josephdeo
Member
- Nov 23, 2015
- 95
- 196
Muandishi:- Joseph .D. Migini
Call/txt:- +255766604683
Josephdeo70@gmail.com
Ndani ya chumba hichi cha wastani kilichoja samani za kufanya kuitwa sebule ya kisasa kwa waingiao. Nilikuwa nimeketi kijana Mimi umri wa miaka thalathini na mbili toka niwepo kwenye ulimwengu huu. Binafsi haiba yangu ni mtu mtaratibu hata nisipende Shari na yeyote.
Majira haya ya asbuhi nilikuwa nikipata kahawa iliyotayarishwa na mke wangu Brenda. Huku hisia za mawazo yangu zikiwa mbali na ulipo mwili wangu. Hata sikuweza kusikia kilio cha binti yangu wa miezi miwili niliyekuwa nimembeba mikononi mwangu.
Hisia hizi zilikuwa zimenichukua na kunirudisha nyuma. Kwa kadri ya miaka mitatu na kunikumbusha ni vitu gani nilipitia katika kipindi hicho. Mawazo mengi yalikuwa ni juu ya kuweka visa na mikasa hiyo kwa njia ya maandishi. Japo sio muandishi mahiri au mashuhuri lakini naweza kuyaelezea vyema haya yaliyonikumba kwa njia hiyo.
Sasa sina jibu la moja kwa moja juu ya sababu inayofanya kuyaandika haya. Zaidi ya nafsi yangu kunisukuma kufanya hivyo. Nilisogea mahali ambapo nahifadhi tarakishishi yangu ili niweze kutimiza haja hizi za moyo wangu.
Maisha yamekuwa fumbo gumu kulipatia ufumbuzi. Unaweza kudhani kuwa maisha yako binafsi yapo chini ya udhibiti wako na Mwenyezi Mungu kumbe hapana!. Bali maisha yako yanatengenezewa njia na binadamu wenzio.
Wapi upite, wapi ukanyage na wapi huruke yote hayo wanadamu wenzio ndio wanakutengenezea. Na mwisho kabisa waamua kuwa uwe wapi na nini kiwe hitimisho lako.
Nami nilikuwa kama wewe hapo unayesoma. Nilikuwa kama wewe kwa kudhani kuwa maisha yangu yapo kwenye udhibiti wangu na Mungu pekee. Mpaka pale yaliponikuta yale ambayo sikuyapanga wala kuyatenda mimi mwenyewe ila yalikuja kuhusu mimi.
Kama bado ujaelewa ninachokisema fuatana nami kwenye mkasa huu.
Nafikiri hii si namna nzuri, bora au pengine ya kufurahisha katika kuanza uandishi wangu. Je, mimi nimeonewa?, Lakini kabla ya kuwapa jibu hilo mnaweza kunijibu uonevu ni nini?. Hakika Mimi sijui ila naweza kuyaelezea yale yaliyo nikuta kisha wewe msomaji ndio unipe majibu kama nilionewa au la!.
***
Maisha yangu yote nimeishi nikiwa na ndoto ya kuwa mwalimu ili niinufaishe jamii iliyonizunguka kwa maarifa yangu. Lakini nilicholipwa ndio imebaki kama kovu moyoni mwangu. Nakumbuka vizuri sana, nakumbuka kila kitu kwa sababu hata ingekuwa vipi nisingeweza kuja kusahau hichi nilicho kipitia. Siwezi kabisa labda niwe mfu.
Nilikuwa mimi pamoja na watu wawili ambao nilikuwa nimewapatia kibarua cha kunilimia shamba langu. Tukiwa tunatoka shambani huku tukiwa kwenye barabara kuu ya kisiwa cha Maisome sehemu ambayo niliamua nifanye biashara ya kilimo. Siku hiyo tulipishana na gari tatu. Ilikuwa ni nadra sana kuliona gari ndani ya kisiwa kile. Achana na gari za kifahari kama hizo zilizotupita kwa kasi.
Nami nikaungana na wanakijiji wengine kushangaa hali ile ngeni sehemu ile iliyo na umasikini wa kutupa. Huku miundo mbinu ikiwa imezorota kiasi cha kufanya umasikini uote mizizi.
Walitupita kwa kasi sana na walipoondoka kwenye upeo wa macho yetu sisi tukaendelea na simulizi zetu zilizokuwa zimekatizwa na kupita kwa magari yale.
Umbali wa kutoka eneo nililokuwa nikiishi mpaka shambani ilikuwa inachukua hadi saa moja kwa mwendo wa haraka haraka na mwendo wa taratibu ilikuwa inachukua saa moja na nusu. Hivyo tulikuwa tunatembea haraka haraka wakati wa asbuhi wakati ambao tulikuwa tukienda shambani na wakati wa kurudi tulitembea taratibu taratibu.
