Riwaya: I died to save my President

Bila kusahau Jamvi la the Football limefunguliwa na kunakucha tyu mambo yameanza kuwa motooooooooooooo, huu mperampera wa the football ni hatareeeeeeeeeeeeeeee…..karibuni kwenye jamvi jipyaaaaaaaaa
 
I DIED TO SAVE MY PRESDANT

Mtunzi Patrick Ck

Simu 0764294499

Season 1

Sehemu 1


hughuli zote zilizopangwa
kufanyika katika kikao
cha bunge zilikamilika na
kabla ya kusitisha shughuli za
bunge kwa siku hiyo hadi siku
inayofuata,spika wa bunge
akamuita waziri anayeshughulika
na bunge mheshimiwa William
Kangoga ili aweze kutoa hoja ya
kutengua kanuni
“Meshimiwa Spika, naomba
kwa ruhusa yako sasa nitoe hoja
kwamba bunge lako tukufu
litengue kanuni ya bunge ili
kuwaruhusu vijana wetu
wanafunzi waliofanya vizuri katika
mithani yao ya kidato cha nne
waweze kuingia bungeni hapo
kesho.Mheshimiwa spika naomba
kutoa hoja”
Baada ya hoja ile kutolewa
wabunge wote wakasimama na
kuiunga mkono halafu spika
akawahoji na wote wakakubalianana hoja ile kwamba kanuni ya
bunge itenguliwe na kuwaruhusu
wanafunzi ishirini waliofanya
vizuri katika mitihani yao ya
kidato cha nne waweze kuingia
bungeni ili waweze kupongezwa na
bunge.
“Ahsanteni sana waheshimiwa
wabunge kwa kukubali watoto
wetu waje bungeni tuwapongeze
na kuwatia moyo ili waweze
kufanya vizuri zaidi huko mbele
waendako.” Akasema spika wa
bunge halafu akasitisha shughuli
za bunge hadi siku inayofuata saa
tatu za asubuhi
*********************
Ni saa tano za usiku sasa
lakini bado Patricia hakuwa na
usingizi.Yeye na mama yake
walikuwa katika chumba kilichoko
ghorofa ya nne ndani ya hoteli hii kubwa mjini Dodoma ijulikanayo
kama Dodoma view hotel.Ni moja
kati ya hoteli yenye hadhi ya juu
kabisa mjini Dodoma na ambayo
wabunge wengi wa bunge la
jamhuri ya muungano wa
Tanzania hupenda kufikia .
“Patricia mbona hulali?Si
unajua siku ya kesho itakakuwa
ndefu? Jitahidi ulale ili usije
ukasinzia katika ukumbi wa
Bunge” akasema Bi Doroth
Mwaukala mama mzazi wa Patricia
“Mama nashindwa kabisa
kupata usingizi siku ya leo.Usiku
nauona mrefu sana” akasema
Patricia binti aliyejaaliwa uzuri wa
kipekee mno
“Una wasi wasi?
“Ndiyo mama lakini si
sana.Nawaza kuhusu kesho sijui
itakuaje pale nitakaposhikana
mkono na mheshimiwa waziri
mkuu huku nikionekana katika
televisheni nchi nzima.Mama sikuwahi kuota siku kama ya
kesho itakuja kunitokea katika
maisha yangu.Bado siamini hadi
hapo nitakaposhikana mkono na
waziri mkuu ndipo nitaamini ni
kweli.Mama kesho ni siku yangu
kubwa mno” akasema
Patricia.Mama yake aliyekuwa
akimtazama mwanae
akatabasamu na kusema
“Usiwe na hofu Patricia.Hii si
ndoto bali ni kitu cha kweli
kinachokwenda kutokea hapo
kesho.Kama ingekuwa ni ndoto
tusingekuwa hapa Dodoma mida
hii katika hoteli kubwa na nzuri
kama hii.Patricia unapaswa
kujivunia mafanikio yako haya
makubwa uliyoyapata.Mwanangu
umenitoa kimaso maso mimi
mama yako kwani hakuna
aliyetegemea kama mwanafunzi
aliyeshika namba moja nchini
Tanzania atakuwa ni kutoka
katika familia masikini kama ya kwetu.Umeidhihirishia nchi na
dunia kwamba hata mtoto wa
masikini anaweza akafanya
mambo makubwa na ya
kushangaza.Umelipandisha
kileleleni jina la familia yetu na
kwa sasa sisi si watu wa
kudharaulika tena kama
ilivyokuwa hapo awali.Laiti baba
yako angekuwa hai kushuhudia
tukio hili sipati picha angekuwa
na furaha ya namna gani…”
akasema Bi Doroth.
“Mama sifa na shukurani
zimwendee mwenyezi Mungu kwa
neema na Baraka zake nyingi
kwangu lakini sifa na shukrani za
pekee pia ni kwako wewe
mama.Wewe ndiye kila kitu
kwangu na ndiye uliyefanikisha
haya yote yakawezekana.Umenipa
ushirikiano mkubwa.Maongozi na
maelekezo yako yameniweka
katika nafasi hii nilipo sasa.Mama
unastahili sifa za kipekee kwa kunijali na kuwa nami na
kunivumilia hata katika nyakati
zile ngumu kabisa.Umejinyima
mambo mengi ili mwanao niweze
kusoma na haya ndiyo matunda
yake” akasema Patricia halafu
akainuka na kuelekea dirishani
,akalifungua na kuutazama mji wa
Dodoma ulivyokuwa usiku hii.
“ Huu ni mwanzo wa safari
yangu ndefu ya maisha.Nina ndoto
nyingi sana za kutimiza maishani
na ndoto ya kwanza ni kuiondoa
familia yangu katika umasikni
huu mkubwa tulionao.Namuonea
huruma mama yangu namna
anavyohangaika
kunisomesha.Lazima nikiri
kwamba si kazi rahisi kwake lakini
amejitahidi kwa kila namna na
kuhakikisha kwamba hakuna siku
nimekosa shule.Huyu ni mama
anayestahili sifa za pekee kabisa.”
Akawaza Patricia halafu akalifunga dirisha na kurejea
kitandani
“ Patricia jitahidi ulale.Muda
umekwenda sana.Kesho
tunatakiwa tuamke asubuhi na
mapema” akasema Bi Doroth
“ Mhh ! mama sijui kama
nitaweza kupata usingizi.Sijazoea
kulala sehemu laini kama hii”
akasema Patricia na wote
wakacheka
“ Patricia unatakiwa uanze
kuzoea vitu kama hivi.Huu ni
mwanzo wako wa safari ndefu ya
maisha yako.Siku moja vitu kama
hivi utaviona vya kawaida.Jitahidi
ulale” akasema Mama yake halafu
akamfunika shuka vizuri akaenda
kuzima taa wakalala.
*********************

Ilikuwa ni mara ya kwanza
kwa Patricia kuingia katika
viwanja vya bunge.Aliustaajabia uzuri wa eneo hili.Hakukaukiwa
na tabasamu.Siku hii alikuwa
amependeza mno.Alivaa gauni
lenye rangi nyeupe chini na juu
likiwa na rangi nyeusi.Miguuni
alivaa viatu virefu vilivyoendana
na gauni alillolivaa.Mavazi haya ya
gharama alizawadiwa na Juliana
mwanamitindo maarufu hapa
nchini ambaye alifurahishwa mno
na matokeo ya Patricia.
Wanafunzi bora ishirini
walipokewa na katibu wa bunge
halafu wakakabidhiwa kwa
wafanyakazi wa bunge ambao
walianza kuwatembeza sehemu
mbali mbali za bunge .Patricia
alionekana kuwa na furaha
pengine kuliko wengine wote kwa
sababu hakujua kama siku moja
angeweza kufika mahala pale.Kati
ya wanafunzi ishirini waliofanya
vizuri mtihani wa kidato cha nne
wengi walionekana kutoka katika
familia bora zenye kujiweza kifedha.Ni Patricia pekee ambaye
alitoka katika familia iliyo masikini
zaidi lakini pamoja na umasikini
wa familia yake iliyokuwa ikiishi
katika chumba kimoja tu cha
kupanga ,aliweza kuwaongoza
wanafunzi wote nchini waliofanya
mtihani wa kidato cha nne na
kushika nafasi yakwanza.
Kwa siku ya leo ingekuwa
vigumu kuamini kwamba Patricia
anatoka katika familia duni
kwanamna alivyokuwa
amependeza kwa mavazi
aliyozawadiwa na mwanamitindo
Juliana.Wakati amekaa na
wenzake wakisubiri kuingia katika
ukumbi wa bunge mara akatokea
mama yake na kumuita pembeni
“ Mama kuna nini mbona
umefurahi namna hiyo?
“ Patricia huwezi
amini.Juliana amekuja .”
“ Juliana?! Patricia akastuka
“ Ndiyo “ Amekuja kufanya nini?
“ Amekuja kukusapoti katika
siku yako kubwa.”
“ Kweli mama ?!! akauliza
Patricia huku akiruka ruka kwa
furaha
“ Ndiyo Patricia.Anasema
kwamba hakutaka kukutaarifu
mapema kwamba atakuja alitaka
akushangaze”
“ mama yuko wapi dada
Juliana? Nipeleke nikaonanane
naye” akasema Patrcia na kwa
haraka wakatembea hadi katika
maegesho ya magari ambako
Juliana alikuwa garini na rafiki
yake aishiye mjini Dodoma.Mara
tu Patricia alipotokea,Juliana
akatoka garini na kumkumbatia
“Wow ! Dada Juliana sikujua
kama utakuja Dodoma”akasema
Patrcia.Juliana akatabasamu na
kusema
“Sikutaka kukutaarifu
mapema kama nitakuja Dodoma.I wanted to surprise you.Siwezi
kukosa katika siku yako kubwa na
muhimu kama hii ya leo.Patricia
najua una wasi wasi sana na
nimeona katika orodha ya watoto
ambao utaambatana nao leo
bungeni ,wote ni kutoka katika
familia zenye uwezo
mkubwa.Usiwe na wasi wasi you
have a huge support” akasema
Juliana na kumshika mkono
Patricia wakaingia
garini,akafungua mkebe mkubwa
wa poda na kuanza kumremba
halafu akavua heleni zake nzuri za
dhahabu
akamvisha.Akamuangalia na
kutabasamu.
“Now you look like a
princes.Go now.Tutaonana
baadae” akasema Juliana ,
Patricia akakimbia kwenda
kuungana na wenzake.Uso wake
ulikuwa na tabasamu zito.Baada
ya Patricia kuondoka,Juliana akaagana na Bi Doroth kwa ahadi
ya kuonana jioni ya siku hiyo
katika sherehe ya kuwapongeza
akina Patricia .
“Juliana nakushukuru sana
kwa msaada wako
mkubwa.Umeweza kunifuta aibu
kubwa siku ya leo. Bila wewe sijui
Patricia angeonekanaje leo.Lakini
kwa saabu yako leo Patricia
ameng’aa na kupendeza kuliko
wenzake wote” akasema Bi Doroth
“ Mama hupaswi
kunishukuru .Patricia ni kama
mdogo wangu.Mimi ni mmoja wa
watu walioguswa sana na matokeo
yake mazuriNinathamini sana
elimu hasa kwa mtoto wa kike na
ndiyo maana nimeamua kwa moyo
wangu kujitolea kumsaidia
Patricia ili aweze kutimiza malengo
yake.Bado ana safari ndefu sana
na ili afikie malengo yake
anahitaji sana sapoti yetu sisi
sote” akasema Juliana halafu akaagana na Bi Dprpth na
kuondoka kwa ahadi ya kukutana
jioni .
***************

Kipindi cha maswali na
majibu kilimalizika , Spika wa
bunge akasoma baadhi ya
matangazo ikiwa ni pamoja na
kuwatambulisha wageni waliofika
hapo bungeni kwa mafunzo halafu
akamuita katibu ili aweze kusema
ni kitu gani kilichokuwa
kinaendelea.Katibu akasimama na
kulitaarifu bunge kwamba ni
wakati wa kuwaruhusu wanafunzi
waliofanya vizuri waingie bungeni
wakabidhiwe vyeti na waziri
mkuu.Spika wa bunge akasimama
na kusema
“Waheshimiwa wabunge ,jana
tulitengua kanuni ya bunge ili
kuwaruhusu watu ambao si
wabunge kuingia ndani ya ukumbi wetu huu.Wageni tuliowaalika ni
wanafunzi ishirini bora katika
mtihani wa kidato cha nne
.Naombeni wakati vijana wetu
wakiingia humu
ukumbini,muwashangilie kwa
makofi kwani wamefanya kazi
kubwa sana” Akasema Spika na
kumuamuru askari wa bunge
awaongoze wanafunzi kungia
ukumbini .Lango kuu
likafunguliwa na wanafunzi
wakaingia wakiwa katika mistari
miwili,mmoja wa wanaume na
mwingine wa wanawake.Makofi
mengi ,vigere gere pamoja na meza
kugongwa vikasikika.Kilikuwa
kipindi cha furaha sana kwa
wabunge kuwashuhudia
wanafunzi wale ishirini bora.Spika
wa bunge akaomba utulivu halafu
akamkaribisha waziri mkuu ili
aweze kusema machache kabla ya
kuwakabidhi vyeti.Waziri mkuu
wa Tanzania mheshimiwa Thobias Kangeba kengaiza akasogea mbele
na kusema
“ Mheshimiwa spika naomba
nikushukuru sana kwa kunipa
nafasi hii niweze kusema
machache kuhusiana na tukio
hili.Napenda nikushukuru wewe
na bunge lako kwa kukubali
kutengua kanuni ili wanafunzi
hawa waweze kukaribishwa
bungeni na kupongezwa.Binafsi
ninafuraha kubwa sana kuwaona
wanafunzi hawa ingawa
ningefurahi zaidi kama
kungekuwa na uwiano sawa baina
ya wavulana na wasichana kwa
sababu naona kati ya wanafunzi
bora ishirini wasichana ni nane tu
na kumi na mbili ni
wavulana.Kuna haja ya kuendelea
kuwekeza zaidi katika elimu ya
mtoto wa kike ili kuwe na uwiano
sawa wa ufaulu.Pamoja na hayo
,kwa niaba ya serikali napenda
kutoa pongezi zangu nyingi kwenu wanafunzi kwa ufaulu huu
mzuri.Haikuwa kazi rahisi
.Yalikuwa ni mapambano na leo
hii mmeibuka
vinara..Nawapongeza pia walimu
na wazazi wenu kwa ushirikiano
wao wa kuwasaidia kuwafikisha
hapa mlipofika.”
“Mheshimiwa spika,mfumo
wetu wa elimu bado unakabiliwa
na changamoto nyingi kama vile
uhaba wa walimu,vitabu,vifaa vya
kufundishia na kujifunzia,lakini
serikali imekuwa ikjitahidi kutatua
changamoto hizi na leo hii
tunashuhudia mwanafunzi wa
kwanza Tanzania ametoka katika
shule ambazo zimejizolea
umaarufu kama shule za kata
ambazo zimekuwa na changamoto
nyingi.”
Makofi mengi yakapigwa
halafu waziri mkuu akaendelea
Mheshikiwa spika,ninaomba
niseme kwamba hata kama tukifanikiwa kutatua changamoto
zote zinazoikabiili sekta ya elimu
hapa nchini lakini bila juhudi
binafsi za wanafunzi wenyewe
kamwe hakutakuwa na ufaulu
mzuri.Kuna shule zenye walimu
wa kutosha na vifaa vya
kufundishia na kujifunzia lakini
hazikufanya vizuri .Kwa hiyo basi
naomba niwaase wanafunzi
waongeze kasi ya kujisomea
.Mwalimu ana nafasi yake lakini
mwanafunzi pia ana nafasi yake.Ni
vyema kila mmoja akaitumia
vyema nafasi yake.”
“Mheshimiwa spika naomba
nimalizie kwa kutoa pongezi zangu
nyingi kwa niaba ya serikali na
kuwatakia kila la heri wanafunzi
hawa katika safari yao
ndefu.Someni kwa bidii na taifa
linawasuri mje
kulitumikia.Hongereni sana”
akamalizia nasaha zake
mheshimiwa waziri mkuu,wabunge wakamshangilia
kwa kugonga meza halafu spika
wa bunge akasimama
“Tunakushukuru sana
mheshimiwa waziri mkuu kwa
nasaha zako.Natumai wanafunzi
wote wamekusikia na
watayafanyia kazi yale uliyowaasa
Waheshimiwa wabunge
kinachofuata sasa ni mheshimiwa
waziri mkuu kuwakabidhi vyeti
vijana wote ishirini.” Akasema
Spika na zoezi la kutoa vyeti
likaanza.Wa kwanza kuitwa
kwenda kupokea cheti alikuwa
Patrcia.Ukumbi wote wa bunge
ukalipuka kwa makofi na
kushangilia wakimpongeza
msichana huyu kwa kushika
namba moja.Zoezi lilipomalizika
baadhi ya wabunge walipata nafasi
ya kusema machache na kuwaasa
wanafunzi kusoma kwa bidii.Kila
aliyesimama hakuacha
kumpongeza na kumtolea mfano


Naitwa Patrick Ck mwandishi wa simulizi mbali mbali kama vile
MISS TANZANIA
SERENA
BEYOND PAIN
BEFORE I DIE
PENIELA
THE FOOTBALL
QUEEN MONICA
I DIED TO SAVE PRESIDENT
I WAS WRONG
TEN CHAPTERS
BRING BACK OUR GIRLS
KIAPO CHA JASUSI
KIKOSI CHA SIRI
Kumekuwa na matumizi mabaya ya baadhi ya riwaya zangu hapa katika jukwa letu.Riwaya kama The football,I died to save president ,Miss Tanzania zimekuwa zinarushwa humu JF bila ruhusa yangu.Tabia hii si nzuri na inakatisha tamaa wandishi ambao wanaumiza vichwa vyao kutunga hadithi na kuburudisha wasomaji lakini anatokea mtu na kuanza kutumia kazi bila ridhaa ya mwandishi.Ninatoa onyo kwa wale wenye kuendelea na mchezo huu wa kutumia riwaya za watu bila ruhusa tayari wanasheria wanalishughulikia suala hili na hatua stahiki zitachukuliwa kwa yeyote asiyeheshimu kazi za watu
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 71

Elizabeth akiwa na waombolezaji
wengine waliokuja kumfariji kufuatia kifo cha mumewe akausoma ujumbe
ulioingia katika simu yake.Ulitoka kwa
Frank
"Naomba tukutane saa moja na
nusu mtaa wa Luvigo nyumba No
63.Kuna jambo zito la muhimu sana
kuhusiana na mipango yetu nataka
tulizungumze.Kuna mtu muhimu sana
ambaye tutakutana naye
atakayetusaidia sana katika masuala
yetu.Hivi sasa niko katika
mazungumzo naye"
Elizabeth akarejea tena kuusoma
ujumbe ule halafu akajibu
"Frank siwezi kufika huko
mahala unakotaka nije.Naomba wewe
na huyo jamaa mfike hapa nyumbani
,nina wageni wamekuja kunifariji
siwezi kuwaacha" akautuma ujumbe
ule na baada ya sekunde kadhaa
ukarejea ujumbe akaufungua na
kuusoma "Ni mtu mzito na hataki
kuonekana na watu wengi hivyo
ametaka tukutane hapo mahala
nilipokueleza.Tafadhali jitahidi ufike
muda huo bila kukosa"
Elizabeth akausoma ujumbe ule
na kutafakari halafu akajibu
"sawa nitafika ila ninaomba
kikao kisichukue muda mrefu ,sitaki
wageni wangu wanaokuja kunipa pole
waboreke"
Baada ya kuutuma ujumbe ule
akampigia simu David
"Madam Elizabeth.Habari za
jioni?
"Habari nzuri David.Naamini
unalo jibu zuri mpaka sasa.Yule mtu
amepatikana?Amekwisha hojiwa
kuhusu Elvis?
"Mpaka sasa bado sijapata
mrejesho wowote kutoka kwa Dr Shafi
ambaye nilimpa jukumu hilo la kuhakikisha Meshack Jumbo
anapatikana.Nilizungumza naye muda
fulani bado hakuwa amepokea taarifa
kutoka kwa watu
aliowatuma.Nitampigia baadae kidogo
kumuuliza alikofikia kwani hivi sasa
hapatikani simuni yuko katika kikao
na rais"
"David nilikuelekeza suala hili
lifanyike haraka sana kabla ya jua
kutua lakini mpaka sasa hakuna
majibu yoyote ya kuridhisha.Hili si
suala la kufanyia masihara David.Ni
suala muhimu mno.Tunahitaji
kujiridhisha kama Elvis kweli amekufa
au yuko hai.Hatuwezi kuzipuuza
taarifa za kuonekana kwake
hai.Endapo ukishindwa kupata taarifa
hadi kesho asubuhi basi itatulazimu
kubomoa kaburi lake na kujiridhisha
kama kweli yumo kaburini au kifo
chake kilikuwa ni kiini macho.Elvis ni mtu hatari sana kuwepo hai" akasema
Elizabeth
"Madam Elizabeth naomba
nikuondoe hofu kwamba jambo hilo
litafanikiwa na nina uhakika kwamba
hadi mida hii tayari watu waliotumwa
kumtafuta watakuwa wamekwisha
mpata na yuko mahala akisubiri
kuhojiwa.Makamu wa rais
atakapomaliza kikao na rais
atanijulisha kila kitu"
"Sawa David.Utanijuliha pindi
ukipata taarifa yoyote kutoka kwa
makamu wa rais"
"Nitakujulisha Madam.Vile vile
kuna suala nataka nikujulishe ingawa
naamini hadi mida hii tayari utakuwa
umekwisha lisikia.Tayari operesheni
imeanza na hadi hivi sasa kuna vurugu
kubwa inaendelea mtaani.Vijana
wanaendelea kupambana na polisi na
tunashukuru kwa siku hii ya kwanza mambo yamekwenda vyema.Mpaka
sasa kuna idadi kubwa ya vifo na
majeruhi.Matukio yote yamerekodiwa
na timu iliyopewa jukumu hilo la
kurekodi kila kitu na kuanzia kesho
matuko yote ya mauaji ya raia
yataanza kurushwa katika vyombo
vya habari vikubwa duniani na dunia
itaanza kupaaza sauti kulaani mauaji
hayo na wakati huo huo maandamano
na vurugu vitaendelea katika mikoa
mingine na itafika mahala ambapo
serikali itashindwa kuyadhibiti
maandamano na hapo ndipo jeshi
litakapoingilia kati na kuchukua nchi"
akasema David
"Kazi nzuri sana David.Sina
wasiwasi kabisa kuhusu suala hili nina
imani mahala ulipo hapaharibiki
kitu.Utakuwa rais wa Tanzania muda
si mrefu sana ila zingatia suala la Elvis"akasema Elizabeth huku
akitabasamu
"Inshaallah.." akasema David na
kukata simu,akajaribu kumpigia
makamu wa rais lakini simu yake
haikuwa ikipatikana
"Bado yuko kwenye kikao"
akawaza na mara ukaingia ujumbe
uliotoka kwa Frank haraka haraka
akaufungua na kuusoma
"David nimeshindwa kupokea
simu zako niko katika kikoa muhimu
na watu fulani muhimu sana ambao
watatusaidia mno katika kufanikisha
mpango wetu.Ninakuomba tukutane
saa moja na nusu mtaa wa Luvigo
nyumba namba 63.Kuna mambo
mazito ya kujadili na hawa jamaa.Fika
bila kukosa" David akatabasamu
baada ya kumaliza kusoma ujumbe ule
"Ninachompendea Frank ni mtu
wa mipango.Naamini atakuwa amepata watu wazito wa kutusaidia
katika operesheni yetu" akawaza
halafu akarejea katika ofisi yake
alipokuwapo Dr makwa.
"Vipi maendeleo Dr Makwa?
"Mpaka sasa kwa taarifa
nilizozipokea kuna watu zaidi ya
ishirini wanaripotiwa kuuawa na
wengine wengi kujeruhiwa wengine
vibaya sana.Nimetaarifiwa kwamba
mapambano bado yanaendelea na
polisi wanaendelea kutumia silaha za
moto kukabiliana na vijana.Mambo
yanakwenda vizuri sana David na
tufanikiwa" akasema Dr Makwa.


*******************

Saa moja na dakika kumi na moja
Elizabeth akiwa na walinzi wake
wawili wakaondoka bila kuaga mtu yeyote.Tayari Steven alikwisha
mjulisha Juliana mpango waliouanda
ili kumuondoa mama yake pale
nyumbani hivyo Juliana alikuwa
makini akimchunguza mama yake na
mara tu alipoondoka akamfuata
Editha mtumishi wa nyumba ile
ambaye anaaminiwa sana na mama
yake
"Mama Editha ninaomba funguo
ya chumbani kwa mama kuna kitu
nakihitaji nimepigiwa simu na watu
wa Uingereza sasa hivi na mama
ametoka" akasema Juliana na yule
mwangalizi wa nyumba ambaye
huishi hapa wakati wao wakiwa
Uingereza hakuwa na wasi wasi hata
chembe akampa funguo ya akiba
Juliana akaenda kufungua chumbani
kwa mama yake na kuchukua
kompyuta mbili ndogo zilizokuwa
mezani akatoka na kumrejeshea yule mama funguo kisha akaingia garini na
kumpigia simu Steve.
"Steve tayari nimezipata zile
kompyuta.Tukutane wapi ili nikupatie
uzipitiea?Inabidi tufanye haraka
haraka kabla mama hajarejea"
akasema Juliana na Steve
akamuelekeza sehemu ya kukutana
"Omola una hakika utaweza
kumaliza kwa haraka kuzikagua
kompyuta zote mbili kabla Elizabeth
hajarejea nyumbani kwake? akauliza
Elvis wakiwa garini wakielekea
nyumbani kwa David
"Sina hakika kama tunaweza
kumaliza kukagua kila kitu kwa muda
huu mfupi.Nashauri tuogozane na
Juliana ili niweze kupata nafasi ya
kuendelea kuzikagua tukiwa garini na
mara tu mtakapomaliza na mimi
nitakuwa nimemaliza" akasema
Omola Hilo haliwezekani.Juliana
hapaswi kujua kama niko hai.Yule ni
mtu wa karibu sana na Patricia"
akasema Elvis
"Tayari anajua kila kitu" akasema
Steve aliyekuwa katika usukani na
Elvis akamtazama kwa mshangao
"Anajua?!!..Amejuaje?akauliza
"Nilimueleza kila kitu"
"Oh Steve kwa nini ukafanya
hivyo?
"Utanisamehe Elvis,nililazimika
kumueleza ukweli ila alielewa na
hawezi kumueleza kitu Patricia"
"Ulifanya kosa kubwa Steve
kumueleza Juliana kwamba niko hai"
" Nilikuwa na Steve alipomueleza
Juliana na hakuwa na namna nyingine
zaidi ya kumueleza na niliyesababisha
hadi akajua ni mimi.Unatakiwa
unisamehe sana kwani sikujua kama Juliana ni mtu wa karibu sana na
mkeo" akasema Omola
"Ok tuachane na hilo.Mnashauri
tufanye nini?akauliza Elvis
"Nashauri tuongozane na Juliana
kama alivyoshauri Omola ili wakati
tukiwa katika operesheni yetu yeye
atabaki garini na atakuwa anatusaidia
kufahamu kila kinachoendelea hapo
kwa David kwa ile kamera maalum
atakayoirusha na wakati huo huo
atakuwa anendelea kuzipitia
kompyuta za Elizabeth" akasema
Steve
"Sawa hakuna tatizo" akasema
Elvis na safari ikaendelea kuelekea
mahala walikopanga kuonana na
Juliana
Saa moja na dakika arobaini na
tatu Elizabeth akawasili mahala
alikoelekezwa na kulikuta gari moja
nje.Kwa mwangaza mkubwa wa taa iliyokuwapo getini aliweza
kumtambua mtu aliyekuwa nje ya lile
gari alikuwa ni David.
"David ?!! akashangaa
"Amefuata nini
hapa?akajiuliza.Akafunguliwa mlango
akashuka na kumfuata David ambaye
alishangaa sana alipomuona Elizabeth
pale
"Madam Elizabeth !! akasema
kwa mshangao
"David " akasema Elizabeth
"Mbona uko hapa mida hii
madam?akauliza akionekana kuwa na
wasiwasi
"Wewe nawe unatafuta nini
hapa?
"Nimeitwa na Frank.Alinitaka
tukutane hapa.Nimefika na kubonyeza
kengele ya getini lakini hakuna
aliyekuja kufungua.Najaribu kupiga
simu yake haipatikani" akasema David Hata mimi Frank amenitumia
ujumbe na kunitaka nikutane naye
hapa mida hii kuna mtu muhimu wa
kuzungumza naye" akasema Elizabeth
Walikaa hapo nje kwa dakika
zaidi ya kumi ndipo David aliyekuwa
ameongozana na walinzi wawili
akamtuma mmoja kujaribu kupanda
ukuta na kuchungulia ndani kama
kuna dalili zozote za kuwepo
watu.Mlinzi yule kwa haraka
akisaidiwa na mwenzake akapanda
ukutani na kuchungulia ndani
akaziona gari mbili
"Naona kuna gari mbili ziko
humu ndani " akasema yule jamaa
"Kama wapo humu ndani kwa
nini hawafungui geti?Hawasikii
kengele? Au yawezekana kengele ni
mbovu" akasema Elizabeth na mmoja
wa wale vijana wa David akalisogelea
getu na kugundua mlango mdogo wa pembeni ya geti haukuwa umefungwa
akausukuma ukafunguka,David
akatabasamu
"Muda wote huu tumekaa hapa
nje hatukukumbuka hata kuangalia
kama mlango uko wazi.Nenda ndani
wajulishe kuwa mimi na madam tuko
hapa nje " akasema David na yule
jamaa akaelekea ndani.Baada ya
dakika tatu akarejea kwa kasi
"What happened? akauliza David
"Mzee hakuna dalili za kuwepo
mtu humu ndani na kilichonistua
nimeona kuna alama za damu
sakafuni"
David na Elizabeth
wakatazamana
"Madam let's get out of
here.Hapa si sehemu salama.Nahisi
kuna hatari" akasema David kwa wasi
wasi No.We're not going anywhere!
akasema Elizabeth na kuwaita walinzi
wake na wale wa David
"Tunaingia humu
ndani,tunakwenda kuangalia hizo
damu zimetoka wapi?Kama kuna
hatari yoyote tutakabiliana nayo"
akasema Elizabeth na akiwa
ameongozana na wale walinzi
wakaingia ndani.Kulikuwa kimya sana
na hakukuwa na dalili zozote za
kuwepo mtu ndani.Walipofika katika
mlango wa kuingilia sebuleni
wakakutana na alama za damu.
"Hizi ni alama za kiatu ambacho
kimepita juu ya damu" akasema
Elizabeth ,mlango wa sebuleni
ulikuwa wazi wakaingia
ndani.Hakukuwa na mtu sebuleni na
zile alama za kiatu zilizokanyaga
damu zikaonekana.Elizabeth
akawataka wale walinzi watawanyike vyumbani kukagua damu ile imetoka
wapi na kama kuna mtu yeyote ndani
ya ile nyumba yeye akabaki sebuleni
akiwa na David.Baada ya dakika mbili
mmoja wa walinzi akaja na kumtaka
Elizabeth aongozane
naye.Akampeleka hadi katika chumba
kulimokuwa na miili ya watu wawili
waliouawa kinyama sana.
"Frank!!! Oh my God !!! akasema
David kwa mstuko mkubwa.Elizabeth
alipigwa na butwaa akahisi baridi
ikimpenya mwilini.David alihisi
kutetemeka mwili kutokana na woga
wa ghafla uliompata
"Madam let's get out of here!
Who ever did this must be around !!
akasema David kwa woga
"Quis unquam hoc esse non
reddere!! akasema Elizabeth kwa
lugha ya kilatini akiwa na maana
yeyote aliyefanya vile lazima alipe.Elizabeth akapiga magoti na
kumtazama Frank.
"Mauaji haya yamefanyika muda
mrefu na si hivi karibuni.Aliyefanya
mauaji haya alitaka tuje tushuhudie
alichokifanya na ndiyo maana
akatumia simu ya Frank kututumia
jumbe akitutaka tufike hapa akiamini
kwamba tukifika hapa tutashuhudia
alichokifanya.Alichokitaka
amefanikiwa na ujumbe
umefika.Tumeona alichokifanya na
kinachofuata naye asubiri salamu
zangu!!! akasema Elizabeth kwa hasira
kisha akamtaka David watoke nje
"Nani lakini kafanya ukatili huu?
akauliza David kwa sauti yenye
kitetemeshi ndani yake
"Kwa mazingira yalivyo ndani ya
chumba kile, inaonekana kulikuwa na
mapambano makubwa lakini
amewaua watu wangu kikatili sana.Mtu aliyefanya mauaji yale
lazima ni mtu mwenye ujuzi wa hali ya
juu na mbinu za
kupambana.Sikutegemea kabisa kama
Frank angeweza kuuawa namna hii
tena kwa wakati huu ambao
tunamuhitaji sana!! akasema Elizabeth
"Madam hapa nilipo
nimechanganyikiwa na sijui nini cha
kufanya.Frank alikuwa ni kila kitu
katika mipango yetu" akasema David
na kuinamisha kichwa chini
"Kuna taarifa zozote kutoka kwa
makamu wa rais kuhusiana na
Meshack Jumbo?akauliza Elizabeth
"Hapana sijapokea taarifa zozote
kutoka kwake mpaka sasa"
"Call him again" akasema
Elizabeth.David akachukua simu na
kumpigia makamu wa rais Dr Shafi
lakini bado simu yake haikuwa
ikipatikana Bado simu yake
haipatikani"akasema David.Elizabeth
akafikiri kidogo kwa muda halafu
akasema
"Twende tuondoke David tusije
tukakutwa hapa na polisi kwani
yawezekana huu ukawa mtego ili
tukutwe hapa na tukaonekana wauaji
"akasema Elizabeth wakaondoka

****************

Steve aliyekuwa dereva
aliendesha gari hadi mahala
walikopanga wakutane na Juliana,
akaegesha gari na kumpigia simu
Juliana akamjulisha kwamba tayari
wamefika na dakika chache baadae
Juliana akawasili na kumpigia simu
Steve akamtaka amuelekeze mahala
walikoegesha gari lao.Juliana
akashuka garini akiwa amebeba kompyuta mbili.Steve akashuka
akampokea kompyuta zile
akamfungulia mlango na kuingia
ndani
"Hallo Juliana" akasema Omola
"Habari Omola." akasema Juliana
"Juliana una hakika kwamba
hakuna mtu aliyekuwa anakufuatilia?
"Naamini hakuna" akasema
Juliana
"Ok good.Let's go" akasema Steve
na kuwasha gari
"Tunaelekea wapi?nahitaji
kurejea nyumbani haraka kabla mama
hajarudi.Huko mlikomtaka aende mna
hakika atachukua muda
mrefu?akauliza Juliana
"Tunahitaji muda kidogo wa
kuweza kuzipitia komputa zote na ili
kupata muda huo inabidi Omola
afanye kazi hii wakati akiwa garini
kwani tunamuhitaji pia huko tuendako.Usijali Juliana hatutachukua
muda mrefu" akasema Steve
"By the way .." akasema Steve
"Kuna mtu muhimu sana ambaye
hatukuwa tumekutambulisha
kwake.Kutana na Elvis" akasema Steve
na kunyamaza kidogo halafu akasema
"Elvis kutana na Juliana"
Elvis aliyekuwa amekaa kiti cha
mbele pembeni ya Steve akageuka na
kumtazama Juliana
"Hallo Juliana"
"Hallo .El..Elvis" akasema Juliana
kwa sauti yenye kitetemeshi
"Juliana ahsante sana kwa kuwa
karibu na Patricia"
"Usijali Elvis.Patricia ni mtu
wangu wa karibu
sana.Nimefahamiana naye muda
mrefu toka angali mnasoma kule
Tanga" akasema Juliana Juliana kuna jambo nataka
niliweke sawa.Umefahamu siri hii
kubwa ambayo ni watu wachache
sana wanaoifahamu hivyo nataka
asifahamu mtu mwingine yeyote hasa
Patricia.Tumeelewana? akauliza Elvis
"Hakuna tatizo Elvis.Your secret
is safe with me" akasema Juliana
"Good." akasema Elvis na safari
ikaendelea
"Omola kuna chochote
umekipata katika kompyuta
hizo?akauliza Elvis baada ya Omola
kuanza kuzikagua kompyuta zile
alizoleta Juliana
"Naendelea kupekua.Nahitaji
muda kidogo" akajibu Omola
Walifika eneo la Chongwe na
kushika njia inayoelekea Chongwe
kwa waziri mkuu.Ni eneo lililo kimya
sana ambako hukaa matajiri na
viongozi.Waliiacha njia inayoelekea nyumbani kwa waziri mkuu mstaafu
wakachepuka na kufuata njia
iliyokuwa inaelekea karibu na
hospitali ya Huruma,wakakunja kulia
na kufuata barabara inayoelekea
katika soko la samaki halafu
wakaingia mtaa wa Uwemba.Kiwanja
cha waziri mkuu mtaafu David
kilikuwa na ukubwa wa ekari kumi na
nane hivyo kiliweza kutokeza hadi
katika mtaa huu wa Uwemba.Kiwanja
kilikuwa kimezungushiwa ukuta
mkubwa na juu ya ukuta huo
kukawekwa nyaya maalum za umeme
kuongeza ulinzi.Sehemu kubwa ya
eneo hili la waziri David lilikuwa ni
shamba la matunda mbali mbali.Steve
akasimamisha gari pembezoni mwa
barabara .
"Hapa panafaa sana.Hili ni eneo
la nyuma na huku kote kuna shamba
la matunda." akasema Steve wakashuka na kufungua boneti ya gari
halafu wakaweka alama za pembe tatu
mbele na nyuma ya gari ili yeyote
atakayewaona ajue gari lile lilikuwa
na hitilafu.Omola akatoa kamera
ndogo iliyotengenezwa mithili ya
ndege akaiweka betri na kuiwasha
halafu akaiunganisha na kompyuta
yake akairusha kuelekea ndani.Kwa
yeyote ambaye angeiona angedhani ni
ndege kutokana na muonekano
wake.Alikuwa anaiongoza kwa
kutumia kompyuta yake na ilikuwa
inaleta picha moja kwa moja katika
kompyuta.Aliipeleka taratibu ili
kusoma hali ya ulinzi ilivyo ndani ya
jengo lile.Wakati kamera ikieleka
ndani Steve na Elvis walikuwa
wanajiandaa kuingia ndani kwa
kupitia ukutani.Kila mmoja alikuwa
ameweka sikioni kifaa maalum cha
kuwawezesha kuwasiliana na Omola ambaye atakuwa akiwaongoza kwa
kutumia ile kamera ndege aliyoirusha
mle ndani.
Walipokuwa tayari wakausogelea
ukuta na kwa haraka Elvis akawa wa
kwanza kuupanda hadi juu na bila
kugusa nyaya zile za umeme akaruka
na kutua ndani,Steve naye akafanya
hivyo kisha wakaanza kuelekea ndani
wakifuata ujia uliokuwepo kati ya
mstari mmoja wa matunda na
mwingine.Walitembea kwa tahadhari
kubwa hadi walipotokeza katika eneo
pana la wazi ambalo kati kati yake
ndipo lilipokuwepo jumba la David.
"Omola ,Omola
unanipata?akauliza Elvis
"Ninakupata Elvis.."
"Vizuri.Tayari tumetokeza katika
eneo la wazi na kutokea hapa
tunaweza kuiona nyumba.Tuelekeze njia kama tayari umepata picha ya
eneo lilivyo"
"Kwa picha nilizozipata hakuna
watu eneo hilo la nyuma na nimeona
kuna walinzi wawili tu wakiwa eneo
hilo lakini waliondoka na hawajarejea
tena.Upande wa mbele kuna walinzi
watatu ambao kwa picha niliyoipata
wamekaa nje wanapata chakula.Piteni
kwa kutumia mlango wa nyuma
uliopo karibu na bwawa la kuogelea"
akasema Omola.
"Nitatangulia" akasema Elvis na
kuchomoka kutoka pale mahala
walipokuwa akaanza kuelekea katika
mlango wa nyuma uliokuwa karibu na
bwawa la kuogelea.Kulikuwa kimya
kabisa na hakukuwa na mtu yeyote
eneo hili.Akaenda kujificha nyuma ya
pipa la maji.Steve naye akafanya kama
alivyofanya Elvis Elvis nimewaona tayari.Hakuna
hatari yoyote mpaka sasa mnaweza
kuendelea" akasema Omola na akina
Elvis wakainuka kutoka pale nyuma
ya pipa la maji wakaangaza halafu
wakatembea kwa tahadhari kuelekea
mlangoni.Mara tu walipofika mlangoni
akasikika mtu akizungumza na simu
akielekea kule kule mlangoni. kwa
haraka sana wakajificha nyuma ya
sanamu ya Simba iliyokuwepo karibu
na mlango.
Mlango ukafunguliwa akatoka
mwanamke mmoja akizungumza na
simu.Hakuwa na hofu yoyote na wala
hakujua kama kulikuwa na watu
wamejificha hapo karibu.Mwanamke
yule aliendelea kuzungumza na simu
na akaenda kukaa katika eneo la
bembea za watoto .Elvis na Steve
wakautumia mwanya huo wakatoka
taratibu katika ile sanamu na kuingia ndani wakazima taa halafu
wakajibanza pembeni ya mlango.Yule
mwanamke alipomaliza kuzungumza
na simu akarejea ndani
"Loh ! taa imeungua ?akasema
baada ya kukuta taa
imezimika.Akaufungua mlango na
kuingia ndani ghafla akajikuta
akikabwa na mkono yenye nguvu na
kuzibwa mdomo
"Ukitaka kuwa salama usipige
kelele yoyote.Nyamaza hivyo hivyo"
akasema Steve aliyekuwa amemkaba
yule mwanamke.
"Tuonyeshe mahala alipo Dr
Makwa yule mgeni wa David"
akasema Elvis
"Naombeni msiniuie jamani
nitawaonyesha mahala alipo" akasema
yule mwanamke kwa sauti ndogo ya
wasi wasi. Kuna watu wangapi humu
ndani?
"Kuna watu saba humu
ndani.Wengine wako sebuleni
wakiangalia runinga" akasema yule
mwanamama
"Haraka tupeleke alipo Dr
Makwa" akasema Elvis na yule
mwanamama akaanza kuwaongoza
kuelekea katika chumba
alimokuwamo Dr Makwa.
"Chumba chenyewe hiki hapa"
akasema yule mwanamama kwa sauti
ndogo.Steve aliyekuwa nyuma ya yule
mama akamkaba na kumpoteza
fahamu akamlaza chini taratibu Elvis
akausogelea mlango na kugonga
taratibu,mlango ukafunguliwa na
jamaa ambaye alikutana na pigo moja
kali la uso akaangukia ndani kisha
Elvis akajitoma ndani akiwa na
bastora yake.Kitendo kile kiliwastua sana wale jamaa waliokuwemo mle
ndani.Mmoja wa wao akachomoa
bastora haraka kutoka katika koti lake
lakini Elvis alikwisha muona na kwa
wepesi wa aina yake akaachia risasi
zilizomsambaratisha na kumrejesha
kwa mola wake.Dr Makwa ambaye
naye alikuwemo mle ndani akapatwa
na mstuko mkubwa sana akajificha
chini ya meza.Elvis akamfuata na
kumtaka atoke haraka sana.Huku
akitetemeka Dr Makwa akatoka chini
ya meza
"Vijana wangu tafadhalilini
nitawapa kila
mnachokihitaji.Nitawapa pesa yoyote
ile mnayoitaka,magari na kitu
chochote kile" akasema huku
akitetemeka
"Shut up !! akasema Elvis
Yule jamaa aliyepewa pigo
akaangukia ndani na kujifanya amepoteza fahamu akatoa bastora
yake taratibu lakini Steve aliyekuwa
amesimama mlangoni alikiona
