4
Niliendesha gari
kwa mwendo wa taratibu ili kumpa
kila mmoja uwezo wa kuona
wanyama vizuri . hali ya hewa
iikuwa tulivu yenye mawingu
mazito kiasi, rasha rasha ya mvua
ilianza kuanguka. baadhi ya
wanyama walionekana kujikunyata
chini ya miti mikubwa. sikuwa na
wasiwasi wowote "vency ona yule
simba amepanda kwenye mti
jamani.. alikuwa lucy simon
aliyekuwa ananionyesha
nilisimamisha gari ili kila mmoja
apate nafasi ya kumuona vizuri,
inapendeza sana nilisema. hii ni
ajabu sana uniani kuona simba
wapandao miti jaman... nilikuwa
nasikia kuwa simba wa manyara
national park wanapanda miti
sikuwahi kuamini. ila leo
nimeamini.. kweli hawa simba ni
waajabu sana duniani. baada
yakusimama kwa muda kidogo
tuliendelea na safari. mbele
kidogo tulikuta twiga akiwa
amezungukwa na kundi kubwala
punda milia na nyumbu wengi.
nikawauliza " ivi majua kwanini
punda milia na nyumbu hudumu
katika makundi ya pamoja? au ni
kwanini wote hao wapo pamoja na
huyu twiga? nhahaha steven
alicheka akasema sasa bloo hilo
nalo swali lakutuuliza sisi?
nikamshangaa na kumuambia kam
unaweza toa jawabu akasema "hii
ni kwasababu twiga anashingo
ndefu hivyo anauwzo wa kuona
mbali, kama akiona mnyama mkali
ambye anaweza kulizuru kundi
huwa anakimbia hivyo punda milia
na nyumbu nao hujihami kwa
kukimbia.... umejibu vyema bloo,
ila mbona kuhusu swali la punda
na nyumbu hujajibu? steven
akajibu weeeh! labda umuulize
man lula (thobias sospeter)
nan tobias tuambie.... nhahaha
alicheka kisha akasema mi sijui
man vency.. nikawaambia
sikilizeni... nyumbu anauwezo
mkubwa wa kunusa mahali mvua
na maji yapo hivyo huwez
kuhakikisha upatikanaji wa
chakula... ila punda yeye anao
uwezo wa kumbukumbu nzuri
hivyo nyumbu mara zote huwa
anongoza msafar wa kwnda lakini
wakati wa kurudi punda huongoza
njia kwa sababu nyumbu huwa
amesha sahau, kuna sababu
nyingine nyingi ambazo
badosiwezi kuzisema. baada ya
kusema hayo niliondoa gari
kuendelea kuzunguka porini.
kiukweli mbuga ilikuwa
inapendeza na hali ya hewa nayo
ilichangia mazingira tulivu
yaliyotufanya tuifurahie safari
yetu. tulibagatika kuona makundi
makubwa ya swala pamoja na chui
waliokuwawame pumzika juu ya
miti. baada ya kuzunguka kwa
takribani masaa matatu tulikuwa
tumesha ona wanyama wengi
nikawaambia sasa hivi tumebakiza
sehemu tatu za kwenda.. tutaenda
bwawa la viboko (HIPPO POOL),
tutenda ziwa manyara na baada ya
hapo tutaenda chemchemi ya maji
ya moto (HOT SPRING). na kuhusu
swala la kula tutaenda kula tukiwa
maji moto. wote waliafikiana na
mimi na safari ya kwenda bwawa
la viboko ilianza. tulitumia dakika
15 kufika pale, tuliangalia viboko
wengi wakubwa na wazuri walio
panda na mto kutoka ziwa
manyara. baada ya kupiga picha
kadhaa tulienda ziwani ambapo
tulikutana na kundi kubwa la
ndege aina ya flamingo,, ziwa
lilikuwa linapendeza sana kwa
muoneko wa hawa flamingo. kwa
mbali tuliona wavuvi wakifanya
shuhuli zo za uvuvi lakini
hatukuangaia nao kwakuwa
hawakuwa katika mpango wetu,
baada ya kutoka ziwani
ilituchukua lisaa lizimakufika
chemchemi ya maji moto, njiani
tulikutana na mchanga mwingi
ambao ulikuwa unazuia gari
lisiende mbele lakini kw kutumia
four wheel tulifanikiwa kuvuka
hatimaye tulifika maji moto.
chemchemi ilikuwa kubwa
inayotoa maji ya moto sana
ambayo yamepaswa moto sana
kwakuwa yanapita katika mwamba
wenye nguvu ya volkano. joyce
alisema "vency nimekuja na mayai
mabichi siulisema ukiweka kwenye
haya maji yanaiva....??
ndio... nilijibu naye akayaweka
mayai ma 5 kwenye maji baada ya
dakika 10 yalikuwa yameiva
tuliyatoa na kuyala, tulirejea garini
na kupata chakula cha mchana
tulichokuwa tumebeba, kwa mbali
tulionakundi la nyati lililo kuwa
limetengwa kwa kuwa umri
ulikuwa umesogea. tulikaa kwa
muda na saa 9 alasiri safari ya
kurejea nyumbani ilianza..
niliendesha gari kwa mwendo kasi
kidogo kwaku muda ulikua
umesha sogea kidogo tulipo fika
pale mahali ule mchanga ulikuwa
unatuzuia nilipunguza mwendo wa
gari kidogo .. nilijitahidi kushika
usukani makini lakini gari lilizidiwa
na nguvu ya mchanga hivyo
nililazimika kusimamisha gari na
nikashuka chini garini. ile nashuka
tu nilikutana na KITABUKIDOGO
kilikuwa kina rangi nyeusi
nilinama i na kukiokota sikutaka
mtu yoyote kukiona nilkficha
mfukoni na nikarudi garini haraka
kwakuwa sikutegemea kukutana
na kitabu mahali pale. nilipo jaribu
kuendesha gari lilikuw bado
linakataa kusogea nikakumbuka
kuhusu maneno niliyo ambiwa
pale mapokezi hofu ikaanza
kuujaa moyo wangu.!!!