Tukiwa njiani mara tukaona zile gari zikirudi na zilipofika usawa ambao tulikuwa mimi na wale wenzangu zikafunga breki za ghafla. Sisi tulikuwa kando ya barabara na tuliweza kulishuhudia hilo vyema. Baada ya kufanikiwa kuzishika breki na gari hizo kusimama wakatoka wanaume kumi kwa idadi yao huku wote wakituelekezea bunduki zao.
Sikuwa mtaalamu wa maswala ya intelijensia ila nilikuwa nimesoma baadhi ya simulizi kadhaa zilizokuwa zinaongelea mambo hayo. Huku pia nikiwa nimetazama filamu nyingi zilizokuwa zinaelezea dhahiri maswala ya kijasusi. Kwa elimu yangu ndogo eneo hilo ikanipa taarifa ya kutofanya chochote kile huku panga ambalo lilikuwa mkononi mwangu likianguka chini.
"weka mikono yenu juu!!". Mmoja kati ya wale wanaume akaamrisha nami nikawa wakwanza kutii.
Katika uelewa wangu mdogo nilielewa vyema saikolojia ya askari kuwa mara zote ujiona anayo mamlaka juu yako. Na yuko juu yako kimaamuzi hivyo haipaswi kumkosoa wala kuonekana wewe huko sahihi huku yeye akiwa kakosea. Hivyo jambo moja muhimu kuwahusu ni kwenda sawa sawa na wanavyotaka. Wote tukanyoosha mikono juu huku nikiwa sina wasi wasi kama wenzangu. Angalau mimi nilikuwa naelewa kidogo maswala hayo kuliko wenzangu ambao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana nayo.
"nani anaitwa Sospiter Muhinga kati yenu?". Moja kati ya Wanaume wale akatuuliza huku wakiongeza umakini zaidi juu yetu.
Hili lilikuwa ni jina langu ambalo nililitumia pote kwenye utambulisho wangu. Hivyo kusikia wanaume wale wakiliita jina langu kwa ufasaha kabisa nikashtuka. Huku hisia mbaya zikijengeka kwenye fikra zangu.
"Sospiter Muhinga ni nani kati yenu?". Mwanaume yule akarudia tena huku awamu hii akitoa sauti ya kuamrisha.
Haraka nikajibu. "mimi hapa boss".
"sogea pembeni mikono yako ikiwa juu!!". Akaongea huku sasa umakini ukiongezeka kwa watu wale huku midomo yote ya bunduki ikinilenga na wakanizunguka.
Japo sikuwa mtaalamu maswala ya kiusalama lakini nilihisi hatari inayonikabili huku nikiwa sina namna ya kujitetea. Kingine kibaya zaidi nilikuwa sijui wale ni wakina nani na wanataka nini kwangu. Haraka wakanisogelea huku wakiwa makini mno na kuanza kunikagua mwili mzima. Bado sikuelewa kile ni nini kwani mpaka wakati huo nilikuwa gizani nisielewe lolote lile.
Walipomaliza ukaguzi wao uliochukua dakika moja wakakunja mikono yangu iliyokuwa juu kutii amri yao. Kuigeuza kwa nyuma huku nikiwa bado kwenye tahamaki bwana yule akachukua pingu na kisha kuivalisha mikono yangu.
Sikutaka kuwa mbishi kwani niliijua saikolojia ya askari kama nilivyokwambia awali. Kuwa hawependi kuonekana wamekosea huku wewe ukiwa sahihi. Baada ya kumaliza zoezi hilo bado walionesha umakini wa hali ya juu kwangu kwa sababu ambazo sikuzielewa sababu tayari nilikuwa kwenye udhibiti wao.
Wakati wananingiza kwenye gari nikajikaza na kuuliza. "boss kuna tatizo gani?". Lakini hakuna aliyeonesha nia ya kunijibu swali langu licha ya kutumia sauti ambayo kila mmoja aliisikia.
Msobe msobe wakaniingiza kwenye gari yao huku maswali lukuki yakinitafuna kwenye kichwa changu. Kama vile hawa ni kina nani?, wanataka nini kwangu? na mengine mengi yaliendelea kuzunguka akilini mwangu pasipo majibu yoyote.
Kati ya yote sikuruhusu akili yangu kuchanganyikiwa juu ya hali hiyo ambayo imenikumba. Niliamini kwenye kutuliza akili hili niweze kutambua ni nini ambacho kinanikabili.
Watu wale wakanivika soksi kichwani mwangu ambayo ikaondoa uwezo wangu wa kuona. Kisha nikahisi kitu kikonichoma ambapo kwa kuhisi ncha yake nikafahamu kuwa ilikuwa sindano. Baada ya kuchomwa na sindano ile nilihisi mwili wangu ukiwa mzito ghafla kisha nikapoteza fahamu.
INAENDELEA......
Kwa maoni na ushauri nifuate kwenye mitandao ya kijamii kama:-
Fb:- falsafa70
Insta:- falsafa70
Twitter:- falsafa70