kitendo alichotaka kukifanya yule
jamaa na hakuchelewa
akamsambaratisha haraka.Dr Makwa
akazidi kutetemeka na Elvis hakumpa
nafasi ya kujieleza akampa pigo kali
akaanguka chini na kupoteza fahamu
"Omola,tayari tumempata Dr
Makwa tunaanza kutoka nje.Vipi hali
ya usalama huko? akauliza Elvis
"Nje ninaona hali nzuri.Hakuna
ulinzi wowote huku nyuma.Walikuja
watu wawili kuchungulia na
kuondoka.Walinzi wote
wamejirundika sehemu ya mbele"
akasema Omola na Steve akambeba Dr
Makwa akamuweka begani wakaanza
kutoka mle ndani wakitumia njia ile
ile waliyopita.Hawakukutana na mtu yeyote hadi walipokaribia kufika
katika mlango wa kutoka nje.
"Omola tunatoka nje kuna mtu
yeyote umemuona? akauliza Elvis
"Hakuna mtu yeyote huku
nje"akasema Omola.Elvis akaufungua
mlango wa kutokea nje wakaanza
kuondoka kwa tahadhari kubwa
wakipita njia ile ya kuelekea katika
shamba la matunda.Wakafika sehemu
ile waliyoitumia kuingilia Elvis
akapanda na kukata zile nyaya za
umeme halafu wakampandisha Dr
Makwa na kumshusha kwa nje
wakampakia katika buti ya gari na
kuondoka kwa kasi
"Kuna chochote umekipata
kutoka katika kompyuta hizo? Elvis
akamuuliza Omola.
"Ninamalizia kupekua" akasema
Omola na safari ikaendelea hadi walipoliacha gari la Juliana.Omola
akamkabidhi kompyuta zake mbili
"Juliana ahsante
sana.Tutakujulisha nini tumekipata
kutoka katika kompyuta hizi.Kwa sasa
jitahidi uweze kuwahi kuzirejesha
ulikozitoa na kama utahisi kuna hatari
yoyote ile kutoka kwa mama yako
tujulishe tafadhali na tutakusaidia"
akasema Elvis
"Ahsanteni sana Elvis
nitaendelea kuwasiliana nanyi na
nitawajulisha kama kutakuwa na
hatari yoyote" akasema Juliana
akaondoka na kuingia katika gari
lake.Akina Elvis walihakikisha
ameondoka ndipo nao wakaondoka
"Kuna kitu umekipata kutoka
katika zile kompyuta? akauliza Elvis
"Kuna vitu vingi nimevipata
kutoka katika komputa zile hasa ile
ndogo nyekundu.Nimekuta kuna taarifa mbalimbali za kifedha ambazo
ili kuzifahamu vyema tutalazimika
kuwa na mtaalamu wa mambo haya ya
fedha.Inaonekana hizi ni taarifa za
fedha anazotumiwa na wataalamu
wake wa mahesabu karibu kila siku.Ni
fedha nyingi sana zinazoonekana
katika taarifa hizo, pamoja na taarifa
hizo kuna kitu kingine
nimekigundua.Nimekuta picha ya aina
ya silaha wanazoziuza.Ni bunduki za
hali ya juu na za kisasa mno.Ukiacha
silaha hizo kuna mawasiliano ya barua
pepe ya mtu anayetumia jina la Stella
Kendrick.Hili ninaamini ni mojawapo
ya majina ya Elizabeth
anayotumia.Katika mawasiliano hayo
Stella anawasiliana na mtu mmoja
anayetumia anuani ya mk3001 na
nilipodukua zaidi nikafahamu jina la
mtu huyo ni Keneth Mwaibuka
ambaye alimjulisha kuhusu kukwama kwa makontena kumi na mbili
bandarini na Keneth akaahidi
kulishughulikia suala hilo kwa
haraka.Vile vile akamjulisha kuwa
magari manne ambayo yamezuiliwa
kwa kigezo cha kodi akamtaka
ahakikishe magari hayo yanatolewa
haraka bandarini.Inaonyesha huyu
jamaa ndiye anayetumika katika
kusaidia kutoa mizigo ya silaha na vitu
mbalimbali bandarini." akasema
Omola
"Tutamchunguza na tutamjua ni
nani.Huyu naye ni mtu muhimu
pia.Kuna kingine ambacho
umekigundua?
"Nimepata pia mawasiliano kati
ya Shanon na Patrice Lwibombe.Mengi
wanayozungumzia ni masuala ya
kifedha.Bado sijafanikiwa kumpata
huyu Patrice ni nani na yuko wapi" Tumeshindwa tena kumpata
Patrice ni nani lakini msikate tamaa
tutamfahamu tu.Kwa kuwa tayari
tumewafahamu wahusika wakuu ni
akina nani tusiumize kichwa sana
kwani kupitia kwao tutaweza
kumfahamu Patrice ni nani.kwa sasa
tuelekeze nguvu katika kuyazima
mapinduzi haya yanayotaka
kufanyika" akasema Elvis
Waliwasili katika makazi yao na
Graca akawafungulia geti.Elvis
akagundua kitu katika sura ya Graca
"Graca kuna tatizo lolote?
akauliza Elvis
"Hali ya Vicky ilibadilika ghafla
na ikamlazimu Dr Philip amuondoe
hapa na kumpeleka hospitali.Alijaribu
kuwapigia simu lakini nyote simu
zenu zilikuwa zimezimwa.Mpaka sasa
hatujui hali yake ikoje" akasema Graca
na ndipo Elvis akakumbuka kweli kwamba alikuwa amezima simu na
kuiwasha akampigia simu Dr Philip
akitaka kufahamu hali ya Vicky
inaendeleaje
"Elvis hali ya Vicky ilibadilika
ghafla na nikalazimika kumleta
hospitali.Nilitaka kuwajulisha lakini
simu zenu zote hazikuwa
zikipatikana"
"Vipi sasa hali yake inaendeleaje?
"Elvis ninajitahidi sana kufanya
kila linalowezekana kuokoa maisha ya
Vicky but I have to be honnest with
you brother,I dont know if she's going
to make it.Mimi ni daktari na ninajua
ninachokisema" akasema Dr Philip na
Elvis akavuta pumzi ndefu.
"Dr Philip sijui niseme nini lakini
nakuomba ufanye kila
kinachowezekana ili kujaribu kuokoa
maisha yake.We still need her"
akasema Elvis kisha akaingia ndani Nimewasiliana na Dr philip hali
ya Vicky si nzuri na hana uhakika
kama atapona.She needs our prayers
right now" akasema Elvis na wote
wakashikana mikono na Graca
akaongoza maombi kumuombea
Vicky.
"Now let's get back to work"
akasema Elvis baada ya kumaliza
maombi.Dr Makwa akachukuliwa na
kuingizwa katika chumba
kinachotumika kama stoo akavuliwa
shati na kufungwa barabara katika kiti
halafu Elvis akachukua kichupa fulani
kidogo akakifungua na kumuwekea Dr
Makwa puani akapiga chafya
mfululizo.Steve akamsogelea na
kumnasa vibao viwili na ndipo Dr
Makwa akapata fahamu
"Please dont kill me!! akasema Dr
makwa kwa uoga mwili ukimtetemeka.Elvis akavuta kiti na
kuketi karibu yake
"Habari yako Dr Makwa.Pole kwa
misukosuko inayokukuta na samahani
sana kwa kukuchukua kwa njia hii"
"Ninyi ni akina nani mnataka nini
kwangu? akauliza Dr Makwa
"Kuna mambo machache ambayo
nahitaki kuyafahamu kutoka
kwako.Nataka kwanza uniambie kwa
nini uko pale kwa waziri mkuu
mstaafu David Sichoma? akauliza Elvis
na Dr Makwa akainamsha
kichwa.Steve akaenda nyuma yake na
kumtandika kofi zito la shingo
"Ukiulizwa unajibu haraka
hatuna muda wa kupoteza!! akasema
Steve kwa ukali.
"Tafadhali msinipige jamani nina
matatizo ya moyo"
"Hautapigwa kama utajibu kila
swali tunalokuuliza" akasema Steve Nitawajibu" akasema Dr Makwa
"David ni rafiki yangu wa muda
mrefu na pale kwake aliniita
nikajihifadhi kwa sababu ninatafutwa
na jeshi la polisi kwa kuandaa
mkutano usiokuwa na kibali na
kusababisha vurugu kubwa
inayoendelea hadi hivi sasa mtaani"
akasema Dr Makwa
"Kwa nini ukafanya hivyo Dr
Makwa? Kwa nini ukahamasisha
kufanywa mkutano usiokuwa na
kibali?Kwa nini ukapuuza agizo la
jeshi la polisi lililopiga marufuku
mkutano huo?
"Sisi ni wanasiasa na tumekuwa
tunaonewa na kunyanyaswa kwa
muda mrefu hivyo tumeona wakati
umefika wa kudai haki.Tunalilia haki
yetu,tunataka nchi itawaliwe kwa
misingi ya haki na si ukandamizaji unaoendelea hivi sasa"akasema Dr
Makwa
"Hakukuwa na njia nyingine ya
kufanya kufikisha ujumbe wenu kwa
serikali badala ya kuchochea vurugu?
"Tumejaribu sana kufikisha kilio
chetu serikalini lakini tumepuuzwa na
sasa tumechoka tumeamua kudai haki
yetu kwa lazima" akasema Dr Makwa
"Sawa nimekuelewa.Nataka sasa
utueleze familia yako iko wapi?
"Familia yangu?
"Ndiyo.Iko wapi?
Dr Makwa akawa kimya.Steve
aliyekuwa nyuma yake akamnasa tena
kofi lingine kali la mgongo
"Jamani mtaniua ...."
"Jibu swali unaloulizwa.Familia
yako iko wapi?
"Familia yangu ipo"
"Ipo wapi?
"Ipo nyumbani" Unaweza kuwapigia simu?
Dr Makwa akasita na kukaa
kimya
"Dr Makwa tafadhali jibu!!
akasema Elvis
"Familia yangu iko nje ya nchi"
"Umeisafirisha familia yako nje
ya nchi na kuwahamasisha watoto wa
wenzako waingie mtaani kufanya
vurugu na kuuawa.Kwa nini ninyi
wanasiasa mnakosa
ubinadamu?Unajua mpaka sasa ni
vijana wangapi tayari wamekwisha
poteza maisha kutokana na vurugu
ulizoziasisi?akauliza Elvis
"Vurugu wamezianzisha jeshi la
polisi.Endapo wangeturuhusu kufanya
mkutano wetu kwa amani mambo
haya yote yasingetokea"
"Nani unashirikiana nao katika
kuandaa machafuko haya? Mimi na wenzangu hatukupanga
machafuko bali tuliungana kwa
pamoja ili kuweza kuandaa mkutano
ambao tungeutumia katika kufikisha
malalamiko yetu kwa serikali."
"DrMakwa nimeanza kukuuliza
maswali kwa upole na nitapenda
kama tukiendelea na maongezi yetu
namna hii hadi mwisho.Tafadhali
usitulazimishe kutumia nguvu.Sisi si
watu wabaya lakini ukitulazimisha
tuwe watu wabaya utatamani
ungekutana na mtoa roho kuliko sisi"
akasema Elvis
"Vijana nimewajibu vizuri sana
kila mnachoniuliza.Sielewi ni kitu gani
hasa mnakitafuta toka kwangu"
akasema Dr Makwa.Elvis akamtazama
kwa hasira na kusema
"David anahusikaje katika
machafuko haya yaliyoanza leo? David ?!! Dr Makwa akastuka
sana
"David hahusiki kwa lolote lile na
haya yanayoendelea yule ni rafiki
yangu tu" akasema Dr Makwa kwa
wasi wasi.
"Dr Makwa tumekuleta hapa
tunafahamu kila kitu.David ni mmoja
wa watu walio nyuma ya haya
mliyopanga kuyafanya.Nini hasa lengo
lenu?akauliza Elvis na Dr Makwa
akawa kimya
"Dr Makwa nataka uniambie ni
akina nani wengine unashirikiana nao
katika mpango huu wa
mapinduzi?nafahamu wazo la kutaka
kuipindua serikali halikuja hivi hivi
lazima kuna watu wako nyuma
yenu.Nani aliyewataka muipindue
serikali? akauliza Elvis
"Lengo letu sisi ni kuondoa
serikali madarakani kwa kutumiamaandamano kama ilivyotokea katika
baadhi ya nchi watu waliandamana na
serikali zilizokuwa madarakani
zikaachia ngazi.Hatuna lengo la
kufanya mapinduzi kwa kutumia
silaha"
"Dr Makwa utaniudhi endapo
utaendelea kuniambia uongo.Nataka
unieleze ukweli mtupu kwani bila
hivyo hautaweza kutoka hapa salama
na mipango yenu yote itashindikana!!
akasema Elvis na kumtaka Steve ailete
kompyuta ya Omola .Steve akileta kwa
haraka na Elvis akamchezea Dr
Makwa mazungumzo yale ya David na
makamu wa rais.Rekodi zile
zilipomalizika Dr Makwa alikuwa
anatiririkwa jasho.Elvis akaiuka na
kuvua shati akamtaka Steve alete
kisanduku chenye vifaa vya
kutesea.Kisanduku kikaletwa na
kuwekwa mezani wakati wa mzaha umekwisha
sasa tunaanza kazi" akasema Elvis
"Hayo uliowasikia ni
mazungumzo ya unayedai ni rafiki
yako waziri mkuu mstaafu David
Sichoma pamoja na makamu wa rais
Dr Shafi.Nadhani umekisikia kila
walichokiongea.Ni wazi
kinachoendelea hivi sasa ni moja ya
mipango yenu ya kuiangusha
serikali.Nani aliyeko nyuma
yenu?Nani anayefadhili mpango huu
wa uhaini?akauliza Elvis huku
akichukua koleo dogo na kumtaka
Steve amvue Dr Makwa suruali
yake.Elvis akamvuta korodani na
kuiminya kwa kutumia ile koleo na Dr
Makwa akapiga ukelele mkubwa kwa
maumivu makali aliyoyapata.
"Huu ni mwanzo tu.Bado utapata
mateso ya kila aina hadi pale
utakapoeleza kila kitu kuhusiana na mipango yenu ya uhaini" akasema
Elvis
"Basi basi...nita...nitawaeleza kila
kitu" akasema Dr Makwa akiwa katika
maumivu makali
"David alinifuata na kunitaka
niwakusanye wakuu wote wa vyama
vya siasa vya upinzani na akatueleza
kwamba anataka atushirikishe katika
mpango wa kuiondoa serikali
madarakani na akasema kwamba
jukumu letu katika mpango huo ni
kuandaa vurugu ambazo
zitasababisha serikali iliyoko
madarakani iachie ngazi.Tukaandaa
mkutano huu uliofanyika leo na hata
pale ambapo jeshi la polisi liliupiga
marufuku sisi tulishinikiza ufanyike
kwa lengo la kuanzisha vurugu na
jeshi la polisi.Kilichotokea leo na
kinachoendelea kutokea ni matokea
ya mipango yetu.Sikujua kama hata makamu wa rais yumo pia katika
mpango huu.Mambo haya ninayosikia
wakiyazungumza hayakuwepo kabisa
katika makubaliano yetu"
"Dr Makwa hili jambo
mlilolipanga ni uhaini na endapo
utafikishwa katika vyombo vya sheria
adhabu yake ni kifungo cha maisha
gerezani.Right now I'm your only
help.Nitakusaidia endapo tu utaamua
kunieleza ukweli wote wa kuhusiana
mipango yenu.Kama utaamua
kufunguka na kunieleza kila kitu
nitafanya kila lililo ndani ya uwezo
wangu kukusaidia kuepuka adhabu
itakayokukabili endapo utafikishwa
mbele ya vyombo vya
sheria.Nitakusaidia uweze kuungana
tena na familia yako kwani vinginevyo
hautaiona tena familia yako
uliyoikimbiza nje ya nchi.Dr Makwa
wewe ni msomi mkubwa unaongoza chama kikubwa cha siasa chenye
wafuasi wengi.Ni mtu mwenye
heshima kubwa katika jamii kwa nini
ukakubali David akutumie kufanikisha
mipango yako?Alikuahidi kitu gani
hadi ukakubali kushiriki katika jambo
hili?Tafadhali nieleze kila kitu kwani
mipango yenu yote tayari imekwisha
julikana na haitaweza kufanikiwa.It's
over !!" akasema Elvis na Dr Makwa
akainamisha kichwa akilia
"Dr Makwa okoa muda tafadhali!!
akasema Elvis
Dr Makwa akamueleza Elvis kila
kitu kuhusiana na mipango yao ya
mapinduzi.Hakuficha kitu chochote.
"Huo ndio ukweli kijana
wangu.Naomba unisaidie kama
ulivyoahidi kuwa utanisaidia
kuninasua katika jambo hili" David anatoa wapi pesa zote hizi
za kugharamia jambo hili kubwa?Elvis
akauliza
"Hajanieleza chochote kuhusu
wapi anatoa fedha ila alichonieleza ni
kwamba nisiwe na wasi wasi na suala
la fedha kwani zipo za kutosha na
kiasi chochote ninachokihitaji
nimueleze atanipatia." akajibu Dr
Makwa halafu akakumbuka kitu
"Kuna kitu
nimekikumbuka.Baada ya wataalamu
wetu kuandaa mchanganuo wa
gharama zote za operesheni hii
nilimpelekea David akanihakikishia
kwamba kila senti tuliyoiorodhesha
itapatikana.Kesho yake akanifuata
ofisini kwangu kijana mmoja
akajitambulisha kwangu anaitwa
Pascal Situmwa na akadai kwamba
yeye na David ni washirika na akaanza
kunihoji kuhusiana na ule mchanganuo na ndipo nilipoanza
kujua kwamba David hayuko peke
yake katika mpango ule ana wenzake
ingawa sikuwahi kuwafahamu zaidi ya
huyo Pascal niliyemuona kwa macho"
akasema Frank
"Pascal is dead now"
"Unamfahamu?Nini
kilimua?akauliza Dr Makwa
"Dr Makwa kama kuna jambo
lingine ambalo unadhani linaweza
kutusaidia kufahamu nani hasa aliye
nyuma ya suala hili tueleze tafadhali"
"Vijana nimekwisha waeleza kila
kitu.Hakuna nilichokificha.Kama
ningekuwa ninafahamu nani aliye
nyuma ya jambo hili ningekwisha
waeleza.Nawaombeni sana jamani
mnisaidie nisijulikane kama
nimeshiriki.Ni tamaa tu ya fedha na
madaraka viliniponza.Niko chini ya
miguu yenu naombeni mnisaidie" akasema Dr Makwa.Elvis akamtazama
kwa makini halafu akamtaka Steve
amchukue akamfungie katika moja
wapo ya vyumba
"Elvis do you believe him?
akauliza Steve
"Yes I do.He's telling the truth.
Kwa maelezo haya ya Dr Makwa tuna
uhakika kwamba mtandao wa akina
Frank ndio hasa uliopanga mpango
huu wa mapinduzi kwa kuwatumia
hawa wanasiasa.Nani ambaye yuko
nyuma ya mpango huu wa kuiondoa
serikali madarakani?Lazima kuna mtu
ambaye anafadhili mpango huu kwa
fedha.Hilo ni swali ambalo tunapaswa
kulitafutia majibu usiku huu kabla
hakujapambazuka"akasema Elvis
"Elvis ulifanya chaguo sahihi
kabisa kuamua kufa kwani bila
kufanya hivyo haya yote
yasingegundulika.Kufa kwako kumeokoa maisha ya watu wengi
ikiwemo na rais ambaye naamini
hawa jamaa wangemuua.Nini
kinafuata baada ya kumpata Dr
Makwa na kufahamu kwa undani
jambo hil...." Steve akanyamaza baada
ya simu ya Elvis kuita .Alikuwa ni Dr
Philip.Elvis akaipokea kwa woga
"hallo Dr Philip"akasema na Dr
Philip akawa kimya kwa sekunde
kadhaa
"Dr Philip!! akaita Elvis
"Elvis,I'm so sorry.She didn't
make it.I'm very sorry" akasema Dr
Philip .Elvis akanyong'onyea ghafla
kwa taarifa zile
"Dah ! akasema na kumtazama
Steve
"She's gone" akasema Elvis na
uso wa Steve ukabadilika kwa mstuko
alioupata
RIP Vicky, dah kama Penny huyu anapeleleza kwa kutumia kizuri chake
 
Naitwa Patrick Ck mwandishi wa simulizi mbali mbali kama vile
MISS TANZANIA
SERENA
BEYOND PAIN
BEFORE I DIE
PENIELA
THE FOOTBALL
QUEEN MONICA
I DIED TO SAVE PRESIDENT
I WAS WRONG
TEN CHAPTERS
BRING BACK OUR GIRLS
KIAPO CHA JASUSI
KIKOSI CHA SIRI
Kumekuwa na matumizi mabaya ya baadhi ya riwaya zangu hapa katika jukwa letu.Riwaya kama The football,I died to save president ,Miss Tanzania zimekuwa zinarushwa humu JF bila ruhusa yangu.Tabia hii si nzuri na inakatisha tamaa wandishi ambao wanaumiza vichwa vyao kutunga hadithi na kuburudisha wasomaji lakini anatokea mtu na kuanza kutumia kazi bila ridhaa ya mwandishi.Ninatoa onyo kwa wale wenye kuendelea na mchezo huu wa kutumia riwaya za watu bila ruhusa tayari wanasheria wanalishughulikia suala hili na hatua stahiki zitachukuliwa kwa yeyote asiyeheshimu kazi za watu
Hii imekaaje
 
Safi sana...

Hakuna mkate mgumu mbele ya chai.. haya sasa Patricia ndiyo kashajiingiza kwenye mapenzi na Godson... na mpaka kuliwa kaliwa...

Inaonekana ataajingiza pia kwa Elvis...


Cc: mahondaw
kanishangaza sana" Yaani kujifanya kuwa mgumu kote kule but kaja kuliwa kiulaini ' kumbe na yeye beki hazikabi tu hana lolote"..... mwanaume mkware kama godson alipaswa kujiweka nae mbali mnoo
 
Write your reply...RIWAYA : I DIED TO SAVE PRESIDENT
SEHEMU YA 11
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Patricia are you ok? Akauliza
“ I’m ok”
“ Mbona unalia? What happened? Kitu gani kinakuliza?
“Sina atizo lolote dada Juliana.I’m just too emotional today.Kila nikikumbuka mambo yote ambayo umenifanyia toka tumefahamiana nashindwa kujizuia kutokwa na machozi.You are very kind” akasema Patricia.Juliana akamkumbatia halafu akamuomba Patricia alale apumzike
“ Patricia ananidanganya.Something is worng with her.Kitu gani kinachomsumbua na kumtoa machozi? Anyway nitatafuta nafasi niongee naye vizuri ili anieleze kitu gani kinachomkwaza.Kwa sasa ngoja apumzike amefanya kazi kubwa sana siku ya leo” akawaza Patricia
ENDELEA…………………………………………….
Ulikuwani usku mrefu mno kwa Patricia.Ilimchukua muda mrefu upata usingizi kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo.
Hatimaye kulipambazuika na baada ya shughuli za usafi kumalizika Patricia na mama yake wakaanza kujiandaa ili warejee nyumbani kwao.Kabla hawajaondoka Patricia akamuita Juliana chumbani kwake halafu akatoa mkufu wa dhahabu mfukoni na kumpatia
“Dada Juliana naomba umpatie Godson mkufu huu.Alinipatia kama zawadi lakini siwezi kuuvaa” akasema Patricia.Juliana akamuangalia na kusema
“ Patricia tell me what happened? Godson amefanya kitu chochote cha kukukwaza?Tell me please” akasema Juliana
“ Hapana dada Juliana.Hajanifanyia jambo lolote baya isipokuwa alinipatia mkufu huu ambao una thamni kubwa tofauti na mimi.Sina thamani ya mkufu huu wa gharama kubwa” akasema Patricia na kuzidi kumshangaza Juliana
“ Patricia wewe ni mdogo wangu.Please be honest with me.Did you and Godson had a fight? Godson aliniambia kwamba umemkubalia muwe wapenzi sasa nashangaa nini kimteokea?
Patricia akavuta machozi na kusema
“ Ni kweli tulikuwa wapenzi but not anymore.” Akasema Patricia
“ Patricia mbona hutaki kunieleza nini kimetokea? Godson amekufanya nini?
Patricia akainama akakosa neno la kusema .Akainua kichwa na kusema
“ Dada Juliana thank you for everything.I have to go” akasema Patricia ,akageuka akafungua mlango na kutoka.Juliana alibaki anashangaa .Akachukua funguo ya gari na kuwarudisha Patricia na mama yake nyumbani.Garini Patricia alikuwa mkimya sana.Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi sana
“ I’m so stupid.Ilikuaje nimruhusu Godson anivue nguo na kunifanyia vile.? I’m so weak and stupid.Nilimepnda sana Godson lakini kwa sasa simtaki tena kwa kushindwa kuyaheshimu mapatano yetu ambayo tulikubaliana kwamba hatutafanya mapenzi hadi pale nitakapokuwa nimemaliza masomo yangu.Lakini amenishawishi hadi tukafanya mapenzi.It was my first ime and I didnt know what to do.Sitaki tena kusikia suala la mahusiano.Sitaki tena kusikia suala la mapenzi.From today,I erase Godson from my heart and evey fibre of my body” akawaza Patricia akiwa garini
Kwa siku zote zilizofuata Patricia hakuwa akitoka numbani.Alikuwa mkimya sana na muda mwingi aliutumia kujisomea.Hakuw
asiliana tena na Godson na hakutaka tena kuonana naye licha ya Godson kujitahidi kumtafuta kwa juhudi zote ili waongee kuweka sawa mambo
**************************************
Hatimaye likizo ikamalizika shule zikafuguliwa .Safari hii Patricia alikwenda shule kwa basi.Hakutaka kupelekwa tena na Juliana kwani alitaka kujizoesha kusafiri mwenyewe.Vile alitaka kuanza kupunguza mahusiano na akina Godson taratibu.
Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Elvis kuonana tena na Patricia.Urafiki wao ukaendelea kama kawaida.
Ilikuwa ni siku ya Jumatano ya wiki ya pili toka walipofungua shule Patricia alisikia kizungu zungu akiwa darasani hivyo ikamlazimu kuondoka na kurejea bwenini ambako alikunywa dawa za kutuliza maumivu na kulala.Siku hiyo yote alishinda kitandani na hakuwa na hamu ya kula kitu chochote
Jioni ya siku hiyo alienda kuonana na Elvis bustanini ili kumtoa wasiwasi kuhusiana na hali yake.Elvis akamchukua na kumpeleka hadi katika mgahawa wa shule ambako huuzwa vyakula mbali mbali akamnunulia sahani moja ya chipsi pamoja na kuku wa kukaanga
“ Patricia siku nyingine usirudie tena kushinda bila kula chakula.Masomo ni magumu sana kwa hiyo unaposhinda bila kula chochote lazima utasikia hiyo hali ya kizungu zungu.Kwa sasa punguza muda wa kusoma hadi hapo hali yako itakapokuwa nzuri tena” akasema Elvis.
“ Elvis sikufanya makusudi kushinda bila kula chochote siku ya leo lakini sikuwa nikijisikia kula kitu chochote kile.Mchana wote nilikuwa najisikia vibaya sana lakini usijali kwa sasa najisikia vizuri .Nadhani hali hii ni kutokana na kusoma sana” akasema Patricia
“ Patricia pamoja na hayo lakini nakushauri pia kwamba kuna ulazima wa kupima na kujua kama unasumbuliwa na maralia.Toka tulipofungua shule nakuona kama umebadilika sana.Umekuwa mtu wa kulala s……” kabla hajamalizia sentensi yake Paticia akainama chni na kutapika.Elvis akaogopa
“ Patricia unaumwa twende nikupeleke katika zahanati ya shule usiku huu huu” akasema Elvis
“ Hapana Elvis.Ngoja kwanza nikalale kwa sababu kuna dawa tayari nimekwisha tumia.Kesho asubuhi kama bado hali yangu haitakuwa nzuri basi nitakwenda zahanati kupima.”
“ Hapana Patricia.Hali yako si nzuri na siko tayari kukuacha ukalale ukiwa katika hali hiyo. Ninakufahamu kwa muda mrefu na sijawahi kukuona ukitapika toka tumefika hapa shuleni” akasema Elvis
“ Nadhani ni kwa sababu ya hii harufu ya kuku” akasema Patricia na kumfanya Elvis ashangae
“ Harufu ya kuku? Mbona tumekuwa tukila kuku hapa shuleni mara kwa mara na hata mara moja haujawahi kuniambia kwamba unadhurika na harufu ya kuku? Akauliza Elvis
“ Hili tatizo nimenza kuliona baada ya kufungua shule.Kuna baadhi ya vyakula ambavyo hapo awali nilikuwa nakula bila matatizo lakini kwa sasa vimeanza kunishinda kabisa na kimojawapo ni kuku wa kukaanga.”
Elvis akamtazama Patricia kwa makini kama kwamba kuna kitu anakisoma usoni kwa Patricia
“ Ouh my gosh ! This cant be..” akanong’ona
“ Nini Elvis? Mbona unaongea mwenyewe? Akauliza Patricia.Elvis akamsogelea akamshika mkono akamuangalia usoni
“ Patricia ! akaita
“ Nini Elvis? Mbona unaniangalia namna hiyo hadi ninaogopa?
“ Usiogope Patricia.Mimi na wewe ni marafiki na tumekuwa tukishirikiana katika kila jambo.Tunalia na kucheka pamoja.Ugonjwa wako ni ugonjwa wangu pia.Binafsi ninakuamini kuliko hata mama yangu mzazi na ninaweza kukueleza kila kitu .Kuna kitu nataka kukuuliza Patricia na ninakuomba uwe muwazi kwangu.Just this once be honest with me Patricia” akasema Elvis
“ Elvis kuna nini? Patricia akauliza
“Ulikutana n a Godson wakati ukiwa likizo?
“ Ndiyo nilikutana naye japo si mara nyingi kwa sababu kwa sasa anafanya kazi katika kampuni ya simu kwa hiyo muda wake ni mchache sana na mimi mwenyewe nilikuwa nimebanwa na kazi nyingi”
“ Katika siku hizo chache mlizokutana mliwahi kufanya mapenzi?
“ What ?! Patricia akastuka
“ Nauliza mliwahi kufanya mapenzi ?
Patricia akainama akajawa na mawazo.Machozi yakaanza kumtoka
“ Ouh my gosh ! you did it” akasema Elvis kwa sauti ndogo.Patricia akaendelea kulia
“ Elvis yes we did it”akasema Patricia huku akifuta machozi.Elvis akashika kichwa kwa mikono yake alihisi miguu yake inaisha nguvu.
“ Patricia mlitumia kinga wakati wa kufanya mapenzi?
Swali lile likamfanya Patricia azidi kutoa machozi na kushindwa kujibu
“ Answer me Patricia….” Akasema Elvis huku naye machozi yakianza kumlenga
“ I’m so stupid Elvis.Hatukutumia kinga.Sielewi ni kwa nini nilijikuta nikikubali kufanya mapenzi na Godson na kusahau kabisa habari ya kinga”
“ Ouh gosh Patricia how could you do that?
“ I’m so fool Elvis” akasema Patricia na kuzidi kulia
“ Nyamaza kulia Patricia lakini naomba niwe muwazi kwako kwamba ulifany a kosa kubwa sana.”
“ What are you trying to say Elvis” akauliza Patricia
“ Patricia wewe ni rafiki yangu mkubwa na siwezi kukufica kitu.Inawezekana ukawa mjamzito”
“ What?!..That cant happen..” Patricia akahamaki
“ Inawezekana Patricia kama mlifanya mapenzi bila kutumia kinga.
“ Ouh Mungu wangu..nitafanya nini mimi kama ni kweli nina mimba? Please help me God” akasema Patricia na kuhisi miguu yake inaisha nguvu akakilaza kichwa chake mezani.Alilia machozi mengi sana.Elvis ambaye alihisi kuchanganyikiwa akamshika begani na kumuinua kichwa.
“ Patricia usilie tafadhali.Bado hatuna uhakika kama ni kweli.Hizi ni hisia tu lakini kuna ulazima wa kufanya vipimo na kubaini kama ni kweli au si kweli na kama ni kweli tujue namna ya kufanya” akashauri Elvis
“ I’m finished Elvis.I’m finished if it’s true.” Akasema Patricia
“Usihofu PatriciaKesho nitaongea na Thadei Yule dereva wa shule na atakwenda kutuletea kipimo cha kupimia ujauzito na baada ya kupima tutapata jibu.Kwa sasa naomba uende ukapumzike” akasema Elvis na kumshika mkono Patricia akamuongoza kuelekea bwenini .
NI KWELI PATRICIA NI MJAMZITO ?
lmfao " Mafisi kweli sio watu wazuri mamaee ".. god girl already gone bad
 
Safi sana...

Nimesikitika sana... Patricia mke wa Elvis analiwa uroda kizembe hivyo na Dr. Steven kisingizio stress za mama mkwe...

Elvis anajaribu kwa kila hali kukwepa vishawishi vya Doreen rafiki yake Patricia yote sababu ya kumpenda mke wake... ila mke ameenda kuliwa uroda...

Haya sasa Elvis ameelekea hoteli ambayo nae Patricia yumo humo humo akigawa utamu...

Ngoja tuone...


Cc: mahondaw
when it comes suala la kugongwa Patricia siku zote huwa analiwa kiboya sana" kumbuka alivyotelewa bikira", huyu demu inaonekana ana tabia kama za wema sepetu'' beki zake hazikabi kabisa Aisee
 
Daah.... Mambo yanakua magumu kwa Elvis, huku anatakiwa kuuwawa kule anagongewa mkewe....
haahaa unaweza pata kichaa" lakini nayeye si ameshalipiza kwa Doreen " kwa hiyo ngoma draw ..mbwa kala mbwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom