Riwaya: Mama wa Kambo(Part 1)

Riwaya: Mama wa Kambo(Part 1)

Simulizika

New Member
Joined
Mar 31, 2019
Posts
4
Reaction score
2
RIWAYA;MAMA WA KAMBO.
MTUNZI;RAJA SAIDY
WHATSAPP;0756920739
SMS;0621047841.

UTANGULIZI

Katika siku hizi watu wengi uwalaumu mama wa kambo kwa sababu za kimsingi,ikiwemo na kuwanyanyasa wanao wasiokuwa wa kuwazaa wenyewe.Mama wa kambo wengine,udiriki hadi kutenda kosa kisa tu.Mtoto siye wake.

Serikali imefanikiwa kwa kiasi fulani kudiri na jambo hili,kwani baadhi ya watoto upeleka mashtaka ya kunyanyaswa katika vyombo mbalimbali vya dola.

Jiunge katika riwaya hii upate kufahamu ni jinsi gani unavyoweza kumlea mtoto asiyekuwa wako pasipo roho ya chuki na manyanyaso vile vile kwani ukimnyanyasa madhara yake ni makubwa.

SEHEMU YA KWANZA.

Hali tulivu ya nyumbani hapo ilizidi kumpa hofu na mashaka Neema,alikuwa ni mwenye mawazo kwani tangia ameishi na mama yake wa kambo hakubahatika kununuliwa kitu chochote,kitakachomuwezesha katika kujistili au kujiona mtu kati ya watu.

Familia yao Neema iliyoonekana kudhohofika kwa nyada zote,na hii ilipelekea kushindwa hata kula hasa ifikapo asubuhi,Baba mzazi wa Neema alikuwa ni mtu asiyejihusisha kabisa na malezi ya familia yake.Alikuwa akiondoka asubuhi na kurudi saa sita usiku huku akiwa amelewa chakali.

Hali hiyo ilimkela sana Neema na hakuipenda kabisa kila siku alizidi kumuomba mungu aweze kumuepusha Baba yake mzazi katika swala zima la unywaji wa pombe....

Pasipo Baba yake Neema,familia ilikuwa haiendelei,Mama wa kambo wa Neema,alijitahidi kwa kila namna ili aweze kupambana na tatizo hilo,yote sababu hali ya nyumbani hapo ilizidi kuwa mbaya na hakuifurahia hata kidogo.

*****

Ilikuwa ni siku pili Neema pamoja na Mama yake wa kambo walikuwa hawajatia kitu chochote mdomoni na hali hii iliwafanya kudhohofika kiafya.

Baba Neema alitoka ndani huku akipiga miayo mfululizo na kutoka nje.

"Jamani kwaherini.."Baba Neema alizungumza kisha akaondoka.

Ilikuwa ni kawaida yake kufanya hivyo kwa kuwaaga kisha anaondoka bila kuacha kitu.

Neema aliaanza kulia mwenyewe baada ya kuona Baba yake mzazi anazidi kupotea na kuishi maisha yasiyofaa.

"Mama nimeacha shule kwa sababu ya maisha haya,tutaishi hivi mpaka lini??"Neema alimuuliza Mama yake huku akimkazia macho.

Mama wa kambo wa Neema alikuwa akimchukia Neema hivyo akaamua kumuangalia Neema na kuanza kuzungumza maneno ya kejeli.

"Kafukue kaburi la Mama yako kisha umuulize alimfanya nini Baba yako!!!Maana tangia niolewe na Baba yako Maisha yangu yamekuwa Mabaya."

"Mama usieme hivyo,nakuomba Mama tujishughulishe tusimtegemee Baba."Neema alizungumza huku akiendelea kulia.

"We igiza hapo na utakufa na njaa,ngoja mimi niende kutafuta mwanaume wa kuwa ananilisha na huyu nitakuwa naishi naye tu."

"Mama usifanye hivyo utapata maambukizi,tufanye kazi zilizohalali na zitakazotupa fedha aghalau tupate cha kuweka kinywani."Neema alizungumza huku akimpigia magoti Mama yake wa kambo.

"fyuuuu fyuuu"

Mama wa kambo wa Neema alifyonza huku akiingia ndani na kumuacha Neema aliendelea kulia muda wote.

Neema aliendelea kulia na kujikuta mpaka sauti inaanza kukata,na kuanza kutoa machozi pekee.

Haikupita muda,Mama wa kambo wa Neema.Alitoka ndani huku akiwa amevalia mavazi yaliochakaa,japokuwa alionekana kuwa tofauti na siku zote.Hali hiyo ilimshtua Neema na kumfanya aache kulia na kumtazama Mama yake wa kambo,Maana kwa haraka haraka aligundua Mama yake anatoka na kwenda mahali.

"Mama unaenda wapi???" Neema alimuhoji Mama yake huku akiendelea kufuta machozi yaliyokuwa yamesalia katika shavu zake.

"We ni nani kwangu??? we ni mume wangu au???"Mama wa kambo wa Neema alizungumza huku akimpiga kofi Neema na kumfanya akae kimya bila ya kuzungumza chochote.

Mama wa kambo wa Neema aliondoka na kwenda,pasipojulikana na kumuacha Neema akiwa nyumbani Peke yake.

*****

Baba Neema aliendelea kunywa pombe mpaka pale alipohisi inatosha kwa siku hiyo.Aliondoka huku akiwa anayumbayumba na kuelekea hadi mahali anapoishi Mke wake mwingine tofauti na Mama Neema.

Palikuwa sio mbali na mahali hapo palipokuwa hususi kwa ajili ya unywaji wa pombe.Baba neema alitumia muda mwingi kufika nyumbani hapo anapoishi Mke wake mwingine kwani kila alipokuwa anatembea alikuwa akidondoka chini na kuamka mwenyewe.

Alijitahidi Mpaka akafika mahali anapoishi Mke mdogo.

"ko! ko! ko!"

Baba Neema aligonga mlango baada ya kukuta umefungwa.

"Ingia!!!"

Sauti ya kike iliitikia.

Baba Neema alianza kuzungumza matusi ya kila aina.Jambo hilo lilipelekea Mke mdogo wake kutoka nje na kuanza kumchapa Baba Neema kwa kutumia chelewa.

Baba Neema alikuwa akipiga kelele kama Mtoto huku akiomba msamaha kwa Mke wake mdogo.

"Samahani Mke wangu sitalewa tena,samahani.."

Aliomba samahani na kumfanya mwanamke huyo kuachana na tendo la kuendelea kumchapa.

Baba Neema alijitahidi kusimama,aliingiza mkono katika nguo yake ya ndani na kuchomoa shilingi Elfu kumi kisha akamkabidhi Mke huyo kwa kufanya amkumbatie.

"Ahsante sana Mme wangu,ila punguza kulewa sawa???"

"Sawa mke wangu.."

Mke mdogo huyo alimnyanyua Baba Neema na kumpeleka ndani hili akapumzike,na sababu iliyofanya mwanamke huyo ampende sana Baba Neema,ni kwa sababu ilikuwa haipiti siku Baba Neema hajatoa matumizi.

Je,nini kitaendelea...............

%Kama unahitaji muendelezo nitafute Whatsapp namba 0756920739 au sms namba 0621047841.
1553078372118.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom