Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 302
- 1,306
NYEMO CHILONGANI
0718069269
Sehemu ya 01.
Ilikuwa ni taarifa mbaya, iliyoshtua ambayo ilianza kwa kusikika katika sehemu mbalimbali jijini Las Vegas nchini Marekani kabla ya kuwafikia polisi.
Kila aliyezisikia taarifa hizo, hakuamini, wengi wakahisi hazikuwa taarifa za kweli, labda kulikuwa na mtu mwingine aliyetaka kuivumisha habari hiyo ambayo ilimsisimua kila mtu aliyeisikia.
Msichana mrembo aliyeitwa kwa jina la Stacie Lawrence, msichana aliyebahatika kunyakua taji la Urembo wa Dunia, alikutwa amekufa ndani ya chumba kimoja cha Hoteli ya Vikings Hill iliyokuwa Las Vegas, Nevada nchini Marekani alipokuwa amepanga huku akisubiri kuonana na Mkurugenzi wa Mtandao wa Google kwa ajili ya kusaini mkataba wa picha zake kutumika katika programu moja ambayo ingetumiwa katika simu zote zinazotumia system ya android.
Stacie aliyekuwa gumzo kwa kipindi hicho duniani kutoka na uzuri wake, alikutwa amekufa baada ya kujiovadosi madawa ya kulevya aina ya Heroine kwa kujichoma sindano katika mkono wake wa kulia wakati kitandani ndani ya hoteli hiyo.
Hiyo ndiyo ilikuwa habari ya mjini, kila aliyeisikia, hakuamini, swali la kwanza kabisa walilojiuliza watu ni juu ya utumiaji wa madawa ya kulevya. Kila mtu alijua Stacie hakuwahi kutumia madawa hayo, si kipindi hicho tu, hata kabla ya kutwaa taji hilo, hakuwa mtumiaji, sasa ilikuwaje mpaka leo hii akutwe chumbani kitandani akiwa amejidunga madawa hayo? Hilo lilikuwa swali lisilokuwa na majibu.
Waandishi wa habari kutoka katika mashirika mbalimbali ya televisheni habari kama CNN, BBC, Sky News na hata wale wa magazeti kama New York Times, 24 News tayari walikuwa nje ya hoteli hiyo, vitendea kazi vyao vyote vilikuwa mikononi mwao, walitaka kupiga picha na kupata habari kuhusu kifo cha msichana huyo mrembo ambaye bado uzuri wake ulikuwa gumzo duniani.
Polisi walitanda kila sehemu nje ya hoteli hiyo, mkanda wa njano ulioandikwa Do Not Cross yaani ‘Usivuke’ ulizungushiwa katika hoteli hiyo kwa muda.
Magari ya wagonjwa mawili yalikwishafika katika hoteli hiyo, kilichosubiriwa ni kuingia ndani na kuuchukua mwili huo.
Waandishi hawakuruhusiwa kabisa kuingia ndani ya hoteli hiyo, waliambiwa wasubiri hapo nje wakati polisi wakiingia ndani kwa ajili ya kufanya kazi yao, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri.
Polisi wakaingia ndani ya chumba kile. Huko wakaukuta mwili wa Stacie ukiwa kitandani, mkono wake wa kushoto kulikuwa na sindano iliyochoma mshipa wake, aliishikilia kwa kutumia mkono wake wa kulia mbali na hivyo, pembeni yake kulikuwa na noti za Dola, Paundi, Yeni na Euro.
Udenda ulikuwa ukimtoka, pale alipokuwa, hakutingishika, kilikuwa kifo kibaya, kilichozua maswali mengi kwa watu wengi, maswali hayo yote, hapakuwa na mtu aliyekuwa na majibu zaidi ya Stacie mwenyewe ambaye kipindi hicho alikuwa marehemu.
“This is the fifth one, what the hell with the drugs?” (Huyu ni mtu wa tano, kuna nini na haya madawa?) alisikika akiuliza mwanaume mmoja huku akionekana kushangaa.
“I don’t know. What the hell with these teenagers, they always test each and every goddamn thing, why?” (sifahamu. Nini kinaendelea kwa hawa vijana, mara nyingi wanapenda kujaribu kila kitu, kwa nini?) aliuliza mzee mmoja huku akionekana kukasirika.
Kila mmoja alishangaa, huyo hakuwa mtu wa kwanza, supastaa aliyejiua baada ya kujiovadozi kwa madawa ya kulevya, huyo alikuwa mtu wa tano, kijana supastaa ambaye aliamua kujiua kwa kujidunga sindano ya madawa hayo.
Mtu wa kwanza kabisa kujiua kwa kujidunga shindano alikuwa Paul McKenz. Huyu alikuwa mcheza kikapu aliyekuwa akichipukia, mwenye sura nzuri, alijitengenezea jina kubwa katika Timu ya La Lakers, akaanza kupata mashabiki wengi, alipendwa na kila mtu aliyekuwa akiupenda mchezo huo, jina lake likaanza kuwa kubwa, akapata mikataba mingi lakini mwisho wa siku, Paul akaja kujidunga sindano yenye madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine chumbani kwake.
Watu wengi walisikitika kwani ndiye alikuwa kijana aliyekuwa akichipukia katika mafanikio makubwa. Hiyo haikuishia hapo, pia kulikuwa na kijana mwingine aliyekuwa na kipaji cha uigizaji. Katika filamu yake ya kwanza ya Fallen Tree, alishinda Tuzo ya Oscar, Global na nyingine nyingi, huyu aliitwa Todd Lewis.
Bahati ikaanza kuonekana upande wake, akapendwa sana, kila kona alisikika yeye tu. Kadiri jina lake lilivyovuma ndivyo alivyozidi kujitengenezea mashabiki.
Wakati akiwa amenunua gari yake ya kwanza ya thamani kabisa aina ya Ferrari Testarossa nyekundu, akakutwa naye akiwa amejidunga madawa ya kulevya ndani ya gari lake nje ya klabu moja huku pembeni kukiwa na noti ya dola, paundi, Yuan na Euro. Watu walisikitika na kulia, vilio vyao, huzuni zao hazikuweza kuwarudisha watu hao duniani.
Mtu mwingine kabla ya Stacie kujiua kwa madawa ya kulevya alikuwa kijana aliyeitwa kwa jina la Carter Phillip. Huyu alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakichipukia katika muziki wa Pop. Alikuwa na sauti kali, yenye nguvu ambapo kila alipokuwa akiitumia katika nyimbo zake, wanawake walichanganyikiwa.
Alikuwa mzuri wa sura, mwili uliojengeka. Kibao chake cha kwanza kabisa cha Come and Get Me Shawty alichokitoa kilitingisha kila kona duniani. Uwezo wake ulionekana, si hapo tu hata kwenye Shindano la American Got Talent, mpaka aliposhinda, watu waliona kipaji kikubwa ndani yake.
Wengi wakatabiri Carter angekuwa mrithi sahihi wa Michael Jackson, wengi wakamtabiria mema, njozi njema ikaonekana mapema kabisa kwani ngoma zake mbili alizozitoa, zote zilishika nafasi za juu kabisa katika orodha ya Billboard.
Akatengeneza fedha nyingi huku ndiyo kwanza akiwa na miaka kumi na tisa. Akapendwa, akawa kipenzi kikubwa cha watu ila baada ya kwenda nchini Uingereza kwenye Tamasha la UKIMWI lililokuwa likifanyika katika Jiji la Southampton, akakutwa akiwa amejiua ndani ya chumba alichochukua hotelini baada ya kujidunga sindano iliyokuwa na madawa ya kulevya aina ya Dextromethorphan huku pembeni kukiwa na noti za dola, paundi, yuan na euro.
Hapakuwa na aliyejua sababu ya vijana hao kujidunga madawa hayo ya kulevya, kila mtu aliyepata habari za vijana hao alishtuka. Mpaka katika kipindi ambacho msichana mrembo, Stacie kujiovadozi madawa hayo.
Bado watu hawakujua sababu ilikuwa nini, ni afadhali kama wangekuwa wamepigika katika maisha yao, ila kilichoshangaza, walikuwa wakianza kupata umaarufu, kupata fedha, na ndipo kipindi hichohicho nao waliamua kujidunga madawa ya kulevya.
Dunia ikatetemeka, watu wakaogopa kuwa mastaa, wengi walisikia kwamba unapokuwa staa, ilikuwa ni lazima kutumia madawa ya kulevya.
Wazazi walipowaona vijana wao wanaanza harakati kupitia vipaji vyao, waliwazuia kwa kuona mwisho wa siku wangejiua kama hao wengine.
Swali kubwa ambalo waandishi wa habari walihoji, mitaani ni sababu gani zilizopelekea vijana hao kujidunga madawa ya kulevya? Kila aliyeuliza swali hilo, alikosa jibu kabisa.
Je, nini kitaendelea?
Kwa sababu gani watu maarufu walikuwa wakijiovadozi madawa ya kulevya?
Tukutane sehemu ijayo.