RIWAYA: Kikosi cha Pili

RIWAYA: Kikosi cha Pili

sehemu ya mwisho

Taarifa yake ilifanyiwa kazi haraka na askari jeshi wapatao mia moja walitumwa kwenda bandarini kuzuia shehena ya silaha lakini pia kikosi cha watu saba kiliondoka kwenda kukabiliana na wanajeshi wanafundishwa huko kitunda ambao hawakuzidi miamoja wakiongozwa na Ibra mbaya.

*****

Kitu pekee walichokuwa nacho mikononi kmwao ilikuwa ni ramani ya eneo husika na wakapanda gari kuelekea huko,hwakuhitaji kupata masaada wa jeshiwao walitosha.

Wlibakiza hatua kadhaa iliwaweze kufika katika kambi ya waasi uchwara na hapo wakagawanyika watatu watatu kuizunguka kambi ile.

Ilikuwa kama mzaha walianza kuwaangusha vijana wa Ibra mbaya walikuwa wamewekwa kuizunguka kambi ile kwa ajili ya ulinzi.

Uwepo wa adui ukawa umegundulika na kilichofuta hapo ni risasi za moto kurindima kila kona lakini wangeliweza wapi ikiwa waliovamia ni makomndo wa kiwango cha juu kabisa wakiongozwa na Meja salim komba.

Ndani ya nusu saa mambo yalikuwa yamekwisha kuwaenda murama vijana wa Ibra mbaya.

*****

Huko ndani hali ilikuwa tete kwa waziri mkuu na waziri wa michezo walitamani kujiharishia kila wakijaribu kusema wakimbie hawakuwa na pa kutokea kabisa na msaada pekee ukabaki kwa Zegera,Seko,Niyankuru, na Ibra Mbaya.

Ibra mbaya na Zegera wakachukua jukumu la kuwalinda mabwanyenye wale huku wakitafuta eneo lillokuwa na nafuu waweze kutoka lakini hawwakujua huko nje hakukuwa na kijana yeyote aliekuwa hai na watui pekee walikuwa hai ni wao tu na walipojaribu kutokeza walikutana na mitutu saba ikiwatizama lakini mtu aliegwaya zaidi ni Zegera baada ya kuwaona vijana aliwasaliti wakiwa mbele yake akajaribu kukimbia na hapo akakutana namtumbaya kuliko alivyodhani a MWITA CHACHA.

Alipigwa bila kujua kapigwaje alikni si yeye tu msala ulikuwa umemwangukia Ibra mbaya liangukia mikononi mwa ziga yaani ni bora nagelipigwana zedi lakini si ziga.

Seko alikutana na Mina huku niyankuru akikutana AFSA zedi alibaki akiwatizama tu huku ulinzi ukiwa umewekwa kwa viongozi wale wasio wazalendo na nchi yao.

Dakika mbili mbele wajinga wale walikuwa metepeta laini Ibra mbaya alikuwa mbali na dunia au tuseme alikuwa ni marehemu baada ya kupokea kipigo safi kutoka kwa Ziga na zegera alikuwa hoi akitema damu tu bada ya kunyukwa na Mwita makame yeye alikutana na Dula na hakumwacha hai huku Deko akiwa amepigwa risasi ya mguu na meja baada ya kutaka kutoroka.

Zegera haustahili kuwa hai vijana wale watatu walimyewshea mvua ya risasi huku wakimwacha akiwa kama tenga kwa wingi wa tundu za risasi.

Mgeni wa kifaransa alikuwa amejikojolea baada ya kuona hana ujnja wa kutoroka.

Ving’ora vya jeshi vilikua vinasikika kwa mbali na punde kundi kubwa la wanajeshi lilifika pale na mtu wa kwanza kutiwa pingu alikuwa ni mnadhimu wa jeshi n a kisha mawziri wale wlifuata,waandishi wqa habari walikuwa tayari wamefika na walianza kupiga picha zisizo na idadi.

******

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliutangazia uma kuhusu majaribio ya kuipindua serikali huku akiweka wazi ubora wa kikosi cha pili mbali na kile cha jeshi kilivyofanya kazi hadi kuwaumbua watu wale,mbali ya kutaka kuipindua serikali lakini walimuua waziri wa afya na kujaribu kumuua waziri wa viwanda baada ya kuona hawasapoti ujinga huo,laini pia aliwataja watu waliokuwa nyuma ya mpango huo kama wabunge na badhi ya wakuu wa mikoa.

Mbali ya yote rais alisitihsa mahusiano na nchi ya ufaransa.

Dunia nzima ilizizima kwa taarifa hiyo hukumataifa makubwa yakiinyoshea serikali ya ufarnsa kushiriki njama hizo.


MWISHO WA SEASON ONE YA KIKOSI CHA PILI HIVI KARIBUNI UTAIPATA SEASON TWO


NDIMI BAHATI MWAMBA(KUDO900)

0758573660,0658564341



asalaamu kudo
Ahsanteni wote tuliokuwa pamoja tangu mwanzo hadi mwisho wa riwaya hii.
 
sehemu ya mwisho

Taarifa yake ilifanyiwa kazi haraka na askari jeshi wapatao mia moja walitumwa kwenda bandarini kuzuia shehena ya silaha lakini pia kikosi cha watu saba kiliondoka kwenda kukabiliana na wanajeshi wanafundishwa huko kitunda ambao hawakuzidi miamoja wakiongozwa na Ibra mbaya.

*****

Kitu pekee walichokuwa nacho mikononi kmwao ilikuwa ni ramani ya eneo husika na wakapanda gari kuelekea huko,hwakuhitaji kupata masaada wa jeshiwao walitosha.

Wlibakiza hatua kadhaa iliwaweze kufika katika kambi ya waasi uchwara na hapo wakagawanyika watatu watatu kuizunguka kambi ile.

Ilikuwa kama mzaha walianza kuwaangusha vijana wa Ibra mbaya walikuwa wamewekwa kuizunguka kambi ile kwa ajili ya ulinzi.

Uwepo wa adui ukawa umegundulika na kilichofuta hapo ni risasi za moto kurindima kila kona lakini wangeliweza wapi ikiwa waliovamia ni makomndo wa kiwango cha juu kabisa wakiongozwa na Meja salim komba.

Ndani ya nusu saa mambo yalikuwa yamekwisha kuwaenda murama vijana wa Ibra mbaya.

*****

Huko ndani hali ilikuwa tete kwa waziri mkuu na waziri wa michezo walitamani kujiharishia kila wakijaribu kusema wakimbie hawakuwa na pa kutokea kabisa na msaada pekee ukabaki kwa Zegera,Seko,Niyankuru, na Ibra Mbaya.

Ibra mbaya na Zegera wakachukua jukumu la kuwalinda mabwanyenye wale huku wakitafuta eneo lillokuwa na nafuu waweze kutoka lakini hawwakujua huko nje hakukuwa na kijana yeyote aliekuwa hai na watui pekee walikuwa hai ni wao tu na walipojaribu kutokeza walikutana na mitutu saba ikiwatizama lakini mtu aliegwaya zaidi ni Zegera baada ya kuwaona vijana aliwasaliti wakiwa mbele yake akajaribu kukimbia na hapo akakutana namtumbaya kuliko alivyodhani a MWITA CHACHA.

Alipigwa bila kujua kapigwaje alikni si yeye tu msala ulikuwa umemwangukia Ibra mbaya liangukia mikononi mwa ziga yaani ni bora nagelipigwana zedi lakini si ziga.

Seko alikutana na Mina huku niyankuru akikutana AFSA zedi alibaki akiwatizama tu huku ulinzi ukiwa umewekwa kwa viongozi wale wasio wazalendo na nchi yao.

Dakika mbili mbele wajinga wale walikuwa metepeta laini Ibra mbaya alikuwa mbali na dunia au tuseme alikuwa ni marehemu baada ya kupokea kipigo safi kutoka kwa Ziga na zegera alikuwa hoi akitema damu tu bada ya kunyukwa na Mwita makame yeye alikutana na Dula na hakumwacha hai huku Deko akiwa amepigwa risasi ya mguu na meja baada ya kutaka kutoroka.

Zegera haustahili kuwa hai vijana wale watatu walimyewshea mvua ya risasi huku wakimwacha akiwa kama tenga kwa wingi wa tundu za risasi.

Mgeni wa kifaransa alikuwa amejikojolea baada ya kuona hana ujnja wa kutoroka.

Ving’ora vya jeshi vilikua vinasikika kwa mbali na punde kundi kubwa la wanajeshi lilifika pale na mtu wa kwanza kutiwa pingu alikuwa ni mnadhimu wa jeshi n a kisha mawziri wale wlifuata,waandishi wqa habari walikuwa tayari wamefika na walianza kupiga picha zisizo na idadi.

******

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliutangazia uma kuhusu majaribio ya kuipindua serikali huku akiweka wazi ubora wa kikosi cha pili mbali na kile cha jeshi kilivyofanya kazi hadi kuwaumbua watu wale,mbali ya kutaka kuipindua serikali lakini walimuua waziri wa afya na kujaribu kumuua waziri wa viwanda baada ya kuona hawasapoti ujinga huo,laini pia aliwataja watu waliokuwa nyuma ya mpango huo kama wabunge na badhi ya wakuu wa mikoa.

Mbali ya yote rais alisitihsa mahusiano na nchi ya ufaransa.

Dunia nzima ilizizima kwa taarifa hiyo hukumataifa makubwa yakiinyoshea serikali ya ufarnsa kushiriki njama hizo.


MWISHO WA SEASON ONE YA KIKOSI CHA PILI HIVI KARIBUNI UTAIPATA SEASON TWO


NDIMI BAHATI MWAMBA(KUDO900)

0758573660,0658564341



asalaamu kudo
Ahsanteni wote tuliokuwa pamoja tangu mwanzo hadi mwisho wa riwaya hii.
Woyooo tanteee sana kudoo,barikiwa
 
Samahani ndugu zanguni lakini inabidi tu iwe hivi
Riwaya hii hapa chini inauzika na ipo mwanzo mwisho bila kuwa na season kwa sababu kitabu chake kinatoka tareh tano mei
Kwa garama ya Tsh 8000/=

Lakini kuna watu wanaeza wasipate Hardcopy kwa sababu ni chache hivyo yule atakaeihitaji softy copy yake tuwasiliane bei ni Tsh 4000/=
0758573660 kimesajiliwa ni marufuku kusambaza bila idhini ya mwandishi

Kionjo

Wakati huu ambapo wadunguaji walikuwa
wakijaribu kila namna ili wafanikishe kuwaona na
kuwapiga adui zao,ghafla ilisikika sauti ya helkopta
mahali hapo. Risasi kutoka helkopta mbili ambazo
zilitokea kusikojulikana zilianza kushambulia
msafara wa magari hayo.Hapo magari ya
kusafirisha pesa yakafunguliwa milango kisha
askari kadhaa waliovalia gwanda nyeusi,kofia
ngumu pamoja na fulana nzito maalum kwa kuzuia
risasi , walitoka kutoka ndani ya magari haya.Hawa
walikuwa ni askari wa weledi kutoka katika kikosi
maalum cha United States Marine Corps Forces
Special Operations Command(MARSOC ).Askari
hawa walianza kuzishambulia helkopta zile kwa
kutumia bunduki zao za kisasa kabisa aina ya HK
MP7.Lakini hawakufua dafu japo walitumia bunduki
za kisasa sana ambazo hutumiwa na Kikosi
maalum kingine maarufu sana cha makomando
kutoka katika taifa lao kijulikanacho kama Navy
Seal DEVGRU. Pengine ni kwa sababu katika
mapambano ni rahisi sana kwa aliye juu
kumuangamiza aliye chini kuliko aliye chini
kumuangamiza aliye juu. Adui waliokuwa katika
helkopta waliendelea kumwaga risasi nzito nzito
kama njugu bila kuwapa upenyo askari hawa
maalum kulenga shabaha.Vikosi vyote yaani askari
wa kitanzania na wale wa Marekani waliendelea
kupambana lakini kazi ilikuwa bado ni nzito sana.
Wakati mapambano makali yakiendelea , helkopta
nyingine ya tatu ikatokea upande wa mashariki.Hii
ilikuwa ya tofauti na hizi helkopta nyingine kiumbo
na ilikuja kwa lengo tofauti kabisa.
Helkopta hii ilikuwaimetundikwa ndoano kubwa
sana ambayo ilichomekwa minyororo minene na
imara sana minne.Minyororo hii kwa pamoja
iliunganishiwa sumaku kubwa sana iliyokuwa na
umbo la mche mraba iliyokuwa kama mita mbili za
mraba kila upande.Helkopta hii ilienda hadi juu ya
gari mojawapo kati ya yale magari yanayotumika
kusafirisha pesa, kisha ikagusisha lile sumaku juu
ya paa la bodi la gari hilo kisha ikaanza kupaa
tena.Kadri helikopta ile ilivyopaa ndivyo gari lile
lilivyoanza kunyanyuliwa polepole.Mwisho gari
lilinyanyuliwa juu zaidi na zaidi kisha kutokomea
angani.
Wakati huu ndipo adui wengine walijitokeza
kutokea porini na kuanza kushambulia.Map
ambano yakawa makali zaidi na kufanya eneo lote
kuwa kama eneo la vita kwa kelele za risasi.Askari
wa weledi wa idara ya C.T.I na wenzao wa kikosi
cha MARSOC waliendelea kupambana na adui
hawa waliokuwa wengi sana na waliopigana kwa
ari ya juu sana.Hata adui waliouawa kwa wingi
bado waliendelea kupambana kwa ari ya juu sana
kitu kilichosababisha vita kuwa ngumu zaidi na
zaidi. Kiongozi wa kikosi cha askari hawa wa
weledi wa kitanzania Kapteni Joshua na yule wa
kikosi cha Marekani cha MARSOC kamanda Lucas
Bradock waliongoza vyema vikosi vyao na
kuonesha uwezo wa hali ya juu kimapambano
.Lakini kutokana na ari na uwingi wa adui, vikosi
hivi vilianza kuzidiwa nguvu.
"We are out numbered,sergent John request for
backup". Kamanda wa kikosi cha MARSOC alitoa
maelekezo kwa askari wake kwamba afanye
mawasiliano kuomba usaidizi. "Okey Cover
me".Alijibu sajenti John akitaka kulindwa wakati
akifanya mawasiliano. Kwa kutumia kifaa maalum
cha mawasiliano alichokivaa katika sikio lake la
kushoto na kuanza kuwasiliana na makao makuu
ya muda kuomba usaidizi. Makao makuu haya ya
muda yaliweka kambi ndani. Huku makao makuu
helkopta tatu za kisasa ziendazo kasi aina ya
'Chinook' zilikuwa ziko tayari na makomando tisa
kutoka vikosi vya Navy SeAL Marekani pamoja na
makomando kutoka JWTZ Tanzania. Kikosi hiki
cha Navy Seal kilikuwepo Tanzania tangu miezi
mitatu iliyopita kwa ajili ya kufanya mazoezi ya
pamoja na vikosi vya makomando vya JWTZ ili
kuwaongezea uzoefu makomando hawa wa
Tanzania.
Kikosi hiki kilichojumuisha watanzania na
wamarekani kilikuwa tayari kutoa usaidizi tangu
walipopata taarifa za kiintelijensia kuwa msafara
ule umevamiwa.Walikuwa wanasubiri amri ya
kwenda kutoa usaidizi tu.Mara tu walipopata
mawasiliano, makomando hawa (Navy Seal na
JWTZ) walipaa na helkopta zao muda huo huo.
Uwanja wa mapambano kulikuwa na kelele za
risasi kutoka katika bunduki za wanausalama na
adui.Majibizano ya risasi yaliendelea huku idadi za
majeruhi na maiti zikiendelea kuongezeka kila
upande.Upande wa kikosi cha ' MARSOC' tayari
askari wawili walipoteza maisha na wanne
kujeruhiwa huku Tanzania ikipoteza askari wa
weledi wanne na mmoja kujeruhiwa. Upande wa
adui, walipoteza askari wengi zaidi kwa idadi
isiyojulikana. "Cease fire and take cover". Amri
nyingine ilisikika kutoka kwa kiongozi wa kikosi
cha 'MARSOC' na ambaye ndiye alikuwa mkuu wa
msafara huu kamanda Bradock.Amri hiibiliwataka
askari wote kuacha kupambana bali
wajifiche.Wakati huu ndipo kundi kubwa la adui
likajitokeza kutokea msituni na kuanza
kuyasogelea magari ya wanauslama wale kutoka
pande zote.Sura zao zilionesha kuwa ni watu walio
na asili ya somalia. Wengi kati yao walionekana
kuwa wachafu sana na wengine wadhoofu wa miili.
Lakini ni hawahawa walionekana kuvipa shida
vikosi hivi kwa muda wa saa moja na dakika
thelathini sasa.
Adui walizidi kuyasogelea magari ambayo
yaliwaficha wanausalama wale ndani yake.
Walionekana kuwa na uchu kama fisi mwenye njaa
aliyeona mzoga mahali.Sasa walizidi kusogelea
magari yale huku wakipiga kelele na kunyoosha
bunduki zao mbele.Wakiwa karibu sana na magari
yale,walisikia kelele za helkopta zaidi ya
moja.Kadri sekunde zilivyosogea ,mvumo ule wa
helkopta uliongezeka kuonesha kuwa pengine
helkopta ilikuwa inaelekea upande ule waliokuwapo
wao. Mara wakaanza kuziona helkopta zile
zikiwaelekea na wakati huo huo risasi zikaanza
kurushwa kuwaelekea adui wale . Adui walianza
kuanguka mmoja baada ya mwingine kwa kasi
kubwa.Vikosi vya uokozi vilikuwa vimefika tayari.
Bunduki aina ya FN Minimi 7.62 zilizofungwa
katika helcopter zilifanya kazi yake ipasavyo.
Makomandoo walioshuka kwa miamvuli mita
chache kabla ya kufika uwanja wa mapambano,
nao wakaanzisha mashambulizi ya ardhini na
kufanya adui kuzidiwa nguvu. Vikosi vya usalama
vilivyojificha ndani ya magari navyo vikaendeleza
mashambulizi kama mwanzo.Maadui wakaanza
kuzidiwa nguvu na kuamua kukimbilia msituni
huku wakibeba maiti za wenzao.
Hadi kufika saa kumi na mbili jioni,hakukuwa na
mapambano tena wala sauti ya risasi. Eneo
palipotokea mapambano , lilizungushiwa utepe
maalum na jeshi la polisi ili mtu yeyote asipite na
kuharibu upelelezi. Kisha askari kadhaa wakaletwa
kulilinda eneo hilo.
*********************************************
****************************************************
Mtaalamu wa teknolojia ya kompyuta ambaye pia
alikuwa mtaalamu wa kuvunjavunja ' password'
bwana Abdallah Yusoof,alifanya kila jitihada
kuhakikisha anafungua loki iliyofunga mlango wa
nyuma wa gari lile. Ni lile gari lililobebwa na
helkopta kule katika uwanja wa mapambano.
Alikwisha wahi kufungua loki nyingi sana lakini hii
ya leo ilihitaji umakini wa hali ya juu zaidi. Loki hii
ilitengenezwa kwa mfumo maalum ambapo
mfunguaji alipewa nafasi mbili za kuifungua.
Kukosea mara ya kwanza kungempa mfunguaji
nafasi ya pili.Kukosea mara ya pili kungesababisha
mlipuko kama wa bomu ambao ungeteketeza gari
pamoja na watu ambao wapo karibu na gari.
Abdallah au kama alivyozoeleka kwa ubini wake
Yusoof,alichukua waya fulani wa 'USB'
akauchomeka katika simu yake iliyokuwa na
programu maalum kisha upande wa pili wa waya
huo akauchomeka mahala fulani pembeni ya
kidubwasha kilichobeba vitufe vilivyo na namba
sifuri hadi tisa.Kidubwasha hiki kilifanana na mita
za umeme wa LUKU za TANESCO. Mara
alipochomeka waya huo, namba fulani zilionekana
zikipita na kubadilika kwa kasi katika kioo cha
simu yake kisha zikajitokeza tarakimu sita. Yusoof
akazibonyeza tarakimu zile katika kidubwasha
kile.Ukasikika mlio 'krack'. Loki ilikuwa
imefunguka.
Yusoof akafungua milango ya gari lile ,ndani ya
gari lile akaonekana mtu mwenye ndevu nyingi na
ndefu sana huku akiwa na upara wa haja. Mtu huyu
alikuwa amesheheni pingu madhubuti sana
zilizofungwa mikononi na miguuni. Yusoof
alizitawanyisha pingu hizi kwa risasi kutoka katika
bastola yake.Yule bwana akashuka kutoka katika
gari.
Naam.Labda ni kimo cha gari like kilichomfanya
atoke akiwa kainama kilichangia kumfanya
aonekane kuwa mtu wa kimo cha kawaida
tu.Aliposhuka kutoka katika gari lile alionekana
sasa kuwa mtu mwenye tambo kubwa na mrefu
sana. Japo alikuwa katika vazi kubwa la asili kama
yale yanayovaliwa na 'Wanigeria', lakini haikusaidia
kuficha kuonekana kwa misuli mikubwa
iliyojengeka katika mwili wake ule.Usoni
alionekana kama mtu aliye na umri wa miaka
mwishoni mwa arobaini au mwanzoni mwa miaka
hamsini.
Mara mtu huyu alipokanyaga ardhi,watu kadhaa
waliokuwepo mahali hapo wakiwa webeba bunduki
zao, walipiga goti moja chini na kukunja mkono wa
kulia mbele huku wakiinamisha ichwa chini usawa
wa mkono uliokunjwa kama ishara ya heshima
kubwa.Kwa kuwaangalia tu, ilionekana huyu
aliyekuwa mbele yao alikuwa mtu mkubwa na
mwenye kuheshimiwa sana na watu hawa.
Bwana yule akawataka watu wale
wasimame,akawakumbatia kila mmoja na
kuwabusu katika paji la uso huku akizungumza nao
kwa lugha ya kiarabu.Wakati huo huo helkopta
nyingine ikawasili eneo hilo.Hii ilikuwa na chapa
ya shirika la utangazaji la CNN. Bwana mkubwa
yule akaongozwa na watu wake hadi katika
helkopta ile na baada ya kupanda ikapaa na
kutokomea kutoka katika eneo hilo. Sekunde
chache baada ya helkopta ile kupaa, ile helkopta
iliyotumika kubeba gari, ililipuka na kuteketea
kabisa.
*********************************************
*****************************************************
"Breaking news".Ndivyo vioo vya luninga
vilivyosomeka siku hiyo.Vituo mbali mbali vya
televisheni vilikatisha matangazo ya kawaida na
kurusha habari hizi mpya zilizokuwa na msisimko
kuliko habari nyingine.Vituo vikubwa vya
televisheni na radio viliripoti moja kwa moja
kutoka eneo la tukio.Makamanda waliohusika
kuongoza msafara ule walihojiwa nao wakatoa
ushirikiano wa kutosha. Vyombo vya habari vya
kimataifa kama BBC,CNN,ALJAZEERA na Sky News
navyo viliripoti kupitia wawakilishi wake.Dunia
nzima ilipata habari hizi za kuogofya moja kwa
moja kwamba yule gaidi aliyeisumbua dunia kwa
uhusika wake katika matukio mbalimbali bwana
'Omar Al-Mahmood' ametoroka tena kutoka katika
ulinzi mkali sana.
Usiku ulipita,siku mpya ikaanza kwa mchaka
mchaka wa hali ya juu.Jua lilichomoza wakati
makachero wa polisi na wanausalama wa vitengo
na idara mbali mbali wakiwa wamemwagwa kila
kona ya nchi. Wanausalama walipewa maagizo ya
kuacha kazi nyingine zote zisizo na uhitaji wa
haraka na kipaumbele chao kiwe ni kesi hii
iliyokuwa mbele yao. Kesi ya kutoroshwa kwa
gaidi aliyesemwa kuwa ni hatari sana zaidi ya
magaidi waliowahi kutokea katika historia ya bara
la Africa.
Baadhi ya wananchi walisikika wakitoa sifa kwa
kituo cha habari cha CNN kwa kuwahi kuelekea
eneo la tukio kabla hata mapambano hayajapoa
vizuri. Watu wengine walienda mbali zaidi kwa
kusema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania
vimelala sana.Wapelelezi waliomwagwa kila kona
ya nchi walisikia habari ya helkopta ya shirika la
habari la ' CNN' kuonekana ikielekea eneo la tukio
kabla hata watu hawajajua ni nini kinaendelea.Lak
ini haikuchukua muda kwa wapelelezi kujua kuwa
ilikuwa ni helkopta ya 'CNN feki'. Magazeti nayo
hayakuwa nyuma kiripoti habari hii.
Gazeti la 'MTANZANIA MZAWA' liliandika " Gaidi wa
kimataifa aliyekamatwa na vyombo vya usalama
vya marekani kwa kushirikiana na Tanzania
ametoroshwa kutoka chini ya ulinzi mkali
alipokuwa anasafirishwa mara baada ya kutokea
mapambano makali sana.Gaidi huyo alikamatwa
katika mpaka wa Tunduma mkoani Mbeya wakati
alipokuwa akitaka kutorokea nchini
Zambia.Mapambano haya yalitokea baada ya
msafara huo kuvamiwa na kundi kubwa la watu
wanaodaiwa kuwa ni magaidi kutoka nchini
Somalia. Aidha maswali ambalo watu wengi
wanajiuliza sasa ni kuwa inawezekana vipi kundi
kubwa la magaidi kuvuka mipaka yetu na kuingia
nchini kwetu bila vyombo vya usalama kung'amua?
Na ni vipi watu hawa wavushe silaha nyingi kiasi
kike bila vyombo vya usalama kuona?"
 
J.K.T MAFINGA
Saa kumi na mbili na nusu jioni.
Ndani ya moja kati ya ofisi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),mlango uligongwa gongwa na mtu aliye nje.Sauti nzito ya mtu aliyekuwa ndani ilisikika ikisema "karibu".Mlango ulifunguliwa kisha ajenti Mick-reuben akiwa amevaa suti nyeusi iliyomkaa vyema ikisindikizwa na shati jeupe na tai nyeusi huku sikioni akiwa amevaa kifaa maalum cha mawasiliano kinachoitwa 'Tube Coiled Earpiece'.Kijana huyu alifunga mlango nyuma yake baada ya kuingia kisha akakaa katika kiti kilichokuwa mbele ya meza huku akitazamana na yule aliyekaa nyuma ya meza, mtu mzima mmoja ambaye alionekana kama mwenye umri kati ya miaka 50 hadi 55 hivi.
"Naitwa Mick-reuben kutoka C.T.I, nadhani ulipata ujumbe kuhusu ujio wangu".Aliongea kwa nidhamu kijana huyu huku akiwa katika hali ya utulivu wa hali ya juu.
"Ok, nimepata habari kutoka makao makuu na ndiyo maana niko ofisini hadi sasa.Mimi naitwa Aloyce Mwasambili.Ni mkuu wa kambi hili la Hapa mafinga.Nimepewa maagizo nikupe ushirikiano kwa kila utakachokitaka.Sijui nikusaidie nini kijana wangu."Aliongea kwa nidhamu pia mzee huyu ambaye mabegani alichafuka kwa nyota kadhaa.Alionekana kuwa mtu kwenye cheo cha juu.
"Kubwa hapa ni kuhusu tukio lililotokea na ambalo bado ni la moto kwa taifa letu na mataifa mengine.Tukio la kutoroka kwa gaidi wa kimataifa Omar al-Mahmood. Namna pekee ya kujua aliko kirahisi ni kwa kuwatambua baadhi ya watu wanaotuhumiwa kusaidia kutoroka kwake. Moja ya watu wanaotuhumiwa kuhusiana na tukio hili ni mtu ambaye hapo mwanzo alidhaniwa kuwa ji marehemu tangu mwaka 1998.Lakini katika upelelezi imegundulika kuwa yupo hai na anahusishwa moja kwa koja kwa kuhusika na tukio hili kwa namna moja au nyingine.Tumemtambua mtu huyu,kwa jina anaitwa John Karobota.Kwa kuwa hakufariki, ninaweza kusema kuwa alipotea akiwa na cheo cha luteni katika jeshi la wananchi,yaani JWTZ."Alianza kujieleza Mick kisha akaacha kwa muda kidogo kumuacha mwenyeji wake ayatafakari haya kabla hajaendelea kumueleza kwa kina.
"Sasa picha iliyopatikana inayotushuhudia kuwa mtu huyu yupo hai , imerekodiwa na kamera za kambi hii kwa hiyo tunaamini mtu huyu alikuwapo ndani ya kambi hii aidha kwa muda mrefu au kwa muda mfupi.Picha yenyewe ya mtu huyo ni hii hapa,sijui kama unaweza kuitambua".Alimaliza kueleza Mick huku akitoa 'Tablet' kutoka katika mfuko wa suruali aliyoivaa, kisha akapapasa kioo hapa na pale kisha picha waliyoipata ya John Karobota ikaonekana vizuri kabisa.Ni picha ya muda mrefu,lakini mkuu wa kambi hii bwana Aloyce alionekana kuitambua mara baada ya kuiangalia kwa sekunde chache tu.
"Picha hii siyo ngeni kwangu......Ahaa....Nadhani nimekumbuka kitu.Miezi kama mitatu hivi iliyopita,nilipigiwa simu kutoka makao makuu ofisi ya C.D.F(Mkuu wa Majeshi Tanzania). Simu hii ilipigwa na katibu muhtasi wa C.D.F, ambaye alinipa maagizo kuhusiana na ujio wa mtu huyu, kwamba atakuja katika kambi hii kwa muda mfupi kwa sababu ya kazi maalum anayoifanya katika mipaka ya nchi upande huu wa nyanda za juu kusini,yaani katika mkoa wa Mbeya kisha ataondoka.Kwamba hapa ndiyo itakua kituo chake kikuu wakati wote atakaokuwa akifanya kazi hiyo. "Alijieleza kwa maelezo ya mwanzo mkuu huyu wa kambi kisha akanyamaza kidogo akionekana kufikilia jambo fulani kwa kina kabla hajaendelea.
"Nilitambulishwa jina lake.Anaitwaaaaaaaa (huku akitafuta kitu katika makabrasha mengi yaliyokuwa katika droo za meza yake na kisha kutoa bahasha moja ya ukubwa wa 'A4'.akaifungua haraka na kutoa karatasi mbili zilizounganishwa kisha akaiangalia kwa haraka), yes....Anaitwa Jeremiah Mwakibinga.Cheochake ni Luteni. Lakini hiyo picha uliyonionesha haina utofauti sana na sura yake.Labda tu hiyo picha naweza kusema inamuonesha akiwa kijana zaidi ya alivyokuja hapa, au labda kama ni ndugu yake aliyefanana kwa asilimia mia."
"Na hii ni barua yake aliyokuja nayo na pia nilitumiwa ' email' kwa anwani ya makao makuu ya jeshi( huku akibonyeza hapa na pale katika keyboard ya kompyuta iliyo mezani pake) ambayo ni hii hapa".Alimaliza kuongea mkuu huyu wa kambi huku akimgeuzia Mick kompyuta yake ili aweze kuona barua pepe ile.
"Wewe umewahi kuzungumza na katibu muhtasi wa C.D.F kabla"Alihoji Mick Reuben.
"Ndiyo nimewahi kuzungumza naye zaidi ya mara ya tatu na hii ilikuwa ni ya nne.Tena kwa namba hiihii tangu nilipoteuliwa kuwa mkuu wa kambi hii miaka mitano iliyopita."Alijibu mkuu huyu wa kambi hii ya JKT.
Kisha mara tu alipojibu akaonekana kukumbuka kitu kwa ghafla ambacho ni kama kilimshitua kidogo.
"Lakini, kuna kitu nimekumbuka ambacho sijawahi kukifikiria hapo mwanzo.Nilipoongea naye mara ya mwisho,sauti yake ilikuwa kama inakwaruza hivi, siyo ile niliyowahi kuisikia kabla.Na siku ile alikuwa akiongea kama mtu aliyechangamka sana tena kirafiki kuliko kawaida ya siku zingine ambapo huwa anazungumza akiwa yupo siriasi , tena kwa sauti kama ya ki-amri amri hivi."Alimalizia kuongea mkuu huyu wa kambi,Aloyce Mwasambili.
Kengere ya hatari ikalia katika kichwa cha Mick.Tayari alikwishaunganisha maelezo haya na mambo ambayo yeye alikuwa akiyahisi, na kung'amua jambo katika kichwa chake.
"Ahsante.Ila kwa kukumbushana tu nadhani unafahamubkuwa tuliyoongea hapa ni siri kubwa na hakuna mtu anatakiwa kufahamu.Nikikuhitaji tena nitakutafuta.Naomba niondoke na barua hii kwa upelelezi zaidi pia naomba unitumie barua pepe hiyo uliyotumiwa katika anwani hii( huku akimuandikia anuani ile)." Akamaliza kuongea Mick.
"Haina shida.Nafurahi tu kama maelezo yameweza kukusaidia kwa lolote.Wakati wowote utakaponihitajiunakaribishwa sana".Aliongea mkuu wa kambi kisha wakapeana mikono na Mick.Mick akaondoka huku akionekana kufikiria mambo kadhaa kichwani.
******;********************************************************************************************
"Nimefanyia utafiti ile barua uliyokuja nayo pamoja na barua pepe.Nikianza na barua.Imefanana na barua za makao makuu ya jeshi kwa asilimia kubwa sana.Asilimia chache zilizobaki kufika asilimia mia iko katika muhuri uliopigwa katika barua hii.Kama unavyoona, muhuri wa jeshi uko katika umbo la duara.Lakini nikifananisha na barua nyingine kutoka makao makuu ya jeshi, zinatofautiana kidogo katika kipenyo kwa milimita moja na nusu.Pia umbali kati ya herufi na herufi umetofautiana kwa umbali ambao haiwezekani kutambua kwa macho ya kawaida.Mimi mwenyewe nimeng'amua hayo baada ya kui'scan' katika kompyuta na kutumia programu maalum ya kompyuta inayoweza kupima vitu hivyo."
"Nimeitafiti barua pepe ambayo ilitumwa kwa mkuu wa kambi ya jeshi Mafinga.Nimetafiti pia na namba ya simu ambayo mkuu wa kambi ya JKT Mafinga anadai kuwa ilipigwa kutoka makao makuu ofisi ya C.D.F na katibu wake.Vyote hivyo,yaani barua pepe na simu vilitumika kuwasiliana kutokea eneo la ofisi za mamlaka ya mapato (TRA) Mbeya. Ninadhani mpigaji simu na mtumaji wa barua pepe hiyo alikuwa mtaalamu au aliwezeshwa na mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano na inawezekana alitumia programu maalum kufanya mawasiliano hayo.Programu hiyo inamsaidia mtumiaji kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine,na hivyo nadhani mawasiliano ya ofisi ya C.D.F yaliingiliwa. Nathubutu kusema mtaalam wa teknolojia aliyehusika kufanya haya yawezekana ni mtaalamu wa hali ya juu sana kuweza ku-'hack' hata mawasiliano ya taasisi kubwa kama ofisi ya mkuu wa majeshi".
"Kwa sababu hiyo ninaweza kuhitimisha kuwa mawasiliano hayo pamoja na barua ile ni feki na wala hazihusiani na ofisi ya C.D.F."Alimaliza kuongea Clara.Wasikilizaji wake walikuwa ni ajenti Mick,mkurugenzi wa C.T.I, Maajenti wengine watatu wa C.T.I pamoja na mtu mmoja aliyekuja pamoja na mkurugenzi wa C.T.I ambaye wengine walikuwa bado hawajamfahamu.
"Kwanza naomba niwatambulishe mgeni wetu huyu. Kutokana na majukumu kuwa mengi, raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa George Katumba amemteua Josephat Moses kutoka idara ya usalama kitengo cha ulinzi wa rais,kuwa makamu mkurugenzi wa idara ya C.T.I. Sahani kwa kuwa mpaka wakati huu amekwisha kuhudhuria kikao chake cha kwanza ndani ya idara bila nyinyi kumgundua.Hii ni kwa sababu rais ameagiza aanze kazi mara moja."Aliongea mkurugenzi wa C.T.I na wanaidara waliokuwemo katika kikao hiki wakapiga makofi kama ishara ya kumkaribisha mgeni huyu.
"Lakini pia ,kutokana na alichokigundua Mick pamoja na maelezo haya ya ajenti Clara, basi ninadhani kuna umuhimu wa ajenti Mick na ajenti Clara kwenda kwenda huko Mbeya ofisi za mamlaka ya mapato TRA mkaanzie hapo.Wengine tutaendelea kutoa usaidizi kutokea hapahapa ofisini. Mtapata usaidizi wote mtakaouhitaji."Alimaliza kuongea mkurugenzi wa C.T.I.
Dakika ishirini baadaye,Ajenti Mick pamoja na Ajenti Clara walikuwa ndani ya helkopta iliyo na chapa ya polisi wakielekea Mbeya .
***************************************
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom