kirafiki huku akishindwa kumuelewa vizuri mwenyeji wake.
Walipotazamana tena wote wakajikuta wakitabasamu.
“Nisamehe mpenzi wangu” Koplo Tsega akaongea kwa sauti ya kubembeleza na
yenye urafiki ndani yake.
“Usijali lakini umeniumiza sana!” Sikawa akaongea kivivuvivu huku donge la
hasira limemnasa kooni.
“Pole mpenzi lakini nilitaka uamke mapema” Koplo Tsega akajitetea huku
akizunguka na kumkumbatia Sikawa kwa nyuma na hapo wote wakaondoa tofauti
zao huku wakitabasamu.
“Unajisikiaje kwa sasa?” Koplo Tsega akamuuliza Sikawa huku akiupeleka mkono
kuzishika korodani zake. Sikawa akiwa ameshtukia hali ile akajitoa mikononi mwa
Koplo Tsega haraka huku akiangua kicheko cha kimahaba.
KEVIN e. MPONDA
“Please don’t touch them,they are still very hot” Sikawa akaongea kwa ujivuni huku
akianza kuvaa nguo zake na hapo wote wakacheka.
“Mwenge unakaa sehemu gani?” Koplo Tsega akavunja ukimya.
“Mtaa wa mama Ngoma nyumba namba 11” Sikawa akaongea huku akiendelea
kuvaa nguo zake.
“Nikija kukutembelea kuna shida yoyote?” Koplo Tsega akauliza huku akiumba
tabasamu usoni.
“Shaka ondoa mpenzi” Sikawa akaongea kwa furaha.
“Naomba namba yako ya simu”
Sikawa hakusita badala yake akaanza kuitaja namba yake ya simu taratibu katika
namna ya kuhakikisha kuwa Koplo Tsega anazinakili namba zile bila usumbufu.
“Mchana utakuwa na ratiba gani?” Sikawa akauliza
“Bado sijafahamu ila huwenda nikawa na mizunguko ya hapa na pale” Koplo
Tsega akaongea kwa utulivu huku akifikiria jambo.
“Basi tutawasiliana mpenzi” Sikawa akaongea baada ya kumaliza kujiandaa.
“Ondoa shaka ila usije humu ndani hadi tuwasiliane kwanza”
“Kama jana?”
Sikawa akachombeza utani huku akielekea sehemu ulipokuwa mlango wa
kile chumba. Alipofika akaufungua ule mlango na kabla hajatoka nje akageuka na
kumkonyeza Koplo Tsega kimahaba kisha akatoka nje ya kile chumba na kutokomea
zake.
_____
MUDA MFUPI BAADA YA SIKAWA kuondoka mle chumbani Koplo Tsega
akaichukua ile kamera yake kutoka kwenye begi lake lililokuwa chini ya uvungu wa
kile kitanda na kuanza kufanya mapitio makini ya zile picha alizopiga usiku wa jana
nje ya Vampire Casino.
Ile kamera aina ya Toymaster ilikuwa imenasa picha nne safi na zenye ubora
wa kuaminika. Katika zile picha nne zilizokuwa kwenye ile kamera picha mbili
zilimuonesha msichana mmoja aliyevaa gauni fupi akishuka kutoka kwenye gari refu
na jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van huku akiwa ameongozana na wapambe
wawili waliovaa suti nadhifu kuificha miili yao imara iliyojengeka vema.
Picha nyingine mbili zilizosalia zilimuonesha msichana yule akisalimiana na
mwanaume mwingine aliyevaa suti nadhifu huku wale wapambe wakiwa wamesimama
kando yake.
Koplo Tsega akaendelea kuzitazama zile picha moja baada ya nyingine kwa utulivu
huku akijaribu kurudisha kumbukumbu zake. Muda mfupi uliyofuata baridi nyepesi
ikaanza kuusimanga mtima wake pale alipogundua kuwa msichana yule kwenye zile
picha ndiye yule aliyemuona kwenye habari picha za magazeti fulani huko siku za
nyuma.
Koplo Tsega akaendelea kukumbuka namna picha zile za magazetini zilivyokuwa zikimuonesha msichana yule wakati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
J.K.Nyerere huku akiwa ameongozana na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa serikali
kuelekea nchi fulani ya ughaibuni katika safari ya kikazi ya kiongozi huyo.
Koplo Tsega akaendelea kukumbuka tena namna ambavyo habari za msichana
yule zilivyovuma huko siku za nyuma baada ya picha zake za ngono na mfanyabiashara
mmoja maarufu wa jijini Dar es Salaam kusambazwa mitandaoni kama rasimu ya
katiba mpya.
Koplo Tsega akajikuta akimkumbuka mwandishi wa habari aliyefahamika kwa
jina la Mtenzi Binagwa ambaye baadaye alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya
kusemekana kuwa ndiye yeye aliyehusika katika kuzipiga picha hizo na kuzieneza
mitandaoni.
Koplo Tsega akajikuta akizikumbuka picha hizo za utupu namna zilivyolitikisa jiji
la Dar es Salaam kwa muda wa wiki kadhaa na kupamba vichwa vya habari magazetini.
Kabla ya kwenda nchini D.R Congo Koplo Tsega akakumbuka kuwa yeye na
Sajenti Chacha Marwa walikuwa katika hatua za mwisho kabisa za kuonana na meneja
wa Vampire Casino baada ya kuhisi kuwa katika casino ile kulikuwa na mambo fulani
ya chinichini yaliyokuwa yakiendelea. Lakini walijikuta wakipigwa chenga na uongozi
wa casino ile mara kwa mara na walipokuwa wakijiandaa kutumia njia mbadala ndiyo
wakapokea wito wa kujumuishwa kwao kwenye mpango wa amani ya kudumu nchini
D.R Congo.
Akili yake ikiwa imezama kwenye tafakuri nzito Koplo Tsega akajikuta akipiga
mwayo mwepesi wa uchovu huku akiendelea kuzitumbulia macho zile picha za
kwenye ile kamera.
 
SASA NILIKUWA NA HAKIKA KUWA yule mtu aliyekufa kwa kuanguka
kutoka juu ya lile jengo la ghorofa la shirika la nyumba la taifa kule mtaa wa
Nkurumah,kuwa kifo chake kilikuwa na mahusiano ya namna fulani na yule
msichana niliyekuwa nikimfuatilia usiku wa jana kutoka kule Vampire Casino. Ingawaje
hadi hapa nilipofikia tukio lile bado lilikuwa halina uhusiano wowote wa kile
nilichokuwa nikiendelea kukichunguza.
Niliendelea kuwaza wakati nilipokuwa nikiegesha gari langu kwenye viunga
vya maegesho ya magari vya Vampire Casino baada ya kutoka kwenye ile nyumba
alipoingia yule msichana usiku wa jana kule mtaa wa Nkurumah na kumkosa. Nilikuwa
nimepitisha msako wa kina kwenye ile nyumba na hatimaye kuja na hitimisho moja
kuwa ile myumba ilikuwa ikikaliwa na mwanaume askari wa jeshi la wananchi wa
Tanzania baada ya kuiona picha yake uliyovunjika mle ndani ya ile nyumba sebuleni
sakafuni na sare za jeshi zilizokuwa kabatini chumbani kwake. Bado sikuweza
kumtambua yule msichana kuwa alikuwa nani hata hivyo niliampa kumfuatilia.
Niliegesha gari langu na nilipoitazama saa yangu ya mkononi nikagundua
kuwa dakika chache zilikuwa zimetoweka tangu ilipotimia saa nne asubuhi. Magari
yaliyoegeshwa mbele ya Vampire Casino hayakuwa mengi na miongoni mwa magari
hayo zilikuwepo teksi za abiria.
Kabla ya kushuka kwenye gari niliyatembeza macho yangu tena nikitathmini hali
ya mandhari yale kisha nikafungua mlango na kushuka nikielekea sehemu ya mlango
wa mbele wa casino ile kulipokuwa na ofisi ya mapokezi na huduma kwa mteja.
Kwa namna nyingine nilifurahi sana kwa kutowaona wale mabaunsa wa mlangoni
waliyonichachafya usiku wa jana wakati nilipokuwa nikitaka kuingia ndani ya casino
ile na badala yake msichana mzuri na mrembo akanipokea kwa bashasha zote huku
akiniweka kwenye kundi la Status conscious customer kutokana na mwonekano wangu nadhifu wenye sura ya kirafiki.
‘Kumbe wasichana warembo bado wapo duniani’ nilijisemea moyoni wakati nikilifikia lile
dawati la mapokezi mbele yangu lililomwifadhi msichana mlimbwende mwenye kila
kionjo cha uzuri.
“Karibu kaka” dada yule alinikaribisha kwa bashasha zote.
“Ahsante sana pole na kazi” nilimwambia huku nikiumba tabasamu la kirafiki
usoni mwangu.
“Nishapoa” dada yule aliongea kwa sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni huku
tabasamu lake usoni likikataa kwenda likizo.
“Tafadhali! naomba nikusikilize” hatimaye yule dada alivunja ukimya baada ya
kuniona nikiendelea kumkodolea macho ya mshangao uliotokana na uzuri wake.
Kabla ya kumjibu yule dada nikageuka nyuma kutazama kule kwenye maegesho
ya magari ya ile casino baada ya kuona gari dogo aina ya Nissan March likiingia eneo lile
na kutafuta maegesho. Kitendo cha kuwaona mwanamke na mwanaume wakishuka
kwenye gari lile kikanifanya niyarudishe macho yangu kumtazama tena yule dada
mbele yangu.
“Nahitaji kuwa mwanachama wa casino” nilimwambia yule dada kwa utulivu huku
tukitazamana.
“Oh! karibu sana na ondoa shaka kaka” yule dada aliniambia huku akivuta
mtoto wa meza yake na kuchukua karatasi fulani na kuziweka juu ya ile meza mbele
yangu. Niliposogea karibu na kuzitazama vizuri karatasi zile nikagundua kuwa
zilikuwa ni fomu kwa ajili ya usajili wa uanachama wa casino ile. Fomu zile zilikuwa
na vitu kama;nembo kubwa ya ile casino,anwani zake zote kama namba za simu za
uongozi,namba za nukushi,tovuti na barua pepe. Chini ya fomu zile kulikuwa na
sehemu za kujaza taarifa ya mtu anayeomba uanachama.
“Jaza taarifa zako humo ndani” yule dada akaniambia huku akinipa kalamu ya
wino.
“Naomba unijazie wewe mimi sijui kusoma wala kuandika” nilimwambia yule
dada nikichombeza utani huku nikimrudishia zile fomu. Tukio lile likampelekea
yule dada anitazame kwa mshangao hata hivyo macho yetu yalipokutana kila mmoja
akajikuta akitabasamu.
Yule dada akaipokea ile fomu na muda mfupi uliyofuata akaanza kuniuliza taarifa
zangu na kila nilipomjibu akawa akinijazia taarifa zile za uongo kwenye ile fomu.
Baada ya muda mfupi tukawa tumemaliza zoezi lile.
“Bado ada ya mwanachama” yule dada akaniambia huku akimalizia kujaza taarifa
zangu kwenye ile fomu.
‘‘Ada ni pesa kiasi gani?” nilimuuliza yule dada na aliponiambia nikatumbukiza
mkono mfukoni kuchukua wallet yangu kisha nikachukua kiasi cha pesa nilizopaswa
kulipa kutoka kwenye wallet ile na kumkabidhi yule dada.
Taratibu za ule usajili zilipokamilika nikakabidhiwa kadi ndogo ya utambulisho
wangu ambayo ningekuwa nikiitumia kuingia kwenye casino. Niliipokea kadi ile na kuitia mfukoni huku nikifurahi kufanikiwa kwa zoezi lile ndani ya muda mfupi.
Hatimaye nikaagana na yule dada na kuelekea sehemu nilipoegesha gari langu
kwenye yale maegesho ya ile casino.
Muda mfupi baadaye niliyaacha maegesho yale na kurudi ofisini kwangu ambapo
asubuhi ile nilikuwa nimemwacha Mwasu akiendelea kuandaa ripoti ya upelelezi wa
mkasa wa MIFUPA 206.
_____
KITENDO CHA KUEGESHA GARI LANGU chakavu aina ya Peugeot 504 toleo
la zamani katikati ya magari mawili ya kifahari na kisasa katika viunga vya maegesho
ya magari vya Vampire Casino usiku huu kilinifanya nijihisi mnyonge wa kipato.
Ningeweza kutafuta sehemu nyingine katika maegesho haya ambayo ingeendana na
hadhi ya gari langu lakini kwa wakati huu nilifahamu kuwa hilo lisingewezekana.
Magari mengi yaliyoegeshwa kwenye eneo lile bila shaka yangeweza kwendana na
thamani ya kiinua mgongo cha wakurugenzi wa kampuni kubwa za hapa nchini na
mgeni yeyote kutoka nje ya Tanzania ambaye ingekuwa ndiyo mara yake ya kwanza
kufika eneo lile huwenda angeshangazwa sana na ile kauli ya kuwa Tanzania ni nchi
masikini.
Eneo la maegesho yale lilikuwa mbioni kufulika magari ya kifahari hata hivyo hali
ile haikunitia mshawasha wowote badala yake nikautia mche wa sigara mdomoni na
kuiwasha huku nikiendelea kutathmini hali ya mandhari yake.
Niligeuka na kuitazama saa ndogo ya gari iliyokuwa kwenye dashibodi na saa ile
ilionesha kuwa dakika chache zilikuwa zimetokomea baada ya kutimia saa mbili usiku.
Nikajishauri kuwa nishuke na kuelekea ndani ya casino ile au niendelee kukaa mle
ndani ya gari huku nikilisubiri lile gari refu na jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van
lililombeba yule mlimbwende wa jana liwasili eneo lile.
Hata hivyo baada ya kufikiri kwa kitambo lile wazo la kulisubiri lile gari refu na
jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van lifike eneo lile hatimaye nikaliweka kando
kwani sikutaka kutengeneza aina yoyote ya kivutio eneo lile.
Hatimaye nikaichukua bastola yangu na kuichimbia kwenye maficho mazuri mle
ndani ya gari kisha nikafungua mlango na kushuka. Kupitia kitabu kidogo chenye
maelekezo ya taratibu zinazopaswa kuzingatiwa na mwanachama wa casino ile
ambacho nilikuwa nimepewa na yule dada aliyenisajili kuwa mwanachama wa casino ile
asubuhi iliyopita. Nilikuwa nimekumbuka kuwa kuingia na silaha mle ndani ya casino
lilikuwa ni jambo lililokatazwa kwa herufi kubwa. Hivyo sikutaka kujiingiza matatani
kwa kuikiuka sheria ile na ndiyo kisa nikaamua kuiacha bastola yangu mle ndani ya
gari.
Nililisubiri gari moja lililokuwa likija ule upande wangu linipite kisha nikavuka
eneo lile na kuanza kutembea taratibu nikielekea kwenye ule mlango wa mbele wa
casino.
Nilifika eneo la mbele la casino ile na kuanza kupanda ngazi zilizokuwa eneo lile na mara tu nilipomaliza kuzipanda ngazi zile njemba mbili matata,mabaunsa wa
mlangoni pale zikajitokeza kunikabili. Niliwatazama mabaunsa wale waliokuwa tayari
kukabiliana na aina yoyote ya ukorofi wangu na hapo nikafurahishwa na utendaji
wao. Hivyo pasipo kupoteza muda nikazama mfukoni kuichukua ile kadi yangu ya
utambulisho wa mwanachama wa casino ile na kuwaonesha. Zile njemba kuona vile
zikanywea na kufungua njia zikiniruhusu niendelee na safari yangu.
Niliirudisha ile kadi yangu mfukoni kisha nikaendelea na safari yangu na baada ya
muda mfupi nikawa nimeufikia ule mlango wa mbele wa vioo wa ile casino ambapo
niliusukuma na kuzama ndani huku nikiwa na hakika kuwa macho ya njemba zile
mbili zenye nguvu za kipigo yalikuwa yakinisindikiza nyuma yangu.
Sasa nilikuwa nimeingia ndani ya Vampire Casino kisima cha starehe chenye bidhaa
zote za kishetani.
Wakati nikipiga hatua zangu kuendelea na safari mle ndani ya ile casino nikajikuta
nikijiuliza kama bado nilikuwa jijini Dar es Salaam au nilikuwa kwenye jiji lingine
mashuhuri duniani. Kwani kwa namna moja au nyingine nilikuwa nimeshangazwa
sana na mambo niliyoanza kuyaona mle ndani.
Kwa tathmini yangu ya haraka ni kuwa idadi kubwa ya watu waliokuwa
mle ndani ya ile casino walikuwa ni watu wa kutoka mataifa yenye afya kiuchumi
kama;wazungu,wachina,waarabu na wahindi. Idadi ndogo ya watu waliosalia mle
ndani walikuwa ni watu weusi kama mimi.
Katika korido fupi na pana niliyoingia niliziona jozi kadhaa za wapenzi wakiwa
wamekumbatiana wakinyonyana ndimi na kufanya matendo mengine ya kishetani.
Nilipowatazama watu wale nikagundua kuwa wanaume walikuwa wa rika tofauti
wadogo kwa wakubwa lakini wale wasichana walikuwa ni mabinti wadogo sana kwa
umri huku wakiwa wamevaa nguo fupi nusu uchi na mienge ya sigara mikononi
mwao.
Hata hivyo watu wale hawakuonekana kushtushwa sana na ugeni wangu mle
ndani badala yake walionekana kuendelea na hamsini zao. Wasichana wawili wadogo
walinisogelea na kujaribu kuniwekea ukuta njiani wakijaribu bahati zao lakini mwendo
na sura yangu viliwaonya hivyo wakawahi kunipa mgongo huku wakiachia misonyo
ya hasira.
Hatimaye nikawa nimetokezea kwenye ukumbi mpana na ndani ya ukumbi ule
kulikuwa na taa za aina tofauti zikimulika huku na kule katika namna ya kupokezana.
Upande wa kushoto wa ukumbi ule kulikuwa na makochi ya sofa yaliyopangwa katika
namna ya kuzizunguka meza fupi za vioo zilizokuwa katikati. Pia kulikuwa na meza
na viti vya kisasa ambavyo baadhi yake vilikuwa vimekaliwa na watu huku juu ya meza
hizo kukiwa na aina tofauti za vinywaji.
Sehemu ya katikati casino ile ndipo palipokuwa pakifanyika mambo ya ajabu.
Wasichana wawili wenye maumbo mazuri ya mvuto wa ngono walikuwa wamevaa
chupi nyekundu za bikini zenye mikanda myembamba zilizokuwa zimeacha wazi
baadhi ya sehemu nyeti za miili yao.
Wasichana wale walikuwa wakinyonyana ndimi na kushikana sehemu zao nyeti
katika namna ya kuwapandisha ashki wanaume waliokuwa wakiwatazama. Wasichana
wale walikuwa juu ya jukwaa dogo la umbo duara lililokuwa likimulikwa kwa mwanga
mkali wa taa tofauti zilizokuwa sehemu ya juu ya eneo lile.
Katika jukwaa lile kulikuwa na bomba moja refu lililokuwa limeshikiliwa na
sehemu ya juu ya paa la ile casino huku sehemu ya chini ya bomba lile ikiwa imejikita
katikati ya lile jukwaa la umbo duara.
Wasichana wale juu ya lile jukwaa walikuwa wakilitumia bomba lile kucheza
muziki uliokuwa ukipigwa mle ndani kwa kujibinua binua katika mitindo tofauti huku
wakizishika nyeti zao. Kwa kufanya watu wengi wa mle ndani walitulia wakiwatazama
wasichana wale katika namna ya kuhamasika na matendo ya ngono
Niliyatembeza macho yangu mle ndani na upande wa kulia wa ule ukumbi
sehemu kulipokuwa na giza hafifu nikaona kuwa kulikuwa na makochi ya sofa na
baadhi ya makochi yale yalikuwa yamekaliwa na watu. Niliutazama vizuri upande
ule na hapo nikawaona baadhi ya mabinti wadogo wakiwa uchi wa mnyama huku
baadhi yao wakiwa wamevaa sketi fupi bila nguo za ndani. Wasichana wale baadhi
yao walikuwa wamepakatwa na wanaume wadogo kwa wakubwa na nilipochunguza
vizuri nikagundua kuwa walikuwa wakifanya ngono na wanaume wale bila wasiwasi
wowote kama sodoma na gomola. Kwa kweli niliwahurumia sana wabinti wale wadogo
lakini sikuwa na namna ya kufanya.
Niligeuka na kutazama mbele ya ukumbi ule na hapo nikaona kaunta kubwa ya
vinywaji ikiwa na wahudumu waliovaa sare. Baadhi ya wahudumu wale walikuwa
wakipishana huku na kule na masinia yao mikononi kupeleka vinywaji kwa wateja na
kuchukua chupa za vinywaji zilizokwisha tumika.
Nilitembea nikikatisha kando ya ukumbi ule wa casino na nilipofika sehemu
fulani upande wa kushoto nikaona ukumbi mwingine mkubwa. Ndani ya ukumbi
ule kulikuwa na mashine nyingi za kamari zilizopangwa katika mtindo unaovutia.
Nilisimama na kutazama eneo lile na hapo nikawaona baadhi ya watu wakiwa
wanaendelea kucheza kamari katika mashine zile.
Upande wa kulia wa ukumbi ule kulikuwa na milango mitatu iliyoongozana.
Katika ile milango mitatu milango miwili ilifanana kwa ukubwa lakini ule mlango
mmoja wenyewe ulikuwa tofauti na mkubwa. Juu ya mlango ule kulikuwa na
maandishi makubwa yakisomeka Bulk transaction Only . maelezo yale yakanitanabaisha
kuwa ndani ya mlango ule kulikuwa na chumba kilichokuwa kikitumiwa cha wacheza
kamari wenye pesa nyingi. Katika ile milango miwili iliyolingana juu yake kulikuwa
na vibandiko vyenye kuelekeza sehemu za maliwato kwa wanaume na wanawake.
Muziki laini uliokuwa ukipigwa kupitia spika fulani zilizokuwa mle ndani uliwaacha
watu katika viwango vya juu vya starehe zao.
Hatimaye nikaendelea na safari yangu nikielekea kwenye eneo la ile kaunta
ya vinywaji ambapo baada ya kufika ningetafuta sehemu nzuri ya kuketi ambayo
ingeniwezesha kuona vizuri kitu chochote ambacho kingekuwa kikiendelea mle ukumbuni. Hata hivyo wakati nikiendelea kutembea mle ndani nikagundua kuwa
kulikuwa na wanaume wawili waliokaa nyuma ya ule ukumbi ambao walikuwa
wakinitazama kwa makini sana.
Nilifika pale kaunta kisha nikavuta stuli moja ndefu na kupanda juu. Watu
wachache waliokuwa kwenye kaunta ile wakijipatia kinywaji wakageuka kunitazama
kidogo kabla ya kuendelea na hamsini zao.
Mhudumu wa kaunta ile mwanaume mrefu mweusi mwenye mwili uliojengeka
vizuri na sura ya ucheshi akiwa amevaa suruali nyeusi,shati jeupe na tai ndogo nyeusi
shingoni alinisogelea haraka na kunisikiliza haja yangu.
“Leapfrog cocktail baridi tafadhali!” nilimwambia mhudumu yule huku nikigeuka
kutazama kule nyuma ya ule ukumbi sehemu walipokuwa wamekaa wale wanaume
wawili. Sikuwaona wale watu hata hivyo hali ile haikunitia mashaka.
Muda mfupi baadaye yule mhudumu wa ile kaunta alinisogezea bilauri ya
kinywaji baridi cha Leapfrog cocktail yenye mrija mrefu na karatasi nyeupe ya tishu
iliyozungushiwa kwa nje.
Niliisogeza bilauri ile karibu yangu na kupitia mrija ule nikavuta funda moja la
kinywaji kile kikali na kukiacha kikiteremka taratibu kifuani kwangu na kutengeneza
starehe ya aina yake.
Kabla ya kuja kwenye casino hii nilikuwa nimetoka mtaa wa Nkurumah kwenye ile
nyumba huku nikitarajia kumuona tena yule msichana niliyemfuatilia kutoka Vampire
Casino usiku wa jana. Hata hivyo juhudi zangu zilikuwa zimegonga mwamba.
Nilikuwa nimejibanza kwa muda mrefu mle ndani ya ile nyumba huku nikimsubiri
yule msichana arudi lakini kitendo cha kuyaona masaa mengi yakitoweka bila msichana
yule kujitokeza nikaamua kutoka nje ya nyumba ile na kuendelea na hamsini zangu
huku nikipanga kurudi tena baadaye.
Bado akili yangu ilikuwa ikiendelea kusumbuka katika kutaka kufahamu kuwa
msichana yule alikuwa nani na kwani alihusika katika kifo cha yule mtu kule ghorofani
mtaa wa Nkurumah. Hata hivyo bado nilijipa matumaini kuwa hatimaye ukweli wa
mambo ungejulikana.
Mara kadhaa nilijikuta nikishawishika kutaka kuwasaidia polisi juu ya muuaji yule
kwani hadi wakati huu ushahidi nilikuwanao ingawa haukuwa wa moja kwa moja.
Lakini nilijikuta nikiachana na mpango hule pale nilipoanza kuhisi kuwa huwenda
msichana yule alikuwa akihusika kwa namna fulani na kile nilichokuwa nikikipeleleza.
Nilivuta tena funda moja la kinywaji kuupoza mtima wangu huku nikiyatembeza
tena macho yangu mle ukumbini. Kutoka pale nilipoketi niliweza kuziona ngazi
upande wa kushoto wa ukumbi ule zilizokuwa zikielekea ghorofa ya juu. Tukio lile
likanipelekea nianze kuhisi kuwa kule ghorofani ngazi zile zilipokuwa zikielekea
kulikuwa na shughuli nyingine za casino ile zilizokuwa zikiendelea. Nilipotazama vizuri
upande ule wenye zile ngazi mara nikakiona kibao kingine kidogo chenye maandishi
ya V.I.P hall and accommodation na hapo nikajua kuwa kule juu kulikuwa na ukumbi
mkubwa wa starehe na sehemu za kulala zilizokuwa zikitumika na watu wa daraja la juu. Kwa kweli ule ulikuwa ni uwekezaji wa aina yake. Niliendelea kuyatembeza
macho yangu mle ndani huku nikivuta sigara yangu taratibu mdomoni.
Niliitazama tena saa yangu ya mkononi kisha nikavuta funda jingine la kinywaji.
Bado kulikuwa na muda mfupi wa kusubiri kabla ya Milla Cash hajaingia mle ndani na
hicho ndiyo nilichokuwa nikikisubiri.
“Vipi hujisikii upweke?” mwanamke mmoja aliyeketi jirani yangu pale kaunta
aliniuliza kwa lugha safi ya kiingereza pengine baada ya kushochwa na ukimya wangu.
Mwanamke yule alikuwa amevaa suruali nyeusi ya jeans na blauzi nyepesi ya rangi ya
cream chafu. Katika vidole vya mkono wake alikuwa amevaa pete mbili za madini ya
Tanzanite na Almasi nyeupe. Nywele zake za rasta alikuwa amezizungusha na kuzifunga
kichwani kwa kitambaa cha rangi nyeusi. Mara nilipotulia na kumsikiliza vizuri yule
mama nikagundua kuwa namna ya matamshi ya kiingereza chake alifaa kufananishwa
na raia wa kutoka nchini Nigeria.
Mwanamke yule alikuwa akivuta sigara ya brand ya kifahari na juu ya meza ile ya
kaunta mbele yake alikuwa na kinywaji baridi cha Cocktail aina ya Manhattan. Kwa
tathmini yangu ya haraka nikahitimisha kuwa mwanamke yule alikuwa ni mtu mwenye
kipato cha kueleweka.
“Nilidhani unahitaji utulivu kidogo bibie” nilimwambia mwanamke yule kwa
lugha yangu safi ya kiingereza kisicho cha kubabaisha huku nikigeuka kumtazama na
kutabasamu.
“Kwa nini unapenda Cocktail ya Manhattan?” nilimchokoza mwanamke yule huku
nikimtupia macho ya udadisi.
“Ni kama wewe unavyopenda Cocktail ya Leapfrog” mwanamke yule aliongea huku
akitabasamu kisha akaendelea
“Hapo zamani nilikuwa mpenzi wa Cocktail aina ya Leapfrog,Negroni naSpritz lakini
nilijikuta nikiachana nazo baada ya kupata company nzuri ya wanywaji wa Manhattan
Cocktail. Hata hivyo sizichukii ingawa kwa sasa sizipendelei sana” mwanamke yule
aliongea huku akiitia sigara yake mdomoni.
Nilimtazama kwa udadisi mwanamke yule na hapo nikagundua kuwa alikuwa
akionekana kuzimudu vizuri starehe za dunia kwa namna yake.
“Mimi huwa ni mpenzi wa Manhattan Cocktail ingawa siyo mnywaji wa mara kwa
mara” niliongea kwa utulivu na baada ya kitambo kifupi cha ukimya nikaendelea.
“Lafudhi yako inaonesha kuwa wewe siyo mwenyeji waTanzania”
“Mimi ni raia wa Nigeria lakini maskani yangu kwa sasa yapo Capetown nchini
Afrika ya kusini” mwanamke yule aliniambia kwa utulivu huku akivuta funda la
kinywaji chake pale juu ya kaunta.
“Umekuja hapa Dar es Salaam kwa safari ya kikazi?” nilimuuliza yule mwanamke
huku taratibu kisha nikaipeleka sigara yangu mdomoni.
“Hapana! nipo hapa Dar es Salaama kwa ajili ya mapumziko mafupi ya likizo
yangu” yule mwanamke akaniambia huku akinitazama na hapo nikapata nafasi ya
kuiona vizuri sura yake.Alikuwa mwanamke wa makamo umri wake huwenda ulikuwa kati ya miaka
ishirini na nane na thelathini na mbili. Macho yake imara yenye nguvu makubwa na
legevu kiasi yalikuwa na kila kitu mwanaume alichopenda kukiona. Tulitazamana
na macho yetu yalipokutana kila mmoja akatabasamu na hapo haraka nikajua kuwa
alikuwa ni mwanamke wa aina yangu.
“Kwa nini ukaichagua Dar es Salaam kama sehemu ya mapumziko ya likizo
yako badala ya miji mingine ya Afrika mashariki kama Nairobi,Kigali,Bujumbura au
Kampala?” nilimuuliza mwanamke yule baada kuvuta funda la kinywaji.
“Nimewahi kufika huko kote lakini mtindo wa maisha ya hapa jijini Dar es Salaam
naweza kusema umenivutia sana” mwanamke yule aliongea huku akitabasamu na
hapo uzuri wake ukajitokeza.
“Kwa vipi?” nikamuuliza.
“Watanzania ni watu wakarimu mno!” yule mwanamke aliongea huku akiangua
kicheko hafifu kilichoniacha njia panda na hapo nikashindwa kuelewa kama kweli sisi
watanzania tulikuwa wakarimu kiasi cha kusifiwa na wageni au tulikuwa waoga katika
kufanya maamuzi ya msingi.
Nilipozikumbuka kashfa mbali mbali zilizokuwa zikiibuka nchini Tanzania kila
kukicha kama;EPA,Richmond,Escrow,kusafirishwa kwa wanyama wetu kwenye ndege kwenda
nchi za nje,kauli za viongozi wakwapuaji wa mamilioni ya pesa zetu bila huruma,chokochoko
za itikadi za kidini,mauaji ya wapigania haki na usawa na ubabe wa vingozi wetu,nikabaki
nikimeza funda kubwa la mate kuitowesha hasira yangu kifuani.
“Karibu sana!” hatimaye niliongea huku nikitabasamu.
“Ahsante!” yule mwanamke akaitikia huku akivuta funda la kinywaji.
Nilivuta funda moja la kinywaji kisha nikayatembeza macho yangu mle ukumbini
kabla ya kuyarudisha kwa yule mwanamke na hapo nikamuuliza huku nikimtazama
usoni.
“Jina lako?”
“Iko–ojo Obaje” mwanamke yule aliongea huku akiitia sigara yake mdomoni na
alipoitoa akaupuliza moshi wake pembeni kisha akaisogeza ile bilauri yake ya kinywaji
na kuvuta mafunda kadhaa kisha akageuka tena na kunitazama.
“Na wewe je?” akaniuliza.
“Naitwa Stephen Masika” nikamdanganya
“Wewe ni mwenyeji wa hapa Dar es Salaam?”
“Ndiyo! nimezaliwa na kukulia hapa”
“Oh! vizuri sana bila shaka sasa nitakuwa nimepata mwenyeji wa kufikia hapa jijini
Dar es Salaam” mwanamke yule akaongea huku akiangua kicheko hafifu cha furaha
nami nikaungana naye kwa kutabasamu kidogo kisha nikavunja ukimya.
“Umekuja na familia yako?” nilimuuliza lakini nikashangaa kumuona akitabasamu
na hatimaye kuangua kicheko.
“Mimi sina familia wala sijaolewa” mwanamke yule aliongea huku akiitia sigara
yake mdomoni huku kicheko chake kikiwa bado hakijafika tamati.
“Kwanini mwanamke mzuri kama wewe hujaolewa na umri wako unakuruhusu?”
nilimuuliza.
“Wanaume wanataka wake zao wawe ni watu wa kukaa nyumbani,wawafulie nguo
zao na kuwapigia pasi,wawapikie vyakula vitamu na kuwazalia watoto. Mimi najiona
kuwa siyo mwanamke wa aina hiyo” yule mwanamke akaongea baada ya kuitua bilauri
yake ya kinywaji pale juu ya kaunta na hapo nikamtazama huku nikimlinganisha na
maneno yake.
“Huna mpango wa kupata mtoto?” nikamuuliza na kuitia sigara yangu mdomoni
huku nikapambana na taswira ya matiti yake yaliyokuwa nusu wazi kifuani mwake.
Harufu nzuri ya manukato yake ikazipumbaza kwa muda hisia zangu. Hata hivyo
nilishangaa kumuona akitabasamu.
“Hujui kuwa mtoto ni sawa na mume wa pili. Itabidi umlishe,umfulie
nguo,umuogeshe,umpeleke hospitali,umpeleke shule. Kwa kweli nawahurumia sana
wanawake wenzangu”
“Mh! basi wewe utakuwa mwanamke wa aina yake” nilimwambia yule mwanamke
huku nikiipeleka bilauri ya kinywaji mdomoni na wakati nikifanya vile mara nikajikuta
nikivutiwa na tatoo iliyokuwa shingoni mwake. Mchoraji wa tatoo ile bila shaka alikuwa
fundi stadi mno ingawa hata hivyo tatoo ile haikunivutia hata kidogo.
Ilikuwa ni tatoo ya kichwa cha nyoka mwenye sumu kali huku akiwa ameachama
kinywa chake wazi na ulimi wake mrefu wenye pacha mbili ukiwa nje. Nikiwa
nimeduwaa kuitazama ile tatoo yule mwanamke ni kama ambaye hakuvutiwa na angalia
yangu hivyo aligeuka katika namna ya kunifanya nisiweze kuiona vizuri ile tattoo. Kwa
kutaka kumpa uhuru zaidi nikatumbukiza hoja mpya.
“Hapa Dar es Salaam umefikia wapi?” nilimuuliza yule mwanamke na hapo
nikamuona akiupeleka mkono wake kwenye pochi yake ndogo ya mkononi.
Alipoifungua ile pochi akatoa kadi ndogo na kunipa. Niliipokea ile kadi na kuitazama
kwa makini. Ilikuwa ni kadi ndogo yenye maelezo ya namba ya chumba cha hoteli
moja ya kifahari iliyopo jijini Dar es Salaam na chini ya kadi ile kulikuwa na namba
za simu.
“Ukipata nafasi unaweza kuja kunitembelea kwani bado nina siku kadhaa za kukaa
hapa jijini Dar es Salaam” yule mwanamke akaniambia huku akivuta tena funda la
kinywaji pale kaunta.
“Ninaweza kukutembelea wakati gani?” nilimuuliza na baada ya kufikiria kidogo
akaniambia
“Muda wowote utakapopata nafasi”
“Nashukuru sana,nitajitahidi” niliichukua ile kadi na kuitia mfukoni na wakati
nikifanya vile macho yangu yakajikuta yakivutwa na msichana aliyekuwa akiingia mle
ndani. Nikageuka na kutazama upande ule wa ukumbi na mara nikamuona Milla Cash
akiingia mle ndani.
Mshangao kidogo ukiwa umenishika nikayapelekea macho yangu nikimtazama
msichana yule kwa udadisi na mara hii niliweza kuubaini vizuri uzuri wake. Alikuwa mwanamke mzuri mno niliyewahi kumuona katika kipindi chote cha maisha yangu.
Nikiwa na hakika kuwa pale nilipokuwa nimekaa isingekuwa rahisi kwake
kunitambua niliyapa macho yangu utulivu huku ubongo wangu ukifanya usajili makini
wa taarifa nilizokuwa nikizihitaji.
Milla Cash alikuwa akitembea kwa madaha katika ule mtindo wa catwalk huku
mwili wake ukinesa taratibu kama mtu aogopaye kukanyaga ardhi. Alikuwa amevaa
gauni jepesi na fupi la rangi nyekundu iliyoiva vizuri lenye utepe mweupe kiunoni
na kulifanya umbo lake adimu lijichore vizuri na kuamsha hisia kwa mwanaume
yeyote ambaye angethubtu kumtazama. Gauni lile fupi liliyaanika wazi mapaja yake
laini yenye minofu ya misuli. Uwazi mdogo ulioachwa na gauni lile kifuani mwake
uliyaacha wazi matiti yake makubwa ya wastani yenye chuchu imara.
Milla Cash aliendelea kutembea kwa madaha huku akiyaacha macho ya wanaume
waliokuwa mle ukumbuni yakimsindikiza kila alipozisimika chini hatua zake. Wale
walinzi wake wawili walimuwekea ngome imara ya ulinzi upande wa kulia na kushoto
huku wakiwa wameshika mabegi mikononi mwao. Nilipowachunguza walinzi wale
vizuri nikatambua kuwa walikuwa walinzi mahiri wasiokuwa na mzaha. Suti zao
nyeusi ziliwakaa vyema na miili yao ilikuwa imejengeka vizuri kuwakabili wakorofi.
Bado macho yangu yalikuwa kwa Milla Cash huku moyoni nikijiuliza kwanini
alikuwa akilindwa namna ile na kwa kweli tukio lile lilinishangaza sana. Nikautia tena
mche wangu wa sigara mdomoni huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu.
Niliendelea kumtazama Milla Cash huku nikitambua kuwa subira na uvumilivu
ndiyo silaha kubwa katika mafanikio yangu. Nilipoitoa sigara yangu mdomoni
nikaupuliza moshi pembeni kisha nikainama na kuvuta funda la kinywaji huku
nikiyatembeza macho yangu mle ukumbini.
Sasa nilimuona Milla Cash na wale wapambe wake wakipanda zile ngazi kuelekea
ile ghorofa ya juu yenye kile kibao cha V.I.P hall and Accommodation. Nikaendelea
kuwatazama hadi pale walipopotea kabisa machoni mwangu na hapo nikabaki
nikitafakari.
Baada ya kitambo kifupi kupita tangu Milla Cash na wale walinzi wake kupanda
kule ghorofani. Mara nikamuona mtu mmoja aliyekuwa ameketi pale kwenye makochi
ukumbini akisimama na kuelekea kule juu ya ghorofa. Kilipita kitambo kirefu huku
macho yangu yakiendelea kutazama juu ya zile ngazi na hatimaye nikamona yule mtu
aliyeelekea kule juu hapo awali akishuka tena zile ngazi.
Yule mtu alipofika pale chini hakurudi tena pale alipokuwa ameketi hapo awali
na badala yake aliambaa na ukuta wa ukumbi ule akielekea nje huku akiwa ameushika
mkoba mweusi wa ngozi mkononi.
Muda mfupi baada ya yule mtu wa awali kutokomea mara nikamuona mtu
mwingine akisimama kutoka pale ukumbini na kuelekea kule juu ghorofani alipotoka
yule mtu wa awali huku akiwa na mkoba mkononi. Hali ikawa kama kwa yule mtu
wa kwanza kwani baada kitambo kifupi kupita mara nilimuona yule mtu akirudi na
mkoba wake mkononi na alipomaliza kushuka zile ngazi hakurudi pale alipokuwa ameketi hapo awali badala yake nilimuona akielekea nje. Mtu wa tatu naye akafanya
vilevile kabla ya kufuatiwa na mtu mwingine. Kwa kweli hali ile ilinishangaza sana.
Niliendelea kuitazama mienendo ya watu wa mle ndani huku nikiendelea kuupisha
utulivu akilini mwangu. Hata hivyo nilishindwa kabisa kuelewa kilichokuwa kikiendelea
mle ndani. Hatimaye nikainama tena na kuvuta mafunda kadhaa ya kinywaji hadi pale
bilauri ile ilipobaki tupu.
Fikra zangu ziliporudi eneo lile nikakumbuka kuwa uchunguzi wangu ulikuwa
umeniweka mbali na maongezi ya Iko-Ojo Obaje aliyekuwa kando yangu pale kaunta.
Hivyo nikageuka na kumtazama Iko-Ojo Obaje huku nikiona aibu kwa kutokuwa
makani na uwepo wake. Yule mwanamke hakuwepo pale alipokuwa ameketi na kiti
chake kilikuwa wazi. Loh! nikaanza kujilaumu kuwa nilikuwa nimepoteza umakini kwa
kiwango cha juu huku nikijiuliza kuwa mwanamke yule angekuwa ameelekea wapi.
Hatimaye nikaitoa wallet yangu kutoka mfukoni ambapo niliifungua na kuchukua kiasi
fulani cha pesa kwa ajili ya kulipia kile kinywaji. Hata hivyo nilishangaa sana kumuona
yule mhudumu wa kaunta ya vinywaji akikataa kuipokea pesa yangu.
“Bro! umeshalipiwa” yule mhudumu wa kaunta akaniambia huku akiondoa bilauri
za vinywaji zilizokuwa pale kaunta halafu kwa kitambaa chake kidogo mfano wa taulo
alichokuwa amekining’iniza begani akaanza kufuta ile meza ya kaunta.
“Una maana gani?” nilimuuliza yule mhudumu wa kaunta kwa makini huku
nikimtazama usoni.
“Umeshalipiwa kinywaji na yule dada aliyekuwa ameketi kando yako” yule jamaa
akaniambia huku akitabasamu. Sikuwa namna hivyo nikaichukua pesa yangu pale juu
ya kaunta na kuitia mfukoni.
“Alikueleza kuwa anaelekea wapi?” nikamuulia yule mhudumu wa kaunta
“Hapana!” yule mhudumu akanijibu huku akiendelea kutabasamu na hapo
nikajua kuwa kile kitendo cha mimi kulipiwa kinywaji na yule mwanamke kilikuwa
kimemfurahisha sana. Nilimuacha yule mhudumu akiendelea kufurahi kisha nikashuka
kutoka kwenye ile stuli ndefu ya kaunta na kushika uelekeo wa upande wa kulia wa ile
kaunta nikielekea eneo la maliwato la ukumbi ule.
Wakati nikitembea kuelekea eneo la maliwato la ukumbi ule nikajikuta nikivutiwa
na ubora wa casino ile. Mikono ya mafundi ujenzi ilikuwa imeitendea haki taaluma
yao. Kila eneo la ndani ya casino ile lilivutia kulitazama na kuta zake zilikuwa safi na
zilizonyooka vizuri na kupambwa kwa nakshi tofauti za kupendeza. Mwanga wa taa za
mle ndani uliakisiwa vizuri na marumaru za kisasa zilizokuwa sakafuni na kutengeneza
mandhari nzuri inayovutia sana kutazama.
Baada ya hatua chache za safari yangu hatimaye niliingia upande wa kushoto
sehemu iliyokuwa na milango miwili. Mlango mmoja ulikuwa kwa ajili ya sehemu
ya maliwato ya wanaume na mlango mwingine ulikuwa ni kwa ajili ya sehemu ya
maliwato ya wanawake.
Nilishika kitasa cha mlango wa maliwato ya kiume kisha nikaufungua mlango ule
na kupotelea ndani. Mara baada ya kuingia mle ndani nikawa nimetokezea kwenye korido pana iliyotazama na milango kumi na mbili ya vyoo. Baadhi ya milango ile
ilikuwa wazi huku mingine ikiwa imefungwa. Hata hivyo hakukuwa na dalili za uwepo
wa mtu yoyote mle ndani. Vyoo vyote vilionekana visafi na kwenye ule ukuta wa
korido iliyokuwa ikitazamana na ile milango ya vyoo kulikuwa na kioo kipana cha
kujitazama.
Pembeni ya kioo kile kulikuwa na masinki ya ukutani kwa ajili ya haja ndogo
pamoja na mifereji midogo ya chini iliyojengewa vizuri kwa marumaru nyeupe kwa
ajili ya kukusanya maji taka na kuyasafirisha nje.
Nilichagua choo kimoja kilichokuwa mwishoni mwa ile korido kisha nikafungua
mlango na kuingia ndani. Nilitaka kwenda haja ndogo kwani kile kinywaji kilikuwa
kimekijaza vibaya kibofu changu.
Wakati nilipokuwa nikijiandaa kwenda haja ndogo mara nikaanza kuhisi kuwa mle
ndani kwenye korido ya vile vyoo kulikuwa na mtu na mtu huyo alikuwa akitembea
taratibu kuvikagua vile vyoo.
Nikiwa nimeanza kuhisi jambo baya sikutaka kumshtua mtu yule hivyo kimiminika
changu nikakitupia ukutani na hapo kikawa kikishuka chini kwa utulivu katika ukimya
wa kifo huku masikio yangu yakifanya kazi ya ziada kusikiliza hatua za mtu yule.
Hatimaye ile sauti ya hatua za yule mtu ikakoma na eneo lote la vile vyoo likawa
kimya. Niliendelea kuyatega masikio yangu na kwa kweli sikuweza kuhisi kitu chochote
eneo lile. Baada ya muda mrefu wa kusubiri hatimaye hisia zikanijia kuwa nje ya ule
mlango wa choo changu kulikuwa na mtu aliyesimama.
Hali ile ikanipelekea nikatishe haraka kile nilichokuwa nikikifanya huku nikiudhika
sana na hali ile. Niligeuka taratibu na kutazama chini ya ule mlango sehemu kulipokuwa
na uwazi mdogo kati ya ule mlango na sakafu ya kile choo. Kupitia mwanga wa taa
iliyokuwa nje ya ile korido ya vile vyoo niliweza kukiona kivuli cha miguu ya mtu na
hapo koo likanikauka ghafla. Muda mfupi uliyofuata mara nikaanza kuona kitasa cha
ule mlango kikizungushwa taratibu na hapo nikajua kuwa sikuwa salama tena.
Nikiwa bado nafikiria kitu cha kufanya ule mlango wa kile choo ulifunguliwa kwa
kasi kisha mkono uliyoshika bastola ukatangulizwa mbele. Niliwahi kuudaka mkono
ule kisha nikaupigiza ukutani kwa nguvu zangu zote na hivyo kuifanya ile bastola
ianguke chini. Hata hivyo yule mtu alikuwa makini sana hivyo akatupa ngumi mbili
zenye kasi ya upepo. Niliwahi kujibanza pembeni hivyo pigo moja la ngumi lilinikosa
na kukata hewa bila majibu.
Pigo la pili lilipotupwa nilichelewa kidogo hivyo ngumi yake makini ikaitandika
vibaya shingo yangu na kunifanya nihisi kichefuchefu huku maumivu makali
yakisambaa mwilini mwangu na kunipelekea mfadhaiko wa aina yake. Halafu
nikapokea mapigo mawili ya ngumi kavu za tumboni zilizolikoroga vibaya tumbo
langu na kunifanya nianze kuhema ovyo. Nilikuwa nimejitahidi kuyadhibiti mapigo
yale bila mafanikio kwani yule mtu alikuwa fundi sana wa mapigano.
Pigo la teke alilolirusha mtu yule huku dhahiri akioneka kudhamiria kuzitawanya
kama siyo kuzipasua vibaya korodani zangu nikalipangulia chini kwa mikono yangu imara. Tukio lile likampelekea yule mtu apoteze mhimili na kuanza kupepesuka ovyo
lakini alikuwa mwepesi sana. Akapepesuka kidogo hadi pale alipopata mhimili wa
ukuta wa kile choo na bila kusubiri akarusha pigo jingine matata la ngumi ya chembe
ya moyo.
Mara hii nilikuwa mtulivu na makini hivyo nikaipangua ngumi ile kama mchezo
huku nikiisukumia kwenye koki ya bomba la maji la mle ndani na hapo nikasikia sauti
kali ya mvunjiko wa mfupa wa mkono wa yule mtu. Yule mtu akapiga yowe kali na
kubweka kama mbwa mwizi lakini hakukata tamaa mapema.
Pigo jingine la teke alilolirusha yule mtu niliwahi kuliona hivyo nikalikwepa kwa
kusogea kidogo pembeni na hapo pigo lile la teke likapita bila shabaha na kujipigiza
ukutani. Mguu wa yule mtu ukavunjika kwenye kifundo na kumpelekea yule mtu
apige yowe kali la aina yake.
Hata hivyo yule mtu alikuwa mkaidi hivyo kwa ule mkono wake mmoja mzima
akawahi kuikota ile bastola yake mle ndani sakafuni hata hivyo alichelewa kwani
ulikuwa ni kama mchezo wa paka na nyoka. Niliwahi kumshika miguu yule mtu na
kumvuta nyuma hivyo ile bastola akawa anaiona kwa mbele yake lakini hakuweza
kuifikia.
“Wewe ni nani na una shida gani na mimi?” nikamuuliza yule mtu huku nikiwa
nimemkwida shati lake mkononi. Yule mtu akaendelea kulalama kutokana na
maumivu makali ya majeraha yake. Alikuwa mwanaume mrefu na mweusi mwenye
mwili uliojengeka vyema. Alikuwa amevaa suruali nyeupe ya jeans na fulana nyekundu
na miguuni alikuwa amevaa buti za askari. Kijana wa makamo mwenye umri wa miaka
thelathini na kitu.
“Nakuuliza bwana wewe ni nani na una shida gani?”
Yule mtu hakunijibu badala yake akaendelea kugugumia maumivu na hapo
nikamchapa makofi mawili ya nguvu usoni kumuweka sawa.
“Nakuuliza wewe una shida gani na mimi mbona tunafuatana fuatana chooni
kama mainzi?” nilimuuliza tena yule mtu na nilipomchunguza vizuri nikagundua
kuwa alikuwa miongoni mwa wale watu wawili waliokuwa wakinitazama kule nyuma
ukumbini.
“Sikufuati wewe bwana” yule mtu akaongea kwa hofu huku akilalama kwa
maumivu.
“Kwani vyoo vyote humu ndani vina watu?” nilimuuliza huku nikizidi kumkwida.
“Hapana!”
“Sasa mbona huna msimamo wewe bwege na yule mwenzako yuko wapi?”
nikamuuliza kwa hasira
“Mwenzangu yupi?” yule mtu akaniuliza huku akinitazama kwa mshangao.
“Mwenzako uliyekuwanaye kule nyuma ya ukumbi”
“Mbona sikuelewi?”
“Hivi nyinyi mna shida gani na mimi?” nilimuuliza yule mtu na kumchapa kofi
jingine usoni na hapo akalalama kwa maumivu.
“Unanionea bure tu mimi sifahamu chochote” yule mtu akazidi kulalama lakini
alikuwa ni mtu mwenye hila kwani wakati akinisemesha kumbe alikuwa akiupeleka
haraka mkono wake nyuma kiunoni mwake ili kuichukua bastola yake nyingine ya
ziada na hapo mshipa wa huruma ukanikatika.
Nilikuwa kwenye nafasi nzuri hivyo lengo lake halikufanikiwa kwani haraka
niliwahi kukipigiza kichwa chake kwenye sinki la choo cha mle ndani. Kichwa chake
kikafumuka na ubongo wake ukaruka na kutapakaa kwenye marumaru za mle ndani.
Yule mtu akahangaika kidogo kabla ya kutulia huku roho yake ikiwa mbali na mwili.
Nilimaliza kumfanyia upekuzi yule mtu pasipo kupata kitu chochote cha maana
kwake hivyo nikanawa vizuri kwenye bomba la mle ndani na nilipomaliza nikarudi na
kumalizia haja yangu kwenye kile choo.
Sikutaka mtu yoyote anikute mle ndani hivyo mara tu nilipomaliza shida zangu
nikatoka na kuufunga ule mlango wa choo halafu kwa msaada wa kalamu niliyokuwa
nayo mfukoni nikaandika kwa maandishi makubwa juu ya mlango ule wa choo kuwa.
CHOO HIKI HAKITUMIKI.
Dakika chache zilizofuata nilikuwa mbali na choo kile huku taratibu sigara yangu
ikiteketea mdomoni.
Mara hii nilijikuta nikimkumbuka tena Milla Cash na wale wapambe wake wakiwa
ubavuni. Hata hivyo macho yangu bado yaliendelea na kazi ya kutathmini sura na
mienendo ya watu waliokuwa mle ndani.
Mambo yangu sasa yalitakiwa kwenda haraka kabla ya uwepo wa yule mtu kule
chooni haujashtukiwa. Niliendelea kutembea mle ndani huku nikikatisha kando ya ile
kaunta ya vinywaji kisha nikapita pembeni ya ule ukumbi wa casino kama mwenyeji.
Sikumuona mtu yeyote akinitazama au kunifuatilia hivyo nikaamini kuwa hali ilikuwa
shwari.
Nilipofika mwisho wa ule ukumbi nikashika uelekeo wa upande wa kulia na muda
siyo mrefu nikawa nimezifikia zile ngazi na kuanza kuzipanda nikielekea kule juu.
Wakati nikiendelea kuzipanda zile ngazi njiani nikapishana na mwanaume mmoja
mwarabu akishuka zile ngazi na mkoba mweusi mkononi. Niligeuka na kumtazama
yule mwarabu huku nikiwa nimevutiwa sana na ule mkoba wake mkononi.
Ule mkoba ulikuwa ukifanana na ile mikoba ya wale watu waliokuwa wakipanda
kule juu ghorofani muda mfupi wakati ule baada ya Milla Cash kufika.
Katika zile ngazi kulikuwa na kamera mbili zilizopandwa katika namna ya kunasa
taswira za watu wanaopanda na kushuka kwenye zile ngazi. Nilizitazama kamera zile
kwa hila hata hivyo nilifurahi kuwa nilikuwa nimevaa kofia yenye kuikinga vizuri sura
yangu.
Wakati nikiendelea kuzipanda zile ngazi mawazo fulani yalikuwa yakipita kichwani
mwangu. Bado nilikuwa nikimkumbuka yule mtu niliyepambana naye kule chooni
muda mfupi uliyopita. Nilikuwa na kila hakika kuwa yule mtu alikuwa amedhamiria
kuniua. Ama kwa tafsiri nyingine ni kuwa uwepo wangu mle ndani tayari ulikuwa
ukifahamika na baadhi ya watu. Kwa kweli nilishindwa kabisa kuelewa kitu kilichokuwa kikiendelea mle ndani.
Nilipomaliza kuzipanda zile ngazi nikawa nimetokezea mbele ya korido nyingine
ya ghorofa ya pili lakini mandhari yale hayakuwa kama ya kule chini nilipotoka.
Nilisimama kidogo pale juu huku nikiyachunguza mandhari yale na hapo nikagundua
kuwa kulikuwa na korido mbili. Korido moja ilikuwa upande wa kushoto na korido
nyingine ilikuwa upande wa kulia. Korido zile zilikuwa zimelizunguka eneo kubwa
la ukumbi mwingine wa pale juu uliyofunikwa wenye umbo kubwa mfano wa koni.
Niliutazama ukumbi ule wenye kiwambo cha kuzuia sauti ama Sound proof na
haraka nikatambua kuwa mle ndani kulikuwa na mambo makubwa zaidi ya kishetani
yaliyokuwa yakiendelea. Nilirudia tena kuitazama korido ile na hapo kitu fulani
kikaanza kujengeka kichwani mwangu.
Kulikuwa na milango mingi iliyokuwa ikitazamana na zile korido na hapo mawazo
fulani yakaanza kujengeka kichwani mwangu. Milango ile mingi ilikuwa ikitazamana
na zile korido mbili kuuzunguka ule ukumbi.
Juu ya milango ile kulikuwa na namba na hapo nikawa na hisia juu ya nini
kilichokuwa kikiendelea mle ndani. Nikashawishika kuisogelea ile milango lakini
kwa kuwa eneo lile lilikuwa likitazamana na zile ngazi niliona kuwa yeyote ambaye
angeniona eneo lile angeweza kunitilia mashaka hivyo niliamua kuifuata ile korido ya
upande wa kulia.
Niliendelea kutembea huku nikiitazama ile milango ya vile vyumba ambapo
kwa wakati huu niliigundua kuwa yote ilikuwa ikifanana kwa mwonekano. Wakati
nikiendelea na safari yangu taswira ya yule msichana Milla Cash ikawa ikiendelea
kuumbika taratibu kichwani mwangu. Tatizo ni kuwa sikuweza kufahamu kuwa Milla
Cash alikuwa ameingia katika chumba kipi miongoni mwa vyumba vile.
Wakati nilipokuwa nikiendelea na uchunguzi wangu ghafla mlango wa chumba
kilichokuwa kikifuatia mbele yangu ulifunguliwa kisha mwanaume mmoja mwarabu
alitoka nje ya chumba kile na kunipita pasipo kunipa salamu huku marashi yake makali
yakiitesa pua yangu.
Niligeuka na kumtazama Mwarabu yule na hapo nikagundua kuwa mkononi
alikuwa ameshika mfuko mweusi uliyofanana na ile mifuko ya wale watu wa awali.
Kwa kweli nilishangazwa sana na hali ile hata hvyo niliendelea kumtazama mwarabu
yule hadi pale alipopotea kwenye zile ngazi za kushukia kule chini nilipotoka kisha
nikayarudisha tena macho yangu kuutazama ule mlango wa kile chumba ambacho
muda mfupi uliyopita yule mwanaume mwarabu alikuwa ametoka mle ndani.
Hatimaye nikazitupa hatua zangu kwa utulivu nikiuendea ule mlango wa kile
chumba huku nikitazama huku na kule kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa
akinitazama. Nilipofika nikakishika kitasa cha ule mlango na kuusukuma taratibu. Ule
mlango haukuwa umefungwa hivyo ulifunguka taratibu bila pingamizi lolote na hapo
nikaingia mle ndani na kuufunga kwa nyuma.
Nikiwa sasa nimeingia mle ndani ya kile chumba niliweza kuinusa vizuri ile harufu
kali ya yale marashi ya yule mwarabu aliyetoka mle ndani muda mfupi uliyopita.
Nilipomaliza kuzipanda zile ngazi nikawa nimetokezea mbele ya korido nyingine
ya ghorofa ya pili lakini mandhari yale hayakuwa kama ya kule chini nilipotoka.
Nilisimama kidogo pale juu huku nikiyachunguza mandhari yale na hapo nikagundua
kuwa kulikuwa na korido mbili. Korido moja ilikuwa upande wa kushoto na korido
nyingine ilikuwa upande wa kulia. Korido zile zilikuwa zimelizunguka eneo kubwa
la ukumbi mwingine wa pale juu uliyofunikwa wenye umbo kubwa mfano wa koni.
Niliutazama ukumbi ule wenye kiwambo cha kuzuia sauti ama Sound proof na
haraka nikatambua kuwa mle ndani kulikuwa na mambo makubwa zaidi ya kishetani
yaliyokuwa yakiendelea. Nilirudia tena kuitazama korido ile na hapo kitu fulani
kikaanza kujengeka kichwani mwangu.
Kulikuwa na milango mingi iliyokuwa ikitazamana na zile korido na hapo mawazo
fulani yakaanza kujengeka kichwani mwangu. Milango ile mingi ilikuwa ikitazamana
na zile korido mbili kuuzunguka ule ukumbi.
Juu ya milango ile kulikuwa na namba na hapo nikawa na hisia juu ya nini
kilichokuwa kikiendelea mle ndani. Nikashawishika kuisogelea ile milango lakini
kwa kuwa eneo lile lilikuwa likitazamana na zile ngazi niliona kuwa yeyote ambaye
angeniona eneo lile angeweza kunitilia mashaka hivyo niliamua kuifuata ile korido ya
upande wa kulia.
Niliendelea kutembea huku nikiitazama ile milango ya vile vyumba ambapo
kwa wakati huu niliigundua kuwa yote ilikuwa ikifanana kwa mwonekano. Wakati
nikiendelea na safari yangu taswira ya yule msichana Milla Cash ikawa ikiendelea
kuumbika taratibu kichwani mwangu. Tatizo ni kuwa sikuweza kufahamu kuwa Milla
Cash alikuwa ameingia katika chumba kipi miongoni mwa vyumba vile.
Wakati nilipokuwa nikiendelea na uchunguzi wangu ghafla mlango wa chumba
kilichokuwa kikifuatia mbele yangu ulifunguliwa kisha mwanaume mmoja mwarabu
alitoka nje ya chumba kile na kunipita pasipo kunipa salamu huku marashi yake makali
yakiitesa pua yangu.
Niligeuka na kumtazama Mwarabu yule na hapo nikagundua kuwa mkononi
alikuwa ameshika mfuko mweusi uliyofanana na ile mifuko ya wale watu wa awali.
Kwa kweli nilishangazwa sana na hali ile hata hvyo niliendelea kumtazama mwarabu
yule hadi pale alipopotea kwenye zile ngazi za kushukia kule chini nilipotoka kisha
nikayarudisha tena macho yangu kuutazama ule mlango wa kile chumba ambacho
muda mfupi uliyopita yule mwanaume mwarabu alikuwa ametoka mle ndani.
Hatimaye nikazitupa hatua zangu kwa utulivu nikiuendea ule mlango wa kile
chumba huku nikitazama huku na kule kama kungekuwa na mtu yeyote aliyekuwa
akinitazama. Nilipofika nikakishika kitasa cha ule mlango na kuusukuma taratibu. Ule
mlango haukuwa umefungwa hivyo ulifunguka taratibu bila pingamizi lolote na hapo
nikaingia mle ndani na kuufunga kwa nyuma.
Nikiwa sasa nimeingia mle ndani ya kile chumba niliweza kuinusa vizuri ile harufu
kali ya yale marashi ya yule mwarabu aliyetoka mle ndani muda mfupi uliyopita. Hata hivyo harufu ile ilikuwa imechanganyikana na harufu ya moshi wa sigara za kifahari
na marashi mengine ya kike. Hisia zikaniambia kuwa huwenda mle ndani kulikuwa na
mtu mwingine ambaye sikuweza kumfahamu mapema.
Nilisimama nikikichunguza chumba kile na mbele yangu nikaliona pazia jepesi la
kamba nyembamba zilizotungwa simbi za baharini. Kupitia uwazi mdogo uliyokuwa
baina ya zile kamba niliweza kuona mle ndani ya lile pazia.
Nyuma ya pazia lile kulikuwa na chumba kikubwa chenye makochi makubwa ya
sofa za kisasa kilichokuwa kikimulikwa kwa mwanga hafifu wa taa za rangi tofauti za
kupendeza na sehemu fulani katika chumba kile sauti ya muziki laini ilikuwa ikisikika.
Nilizitupa hatua zangu taratibu kulisogelea lile pazia na nilipolifikia nikalisogeza
pembeni kuchungulia mle ndani na hapo nikaiona taswira kamili ya mandhari ya kile
chumba.
Mbali na yale makochi ya sofa niliyoyaona pale awali mle ndani pia kulikuwa na
meza pana ya kioo na juu ya meza ile kulikuwa na bilauri mbili na chupa nne za
kinywaji cha kilevi aina ya Russian Standard. Chupa tatu miongoni mwa zile chupa
nne zilikuwa tupu. Pembeni ya chupa zile kulikuwa na kibeseni kidogo cha majivu ya
sigara chenye umbo mfano wa kifaranga cha bata na ndani yake kulikuwa na kipisi
kidogo cha sigara kilichokuwa kikiteketea.
Niliyatembeza macho yangu mle ndani na sehemu fulani kwenye kona ya chumba
kile kulikuwa na simu ya mezani juu ya meza ndogo yenye ua jekundu. Upande
wa kulia wa chumba kile kulikuwa na runinga kubwa ukutani na katika runinga ile
kulikuwa na filamu ya ngono iliyokuwa ikioneshwa lakini hapakuwa na mtu kwenye
kile chumba ambacho sasa nilianza kukifananisha na sebule ya aina yake. Pembeni
ya seti ile ya runinga kulikuwa na jokofu jembamba na refu lenye kuta za vioo zenye
kumuwezesha mtu yeyote kuona mle ndani ambapo kulikuwa na lukuki ya chupa za
vinywaji.
Chumba chote kilikuwa kimefunikwa kwa zulia zuri la manyoya laini lililodariziwa
kwa maua mazuri ya rangi tofauti za kuvutia. Nilisimama nikiyatazama mandhari yale
huku nikiendelea kushangazwa na uwekezaji ule wa aina yake.
Upande wa kushoto wa chumba kile kulikuwa na mlango. Mlango ule sasa ulikuwa
wazi ukitenganishwa na chumba kile cha sebule kwa pazia jepesi linalomwezesha mtu
yoyote kuona mle ndani ya kile chumba kwa shida.
Adha ya hali ya joto kali la jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepelekwa likizo na
kiyoyozi makini kilichokuwa kikisambaza hewa ya baridi nyepesi isiyokinaisha.
Nilizitupa hatua zangu taratibu kukiendea kile chumba kilichokuwa upande wa
kushoto na mara hii nilijikuta nikivutiwa na kitu.
Katika kochi moja lililokuwa pale sebuleni nililiona vazi la kike aina ya sidiria
ya rangi ya pinki. Nilipoendelea kusogea mbele kidogo chini ya sakafuni usawa wa
kuelekea kwenye kile chumba nikaiona chupi ya bikini ya rangi nyekundu. Hatimaye
nikausogelea ule mlango na kulisogeza lile pazia nikichungulia mle ndani.
Msichana mzuri alikuwa amelala ndani ya beseni kubwa la kuogea huku baadhi ya sehemu za mwili wake kama magoti na mikono zikionekana bila kificho. Msichana
yule mzuri alikuwa amelala mle ndani ya lile beseni huku sehemu zake nyingine za
mwili wake zikishindwa kuonekana vizuri kutokana na mapovu ya sabuni nzuri ya
kunukia yaliyokuwa yametanda juu ya maji yale.
Kifua chake laini chenye mzigo wa matiti yenye ukubwa wa wastani yaliongeza
chachu nyingine katika uzuri wake. Msichana yule alikuwa amejilaza chali akitazama
juu huku kichwa chake chenye nywele ndefu,nyeusi na laini akiwa amekiegemeza
sehemu ya mbele kwenye ukingo wa lile beseni la kuogea. Mkono wake mmoja alikuwa
ameukunja na kuuegemeza upande wa kushoto kwenye lile beseni huku kiganja cha
mkono huo kikipotelea ndani ya lile povu la sabuni. Mkono wake mwingine ulikuwa
umeibana sigara katika pacha ya vidole vyake huku mkono huo ukibembea taratibu
nje ya beseni lile.
Mwanzoni nilidhani kuwa huwenda msichana yule alikuwa mfu kwa namna
alivyokuwa ameyatuliza macho yake kutazama juu kwenye dari ya chumba kile lakini
kitendo cha kumuona akiupeleka tena mkono wake mdomoni kuivuta ile sigara
kikanihakikishia kuwa msichana yule alikuwa hai na hapo nikatabasamu kidogo.
“Naomba unaniruhusu niingie mrembo” nilivunja ukimya na hali ile ikampelekea
msichana yule mrembo ashtuke na kugeuka akinitazama pale nilipokuwa nimesimama
huku akiwa ameshikwa na mshangao. Msichana yule aliendelea kunitazama kwa
mshangao halafu taratibu akalegeza uso wake na hapo tabasamu la kibiashara
likaumbika usoni mwake.
“Ondoa shaka unakaribishwa” msichana yule akaniambia huku akifanya jitihada
kidogo za kukaa vizuri kwenye lile beseni na hapo nikapata nafasi nzuri ya kuziona
chuchu zake imara zilizoupumbaza kwa muda mtima wangu.
Nilipoingia mle ndani nikaweza kuona vizuri mandhari ya kile chumba. Kilikuwa
chumba kipana chenye seti nyingine ya runinga pana ukutani na makochi ya sofa ya
ngozi nyeusi. Upande wa kulia kulikuwa na kioo kikubwa cha kujitazama na chini ya
kioo kile kulikuwa na chupa za mafuta mazuri ya kunukia pamoja na sabuni tofauti za
kuogea huku pembeni yake kukiwa kumening’inizwa mataulo mawili meupe. Sakafu
ya chumba kile kilichofaa kifananishwa na bafu la kisasa ilitengenezwa kwa marumaru
zenye rangi tofauti za kuvutia.
Niliyatembeza kwa utulivu macho yangu mle ndani na upande wa kushoto wa
chumba kile kulikuwa na sehemu ya kukaa iliyokuwa imetengenezwa kwa foronya
laini. Ile runinga ya kile chumba ilikuwa ikionesha filamu ya ngono kama ya kule
sebuleni na hapo nikajua runinga zote mbili za mle ndani zilikuwa zimeungwanishwa
na king’amuzi kimoja.
“Ahsante!” niliitikia kwa utulivu kisha taratibu nikapita na kwenda kukaa kwenye
ile sehemu yenye foronya laini huku nikiendelea kuyapeleleza mandhari yale.
“Yule rafiki yako ameenda wapi?” nilimuuliza yule msichana huku akiendelea
kunitazama.
“Rafiki yangu yupi?” yule msichana akaniuliza kwa mshangao.
“Mwarabu aliyetoka humu ndani muda mfupi uliopita!”
“Oh! sahau kuhusu yeye,huduma yake tayari imekwisha” msichana yule aliongea
kwa bashasha zote za kirafiki huku akiumba tabasamu usoni na nilipomchunguza
nikatambua alikuwa amelewa kidogo.
“Biashara inakwendaje?” nilimuuliza msichana yule huku nikimtazama.
“Dola mia moja kwa muda wa saa moja na huduma yangu utaifurahia” yule
msichana akaongea huku akiangua kicheko hafifu na hapo nikagundua kuwa alikuwa
akijitahidi kutengeneza mazingira ya kirafiki kama maadili ya kazi yake yalivyokuwa
yakimtaka. Kazi ya kuuza mwili wake.
“Haipungui?” nilimuuliza huku nikitabasamu hata hivyo umri wake mdogo
ukapeleka simanzi moyoni mwangu.
“Bei zetu ni nafuu sana ukifananisha na maeneo mengine hapa jijini Dar es
Salaam” msichana yule akaongea kwa kujiamini baada ya kuitoa sigara yake mdomoni
na nilipomchunguza nikagundua umri wake haukuwa zaidi ya miaka kumi na sita.
“Hakuna mkopo?” nilimuuliza yule msichana huku nikitumbukiza utani.
“Kama unataka mkopo nenda Pride au Faidika huko utapewa kwa masharti
nafuu” akaniambia kwa hasira huku akihisi kuwa nilikuwa nikitaka kuleta dharau
na kazi yake. Nilimtazama msichana yule huku nikimuonea huruma kwa namna
alivyokuwa mwathirika wa biashara ile ya ngono huku akiwa na umri mdogo ingawa
yeye mwenyewe hakuonekana kujali kitu.
“Dola mia moja ni pesa ndogo sana kwa mwanaume anayejua nini maana ya
starehe” yule msichana akaniambia huku taratibu akiipeleka mdomoni ile sigara
iliyokuwa mkononi mwake na kuanza kuivuta pasipo kunitazama. Alipoitoa akageuka
na kutabasamu huku akiniambia
“Napenda sana wanaume weusi wenye nguvu na warefu kama wewe” msichana
yule mdogo akaongea na hapo nikaanza kuilaani dunia kwa namna ilivyoharibika
namna ile. Hata hivyo nilitabasamu kidogo kuununua urafiki.
“Kwa nini?” nilimuuliza huku nikitabasamu.
“Huwa wananiacha nikiwa nimeridhika” yule msichana akaongea kwa sauti ya
mahaba.
“Jina langu naitwa Stephen Masika!” nilivunja tena ukimya.
“Mimi naitwa Zera”
“Jina lako tamu sana masikioni mwangu” niliongea kwa utulivu huku nikimtazama
msichana yule.
“Mh! kila mwanamume anaongea hivyo utasema mmeambizana” yule msichana
akaongea hukua akiipeleka sigara yake mdomoni na kuivuta taratibu.
“Unatumia kilevi gani?” hatimaye akaniuliza baada yakuitoa ile sigara mdomoni.
“Oh! usijali mrembo kilevi kwa sasa hapana!”
“Kwa nini?” akaniuliza kwa mshangao kidogo.
“Nina dozi ya Malaria” nilimwambia huku nikitabasamu na hapo akazidi kunikata
jicho kwa mshangao.
“Sasa kama unaumwa malaria unafanya nini humu ndani?. Si ungeenda hospitali
ya Ocean Road,Muhimbili au TMJ badala ya kuja hapa?”
“Kwani wagonjwa hatuna haki ya kununua huduma hii?” nilimuuliza kwa utulivu
huku nikimtathmini vizuri msichana yule.
“Nenda kauguze ugonjwa kwanza usije ukanifia kitandani” yule msichana
akaongea kwa dhihaka na hapo nikaingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda cha
shilingi laki moja na kumrushia pale kwenye lile beseni la kuogea. Yule msichana
ambaye sasa nilimfahamu kwa jina la Zera akakidaka kibunda kile cha pesa kama
mbwa mwenye njaa adakavyo mfupa aliorushiwa kisha akaanza kuzihesabu zile noti
chapuchapu kwa vidole vyake virefu kama mashine ya ATM huku ile sigara yake
akiwa ameibana kwenye pembe ya mdomo wake. Alipomaliza kuzihesabu zile noti
akageuka na kunitazama kwa shauku kama atarajiaye maelekezo juu ya zile pesa.
Alipoona kuwa nakawia kuongea akavunja ukimya
“Nimesema dola mia moja ya kimarekani siyo shilingi laki moja ya kitanzania?”
Zera akaongea huku akinitazama kwa udadisi.
“Vuta subira mrembo haraka ya nini?” nilimwambia yule msichana hata hivyo
hakusema neno badala yake nilimuona akianza kutoka kwenye lile beseni la kuogea
na mara hii mapigo yangu ya moyo yakasimama huku akili yangu ikishindwa kufanya
kazi kwa sekunde kadhaa.
Uzuri wake ama kwa hakika ulikuwa umefanikiwa kuzichukua mateka hisia zangu.
Pamoja na kuwa niliwahi kukutana na wasichana wengi warembo na wazuri katika
harakati zangu lakini Zera alikuwa ni matokeo ya kazi bora kabisa ya mfinyanzi.
Alikuwa mrefu lakini nilimzidi kwa sentimita chache za hisabati. Nywele zake
ndefu laini na nyeusi ziliteleza taratibu kutoka kwenye yale maji ya povu la sabuni
kama samaki aina ya kambare kwenye tope jepesi la udongo mfinyanzi. Niliendelea
kumkodolea macho Zera na hapo nikamuona akizikamua maji zile nywele zake kwa
viganja vya mikono yake katika namna ya kuzichuja maji kistaarabu.
Macho yake makubwa meupe na legevu yalizungumza kuwa alikuwa tayari kwa
kazi. Pua yake ndefu na nyembamba na midomo yake yenye kingo laini na pana
viliutanabaisha vizuri uzuri wa sura yake nyembamba kiasi yenye mvuto wa kipekee
kuwahi kutokea duniani.
Matiti yake yaliyosimama wima yenye chuchu nyeusi katikati yalitikisika kidogo
wakati alipokuwa akiutua mguu wake wenye kikuku sakafuni mara baada ya kutoka
kwenye lile beseni la kuogea huku akiwa uchi bila ya nguo yoyote ya kujisitiri maungoni
mwake.
Zera aliposimama mwili wangu ukashikwa na ganzi na akili yangu ikayumba na
kupoteza uelekeo kama bondia aliyeshambuliwa kwa pigo la konde la nguvu kichwani
kutoka kwa mpinzani wake. Kiuno chake chembamba chenye aina tofauti za shanga
kilikuwa kimechongwa vizuri kuushikilia mzingo wa makalio yake usiokinaisha
kuutazama. Kitovuni alikuwa ametoga kipini kimoja cha dhahabu. Niliendelea
kumkodolea macho na hapo nikayaona yale mapovu ya sabuni nzuri ya kunukia kutoka kwenye lile beseni la kuogea mle ndani yakichuruzika taratibu na kutengeneza
ziada nyingine katika uzuri wake wa kustaajabisha.
Mikono yake mirefu,laini na yenye kucha ndefu zenye rangi ya kuvutia aliipeleka
kiunoni mwake na kujishikashika kisha akajitikisha kidogo katika namna ya kuzidi
kuzitaabisha vibaya hisia zangu ambazo tayari zilikuwa mahututi.
Zera alipoanza kutembea taratibu akinifuata pale nilipokuwa nimeketi mitetemo
ya mapaja yake laini na mang’avu yenye misuli imara yakaupelekea ule mzigo wake wa
makalio makubwa na laini uanze kuweweseka kama mshumaa unaopulizwa na upepo
mkali wa baharini.
Taswira ile mbele yangu ikanipelekea nianze kuhisi kuwa nilikuwa nimepotea njia
na hatimaye kujitumbukiza kwenye kiumbe kile kilichohitimu vizuri katika kucheza
na hisia za wanaume.
Zera alitembea taratibu na hatimaye kuketi pembeni yangu. Nilipogeuka
kumtazama mkono wake mmoja tayari ulikuwa umepenya ndani ya fulana yangu na
kuanza kufanya ziara ya taratibu tumboni na kifuani mwangu. Tukio lile likanifanya
nijihisi kama niliyepigwa na shoti kali ya umeme. Muda mfupi badaye nikaanza kuhisi
kuwa endepo ningeendelea kuiruhusu hali ile basi mawasiliano ya ubongo na kazi za
viungo vyangu mwilini yangekatika. Hivyo nikajitahidi kujinasua kwa jitihada zangu
zote.
“Subiri kidogo mpenzi” nilinong’ona taratibu kando ya sikio lake hata hivyo Zera
hakutaka kunisikia badala yake akaendelea kunipapasa maungoni mwangu.
“Mpenzi…!” nilimuita huku nikifanya jitihada za kujinasua mikononi mwake bila
mafanikio. Kufumba na kufumbua ulimi wake laini ulikuwa kwenye tundu la sikio
langu huku ukisababisha kiwango kikubwa cha hisia kuwahi kunitokoea mwilini.
Sikutaka kuendelea kuiruhusu zaidi hali ile hivyo hatimaye nikaamua kutumia nguvu
katika kujinasua mikononi mwake. Jitihada zangu zikafua dafu kwani hatimaye
nikafanikiwa kumshinda shetani na vishawishi vyake.
Zera akaondoa mikono yake haraka maungoni mwangu na kunikata jicho lenye
chuki na hasira halafu akanisukuma kando kiasi kwamba kama nisingekuwa makini
ningeweza kupiga mwereka mbaya.
“Wewe ni mwandishi wa habari?” hatimaye Zera akaniuliza kwa hasira.
“Habari zipi mpya huyo mwandishi wa habari anaweza kuzitafuta humu ndani
bibie?” nilimuuliza Zera huku nikijitahidi kuurudisha urafiki wetu ulionza kuingia
nyufa.
“Sasa umefuata nini humu ndani?” Zera akaniuliza kwa jazba.
“Tafadhali! hebu keti kwanza unisikilize mpenzi” nilimwambia Zera ambaye
wakati huu alikuwa tayari amesimama kwa hasira huku akinikata jicho.
“Sitokurudishia pesa zako” hatimaye Zera akavunja ukimya baada ya kitambo
kirefu cha ukimya kupita mle ndani huku tukitazamana.
“Ondoa shaka!” nilimwambia na hapo Zera akanitazama kwa mshangao na kuketi
taratibu kando yangu.
“Zungumza shida yako” hatimaye akaniuliza kwa sauti tulivu ya upole.
“Nitachukua dakika chache za muda wako” nilimwambia huku nikigeuka na
kumtaza wakati huo mkono wangu ukifanya ziara fupi kwenye sehemu za mapaja
yake.
“Zungumza!” akaniambia huku akiendelea kunitazama na hapo nikaichukua
ile sigara mkononi mwake na kuivuta mapafu kadhaa kisha nikamrudishia huku
nikiupuliza moshi taratibu katika namna ya kuipa utulivu akili yangu kisha nikavunja
ukimya
“Nahitaji kuonana na Milla Cash bila shaka unaweza kunisaidia kumpata”
nilimwambia Zera huku nikimtazama usoni na nilichokiona machoni mwake ni
mshangao wa hali ya juu.
“Hicho ndiyo kilichokuleta humu ndani?” hatimaye Zera akaniuliza kwa utulivu
huku akiutikisa mguu wake uliokuwa juu ya mwingine huku macho yake yakitazama
mbali na eneo lile kama mtu anayetafakari kitu.
“Nahitaji msaada wako” nilimwambia kwa utulivu.
“Sasa utamuuliziaje Milla Cash wakati upo na mimi. Huoni kuwa unanivunjia
heshima?” Zera aliongea kwa hasira kidogo lakini sauti yake bado ilikuwa na utulivu na
hapo nikacheka moyoni huku nikijiuliza kahaba kama yule ni heshima gani aliyokuwa
akiizungumzia.
“Sina maana hiyo mpenzi” nilimwambia kwa utulivu.
“Unadhani Milla Cash ni msichana mzuri na mrembo zaidi yangu?” Zera akaniuliza
na swali lake likanifanya nifahamu kuwa alikuwa akihisi wivu kwa kumuulizia Milla
Cash na siyo yeye na hapo nikatabasamu kidogo
“Ungekuwa hujathubutu kuzigaragaza vibaya hisia zangu huwenda ningekubaliana
na maneno yako” nilimwambia huku nikiangua kicheko hafifu cha kirafiki.
Zera akatabasamu kidogo huku akiipeleka sigara yake mdomoni. Nilipomtazama
usoni nikagundua kuwa maneno yangu yalikuwa yameukosha vizuri moyo wake.
Nijuavyo mimi ni kuwa ukitaka mwanamke akusikilize basi anza kwa kumsifia juu ya
uzuri wake lakini Zera alistahili sifa.
“Nina shida naye binafsi”hatimaye niliongea kwa utulivu
“Shida gani?”
“Binafsi”
“Sasa si ungemuulizia kule mapokezi badala ya kuja kwangu?”
“Nilihisi kuwa huwenda nisingepata ushirikiano wa kutosha” nilimwambia Zera
huku nikimtazama usoni.
“Wewe ni Njagu?” Zera aliniuliza kwa utulivu huku akigeuka na kunitazama na
hapo nikajua kuwa alitaka kufahamu kama mimi nilikuwa askari polisi au lah!
“Kwanini unaniuliza hivyo?” nilimuuliza kwa udadisi.
“Unaonekana kama polisi na sisi humu ndani polisi hatuwataki” maneno ya Zera
yakawa yamenivuta na hapo nikageuka na kumtazama kwa makini.
“Mimi siyo polisi lakini kwa nini hamuwapendi polisi na wakati wao ndiyo wanaolinda usalama wenu?” nilimuuliza Zera na hapo nikamuona akiupisha utulivu
kichwani mwake. Kitendo kile cha kuchelewa kunijibu kikanifanya nihisi kuwa
alikuwa akijipanga namna ya kukwepa kunieleza ukweli wa jambo fulani la mle ndani
ambalo mimi sikulifahamu.
“Polisi huwa wanatusumbua mara kwa mara wakidai biashara yetu ni kinyume na
sheria za nchi na wakati baadhi yao ni wateja wetu wa kuaminika”
Nilimsikiliza Zera pasipo kutia neno lolote badala yake nikatabasamu kidogo huku
nikifahamu fika kuwa lile halikuwa jibu sahihi la swali nililomuuliza huku mashaka
juu ya kilichokuwa kikiendelea ndani ya casino ile yakizidi kuniingia. Nilitulia kidogo
nikiikumbuka ile mifuko myeusi niliyowaona nayo wale watu mle ndani ya casino na
hapo akili yangu ikapoteza kabisa utulivu.
“Milla Cash yupo chumba namba ngapi humu ndani?” nilimtupia swali Zera
nikinuia kumrudisha kwenye msingi wa maongezi yetu. Zera aligeuka tena na
kunitazama kisha akaongea kwa utulivu baada ya kuitoa sigara mdomoni.
“Hakuna mtu yeyote miongoni mwetu anayefahamu. Humu ndani kuna idadi ya
vyumba vipatavyo sitini na nane na kila mmoja ana chumba chake kama unionavyo
mimi humu ndani na mbaya zaidi wengine hatufahamiani”
“Kwa nini msifahamiane?” nilimuuliza Zera kwa udadisi.
“Huwa tunaingia humu ndani kwa zamu. Kuna wanaoingia asubuhi saa mbili
asubuhi na kutoka saa mbili usiku na tupo wale tunaoingia saa mbili usiku na kutoka
saa mbili asubuhi ya siku inayofuata. Hivyo katika mazingira kama hayo unaweza
kuona mwenyewe kuwa ni kwa nini inakuwa vigumu kufahamiana miongoni mwetu”
Zera aliongea huku akiipeleka sigara yake mdomoni na hapo nikageuka na kumtazama
tena kwa udadisi. Kwa mara nyingine tena nafsi yangu ikajikuta ikiridhika kuwa Zera
alikuwa miongoni mwa wasichana wachache wazuri sana kawahi kuonekana kwenye
sayari hii. Niliupisha tena utulivu kichwani mwangu huku nikianza kuhisi ugumu wa
kazi iliyokuwa mbele yangu.
Wakati nikizama katika tafakuri ile mawazo juu ya yule mtu aliyenivamia kule
chooni yakaanza kuchipua upya katika fikra zangu huku nikijiuliza kuwa kwanini mtu
yule alitaka kuniua. Ina maana kuna watu waliokuwa wakifahamu sababu ya uwepo
wangu mle ndani?. Watu hao walifahamu vipi na nani aliyewaambia?. Nikaendelea
kujiuliza bila kupata majibu.
Nikajikuta nikizikumbuka pia sheria za casino ile kwenye kile kitabu kidogo
nilichopewa na yule binti asubuhi ile. Mojawapo ya sheria zile ni kuwa hakuna mtu
aliyekuwa akiruhusiwa kuingia na silaha mle ndani. Swali likabaki kuwa yule mtu
aliyenishambulia kule chooni aliwezaje kuingia na bastola humu ndani ya casino?.
Niliendelea kujiuliza bila kupata majibu huku mbele yangu nikihisi bado kulikuwa na
kiza kinene katika kuyapatia uvumbuzi maswali yangu.
Niliuinua mkono wangu na kuitazama saa yangu ya mkononi na hapo nikaridhika
na mwenendo wa majira yake. Baada ya muda mfupi ile maiti ya yule mtu kule chooni
ingeshtukiwa na sikutaka suala hilo litokee huku mimi nikiwa bado nipo mle ndani ya casino. Hivyo nikageuka kumtazama Zera kwa tabasamu langu la kichokozi.
“Wasichana wote wa humu ndani wanaofanya kazi kama yako huwekewa ulinzi
kama ilivyo kwa Milla Cash?” nilimuuliza Zera huku nikimtazama machoni. Zera
akanitazama kama anayefikiria jambo fulani na alipoitoa sigara mdomoni na kuupuliza
moshi pembeni akaongea kwa utulivu pasipo kunitazama.
“Hapana!”
“Wewe huwa unafikaje hapa casino?”
“Huwa tunapitiwa na basi dogo la hii casino kutoka majumbani mwetu tunapoishi”
Jibu la Zera likanifanya nimkumbuke Milla Cash na lile gari jeusi linalomleta
casino nyakati za usiku aina ya Texas Laghorn Tailgate Van na hapo hoja fulani ikaanza
kujengeka kichwani huku nikijiuliza ni kwa nini yeye peke yake ndiye aliyekuwa
akiletwa na gari lile pale casino. Bado jibu sikulipata hivyo nikayaacha mawazo yangu
yakielea hewani pasipo kupata mhimili mzuri wa hoja.
Nilipomtazama Zera pale pembeni yangu nikahisi kuwa huwenda alikuwa
akijiuliza maswali kadhaa juu ya uwepo wangu mle ndani.
“Unamuhitaji Milla Cash?” hatimaye Zera akaniuliza kwa utulivu huku macho
yake yakizitazama kuta za kile chumba.
“Ndiyo! nitafurahi sana endapo utanisaidia kuonana naye” nilimwambia Zera kwa
utulivu.
“Sifahamu mahali anapoishi hapa jijini Dar es Salaam hata hivyo bado ninaweza
kukusaidia mahali utakapoweza kuonana naye ingawa utalazimika kuwa na subira
kidogo” Zera alimaliza kuongea kisha akaipeleka sigara yake mdomoni. Niligeuka na
kumtazama Zera huku moyo wangu ukiwa umeanza kupata matumaini.
“Kweli?” nilimuuliza Zera kwa kutaka kuhakikisha maneno yake.
“Nakuahidi ondoa shaka kaka hata hivyo itabidi unilipe kwani ni kazi ya hatari“
Zera akaongea kwa msisitizo.
“Hatari iko wapi?” nilimuuliza Zera kwa shauku.
“Siwezi kukueleza chochote ila utakapofanikiwa kuonana na Milla Cash utamuuliza
swali hilo” Zera akaniambia kwa utulivu huku akionekana kutokuwa tayari kunieleza
chochote juu ya hatari hiyo nami sikutaka kumlazimisha.
“Utanitoza pesa kiasi gani?” hatimaye nikamuuliza
“Shilingi laki mbili” Zera akatamka haraka kama aliyekwisha kupanga kiwango
kile cha pesa hapo kabla.
“Usijali fanya kazi yangu pesa yako nitakulipa. Unadhani hadi lini utakuwa
umeikamilisha?” nilimuuliza Zera na baada ya kufikiria kidogo akanijibu.
“Mpaka kesho jioni kabla ya kuja hapa huwenda kazi yako tayari nikawa
nimeikamilisha”
“Nitafurahi sana” niliongea huku nikiingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda
kingine cha pesa zenye thamani ya shilingi laki moja kisha nikampa Zera.
“Chukua pesa hii kama malipo ya awali ya kazi yangu” nikamwambia.
“Wala usihofu kazi yako nitaifanya” Zera akaniambia huku akizihesabu zile noti na alipomaliza akageuka na kunitazama
“Wapi tutakutana?” hatimaye akaniuliza.
“Hapa hapa kesho usiku muda na wakati kama huu” nilimwambia huku nikiumba
tabasamu.
“Hapana!” Zera akakataa na kunikazia macho
“Vipi kutakuwa na shida yoyote?” nilimuuliza Zera kwa mshangao.
“Hii ni sehemu ya kazi na kazi yako haihusiani na hapa” Zera akaniambia kwa
utulivu huku akinikata jicho la kunionya juu ya kuleta mazoea na kazi yake. Ukimya
ukapita kidogo huku nikiupisha utulivu kichwani mwangu kisha nikamuuliza tena
Zera.
“Mmiliki wa hii casino ni nani?”
Swali langu bila shaka lilimshangaza sana Zera na hapo akageuka na kunitazama
kabla ya kuangua kicheko cha kikahaba.
“Vipi unataka kuinunua?”
“Hapana! nilipenda tu kufahamu” nilimwambia Zera kwa utulivu huku
nikitabasamu.
“Hakuna anayemfahamu mmiliki wa casino hii kaka” Zera akaniambia huku
akiendelea kucheka na nilipoyatafakari maneno yake nikagundua kuwa alikuwa
akizungumza ukweli.
“Kwa hiyo tutakutana wapi?” Zera alipomaliza kucheka akaniuliza kwa utulivu.
Nilitulia kidogo nikifikiria juu ya sehemu ya kukutana halafu nilipokuwa mbioni kutoa
jibu ghafla nikapata wazo na hapo nikaichukua wallet yangu kutoka kwenye mfuko wa
suruali yangu na kuifungua. Nikatoa kadi ndogo ya biashara ama business card yenye
kila kitu feki kama;jina la kampuni,tovuti,barua pepe,jengo na mtaa wa kampuni hiyo
inapopatikana pamoja na nukushi isipokuwa namba ya simu tu ambayo ilikuwa mpya
kabisa ambapo nilimpa Zera.
“Utanipigia simu pale utakapokuwa umekamilisha kazi yangu” nilimwambia
Zera na hapo akaipokea ile kadi na kuitazama kwa makini huku wasifu wangu batili
wa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kukata na kusafisha madini ukiwa umeanza
kumzuzua. Zera alirudia kusoma wasifu wangu kwenye ile kadi huku akinitazama.
“Unaishi wapi hapa jijini Dar es Salaam?” nilimuuliza Zera.
“Naishi eneo la Kinondoni B mtaa wa Ukutavuka. Ukifika eneo la Biafra kituo cha
Kanisani unaingia upande wa kushoto ukiifuata barabara ya mtaa wa Bolingonanga halafu
mbele kidogo upande wa kushoto unaingia barabara ya mtaa wa Isere. Hutosafiri
sana na barabara ya mtaa huo mbele kidogo utakutana na barabara nyingine ya lami
inayoingia upande wa kulia kwako. Hiyo ndiyo barabara ya mtaa wa Ukutavuka.
Huwezi kupotea kwani kuna kibao cha barabara kinachoelekeza jina la mtaa huo.
Ukifika kwenye huo mtaa niulizie kwa jina la Zera utanipata kwani kila mtu wa mtaa
huo ananifahamu.
“Unaishi nyumba namba ngapi ya mtaa huo?” nilimkatisha Zera.
“Naishi nyumba namba 12 ina geti jekundu kwa mbele na ina tazamana na duka kubwa la madawa lenye jina la MM Pharmacy”
Mojawapo ya kigezo kilichotumika kunitunuku nishani ya juu ya masuala ya
upelelezi ni wepesi wa akili yangu katika kunasa na kuhifadhi taarifa za namna yoyote
kwa muda mrefu. Hivyo maelezo ya Zera nilikuwa nimeyanasa vyema kichwani.
Niligeuka na kumtazama Zera huku nikiyapapasa mapaja yake kisha nikatazama
muda kwenye saa yangu ya mkononi. Sikuwa na kitu kingine cha kufanya mle ndani
hivyo nikawa nimeamua kuondoka lakini wakati nikiwa kwenye hali ile mara simu
ya mezani iliyokuwa kule kwenye kile chumba cha awali ikaanza kuita. Mwito wa
simu ile ukamshuta Zera na hapo akageuka na kunitazama kwa mashaka kabla ya
kusimama haraka na kuelekea kule kwenye kile chumba kuipokea ile simu. Wasiwasi
niliouona machoni mwa Zera ukanisukuma na mimi kusimama na kumfuata Zera
kule kwenye kile chumba. Hivyo wakati Zera akiipokea ile simu mimi nilikuwa kando
yake nikimsikiliza.
“Haloo!” sauti ya upande wa pili iliita.
“Haloo nakusikia zungumza” Zera akaongea kwa utulivu huku akinitazama.
“Bila shaka naongea na chumba namba 26,sivyo?” ile sauti ya upande wa pili
iliuliza na niliweza kuihisi sauti ile kuwa ilikuwa ya kiume.
“Ndiyo chumba namba 26 hapa zungumza nakusikia” Zera akasisitiza.
“Kuna mwanaume yoyote chumbani kwako?” ile sauti ya upande wa pili iliuza tena
na niliweza kuisikia kwa mbali kutoka pale Zera aliposimama. Swali lile likamfanya
Zera ageuke na kunitazama kwa mashaka lakini niliwahi kumuonya kwa kumfanyia
ishara ya kukataa. Zera alikuwa mwepesi kunielewa.
“Hakuna mtu yoyote” hatimaye Zera akaongea kwa utulivu kwenye ile simu
“Una hakika?” ile sauti ya upande wa pili wa simu ikauliza kwa msisitizo
“Ndiyo! mteja wangu wa mwisho alikuwa ni yule mwarabu na naye ameshatoka”
“Okay! mwanaume yeyote atakayeingia chumbani kwako kuanzia sasa utanijulisha”
“Sawa!” Zera akaitikia kwa utulivu na ile simu upande wa pili ilipokatwa Zera
akairudisha mahala pake na hapo akageuka na kunitazama kwa wasiwasi.
“Mbona kama wanakuuliza wewe?” Zera akaniuliza huku uso wake ukionesha
mashaka,
“Bila shaka!” nikamjibu Zera huku nikifikiria uongo wa kumwambia utakao
karibiana na ukweli kwani endapo ningekataa kuwa siyo mimi niliyekuwa nikiuliziwa
kwenye ile simu Zera angeanza kuingiwa na mashaka na mimi.
“Sasa kwa nini ukanikataza nisiitikie?” Zera akaniuliza kwa mshangao.
“Kuna rafiki yangu nimekutana naye humu ndani sasa ananing’ang’ania na
anataka kunichomoa pesa ndiyo ikabidi nimtoroke nikamwambia kuwa nakuja huku
vyumbani kutafuta mrembo wa kustarehe naye. Sasa naona jamaa kapatwa na mashaka
baada ya kuona sipatikani kwenye simu kwani simu yangu nimeizima” niliongea huku
nikijichekesha mbele ya Zera katika namna ya kumzuga ingawa akilini nilishaanza
kuhisi kuwa huwenda ile maiti ya yule mtu kule chooni ilikwisha gundulika.
“Kama ni hivyo basi una haki ya kumkimbia” Zera akaongea kwa utulivu na nilipomtazama usoni nikafurahi kuwa angalau nilikuwa nimefanikiwa kumlainisha
hata hivyo sikutaka kuendelea kukaa mle ndani. Huku nikifahamu kuwa baada ya
muda mfupi polisi wangefika pale kwenye casino na kuanza uchunguzi wao nikaamua
kuagana na Zera kisha nikaelekea mlangoni ambapo niliufungua na kutoka nje.
Nilikuwa nimejiandaa kwa hali yoyote hivyo mara tu nilipotoka nje ya kile chumba
cha Zera niliigeuza kofia yangu nyuma kisha nikachukua miwani mfukoni na kuivaa
huku nikiharakisha kuelekea kwenye zile ngazi za kushukua ukumbi wa chini wa
casino. Lakini kabla sijashuka nilitazama kule chini kwenye ule ukumbi wa casino na hali
ya mambo haikuniruhusu kutimiza adhma yangu.
Watu wote mle ukumbini walikuwa wakielekea kule nyuma kwenye lile eneo la
maliwato ya casino na baadhi ya wanawake walikuwa wakilia. Nikajua ile maiti ya mtu
niliyepambana naye kule chooni ilikuwa tayari imegundulika na baadhi ya mabaunsa
wa casino ile walikuwa wakihaha haku na kule kumtafuta mtu aliyehusika na mauaji
yale.
Sikushuka tena kule chini ya ule ukumbi wa casino na badala yake nikashika uelekeo
wa kule nilikotoka nikitafuta njia nyingine mbadala ya kutokea nje ya jengo lile pasipo
kupitia kwenye ule mlango mkubwa wa mbele wa ile casino. Nilitembea kwa haraka
huku macho yangu yakizunguka huku na kule kutafuta sehemu ya kutokea.
Hatimaye nikakutana na milango miwili iliyokuwa upande wa kulia. Nilipoichunguza
milango ile nikagundua kuwa ilikuwa ni milango ya vyoo kama vile vya ule ukumbi wa
chini. Choo cha kiume na cha kike. Bila kupoteza muda nikaufungua ule mlango wa
choo cha kiume na kuzama ndani. Mandhari ya mle ndani hayakutofautiana kabisa na
vile vyoo vya kule chini kwenye ule ukumbi wa casino.
Nikaanza kuzunguka mle ndani nikitafuta sehemu ya kutokea nje lakini nilishindwa
kwani mle ndani hapakuwa na upenyo wa namna yoyote na kila sehemu ilikuwa
imezibwa kwa kuta nene. Sehemu ya juu ya dari ya kile choo ilikuwa imefunikwa kwa
ukuta wa zege kwa ajili ya sakafu ya ghorofa inayofuata. Nikiwa nimeridhika kuwa
nisingeweza kuitimiza adhma yangu ya kutoka nje ya lile jengo la casino kwa kupitia
mle ndani sikutaka kupoteza muda mle ndani. hivyo nikafungua mlango wa kile choo
na kutoka nje.
Mara tu nilipotoka nje ya kile choo nikawaona wanaume wawili mabaunsa wa
ile casino wakija upande wangu. Sikutaka wale mabaunsa wanifikie hivyo nikashika
uelekeo wa upande wa kushoto nikiharakisha kwenda mbele huku macho yangu
yakitazama huku na kule nikiendelea kutafuta sehemu ya kutokea. Hata hivyo kabla
sijafanikiwa wale mabaunsa walikwishanifikia na kunitahadharisha.
“Oyaa! braza hebu simama” baunsa mmoja alinionya hata hivyo niliendelea na
safari yangu huku nikijidai sijamsikia.
“Oyaa! vipi unajidai hutusikii au ndiyo unaleta kiburi?” mwenzake akasisitiza.
Haraka nikatazama kule mbele yangu na bado sikuona matumaini ya kutoka mle
ndani kwa hila hivyo ikanibidi nipunguze mwendo na kugeuka nyuma.
“Vipi mnaniongelesha mimi?” niligeuka na kuwauliza.
“Sasa unadhani tunamwambia nani mwingine kama siyo wewe!” mmoja akafoka
huku akiongeza hatua zake kunikaribia.
“Mimi siitwi wewe bwana hebu tumieni majina ya heshima basi” niliwaambia wale
mabaunsa huku nikizipima vizuri hatua zao kadiri walivyokuwa wakizidi kunikaribia.
“Huku unaelekea wapi?” mmoja aliniuliza pindi waliponifikia.
“Kwani nyinyi mnaenda wapi?” nikawarudishia lile swali.
“Oyaa mbona unajitia kiburi hebu jibu ulivyoulizwa” mwenzake akadakia huku
akizidi kunisogelea.
“Mna shida gani na mimi hadi mniulize mahali ninapoelekea wakati mnaniona
bado nipo humu ndani ya casino?” niliwauliza huku nikawatazama wale mabaunsa.
Miili yao ilikuwa mikubwa iliyotuna na yenye misuli iliyokaza na kugawanyika vizuri
kwa mazoezi makali yenye ratiba inayozingatiwa vizuri. Nguo walizovaa;fulana nyeupe
na suruali nyeusi za jeans hazikufanikiwa kuificha miili yao.
“Geuka nyuma na tunaenda na wewe” baunsa mmoja alinionya baada ya
uvumilivu wake kuonekana kufika kikomo na hapo kwa pamoja nikaanza kuwaona
wakinisogelea pale niliposimama.
”Niende wapi na nyinyi kwani mmekuja na mimi humu ndani?” niliwauliza kwa
jazba za kuchelewesha na hapo baunsa mmoja akawahi kunishika kwa nyuma na
kunikwida na kutokana na ukubwa wa mwili wake nikawa nimeenea vizuri kwenye
kabari matata ya mkono wake wenye nguvu.
“Mnanipeleka wapi nyie mabwege?” niliwauliza kwa hasira huku nikijitahidi
kufurukuta.
“Agh! sisi mabwege siyo eh! basi subiri uone kazi yetu” yule baunsa aliyenikwida
akaongea kwa hasira huku akizidi kunibana kwa nguvu kisha akamwambia mwenzake.
“Oyaa! Kibusta atatusumbua sana huyu fala hebu mlegeze kidogo”
Sikuelewa maana ya maneno yale hadi pale nilipoziona ngumi mbili za nguvu na za
chapuchapu zikitua tumboni mwangu na kunisababishia maumivu makali yasiyoweza
kusimulika huku nikianza kuhisi kichefuchefu. Tumbo lango lilikuwa limekorogeka
vibaya na kwa mbali ladha chungu ya nyongo ikaanza kutembea kwenye ulimi wangu
na hapo nikaanza kuifikiria roho yangu.
Ngumi nyingine zilipotupwa niliikaza vizuri misuli ya tumbo langu kukabiliana
na maumivu yake hata hivyo kuendelea kuruhusu kichapo cha namna ile tumboni
nilitambua kuwa kingezidi kuidhoofisha afya yangu. Hivyo nilikusanya nguvu za
kutosha kisha nikajipinda na kumtandika kichwa cha nguvu yule baunsa aliyenishika
nyuma yangu na hapo nikasikia kelele za yowe kali la maumivu. Yule baunsa akaniachia
mwenyewe bila kupenda. Kile kichwa nilichomtandika kilikuwa kimeupasua na
kuusaga vibaya mwamba wa pua yake huku sehemu ya mbele ya mdomo wake
ikichanika na kuvuja damu. Wale mabaunsa walikuwa na nguvu za ajabu lakini
walikuwa hawafahamu mbinu za mapigano hivyo hawakuweza kufua dafu mbele
yangu.
Wakati yule baunsa mwingine niliyemtandika kichwa akijishika usoni kuugulia maumivu yule mwenzake akasogea haraka kunikabili huku akirusha ngumi moja
ambayo niliiona mapema nikainama kidogo na kuikwepa kisha nikamtandika ngumi
moja ya nguvu mbavuni. Yule baunsa akapiga yowe kali la maumivu na kubweka kama
mbwa na kabla hajatulia vizuri nikamsindikiza na teke zito la mgongoni lililompekea
ajibamize vibaya kwenye ukuta wa ile korido na hapo tusi zito likamponyoka. Alipotaka
kugeuka nikamzaba ngumi kavu mbili za shingo zilizompotezea mawasiliano na
ubongo na hapo akaangua chini na kutulia.
Yule mwenzake niliyekuwa nimemtandika kichwa pale awali akaanza kunifuata
kwa hasira. Aliponifikia akarusha teke lakini nilikua makini kuishtukia dhamira yake
hivyo nikawahi kujitupa pale chini huku nikiliacha lile teke lake likikata hewa bila
mafanikio. Ilikuwa nafasi nzuri kwangu hivyo nikajizungusha na kumchota mtama
wa aina yake na hapo yule baunsa akapaa hewani mzobemzobe alipotua chini akatulia
kimya huku fahamu zikiwa mbali na nafsi yake.
Nikayumbayumba hadi pale nilipopata mhimili mzuri wa ukuta wa ile korido na
hapo nikajiegemeza huku nikihema ovyo kuirudisha pumzi mwilini mwangu. Yale
madubwana mawili yalikuwa yamelala pale chini sakafuni huku yakiwa hayajitambui.
Nikiwa bado nimeegemea ule ukuta huku nikiendelea kuhema ovyo mara nikasikia
sauti ya hatua za mtu mwingine akija upande ule. Sikutaka kusubiri hivyo nikaanza
tena kuharakisha nikielekea kule mbele ya ile korido ingawa sikuweza kufahamu kuwa
nilikuwa nikielekea wapi. Hatimaye bahati ikaangukia kwangu kwani mbele kidogo ya
korido ile upande wa kulia nikaziona ngazi nyembamba zinazoelekea sehemu ya juu
ya lile jengo la casino. Chini ya ngazi zile kulikuwa na mlango mdogo kwenye chumba
kidogo kisichoeleweka ujenzi wake. Ingawa sikuwa na utaalam wowote katika masuala
ya ujenzi lakini kuiona sehemu ile nikakumbuka kitu.
Kilikuwa chumba kidogo chenye Mainswitch ya umeme wa lile jengo lote la
casino. Ufundi umeme ulikuwa miongoni mwa fani zangu hivyo niliufungua ule
mlango mdogo wa kile chumba kisha nikaanza kufanya utundu wangu. Kufumba na
kufumbua jengo lote la ile casino likagubikwa na giza zito na hapo kazi iliyosalia ikawa
rahisi sana kwangu.
Haraka nikarudi kule chini kwenye ule ukumbi wa casino na kwa kuwa hakuna
mtu yeyote aliyeweza kuniona kutokana na giza la mle ndani hivyo ikawa rahisi sana
kwangu kujichanganya kwenye kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbilia mlango
wa kutokea nje ya ile casino huku wengi wao wakiwa ni wanawake waliokuwa wakipiga
makelele ya hofu.
Kwa uzoefu niliokuwanao nilifahamu fika kuwa jengo kama lile lisingekosa
jenereta kubwa la kusambaza umeme pale inapotekea kuwa ule umeme wa gridi ya
taifa umekatika. Hata hivyo nilikuwa na hakika kuwa kutokana na ukorofi niliyoufanya
kwenye kile chumba cha umeme wa jengo lile la casino hata jenereta hilo lisingeweza
kufua dafu.
Hapakuwa na namna ya kuwazuia watu wasitoke nje ya lile jengo la casino kwa
kuzingatia kuwa usalama wa watu lilikuwa zingatio la kwanza katika biashara za namna ile. Hivyo nikajichanganya katika kundi lile kubwa la watu waliokuwa wakikimbia
ovyo kwenda nje huku tabasamu maridhawa likifanya ziara usoni mwangu.
Kitu kilichozidi kuwachanganya watu ni kuwa majengo yote ya jirani na lile jengo
la ile casino yalikuwa na umeme. Hali ile ikampelekea kila mmoja aanze kuongea lake.
Baadhi ya watu niliwasikia wakiwashuku magaidia kuwa walikuwa wakihusika na
lile tukio la kifo cha yule mtu kwenye ile casino na baadaye kukatika kwa umeme.
Wengine nikawasikia wakiilaani miundo mbinu ya umeme wa jengo lile kuwa ilikuwa
mibovu tangu siku nyingi bila kubadilishwa.
Wengine nikawasikia wakidai kuwa umeme wa lile jengo la casino ulikuwa
umezimwa makusudi ili kufanikisha mpango wa mauji ya watu uliyoanza kutekelezwa
mle ndani. Ili mradi kila mtu alikuwa huru kuzungumza vile alivyojisikia lakini ukweli
wa mambo niliufahamu mimi.
Nje ya lile jengo la casino kila mtu aliharakisha kuliendea gari lake na wale wasiokuwa
na magari wao waliekea kwenye geti la kutokea nje ya eneo lile la casino kisha kila
mmoja akashika uelekeo wake.
Nililifikia gari langu nikafungua mlango na kuingia ndani kisha nikaipekua bastola
yangu na kuridhika kuwa bado ilikuwa kwenye maficho yake salama. Niliwaza kuwa
kuondoka kwangu eneo lile mapema kungeweza kutengeneza chanzo kizuri cha
upelelezi wa tukio lile la mauaji kwenye ile casino. Hivyo niliendelea kusubiri mle ndani
ya gari na baada ya magari manne kunitangulia kuondoka kwenye yale maegesho
na mimi ndiyo nikaunga mkia nyuma yao huku mche wa sigara ukiteketea taratibu
mdomoni mwangu.
Usiku ulikuwa mbioni kushamiri na kwa mbali manyunyu hafifu ya mvua yalianza
kuanguka kutoka angani nami nikayaondoa mbele yangu kwa kuwasha wiper za kioo
cha mbele cha gari langu. Mvua za masika bado zilikuwa zikiendelea kunyesha sehemu
mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
_____
MUDA MFUPI BAADAYE mafundi umeme kutoka kitengo cha dharura cha
shirika la umeme la Tanesco walikuwa ndani ya lile jengo la Vampire Casino wakifanya
kazi waliyoitiwa.
Kwa weledi wao na maarifa ya masuala ya umeme waliyokuwa nayo wakamtoa
hofu meneja wa casino ile mwanaume mrefu na mwembamba aliyeshindwa kabisa
kuitowesha hasira yake usoni tangu kugundulika kwa yale mauaji kule chooni na
hatimaye kukatika kwa umeme katika lile jengo la casino.
Mafundi wale wa umeme wakamuweka bayana meneja wa casino ile kwa kumueleza
kuwa tatizo lile la kukatika kwa umeme kwenye lile jengo la casino lilikuwa limetokana
na fyuzi chache muhimu zilizochomolewa kutoka kwenye Mainswitch iliyokuwa
ikisambaza umeme kwenye lile jengo la casino. Huku wakisisitiza kuwa hakukuwa na
uharibifu wowote uliokuwa umetokea katika miundo mbinu ya umeme wa lile jengo.
Hatimaye wakarudishia zile fyuzi na hapo umeme wa lile jengo ukawaka.
Wakati wale mafundi umeme wa kitengo cha dharura kutoka Tanesco wakiondoka
kwenye lile jengo la casino baada ya kukamilisha kazi yao mlangoni wakapishina na yule
mkuu wa kituo cha polisi cha mjini kati ASP O.J.Mkwaju Ngoma akiwa ameongozana
na askari wake watatu vijana wa kazi huku wote wakiwa wamevaa sare zao za polisi.
Taarifa za mtu aliyeuwawa katika choo cha Vampire Casino zilikuwa zimeifikia ofisi
yake kupitia simu ya mlinzi mmoja wa casino ambaye hakupenda kujitambulisha jina
lake. Askari wale walipoingia ndani ya casino wakafahamiana na baadhi ya uongozi wa
casino ile kisha wakaelekea moja kwa moja hadi kwenye eneo la tukio.
Kulikuwa na watu wachache waliosalia wakiitazama ile maiti ya yule mtu aliyeuwawa
kwenye kile choo cha casino. Miongoni mwa watu hao walikuwa ni wafanyakazi wa ile
casino ambao walikuwa wakimsikiliza kwa makini kijana mmoja ambaye alijinadi kuwa
yeye ndiye aliyekuwa shuhuda wa kwanza kulishtukia tukio lile la mauaji. Kijana yule
akaacha kusimulia mara baada ya kumuona ASP O.J.Mkwaju Ngoma akiingia eneo
lile huku ameongozana na askari wake.
“Poleni sana jamani!” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akasimama na kuisalimia
kadamnasi ile.
“Tumeshapoa Afande” wote wakaitikia na hapo ASP O.J.Mkwaju Ngoma akaanza
kujitambulisha.
“Sisi ni askari tunaotokea kituo cha polisi cha mjini kati. Tafadhali! tunaomba
mtupishe kidogo tufanye kazi yetu. Hata hivyo tungeomba maelezo machache kama
kutakuwa na shuhuda yeyote mwenye taarifa za kutusaidia” ASP O.J.Mkwaju Ngoma
alimaliza kuongea kisha akachezesha sharubu zake na kujivika tabasamu la kirafiki.
Wale mashuhuda kuona vile wote wakageuka na kumtazama yule kijana aliyekuwa
mstari wa mbele akiwasimulia namna alivyokuwa wa kwanza kuishtukia ile maiti ya
yule mtu pale chooni na hiyo ikiwa ishara nzuri kwa ASP O.J.Mkwaju Ngoma kupata
kupata sehemu ya kuanzia mahojiano yake. Hivyo akageuka na kumtazana yule kijana
aliyekuwa akitazamwa na wale watu eneo lile huku akitengeneza tabasamu hafifu
usoni mwake.
“Ulikuwepo hapa wakati mauaji haya yalipofanyika?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma
akauliza huku akimtazama kijana yule kwa makini.
“Sikuwepo ila nilikuwa shuhudua wa kwanza kuishtukia maiti hii” yule kijana
akaongea kwa kujiamini na hapo askari mmoja miongoni mwa wale watatu akasogea
na kuanza kuchukua maelezo yake.
“Nyinyi wengine mnaweza kwenda ili mtupe uhuru wa kufanya kazi yetu” ASP
O.J.Mkwaju Ngoma akawataka wale mashuhuda wengine waondoke eneo lile na
wakati wale watu wakiondoka akawaambia
“Naomba mtuitie na meneja wa hii casino”
Wakati wale mashuhuda wakitawanyika wale askari polisi wawili waliosalia
wao walikuwa wakishughulika na kuufungua ule mlango wa kile choo kwani wale
mashuhuda walikuwa wameitazama ile maiti ya yule mtu kwa kuchungulia kwa juu
kupitia choo cha jirani.Ule mlango ulipofunguka askari wote wakasogea karibu na kuitazama ile maiti
ya yule mtu. Kichwa cha ile maiti kilikuwa kimepasuka vibaya baada ya kubamizwa
kwenye sinki la choo cha mle ndani na hivyo kupelekea ubongo wake na damu nyingi
kutapakaa eneo lile huku mguu na mkono wake mmoja ukiwa umevunjika.
“Jina lako?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamuuliza yule kijana huku yule askari
wake pembeni akiendelea kuchukua yale maelezo. Baada ya yule kijana kujitambulisha
mahojiano yakaendelea.
“Wewe ni mteja au mfanyakazi wa hii casino?”
“Mfanyakazi”
“Kazi yako?”
“Kusafisha vyoo vya hii casino” yule kijana akaendelea kutoa maelezo huku akianza
kuingiwa na woga wa kuhojiwa na polisi.
“Ilikuwa majira ya saa ngapi wakati ulipoishtukia maiti ya huyu mtu?”
“Kati ya saa tatu na nusu na saa nne kasoro usiku huu”
“Ilikuwaje?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamuuliza yule kijana huku akimkazia
macho.
“Mimi kazi yangu ni kusafisha vyoo vyote vya hii casino hivyo mara kwa mara huwa
napita kufanya usafi. Sasa wakati naingia humu ndani kusafisha ndiyo nikashtuka
baada ya kuona damu nyingi ikitoka na kusambaa chini ya huu mlango wa choo” yule
kijana akamaliza kuongea huku akizitazama nyuso za wale askari.
“Sasa ulihisi nini baada ya kuiona hii damu?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamuuliza
yule kijana huku akiyapeleka macho yake tena kuitazama ile maiti.
“Nilihisi jambo la hatari ndiyo nikatoka kwenda kuwaita wenzangu” yule kijana
akajibu kwa woga.
“Relax kijana wangu!” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamwambia yule kijana huku
akimpigapiga mabegani baada ya kumuona akianza kuongea kwa woga.
“Wakati ukiingia humu ndani hukumkuta au kupishana na mtu yeyote akitoka?”
“Hapana!”
ASP O.J.Mkwaju Ngoma akamtazama tena yule kijana kwa uyakinifu kisha
akayahamisha macho yake tena kuitazama ile maiti ya yule mtu pale chini kabla ya
kuuliza tena.
“Hiki choo ni kibovu?”
“Hapana!” yule kijana akajibu kwa kujiamini.
“Una hakika?”
“Kabisa!,humu ndani ya hii casino hatuna choo kibovu na kama kingekuwepo
ningekuwa tayari nimekiripoti kwenye uongozi”
“Sasa nani aliyeandika hapa kuwa CHOO HIKI HAKITUMIKI?”
“Hata mimi pia nashangaa” yule kijana akaongea huku akionesha kutofahamu
kabisa kilichokuwa kikiendelea juu ya maelezo yake kwenye ule mlango wa kile choo.
Kikafuatia kitambo kifupi cha ukimya huku yule askari mwingine akiendelea kuandika
maelezo ya kile walichokishuhudia pale chooni.Baada ya hapo kukafuatiwa na mahojiano mengine ya hapa na pale kisha yule
kijana akaruhusiwa aondoke ili akaendelee na kazi zake huku akisisitizwa kuwa awe
tayati kutoa ushirikiano kwa polisi pale atakapohitajika kufanya hivyo. Yule kijana
akaondoka.
Muda mfupi baada ya yule kijana kuondoka eneo lile ASP O.J.Mkwanju Ngoma
na vijana wake wakaanza kazi ya kuchukua vipimo vyote muhimu vya upelelezi eneo
lile.
Wakati ASP O.J.Mkwanju Ngoma na askari wake wakiwa wanaendelea na kazi
yao meneja wa casino ile akawa tayari amefika eneo lile huku akiwa ameongozana na
vijana watatu ambao miongoni mwao ASP O.J.Mkwaju Ngoma alimtambua mmoja.
Akajiuliza ni wapi alikutana na kijana yule na baada ya kufikiri kwa muda akakumbuka
na hapo mshangao ukamshika. Hata hivyo akajitahidi kuumeza mshtuko wake.
“Habari za kazi Afande?” mtu mmoja miongoni mwa wale watu wanne akamsalimia
ASP O.J.Mkwaju Ngoma huku uso wake ukishindwa kuonesha tashwishwi yoyote.
“Nzuri! wewe ndiye meneja wa hii casino?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akauliza
huku akimtazama yule mtu.
“Ndiyo!”
“Nahitaji kufanya mahojiano na wewe kufuatia hili tukio la mauaji” ASP
O.J.Mkwaju Ngoma akaongea kwa utulivu huku akimtazama meneja wa ile
casino,manaume mrefu na mweusi mwenye umri wa miaka arobaini na ushei.
“Mimi siyo msemaji wa hii casino” yule meneja wa casino akaongea huku akionekana
kukasirishwa na uwepo wa askari eneo lile.
“Wewe si ndiye meneja wa hii casino?” ASP akauliza huku akishindwa kumuelewa
vizuri yule mtu.
“Ndiyo! lakini kuzungumzia masuala ya hapa siyo kazi yangu” yule mtu akasisitiza
kwa kiswahili chake chenye kasoro na hapo ASP O.J.Mkwaju Ngoma akatulia kidogo
akimtazama yule mtu katika namna ya kushangazwa na maelezo yake.
“Sasa msemaji wa hii casino ni nani?” ASP O.J.Mkwaju Ngoma hatimaye akauliza
kwa udadisi.
“Yupo likizo!”
Jibu la mkato la yule meneja wa casino likazidi kumchanganya ASP O.J.Mkwaju
Ngoma na wale askari wake na hapo wakatazamana kwa muda huku ukimya ukichukua
nafasi. Ukimya ule ulipokuwa mbioni kushika hatamu kijana mmoja miongoni mwa
wale vijana watatu waliofika eneo lile huku wakiwa wameongozana na yule meneja wa
casino akavunja ukimya huku akipiga hatua kusogea mbele
“Mzee unanikumbuka?” yule kijana akauliza huku akitabasamu na ASP
O.J.Mkwaju Ngoma alipomtazama haraka akamkumbuka vizuri yule kijana. Alikuwa
ni Fulgency Kassy,yule kijana aliyekuja ofisini kwake kule kituo cha polisi cha mjini
kati akiulizia taarifa za upelelezi za kifo cha Guzbert Kojo kilichotokea kule mtaa wa
Nkurumah siku ya jana. Vijana wengine wawili waliosalia mmoja alikuwa Pweza na
yule mwingine alikuwa Kombe.
“Ndiyo nakukumba” ASP O.J.Mkwaju Ngoma hatimaye akaongea huku akili
yake ikisumbuka kutafuta sababu ya swali lile.
“Naomba hilo faili lenu lenye maelezo halafu wachukue askari wako mwondoke
eneo hili kwani hii kesi haiwahusu” Fulgency Kassy akaongea huku usoni akitabasamu
na wenzake nao wakafanya vilevile huku mikono yao wakiwa wameikunjia vifuani
mwao. Hata hivyo yule meneja wa ile casino hakuonesha kushtushwa hata chembe na
yale maneno ya Fulgency Kassy,tukio ambalo liliwastaajabisha sana ASP O.J.Mkwaju
Ngoma na askari wake.
“Mnaonekana kuwa mna ajenda yenu binafsi,sivyo?”ASP O.J.Mkwaju Ngoma
akaongea kwa jazba huku akiwakata jicho la hasira wale vijana.
“Hupaswi kulalamika Afande hiki tunachokifanya ni kukurahisishia kazi wewe
na askari wako. Huoni kuwa umri wako haukuruhusu kujishughulisha na masuala
magumu kama haya!” Pweza akadakia.
“Nyinyi vijana hamna mamlaka yoyote ya kunielekeza kitu cha kufanya na
mkiendelea na hiyo tabia yenu ya kunifuatafuata nitawafahamisha kwanini nilipewa
jina la Mkwaju Ngoma” ASP O.J.Mkwaju Ngoma akafoka kwa hasira lakini wakati
akifanya hivyo Fulgency Kassy alikuwa akimalizia kibonyeza kitufe cha tarakimu ya
mwisho kwenye simu yake kisha akaiweka simu yake sikoni. Ile simu ilipopokelewa
upande wa pili Fulgency Kassy akaongea kidogo kabla ya kuitoa sikioni mwake na
kumpa ASP O.J.Mkwaju Ngoma huku akiendelea kutabasamu.
“Afande zungumza na huyu mtu badala ya kuendelea kushikilia msimamo wako
usiyo na maana” Fulgency Kassy akaongea kwa ujivuni na hapo ASP O.J.Mkwaju
Ngoma akaipokea ile simu na kuiweka sikioni na baada ya mazungumzo mafupi na
mtu wa upande wa pili wa ile simu akatoa ile simu sikioni na kuirudisha kwa Fulgency
Kassy huku uso wake ukiwa umetahayari. Kisha akameza funda kubwa la mate
kuitowesha hasira iliyonasa kwenye koo lake kabla ya kuwageukia wale askari wake
na kuwaambia.
“Twendeni” wale askari wakiwa wameshajiweka tayari kusubiri jibu la namna ile
wakaacha kile walichokuwa wakikifanya. Yule askari aliyekuwa akiandika yale maelezo
ya awali ya lile tukio la mauaji ya yule mtu akamkabidhi Fulgency Kassy lile faili lenye
maelezo kisha wale askari wote kwa pamoja wakaanza kuondoka huku wameinamisha
vichwa vyao chini kama kondoo.
Taarifa juu ya mauaji yalitokea kwenye kile choo cha Vampire Casino zilikuwa
zimewafikia Fulgnecy Kassy,Pweza na Kombe kutoka kwa afisa mmoja wa usalama
wa ngazi ya juu serikalini mara baada ya afisa huyo kupokea simu kutoka kwa meneja
wa casino.
Mara baada ya ASP O.J.Mkwaju Ngoma na wale askari wake kuondoka Fulgency
Kassy akageuka na kumtazama meneja wa casino ile kabla kumuuliza.
“Una mfahamu huyu mtu aliyeuwawa?”
“Ndiyo!” yule meneja akaitikia huku akionekana kuanza kuchoshwa na mchokato
wa matukio yote yaliyokuwa yakitokea mle ndani ya casino.
“Unamfahamu vipi?”
“Ni mmoja wa walinzi wangu wa hapa casino”
“Una sababu yoyote unayodhani huwenda ikawa imepelekea kifo chake?” Pweza
akauliza huku akiziokota bastola mbili juu ya dimbwi la damu mle chooni ambapo
alipoanza kuzikagua akagundua kuwa zote zilikuwa zimejaa risasi.
“Taarifa nilizozipata kwa walinzi wenzake wa humu ndani ni kuwa yeye alikuwa
akimfuatilia huyo mtu aliyemuua baada ya kumtilia mashaka mtu huyo wakati
alipoingia kwenye hii casino. Sasa sijafahamu kipi kilichotokea hadi mlinzi wangu
akauwawa” meneja wa casino akaongea kwa masikitiko.
Kombe akaisogelea ile maiti ya yule mlinzi na kuanza kuifanyia uchunguzi kwa
ukaribu na baada ya muda mfupi akaja na hoja.
“Yeyote aliyehusika katika kumuua huyu mlinzi ni mtu mzoefu katika mapambano”
“Kwa nini?” Fulgency Kassy akauliza huku akiyapeleka macho yake kuitazama ile
maiti ya yule mlinzi pale chini.
“Inavyoonekana ni kuwa kulitokea patashika ya mapambano makali baina ya huyu
mlinzi na huyo mtu aliyemuua lakini huyu mlinzi hakuweza kufua dafu kwa huyo
mtu ingawa huyu mlinzi anaonekana kuwa alikuwa na bastola mbili na zote zilikuwa
zimejaa risasi” Kombe akaongea huku akizigeuzageuza zile bastola na kuzikagua kwa
makini.
“Ni kweli anavyosema Kombe” Pweza akadakia ”Inavyooneakana ni kuwa huyu
mlinzi ndiye aliyemvamia huyo mtu aliyemuua lakini alishindwa kuitumia nafasi hiyo
vizuri”
Flugency Kassy akageuka na kumtazama yule meneja wa casino kabla ya kumuuliza.
“Huwa mna utaratibu kuweka kumbukumbu za watu wote wanaoingia kwenye
hii casino?”
”Ndiyo!,mtu hawezi kuingia humu ndani mpaka awe na kadi ya mwanachama wa
casino” yule meneja akafafanua
“Nani aliyekueleza kuwa huyu mlinzi alikuwa akimfuatilia huyo mtu aliyepambana
naye hadi kufikia kuzidiwa na hatimaye kuuwawa?” Fulgency Kassy akaendelea
kuyaelekeza maswali yake kwa yule meneja wa casino.
“Nimeambiwa na mlinzi mwenzake”
“Tunaweza kuonana na huyo mlinzi?” Fulgency Kassy akauliza huku akimtazama
meneja yule kwa makini.
“Ondoa shaka!” meneja wa casino akaongea kisha akaichukua simu yake ya
kiganjani na kupiga namba fulani. Baada ya pale haukupita muda mrefu kijana
mwenye umri kati ya miaka ishirini na saba hadi thelathini akaingia mle ndani huku
akiwa ameongozana na mabaunsa wawili wenye sura za huzuni. Walikuwa ni wale
mabaunsa waliopambana na Chaz Siga kule kwenye ile korido ya ghorofa ya pili na
kuambulia kupigo kibaya hadi kupoteza fahamu.
Wale mabaunsa huku wakiwa wanaona aibu mara walipofika eneo lile wakaanza
kusimulia mkasa wote uliowapata juu ya yule mtu waliyepambana naye kule kwenye gorofa ya pili ya casino. Walipomaliza kusimulia Fulgency Kassy akageuka na
kumuuliza yule mlinzi mwingine aliyeitwa kutoa maelezo.
“Maelezo ya hawa wenzako juu ya huyo mtu waliyepambana naye yanawiana na
kile ulichotoka kutueleza?”
“Ndiyo!” yule mlinzi akaongea kwa unyonge
“Yupoje huyo mtu?” Pweza akadakia.
“Alikuwa mwanaume mrefu na mweusi mweupe mwenye mwili imara na alikuwa
amevaa suruali ya jeans na fulana nyeusi na kichwani alikuwa amevaa kofia” yule mlinzi
akafafanua.
“Atakuwa ndiye huyo huyo tu” Kombe akaongea kwa sauti tulivu.
“Unadhani ni kwa nini mlimtilia mashaka huyu mtu wakati alipokuwa akiingia
humu ndani ya casino?” Fulgency Kassy akamuuliza tena yule mlinzi.
“Alikuwa mgeni na alionekana kuchunguza mambo yaliyokuwa yakiendelea
humu ndani” maelezo ya yule mlinzi yakawapelekea wote wageuke na kumtazama
yule mlinzi kwa makini huku wakitafakari.
“Mnadhani ni kwa nini huyo mtu alipanda kule juu ghorofani?” Fulgency Kassy
akawatupia swali wale mabaunsa huku akiwatazama.
“Hatufahamu” wote wakaitikia
“Mimi nafikiri kitu cha kufanya hapa ni kupitia kamera zote za humu ndani na
hapo tutamfahamu huyo mtu ni nani” Pweza akasisitiza.
“Yes! hilo ni wazo zuri kwani kupitia kamera za humu ndani tunaweza kumuona
huyo mtu aliyehusika na haya mauaji” Fulgency Kassy akaongea akiunga mkono hoja
ya Pweza huku akionekana kufurahi na kabla yule meneja wa ile casino hajaondoka
eneo lile akawahi kumtahadharisha.
“Hakikisha hakuna mtu yeyote humu ndani atakayefungua mdomo wake
kuzungumza na waandishi wa habari kwani unafahamu madhara ya kufanya hivyo”
“Ondoa shaka!” meneja wa casino akaongea kwa utulivu kisha akafungua mlango
wa kile choo na kutoka nje huku akiwa ameongozana na wale walinzi wake.
Muda mfupi uliyofuata baada ya yule meneja wa casino kutoka Fulgency
Kassy,Pweza na Kombe walianza kuushughulikia mwili wa yule mlinzi wakichukua
vipimo ambavyo vingewasaidia katika uchunguzi wao. Zoezi lile lilipokamilika mwili
wa yule mlinzi wakautumbukiza ndani ya mfuko wa nailoni mkubwa na mweusi
uliokuwa na zipu ndefu. Kisha wakaisafisha ile damu iliyotapakaa pale chooni sakafuni
kama namna ya kuondoa vielelezo vyovyote kwa mtu au watu ambao wangefika eneo
lile baadaye.
Walipomaliza kazi yao majibu yaliyopatika kutoka kwenye kamera za mle ndani
na taarifa kutoka eneo la mapokezi la ile casino yalikuwa juu ya meza ya ofisi ya yule
meneja wa casino. Mshukiwa namba moja wa mauaji ya yule mtu kule chooni alikuwa
amefahamika kwa jina la Stephen Masika na hata uvaaji wake ulishabihiana na maelezo
ya walinzi wa mle ndani ya casino.
Baadhi ya kamera za ile casino zilionesha kuwa katika vipindi tofauti Stephen Masika alionekana akiwa amekaa eneo la kaunta huku akijipatia kinywaji. Kamera
hizo baadaye zilimuonesha akielekea kule sehemu ya maliwato ambapo yale mauaji
ndipo yalipokuwa yametokea.
Stephen Masika alipotoka kule sehemu ya maliwato akaonekana akipanda zile
ngazi za kule ghorofani na hatimaye kuingia chumba namba 26 ambapo humo
alikaa kwa muda na alipotoka akaonekana akipambana na wale walinzi wa casino na
hatimaye kuwadhibiti vizuri kwenye ile korido. Baada ya hapo mtu yule aliyejulikana
kwa jina la Stephen Masika haikufahamika alitoka vipi nje ya jengo lile la casino ingawa
hisia zilimuhusisha na kukatika kwa ule umeme mle ndani na huwenda alitoka kwa
kujichanganya na watu waliokuwa wakitoka nje ya casino muda mfupi baadaya ya ule
umeme kukatika.
“Nyinyi endeleeni na kazi yenu sisi tutajua nini cha kufanya” Fulgency Kassy
akamwambia meneja wa ile casino baada ya majadiliano ya hapa na pale kufika tamati
kisha wakasogeza viti vyao nyuma ya meza kubwa ya ofisini na kusimama wakiagana
na meneja wa casino ile kabla ya kutoka mle ndani. Muda mfupi baadaye walikuwa
ndani ya gari aina ya Landcruiser nyeupe na mwili wa yule mlinzi wakiupeleka mochwari
hospitali ya Muhimbili.
 
UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU J.K.NYERERE
asubuhi hii ulikuwa umechukua sura mpya. Baadhi ya shughuli za uwanjani
hapo zilikuwa zimesimama kwa muda ili kupisha tukio la heshima na la
kizalendo kufanyika. Baadhi ya makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la wananchi wa
Tanzania walikuwa wamefika kiwanjani pale katika mwonekano wa suti nadhifu za
kijeshi. Pia kulikuwa na wanajeshi wengine wenye madaraja ya chini ya vyeo ambao
wengi wao walielekeana kwa urefu kama siyo umri.
Wanajeshi wote walivaa vitambaa vyeusi mikononi mwao kuashiria kuwa
hawakuwa katika hali ya furaha bali walikuwa katika hali ya tanzia na huzuni ya kusubiri
kuipokea miili ya ndugu wazalendo waliopoteza maisha yao wakati wakilitumikia taifa
la Tanzania katika harakati za kijeshi chini ya mwamvuli wa MONUSCO ama umoja
wa jeshi la Afrika linalolinda amani huko nchini D.R Congo eneo la mashariki na Kivu
ya kaskazini.
Kwa upande wa viongozi wa kisiasa kulikuwa na amiri jeshi mkuu na rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi
wengine wa kisiasa akiwemo waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa. Wote wakiwa katika nyuso za masikitiko.
Kundi la mwisho lilikuwa ni lile la ndugu wafiwa jamaa na marafiki ambao walifika
kiwanjani pale kuipokea miili ya askari jeshi wazalendo watatu wa jeshi la wananchi wa
Tanzania waliokufa katika harakati za kijeshi huko nchini D.R Congo. Miongoni mwa
watu wale kulikuwa na wajane wa marehemu,watoto,wazee,ndugu,jamaa na marafiki
na wote walikuwa wamevaa mavazi meusi ya kuashiria hali ya simanzi.
Koplo Tsega akiwa miongoni mwa watu wa kundi lile alikuwa amefika kiwanjani
pale ili kushuhudia kile kinachosemekana mapokezi ya heshima ya miili mitatu ya
wanajeshi waliopoteza maisha katika harakati za kijeshi huko Kivu ya kaskazini nchini D.R Congo. Huku yeye akiwa ni mmoja wa askari jeshi hao watatu waliopoteza
maisha.
“Huu ni mkasa wa aina yake” Koplo Tsega akajikuta akijisemea moyoni huku akiwa
na hakika kuwa hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumtambua kuwa yeye ni nani
eneo lile. Makachero wa usalama wa taifa walionekana kutanda kila kona katika hali ya
kuhakikisha kuwa itifaki ya ulinzi na usalama inazingatiwa vizuri eneo lile.
Koplo Tsega akiwa amejichanganya katikati ya lile kundi la raia,ndugu,jamaa na
marafiki alikuwa akifahamu vizuri kila kitu kilichokuwa kikiendelea eneo lile. Kila
mara aliyatembeza macho yake huku na kule akizichunguza nyuso za watu mbalimbali
waliofika eneo lile huku akitarajia kuziona nyuso za watu fulani.
Mara kwa mara Koplo Tsega alijaribu kujitathmini juu ya mwonekano wake
mpya na kuridhika kuwa hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumtambua kuwa
yeye ni nani eneo lile. Alikuwa amejibadilisha katika kila eneo ambalo alihisi huwenda
lingeweza kumvuta mtu yeyote aliyekuwa akimfahamu. Akianzia mavazi hadi namna
ya utembeaji wake. Kabla ya kufika kiwanjani pale alikuwa amepitia katika duka
moja maarufu la nguo lililopo mtaa wa Kongo eneo la Kariakoo kununua mahitaji yote
muhimu ya kazi yake. Mahitaji ambayo wakati huu yalimfanya aonekana mwanamke
mstaarabu na anayejua kuyazingatia vizuri maadili ya dini yake. Mwonekano wake
mpya wa mavazi meusi ya baibui, juba, nikabu, soksi na glovu nyeusi ulikuwa amempa
nafasi nzuri ya kufanya kazi yake pasipo bugdha wala hisia zozote za kutiliwa mashaka
na mtu yeyote aliyekuwa akimfahamu eneo lile.
Kila alipokumbuka sababu iliyomfanya afike kiwanjani pale tabasamu lake hafifu
lilijivinjari usoni mwake na hapo kurasa za kitabu cha kumbukumbu za matukio yote
yaliyotokea katika msitu mnene wa Govender nchini D.R Congo zikaanza kijifunua
taratibu moja baada ya nyingine. Huku kurasa hizo zikitonesha majeraha makubwa
katika mtima wake na kupeleka simanzi iliyolifukuzia mbali tabasamu lake na
kusababisha hasira isiyoelezeka.
Koplo Tsega alikuwa amefika kiwanjani pale kushuhudia mapokezi ya mwili wake
na ile miili mingine ya askari jeshi wenzake wawili wote wakiwa wameuwawa katika
harakati za kijeshi huko D.R Congo.
Akiwa katikati ya kundi kubwa la raia waliofika kiwanjani pale Koplo Tsega
aligeuka na kuwatazama kwa siri ndugu zake waliofika kiwanjani pale akiwemo mama
yake mzazi,kaka na dada zake. Pamoja na ndugu wengine,jamaa na marafiki zake
ambao walikuwa wakiendelea kutokwa na machozi ya kuomboleza msiba wake kwa
huzuni tangu walipopata taarifa ya kifo chake.
Koplo Tiglis Tsega akaendelea kuwatazama watu wale huku moyoni akisikitika
sana kwa kuumia kwao ingawa hakuwa na namna ya kufanya katika kuhakikisha kuwa
lengo lake linatimia.
Koplo Tsega akiwa karibunao aliendelea kuwatazama ndugu zake na pale hisia za
huzuni zilipokuwa mbioni kumzidi nguvu akaacha kuwatazama na kugeuka akitazama
upande mwingine sehemu kiliposimama kikundi cha wanajeshi shupavu waliovaa suti nadhifu za heshima. Wanajeshi hao wakiwa wamejipanga vyema katika mistari miwili
minyoofu huku wakisubiri kuyapokea majeneza matatu yenye miili ya askari jeshi wa
Tanzania iliyokuwa ikiletwa na ndege kutoka huko eneo la Kivu ya kaskazini nchini
D.R Congo. Zinapofanyika operesheni za umoja wa jeshi la Africa-MONUSCO chini
ya mwamvuli wa umoja wa mataifa-UNITED NATIONS katika mpango wa kuleta
amani ya kudumu. Nchi za Tanzania,Afrika ya kusini na Malawi zikiunda jeshi hilo
lenye lengo la kuvidhibiti vikundi vyote vya waasi nchini D.R Congo na hatimaye
kuvipokonya silaha.
Koplo Tsega akajikuta akitabasamu tena pale alipokumbuka maelezo ya Guzbert
Kojo kuwa jina lake yaani yeye KopoTiglis Tsega lilikuwepo katika orodha ya majina
ya askari jeshi watatu wa Tanzania waliopoteza maisha yao katika harakati za kijeshi
huko nchini D.R Congo dhidi ya kikundi cha waasi cha M23 kinachopigana dhidi ya
majeshi ya serikali ili kuiondoa madarakani serikali ya rais Joseph Kabila.
Orodha ya majina ya wanajeshi hao watatu watanzania waliopoteza maisha katika
harakati hizo za kijeshi nchini D.R Congo yakisomeka kama ifuatavyo;Koplo Tsega
askari jeshi komandoo wa daraja la kwanza na mdunguaji mahiri kutoka kikosi cha
kijeshi namba 92 cha makamandoo hatari zaidi cha Sangasanga mkoani Morogoro.
Sajenti Chacha Marwa wa kutoka kikosi cha kijeshi namba 36 cha askari wa miguu
kambi ya Msangani wilayani Kibaha. Wa mwisho akiwa ni Meja Khalid Makame
kutoka kambi ya kijeshi namba 521 ya Chukwani huko kisiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa ratiba kamili iliyosomwa na msemaji mkuu wa masuala ya
operesheni za kijeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania,Brigedia Jenerali Mchwa
Mpaka ni kuwa ndege ya kijeshi ya jeshi la wananchi wa Tanzania aina ya Jet Fighter
302 ingetua kiwanjani pale muda wa saa nne na nusu asubuhi huku ikiwa na miili ya
wanajeshi hao watatu kutokea eneo la Kivu ya kaskazini nchini D.R Congo.
Koplo Tsega alivuta vazi lake refu na jeusi na kuitazama saa yake ya mkononi.
Mwenendo wa majira wa saa yake ukamfanya atabasamu kwani alikuwa hajachelewa
wala hajawahi sana kwa mujibu wa ratiba ile iliyosomwa muda mfupi uliyopita.
Hatimaye akaushusha chini mkono wake na kuitengeneza vizuri miwani yake myeusi
machoni katika kuhakikisha kuwa anaiona vizuri taswira ya kila kitu kilichokuwa
kikiendelea mbele yake.
Kulikuwa na muda wa robo saa zaidi wa kuendelea kusubiri kabla ya ndege
hiyo ya kijeshi iliyobeba miili ya wanajeshi hao haijatua pale kiwanjani na kupelekea
simanzi zaidi kwa watu waliofika uwanjani pale. Koplo Tsega aliendelea kuwaza huku
akiyatembeza macho yake kwenye halaiki ile ya watu yenye mchanganyiko mkubwa
wa wanausalama waliojificha katika mavazi ya kiraia ya miwani myeusi machoni mwao
na vinasa sauti vya mawasiliano vyenye nyaya nyeusi na nyembamba zilizopotelea
katika kola za makoti yao meusi ya suti.
Wakati Koplo Tsega akiendelea kuzitazama nyuso za watu kwenye kadamnasi ya
uwanjani pale macho yake makali yaliyompa daraja la juu kabisa jeshini katika medani
za shabaha yakasimama maeneno fulani yakizitazama kwa makini sura tofauti za wanausalama waliokuwa eneo lile. Kuziona sura hizo kukampelekea aachie msonyo
mwembamba wa hasira na kuhitimisha kwa tusi zito la chuki dhidi ya watu hao.
Mtu wa kwanza alikuwa Fulgency Kassy ambaye kwa wakati huu alikuwa
amesimama nyuma ya kundi la viongozi wa kisiasa waliofika kiwanjana pale. Mwingine
alikuwa Pweza ambaye yeye wakati huu alikuwa amesimama nyuma kabisa ya eneo
alilokaa amiri jeshi mkuu huku akizungumza na mwanamke fulani ambaye Koplo
Tsega hakuweza kumfahamu. Mtu wa mwisho alikuwa Kombe. Kombe alikuwa
amesimama upande wa kushoto wa eneo walilokuwako mabalozi wawakilishi wa
nchi zao hapa nchini Tanzania. Kombe alikuwa amevaa suti nadhifu nyeusi huku
macho yake yakijificha nyuma ya vioo vipana na vyeusi vya miwani ya jua sun goggles .
Njama yeye alikuwa amejitenga kando ya watu akiongea na simu nyuma ya gari moja
Landcruiser nyeupe. Wingine hakufanikiwa kuwaona.
Koplo Tsega aliendelea kuwatazama watu hao katika maeneo yao tofauti
waliosimama. Hata hivyo hakushtuka kabisa kuziona nyuso zao zikiwa na furaha
kana kwamba lile halikuwa tukio la kusikitisha kama watu wengine waliofika eneo lile
walivyokuwa wakionekana.
Nyuso za watu wale zilionekana kwa kila hali kufurahia kile kilichokuwa
kikisubiriwa kufanyika kiwanjani pale muda mfupi baadaye. Furaha katika msiba!...
Koplo Tsega akaendelea kuwaza huku akimeza funda kubwa la mate kuitowesha upya
hasira kali iliyoanza kuchipua kifuani mwake.
Kelele mbaya za ndege ya mapigano ya kijeshi aina ya Jet fighter 302 ya jeshi la
wananchi wa Tanzania zilianza kuhanikiza angani na hapo watu wote waliokuwa eneo
lile wakageuka na kuitazama ndege hiyo yenye sauti mbaya.
Muda mfupi uliyofuata ndege ile ya kijeshi yenye sauti mbaya ikatua pale kiwanjani
kwa kasi ya ajabu na mbwembwe za aina yake na kwenda kusimama kando ya kile
kikundi cha wanajeshi wa mapokezi waliojipanga katika mistari miwili minyoofu tayari
kuipokea miili ile.
Kitendo cha kutua kwa ndege ile kikawapelekea baadhi ya watu waliofika eneo
lile waanze kuangua kilio cha mayowe ya huzuni na hapo eneo lote likagubikwa na
simanzi ya aina yake.
Muda mfupi baada ya ndege ile kusimama itifaki za kijeshi zikaanza kufuatwa
katika ukimya wa aina yake. Mlango wa ndege ile ulipofunguliwa sura ya mwanaume
mrefu,mweusi na mwenye macho makali aliyevaa sare za jeshi ikachungulia kidogo
baada ya mlango wa ndege ile kufunguliwa na hatimaye mtu huyo kutoka.
Koplo Tsega akayapeleka macho yake kumtazama mwanaume yule mwenye umri
wa miaka hamsini na ushei na hapo akamkumbuka vizuri. Alikuwa ni Luteni Kanali
Ngozikavu Binamwamba. Kamanda mkuu wa vikosi vya jeshi la MONUSCO ama
muungano wa vikosi vya kijeshi kutoka nchi ya Tanzania,Afrika ya kusini na Matawi
vilivyopo kwenye harakati za kuleta amani ya kudumu nchini D.R Congo huko eneo
la mashariki na Kivu ya kaskazini.
Koplo Tsega akaendelea kumtazama kwa makini kamanda yule wa kijeshi wakati alipokuwa akishuka kwenye ndege ile kikakamavu sana tofauti kabisa na umri wake
na hapo akajikuta akitabasamu baada ya kukumbuka vizuri tabia ya ucheshi na roho
nzuri ya kamanda yule. Tabia nzuri zilizokuwa zikipingana na sura yake ya kikauzu
isiyokuwa na chembe ya huruma kwa askari jeshi yeyote mzembe kazini.
Pamoja na tofauti kubwa ya vyeo baina yao lakini Koplo Tsega na Luteni
Kanali Ngozikavu Binamwamba walikuwa marafiki wazuri sana huku Koplo Tsega
akimchukulia kamanda huyo wa kijeshi kama baba yake mzazi.
Urafiki wa Koplo Tsega na Luteni Kanali Ngozikavu Binamwamba ulianza pale
kamanda huyo wa kijeshi alipokuja kufahamu na hatimaye kushangazwa na uwezo
mkubwa wa Koplo Tsega katika kulenga shabaha baada ya faili lake la utendaji wa kazi
kuifikia ofisi yake wakati jina lake lilipopendekezwa na kujumuishwa kwenye orodha
ya askari jeshi wa Tanzania waliochaguliwa kutekeleza mpango wa amani ya kudumu
nchini D.R Congo. Tangu hapo wakawa marafiki wa chanda na pete kama ilivyokuwa
kwa baba na binti yake mpendwa.
Lakini wakati huu Koplo Tsega alimtazama Luteni Kanali Ngozikavu
Binamwamba katika mtazamo tofauti kabisa huku akijaribu kuvuta picha ya simanzi
ambayo kamanda yule wa kijeshi aliipata tangu pale alipopewa taarifa za kifo chake.
Koplo Tsega akajikuta akiwaza.
Mara baada ya Luteni Kanali Ngozikavu Binamwamba kushuka kwenye ile ndege
ya kijeshi huku akiwa ameongozana na maafisa wengine watano wa ngazi za juu
jeshini,majeneza matatu ya miili ya wanajeshi wa Tanzania yaliyofunikwa kwa bendera
ya taifa yakaanza kushushwa taratibu na kile kikundi cha askari jeshi wa mapokezi ya
heshima.
Majeneza yale yakapokewa kwa heshima zote na kile kikundi cha wanajeshi
waliokuwa wamejipanga katika mistari miwili minyoofu huku wakiacha nafasi ndogo
kati ya mstari na mstari. Nafasi ambayo ilichukuliwa na yale majeneza ambayo
wanajeshi wale waliyabeba mabegani mwao huku wakitembea kwa mwendo wa pole
kama itifaki za jeshi zilivyowataka.
Tukio lile likaambatana na kuhanikiza kwa sauti za vilio vya huzuni ya aina
yake kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki wa marehemu waliofika kiwanjani pale.
Wanajeshi wale wa mapokezi ya heshima wakaendelea kutembea mwendo wa pole
hadi walipoyafikisha majeneza yale ya askari wazalendo na kuyaweka mbele ya jukwaa
la amiri jeshi mkuu.
Bendi ya jeshi ilipomaliza kazi yake amiri jeshi mkuu akasimama na kuwasalimia
watu wote waliofika eneo lile huku akiwafariji wafiwa. Baada ya hapo akaanza kusoma
hutoba fupi lakini yenye ujumbe mzito kwa watu wenye mapenzi mema na wazalendo
wa nchi ya Tanzania. Huku akimalizia kwa kusoma wasifu wa wapiganaji wale ambao
miili yao sasa ilikuwa imefunikwa kwa bendera ya taifa.
Koplo Tsega akasikiliza kwa makini hotuba ile ya amiri jeshi mkuu wakati alipokuwa
akisoma wasifu wake kama ilivyokuwa kwa wale marehemu wengine wapiganaji. Hata
hivyo akajikuta akiuchukia wasifu ule pale alipohisi kuwa kila kilichokuwa kikisomwa hakikuwa sahihi na baadhi ya ukweli ulikuwa umefichwa. Hatimaye wasifu ule
ukamalizia kwa kusema
“Koplo Tsega! mpiganaji huyu hodari ameacha pengo kubwa jeshini lisiloweza kuzibika kwa
urahisi na kamwe hatutoacha kumkumbuka na kuuenzi mchango wake. Mungu na azilaze pema
peponi roho za mashujaa hawa wazalendo.
Wakati amiri jeshi mkuu akimalizia kusoma wasifu wa wapiganaji wale Koplo Tsega
alikuwa akiyatembeza macho yake kuwatazama wale watu aliokuwa akiwatazama pale
awali. Katika kufanya vile akagundua kuwa nyuso za watu wale zilikuwa na furaha
sana kana kwamba ule msiba haukuwa na maana yoyote kwao. Akasikitika sana na
kuzidi kuwalaani.
Hotuba ile ya amiri jeshi mkuu ilipofika kikomo taratibu nyingine za kijeshi
zikaanza kufuatwa ikifutiwa na watu waliofika eneo lile kuanza kutoa heshima zao
za mwisho.
Wakati wa kuaga ile miili majeneza mawili hayakufunuliwa. Jeneza la Meja Khalid
Makame lenyewe halikufunuliwa kwa kufuata taratibu za kidini na lile la Koplo Tsega
kwa kigezo kuwa mwili wake ulikuwa umeharibika sana. Hivyo ni jeneza la Sajenti
Chacha Marwa tu ndiyo lililofunuliwa kiwanjani pale na watu kuweza kutoa heshima
zao za mwisho.
Koplo Tsega akaendelea kutazama namna ambavyo mambo yalivyokuwa
yakiendelea eneo lile huku akitabasamu. Labda kitendo cha mtu kuhudhuria mazishi
yake mwenyewe,kusikia wasifu wake ukisomwa mbele ya halaiki ya watu na hatimaye
kuuaga mwili wake mwenyewe lilikuwa ni tukio la kwanza kuwahi kumtokea binadamu
duniani.
Amiri jeshi mkuu alikuwa wa kwanza kapita mbele ya majeneza ya wapiganaji wale
kutoa heshima zake za mwisho huku akiwa amefuatana na baadhi ya viongozi wake
wa juu serikalini. Kisha likafuata kundi la mabalozi wawakilishi na wageni wengine
wa kitaifa. Ndugu,jamaa na marafiki likawa kundi la mwisho kupita na kutoa heshima
zao.
Koplo Tsega alisimama kwa mbali huku akiwatazama watu wote waliokuwa
wakipita mbele ya yale majeneza kutoa heshima zao za mwisho. Simanzi ikamuingia
pale alipomuona mama yake mzazi na ndugu zake wakiwa hawajiwezi kwa kilio na
hivyo kusaidiwa na ndugu na marafiki wa karibu. Hali ile ikamtia huzuni kubwa Koplo
Tsega na kumpelekea ageuke na kutazama pembeni ili kuyazuia machozi yake.
Katika mstari ule wa watu waliokuwa wakipita mbele ya yale majeneza ili kutoa
heshima zao za mwisho kwa marehemu. Koplo Tsega pia aliweza kuwaona Fulgency
Kassy,Pweza na Kombe wakiwa wameongozana wakipita kutoa heshima zao
kando ya yale majeneza. Walipolifikia jeneza lake Koplo Tsega akawaona Fulgency
Kassy,Pweza na Kombe wakipeana ishara fulani na kusimama kidogo kando ya
jeneza lile wakilitazama kwa tabasamu la chinichini kabla ya kuendelea mbele.
Koplo Tsega akajikuta akitabasamu pale alipokumbuka kuwa jeneza lake halikuwa
limefunuliwa kwa kile kinachosemekana kuwa mwili wake ulikuwa ameharibika vibaya. Hivyo watu wale wakaishilia kuitazama picha yake ya kijeshi iliyokuwa imewekwa juu
ya jeneza lile. Lilikuwa ni tukio la kushangaza sana ambalo lilimuacha Koplo Tsega
akiendelea kutabasamu pale alipokuwa amesimama.
Zoezi lile la kuiaga miili ya marehemu lilipofika tamati lile jeneza lenye mwili wa
Meja Khalid Makame likabebwa na wale wanajeshi wa mapokezi na kurudishwa tena
kwenye ile ndege ya kijeshi tayari kwa kupelekwa nyumbani kwake huko kisiwani
Zanzibar kwa ajili ya mazishi. Yale majeneza mawili yaliyosalia yakabebwa na wanajeshi
na kuingizwa kwenye malori mawili ya kijeshi kisha baadhi ya wanajeshi wakapanda
huku wakifuatiwa na ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu tayari kusafirishwa.
Mwili wa Sajenti Chacha Marwa ulikuwa ukisafirishwa na kupelekwa kijijini kwao
Nyasicha wilaya ya Tarime mkoani Mara. Kwa vile mwili wa Koplo Tsega ulikuwa
unasemekana kuharibika vibaya hivyo ndugu wa marehemu walikuwa wamekubaliana
kuwa mazishi yake yangefanyikia katika makaburi ya Mwananyamala jioni ile ile mara
tu baada ya kutoka pale kiwanjani.
Koplo Tsega akaendelea kuwatazama ndugu,jamaa na marafiki waliokuwa
wakipanda lori lile la kijeshi lililoubeba mwili wake. Watu walikuwa wengi sana na
hali ile ikampa faraja kidogo kuwa angalau kulikuwa na watu waliokuwa wameguswa
na kifo chake. Msafara wa lile lori la kijeshi lililoubeba mwili wake kuelekea makaburi
ya Mwananyamala ulipoanza Koplo Tsega naye akaingia kwenye gari lake na kuunga
msafara kwa nyuma.
Kulikuwa na magari mengi sana yaliyokuwa yakiusindikiza mwili wake makaburini.
Baadhi ya magari yale akayakumbuka kuwa yalikuwa ni ya marafiki zake wa kazini na
mitaani na mengine yalikuwa ya ndugu zake waliokuwa wakiendelea kulia.
Koplo Tsega akiwa nyuma ya msafara ule wa mazishi ndani ya gari lake lenye vioo
tinted mara akaliona gari dogo aina ya Nissan Skyline jeusi likimpita kwa kasi na kwenda
kuunga msafara nyuma ya lile lori la jeshi lililobeba mwili wake. Kitendo cha kuliona
gari lile kikamjulisha kuwa Fulgency Kassy,Pweza Kombe na wanausalama wengine
walikuwa wamejigawa katika misiba ile bila shaka kufuatilia hadi chepe la mwisho la
udongo kwenye kaburi. Vioo vya lile gari jeusi lililompita havikuwa tinted hivyo ilikuwa
rahisi sana kumuona Pweza akiwa nyuma ya usukani wa gari hilo.
_____
SAA TISA KAMILI ALASIRI msafara wa mazishi ya Koplo Tsega ulihitimisha
safari yake katika makaburi ya Mwananyamala eneo la Kinondoni jijini Dar es
Salaam. Lori lile liliposimama jeneza lenye mwili wa Koplo Tsega likashushwa chini
na wanajeshi huku ndugu jamaa na marafiki wakishindwa tena kujizuia na kujikuta
wakiangua kilio kisichoelezeka.
Koplo Tsega akiwa nyuma ya msafara ule mara alipofika kwenye makaburi
yale akaegesha gari lake mbali kidogo na eneo lile la makaburini kisha akashuka na
kujichanganya kwenye kundi la watu waliofika eneo lile na kuelekea kule makaburini.
Idadi ya watu waliofika eneo lile la makaburini ilikuwa imeongezeka zaidi ukifananisha na kule kwenye kile kiwanja cha ndege walipotoka.
Macho ya Koplo Tsega yakasumbuka kidogo yakitazama huku na kule eneo lile
kabla ya kumuona Pweza akiwa amesimama hatua chache kando ya shimo la kaburi
katika mwonekano wa suti yake nadhifu nyeusi huku akiwa amevaa miwani ya jua.
Koplo Tsega akatembea taratibu akielekea kwenye eneo lile la maziko na
wakati akifanya hivyo mara akamuona mama yake mzazi akiwa hoi kwa kulia huku
ameshikiliwa na wanajeshi wawili wanawake ambao haraka aliwatambua kuwa
walikuwa ni Koplo Salma na Sajenti Kiege,marafiki zake wa kazini.
Kaka yake alikuwa amesimama upande wa kushoto wa lile shimo la kaburi huku
mara kwa mara akijifuta machozi kwa kitambaa chake cha leso alichokuwa amekishika
mkononi. Pembeni yake alikuwa amesimama Dan,rafiki wa kaka yake wa siku nyingi.
Dada zake wawili Loth na Tsion walikuwa wamepoteza fahamu mara mbili kabla ya
kukimbizwa hospitali.
Mara baada ya jeneza la Koplo Tsega kushushwa na kusogezwa karibu na lile
kaburi watu wote eneo lile wakaombwa kutulia na hapo mchungaji wa kanisa akaanza
kutoa neno fupi la kuwafariji wafiwa huku akiwataka watu wote waliofika eneo lile
kutubu dhambi zao na kumrudia Mungu. Huku mchungaji huyo akiyafananisha
maisha ya mwanadamu na saa ya ukutani isiyojulikana muda wa kusimama kwake.
Mchungaji yule alipomaliza kutoa neno lake fupi kwa watu waliofika eneo lile
taratibu za mazishi ya kijeshi zikafuatia na hapo vilio vikaanza kusikika tena huku
ndugu jamaa na marafiki wakipata nafasi ya kutupia udongo ndani ya kaburi lile kama
sehemu ya kuhitimisha safari ya mwisho ya Koplo Tsega hapa duniani.
Pweza alikuwa miongoni mwa watu waliotupia udongo kwenye kaburi lile mara
baada ya jeneza la Koplo Tsega kuteremshwa mle shimoni kwa kamba na wanajeshi
waliokuwa eneo lile. Ushiriki wa Pweza ulikuwa wa kiwango cha juu kupita hata na
ndugu wa karibu wa marehemu na marafiki waliofika eneo lile huku yeye akitupia
machepe mengi zaidi ya udongo yasiyo na idadi. Pweza alipomaliza kutupia udongo
kwenye kaburi akamsogelea mama wa Koplo Tsega na kumpa mkono wa pole.
Saa kumi na moja na nusu jioni ilipotimia mazishi ya mdunguaji hatari Koplo
Tsega yakawa yamefikia ukomo huku wanajeshi wenzake wakifyatua risasi kadhaa
hewani kuhitimisha safari ya wenzao.
Kwa kuwa wingu zito la mvua lilikuwa limetanda angani hivyo mara tu mazishi
yale yalipofika tamati watu wakaanza kutawanyika haraka kuikwepa mvua ile kubwa
iliyokuwa ikijiandaa kunyesha. Pweza alikuwa miongoni mwa watu wale kwani
mara tu baada ya mazishi yale kuisha akaelekea sehemu alipoegesha gari lake kisha
akafungua mlango kuingia ndani. Muda mfupi uliyofuata simu yake ya kiganjani
ilikuwa hewani ikitafuta mtandao na simu hiyo alipopokelewa upande wa pili Pweza
hakusita kuonesha furaha yake.
“Kazi kwisha mkuu!” Pweza akaongea huku akiangua kicheko hafifu.
“Vipi mazishi yake?” sauti ile upande wa pili wa simu ikauliza.
“Watu ni wengi sana kama Kanumba” Pweza akaongea huku akishindwa kuificha furaha yake.
“Una hakika kuwa umefika hadi makaburini?” ile sauti ya upande wa pili ikauliza
tena.
“Hivi ninavyozungumza na wewe bado nipo eneo la makaburi ya Mwananyamala
na amini usiamini huwenda mimi nikawa mtu wa kwanza kwa kutupia idadi kubwa ya
machepe mengi ya udongo kwenye kaburi lake”
“Waandishi wa habari walikuwepo?” ile sauti ikauliza tena
“Walikuwepo lakini hawana madhara”
“Safi sana! njoo na picha za tukio zima unitoe shaka. Sitaki yale mambo ya Daudi
Balali” yule mtu akasisitiza huku akiangua kicheko hafifu.
“Sawa mkuu!” Pweza akaitika kwa mashaka kidogo baada ya kukumbuka
kuwa alikuwa hajachukua kielelezo chochote cha ushahidi wa mazishi yale. Kwa
kulikumbuka suala hilo Pweza akafungua dashibodi ya gari na kuchukua kamera
yake ndogo ya digital yenye nguvu za ajabu katika uchukuaji wa picha kisha akafungua
mlango wa gari na kushuka akielekea kule makaburini.
Manyunyu hafifu ya mvua yaliyokuwa yameanza kuanguka kutoka angani
yakampelekea Pweza aharakishe hatua zake huku akililaani giza hafifu lililokuwa
limeanza kuingia. Pweza alikuwa akiikumbuka vizuri sehemu lilipokuwa lile kaburi la
Koplo Tsega ambaye mazishi yake yalikuwa yamefanyika muda mfupi uliyopita. Watu
wote walikuwa wametawanyika eneo lile hivyo eneo lote la makaburi yale lilikuwa
limemezwa na ukimya wa kipekee.
Wakati Pweza alipokuwa akilifikia kaburi la Koplo Tsega mara kitu fulani
kikawa kimemvutia. Pembeni ya kaburi lile alikuwa amesimama mwanamke fulani.
Mwanamke huyo mwembamba kiasi na mrefu mwenye umbo la kuvutia alikuwa
amevaa miwani myeusi machoni na mwili mzima alikuwa amejifunika mavazi meusi
hivyo mtu yeyote asingeweza kumtambua kwa urahisi. Mwanamke huyo alikuwa
amesimama kwa heshima zote akilitazama lile kaburi kama mtu aliyekuwa kwenye
hisia kali za kumpoteza mpendwa wake.
“Habari yako dada?” Pweza aliwahi kumsalimia yule mwanamke hata hivyo
hakujibiwa badala yake yule mwanamke akageuka na kumtazama Pweza kisha
akatingisha kichwa chake akiitikia ile salamu.
“Kifo chake kimetugusa wengi!” Pweza akaendelea kuongea bila kujibiwa huku
akishangazwa na uwepo wa mwanamke yule peke yake katika mazingira kama yale.
Yule mwanamke aliyesimama kando ya lile kaburi alikuwa ni Koplo Tsega. Mara
baada ya mazishi yale kufika tamati na watu wote kutawanyika Koplo Tsega alikuwa
ameitumia nafasi ile kuomboleza na kutoa heshima zake za mwisho kwa rafiki yake
mpendwa na mpiganaji hodari wa jeshi la wananchi wa D.R Congo,Private Gina
Yhombi-Opango Makiadi codename Lovebird. Ambaye mwili wake ndiyo uliyokuwa
ndani ya lile jeneza ingawa hadi wakati huu watu walikuwa wakiamini kuwa ule
mwili uliokuwa ndani ya lile jeneza kutoka D.R Congo ulikuwa ni wa Koplo Tsega
komandoo na mdunguaji hatari wa jeshi la wananchi wa Tanzania.Koplo Tsega akakumbuka namna alivyobadili gwanda zake na kumvalisha Lovebird
kule msituni nchini D.R Congo na hivyo kuwafanya watu waamini kuwa mwili ule
uliyokuwa ndani ya lile jeneza ulikuwa ni wa Koplo Tsega.
Makosa makubwa bila shaka yalikuwa yamefanyika katika kufanya utambuzi
makini wa ule mwili. Mtu yoyote aliyekuwa wa kwanza kuiona maiti ya Lovebird kule
msituni bila shaka hakutaka kufanya uchunguzi mara mbili kwani mwili wa Lovebird
ulikuwa na magwanda ya kijeshi yenye utambulisho wa Koplo Tsega na beji ya taifa la
Tanzania. Hivyo hatimaye mahesabu yalikuwa yamekaa vizuri.
Koplo Tsega aligeuka tena kumtazama yule mtu aliyemsemesha pale makaburini
na kitendo cha kumuona tena Pweza eneo lile moyo wake ukamlipuka ghafla hata
hivyo akajitahidi kwa kila hali kuumeza mshtuko. Koplo Tsega hakusema neno lolote
kwa kukwepa sauti yake kushtukiwa na Pweza badala yake akauinua mkono wake
kidogo na kupunga hewani akiashiria kuwa alikuwa kwenye majonzi ya hali ya juu
huku akishindwa kuelewa ni kwa nini Pweza alikuwa amerudi tena pale kaburini baada
ya watu wote kutawanyika.
Wakati Koplo Tsega akitafakari mara akakumbuka kuwa bastola yake ilikuwa ndani
ya pochi yake ndogo ya mkononi na hapo akaanza kupiga mahesabu ya haraka ya
namna ya kuifikia bastola ile na kumzimisha Pweza pale pale kaburini kabla hajabadili
mawazo na kuondoka. Koplo Tsega akavuta pumzi taratibu huku akimtazama Pweza
kwa jicho la pembe. Pweza akamtazama kidogo yule mwanamke kisha akachukua
kamera ndogo ya digital kutoka mfukoni na kuanza kulizunguka lile kaburi taratibu
katika namna ya kupata picha tofauti za kaburi lile. Pweza akalifanya zoezi lile kwa
muda mfupi sana na hivyo kumnyima nafasi nzuri Koplo Tsega kuifikia bastola yake
mafichoni.
“Pole sana dada yangu Mungu na akutie nguvu. Koplo Tsega alikuwa mtu
muhimu sana kwetu lakini kwa sasa hatunaye tena. Sisi tulimpenda lakini Mungu
amempenda zaidi” Pweza akaongea huku akiitia mfukoni ile kamera yake. Koplo
Tsega akageuka kidogo na kumtazama Pweza kisha akatingisha tena kichwa chake
akionesha kukubaliana na hoja ile.
Koplo Tsega akiwa anamvizia Pweza ageuke ili apate nafasi nzuri ya kutimiza
lengo lake akajikuta akighairi kufanya hivyo baada ya kuliona kundi kubwa la vijana
waliotoka mpirani wakikatisha pale makaburini. Hivyo ikabidi awasubiri kwanza vijana
wale wapite eneo lile lakini wakati akifanya hivyo Pweza akamuaga kwa kumpungia
mkono huku akielekea sehemu alipoegesha gari lake mbali na eneo lile. Koplo Tsega
hakuwa na jinsi hivyo ikabidi na yeye ampungie mkono Pweza akimuaga huku kooni
akiwa ameshikwa na donge la hasira.
Wakati wale vijana wakimaliza kukatisha kwenye lile eneo la makaburi Pweza
alikuwa amekwishatoweka eneo lile. Koplo Tsega akabaki amesimama pale makaburini
huku akililaani tukio lile. Mvua iliyoonza kunyesha hatimaye ikamfanya aondoke
taratibu eneo lile akielekea sehemu alipoegesha gari lake. Muda mfupi uliyofuata
alikuwa mbali na eneo lile.
 
Kama nilivyoahidi hapo jana kuwa mwandishi wetu wa riwaya ya mtutu wa bunduki ameniomba niwajulishe kuwa adithi yetu itaendelea kuanzia ijumaa ijayo. Hii inatokana na kutingwa na majukumu mengine katika ujenzi wa taifa. Lakini pamoja na hayo amenipa jukumu la kuwaletea riwaya yake ya MIFUPA 206. Nawaomba muwasiliane na mtunzi kwa namba
0688058669 kwa ajiri ya kupata nakala za vitabu vifuatavyo
1.Tai kwenye mzoga (hiki nacho nitakileta humu mpaka nitakavyoelekezwa tofauti na mtunzi)
2.Msitu wa madagascar
3.Mifupa 206
Nawaomba tuthamini kazi za watunzi wetu kwa kuwaunga mkono kwa kununua kazi zao ili wafaidi matunda ya vipaji vyao. Twende kazi.......
Mods naomba mnisaidia kuexpand hiyo attachment ambayo ni cover ya kitabu
mkurugenz mpondaaa..hadi huku..kweli unapambanisha
 
FUKUTO KALI LA JOTO LA JIJI LA DAR ES SALAAM likampelekea Zera
aendelee kufurahia maji baridi yaliyokuwa yakitiririka kwenye bomba la bafuni
kwake nyuma ya kioo kikubwa cha kujitazama. Muda wowote baada ya pale
mvua kubwa ingeweza kunyesha na hiyo ingekuwa nafuu kubwa kwa wakazi wa jiji
la Dar es Salaam. Zera akageuka tena na kujitazama kwenye kioo kikubwa cha mle
bafuni na hapo tabasamu jepesi likapita usoni mwake. Kwa mara nyingine taswira ya
umbo lake zuri ilikuwa imefufua upya hisia zake.
Kupitia taswira iliyofanyika kwenye kioo kile Zera akafurahishwa na michirizi
ya maji ya bomba yaliyokuwa yakichuruzika taratibu mwilini mwake. Michirizi hiyo
ya maji ikianzia kichwani halafu mabegani na kisha kifuani ikiziburudisha chuchu
zake laini halafu ikaendelea kushuka chini sehemu ya kiunoni mapajani na kumalizia
miguuni. Zera alijifahamu kuwa alikuwa msichana mzuri sana na kamwe hakuchoka
kujitazama kwenye kioo kila alipopata nafasi hiyo.
Kama kungelikuwa na kazi nyingine yenye kipato chenye afya Zera alikuwa tayari
kuacha kazi ya kujiuza mwili wake kwa wanaume kule Vampire Casino ili aendelee
kuulinda uzuri wake kwa miaka mingi zaidi huku akifurahishwa na kuweweseka kwa
nyoyo za mwanaume kila wamwonapo. Lakini suala hilo hadi wakati huu lilikuwa
limeshindikana kabisa. Pamoja na uzuri aliokuwa nao lakini kazi nyingi zenye
mishahara mikubwa jijini Dar es Salaam ziliwahitaji wasomi mwenye elimu za vyuo
vikuu wakati yeye alikuwa ameishia elimu ya darasa la saba huko kijijini kwao mkoani
Singida.
Kama ilivyokuwa kwa vijana wengi wenye kupenda maisha mazuri ya haraka Zera
hatimaye akatoroka nyumbani kwao kijijini na kukimbilia jijini Dar es Salaam baada
ya kushawishiwa na marafiki waliokuwa wakirudi mara kwa mara kijijini kwao na hali
nzuri za maisha.
Alipofika jijini Dar es Salaam Zera akagundua kuwa hali ya maisha ilikuwa tofauti
kabisa na vile alivyokuwa akifikiri. Marafiki zake wote walikuwa wakiendesha maisha
kwa kujiuza miili yao katika sehemu za starehe na kumbi mbali mbali za za starehe
jijini Dar es Salaam. Zera akawalaani kwa vitendo vile na kukataa kuambatana nao.
Lakini halikuwa jambo rahisi kwani huduma zote muhimu kama chakula,malazi na
matibabu alikuwa akiwategemea wao.
Marafiki hatimaye wakamchoka na hivyo maisha yakazidi kumuwia magumu.
Ukali wa maisha ya jiji la Dar es Salaam bila kazi bila ndugu ukamshinikiza Zera
na hapo taratibu akaanza kuambatana na marafiki kwenye biashara yao ya ukahaba
huku akijifunza mbinu mpya na vichochoro vya jiji la Dar es Salaam. Baada ya miezi
michache kupita Zera akageuka na kuwa kahaba mashuhuri huku wateja wake
wakubwa wakiwa ni wanaume wenye vipato vya juu.
Tangu alipoanza kufanya biashara ya ukahaba jijini Dar es Salaam alikiri kuwa
hakuwahi kukutana na mwanaume yoyote aliyetokea kuugusa moyo wake kama
ilivyokuwa kwa Stephen Masika. Yule mwanaume aliyeonana naye kule Vempire
casino usiku wa jana. Uzuri wa Stephen Masika,ucheshi na utanashati wake vilikuwa
vimempelekea Zera usiku mzima ajikute akiweweseka kitandani kumuwaza
mwanaume yule utasema hakuwahi kulala na mwanaume yoyote.
Zera alipoamka asubuhi akaanza kufanya ile kazi aliyopewa na Stephen Masika ya
kupeleleza mahali alikokuwa akiishi Milla Cash. Kazi ilikuwa rahisi tu kwani ilipofika
saa nne asubuhi Zera alikuwa amepata taarifa zote muhimu kupitia kwa marafiki zake
aliyoongea nao kwa njia ya simu.
Muda wa masaa machache baadaye Zera alikuwa amepanga kumpigia simu
Stephen Masika na kumtaka waonane ili aweze kumpa taarifa alizozipata.
Kumbukumbu ya taswira ya Stephen Masika ikiwa inaendelea kuzitongoza fikra
zake Zera akajikuta akizidi kumpenda mwanaume huyo aliyeonekana mkwasi na
mzuri wa aina yake kuwahi kumuona jijini Dar es Salaam.
Zera alipomaliza kuoga akafungua mlango wa bafu na kutoka nje akielekea
chumbani kwake huku akiwa amejifunga taulo kiunoni katika nyumba ile aliyopanga
yenye vyumba viwili vya kulala,sebule na jiko.
Simu iliyoanza kuita ikamkumbusha Zera kuwa kabla ya kwenda kuoga alikuwa
ameiacha simu yake kwenye kochi sebuleni. Hivyo akaelekea kule sebuleni simu ile
ilipokuwa ikiita. Mara alipoichukua simu ile na kuitazama akashangaa kuiona namba
mpya ikiita hata hivyo Zera hakusita kuipokea simu ile huku maswali mengi yakipita
kichwani mwake.
“Hujambo mpenzi?” sauti nzito ya kiume iliongea kwa utulivu upande wa pili
wa simu ile. Zera akaituliza akili yake huku akijaribu kuitathmini sauti ile hata hivyo
ilikuwa sauti ngeni kabisa masikioni mwake.
“Sijambo nani mwenzangu?” hatimaye Zera akauliza kwa utulivu.
“Nahitaji kuonana na wewe mrembo” ile sauti ya mtu wa upande wa pili wa simu
ikaongea kwa utulivu ikilipuuza swali la Zera.
“Naongea na nani?” Zera akauliza tena
“Mteja wako”
“Mteja wangu nani?”
“Usijali Zera utanikumbuka utakaponiona. Chungulia nje utaliona gari jeusi.
Nimemtuma dereva wangu aje kukuchukua mimi utanikuta ufukwe wa Coco beach” ile
sauti ya upande wa pili wa simu ikazungumza kwa utulivu. Zera akaisikiliza sauti ile kwa
makini huku akisogea dirishani na kusogeza pazia akitazama nje kupitia uwazi mdogo
ulikuwa baina ya geti la nyumba ile na ukuta. Kwa kufanya hivyo Zera akaliona gari
dogo jeusi limesimama mbele ya geti lile.
“Sikiliza kaka mimi siwezi kuja kwa mtu nisiyemfahamu istoshe nakaribia kuingia
kazini” Zera akaongea kwa tahadhari.
“Kazi gani unayoiwahi mrembo tofauti na hii ninayokuitia yenye malipo mazuri
au hutaki tufurahi pamoja mpenzi. Ningekuwa nataka kukupotezea muda wako
nisingemtuma dereva wangu akufuate nyumbani” ile sauti ya upande wa pili iliongea
na hapo Zera akasogeza tena lile pazia dirishani na kutazama nje. Lile gari jeusi bado
lilikuwepo.
“Kuna mtu nahitaji kuonana naye jioni hii hivyo nahisi huwenda nikachelewa
nikija huko”
“Usijali dereva wangu atakurudisha mapema zaidi” ile sauti kwenye simu
ikaendelea kusisitiza.
Zera akatulia kidogo akitafakari kisha akachukua karatasi na kalamu vilivyokuwa
chini ya meza ndogo iliyokuwa pale sebuleni na kuanza kuandika jina la hoteli yenye
ufukwe aliyotajwa na mtu yule kwenye simu kama sehemu ya kumbukumbu baada ya
simu ile kukatwa.
Muda mfupi baada ya simu ile kukatwa Zera alikuwa chumbani kwake akijiandaa
huku mawazo mwengi yakipita kichwani mwake. Alipomaliza akatoka nje na kufunga
mlango. Lile gari jeusi bado lilikuwa nje ya geti la ile nyumba na Zera alipofika dereva
wa gari akamfungulia mlango na kumtaka aingie.
Dereva wa gari lile alikuwa kijana mrefu kiasi mwenye mwili imara huku akiwa
amevaa suti nadhifu ya rangi ya kijivu. Dereva yule akamtazama Zera kwa makini
wakati akiingia kwenye gari huku tabasamu jepesi likipita usoni mwake. Mlango wa
gari ulipofungwa safari ikaanza. Dereva wa gari lile alikuwa Pweza na wakati huu
alikuwa akifurahi namna mambo yalivyokuwa yakienda.
Gari lilipoingia barabara ya Morocco likashika uelekeo wa upande kulia kama
linaloelekea eneo la Magomeni lakini baada ya safari ya kitambo kifupi gari hilo
likakunja kona upande wa kutosho likiifuata barabara ya Kinondoni. Wakati safari
ikiendelea Zera alikuwa akimtaza Pweza huku mawazo mengi yakipita kichwani
mwake. Pweza hakuzungumza kitu chochote badala yake aliendelea kuendesha gari
huku mara kwa mara akirekebisha redio ya gari iliyokuwa mle ndani.
Baada ya safari ndefu wakajikuta wametokezea katika makutano ya barabara ya
Kinondoni na ile barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Walipofika kwenye makutano yale
Pweza akaingia upande wa kulia halafu baada ya safari fupi akakunja kona kuingia
upande wa kushoto akiifuata barabara ta Kenyatta drive. Walipoingia kwenye barabara
ile wakawa wakiiona bahari ya Hindi kwa upande wa kulia halafu walipofika mbele
kidogo wakaingia barabara ya Toure drive huku bahari ya Hindi wakiendelea kuiona
upande wa kulia kwa baadhi ya maeneo.
Mandhari ya bahari ya Hindi kwa wakati huu yalikuwa yakivutia sana. Upepo
mwanana wa bahari ulivuma na kupelekea starehe ya aina yake kwa msafiri wa
barabara ile ya Toure drive. Meli ndogo na kubwa zilionekana kutia nanga katika
baadhi ya maeneo huku majengo marefu ya hoteli na majumba makubwa ya kifahari
yakichomoza katikati ya vichaka vya miti ya fukwe ya bahari.
Pweza akiwa anafahamu vizuri wapi walipokuwa wakielekea aliendelea kuingiza
gia na kukanyaga mafuta. Baada ya muda wakawa wamefika eneo fulani lisilokuwa
na makazi ya watu huku barabara ile ikikatisha katikati ya msitu wa miti ya mikoko.
Walipofika eneo lile Pweza akapunguza mwendo na kukata kona kuingia upande wa
kulia sehemu kulipokuwa na njia hafifu ya nyasi iliyoonekana kutelekezwa kwa muda
mrefu bila kutumika.
Zera akashtukia baada ya kuona gari lile likishika uelekeo ule kwani kulikuwa na
kila dalili kuwa kule mbele hapakuwa na hoteli wala makazi ya watu na hali ile ikazidi
kumpa mashaka zaidi.
“Huku tunaelekea wapi?” Zera akauliza kwa mashaka
“Usihofu tumekaribia kufika” Pweza akaongea huku akionekana kulipuuza swali
la Zera.
“Lakini ufukwe wa Coco beach haupo huku?” Zera akazidi kuongea huku wasiwasi
ukianza kumuingia.
“Subiri na baada ya muda mfupi utaona” Pweza akasisitiza huku akizidi kushuka
na ile barabara hafifu ya nyasi.
Muda mfupi baadaye gari lile lilikwenda na kusimama katikati ya kichaka hafifu
cha miti ya mikoko na hapo Pweza akafungua mlango wa gari na kushuka. Wakati
akilizunguka lile gari upande wa pili akatumia fursa ile kuichomoa bastola yake Glock
32 kutoka kwenye koti lake la suti. Alipoufikia ule mlango wa nyuma wa gari alipoketi
Zera akaufungua huku bastola yake ikiwa mkononi. Mlango ulipofunguka Zera
akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola na hapo moyo wake ukamlipuka kwa
hofu.
“Shuka chini tumefika” Pweza akaongea lakini Zera akashtuka kuwa sauti ya
Pweza ilikuwa haina urafiki.
“Unataka kunifanya nini?” Zera akauliza kwa hofu huku akihisi hatari mbele yake.
“Bado hatujafika,sehemu ya safari yetu iliyobaki tutaimaliza kwa miguu” Pweza
akaongea kwa utulivu.
“Sishuki!...” Zera akaongea kwa hofu na kabla hajamalizia Pweza akamrukia na
kumzaba makofi mawili ya nguvu yaliyompelekea Zera ajihisi kuchanganyikiwa huku
akitema damu kisha Pweza akamshika mkono na kumvuta nje
“Sikiliza wewe kahaba! kuanzia sasa utafuata kile nitakachokueleza na usithubutu
kuleta hila yoyote kwani tambua kuwa sitokuvumilia. Ongeza mbele!” Pweza akafoka
huku amemkwida Zera kwa nyuma na bastola yake mkononi. Safari ya kushuka eneo
la chini la ile fukwe ikaanza huku Zera akitangulia mbele na pale alipotaka kuleta
upinzani akajikuta akikabiliana na kipigo.
Waliendelea kushuka kule chini na baada ya muda mfupi wakawa wametokezea
kwenye ufukwe mpana wa bahari ya Hindi. Ulikuwa ni mwendelezo wa ufukwe
mrefu wa bahari lakini usiokuwa na dalili za uwepo wa kiumbe hai chochote eneo lile
mbali na wanaume wawili ambao waliwakuta wakiwasuburi kule chini. Wanaume hao
walikuwa ni Fulgency Kassy na Kombe. Zera kuwaona watu wale kukazidi kumtia
hofu.
Pweza, Fulgency Kassy na Kombe walikuwa wameshirikiana katika kusuka
mpango mzuri wa kumnasa Zera mara tu baada ya kutoka kule Vampire Casino usiku
wa jana. Namba za simu ya Zera walikuwa wamezipata kupitia kwa yule meneja wa
Vampire Casino.
Kulikuwa na umbali mrefu kutoka kule ilipokuwa hoteli ya kifahari ambayo hapo
awali Zera alipopigiwa simu alikuwa ameahidiwa na yule mtu kuwa wangeonana
kwenye hoteli ile. Lakini katika ufukwe huu uliojitenga hapakuwa na dalili zozote
za uwepo wa mtu mwingine zaidi ya wale watu hatari na wala fukwe yenyewe
haikuonekana kufanyika shughuli zozote za kibinadamu. Kitendo cha Zera kumuona
Kombe akiwa ametundika chepe begani kikazidi kumwogopesha na hapo machozi
yakaanza kumtoka.
“Mfunge kamba hatuna muda wa kupoteza hapa” Flugency Kassy akamwambia
Kombe na hapo Kombe akaweka chepe lake pembeni na kumshika Zera. Zoezi la
kumfunga kamba Zera likafanyika kwa muda mfupi huku Zera akifungwa mikono
na miguu kama mnyama anayetayarishwa kuchinjwa na pale alipoleta ukorofi
akajikuta akiambulia kipigo cha nguvu. Kombe alipomaliza kumfunga kamba Zera
akamnyanyua Zera kama gunia na kujitwisha begani halafu wote wakaanza kutembea
taratibu wakielekea upande wa kulia wa fukwe ile. Baada ya hatua chache za safari
ile wakawa wametokezea kwenye sehemu nyingine ya fukwe iliyopakana na kichaka
kizito cha miti ya mikoko.
“Mshushe chini“ Fulgency Kassy akamwambia Kombe na hapo Kombe
akambwaga Zera chini kama gunia. Zera akapiga yowe kali la maumivu lakini hakuna
mtu aliyeonekana kumjali.
“Sikiliza wewe kahaba hivi unafahamu kwanini upo hapa?” Fulgency Kassy
akafoka huku akikiinua kichwa cha Zera ili waweze kutazamana vizuri
“Mnataka nini kwangu nyinyi wauaji?” Zera akaongea kwa hasira na hapo
Fulgency Kassy akamchapa kofi zito usoni.
“Funga mdomo wako wewe kahaba”
“Niueni tu si ndiyo mlivyopanga!” Zera akaongea kwa kinyonge huku damu
nyingi ikimtoka mdomoni baada ya kuchapwa makofi ya nguvu mfululizo.
“Tuambie huyu mtu anayeitwa Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani
wakati alipokuja kuonana na wewe kule Vampire Casino?” swali la Fulgency Kassy
likampelekea Zera ashikwe na mshangao.
“Mimi sielewi mnazungumza nini!” Zera akaongea kwa kulalama
“Tunajua kuwa unamfahamu ndiyo maana tukakuleta hapa. Kama utatupa
ushirikiano wa kutosha tutakurudisha nyumbani kwako ukiwa salama lakini kama
utaendelea na msimamo wako tutakulazimisha utuambie kwa namna nyingine
ambayo ni hatari zaidi” Fulgency Kassy akaongea kwa hasira.
“Kweli mimi sifahamu chochote” Zera akaongea kinyonge huku akimkumbuka
yule mwanaume aliyeonana naye usiku wa jana kwenye kile chumba kule Vampire
Casino aliyejitambulisha kwa jina la Stephen Masika.
“Tunataka utueleze vizuri kuhusu yule mtu uliyeonana naye jana usiku kule casino.
Mtu yule ni nani na alikuwa na shida gani mle ndani?” Kombe akaongea kwa msisitizo.
“Tuambie na usithubutu kutuficha kwani yule mtu ni hatari na ndiye aliyehusika
na kifo cha yule mlinzi kule casino” Pweza akasisitiza.
“Nyinyi ni akina nani?’ badala ya kuwajibu Zera akawauliza huku akiyatembeza
macho yake kuwatazama na hapo wote wakatabasamu kwa hasira.
“Askari wa usalama” Fulgency Kassy kaongea kivivuvivu huku akitazama
pembeni.
“Sasa kama nyinyi ni askari mbona hapa siyo kituo cha polisi?” Zera akauiliza kwa
mashaka.
“Hilo siyo kazi yako wewe jibu swali uliloulizwa” Pweza akaongea kwa hasira.
“Mimi sijui chochote” Zera akaongea kwa utulivu. Fulgency Kassy hakusema
neno badala yake akamgeuki Kombe na kumwambia
“Hebu mueleweshe vizuri huyu kahaba naona bado hajatuelewa”
Maelezo yale yakaambatana na kichapo cha nguvu huku Zera akishindiliwa
makonde na makofi mazito ya Kombe na Pweza kila mahali. Hali yake ilipoanza kuwa
mbaya Fulgency Kassy akaingilia kati na kuwataka wasitishe.
“Hebu mwacheni huwenda sasa yupo tayari kutueleza” Kombe na Pweza
wakaacha kumshushia kipigo Zera na hapo Fulgency Kassy akamsogelea Zera na
kuinama karibu yake akianza kuongea kwa utulivu.
“Unajua ni kwanini tumekuleta kwenye hii fukwe. Hapa ni sehemu tulivu zaidi
tunapoweza kukuua pasipo mtu yeyote kufahamu wala sauti yako kusikika hivyo
usijidanganye kuwa msimamo wako utakusaidia. Hebu tuambie Stephen Masika ni
nani na alikuwa na shida gani mle ndani casino?”
“Mteja wangu” Zera akaongea kwa unyonge huku macho yamemtoka kwa hofu
“Mteja wako!...” Pweza akadakia ”Sasa mbona hukutuambia mapema tulipoanza
kukuuliza”
“Unaweza kutueleza ni kwa nini ulipopigiwa simu usiku ule kuulizwa kama
ulikuwa na mwanaume yeyote chumbani kwako ulikataa kusema ukweli?” Pweza
akauliza kwa hasira.
“Tuambie huyu mtu anayeitwa Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani
wakati alipokuja kuonana na wewe kule Vampire Casino?” swali la Fulgency Kassy
likampelekea Zera ashikwe na mshangao.
“Mimi sielewi mnazungumza nini!” Zera akaongea kwa kulalama
“Tunajua kuwa unamfahamu ndiyo maana tukakuleta hapa. Kama utatupa
ushirikiano wa kutosha tutakurudisha nyumbani kwako ukiwa salama lakini kama
utaendelea na msimamo wako tutakulazimisha utuambie kwa namna nyingine
ambayo ni hatari zaidi” Fulgency Kassy akaongea kwa hasira.
“Kweli mimi sifahamu chochote” Zera akaongea kinyonge huku akimkumbuka
yule mwanaume aliyeonana naye usiku wa jana kwenye kile chumba kule Vampire
Casino aliyejitambulisha kwa jina la Stephen Masika.
“Tunataka utueleze vizuri kuhusu yule mtu uliyeonana naye jana usiku kule casino.
Mtu yule ni nani na alikuwa na shida gani mle ndani?” Kombe akaongea kwa msisitizo.
“Tuambie na usithubutu kutuficha kwani yule mtu ni hatari na ndiye aliyehusika
na kifo cha yule mlinzi kule casino” Pweza akasisitiza.
“Nyinyi ni akina nani?’ badala ya kuwajibu Zera akawauliza huku akiyatembeza
macho yake kuwatazama na hapo wote wakatabasamu kwa hasira.
“Askari wa usalama” Fulgency Kassy kaongea kivivuvivu huku akitazama
pembeni.
“Sasa kama nyinyi ni askari mbona hapa siyo kituo cha polisi?” Zera akauiliza kwa
mashaka.
“Hilo siyo kazi yako wewe jibu swali uliloulizwa” Pweza akaongea kwa hasira.
“Mimi sijui chochote” Zera akaongea kwa utulivu. Fulgency Kassy hakusema
neno badala yake akamgeuki Kombe na kumwambia
“Hebu mueleweshe vizuri huyu kahaba naona bado hajatuelewa”
Maelezo yale yakaambatana na kichapo cha nguvu huku Zera akishindiliwa
makonde na makofi mazito ya Kombe na Pweza kila mahali. Hali yake ilipoanza kuwa
mbaya Fulgency Kassy akaingilia kati na kuwataka wasitishe.
“Hebu mwacheni huwenda sasa yupo tayari kutueleza” Kombe na Pweza
wakaacha kumshushia kipigo Zera na hapo Fulgency Kassy akamsogelea Zera na
kuinama karibu yake akianza kuongea kwa utulivu.
“Unajua ni kwanini tumekuleta kwenye hii fukwe. Hapa ni sehemu tulivu zaidi
tunapoweza kukuua pasipo mtu yeyote kufahamu wala sauti yako kusikika hivyo
usijidanganye kuwa msimamo wako utakusaidia. Hebu tuambie Stephen Masika ni
nani na alikuwa na shida gani mle ndani casino?”
“Mteja wangu” Zera akaongea kwa unyonge huku macho yamemtoka kwa hofu
“Mteja wako!...” Pweza akadakia ”Sasa mbona hukutuambia mapema tulipoanza
kukuuliza”
“Unaweza kutueleza ni kwa nini ulipopigiwa simu usiku ule kuulizwa kama
ulikuwa na mwanaume yeyote chumbani kwako ulikataa kusema ukweli?” Pweza
akauliza kwa hasira
“Tuambie huyu Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani mle ndani”
Fugency Kassy akauliza huku akionekana kuanza kuchoshwa na hali ile.
“Alikuwa mteja wangu!” Zera akaongea kinyonge.
“Kwa nini ulificha pale ulipoulizwa?” Kombe akauliza lakini Zera hakuwa na jibu.
Fulgency Kassy akamtazama Zera kwa hasira kisha akageuka na kuwatazama
Pweza na Kombe kabla ya kuwaambia.
“Hebu mshughulikieni vizuri hadi atueleze”
Kichapo cha nguvu kikafuata huku Kombe na Pweza wakimshushia Zera kipigo
cha aina yake cha mateke,ngumi na makofi mazito. Hali ya Zera ikazidi kuwa mbaya
hata hivyo hakuna aliyemuonea huruma. Kipigo kile kilipozidi Fulgency Kassy
akaingilia kati tena na kuwaambia.
“Mwacheni”
“Tueleze wewe malaya usitupotezee muda wetu” Fulgency Kassy akaongea kwa
hasira huku akiinama na kumtazama Zera usoni kisha akaendelea
“Stephen Masika ni nani na alikuwa na shida gani?”
Zera akamtazama Fulgency Kassy kwa utulivu kisha akageuka na kuwatazama
Kombe na Pweza pembeni yake huku akionekana kukata tamaa sana. Kipigo kile
kilikuwa kimechanganya na kumpelekea maumivu makali mwilini huku akilia.
Mdomo wake ulikuwa umechanika,meno yake mawili yalikuwa yamevunjika na jicho
lake lilikuwa limeanza kuvimba na kuvilia damu.
“Alikuwa akitaka kuonana na Milla Cash” hatimaye Zera akaongea kwa shida na
hapo wote wakatazamana kabla ya Pweza kuuliza
“Kwa nini alitaka kuonana na Milla Cash?” Pweza akauliza.
“Alisema kuwa alikuwa na shida naye binafsi ambayo mimi sikupaswa kuifahamu”
Zera akaendelea kuongea.
“Kwa nini hakusema mapema wakati tulipoanza kukuuliza?” Kombe akadakia na
hapo Zera akabaki kimya akitazama chini.
“Wewe ukamwambiaje?” Fulgency Kassy akauliza.
“Nilimwambia akamuulizie Milla Cash kwenye ofisi ya mapokezi ya casino”
“Alipotoka chumbani kwako alikwambia anaelekea wapi?” Pweza akauliza
“Eneo la mapokezi la casino kumuulizia Milla Cash” Zera akaongea kwa woga
“Mlipanga tena kuonana wapi?” Fulgency Kassy akauliza na hapo Zera akatulia
tena kidogo huku akifikiria kuwa azungumze ukweli au adanganye lakini alipokumbuka
hatari ya kushushiwa kipigo zaidi akaongea ukweli.
“Alinipata business card ”
“Iko wapi?” Fulgency Kassy akauliza huku uso wake ukionesha matumaini.
“Ndani ya pochi yangu” Zera akaongea kinyonge huku Kombe akiichukua pochi
yake na alipoifungua ndani akakuta pakiti mbili za mipira ya kondomu za kiume,noti
mbili za shilingi elfu kumi na business card ndogo. Akaichukua ile business card na hapo
wote wakasogea karibu na kuanza kusoma maelezo yaliyokuwa kwenye business card
ile. Taarifa zilizokuwa kwenye business card ile zilijitosheleza na hapo Fulgency Kassy
akamtazama Pweza pembeni yake na kumpa ishara fulani ambayo haraka Pweza
aliielewa.
Pweza hakupoteza muda haraka bastola yake akailekezea kifuani kwa Zera kisha
akazisukuma risasi mbili ambazo ziliacha matundu mawili makubwa yakivuja damu
kifuani kwa Zera. Zera akapiga yowe kidogo na kulala pale chini huku roho yake ikiwa
mbali na mwili.
Shimo la kuuzikia mwili wake lilikuwa tayari limeshachimbwa kiasi cha umbali wa
hatua ishirini kutoka eneo lile. Shimo lile lilikuwa limechimbwa na Fulgency Kassy
na Kombe wakati ule Pweza alipokuwa ameenda kumchukua Zera kule nyumbani
kwake. Hivyo bila kupoteza muda Kombe akaibeba maiti ya Zera begani halafu wote
wakaanza kutembea wakielekea kwenye lile shimo.
Lilikuwa shimo refu kiasi lililochimbwa kando ya ule ufukwe hivyo walipofika
Kombe akainama na kuitupia maiti ya Zera kwenye lile shimo kisha kwa kutumia lile
chepe ambalo walikuwa wamekuja nalo hapo awali wakaanza kulifukia lile shimo.
Baada ya muda mfupi wakawa wamemaliza zoezi lile hivyo wakachukua lile chepe na
kuelekea kwenye lile gari huku wakiamini kuwa pindi maji ya bahari yatakapojaa jioni
ile yangelifunika kaburi lile vizuri na hivyo kuondoa ushahindi wowote wa kuzikwa
mtu eneo lile.
Muda mfupi uliyofuata walikuwa njiani wakirudi mjini na mkakati mpya wa
kumtafuta Stephen Masika.
_____
SIGARA NYINGI NILIZOZITEKETEZA WAKATI nikiisubiri simu ya Zera
nje ya mgahawa ule zilikuwa zimeyapasha moto mapafu yangu kiasi cha kutosha na
kwa kweli sikuzitamani tena kwa wakati huu. Ingawa ilikuwa ni starehe nzuri kwangu
lakini kila nilipokumbuka athari za uvutaji wa sigara nilijikuta nikiyaonea huruma
mapafu yangu.
Mara kwa mara nilikuwa nimepanga kuonana na kiongozi yeyote wa kiroho ili
anipatie mwarobaini wa kukata kiu ya starehe ile yenye madhara ya aina yake. Lakini
huwenda nikasema kuwa shetani alikuwa ameishtukia mapema dhamira yangu ya
kutaka kuikimbia bidhaa yake na hivyo kuninyima muda huo.
Niliitupia tena macho saa yangu ya mkononi na hapo nikayalaani masaa
yalivyokuwa yakitokomea. Ilikuwa ikielekea kutimia saa kumi na moja kasoro jioni
na matumaini ya kupokea simu ya Zera nayo yalikuwa yakiendelea kufifia. Mara kwa
maara nilijikuta nikishawishika kutaka kumpigia simu lakini nikajikuta nikiachana na
mpango huo pale nilipokumbuka kuwa sikuwa na namba ya Zera kwenye simu yangu.
Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na kwa kweli mvua ile ilikuwa ikiendelea
kuleta madhara katika baadhi ya sehemu za jiji la Dar es Salaam. Lakini kwa wakulima
wa mashambani mvua ile ilikuwa ni neema ya aina yake.
Nilikuwa nimeamua kusogea karibu na makazi ya Zera ili pindi atakaponipigia
simu niweze kumfikia kwa haraka. Hivyo katika kufanya utafiti nikajikuta nimevutiwa
na mgahawa huu wa kisasa uliyopo Biafra eneo la Kinondoni B. Sikuwa nikihisi njaa
hivyo nikaagiza kikombe kimoja cha maziwa fresh na kuketi nje ya magahawa ule
sehemu yenye viti na meza inayotazamana na barabara kubwa ya lami.
Niliendelea kukaa eneo lile kwa muda mrefu huku nikisubiri simu ya Zera inifikie.
Mara kwa mara niliichukua simu yangu na kuitazama katika namna ya kutarajia
kuiona namba mpya ikianza kuita lakini hilo halikutokea. Mvua ilinyesha ikaacha
kisha ikanyesha na kuacha tena katika vipindi tofauti lakini simu ya Zera haikunifikia.
Kikombe cha maziwa kilipoisha nikaagiza kingine huku nikiendelea kuununua muda.
Watu walikuja na kuondoka wakiniacha bado nikiwa nimeketi eneo lile hata hivyo
simu ya Zera bado haiukunifikia. Mwishowe nikakata tamaa kabisa na kuamua
kufanya maamuzi ya kuondoka eneo lile.
Maelekezo juu ya wapi yalipokuwa makazi ya Zera nilikuwa bado nikiyakumbuka
vizuri hivyo nilipofika kwenye kituo cha daladala cha Kanisani katika barabara ya
Morocco nikaingia upande wa kulia nikikatisha katika barabara za mitaa. Haikuwa kazi
ngumu kuufikia ule mtaa wa Ukutavuka na baada ya kuchunguza na kuuliza hatimaye
nikaifikia nyumba aliyokuwa akiishi Zera. Nyumba hiyo ilikuwa ikitazamana na duka
kubwa la madawa liitwalo MM Pharmacy kama alivyokuwa ameniambia Zera mara ya
mwisho tulipokutana.
Niliegesha gari langu hatua chache kabla ya kulifikia geti la nyumba ile kisha
nikashuka na kuzitupa hatua zangu kwa utulivu kuiendea nyumba ile. Kulikuwa na
watu wachache waliokuwa wameketi nje ya baraza za nyumba za jirani zilizokuwa
zikitazamana na ile nyumba aliyokuwa akiishi Zera. Watu hao waligeuka wakinitazama
wakati nilipokuwa nikilikaribia geti la ile nyumba hata hivyo sikuwatilia maanani.
Nilipolifikia lile geti nikagundua kuwa mlango mdogo wa lile geti ulikuwa
umefungwa nje kwa komea hivyo nikalifyatua lile komea kisha nikausukuma ule
mlango na kuzama ndani. Kitendo cha kuuona ule mlango wa geti ukiwa umefungwa
kwa nje sikuwa nimetarajia kumuona mtu yeyote akija na kunikaribisha kwenye
nyumba ile kama siyo kuchungulia dirishani na hilo halikutokea. Ile nyumba ilikuwa
kimya bila dalili za uwepo wa mtu yeyote eneo lile.
Ilikuwa nyumba ndogo ambayo ujenzi wake ulikuwa ni wa namna ya kizamani
na usiyo wa gharama kubwa. Nje ya nyumba ile kulikuwa na bustani ndogo ya maua
yaliyopandwa bila kufuata mpangilio mzuri lakini bado yalipendeza. Nilimaliza
kuzipanda ngazi za baraza ya nyuma ile na hapo nikajikuta nikitazama na mlango wa
mbele wa ile nyumba.
Nilisimama kidogo nikiupima utulivu wa eneo lile kisha nikaanza kubisha hodi.
Hata hivyo nilibisha hodi mara kadhaa lakini hakuna mtu aliyeniitikia na hapo nikahisi
kuwa mle ndani ya ile nyumba hapakuwa na mtu. Hivyo nikapachika funguo zangu
malaya kwenye kufuli la mlango wa grill na baada ya muda mfupi kufuli lile likafunguka
hivyo nikaufungua ule mlango wa grill na kujikuta nikitazama na mlango mwingine
wa mbao ambao pia kwa msaada wa zile funguo mlango ule ulifunguka na hapo
nikausukuma na kuingia ndani.
Niliingia ndani ya nyumba ile na kusimama huku nikiyatembeza macho yangu.
Mandhari ya sebule ya nyumba ile yakanitanabaisha kuwa Zera alikuwa ni msichana
aliyekuwa akijipenda.
Kulikuwa na seti moja ya makochi ya sofa za kisasa,jokofu kubwa lililokuwa
kwenye kona ya sebule ile,sistimu nzuri ya muziki,meza fupi ya mbao iliyokuwa
katikati ya makochi yale na ukutani kulikuwa kumetundikwa picha ya Zera. Zaidi ya
pale sikuona kitu chochote cha kunivutia hivyo nikaelekea vyumbani.
Baada ya muda mfupi nikawa nimemaliza uchunguzi wangu mle ndani pasipo
kupata kitu chochote cha maana. Zera pia hakuwepo mle ndani na hapo nikaanza
kuhisi kuwa uchunguzi wangu mle ndani haukuwa na maana yoyote. Nilirudi tena
kule sebuleni huku nikiwa nimekata tamaa juu ya kile nilichokuwa nikikichunguza.
Nilitulia nikifikiri na hapo nikaanza kuhisi kuwa Zera alikuwa msichana tapeli
aliyekuwa akitaka kucheza na akili yangu. Hatimaye nikaketi kwenye kochi moja la
pale sebuleni huku nikitafakari namna ya kufanya. Nilipoitupia macho saa yangu ya
mkononi fikra mpya zikachipuka akilini wangu.
Ulikuwa umesalia muda mfupi kabla ya kutimia saa kumi na mbili jioni na kwa
mujibu wa kumbukumbu zangu ni kuwa ratiba ya Zera kuingia kule Vampire Casino
ilikuwa saa mbili usiku. Kwa dhana ile ni kuwa kulikuwa na muda wa masaa mawili na
ushei kabla ya kutumia saa mbili usiku. Hivyo muda huo wa masaa mawili ungeweza
kumtosha Zera kurudi kutoka huko alikokuwa na kujiandaa tayari kwenye kazini.
Fikra zile zikanirejeshea matumaini moyoni mwangu huku nikiuachia mwili wangu
ustarehe vizuri kwenye lile kochi nililoketi pale sebuleni. Subira ilikuwa silaha kubwa
katika harakati zangu hivyo niliendelea kuketi pale kwenye kochi sebuleni nikisubiri
huku nikiyatembeza macho yangu huku na kule.
Hatimaye macho yangu yakatua juu ya karatasi ndogo iliyokunjwa iliyokuwa chini ya
ile meza ndogo ya mbao pale sebuleni. Nikaichukua karatasi ile na kuanza kuichunguza
na wakati nikifanya hivyo kalamu ndogo ya wino ikaanguka chini. Nikaiokota kalamu
ile na kuanza kuichunguza na kwa kufanya hivyo mikono yangu ikapata muambukizi
wa harufu nzuri ya manukato ya kike. Hali ile ikanitanabaisha kuwa ile kalamu ilikuwa
imetoka kutumika muda mfupi uliyopita. Hatimaye nikaichukua ile karatasi na kuanza
kuipekua katika namna ya kutafuta wino wa kalamu ile ulipotumika.
Ilikuwa karatasi ndogo iliyochanwa kutoka sehemu fulani na mara tu nilipoifunua
karatasi ile nilichokiona lilikuwa ni jina la hoteli moja maarufu iliyopo kwenye ufukwe
wa Coco Beach jijini Dar es Salaam. Nilikuwa nikiifahamu vizuri hoteli ile kwani mara
kwa mara niliwahi kufika kwenye hoteli ile wakati nilipokuwa kwenye harakati zangu
huko nyuma.
Nililitazama jina la hoteli ile kwa uyakinifu huku nikishindwa kuunda hoja yoyote
kichwani mwangu. Hati iliyotumika kuandika jina la hoteli kwenye ile karatasi ilikuwa
mbaya sana kwani huwenda mwandishi alikuwa na haraka sana wakati alipokuwa
akiandika. Nikayapeleka macho yangu nikitazama pale juu ya ile meza na hapo
nikauona waya wa chaja ya simu ukiwa umetelekezwa.
Akili yangu ikaanza kufanya kazi haraka na kuniletea majibu kuwa kulikuwa na
simu iliyokuwa ikichajiwa pale mezani na simu hiyo ilipoanza kuita huwenda mpokeaji
alikuja na kuipokea kisha akatumia kalamu ile kuandika jina la hoteli ile kwenye
ile karatasi akiwa na nia ya kuweka kumbukumbu ya jina la hoteli aliloambiwa na
mpigaji wa simu hiyo. Hisia zangu zikaniambia kuwa sikupaswa kuendelea kukaa pale
sebuleni na kumsubiria Zera arudi mle ndani na badala yake nilipaswa kumfuta huko
alipokuwa.
Nilitoka nje ya nyumba ile na kufunga milango. Nilipotoka nje ya geti la ile nyumba
nikaharakisha kuliendea gari langu na muda mfupi baadaye nilikuwa mbali na mtaa
ule.
Nilikuwa na hisia kuwa endapo ningepita barabara kubwa ningeweza kuchelewa
kule niendako kutokana na foleni kubwa ya magari wakati ule wa jioni. Hivyo mara
baada ya kuingia barabara ya Morocco mbele kidogo upande wa kulia nikaingia barabara
ya mtaa wa Magangamwanza. Barabara ile ikanisafirisha hadi pale nilipokuja kukutana na
barabara ya mtaa wa Ruhinde halafu mbele kidogo nikaingia upande wa kulia nikiifuata
barabara ya Madai crescent. Mara tu nilipoingia kwenye bararabara ile nikapishana na
daladala chache zilizokatisha safari hata hivyo hakukuwa na foleni kubwa hivyo muda
mfupi baadaye nikaja kutokezea kwenye barabara kubwa ya magari ya Ali Hassan
Mwinyi.
Nilipoingia kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi nikasafiri kidogo kama
ninayeshika uelekeo wa eneo la posta kuu lakini sikwenda mbali hivyo mbele
kidogo nikaingia upande wa kushoto nikiifuata barabara ya Bongo clos. Barabara ile
ikanikutanisha na barabara ya Kenyatta drive ambayo kwa mbele ilikuja kunikutanisha
na ile barabara ya Toure drive. Hivyo bahari ya Hindi nikawa nikiiona kwa upande wa
kulia kwangu.
Kulikuwa na foleni kubwa kiasi katika barabara ya Toure drive wakati huu wa jioni
hata hivyo ilinilazimu kwa mara kadhaa kuvunja sheria za barabarani na hatimaye
nikapata upenyo mzuri na kukanyaga mafuta na kuendelea na safari yangu. Niliendelea
kuendesha gari langu na baada safari fupi nikawa nauona ufukwe wa Coco beach kwa
upande wa kulia.
Usiku ulikuwa umeanza kuingia hivyo wakati huu mandhari ya bahari ya Hindi
yalikuwa ya kupendeza sana. Katika sehemu fulani niliziona taa kubwa za meli
zilizokuwa zikisogea taratibu kutia nanga katika bandari salama jijini Dar es Salaam.
Fikra zangu zilipotulia taswira ya Zera ikaumbika tena kichwani mwangu huku
nikianza kujiuliza maswali chungu mzima kichwani. Barabara ya Toure drive ilikuwa
tulivu kiasi na katika maeneo fulani barabara hiyo ilikatisha katikati ya vichaka vidogo
vya miti ya mikoko huku ikipakana na majumba makubwa na hoteli za kifahari
zilizokuwa zikitazamana na bahari.
Hatimaye nikakiona kibao kikubwa cha barabarani kinachoelekeza mahali
ilipokuwa ile hoteli ambayo jina lake nilikuwa nimeliona kwenye ile karatasi iliyokuwa
juu ya meza sebuleni kwa Zera. Kukiona kibao kile cha barabarani nikapunguza
mwendo na kukata kona nikiufuata uelekeo wa kile kibao upande wa kulia. Baada ya
umbali mfupi mara nikaiona ile hoteli.
Ilikuwa ni hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota nne. Hoteli hiyo ilikuwa ikitazamana
na ufukwe wa bahari ya Hindi. Kulikuwa na magari machache yaliyokuwa yameegeshwa
nje ya hoteli ile hivyo nikatafuta sehemu nzuri ya maegesho na kuegesha gari langu.
Kabla ya kushuka nilitulia kidogo ndani ya gari huku nikiyachunguza mandhari
yale na wakati nikifanya hivyo nikaanza kuhisi ni kama niliyekuwa nikiendeshwa zaidi
na hisia zangu kuliko uhalisia wa mambo ulivyokuwa. Nilimkumbuka Zera na hapo
nikaanza kuhisi ugumu wa kumtafuta msichana yule niliyekuwa nikimfahamu kwa
jina moja tu katika hoteli kubwa kama ile kwani sikuwa na namba yake ya simu wala
anwani yake yoyote ambayo ingeniwezesha kumfikia. Kwa kweli nilikuwa nimefanya
makosa makubwa sana kwa kutokuchukua namba yake ya simu mara ya mwisho
tulipokutana kule kwenye kile chumba cha Vampire Casino.
Hatimaye niliyapeleka macho kuitazama saa ya kwenye dashibodi ya gari kisha
nikafungua mlango wa gari na kushuka nikielekea sehemu ya mapokezi ya ile hoteli.
Msichana mzuri mhudumu wa mapokezi yale akanikaribisha kwa bashasha zote
wakati nilipokuwa nikifika eneo lile.
“Karibu kaka”
“Ahsante!” nilimwambia msichana yule mrembo huku usoni nikitengeneza
tabasamu la kirafiki.
“Namuulizia rafiki yangu” nilimwambia msichana yule aliyekuwa ameketi nyuma
ya meza yenye umbo la nusu duara na kompyuta moja ya mezani mbele yake.
“Yupo hapa hotelini?”
“Bila shaka!” nilimwambia kwa kujiamini.
“Nitajie jina lake” yule msichana akaniambia na kwa kuwa sikuwa nikiyafahamu
majina yote ya Zera nikapata kigugumizi kidogo.
“Anaitwa Zera” nilimwambia yule mhudumu wa mapokezi na hapo nikamuona
akianza kushughulika na kompyuta yake pale mezani. Nilitulia huku nikiyatembeza
macho yangu mle ndani ukumbini na wakati huo pia nikiomba uchunguzi wangu
ufanikiwe.
“Alikuambia kuwa angefika hapa saa ngapi?” yule msichana akaniuliza huku
akiendelea kushughulika na kompyuta ya pale mapokezi.
“Kati ya saa nane na saa tisa mchana wa leo” nilimwambia yule msichana huku
nikifikiria na hapo nikamuona yule dada akiyapeleka macho yake tena kwenye kioo
cha ile kompyuta na hapo ukimya ukafuatia. Yule msichana akaendelea kushughulika
na ile kompyuta na baada ya muda akainua macho yake akinitazama.
“Katika orodha ya majina ya watu walioingia leo hotelini hapa hakuna jina hilo”
yule msichana akaniambia na nilipomchunguza nikaona hakika katika maneno
yake na hapo nikajisikia kukata tamaa.
“Anaitwa Zera” nilirudia kumwambia yule dada kwa msisitizo.
“Hatuna mteja mwenye hilo jina na kila mteja anayeingia ndani ya hii hoteli taarifa
zake ni lazima tuwenazo hapa mapokezi. Huna namba yake ya simu?” yule msichana
akaniuliza.
“Hapatikani kwenye simu” nilimwambia yule msichana huku nikifikiria nini cha
kufanya. Mashaka juu ya Zera yalikuwa yameanza kuniingia taratibu na kwa kweli
sikufahamu nilipaswa kufanya nini. Kulikuwa na hoteli nyingine za jirani na eneo lile
hata hivyo wazo la kwenda kwenye hoteli zile na kumuulizia Zera nikaliweka kando
pale nilipohisi kuwa huwenda mambo yangekuwa yaleyale.
“Nashukuru sana dada wacha niende kwani huwenda yeye ndiye aliyekosea
kunipa maelekezo”
“Karibu tena!”
Niliagana na yule msichana wa mapokezi na hapo nikaanza kuondoka eneo lile
nikielekea kwenye yale maegesho sehemu nilipokuwa nimeegesha gari langu. Wazo
la kuelekea Vampire Casino lilikuwa limenijia haraka akilini na sikutaka kujiuliza mara
mbili.
Niliingia kwenye gari langu na hapo nikaanza safari ya kuelekea Vampire Casino
huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu juu ya Zera. Niliendesha gari langu
taratibu huku akili yangu ikisumbuka kufikiria. Muda mfupi uliyofuata nikawa
nimetokezea kwenye barabara kuu ya lami iliyokuwa ikikatisha mbele kidogo ya
hoteli ile. Niliendelea kuendesha gari langu taratibu huku nikiyatembeza macho yangu
huku na kule katika namna ya kutafuta majibu ya maswali mengi yaliyokuwa yakipita
kichwani mwangu.
Niliendelea kuendesha gari langu huku mjadala mzito ukiendelea kupita kichwani
mwangu. Usiku ulikuwa umeingia na mvua kubwa ilikuwa imeanza kunyesha. Nikiwa
naendelea na safari yangu kwenye barabara ile kuu ya lami mara macho yangu
yakajikuta yakivutika na barabara nyingine ya lami ya zamani iliyokuwa ikichepuka
kuingia upande wa kushoto.
Kuiona barabara ile kukanipelekea nipunguze mwendo wa gari na kugeuka
nikiitazama vizuri ile barabara na hatimaye nikajikuta nikishawishika kuifuata barabara
ile. Hivyo nikaingiza gia na kukanyaga mafuta nikikunja kona kuufuata uelekeo wa
barabara ile hafifu ya lami ya zamani.
Ilikuwa ni barabara nyembamba ya lami iliyokuwa ikishuka kuelekea kwenye
fukwe ya bahari. Barabara ile yenye mashimo madogo madogo ilikuwa ikikatisha
katikati ya vichaka vya miti ya mikoko huku ikiwa imesongwa na nyasi ndefu zilizoota
kando yake.
Niliendesha gari langu taratibu huku nikiendelea kuichunguza barabara ile na kwa
kufanya vile haraka nikajua kuwa ilikuwa ni barabara isiyotumika mara kwa mara.
Niliendelea kuifuata barabara ile na mwisho nikakutana na magofu chakavu sana
yaliyotelekezwa miaka mingi.
Nilishuka kwenye gari na bastola yangu mkononi huku nikielekea kwenye yale
magofu. Nilipofika nikaanza kuyachunguza magofu yale chakavu na kwa wakati ule
yalikuwa yakionekana kama kuta mbovu za jengo la kale zilizosimama. Paa la gofu lile
lilikuwa limeezuliwa na milango na madirisha yake yalikuwa yameondolewa na kuacha
matundu makubwa yanayotisha kuyatazama gizani.
Niliingia ndani ya gofu lile na katika sehemu zake za ndani kulikuwa na nyasi
nyingi zilizoota na kutengeneza vichaka vidogovidogo.
Nilimaliza kuyazunguka magofu yale yaliyotelekezwa miaka mingi na matokeo ya
uchunguzi wangu yakanitanabaisha kuwa magofu yale yalikuwa ya Beach resort moja
maarufu iliyotelekezwa miaka mingi iliyopita. Magofu yale yakitazamana na fukwe
kubwa ya bahari ya Hindi yenye upepo mwanana.
Nilisimama mbele ya magofu yake huku nikiutazama ufukwe wa bahari ya Hindi
na kwa kweli hata ufukwe ule ulikuwa umetelekezwa kwani vichaka vya nyasi ndefu
vilikuwa vimeota kila mahali. Nilitazama upande wa kushoto na hapakuwa na njia ya
kuelekea mbele zaidi kwani sehemu ya ufukwe kwa upande ule ilikuwa imemezwa na
mwamba mkubwa wa matumbawe ya baharini hivyo hapakuwa na uelekeo wowote
kwa upande ule.
Upande wa kulia wa fukwe ile kulikuwa na mchanga mwingi hata hivyo baada
ya kuwasha kurunzi yangu na kumulika upande ule nikagundua kuwa hapakuwa na
dalili zozote za uwepo wa kiumbe hai eneo lile. Upepo mkali wa baharini ulikuwa
ukivuma na kwa mbali niliweza kuiona mandhari ya kupendeza ya jiji la Dar es Salaam
iliyotawaliwa na majengo marefu ya ghorofa yaliyokuwa yakiwaka taa usiku ule.
Kwa kweli sikuwa nimeongeza kitu chochote katika uchunguzi wangu eneo lile
na badala yake ni kama niliyekuwa nimeongeza idadi ya vificho vipya vya jiji la Dar
es Salaam nilivyowahi kuvifika. Hivyo hatimaye niliondoka sehemu ile na kurudi kule
nilipokuwa nimeegesha gari langu. Nilipofika nikafungua mlango na kuingia ndani
nikianza safari ya kurudi kule nilipotoka.
Usiku ulikuwa ukiendelea kunawiri na saa ya kwenye dashibodi ya gari mle ndani
ilionesha kuwa dakika chache zilikuwa zimesalia kabla ya kutimia saa mbili usiku.
Muda wa Zera kuingia kule Vampire Casino kama alivyokuwa amenieleza wakati
tulipoonana kwa mara ya mwisho.
Niliendelea kuwaza lakini kamwe sikuiruhusu papara katika harakati zangu. Hivyo
niliendesha gari langu taratibu na wakati nikifanya vile mawazo mengi yalikuwa
yakipita kichwani mwangu na kunifanya nihisi kuwa harakati zangu zilikuwa zikienda
taratibu sana tofauti na nilivyokuwa nikidhani hapo awali.
Niliendelea kuendesha gari langu taratibu na baada ya muda nikawa nimefika
sehemu fulani ambayo nilisimama baada ya kuona kuwa kando yangu upande wa
kushoto wa eneo lile kulikwa na barabara hafifu ya nyasi iliyokuwa ikishuka katikati
ya miti ya mikoko kuelekea chini kwenye ufukwe wa bahari. Nikashusha kioo cha
gari cha ubavuni na kuitazama vizuri barabara ile. Kwa kufanya vile nikagundua kuwa
barabara ile hafifu ya nyasi ilikuwa imepitiwa na gari muda mfupi kama siyo masaaa
machache yaliyopita.
Unapokuwa huna chanzo muhimu cha upelelezi kila kitu mbele yako unaweza
kukishuku hivyo nikaegesha gari langu kando ya barabara ile. Mvua kubwa ilikuwa
ikiendelea kunyesha hivyo nikalichukua koti langu refu na jeusi la mvua nililokuwa
nimeliweka kwenye siti ya nyuma na kulivaa kisha nikavuta droo ya kwenye dashibodi
ya gari na kuchukua bastola yangu mkononi. Hatimaye nikafungua mlango wa gari na
kushuka huku kwa msaada wa ile kurunzi yangu ndogo yenye mwanga mkali nikaanza
kumulika nikishuka kule chini kuifuata ile barabara hafifu ya nyasi ielekeayo ufukweni.
Hisia mbaya zikawa zikiongezeka taratibu kichwani mwangu kwa kadiri niliyokuwa
nikizitupa hatua zangu zilizopwaya kushuka kule chini. Wakati nikiendelea kutembea
nikaanza kuhisi kuwa hata mapigo ya moyo wangu nayo yalikuwa yameanza kwenda
mbio sambamba na baridi nyepesi iliyoanza taratibu kuutafuna mtima wangu. Hali ile
ikanipelekea niikamate vema bastola yangu mkononi.
Niliendelea kushuka kule chini huku nikiwa nimechukua tahadhari zote na baada
ya muda nikawa nimefika sehemu ambayo alama za magurudumu ya lile gari lililoingia
kwenye ile barabara hafifu ya nyasi zilikuwa zimekomea pale kabla ya gari hilo baadaye
kugeuza na kurudi lilipotoka.
Nilisimama eneo lile nikalichunguza kwa hadhari na kwa kweli sikuona viashiria
vyovyote vya sababu ya mtu kuingia na gari eneo lile na kusimama. Au labda ufanyaji
wa ngono ya wizi kwa watu maarufu waliokuwa wakiyakimbia macho ya watu.
Nilijikuta nikiwaza baada ya kukumbuka kuwa mchezo huo wa kishetani ulikuwa
umekithiri sana katika baadhi ya maeneo ya vificho vya jijini Dar es Salaam hususan
sehemu za fukwe ya bahari ya Hindi.
Nilimulika vizuri kwa kurunzi yangu eneo lile na hapo nikaziona alama za
magudurumu ya gari namna yalivyogeuza eneo lile na kurudi yalipotoka. Nikaendelea
kutazama alama ya magurudumu yale huku nikijiuliza kama dereva wa gari lile alikuwa
amekosea njia au lah!. Hata hivyo wazo langu liliyeyuka ghafla baada ya kuona alama za
viatu vya watu zilizoshuka kuelekea chini kwenye ile fukwe ya bahari. Nilipozimulika
alama zile za viatu nikagundua kuwa zilikuwa ni za viatu vya watu tofauti vikiwemo
viatu vya kike kwa namna visigino vyake vilivyochimba mchanga. Alama zile za viatu
ziliendelea kushuka kule chini zikikatisha katika vichaka vya miti ya mikoko.
Tukio lile likanistajaabisha sana na mara ile nikazidi kuwa makini nikizifuatilia
alama za viatu vile vya watu kwa nyuma. Niliendelea kuzifuatilia alama zile nikikatisha
katikati ya vichaka hafifu vya miti na hatimaye nikawa nimetokezea kwenye ufukwe
wa bahari. Kulikuwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma eneo lile na matundu ya pua
yangu yalikaribishwa na harufu kali ya chumvi ya maji ya bahari.
Nilisimama kwa utulivu nikiutazama ufukwe ule ingawaje giza zito la eneo lile
halikunipa nafasi nzuri ya kufanya vizuri uchunguzi wangu. Nadharia ya wanajiografia
juu ya kupwa na kujaa kwa maji baharini ilikuwa ikifanya kazi eneo lile kwani wakati
ule wa usiku maji ya bahari yalikuwa yamejaa na kufunika sehemu kubwa ya fukwe ile.
Zile alama za viatu sasa zilionekana zimesimama eneo lile kwa namna mchanga
wake ulivyokuwa ardhini. Nilimulika eneo lile kwa kurunzi yangu mkononi huku
nikiendelea kuchunguza na badala ya kuona viashiria vyovyote vya matendo ya ngono
kama;nguo ya ndani ya kike au boksa ya kiume iliyosahaulika au mipira ya kondomu
iliyotumika nikashangaa kuona kikuku kilichotelekezwa kama siyo kusahaulika eneo
lile.
Niliinama na kukiokota kikuku kile mchangani na mara nilipokichunguza vizuri
koo langu likanikauka kwa mshtuko. Kile kikuku kilifanana na kikuku kilichokuwa
kimevaliwa na Zera mguuni wakati ule nilipoonana naye kule kwenye kile chumba
cha Vampire Casino. Kile kikuku kilikuwa ni kikuku cha aina yake kilichopambwa kwa
madini tofauti yanayometameta na kupendeza sana. Niliendelea kuchunguza eneo
lile na sikuona kitu kingine cha kuyavuta macho yangu hivyo kile kikuku nikakitia
mfukoni na kuendelea kuzifuatilia zile alama za viatu. Katika kuendelea kuzichunguza
alama zile nikashangazwa na kutoweka kwa zile alama za viatu vya kike hata hivyo
tukio lile halikunifanya nisitishe kuendelea na uchunguzi wangu.
Niliendelea kumulika eneo lile huku nikizifuata zile alama za viatu ambazo kwa
wakati huu zilikuwa ni alama tofauti za viatu vya wanaume watatu kwani zile alama za
vile viatu vya kike hazikuonekana tena na katika maeneo fulani niliziona alama zile za
viatu vya kiume zikiwa zinarudi kule zilipotoka.
Hatimaye nikawa nimefika eneo fulani lenye kichaka kikubwa zaidi cha miti ya
mikoko na hapo nikasimama baada ya kuvutiwa na vitu fulani. Mandhari ya eneo lile
yalikuwa yamekosa utulivu kwani nyasi zake hafifu zilikuwa zimekanyagwa ovyo na
zile alama za viatu zilikuwa zimeutibua mchanga wa eneo lile kila mahali.
Niliendelea kuchunguza zaidi eneo lile na mara nikashangazwa kuziona tena zile
alama za viatu vya kike vyenye visigino virefu zikionekana tena eneo lile.
Nilitulia kidogo nikifikiri katika namna ya kuunganisha mlolongo wa matukio
kichwani mwangu na majibu niliyoyapata yakanipelekea nizipanguse taratibu kingo za
mdomo wangu kwa ulimi.
Sasa nilifahamu kuwa yule mwanamke ambaye alama za viatu vyake nilikuwa
nimeziona kule mwanzo kuwa alikuwa amebebwa kutoka kule nilipoziona alama za
viatu vyake hadi sehemu ile niliposimama. Nilipoendelea kuchunguza zaidi nikaona
kuwa kulikuwa na damu katika maeneo fulani ya mchanga wa eneo lile na hali ile
ikazidi kunishangaza.
Hatimaye nikachuchumaa eneo lile na kuanza kuichunguza vizuri ile damu
ambayo sasa nilikuwa na hakika kuwa ilikuwa imetokana na majereha makubwa
mwilini yaliyotokana na shambulizi la risasi au kitu kingine chenye ncha kali kama
kisu. Nilipoendelea kuchunguza vizuri eneo lile mara nikaziona alama za viatu vya
kiume miongoni mwa zile alama tatu za vile viatu vya kiume zikitoka kwenye kile
kichaka na kuelekea mbele ya ule ufukwe.
Nilipozifuatilia kwa karibu alama zile za viatu mara nikaziona kuwa zilikuwa
zimepotelea kwenye yale maji ya bahari huku zikiwa zimechimba zaidi kwenye
mchanga na hapo hisia kamili zikajengeka kichwani mwangu. Hisia zikaniambia kuwa
sehemu fulani katika yale maji ya bahari yaliyojaa na kufunika ile fukwe kulikuwa na
kaburi la kificho. Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu pale nilipojikuta nikimfikiria Zera
Niliyatazama maji yale ya bahari na hapo nikayaona ni kama yaliyokuwa yameficha
siri kubwa sana za tukio lililotokea eneo lile masaa machache yaliyopita.
Usiku huu maji ya bahari yalikuwa yamejaa na hivyo kuimeza sehemu kubwa
ya fukwe ile hata hivyo nilikuwa makini sana kwenye hesabu za makadirio. Kwani
niliwaza kuwa kwa vyovyote vile endapo kungekuwa na kaburi eneo lile basi kaburi
hilo lisingekuwa mbali sana kutoka katika ufukwe ule wa bahari. Nilitaka kulithibitisha
hilo mapema kwani kusubiri hadi kesho kupambazuke huwenda kusingenipa nafasi
nzuri ya kufanya uchunguzi wangu.
Hivyo nikavua nguo zangu na kuziweka kando ya fukwe ile kisha nikaanza kuingia
kwenye yale maji ya bahari nikiufuata uelekeo wa zile alama za viatu. Niliingia kwenye
maji yale taratibu huku nikijaribu kuvuta hisia juu ya kile nilichokuwa nikikikanyaga
chini. Maji yalikuwa mengi na uzito wa mawimbi ya bahari mara kwa mara uliiyumbisha
miguu yangu pale nilipokuwa nikijaribu kukanyaga chini.
Baada ya hangaika ya hapa na pale hisia kutoka kwenye nyayo za miguu yangu
zikanitanabaisha kuwa nilikuwa nimekanyaga tuta dogo la mchanga sehemu ambayo
yale maji ya bahari yalikuwa yamenifikia kiunoni. Nilisimama eneo lile huku nikijaribu
kuvuta hisia juu ya kile nilichokuwa nimekikanyaga.
Hatimaye niliinama eneo lile na kuanza uchunguzi wangu. Sikuwa na nyenzo
yoyote ya kufukulia tuta lile la mchanga hivyo ilikuwa kazi ngumu. Mara kwa mara
maji yale ya bahari yalinisukasuka hata hivyo niliongeza jitihada zangu katika kulifukua
tuta lile la mchanga kwa mikono yangu na hatimaye nikafanikiwa.
Baada ya kufukua kwa muda mrefu tuta lile la mchanga hatimaye nikawa
nimefanikiwa kuushika mkono wa mtu. Kwa kweli roho iliniuma sana kila nilipojikuta
nikimfikiria Zera. Hata hivyo nikaendelea kufukua lile tuta la mchanga huku nikiuvuta
ule mkono. Baada ya kitambo kirefu cha lile zoezi likawa limekamilika.
Ulikuwa mwili wa mtu kwa namna mikono yangu ilivyohisi. Nikauvuta ule mwili
taratibu hadi kando ya ile fukwe ya bahari. Ilikuwa kazi ngumu kwa vile mwili ule
ulikuwa umeanza kuwa mzito kutokana na kukaa kwenye maji kwa muda mrefu.
Nilivyomaliza zoezi lile nikazichukua zile nguo zangu na kuzivaa kisha nikarudi pale
nilipouweka ule mwili wa yule mtu huku nikiwa na kurunzi yangu mkononi.
Nilifika pale nilipouweka ule mwili na kuanza kumulika kwa ile kurunzi yangu.
Nilichokiona pale chini kikapeleka simanzi kubwa moyoni mwangu. Mwili wa Zera
ulikuwa mbele yangu ukinitazama huku mdomo wake ukiwa wazi. Mikono na miguu
yake ilikuwa imekakamaa na nilipouchunguza uso wake nikaona kuwa ulikuwa na
majereha katika baadhi ya maeneo. Mdomo wake ulikuwa umechanika na damu
nyingi ilikuwa imevilia jichoni. Zera alikuwa amevaa mavazi yake vizuri mwilini na
hivyo nilipomchunguza nadharia ya kubakwa iliyoanza kujengeka kichwani mwangu
ikatoweka.
Niliendelea kuuchunguza vizuri ule mwili wa Zera na wakati nikifanya hivyo
nikagundua kuwa kulikuwa na matundu mawili ya risasi kifuani mwake na sumu ya
risasi hizo ilikuwa imeupelekea mwili wake kuanza kuvimba eneo lile. Kwa kweli
nilisikitika sana huku roho ikiniuma kwa kumpoteza rafiki yangu Zera. Kilichoniumiza
zaidi ni pale nilipohisi kuwa kifo chake kwa namna moja au nyingine kilikuwa
kimesababishwa na kule kuonana kwetu.
Swali likabaki kuwa ni kwa nini Zera aliuwawa kikatili namna ile?. Kipi kibaya
alichokuwa amekifanya hadi kosa lake lithaminishwe na kifo cha kikatili namna ile?.
Niliendelea kujiuliza pasipo kupata majibu na tukio lile lilikuwa limenisikitisha sana.
Sasa nilifahamu kuwa nilikuwa nikishughulika na mkasa hatari nisioufahamu
mwanzo wala mwisho wake. Sikuwa na shaka kuwa uwepo wangu sasa ulikuwa
ukifahamika na watu hao hatari na kwa maana nyingine ni kuwa watu hao walikuwa
tayari kuinunua roho yangu kwa gharama yoyote.
“Yeyote aliyehusika na kifo cha Zera alipaswa kujiandaa kulipa fidia” nilijiapia
huku nikiusogeza vizuri ule mwili wa Zera na kuulaza kwenye nyasi laini za eneo lile.
Sikutaka kuendelea kupoteza muda eneo lile hivyo niliusogeza mwili wa Zera na
kuuweka katika eneo lisiloweza kufikika na maji yale ya bahari yaliyokuwa yakiendelea
kuongezeka ili uweze kuonekana kwa urahisi. Nilipomaliza nikaanza kuondoa
viashiria vyote vya uwepo wangu eneo lile ili uchunguzi wowote ambao ungefanywa
na polisi usiweze kunihusisha. Kupitia kamera yangu ndogo ya digital iliyokuwa
mfukoni nikachukua picha chache za ile maiti ya Zera kama kielelezo makini cha
uchunguzi wangu.
Nilipomaliza nikaondoka eneo lile nikielekea kule barabarani nilipokuwa
nimeegesha gari langu. Zera alikuwa ameuwawa pamoja na taarifa muhimu ambazo
huwenda zingeweza kunisaidia katika upelelezi wangu. Sikuwa na namna ya kufanya
badala yake nilihitaji utulivu mkubwa katika kupanga juu ya hatua inayofuata.
Nilibonyeza kitufe cha mwanga na kutazama majira kwenye saa yangu ya mkononi
na hapo nikagundua kuwa dakika chache zilikuwa zimesalia kabla ya kutimia saa nne
usiku. Nilikatisha kwenye kichaka kile hafifu cha miti ya mikoko na baada ya muda
mfupi nikawa nimelifikia gari langu kando ya barabara ile ya lami pale nilipokuwa
nimeliegesha kisha nikafungua mlango na kuingia ndani. Sikuona kama lingekuwa
ni jambo la busara kuitelekeza ile maiti ya Zera katika ufukwe ule hivyo kupitia simu
yangu nikawapigia polisi na kuwafahamisha uwepo wa maiti ya Zera eneo lile huku
nikikwepa maswali mengine yasiyokuwa na msingi. Usiku bado ulikuwa na mengi ya
kusimulia.
 
KIJIOGRAFIA JENGO LA Vampire Casino lilikuwa kivutio kwa wateja
wastaarabu wasiopenda rabsha kwa namna lilivyokuwa kwenye mandhari
tulivu katikati ya majengo marefu ya ghorofa na majumba makubwa ya
kifahari ya watu waliowekeza vizuri duniani.
Kwa upande wa kushoto jengo laVampire Casino lilipakana na jengo refu la ghorofa
la kampuni moja maarufu ya mawasiliano. Kulia kwake jengo hilo lilipakana na hekalu
kubwa la mabaniani na baadhi ya maghorofa ya shirika la nyumba la taifa.
Nyuma yake jengo lile lilikuwa likitazamana na uwanja mkubwa wa golf,mabwawa
makubwa matatu ya kuogelea na viwanja vingine vya mazoezi ambavyo vilikiwa ndani
ya uzio mkubwa wa ukuta mrefu.
Ili kupata taswira nzuri ya kitu kilichokuwa kikiendelea upande wa mbele wa
Vampire Casino ingemlazimu mtu asimame mbele au kupanda juu ya jengo refu la
biashara la Rupture & Capture lililokuwa mbele kiasi cha umbali usiyopungua mita mia
mbili likitazamana na Vampire Casino kando ya barabara ndogo ya lami.
Uwepo wa ofisi nyingi tofauti katika jengo refu la ghorofa la biashara la Rupture
& Capture kulikuwa kumetengeneza mwanya mzuri kwa mtu yeyote kuweza kuingia
kwenye jengo lile la ghorofa la biashara bila kuulizwa wala kutiliwa mashaka na mtu
yeyote na kwa wakati wowote.
Muda wote wa mchana Koplo Tsega alikuwa ameutumia katika kufanya
uchunguzi kwenye lile jengo la Rupture & Capture akitathmini hali ya ulinzi na usalama
na miundombinu ya jengo lile kama mfumo wa lifti na ngazi zilizokuwa zikitumika
kutoka kwenye ghorofa moja kwenda kwenye ghorofa jingine. Mfumo wa nishati ya
umeme,vipenyo visivyo ramsi kama nafasi ndogo zilizokuwa baina ya bomba la maji
na kuta za jengo. Milango na madarisha ya dharura,sehemu za maliwato na eneo la
maegesho ya magari.
Ilipofika muda wa alasiri Koplo Tsega akawa amehitimisha uchunguzi wake hivyo
akashuka chini ya jengo lile la Rupture & Capture na kuliendea gari lake lililokuwa
sehemu ya maegesho ya magari ya jengo lile. Muda mfupi baadaye akaondoka eneo lile
huku kichwani akiwa na picha kamili ya mandhari yale ili wakati wa usiku atakaporudi
tena kwenye jengo lile aifanye kazi yake kwa hakika.
Kwa upande mwingine Koplo Tsega alikuwa akijivunia matunda ya utafiti wake.
Kabla ya kufika kwenye jengo lile la biashara la Rupture & Capture alikuwa amepeleleza
taarifa zote muhimu za mienendo ya mtu aliyefahamika kwa P.J.Toddo. Afisa
usalama,mwana itifaki na mkuu wa intelijensia ya tume ya upambanaji na udhibiti wa
biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
Miongoni mwa taarifa alizokuwa amezipata Koplo Tsega kutoka kwenye vyanzo
mbalimbali vya kuaminika ni kuwa mojawapo ya ratiba za P.J.Toddo ni kupenda
kuhudhuria Vampire Casino kila siku usiku baada ya masaa ya kazi. P.J.Toddo alikuwa
akiishi eneo la Mbezi beach na alikuwa ametengana na mkewe. Watoto wake watatu
wote walikuwa masomoni nchi za nje.
_____
SAA KUMI NA MBILI NA NUSU JIONI ILIPOTIMIA Koplo Tiglis aliegesha
gari lake kwenye viunga vya maegesho ya magari vya jengo la biashara la Rupture &
Capture. Wakati huu wa jioni magari yaliyoegeshwa kwenye yale maegesho ya magari
ya jengo lile yalikuwa yamepungua kidogo ukifananisha na ule wakati wa asubuhi na
mchana.
Baadhi ya wafanyabiashara wa jengo lile tayari walikuwa wamefunga biashara zao
na kuondoka hivyo Koplo Tsega hakusumbuka sana katika kupata sehemu nzuri ya
kuegesha gari lake. Muda mfupi uliyofuata Koplo Tsega akashuka kwenye gari lile
huku akiwa amebeba begi jeusi,refu na jembamba mgongoni mwake mithili ya begi la
kuhifadhia gitaa la mwanamuziki.
Jioni hii mwonekano wake ulikuwa tofauti na ule wa siku za nyuma tangu alipoingia
jijini Dar es Salaam. Alikuwa amevaa kofia pana na nyeusi aina ya Sombrero ivaliwayo
aghalabu na watu wa Hispania na Meksiko.
Zile Nywele zake ndefu na laini alikuwa amezinyoa katika mtindo wa kupendeza
uitwao Lowcut. Usoni alikuwa ameyaficha macho yake nyuma ya miwani myeusi
iliyoipendezesha vizuri sura yake. Mdomo wake wenye kingo nyeusi pana na laini
zilizokuwa zimekolea vizuri rangi nyekundu ya Lipstick ulikuwa umeongeza ziada
nyingine katika uzuri wake.
Koplo Tsega alikuwa amevaa Pullneck nyeusi iliyokishika vizuri kiwiliwili chake
huku chini akiwa amevaa suruali nyeusi ya jeans iliyoing’ang’ania vizuri misuli ya nyama
zake mapajani. Buti zake ngumu za ngozi miguuni aina ya Travolta zilimfanya atembee
vizuri kwa kujiamini huku akizitupa hatua zake ndefu kuelekea ndani ya lile jengo refu
la ghorofa la biashara la Rupture & Capture.
Koplo Tsega hakutaka kuyavuta macho ya watu eneo lile hivyo alizitupa hatua
zake kwa haraka akipotelea kwenye lifti ya jengo lile. Alipoingia kwenye chumba kile
cha lifti akabonyeza kitufe cha Top floor na kuiamuru lifti ile imfikishe kwenye ghorofa
ya juu kabisa ya lile jengo. Ile lifti haikuwa busy hivyo ndani ya muda mfupi akajikuta
amefika kwenye ile ghorofa ya juu ya lile jengo.
Kile chumba cha lifti kilipofika ghorofa ya juu na ule mlango wake kufunguka
Koplo Tsega akatoka na kujikuta katikati ya korido pana iliyokuwa ikitazamana na
milango ya ofisi za shirika la bima la Mwananchi Insuarance.
Kupitia milango ya vioo vya ofisi ile baadhi ya wafanyakazi walionekana wakiwa
wameinamia kompyuta zao mezani na wengine wakifanya shughuli nyingine tofauti
za kiofisi. Wafanyakazi wale wakionekana kuzama katika shughuli zao hakuna
aliyejisumbua kuinua kichwa chake na kutazama kwenye ile korido wakati Koplo
Tsega alipokuwa akipita. Milango ya ofisi zile ilikuwa imefungwa na hewa safi ya
kiyoyozi ilikuwa ikikazana kupeleka burudani ya aina yake kwa wafanyakazi wale.
Koplo Tsega aliendelea kutembea kwa haraka akiyakwepa macho ya wafanyakazi
wa ofisi zile na alipofika mwisho wa korido ile upande wa kushoto akajikuta
akitazamana na mlango mfupi mweusi ulioandikwa kwa maandishi meupe FOR
ADMINISTRATIVE USE ONLY.
Akiwa na hakika ya kule alipokuwa akielekea Koplo Tsega akafanya jitihada kidogo
za kufyatua kufuli la mlango ule mdogo. Kufuli lilipofyatuka haraka akaufungua ule
mlango na kuingia mle ndani kisha akaufunga ule mlango nyuma yake bila ya mtu
yeyote kumuona.
Kulikuwa na giza zito ndani ya chumba kile kidogo alichoingia Koplo Tsega hata
hivyo kwa msaada wa penlight ama kurunzi yake ndogo ya kijasusi na nyembamba
mithili ya kalamu ya wino aliweza kuona vizuri mbele ya chumba kile.
Upande wa kushoto wa chumba kile kidogo kulikuwa na Mainswitch iliyokuwa
ikisambaza umeme katika sehemu zote za lile jengo. Mainswitch ile ilikuwa na fyuzi
nyingi zilizopangwa kwa kufuatana na mpangilio wa ghorofa ya kwanza hadi ya
mwisho.
Mbele ya chumba kile kidogo kulikuwa na ngazi nyembamba. Ngazi hizo zilikuwa
zikielekea sehemu ya juu kabisa ya lile jengo la ghorofa la biashara la Rupture & Capture.
Koplo Tsega akazitazama kwa makini ngazi zile huku akiwa na picha kamili ya ile
sehemu ngazi zile zilipokuwa zikielekea. Aliporidhika na kumbukumbu zake akaanza
kuzikwea ngazi zile taratibu.
Alipofika mwisho wa ngazi zile akajikuta akitazamana na mfuniko mdogo wa
mlango wa chuma uliyobanwa vizuri kwa kufuli. Koplo Tsega akaifyatua kufuli ya
mfuniko ule kisha akausukuma ule mfuniko kwa juu na hapo akamalizia kuzikwea
zile ngazi. Muda mfupi baadaye akawa ametokezea sehemu ya juu kabisa ya lile jengo
la biashara la Rupture & Capture.
Mvua ilikuwa imeacha kunyesha hata hivyo manyunyu hafifu hayakukoma
kuanguka kutoka angani ingawa manyunyu hayo bado yasingeweza kumzuia mtembea
kwa miguu. Koplo Tsega mara alipofika kule juu akaurudishia vizuri ule mfuniko
mahala pake na hapo akajikuta akitazamana na mandhari ya sehemu ile ya juu kabisa
ya lile jengo la ghorofa yenye matenki makubwa ya maji. Mfumo wa mabomba mengi
ya maji yaliyotandazwa na kupishana kwenye sakafu ya juu ya jengo lile. Nyungo
nyingi za kunasa matangazo ya runinga pamoja na minara mitatu ya mawasiliano ya
kampuni za mawasiliano zilizokuwa na ofisi zao kwenye jengo lile.
Mandhari ya eneo lile yakampelekea Koplo Tsega atabasamu na kujipongeza
moyoni kwa kufanya uchaguzi makini wa jengo lile kwa kigezo kuwa lilikuwa ni
jengo refu zaidi kupita majengo mengine ya ghorofa yaliyokuwa eneo lile na hivyo
asingeweza kuonekana kirahisi na mtu yoyote wakati akiifanya kazi yake.
Akiwa sehemu ya juu kabisa ya jengo lile la ghorofa la Rupture & Capture. Koplo
Tsega akajikuta akivutiwa na muonekano mzuri wa mandhari ya jiji la Dar es Salaam
kwa baadhi ya sehemu. Mandhari hiyo ikiundwa na barabara nzuri za lami,mpangilio
mzuri wa makazi ya watu katika baadhi ya sehemu,bandari salama na majengo marefu
ya ghorofa yaliyokuwa yakiendelea kupandwa katika baadhi ya maeneo.
Koplo Tsega akayatembeza macho yake akiyatazama mandhari yale kwa utulivu
na hatimaye kuweka kituo akitazama kwenye uwazi mdogo uliofanywa baina ya tenki
moja la maji na ungo mdogo wa Dstv uliokuwa karibu na ukingo wa jengo lile na
hapo tabasamu hafifu likajivinjari usoni mwake. Muda mfupi uliofuata tayari akawa
amelifikia eneo lile na kuanza kazi yake.
Koplo Tsega akalivua begi lake kutoka mgongoni na kuliweka chini kisha
akasogea kwa tahadhari na kuchungulia chini ya jengo lile. Mahesabu yake yalikuwa ya
hakika kwani sehemu ya mbele ya lile jengo la Vampire Casino kutoka pale juu ilikuwa
ikionekana vizuri kuanzia kwenye mlango wa mbele hadi lile eneo la maegesho ya
magari.
Koplo Tsega aliyatuliza macho yake akitazama kule chini ya lile jengo huku
tabasamu jepesi likichomoza usoni mwake kisha akarudi kule alipoliacha begi lake
na kulifungua. Ndani ya begi lile kulikuwa na vifaa vingi tofauti vilivyotenganishwa ili
kurahisisha ubebaji wake. Koplo Tsega akavichukua vifaa vile na kuanza kuunganisha
kifaa kimoja akikipachika juu ya kifaa kingine kwa mikono yake imara iliyokuwa ndani
ya glovu nyeusi.
Muda mfupi uliofuata taswira kamili ya kazi ya mikono yake ikaanza kuumbika
machoni mwake. Mashine ya kutolea uhai wa binadamu kwa wepesi wa aina
yake. Bunduki ya kudungulia. Sniper rifle aina ya 338 Lapua Magnum ilikuwa mbioni
kukamilika. Koplo Tsega alipomaliza zoezi lile akaanza kuzipanga vizuri risasi kwenye
magazine ya bunduki ile na kisha kuipachika mahala pake. Mvua ilikuwa imeanza
kunyesha tena lakini hali hiyo haikuleta kikwazo chochote kwa Koplo Tsega.
Alipomaliza kuzipanga zile risasi akaingiza mkono kwenye lile begi na kuchukua
kifaa cha optic ama darubini kali ya kunasia taswira ya windo kwa wepesi wa aina yake
ambacho alikipachika juu ya ile bunduki na kulifinya jicho lake moja akirekebisha lenzi
hadi pale taswira nzuri ilipoweza kuonekana.
Muda mfupi uliyofuata kazi yote ikawa imekamilika hivyo Koplo Tsega akaichukua
ile bunduki ya kudungulia na kuisogeza kwenye upenyo mzuri uliokuwa ukitazamana
na ile sehemu ya mbele ya Vampire Casino. Alipopata pembe nzuri ya shabaha
akaifyatua Adjustable bi-pod stand ya 338 Lapua Magnum na kuitega vyema. Kilichofuata
baada ya pale ilikuwa ni kusubiri ule muda wa kufanya tukio ufike na tukio lifanyike
kama lilivyopangwa.
Koplo Tsega akajilaza kifudifudi huku kitako cha bunduki ile kikiwa kimetulia
vyema kwenye titi lake la kushoto. Mkono wake wa kushoto kwenye kilimi cha
bunduki na jicho lake moja kwenye Eyepiece lens ya darubini ya bunduki ile.
Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na hali ile haikumfurahisha hata kidogo Koplo
Tsega kwani mbele ya Vampire Casino kila mtu aliyefika na kushuka kwenye gari
alikimbia kwa haraka ndani ya casino ile kwa lengo la kujiepusha na mvua ile kubwa
iliyokuwa ikiendelea kunyesha na hivyo kutengeneza mazingira magumu ya kupata
shabaha nzuri kwa windo lake.
Kupitia ile darubini kali iliyokuwa juu ya bunduki yake Koplo Tsega aliweza
kuyachunguza kwa wepesi magari yote yaliyokuwa yameegeshwa kwenye eneo la
maegesho la Vampire Casino. Hakuliona gari la mtu aliyekuwa akimtafuta na hali ile
ikamtia mashaka huku akiwaza kuwa huwenda mtu huyo alikuwa amepata dharura
ambayo ilishindwa kumfikisha eneo lile kwa wakati kama siyo kutokufika kabisa. Hata
hivyo bado hakukata tamaa zaidi ya kuendelea kusubiri.
Mvua kubwa iliendelea kunyesha kisha ikaacha kabla ya kunyesha tena na hatimaye
kuacha katika vipindi tofauti.
Koplo Tsega aliendelea kujipa uvumilivu akisubiri huku mara kwa mara akiitazama
saa yake ya mkononi. Alipoitupia macho saa yake mara ya mwisho akagundua kuwa
muda wa masaa matatu tayari ulikuwa umetoweka tangu alipojibanza kwenye maficho
yale bila ya mtu aliyekuwa akimsubiri kujitokeza. Hatimaye akaanza kukata tamaa.
Koplo Tsega alipokuwa katika harakati za kutafuta mbinu nyingine mbadala ya
kutimiza lengo lake baada ya kuona masaa yanaenda bila ya mtu aliyekuwa akimsubiri
kujitokeza eneo lile mara darubini ya bunduki yake ikanasa taswira ya gari jeusi aina ya
Vw Amarok tdi likiingia na kutafuta maegesho kwenye lile eneo la maegesho ya magari
la Vampire Casino.
Tukio lile likampelekea Koplo Tsega aishike vizuri lenzi ya darubini ya bunduki
yake na kuirekebisha. Taswira nzuri ya sahani ya namba za gari lile ilipoenea vizuri
kwenye lenzi ya bunduki yake tabasamu maridhawa likajipenyeza usoni mwake na
hapo akapiga mruzi mwepesi wa kujipongeza kwa matokeo mazuri ya uvumilivu
wake.
Lile gari jeusi aina ya Vw Amarok tdi liliingia kwenye maegesho ya Vampire Casino
na kwenda kusimama umbali wa hatua chache kutoka kwenye ule mlango wa casino
kisha kikapita kitambo kifupi bila ya mtu yeyote kushuka kwenye gari lile.
Koplo Tsega alipokuwa mbioni kukata tamaa mara akauona mlango wa dereva
wa lile gari ukifunguliwa. Mwanaume mrefu mnene na mweusi mwenye kitambi
cha ukwasi aliyevaa suti nadhifu ya kodrai ya rangi ya ugoro akashuka kwenye gari
lile na kufunga mlango. Kisha akaanza kutembea taratibu kwa kujiamini akielekea
kwenye ule mlango wa mbele wa Vampire Casino. Umri wake alikuwa miaka hamsini
na ushei na alikuwa ameshika simu kubwa ya kifahari ama smart phone na funguo za
gari amening’iniza mkononi mwake.
Koplo Tsega akajisogeza vizuri kwenye ile bunduki yake huku akilifinya jicho lake
moja ili kuliruhusu jicho lake jingine kuona vizuri taswira ya kiumbe kile kilichokuwa
mbele yake kupitia ile darubini kali iliyokuwa juu ya bunduki yake ya kudungulia.
Alichokiona mbele yake kupitia darubini ile akapata hakika kuwa yule mtu
aliyekuwa akimsubiri kwa muda wa masaa matatu yaliyopita juu ya jengo lile la ghorofa
la biashara la Rupture & Capture alikuwa ndiye yule aliyekuwa akimuona mbele yake.
Mtu yule alikuwa ni P.J.Toddo.
Koplo Tsega aliendelea kumtazama P.J.Toddo kwa makini huku akiirekebisha
vizuri darubini ya bunduki yake. Taswira ya mgongo wa P.J.Toddo ilipoenea vizuri
kwenye msalaba wa shabaha Koplo Tsega akavuta pumzi nyingi na kuibana kifuani
kisha kwa utulivu wa hali ya juu akavuta kilimi cha 338 Lapua Magnum.
P.J.Toddo hakumaliza kupanda ngazi ya mwisho ya baraza ya Vampire Casino. Ile
risasi moja ya Sniper rifle yenye ukubwa sawa na ule wa kidole gumba cha mtu mzima
ikapenya mgongoni kwenye koti lake la suti upande wa kushoto na kumtupa hewani
huku ikiacha tundu kubwa kwenye moyo wake. Risasi ile ikatokezea mbele yake na
kusafiri ikienda kukichangua vibaya kioo cha mlango wa mbele wa ile casino na hapo
sauti mbaya ya mpasuko wa kioo kile ikasikika.
P.J.Toddo alipokuwa akitua chini risasi nyingine ikaichangua vibaya shingo yake
na kumtupa mbele huku funguo ya gari na ile simu yake mkononi vikimponyoka.
P.J.Toddo hakupata nafasi ya kuomba maji kwani alipotua chini ya sakafu ya
baraza ile kiwiliwili chake kilitikisika kidogo na kutulia huku majeraha yake yakivuja
damu nyingi.
Koplo Tsega akiwa ameridhika na kazi yake akachukua kitabu kidogo na kalamu
kutoka mfukoni mwake. Kitabu hicho kilikuwa na orodha ya majina ya watu aliokuwa
akiwatafuta. Akaanza kuyapitia majina yale hadi pale alipolifika jina la P.J.Toddo
ambapo aliweka kituo na kuchora alama ya X juu ya jina lile huku tabasamu jepesi
likijivinjari usoni mwake. Alipokirudisha kitabu kile mfukoni akachukua pipi ya kijiti
na kuimenya taratibu kisha akaitia mdomoni.
“Rest in fire P.J.Toddo,rafiki zako watakufuata hivi karibuni” Koplo Tsega akajikuta
akinong’ona huku akiifyatua na kuikunja vyema stendi ya Sniper rifle 338 Lapua Magnum
na kuelekea sehemu alipoliacha begi lake.
_____
NILIKUWA MIONGONI MWA WATU WACHACHE walioshuhudia kwa
ukaribu tukio lile la kupopolewa vibaya na risasi la mwanaume mmoja kwenye baraza
ya Vampire Casino. Muda mfupi uliyopita nilikuwa nimeingia na kuegesha gari langu
kwenye eneo la maegesho ya magari la Vampire Casino nikitokea kule kwenye ile fukwe
ya bahari ya Hindi alipouwawa Zera.
Akili yangu bado ilikuwa ikitafunwa na jinamizi la hisia mbaya za kifo cha Zera
hata hivyo kifo kile kilikuwa kimenijengea dhana timilifu katika fikra zangu. Dhana ya
kuwa wale watu waliomuua Zera walikuwa wakiutambua vizuri uwepo wangu. Hivyo
nilipaswa kuwa makini katika harakati zangu.
Wauaji walikuwa wakiniwinda na hali ile niliipenda sana kwani tafsiri yake ni kuwa
kadiri wauaji hao walivyokuwa wakinikaribia walikuwa wakiniweka karibu na majibu
ya maswali yangu. Niliwaona adui zangu kama watu waoga mno wasiokuwa na ujasiri
wa kunifikia na badala yake walikuwa wakijaribu kuniogopesha kwa kumuua Zera.
Mara baada ya kuegesha gari langu kwenye lile eneo la maegesho ya magari la
Vampire Casino nilikuwa nimeamua kutoshuka kwenye gari langu hasa baada ya
kukumbuka vizuri ule mtafutano niliyousababisha mara ya mwisho wakati nilipoingia
ndani ya casino ile na kuonana na Zera.
Hadi wakati huu nilikuwa na hakika kuwa taarifa zangu zilikuwa tayari zimeufikia
uongozi wa ile casino na polisi huku nikihusishwa moja kwa moja na lile tukio la kifo
cha yule mtu kwenye kile choo cha casino siku ya jana. Zera alikuwa amekufa katika
harakati za kunisaidia nionane na Milla Cash,msichana kahaba professional wa jiji la Dar
es Salaam. Lakini lengo lake lilikuwa halijatimia na hivyo nilikuwa nimeamua kuanza
kazi hii upya kabisa.
Ingawa nilikuwa sina ratiba kamili ya Milla Cash juu ya kuingia na kutoka kwake
kwenye casino ile hata hivyo nilikuwa nimeazimia kusubiri nikiwa ndani ya gari langu
hadi hapo nitakapoliona lile gari jeusi aina ya Texas Longhorn Tailgate Van linalomleta
na kumchukua Milla Cash ili nianze kazi yangu.
Nikiwa ndani ya gari langu niliendelea kuyatembeza macho yangu nikichunguza
vizuri kila mtu aliyekuwa akiingia na kutoka kwenye ule mlango wa casino. Huku
nikiamini kuwa huwenda kwa kufanya vile majibu ya maswali yangu mengi kichwani
yangeweza kupatikana kwa urahisi.
Nikiwa naendelea kusubiri ndani ya gari langu nje ya eneo lile la maegesho ya casino
mara macho yangu yakajikuta yakivutiwa na gari jeusi la kifahari aina ya Vw Amarok
tdi lililokuwa likiingia kwenye viunga vya maegesho ya magari ya casino ile na kutafuta
sehemu nzuri ya maegesho. Gari lile liliposimama mara nikauona mlango wa dereva
ukifunguliwa kisha mwanaume fulani akashuka huku mkononi akiwa ameshika simu
na amening’iniza funguo za gari.
Mwanaume yule mnene na mweusi mwenye kitambi cha ukwasi alikuwa amevaa
suti nadhifu ya kodrai ya rangi ya ugoro. Mara aliposhuka kwenye lile gari mwanaume
yule akaanza kutembea akielekea kwenye ule mlango wa casino.
Ilikuwa ni wakati mtu yule alipokuwa akimaliza kupanda ngazi ya mwisho ya baraza
ya casino pale kilipotokea kitu kilichonishtua sana. Ghafla nilimuona mwanaume yule
mrefu akisombwa hewani na kutupwa mbele ya baraza ya casino ile kama kishada.
Halafu muda uleule nikasikia sauti kali ya mpasuko wa kioo cha mlango wa ile casino
huku ile simu ya yule mtu ikiangukia kwenye sakafu ya baraza ile na kuchanguka ovyo
Watu wachache walioliona tukio lile wakashikwa na taharuki hata hivyo mimi
sikuwa miongoni mwao na badala yake fikra zangu zilijikita katika kutaka kujua nini
kilichokuwa kimemsibu mtu yule.
Nilifungua mlango wa gari langu haraka na kushuka huku uzoefu wangu ukinieleza
kuwa ile ilikuwa ni kazi ya kitaalam sana na ya aina yake kuwahi kutokea jijini Dar es
salaam. Wakati nikimkaribia yule mtu aliyeangushwa kwa risasi ambaye wakati huu
alikuwa amelala chali kwenye ile baraza ya casino huku akiwa hajitambui,fikra zangu
zikahamia kwa mdunguaji.
Yoyote aliyefanya tukio lile alipaswa kuitwa mdunguaji hatari wa daraja la kwanza
kabisa kwa ubora wa kazi yake na asiyekubali risasi yake ipotee bila majibu. Wazo hilo
likanifanya nigeuke haraka na kuanza kuyachunguza majengo ya ghorofa yaliyokuwa
jirani na eneo lile.
Nilikuwa sahihi kabisa na kama ningechelewa huwenda nisingefahamu haraka
kilichokuwa kikiendelea eneo lile. Juu ya jengo lile la ghorofa la biashara la Rupture &
Capture lililokuwa likitazamana na ile casino nilimuona mtu fulani aliyevaa kofia nyeusi
ya Sombrero na mavazi meusi akitokomea kwenye ukingo wa jengo lile. Hisia zangu
zikaniamba kuwa mtu yule alikuwa mwanamke kutokana na mwonekano wa umbo
lake na hapo maswali mengi yakaanza kupita kichwani mwangu huku nikishindwa
kuelewa kilichokuwa kikiendelea eneo lile. Hata hivyo wazo fulani likanijia kichwani
kuwa endapo ningeweza kucheza vizuri na muda ningeweza kulifikia lile jengo la
Rupture & Capture na kumtia mikononi yule muuaji ambaye nilikuwa na kila hakika
kuwa wakati ule bado alikuwa katika harakati za kulitoroka jengo lile.
Sikutaka kupoteza muda hivyo nilimsogelea yule mtu aliyedunguliwa vibaya kwa
risasi ambaye wakati huu alikuwa amelala chali kwenye ile balaza ya casino huku damu
nyingi kutoka kwenye majeraha yake ikiendelea kusambaa pale chini sakafuni.
Nilitaka kufahamu kuwa mtu yule alikuwa nani kabla ya mashuhuda wengine
hawajafika eneo lile. Hivyo haraka niliinama na kumchunguza vizuri yule mtu kwa
makini. Hata hivyo sikufanikiwa chochote kwani sura ya yule mtu ilikuwa ngeni kabisa
machoni mwangu. Bila kupoteza muda mikono yangu ikaanza kufanya ziara fupi
kwenye mifuko ya suti ya mtu yule.
Nilipomaliza upekuzi wangu nikawa nimefanikiwa kupata kadi ndogo ya
kitambulisho cha kazi cha yule mtu,leseni yake ya udereva na kadi ndogo ya mwanachama
wa Vampire Casino. Niliposoma maelezo yaliyokuwa kwenye kitambulisho cha kazi
cha yule mtu nikagundua kuwa yule mtu alikuwa ni mwanausalama mwenye cheo cha
juu sana na jina lake aliitwa P.J.Toddo.
Nilivirudisha vitambulisho vile mfukoni mwake na hapo nikaendelea kufanya
upekuzi kwenye sehemu nyingine za mwili wake. Bastola yake 38 Police automatic ilikuwa
kwenye mfuko wa koti lake la suti. Niliichukua haraka bastola ile na kuichunguza
na hapo nikagundua kuwa ilikuwa imejaa risasi. Hata hivyo sikuichukua badala yake
nikairudisha kwenye ule mfuko huku nikimwacha yule mtu na kusogea jirani kidogo
na eneo lile sehemu ilipoangukia ile simu yake ya mkononi.
Ile simu ilikuwa imechanguka na kila kitu kilikuwa kimesambaratikia sehemu yake.
Niliyatembeza macho yangu haraka eneo lile na hapo nikaiona Simcard ya ile simu ya
yule mtu iliyochanguka pale chini sakafuni. Nikaichukua ile Simcard haraka na kuitia
mfukoni.
Watu wachache waliokuwa wameanza kusogea eneo lile sikuwapa nafasi ya
kunishangaa na badala yake haraka nikajichanganya kati yao na kuwatoroka. Nilipofika
nje ya lile eneo la Vampire Casino nikaanza kutimua mbio nikielekea kwenye lile jengo
la ghorofa la biashara la Rupture & Capture lililokuwa likitazamana na lile jengo la
Vampire Casino.
Nilifika kwenye lile jengo la ghorofa la biashara la Rupture & Capture ndani ya muda
mfupi sana huku mawazo yangu yakanituma nielekee sehemu ilipokuwa lifti ya jengo
lile. Lakini kitendo cha kuiona lifti ile ikifika chini kwenye Ground floor kikanipelekea
nisite kukikaribia kile chumba cha lifti na hivyo kujibanza pembeni nyuma ya nguzo
moja ya jengo lile.
Mlango wa kile chumba cha lifti ulipofunguka mtoto mdogo wa kike aliyevaa sare
ya shule ya msingi akatoka huku akionekana kufurahia safari yake kwenye ile lifti na
mbali na pale hakukuwa na mtu mwengine yeyote ndani ya chumba kile. Kwa kweli
nilishangazwa sana na tukio lile.
Machale yakanicheza pale nilipowaza kuwa yule mdunguaji bado alikuwa ndani ya
lile jengo na huwenda alikuwa ameachana na wazo la kushuka chini ya lile jengo kwa
kutumia lifti baada ya kuhisi hatari ya kushindwa kulitoroka jengo lile.
Hisia zile zikanipelekea niharakishe haraka kuelekea upande wa kushoto mwisho
wa lile jengo sehemu kulipokuwa na ngazi za kuelekea ghorofa za juu za lile jengo.
Nilipozifikia zile ngazi nikaanza kuziparamia haraka nikizikwea huku nikiwa
nimechukua tahadhari za aina zote. Nilipofika ghorofa ya pili ya lile jengo sikumwona
yule mtu hivyo nikaendelea kuzikwea tena zile ngazi nikielekea ghorofa ya tatu.
Katika korido ya ghorofa ya tatu nilipofika nikakutana na kijana mmoja wa kiume
mfanyakazi wa ofisi za mawasiliano zilizokuwa eneo lile. Nikamuuliza kijana yule
kama alikuwa amemuona mtu aliyekuwa akifanana na maelezo yangu. Yule kijana
hakuonekana kuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea kwenye jengo lile hivyo
nikaachana naye na kuzidi kukwea ngazi za kueleka ghorofa ya nne ya lile jengo.
Mara tu nilipoingia kwenye korido ya ghorofa ya nne ya lile jengo ghafla nikakutana
na yule mtu ambaye nilikuwa nimemuona kule sehemu ya juu ya lile jengo muda
mfupi baada ya yule mtu kupopolewa vibaya na risasi kwenye ile baraza ya Vampire
Casino. Nilikutana na mtu yule katikati ya korido pana ya ile ghorofa.
Alikuwa msichana wa makamo aliyevaa mavazi meusi na kofia ya Sombrero
kichwani. Mgongoni alikuwa amebeba begi jeusi,jembamba na refu la ngozi huku
macho yake akiwa ameyafunika kwa vioo vyeusi vya miwani yake. Sikupata nafasi ya
kumtathmini vizuri msichana yule usoni ingawa niliweza kuukadiria umri wake kuwa
ulikuwa ni kati ya miaka ishirini na tano hadi ishirini na saba.
Ingawa msichana yule alikuwa amevaa viatu virefu vya ngozi aina ya Travolta lakini
alikuwa akitembea haraka na kwa kujiamini huku mjongeo wake ukitengeneza starehe
ya kipekee iliyotokana na mtikisiko wa umbo lake la kike lakini kakamavu.
Mara tu nilipoingia kwenye korido ile yule msichana alikuwa akija mbele yangu
hivyo tulipishana huku akili yangu ikianza kufanya kazi haraka katika kutaka kuamua
nifanye nini. Hata hivyo sikuendelea mbele na safari yangu hivyo mara tu tulipopishana
na msichana yule nikageuka haraka na kumtazama. Bahati mbaya au nzuri ni kuwa
na yeye alikuwa na lengo kama langu la kugeuka na kunitazama. Hivyo macho yetu
yakakutana.
Nilichoweza kukiona katika uso wa msichana yule ni hasira na chuki mbaya
iliyoshindwa kujificha. Hisia zilikuwa ni jambo muhimu sana katika kazi yangu na
kamwe sikutaka kuzipuuza. Macho ya dada yule yaliyojificha nyuma ya miwani myeusi
yalipokutana na macho yangu yule dada aligeuka na kuendelea tena na safari yake
mara hii kwa haraka zaidi.
“Hey…!” nilimuita yule dada.
“Haloo...!” nilimwita tena yule dada lakini ilikuwa kazi bure kwani yule dada
hakuniitikia wala kusimama badala yake aliendelea kuharakisha akielekea mwisho wa
ile korido na hapo fikra fulani zikanijia akilini kuwa alikuwa akiiwahi lifti ya lile jengo.
Sikutaka kuendelea kumsubiri yule dada ageuke tena na kuniitikia hivyo nikageuka
na kuanza kutimua mbio nikimfukuza. Hata hivyo nilikuwa nimechelewa kwani
kile chumba cha lifti tayari kilikuwa kimefika kwenye ile ghorofa na mlango wake
ulipofunguka mwanaume mmoja alitoka. Tukio lile likampa fursa nzuri yule dada
niliyekuwa nikimfukuza aingie ndani ya chumba kile cha lifti huku akigeuka na
kunitazama kwa uso wa tabasamu jepesi lenye kunicheka.
Nilikuwa nimechelewa kwani wakati nilipokuwa nikikikaribia kile chumba cha lifti
mlango wake ukawahi kujifunga nikiwa nimesaliwa na hatua chache tu kukifikia kile
chumba.
Nikasimama ghafla huku nikiilaumu akili yangu kwa kuchelewa kung’amua
haraka hila ile. Hata hivyo sikukubali kushindwa hivyo haraka nikaanza kutimua mbio
kuzirudia tena zile ngazi za kushukia ghorofa ya chini ya jengo lile zilizokuwa mwisho
wa ile korido. Nilipofika nikaanza kushuka chini haraka.
Nilipofika chini kwenye ghorofa ya tatu ya jengo lile nikakiona kile chumba cha
lifti kikiendelea kushuka ghorofa ya chini bila kusimama. Hivyo nikaendelea kushuka
zile ngazi nikielekea ghorofa ya pili huku hasira ikizidi kuchemka mwilini mwangu
kwa kile kitendo cha kupigwa chenga kama mtoto.
Kile chumba cha lifti kilipofika ghorofa ya pili kikasimama na mlango wake
ukafunguka. Nikiwa katika hali ya kusubiri mara nikamuona yule dada akitoka kwenye
kile chumba cha lifti lakini kutokana na msongamano mkubwa uliyosababishwa na
wafanyakazi wengi waliokuwa wakitoka kwenye ofisini za jengo lile sikupata nafasi ya
kumfikia yule dada kwa urahisi.
Hivyo nikaanza kulipangua lile kundi la wafanyakazi waliokuwa wakitoka kwenye
zile ofisi nikimfuata tena yule dada. Kitendo kile kikawa kimemshtua yule dada
niliyekuwa nikimfukuza. Yule dada alikuwa tayari ameshajichanganya kwenye lile
kundi la wafanyakazi waliokuwa wakitoka maofisini na aliponiona nikilipangua lile
kundi la wafanyakazi kumfuata akawahi kuichomoa bastola yake mafichoni.
Muda uleule nikasikia milio mitatu ya risasi kwenye ile korido na ghafla kukawa
na giza zito mle ndani. Kilichofuata baada ya pale zilikuwa ni sauti za vilio na mayowe
zikihanikiza kila pembe kwenye korido ile. Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu
baada ya kuhisi kuwa kwa mara nyingine nilikuwa nimezidiwa ujanja na na yule dada.
Kuzidiwa ujanja kwa mara ya pili,hali ile iliusononesha sana moyo wangu. Hata
hivyo sikuwa na namna ya kuusuluhisha mgogoro ule mkubwa uliokuwa ukiendelea
kwenye nafsi yangu. Hivyo nikapiga moyo konde na kuitupa karata yangu ya mwisho
iliyosalia mkononi.
Ramani ya jengo lile hadi kwenye ghorofa ya nne sasa nilikuwa nikiifahamu vizuri
kwa muda mfupi niliyofanikiwa kuwa mwenyeji wa jengo lile. Kutoka pale nilipokuwa
nilikuwa nimebakisha ngazi chache tu kufika ghorofa ya chini kabisa ya lile jengo.
Kutoka pale nilipokuwa sikuwa mbali sana na zile ngazi za kushukia ghorofa
ya chini kabisa ya lile jengo. Hivyo nilianza kutimua mbio nikilipangua lile kundi la
wafanyakazi waliokuwa wakihaha huku na kule baada ya ile milio ya risasi kusikika.
Nilizifikia zile ngazi na kuanza kushuka chini haraka huku nikiwapita wale
wafanyakazi ambao nao walikuwa wakitimua mbio kushuka kwenye ile ghorofa
ya chini. Nilipofika kwenye ghorofa ya chini ya lile jengo nikashika uelekeo wa
kilipokuwa kile chumba cha lifti lakini safari hii nikiwa nimeikamata vyema bastola
yangu mkononi tayari kujibu shambulizi lolote ambalo lingejitokeza mbele yangu.
Wakati nikikifikia kile chumba cha lifti mara nikauona mlango wake ukianza
kujifunga na nilipochungulia mle ndani hapakuwa na mtu yoyote. Nikasimama huku
nimeshikwa na mshangao usioelezeka.
“Yule dada alikuwa ameshatoka kwenye kile chumba cha lifti na kutokomea?”
nilijiuliza pasipo kupata majibu na nikiwa katika hali ile mara wazo fulani likanijia
akilini. Nikageuka haraka kutazama eneo la maegesho ya magari ya lile jengo na hapo
nikaliona gari dogo jeupe,teksi ya abiria aina ya Corolla limited likiacha maegesho ya
jengo lile na kuingia barabarani. Machale yakanicheza tena hivyo nikaanza kutimua
mbio nikiifukuza ile teksi. Sikufanikiwa kwani huwenda kila kitu kilikuwa kimepangwa.
Gari lile Corolla limited nyeupe yenye kibandiko cha teksi juu yake na ufito wa njano
ubavuni likaondoka kwa kasi eneo lile na kuingia barabarani huku mimi nikiwa umbali
usiopungua mita hamsini kutoka pale nilipokuwa.
Nikaendelea kutimua mbio nikilifukuza lile gari lakini nilikuwa ni kama mtu
niliyekuwa nikiendeshwa na nguvu za mwili na siyo utashi wangu kwani hapakuwa na
uwiano wowote kati ya mbio zangu za miguuni na magurudumu ya gari lile yaliyokuwa
yakizunguka kwa kasi ya ajabu. Hatimaye mdunguaji akawa ameniacha huku nikiwa
siamini macho yangu.
Nilisimama nikilitazama gari lile namna lilivyokuwa likitokomea mbele yangu
huku donge la hasira likiwa limenikaba kooni. Kwani kwa maana nyingine ni kama
niliyekuwa nimepoteza pointi zote muhimu za ushindi katika pambano langu.
Mwishowe nilikata tamaa kabisa na kuanza kutembea kivivuvivu nikirudi kule kwenye
eneo la maegesho ya magari la Vempire casino huku mawazo mengi yakipita kichwani
mwangu.
Kitu kingine cha kushangaza ni kuwa wakati nikilifikia lile eneo la maegesho la
Vampire Casino ule mwili wa yule mtu aliyedunguliwa vibaya kwa risasi kwenye baraza
ya casino ile muda mfupi uliyopita ulikuwa tayari umeondolewa na ile sehemu ya
baraza ilikuwa imesafishwa vizuri kiasi kwamba mtu yeyote ambaye angefika eneo lile
asingeweza kufahamu kitu kilichokuwa kimetokea muda mfupi uliopita.
Hali ile ikanishangaza sana huku nikijiuliza kama kulikuwa na ulazima wowote wa
polisi kufanya uchunguzi wao na kuuondoa haraka mwili wa yule mtu. Niliendelea
kulichunguza eneo lile na hapo nikagundua kuwa hata kile kioo cha mlangoni
kilichokuwa kimechanguliwa kwa risasi za mdunguaji nacho kilikuwa kimerudishiwa
kipya. Yaani mambo yalikuwa yameenda haraka mno kiasi cha kuzishangaza sana
fikra zangu huku nikishindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwenye casino ile.
Wakati huu yalikuwa yamesalia magari machache kwenye lile eneo la maegesho
la Vampire Casino. Hisia za kutopiga hatua yoyote katika harakati zangu bado zilikuwa
zikiisimanga nafsi yangu na kwa kweli hali ile iliidhoofisha sana akili yangu.
Nilimfikiria Milla Cash na kuanza kuhisi kuwa huwenda angekuwa chanzo
muhimu cha kusonga katika harakati zangu. Hata hivyo nilitambua kuwa suala lile
kwa sasa lisingewezekana kwa urahisi. Hivyo nikaingia kwenye gari langu na kuyaacha
maegesho yale.
_____
“NYINYI MNADHANI NI KITU GANI KINACHOENDELEA?” Fulgency
Kassy akawauliza wenzake ikiwa ni muda mfupi mara baada ya mwili wa P.J.Toddo
kuondolewa na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifidhia maiti katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili.
“Mimi ninahisi kuwa huwenda kuna mtu au watu fulani waliopo nyuma ya mpango
huu” Pweza akaongea kwa tafakuri na hapo Fulgency Kassy akageuka na kumtazama.
“Sitaki kukubali akilini mwangu kuwa vifo vya Guzbert Kojo na huyu P.J.Toddo ni
vya bahati mbaya kwani mkitafakari vizuri mtagundua kuwa watu hawa wameuwawa
nyuma ya mipango timamu” Pweza akaongea kwa msititizo.
”Taratibu hata mimi naanza kukubaliana na hoja yako lakini swali la msingi
linaendelea kubaki palepale kuwa ni nani aliyeko nyuma ya mpango huu?” Fulgency
Kassy akaongea huku akiendelea kufikiri.
“Hilo ndiyo suala tunalotakiwa kushughulikanalo kuanzia sasa vinginevyo kama
wangekuwa hai tungeweza kusema moja kwa moja kuwa ni wale Tumbili” Pweza
akaongea kwa utulivu
“Tumbili gani?” Kombe akauliza
“Koplo Tsega na Sajenti Chacha Marwa” Pweza akafafanua
“Mimi nina wazo moja” Kombe akaingilia kati na kuwapeleka wenzake wageuke
na kumtazama kwa shauku.
Wote walikuwa wamesimama nje ya jengo la Vampire Casino. Taarifa za kuuwawa
kwa P.J.Toddo zilikuwa zimewafikia muda mfupi uliyopita wakati walipokuwa
wakitoka kwenye ule ufukwe wa bahari walipomzika Zera. Walichokifanya mara
baada ya kufika pale casino ilikuwa ni kufanya taratibu za haraka za kuuondoa mwili
wa P.J.Toddo pasipo kuwashirikisha polisi kwa sababu walizokuwa wakizijua wao.
“Wazo gani?” Pweza akamuuliza Kombe kwa shauku. Kombe alikuwa
amechuchumaa nje ya baraza ya casino huku macho yake yakiendelea na uchunguzi.
“Risasi zilizomzimisha P.J.Toddo huwenda zikawa zimetokea pale juu” Kombe
akaongea kwa utulivu.
“Wapi?” wote wakauliza kwa shauku.
“Juu kabisa ya lile jengo la biashara la Rupture & Capture” Kombe akaongea na
hapo wote wakageuka na kutazama sehemu aliyokuwa akitazama.
“Kwanini unadhani hivyo?” Fulgency Kassy akauliza huku akiendelea kutazama
kule juu ya lile jengo.
“Ukitazama vizuri kule juu utagundua kuwa kuna pembe nzuri sana ya shabaha
inayoweza kutumiwa na mdunguaji” Kombe akaendelea kufafanua.
“Mdunguaji katika jiji la Dar es Salaam?” Pweza akauliza kwa mshangao
“Dar es Salaam bado haijafikia kuwa na matukio ya uhalifu wa namna hiyo”
Fulgency Kassy akaongea akionekana kupingana na wazo la Kombe.
“Nimelitumikia jeshi kwa zaidi ya miaka nane kwa hivyo ninauzoefu mzuri na
hiki ninachokizungumza. Mtu wa kawaida hawezi kuwa na ufundi wa kumdungua
mtu katika umbali huu tena bila kupoteza risasi hata moja” Kombe akaongea kwa
msisitizo huku akiendelea kutazama kule juu.
“Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa P.J.Toddo ameuwawa kwa risasi za
mdunguaji?” Fulgency Kassy akauliza tena huku akimtazama Kombe kwa uyakinifu.
“Sina hakika lakini hilo linawezekana kufanyika” Kombe akaongea huku
akiendelea kufikiri.
Maelezo ya Kombe yakawapelekea Fulgency Kassy na Pweza wageuke na
kutazamana kisha ukimya ukafuatia baina yao huku kila mmoja akizishirikisha vizuri
hisia zake.
“Yeyote aliyemdungua P.J.Toddo anapaswa kuwa askari mzoefu na mdunguaji
makini” Kombe akaendelea kufafanua.
“Askari jeshi au polisi?” Fulgency Kassy akauliza kwa makini.
“Anaweza kuwa ni yeyote kati yao” Kombe akafafanua.
“Kwanini unadhani hivyo?” Pweza akauliza.
“Mara nyingi protokali za kijeshi hufuatwa pale siasa inapoonekena kushindwa
kufanya kazi” maneno ya Kombe yakawapelekea wenzake wageuke kumtazama kwa
shauku.
“Una maana gani kusema hivyo?” Fulgency Kassy akauliza kwa shauku.
“Huelewi nini hapo mbona kila kitu kipo wazi na kinajieleza. Nyinyi wote si
mnajua kuwa kazi tunayoifanya hapa kwa kiasi kikubwa ni kwa minajili ya kulinda
maslahi ya wanasiasa. Kumbukeni kuwa katika hii tume kulikuwa na wanajeshi ambao
kwa sasa tumewazika. Lakini hatuwezi kujua kuwa hao wanajeshi waliokuwa kwenye
hii tume kama walikuwa wao peke yao au lah!”
Maelezo ya Kombe yakawapelekea Fulgency Kassy na Pweza waupishe utulivu
vichwani mwao huku kila mmoja akionekana kuzama kwenye tafakuri nzito. Kitambo
cha Ukimya kikapita kabla ya Pweza kukohoa kidogo na kuvunja ukimya.
“Jambo la kwanza muhimu ni kuhakikisha kuwa polisi hawajitumbukizi katika
suala hili” Fulgency Kassy akaongea kwa utulivu.
“Mimi naona sasa ipo haja ya kumshirikisha mkuu” Pweza akaongea huku akifikiri
“Hilo ni wazo zuri lakini kwa sasa nafikiri bado tunayo nafasi ya kulimaliza suala
hili sisi wenyewe” Fulgency Kassy akadakia.
“Mimi nadhani suala hapa siyo nafasi ila ni kukaa chini mapema na kulipima
jambo lenyewe kama litaweza kutatulika kwa kigezo cha muda. Wakati fulani
unaweza kupewa muda mrefu wa kufanya mtihani uleule na kujikuta ukifeli. Hivyo
mimi nadhani tulitafakari hili suala kwa mapana yake kwani sote tuliamini kuwa
kwa kuwafumba mdomo Koplo Tsega na Sajenti Chacha Marwa ndiyo lingekuwa
suluhisho. Lakini sasa nafikiri kuwa huwenda hatukuwa sahihi. Guzbert Kojo na
P.J.Toddo wameuwawa na huwezi kujua nani atakayefuatia baada ya hapa. Hivyo
tusipokuwa makini kadhia hii itahamia kwetu” Kombe alimaliza kuongea huku
akisimama pale chini.
“Huwenda ukawa upo sahihi ingawa mimi nayaona mawazo yako ni kama
yanayoegemea upande mmoja. Sote tunajua kuwa P.J.Toddo alikuwa ni mkuu wa
kurugenzi ya mawasiliano ya rais Ikulu. Kama ni hivyo kwanini tusilichukulie hili suala
katika mtazamo wa kisiasa?. Mfano labda kifo chake kimetokana na yeye kuvujisha
siri za serikali kwa vyama vya upinzani baada ya kupewa pesa nzuri na vyama hivyo
vyenye nia ya kushika dola” Fulgency Kassy akaunda hoja nzuri iliyompelekea Pweza
atabasamu lakini uso wa Kombe haukuonesha tashwishwi yoyote.
“Huwenda ukawa upo sahihi” hatimaye Kombe akaongea kwa utulivu.
“Hatuna haja ya kuwa na wasiwasi. Mimi nafikiri ngoja kwanza tuone mambo
yatakavyokuwa halafu tutajua cha kufanya” Fulgency Kassy akahitimisha kwa
kuyaweka kando mawazo ya Kombe.
“Twendeni kule juu ghorofani tukachunguze huwenda tukapata chochote”
Kombe akavunja ukimya na wote wakakubaliana na wazo lake.
Muda mfupi baadaye walikuwa juu ya lile jengo la biashara la Rupture & Capture
na baada ya uchunguzi wa hapa na pale wakajikuta wakikubaliana na hisia za Kombe.
Pweza,yeye aliokota maganda mawili ya risasi za mdunguaji zilizotumika katika
kuupokonya uhai wa P.J.Toddo kwenye ile baraza ya casino. Huku Fulgency Kassy
akiokota ganda la pipi ya kijiti sawa na lile aliloliokota kule nyumbani kwa Guzbertkojo usiku ule alipouwawa
“Maganda haya ni ya risasi za bunduki nzito ya kivita na hakuna raia anayeruhusiwa
kumiliki silaha ya namna hii” Kombe akaongea kwa hakika huku akiendelea
kuyachanguza kwa ukaribu yale maganda ya risasi baada ya kuyachukua kutoka
mkononi mwa Pweza.
“Sasa naanza kupata picha kamili kuwa mtu aliyehusika na kifo cha Guzbert Kojo
ndiyo huyu pia aliyehusika na kifo cha P.J.Toddo” Fulgency Kassy akaongea kwa
utulivu huku akilifikicha lile ganda la pipi ya kijiti mkononi.
“Kwa vipi?” Kombe akauliza.
“Angalieni hili ganda la pipi” Fulgency Kassy akawaambia wenzake na kuwapelekea
wote wasogee karibu na kulitazama ganda lile la pipi mkononi mwake.
“Ganda la pipi lina shida gani?” Pweza akauliza huku akishindwa kuelewa.
“Niliokota ganda la pipi kama hili nyumbani kwa Guzbert Kojo usiku ule
alipouwawa na sasa nimeokota ganda la pipi kama lile hapa” Fulgency Kassy akaongea
huku akionesha mshango.
“Kwa hiyo unataka kusema kuwa muuaji ni mtu anayemumunya pipi ya kijiti
kila anapokamilisha dhamira yake?. Mh! hii ni ajabu sana na hainiingii kabisa akilini”
Pweza aliongea kwa mshangao huku akiendelea kulitazama lile ganda la pipi.
“Mauaji haya yanafanywa na mtu mmoja” Fulgency Kassy hatimaye akavunja
ukimya na kuongea kama mtu aliyezama kwenye tafakuri nzito.
“Unadhani mtu huyo anaweza kuwa ni yule Stephen Masika?” Kombe akauliza.
“Hakuna mwenye hakika ingawa miongoni mwetu tunaweza kuwaza hivyo.
Tunachotakiwa kufanya sasa ni kutafuta ukweli wa hisia zetu kwani hiyo ndiyo kazi
iliyoko mbele yetu kwa sasa. Tumtafute huyu muuaji na kumalizana naye mapema
kabla hajaendelea kutabaruku na roho zetu” Fulgency Kassy akaongea kwa hakika.
“Sasa tunaanzia wapi?” Pweza akauliza.
“Tunaanzia kwenye hili jengo kutafuta taarifa zitakazoweza kutusaidia kumnasa
huyu Tumbili mwingine”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom