RIWAYA: Hamunaptra - Mji uliopotea

bioto

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
1,261
2,095
RIWAYA: HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA
MTUNZI: Richard MWAMBE
MAHALI: BAGAMOYO
SIMU: 0766974865

Riwaya ya kufikirika, itakayokupa taharuki, tafadhalisoma kwa makini ikiwezekana rudia mara kadhaa iliupate uhusiano wa mtukio yaliyoitengeneza riwayahii kali, tamu, haijawahi tokea katika kare hii

CHAPISHO LA 1

Seidon alipita kwa kasi na farasi wake mweupe,mwendo aliokuwa akienda ulikuwa si wa kawaidahata kidogo, kwa kuwa farasi huyo alimjua vyemabwana wake, alitii kila amrisho apewalo.

Kila alipogeuka nyuma, Seidon alishuhudia vumbilikitimka katika jangwa lile umbali mfupi kutokayeye alipo, aliongeza mwendo, na farasi wake alitii.Njia ilikuwa na mchanga mwingi, jua kali la utosililimfanya Seidon alowe kwa jasho, akiwa mkonommoja kashika lijamu ya farasi wake, mkonomwingine ulikuwa umeshika mfuko mweusi,hakukubali kuachia hata kimoja wapo kati ya vyote.Alimaliza kijangwa kile kwa tabu na kuuanza msitumdogo lakini wenye miti mingi na mirefu, vichakavilivyofungamana, aliangalia nyuma kwa maranyingine, bado aliona vumbi lile na sasa halikuwambali sana na hapo, moyo ulimdunda kwa kasi, kiuilimshika koo na kuipoza kwa jasho lililokuwalikitiririka usoni mwake.

Mara ghafla alijikuta akipaajuu na kujibwaga chini kama mzigo, mfuko mweusiulimtoka mikononi na kuangukia pembeni, farasiwake alikuwa akijaribu kuinuka kutoka palealipoanguka.“Ha ha ha ha aaaaaa, mbio za sakafuni huishiaukingoni!” sauti ilisikika kutoka katika kichaka chajirani. Seidon alishtuka na kujaribu kunyanyuka lakinialishindwa, kumbe alipoanguka aliteguka mgongo,alibaki kugugumia tu.Mwanaume mrefu aliibuka kutoka kichakani akiwaamevaa nguo nyeusi na kichwani kajifungakitambaa cheusi, kiunoni mwake alikuwa na jisukubwa, aliuokota mfuko ule na kuuchungulia ndani,kisha akatikisa kichwa kuashiria kuwa kilichomohumo ndani ndicho hasa akitakacho.

Akapiga mbinja kali, na mara katika vichaka vile waliibukawatu takribani kumi na tano wenye mavazi yakufanana na wote wameweka majisu makubwaviunoni mwao, wakakaribia eneo lile ambalo Seidonameangukia, wakamzunguka. Yule mkubwa waoakasogea jirani na Seidon, akamwinamia kamaanataka kumwambia kitu. Akamtazama, Seidonalikuwa nusu mfu.Yule kiongozi wao akatwaa upanga wake nakumchoma kidogo shingoni, Seidon aliinua kichwakumtazama.“Hata nikikukata kichwa nitapoteza nguvu zangu tu.Hao wanaokuja ndiyo watakaokuua.”

Yule kiongozi alirudisha upanga wake alani na kuwatazama vijanawake “Ale!” alito amri na mara farasi kwa idadi yaowalitoka porini na kufika eneo lile, wakapanda nakutokomea zao porini.∞∞∞“Shit!!!” aling’aka kwa hasira Bw. Kalban. Alimwangalia Seidon pale chini akiwa hajitambui.Alijishika nywele zake ndefu na kuzitimuatimua hukuakizungukazunguka bila mpangilio, aliona wazi kuwawamewahiwa kwa kila hali.“Kichwa kiko wapi?” alimuuliza Seidon kwa hasirahuku akimnyooshea upanga wake mkali.Seidon kwa shida aliinua mkono kumuonesha jamaawalipoelekea.

Bw. Kalban aliwageukia wafuasi wakeambao bado walikuwa juu ya farasi zao,“Wahamsud, wametuwahi!” aliwaambia vijana wake,ambao wote walionekana kugadhibika kwa hilo,wakifikiri jinsi walivyo mkimbiza kutoka mbali sanana wasipate wanachotaka.“Hatuwezi kukata tamaa, lazima tukipate kilekichwa, twendeni tuwafuate” Bw Kalban na wafuasiwake walipotelea porini kuwafuata waamsud nakumuacha Seidon palepale akiwa hajiwezi kwalolote.“Ha ha ha ha ha !!!” Bw. Hamsud alicheka akiwakashika fuvu la kichwa mikononi mwakeakiligeuzageuza “Mmmmh! Hapa ndiyo kila kitu,neema zote za ‘Klakos’ ziwe juu yetu” alipomalizakusema hayo wale wafuasi wake wakapiga magotina kuinamisha vichwa vyao, kwa pamoja wakaitikia“Amin, viwe kwetu sote”Kisha kwa pamoja walielekea kwenye jingo la kale,hamamu la Kipersia lililojengwa miaka zaidi ya miatano nyuma na kuingia, ndani humo kulijawa na gizanene lakini walipoingia tu lile fuvu likang’aa nakufanya mwanga ndani ya lile hamamu, mwangawake ulikuwa ni zaidi ya wa mchana unaoujuawewe.

Wakiwa ndani ya mavazi meusi, walizivutakofia zao zilizounganishwa na maguo yao meusiambazo daima huning’inia kwa mgongoni,wakajifunika na kukaa kwa kutumi amagoti katikamtindo maalumu.Bw. Hamsud akiwa na fuvu lile alitembea taratibuhuku akisemasema maneno Fulani kwa sauti yachinichini, mara akafika sehemu ya mbele kabisa,ambapo palikuwa na kitu kama sanamu ya mtulakini hakikuwa na kichwa, akainua lile fuvu nakukipachika kile kichwa juu yake. Radi kali ilipigana kulikata anga lote, vishindo vya kutishavikaendelea kusikika, wafuasi Wahamsud ndani yalile hamamu walilala kifudifudi wakisema manenoFulani Fulani.Wingu zito lilifunika anga lote na mvua yenye upepoikaanza kunyesha kwa fujo.“Shusha mema yako ee Klakos,” walirudiarudiamaneno yale wakiwa bado katika hamamu lile.Wahamsud, walikuwa ni jamii ya watu iliyoishi hukopembezoni mwa mto Ganges, jamii ya wakulimailiyokuwa na roho mbaya ya ubinafsi, kijiji chaokilikuwa ni kijiji chenye kila uhai, ardhi yenye rutuba,mazao na uoto wenye afya.

Lakini daima walipendakunyenyekewa na majirani zao, walipendakuonekana wao ni Miungu watoto , walizuia majiyam to Ganges yasiende kwa wengine, daimaalipora mali za majirani zao na kujilimbikizia wao,walikuwa hata wakipita maeneo mengine, wakionawanawake wazuri huwateka na kuwapeleka kijinikwao.Mara hii walipata habari juu ya fuvu la Klakos,Mungu wa zamani wa Wahabesiani, kihistoriailiaminika Mungu huyo aliishi miaka zaidi yamamilioni yaliyopita huko Hamunaptra, India.Ilisemekana kuwa Klakos aliweza kukupa kilautakacho, mvua, jua, mali, mazao, kuishi mudamrefu, kushinda vita na kila utakacho.

Tamaailimjaa Bw Hamsud, kiongozi wa jamii hiyo, aliwaitavijana wake wakakamavu na kuwapa habari hiyo, nakuamua kufunga safari kwenda Hamunaptra kutafutafuvu hilo kwa hali yoyote ile, wakafanya hivyo. Safariyao haikuwa rahisi kama walivyofikiria, ilikuwangumu sana ukizingatia wao hawakuwahi kuishijangwani, ilibidi wakatishe jangwa kubwa ili kufikahuko. Kama walitegemea wafike na kulichukua fuvuhilo na kuondoka basi haiakuwa hivyo, walikutajamii nyingi za watu wakitafuta kitu hicho hicho,achana na wale ambao wamekuja huko kujifunza‘study tour’ kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu.Kulikuwa na mchanganyiko wa watu wengi eneohilo.∞∞∞Warelvesh, walikuwa wakiishi kwa shida sana katikajangwa kubwa la Persia, wao walikuwa niwafanyabiashara lakini mara nyingi walikuwawakiporwa biashara zao na Wahamsud kilawaendapo kupeleka bidhaa zao sehemu mbalimbaliza ulimwengu.

Wakawa masikini, mji wao haukuwa na rutuba sanaya ardhi, walitegemea vitu vingi kutoka nje ya mjiwao kwa kununua au kubadilishana. Walikuwawema, wakarimu, hata wasafiri wakipita hapoilikuwa lazima wasimame na kupata japo chakulaau kinywaji.Walisikia habari fuvu lile wakiwa katika misafara yabiashara katika nchi za bara Hindi.Miaka 1200 iliyopitaSiku moja wakiwa katikati ya mji wa Jamunah, mtummoja aliyeonekana kama kichaa alikuwaakipayuka huku na huko habari juu ya fuvu hilo.Watu walimsikiliza na kumpuuzia.

Vernadalisimamisha farasi wake mweusi mwenye manyoyamengi ya kuvutia mbele ya kichaa huyo, alimtazamakwa tuo, juu mpaka chini, watu walikuwawakimfukuza kila apitapo na kelele zake. Vernadalimsikiliza kwa makini sana mtu huyo mwenyenywele ndefu na nguo chafu. Alipoona watuwatamshtukia kwa jinsi alivyomwangalia kichaa yulealimuamuru farasi wake kusonga mbele, baada yaumbali mfupi alisimama na kushuka kwenyemgahawa mmoja ili kupata kahawa.“Huyu mtu mbona ana kelele sana?” alimuulizammoja wa wahudumu wa mgahawa huo hukutaratibu akinywa kahawa yake na kashatazilizotengenezwa kwa karanga.“Ah huyo ni kichaa tu hana lolote, kila siku yeye nikelele hizo hizo, amechanganyikiwa” alijibiwa.“Mh!” Vernad aliguna na kumkazia macho mhudumuyule, kisha akaendelea “Fuvu! Fuvu ganianazungumzia?”“Aaah habari za zamani hizo kaka!”“Za zamani?! Kivipi?”“Huyu jamaa wanasema ni mchunguzi wa mamboya kale, sasa amechanganyikiwa na mambo mengiya ajabu aliyokuwa akiyaona wakati huo.

Hakunaanayejua kuhusu hilo fuvu, yeye anakazania ‘ukilipatalinakupa kila kitu’”Vernad alipotelea katika mawazo mazito, moyonimwake hakuona chembe ya uongo hata kidogokatika kelele zile za kichaa.Alitafakari kwa kina na akaona hakuna la kufanyalazima juu chini ampate kichaa yule ili apate ukweliwa habari hiyo na ikibidi ahakikishe fuvu hiloanalitia mkononi. Aliinua kichwa chake nakumtazama yule mhudumu, hakumuona, moyoulienda mbio au alikuwa anaongea na Jini?Hakupata jibu. Aliuvuta mkoba wake na kutoa dinarikadhaa na kuziweka mezani pale, moyoni aliazimiawazi kuwa lazima alale katika mji huo wa Hampustana kuhakikisha usiku huo ampate kichaa yule.Alitoka nje ya mgahawa ule na kushangaa kukutanana giza lililotanda nje, watu wakikimbia kimbia hukuna huko, alitazama vizuri angani na kuona ni kundikubwa la nzige likipita na kuzuia mwanga wa juakuifikia dunia.

Alipiga hatua chache na kuchukuafarasi wake kisha kurejea kule alikomuona kichaayule.Alikodi chumba kwenye nyumba ya kulala wagenikatikati ya mji ule. Baada ya kujipumzisha jioni ilealitoka na kutembeatembea mitaani, hakuchukuamuda mrefu sana mbele yake alikuta jumba kubwala kifahari lenye kila nakshi za kisultani,liliyapendeza macho yake hata kumfanya asimamekuliangalia.

Akiwa katika kulishangaa jumba hilondipo alipohisi kama kuna mtu nyuma yake,akageuka taratibu huku mkono wake ukiwaumeshika mpini wa jambia lake tayari kwashambulizi la aina yoyote ile.“Ha ha ha ha ha!!!!” kicheko cha kutisha kilizifanyanywele zake kusimama, hakuelewa aliyetazamanana ye ni binadamu au ni nani. Katika mtu huyo maraaliona sura ya yule kichaa mara kwa mchanganyikoiligeuka na kuwa ya nyoka, mara ya kobe. Vernadalirudi nyuma hatua kadhaa sasa jmabia lake likiwamkononi.“Unanitafuta! Umenipata, haya sema shida yako”Vernad alisikia sauti kama kumi na tano zikitokakatika kinywa cha mtu yule. Alishindwa afanyeje,aliendelea kurudi nyuma lakini bado alimuona mtuyule bado akiwa umbali ule ule kutoka kwake,aliamua kutimua mbio.

Kelele nyingi zilimfuatianyuma yake kana kwamba kuna watu walikuwawakimfukuza. Aliongeza mwendo kukimbia, hamad!Alijikwaa na kuanguka chini, alipojigeuza kutazamajuu kwa mtindo wa ‘chali’,radi kali ilimpiga usonihata kuhisi kuwa amepoteza nuru ya kuona.

USIKOSE SEHEMU YA 2
 
“Unanitafuta! Umenipata, haya sema shida yako”Vernad alisikia sauti kama kumi na tano zikitokakatika kinywa cha mtu yule. Alishindwa afanyeje,aliendelea kurudi nyuma lakini bado alimuona mtuyule bado akiwa umbali ule ule kutoka kwake,aliamua kutimua mbio. Kelele nyingi zilimfuatianyuma yake kana kwamba kuna watu walikuwawakimfukuza. Aliongeza mwendo kukimbia, hamad!Alijikwaa na kuanguka chini, alipojigeuza kutazamajuu kwa mtindo wa ‘chali’,radi kali ilimpiga usonihata kuhisi kuwa amepoteza nuru ya kuona.

CHAPISHO LA 2

Kaupepo katamu kalimpitia Vernad, alijaribu kuamkapale alipokuwa lakini ilikuwa ni vigumu kwake.Alilala tena kwa utaratibu katika vumbi lile, kwaharaka haraka hakujuwa ni wapi alipo, jangwakubwa lilimzunguka na jua kali lilimchoma uso,alichokiona sehemu hiyo ni misafara ya ngamiakutoka eneo moja kwenda lingine.

Alifanikiwakunyanyuka baada ya kukusanya nguvu nyingi sana,aliinuka na kujipukuta vumbi lilioujaza mwili wakena kumfanya awe kama kinyago. Aliyaficha machoyake kwa viganja vya mikono yake ili kupambana nanuru kali ya jua iliyomlenga moja kwa mojamachoni kwake.Kutoka mbali aliona farasi aliyekuwa akielekea palealipo kwa kasi sana, Vernad alitulia kuonakitachoendelea.

Punde si punde farasi yulealisimama mbele yake na mtu aliyekuwa kapandajuu yake aliteremka na kuuvuta mkoba wake tokamgongoni, akatoa kibuyu cha maji na kumpaVernad aliyekuwa amekaushwa kwa jua kali lenyehasira.“Asante bwana! Bila shaka wewe ni mtu wa Mungu”Vernad alimshukuru yule mtu.“Ha ha ha ha ha !!!” yule mtu alitoa chekolililomfanya Vernad akumbuke yaliyompata usikuule.“Umejuaje niko hapana nahitaji maji?”“Nimekuona tangu mbali sana, na lengo lako lakusaidia watu wako, Warelvesh. Vernad! NaitwaIsmokum, mimi ni mtu kutoka kuzimu, nilishakufamiaka mingi nyuma na sasa naishi katika hii duniaya chini, mji wa Hamunaptra.” Alikohoa kidogo,huku akishuka kutoka katika farasi wake nakusimama chini katika ardhi yenye mchangamwingi.

Alimsaidia Vernad kunyanyuka na pamojawakasogea pembani palipokuwa na jabali kubwawakakaa hapo.“Sijaelewa! Umesema wewe ni mtu uliekwishakufa?”“Ndiyo, bila shaka, mimi nilishakufa miaka mingiambayo hata babu yako alikuwa hajazaliwa.”“Hamunaptra ni kitu gani?” Vernad aliendelea kwamaswali.“Huo ni mji wanaokaa watu waliokufa zamani, mjiwa wafu, mji uliopotea. Mji ambao sasa upo chiniya ardhi, mji usio na shida wenye kila kitu utakachoisipokuwa mapenzi.” Yule mtu alimjibu Vernad.Vernad alimkazia macho mtu yule mwenyemanywele na mandevu marefu sana, midomomyekundu kama aliyekula nyama mbichi, machoyake ambayo yalikuwa yameangalia kilamojaupande wake, hakika alikuwa marehemu jinsialivyoonekana.“Na hapa nimefikaje?”“Jana usiku ulikuwa ukinifatilia mimi, na nilijuaunachotaka kwangu, sasa usihofu, umepata.

Fuvu laCleopas! Kulipata si kazi ndogo, kwanza Cleopasmwenyewe analitafuta pepo zote nne za dunia”Vernad, alistuka kidogo ‘analitafuta?’“Ndiyo, analitafuta!” yule mtu alimwambia Vernad,ambaye alistuka kwa mara ya pili, ‘kajuaje kamanimejiuliza analitafuta?’. Vernad alijua kuwa, haswakujiingiza katika kutafuta kitu usichokijua ni hatarilakini afanye nini? Kwa ajili ya watu wake. Yule mtualivuta hatua chache mbele na kumpita kwa karibuVernad, alipompita aligeuka kumwangalia, hakuwamtu yule, sura yake ilionekana kama iliyoozaikibubujika mabonge ya damu, meusi, mdomoni,puani na machoni. Vernad alitetemeka kwa woga,hakujua kama akimbie au abakie pale pale.“Ukilipata fuvu hilo ulirudishe kwenye mji waHamunaptra na ulipachike kwenye shingo yaCleopas na hapo Clakos atakupa utakacho.

Ukikaidilitakuteketeza wewe na jamaa yako yote”. Upepo waghafla ulipita kati yao na vumbi la jangwalikawatenganisha, lilipotulia Vernad hakuona mtuwala kitu mbele yake. Sauti zilifikia masikioni, sautiza ajabu zikijirudiarudi ndani yake zikitamka jinaHamunaptra, Hamunaptra, Vernad aligeuka huku nahuku, akisumbuliwa na sauti zile lakini hakuonaaliyeongea wala hakujua zimetoka wapi, alizibamasikio lakini bado aliendelea kuzisikia kwa nguvu sana.1850Sehemu Fulani huko IndiaJua liliwaka kwelikweli, vibarua walifanya kazingumu ya kuvunja mawe na kusogeza hapa na pale,kukusanya vyuma ili kutandika reli mpya kwamanufaa ya koloni la Uingereza.

Askari wa
Kiingereza walisimama kando wakipuliza moshi wakiko na cigar, huku mijeledi ikiwa viunoni mwao,hutakiwi kusema umechoka wala unaumwa, utafanyakazi mpaka pumzi yako iishe. Haikuwa rahisi hata kidogo, mataruma mazitoyalivutiwa hapo na kazi ya kuunganisha njia ya reliiliendelea chini ya engineer wa kiingereza aliyejawana dharau na nyodo kupita kiasi.Ili kupata mawe yanayotakiwa hasa katika kazi hiyoiliwabidi kupasua majabali makubwa na miamba yakutisha, vibarua wengi walipoteza maisha kwakupigwa na mawe hayo yaliyoruka huku na huko.Baada ya kupasua mawe hayo an kuyamaliza sasawalianza kuchimba kuelekea chini. Hakukuwa namashine kama hizi tulizo nazo wao walichimba kwadhana duni lakini zilikuwa bora kwa wakati huo.Prakesh Minto, kibarua aliyeipenda kazi yake aliinuajuu sururu yake na kuitelemsha ili kupiga jiwelililoonekana kujitokeza katika shimo hilo, kablasururu ile haijatua alijikuta ikimtoka mikononi nakuruka pembeni, kisha alisikia sauti zikiongeamaneno yasiyoeleweka. Prakesh alichanganyikiwana kuanza kukimbia hovyo.

Waingereza walewaliokuwa hapo katika kusimamaia shughuli ilewalimuona Prakesh kama aliyeruykwa na akili,walimpiga risasi na kumuua.Kisha wakasogea eneo lile, kijana mwingine alikuwaakichimba lufuata kitu kama ukuta. Walipoona ukutaule hauna dalili ya kufika mwisho ndipo walipoombawataalamu kutoka Uingereza kuja kutoa msaadakatika hili.Baada ya Miezi kadhaa ya kuchimba na kusafishaeneo lile walijikuta mbele ya mji mkubwa, mji wakale ambao kwa wakati huo ulikuwa umesha zamaardhini kwa karne na karne, hata waenyeji walikuwawakiishi hapo miaka hiyo hawakulijua hilo.

Kutazenye nguvu, nguzo kubwa, milango iliyotengenezwakwa mbao ngumu ambazo zilidumu hapo bilakuliwa na nondo.Paul Smith, aliivua kofia yake aina ya pama namkono mmoja alikuwa kajishika kiuno. Mtaalamhuyo wa mambo ya kale, alijivunia sana ugunduziwake, aliendelea kupiga mluzi akiimba moja yanyimbo za kwao. Baada ya kuhakikisha kuwa eneolote liko safi, waliadhimia sasa kuingia ndani ya mjihuu kujionea kilichopo, mioyoni mwao waliaminikuwa sasa utajiri upo jirani. Walijaribu kuvunjamlango lakini hata hawajathubutu mlango ulifungukawenyewe na kiza kinene kiliwa karibisha.∞∞∞Vernad aliitoa mikono yake masikioni, nyuma yakealikuwa amesimama mtu mmoja wa makamoaliyeva kanzu la hariri, kichwani kajiviriga kilembacha rangi ya hudhurungi.

Vernad alimtazama mtuhuyu kwa woga hakujua kama ni yule aliyeondokakwanza au huyu ni mwingine, aliendelea kumtazamahuku kasimama kidete mono wake wa kulia ukiwatayari umeshika mpini wa jambia lake.“Ha! ha! ha! ha! ha! Vernad, karibu sanaHamunaptra. Huku hatutumii silaha kwa kuwa wotetunaoishi hapa ni wafu, huu ni mji wa wafu, wafusiku zote hawafi tena” yule mtu alimaliza kauli yakena kuelekea upande wa maghalibi wa jangwa lile,naye Vernad alimfuata uko huko.“Wewe ni nani?” Vernad alimuuliza mtu yule hukuakimfuata nyuma kwa kukimbia maana mwendoaliyekuwa akitembea haukuwa wa kawaida.“Mimi ni Maghalibi” alimjibu Vernad ambaye sasaalikuwa amesimama akimtazama mtu yuleakitokomea vumbini na kadiri alivyokuwa akiendaaligeuka kuwa vumbi.

Vernad alisikia sauti za watuwakimpita huku na huko lakini hakuweza kuona mtuyoyote, alihisi kama yuko sokoni lakini badohakuona chochote zaidi ya mchanga mwingi uliyojaakatika eneo laote hilo. Kwa namna moja au nyingineVernand alikuwa anahangaika hakujua yuko wapi,anakwenda wapi na anatoka wapi.IIMiezi michache nyuma…“Seidon!” sauti ya kizee iliita“Naam!” Seidon aliitikia huku akikurupuka kutokaalipolala na kumuwahi babu yake ambaye alikuwamzee sana na katika uzee huo daima alipendakukaa na mjukuu wake, Seidon.“Seidon!” yule babu aliita tena, sekunde chache zaukimya zikapita kati yao, “Umeshakuwa kijana sasa!Watu wetu wanaishi kwa shida sana, hatuna maji,hatuna mvua, ardhi imepoteza rutuba kabisa, hii nilaana kwetu.

Inabidi ukatafute fuvu la Cleopas”,Seidon alistuka kidogo aliposikia hilo, babu yakeakampigapiga mgongoni kwa upole “Usiogope, siriya fuvu la Cleopas na baraka za Klakos, ziko na sisiwatu wa Relvelsh, chukua farasi wangu, piga mbiokuelekea Maghalibi mapaka Hamputra, pita kijiakidogo cha kuelekea katika mpaka wa Pakistan naIndia, ingia kwenye mapango ya Dosh na utatokea Mesopotamia, funga safari mpaka kwenyemapiramid ya Misri kwa njia ya chini, nenda kaletefuvu la Cleopas”.Seidon aliangalia chini, hofu kuu ilimjaa moyoniakijaribu kupima ugumu wa safari hiyo na umbaliwa njia lakini hofu ilimuondoka mara tualipokumbuka kuwa farasi wa babu yake alikuwa nambio za ajabu.“Sogea hapa Seidon,” babu yake alimwita Seidon nakuichukua mikono yake na kuipachika mapajanikama ishara ya kula kiapo.“lazima uwe muaminifu, babu wa babu zako Vernadalifanikiwa kulipata fuvu hilo kutoka katika mikonoya Wamisri baada ya kupambana kiume na shujaaOrion, na sasa lipo katika mikono ya Waajemibaada ya kuja na kutunyang’anya apa hapa kwetu,ukiwa njiani usitamani mwanamke wala kulala nae,la, utapata nuksi ambayo kazi niliyokupaitakushinda” Babu yake alimaliza wosia na seidonakatoka na kuketi chini.“Babu nitahakikisha nafanikisha hilo kwa uaminifu.”Alijibu kwa utii.“Chukua upanga wa Vernad hapo juu, na roho yakeikuangazie katika mapito yako.

”KUMEKUCHA ..... KAA NAMI MPAKA MWISHO
 
“lazima uwe muaminifu, babu wa babu zako Vernadalifanikiwa kulipata fuvu hilo kutoka katika mikonoya Wamisri baada ya kupambana kiume na shujaaOrion, na sasa lipo katika mikono ya Waajemibaada ya kuja na kutunyang’anya apa hapa kwetu,ukiwa njiani usitamani mwanamke wala kulala nae,la, utapata nuksi ambayo kazi niliyokupaitakushinda” Babu yake alimaliza wosia na seidonakatoka na kuketi chini.“Babu nitahakikisha nafanikisha hilo kwa uaminifu.”Alijibu kwa utii.“Chukua upanga wa Vernad hapo juu, na roho yakeikuangazie katika mapito yako.”

CHAPISHO LA 03

Jioni hiyo Seidon alichukua farasi wa babu yake,farasi mweupe, na kujifutika upanga wa Vernadkiunoni, kisha kutokomea kuelekea jua linapozama.Safari ilikuwa nyepesi sana mwanzoni, farasi alipigambiyo za kutosha zilizofanya Seidon kuifurahiasafari hiyo, alipita miji mbalimbali, majangwa namapori akiutafuta mji wa Hamputra.

Usiku mnenesana alifika Hamputra, mji mtulivu kila mtu alikuwaamejifungia ndani na kuota ndoto zake. Ni kiumbemmoja tu, Seidon alikuwa nje akipita taratibu katikabarabara ya mawe iliyopita katikati ya mji huo,mwendo mfupi mbele akasimama, akatoa kibegichake na kufungua kishapo akaketi chini ya mti nakula chakula chake taratibu akishushia na maji. Kwambali aliona mtu akielekea upande ule alioketi yeye,alimwangalia kwa makini sana, hakuamini machoyake, akayafikicha, maana aliona labda kasinzia.Msichana mrembo wa sura, mwenye rangi mororoya kuvutia alikaribia eneo lile aliloketi Seidon,mwendo wake wa kunesa ulianza kuusumbua moyowa Seidon, shujaa wa Relvesh ‘njiani usitamanimwanamke wala kulala nae’, kauli hii ya babu yakeilimkosesha raha kila alipoikumbuka.

Aliendelea kumkodolea macho kiumbe yule ambaye sasaalikuwa kasimama umbali wa kurusha jiwe tu,alimtazama kuanzia macho mapaka miguu nakuridhika na uzuri wake, Seidon akajikuta hali yakeinakuwa mbaya, mate ya utu uzima yakamtoka.Msichana yule alimsogelea Seidon na kumshikamkono akamuinua.“Ewe mpiga mbio, mpanda farasi hodari, kwa niniwateseka hapa ilhali nyumba na wenyeji wakukukarimu tupo?! Ondoa kongwa lako, njooupumzike mahali salama” msichana yule alitumialugha laini na nyepesi kumshawishi Seidon kwa hilahiyo.

Seidon alisahau wosia wa babu yake aliinukataratibu na kumfuata msichana yule.Seidon alijikuta katika ukumbi mkubwa wenyeharufu nzuri za kuvutia, udi uliozungushwa kila konaya nyumba hiyo uliijaza kwa moshi, zuria lenyemanyoya safi ya sufu, nakshi za kiajemi, matundaya kila aina yalijaa mezani. Kwa hatua za kujivutaSeidon alitembea juu ya zuria lile akitanguliwa namsichana yule ambaye sasa alikuwa amezifunguanywele zake na urefu wake ulifika kiunoni, akiwaanatembea huku anawasha udi ambao ulikuwa badokuwashwa, alikuwa akiongea maneno kwa lugha yaKiajemi, Seidon hakuelewa chochote katika hayo.“Unaitwa nani?” Seidon alivunja ukimya kwakebaada ya kupaliwa na ule moshi wa udi“Sherhazad binti Sahib” alijibu yule msichana.“Nyumba hii yote unaishi peke yako?”“Ooooh, mpiga mbio, niambie kwanza unaitwanani.” Badala ya kumpa jibu lake; alimgeukia nakumshika mabegani kabla ya kumuuliza swali hilo.“Sei…”“Seidon!” yule msichana alimalizia jina hilo kalaSeidon hajamaliza.

Seidon alijiuliza imekuwa hataakajua jina lake na kulimalizia, “Umejuaje, hataukamalizia jina langu?”“Bwana wangu, Seidon!” Sherhazad alipiga magotina kubusu kiganja cha Seidon, kisha akainua usowake kumwangalia Seidon usoni ambapo Seidon,mono mmoja ukiwa kiunoni na mwingineumeshikwa na Sherhazad, “Nilikuona tangu ukitokaRelvesh kupitia njia ya maghalibi, watu wanguwalikusindikiza kwa sababu tunajua nini unatakiwakufanya.”Seidon, alitafakari kwa sekunde kadhaa,akakumbuka kuwa alivyokuwa akija hakuona mtuyeyote kumfuata. Aliinua uso wake kutoka kwaSherhazad na macho yake moja kwa mojayakaangukia ukutani, picha kubwa ya mtualiyepanda farasi akiwa ameuvuta uta wake kanakwamba analenga mtu au kitu iliupamba ukuta huona kuyavutia macho ya Seidon.“Mimi ni Malkia wa Soria, nilikuwa nakusubiri hapamuda mrefu, nilijua kuwa siku moja utapita tu.Sikiliza, Seidon, nitakupa kila utakacho hata nusu yatawala yangu iwe chini yako ukinitimizia jambomoja tu.”“Jambo gani, Sherhazad?” Seidon aliuliza kwashauku“Nijibu kwanza kama utafanya hivyo naminitakwambia ni jambo gani.”Seidon alitafakari, hakupata jibu ‘majaribu’,alijiwazia, “Naahidi, ee Malkia uliyetukuka kutokaSoria”Sherhazad, Malkia wa Soria alitembea taratibuakimuacha nyuma Seidon, moja kwa mojaakaelekea kunako ile picha kubwa “Huyu anaitwaOrion, muindaji maarufu kutoka Misri, shabaha yakehaina makosa, pigo lake halina huruma.

Daimahuonekana wazi majira ya mwisho wa mwaka, usikuwa giza nene, usio na mawingu. Kamwe huwezikupambana nae, kwa maana wengi hata sasawanasubiri, kwa kuwa wanashindwa kupambananae. Wewe u peke yako, wenzako wapo jeshi lakiniOrion amewadhibiti.Bwana wangu, utakapolipata fuvu la Cleopas, nileteehapa nami nitakutimizia ahadi yangu kwani kwaMuungwana ahadi ni deni”, Sherhazad aligeuka nakumtazama Seidon. Seidon alitikisa kichwa kamaishara ya kutokubaliana na Sherhazad, alikumbukawosia wa babu yake kuwa asitamani wala kulala namwanamke katika safari yake hiyo. Sherhazadalimsogelea Seidon na kumuwekea mikono yakemabegani, sasa walikuwa wakitazamana, Seidonaliangali chini kwa aibu, Sherhazad akamvutiakwake na kukutanisha kifua chake na cha Seidon,Seidon alihisi kitu ambacho hakuwahi kukihisi kablakatika maisha yake, chuchu zilizochongoka zaSherhazad zilizojaa sawa sawa japo zilifunikwa kwanguo ya hariri zilimchoma Seidon hata akaishiwanguvu, alihisi kama ganzi kuanzia kifuani kwakempaka katika nyayo za miguu yake.

Sherhazadalimuweka kichwa chake vizuri na kukutanishamidomo yake na ya Seidon, ulimi wa moto waSherhazad ulipenya kinywani mwa Seidonukazungukazunguka ndani humo na kumpa Seidonladha ya ajabu, alisahau kila kitu, alisahau kama anasafari ngumu inayomkabili mbele yake, alijikutamikono yake ikikikamata kwa nguvu kiunochembamba cha Sherhazad, ikikivuta karibu nachake.“Subiri kidogo, mbona una haraka?” Sherhazad,alimwambia Seidon huku akijitoa katika himayayake, akamuoneshea ishara ya kidole ya kumkataliajambo hilo, huku akirudi nyuma. Seidon alibakikumtazama, midomo yake bado ikiwa wazi kiasi,Punjabi alilovaa lilikuwa limetuna kwa mbele chinikidogo ya kitovu likiashiria shughuli, alivuta hatuachache kumfuata Sherhazad ambaye bado alikuwaakirudi kinyumenyume “Timiza nililokuomba utapatavyote” alimwambia Seidon.“Nitakutimizia, nitakuletea fuvu hilo siku kama hii namuda kama huu” Seidon alimjibu Sherhazad.“Nenda, kakamilishe kazi yako kisha urudi hapa nafuvu, nami nitakutimizia niliyokuahidi hapa hapa”Sherhazad sasa aliongea kwa amri kidogo.

Seidonaliinamisha kichwa kama ishara ya heshima kwamsichana huyu ambaye sasa alikuwa ameketi juu yakiti chake cha enzi, kiti kikubwa kilichowekwanakshi za dhahabu na kufanya urembo mzuri wakihindu na kiajemi.“Sawa Malkia mtukufu wa Soria” Seidon alivaa kofiayake na kuuweka upanga wake vizuri kiunoni, alirudikinyumenyume kama hatua saba na kuinamishakichwa chake tena, akageuka na kuondoka.“Seidon!” Sherhazad aliita, Seidon akasimama nakugeuka mzima mzima“Malkia!” aliitika“Ukikamilisha kazi yako huko Hamunaptra, rudi kwakupitia njia ya kusini na si Mashariki kama ilivyokawaida” Sherhazad alimwambia Seidon hukumkononi akiwa na zabibu kadhaa na kurushiakinywani.Mwaka 2010Chuo Kikuu cha Dar es salaam.Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika kitengo chamambo ya kale (ALCHEOLOGY) walikuwa kwenyelecture, katika ukumbi wa Nkurumah.

Utulivu ulitawala ukumbini humo, mkufunzi professorMasati alikuwa akieleza juu ya chunguzi zilizowahikufanya na mchunguzi maarufu wa Kiingereza BwPaul Smith hasa ile ya Hamunaptra ambayo ilivutamasikio ya watu wengi duniani.Maelezo yake kwa vijana hawa yalikuwa ya kinasana kwa akili yao, yaliwagusa kwa namna moja aunyingine hata wakavutiwa siku moja wafanye studytour huko. Wazo ambalo lilikubaliwa na wengi.Hata lilipofika mezani kwa Pof. Mkandala, halikuwana ubishi, liliandikiwa na kupelekwa wizara husika,siku si nyingi lilipitishwa na mipango ya safari hiyoilianza.***Wanafunzi ishirini na wakufunzi watatu walikuwamokatika msafara ndani ya ndege kubwa ya Egypt Air,kuelekea Misri kisha kuchukua usafiri wa merikebukupitia mto Nile mpaka mji wa Gosheni ambapokwa usafiri wa ngamia wangefika Hamunaptra kwamwendo wa masaa 6 jangwani.Anna Davis, alikuwa miongoni mwa wanafunzi hao,kila wakati alishtukashtuka hasa alipokumbuka kuwawanakoelekea ndiko kunakosemekana kuwa kunamakaburi mengi ya kale yenye miujiza ya kutisha,makaburi ya mafarao wa Misri.

Hata hamu ya kulailimwishia kabisa katika safari hiyo.Baada ya kukaa ndegeni kama masaa matano hivi,sauti nyororo ya msichana iliyoongea kwa lugha yakiingereza na kiarabu iliwaashiria kuwa sasawanapita juu ya anga ambalo chini yake kunamapiramidi makubwa, mji wa Giza, ambayo dunianikote yanapatikana hapo tu na kuwa historia ya nchiya Misri ilikuwa hapo katika mapiramidi hayo.Anna aliangalia kwa makini majumba yale makubwayaliyojengwa miaka na miaka yakiwa yamejipangakatika safu za kupendeza.Punde si punde walikuwa katika ardhi ya HosniMubaraka, ardhi ya Misri, jiji la Cairo, jualiliwachoma kweli kweli lakini uvumilivu ulishikahatamu. Hamu ya kufika kujionea Hamunaptrailikuwa imezidi mioyoni mwa vijana hawa,walionekana kuchangamka sana.

Siku hiyowalipumzika Cairo na kesho yake walianza safarikuelekea mji wa Giza kupitia mto Nile.“Hapa si Hamunaptra, lakini hamuwezi kuielewahistoria ya Hamunaptra bila kupita hapa Giza” sautiya kitetemeshi ya mmoja wa wazee waliokuwawakifanya kazi ya kuongoza na kutembeza wataliikatika hayo mapyiramid, alisafisha koo kidogo kwakujikooza na kuendelea “Na lazima mjue kwambaHamunaptra ni mji uliopotea miaka mingi iliyopita,ni mji wenye historia kubwa sana duniani, mji huukiuhalisia upo India na si Misri, ila hapa Giza, kunapiramidi kubwa sana ambalo ndani yake, chinikabisa kuna pango kubwa sana, ukipita ndani yakeutatokea Mesopotamia halafu linaendelea kutokeaIndia katika eneo ambalo huo mji ulikuwaumefukiwa na mchaga kwa miaka mingi sana.”Walivuta hatua chache kidogo na kuanza kuyaonakwa karibu na hata kuyashika kwa mikono yao hukuwakiuliza maswali mengi.HamunaptraHamunaptra (Mji wa wafu), uligundulika huko Indiamnamo mwaka 1850, wakati mainjiania wakiingereza walipokuwa katika kujenga njia ya relindipo walipougundua. Mwaka wa 1920 ndipowataalamu walipofanya kazi ngumu ya uchunguzi,chini ya ardhi walikuta mji mkubwa sana na wenyemambo mengi, ilisemekana kuwa kulikuwa viumbewalioishi huko miaka ya 1900-1700 kabla ya Kristu.

Mji uliotulia ardhini, ulijulikana hivyo kwa kuwaulionekana huko, wachunguzi wengi waliojaribukupita pango hilo walipoteza maisha, wengine kuwavipofu na wengine walipatwa na hali za ajabu ajabu.Lakini ilisemekana kuwa miaka hii maajabu hayohayakuwapo tena hivyo wengi waliingia ndani humona kujionea yaliyokuwamo.Karne kadhaa nyuma…Wachawi kutoka Misri waliingia ndani ya piramidihilo kubwa, lengo lao lilikuwa ni kwenda kuchukuafuvu la Cleopas. Walishuka mpaka chini kabisa yapiramidi hilo mpaka kwenye mdomo wa pangokubwa lililopo huko. Huku wakifanya matambikokwa lugha zao za kichawi, walipita katika pango hilona katikati yake wakaingia sehemu Fulani na kukutachumba cha wastani kilichonakshiwa kwa maandishiya kimisri na kihindu, michoro mbalimbaliilizunguka kuta zake zote. Walisimama bilakutikisika na kutazama mbele kabisa ya chumbahicho cha chini.

Mbele hapo kulikuwa na kitu kamajukwaa lenye ngazi ngazi na juu yake kulikuwa naskeleton ya kiumbe Fulani aliyekaa kwa kukunjamiguu yake, pembeni kulikuwa na skeletoni zinginenne lakini zilikuwa na maumbo madogo kuliko ileya katikati, zilionekana kuwa zimemuinamia kamaishara ya heshima kwake.

Lakini ile skeleton kubwahaikuwa na kichwa! Cleopas.“Wamechukua…” kiongozi wa wale wachawialiwaeleza wenzake kwa lugha yao ya kichawi.Wengine walibaki midomo wazi. Walipanga kuingiakuchukua kichwa cha Cleopas ili kufanikishiamambo yao ya kichawi lakini hawakulikuta,walijiuliza nani mwenye nguvu za kulichukuwa fuvuhilo, hawakupata jibu kwa kuwa wao walijiona kuwandiyo wachawi bora duniani. Walibaki wameduwaa,hata wao walishangaa siku hiyo wakiingia kiulainisana tofauti na karne za nyuma, walishawahi kufanyajaribio hilo mara kadhaa kizazi hata kizazi lakinihawakufanikiwa kufika hapo.

DUNIA YA KALE INAKUTANA NA DUNIA YA SASANINI KITAENDELEA?
 
“Wamechukua…” kiongozi wa wale wachawialiwaeleza wenzake kwa lugha yao ya kichawi.Wengine walibaki midomo wazi. Walipanga kuingiakuchukua kichwa cha Cleopas ili kufanikishiamambo yao ya kichawi lakini hawakulikuta,walijiuliza nani mwenye nguvu za kulichukuwa fuvuhilo, hawakupata jibu kwa kuwa wao walijiona kuwandiyo wachawi bora duniani. Walibaki wameduwaa,hata wao walishangaa siku hiyo wakiingia kiulainisana tofauti na karne za nyuma, walishawahi kufanyajaribio hilo mara kadhaa kizazi hata kizazi lakinihawakufanikiwa kufika hapo.

CHAPISHO LA 04


Siku chache baadae …Wachawi na waganguzi wote wa Misri walikutanakwenye vikao vyao lengo ni kutaka kujua nanikachukua fuvu lile. Baada ya kikao kirefu, nakutumia mbinu zote za kichawi waligundua kuwafuvu lile limechukuliwa na Waingereza miaka minginyuma.“Haiwezekani!” Kiongozi wao alisema“Watu wa Maghalibi hawawezi kutuzidi maarifa”mwingine aliongeza“Haina haja kulumbana, tuangalie tunafanya ninikurejesha fuvu lile mahali pake”Baada ya majadiliano marefu walifikia muafaka wajinsi gani ya kurejesha fuvu lile.

Walikubalianakumtafuta muindaji maarufu wa Misri Orion, ambayealikuwa ni shujaa katika mambo mengi, mpigashabaha maarufu duniani mpaka sasa. Baada yamapigano makali huko kusini mwa Londonalifanikiwa kulipata fuvu hilo akisaidiwa na uchawiwa Kimisri. Alipolirejesha fuvu hilo liliwekwa ndaniya piramidi kubwa kabisa huko katika mji wa Giza.Watu wa makabila ya kiajemi waliijua habari hiyo,hapo ndipo ilipoanza vurugu ya kila kundi kufanyambinu ya kulipata fuvu hilo. Tatizo lililowakabili niubinafsi, kila mmoja alitaka alipate ili ajinufaisheyeye na watu wake.

Lakini Klakos ilitaka fuvu lilelilirejeshwe kwa Cleopas na huyo atakayelirejeshandiye atakayepata neema za Klakos, yeye na watuwake.Kazi haikuwa ndogo kwani Orion alidhibiti pandezote nne za dunia watu wasiweze kulipata fuvu hilo,kila aliyejaribu alitoka kapa.Vernad alipokutana na Orion, haikuwa kazi ndogokwake kufanikiwa kulipata fuvu hilo, mapiganoyaliyoandamwa na nguvu za nyingi yalitawala katikamji wa chini ya ardhi. Si kwamba Orion alishindabali alizidiwa maarifa na Vernad wa Relvesh.Wahamsud walifuatilia mapigano hayo toka mbali,wakitaraji kwa kwa vyovyote lazima mmojaashindwe, hawakuamini waliposhuhudia Vernadakimshinda ujanja Orion na kutoroka na fuvu hilo.Relvesh ilijawa na furaha sana kwa kumpokeashujaa wao huyo akiwa na mkoba mweusi mkononiuliowekwa fuvu hilo la ajabu, walilihifadhi vizuri,wakiwa na nia njema tu ya kulitumia kwa manufaayao.

Lakini hawakujua kuwa pembeni yao kunawanaowaangalia kwa jicho la husuda.Ndipo walipojikuta usiku mmoja wamevamiwa nawapiganaji walio juu ya farasi, wenye mijeledi namajambia, kijiji kizima walipigwa na wenginekuchomwa moto, ilikuwa hali ya kutisha sana.Waajemi walifanikiwa kulichukuwa fuvu lile nakutokomea nalo.Warelvesh waliapa kulirejesha fuvu hilo mikononimwao wakati Wahamsud walilimezea mate, achanana Sherhazad ambaye yeye kama mwanamkeasingeweza kulishika fuvu hilo. Tukio likawahistoria, watu wakafa na wengine wakazaliwa,historia ikawa ni simulizi ya kuvutia, simulizi ikawariwaya tamu unayoisoma sasa.Rejea …

SasaUpepo si upepo wala si mvumo wake, mara kwamara Anna Davis alikuwa akisikia kitu hikokikimsumbua, aligeukageuka mara kushoto na marakulia, mara alizunguka kama pia, ilikuwa ngumukwake kufuatia maelekezo yatolewayo na mtaalamuhuyo.“We una nini? Mbona hutulii?” mwenzake alimuuliza“Hata sijui mwenzangu, naona kama vitu vinanipitahapa mara vinanizungukazunguka. Yaani mwili woteunanisisimka”“Acha uoga wewe, mbona wenzako hatuvioni!”alijibiwa na mwanafunzi mwenzake, kisha wotewakaendelea kusikiliza maelekezo.

Kitu kama nyoka kilipita katikati ya wanafunzi walena Anna lakini cha kushangaza wenzakehawakukiona ila yeye alishuhudia mchanga ukitimkambele yake na mara nyuma yake, sauti kama mruzimkali ulipenya masikio yake na kumfanya apigekelele. Muelezaji alinyamaza kwanza nakumwangalia Anna, ilionekana wazi hakufurahishwana kitendo cha Anna.“Msichana! Hutakiwi kupiga kelele ukiwa humundani, utaamsha waliolala” yule mzee alimkaziamacho Anna na kumueleza hayo.Macho ya Anna hayakuwa matulivu hata kidogo, kilaalipoangalia michoro ya watu iliyochorwa katika kutazile au wanyama yeye aliona kama zikimwambiakitu Fulani, aliona kama ni viumbe hai. Hali hiiilimfanya aogope sana, muda wote hakuwa naamani kabisa.

Alitembea kwa hadhari kubwa hukuakigeukageuka nyuma, maana alihisi kama kuna vituvinamfuata na alipogeuka vilitulia. Katika moja yakugeukageuka ndipo alipojigonga kwenye kigingikikubwa cha jiwe, alianguka chali na kukosa pakujishikia, bahati mbaya au nzuri mikono yakeiligonga tofali mojawapo lililoshikia ukuta ule imara,mara juu yake aliona kukifunguka na kitu kamasanduku likianguka kuelekea alipo yeye, Annaalipiga kelele huku akiwa kafumba macho, hana lakujitetea.

Wanafunzi wenzake walishtushwa kwa kelele zamwenzao walipogeuka nyuma walishuhudia vumbizito likitimka na kuweka kama ukuta kati yao naAnna, kwa mbali walianza kusikia kama watuwanaoswali, sauti nyinginyingi zilisikika humo ndaniya piramidi“Tuondokeni haraka! Tutoke nje, nifuataeni mimi”yule mzee aliongea kwa kelele, wanafunzi walewalianza kukimbia kumfuata.

Kipenzi cha Anna,alishindwa kumuacha shoga yake, alisimama nakugeuka nyuma huku akiwa amejishika mkonokujiziba mdomo.“Annaaaaaa!!!!!” aliita kwa nguvu na kelele ileililijaza piramidi lote, kabla hajatahamaki jiwe kubwalilianguka na kumponda kichwani, alianguka nakuumia vibaya, hakuweza kujinasua kwani tofali lileni kama kilo mia mbili, alipoteza maisha.“Msisimame, twendeni!” yule mzee alizidi kuwahasaviajana wale ambao sasa walikuwa wakikimbia nakupoteana wengine wakitamani kubaki kuwasaidiawenzao.

Piramidi lote lilianza kutikisika na kutazake kuanza kuchezacheza kwa mtindo ule ule,vumbi likazidi kujaa ndani mle kiasi kwamba ilikuwangumu kuona njia hasa zile za kupanda juu.Wanafunzi wale walipata shida kujiokoa lakini kwamaelekezo ya yule mzee walifanikiwa kutoka nje nakuliona jua waliloliaca likichomoza sasa lipokatyikati ya utosi.“Nyie, yule mwenzenu ana matatizo gani?” yulemzee aliongea kwa ukali“Matatizo kivipi?” kiongozi wa msafara alijibu kwakuuliza.“Hii hali yote kaisababisha yeye, unapoingia mlendani hutakiwi kugusagusa vitu”Vilio vilitawala kati ya wanafunzi waliobakiwakiwaomboleza wenzao waliosadikiwa kufashimoni, hali ilikuwa tete.***Amata ga Imba, akiwa amelewa sana na pombeyake nyingine mkononi alisimama ghafla, akashukakutoka katika farasi wake na kutua chini taratibu,aliliweka guo lake vizuri mwilini na kurudishia pamalake kichwani.

Alifikicha macho yake kutazamakilichopo mbele yake; ‘huyu mtu au kitu gani?’,alijiuliza huku akijongea kwa hatua za taratibumpaka pale, alichuchumaa na kuinua kichwa chamajeruhi yule taratibu, akaweka mkono wake kifuanikwa mtu yule, akagundua kuwa bado uhai upo kwambali sana, mtu yule hakuwa na fahamu. Akamnyanyua na kumlaza juu ya farasi wake, kwapembeni alimuona farasi mweupe aliyelala nyasini,akampigia mruzi na farasi yule akainuka kutokapale, kisha akaondoka na mtu yule pamoja na farasiwake mpaka katika kijiji alichokuwa akiishi.Siku zote alikuwa akimpa tiba mtu huyu asiyemjuakwa muda wa takribani wiki moja mtu yule aliamkakutoka katika usingizi mzito, alikuwa akihema kwanguvu na haraka haraka“Likowapi, likowapi? Nipe, nipe haraka” Seidonaliamka na kupiga kelele za maweweseko.

Amata alimtuliza na kumlaza taratibu pale katika tandikolake.“Tulia, tulia, usijitikise sana” Amata alimbembelezaSeidon ambaye alitii na kujilaza tandikoni.“Hapa nipo wapi?” aliuliza“Hapa ni kijiji cha Mshariki, kijiji cha wema kisichona wabaya” Amata alimjibu Seidon kwa upole,akamtazama usoni na kuendelea “naitwa Amata gaImba, nilikukuta porini karibu na jangwa la Shebanikakubeba na kukuleta huku” akajikohoza kidogokuweka koo lake vyema “pole sana! Hakikaungekufa lakini Mungu mkubwa nilikuwhi. Wewe ninani?”“Mimi ni Seidon kutoka Relvesh, nilikuwa safarininikitokea Hamunaptra kupitia Mesopotamia,Wakalban walikuwa wakinikimbiza wakiwa kundi, walitaka nilichonacho, lakini nikiwa katika kasikubwa niliona kitu kama kamba mbele yanguambayo ilimnasa farasi wangu miguuni na mikuanguka vibaya.

Wahamsud walinifanyia hivyo nakuchuku fuvu la Cleopas wakatokomea nalo” Seidonalitokwa machozi na kamasi jembamba akendelea“Babu wa babu zangu Vernad alikuwa na mpangowa kulipata fuvu hilo kwa ajili ya kusaidia kijiji chetucha Relvesh dhidi ya laana tulizonazo...Rejea Vernad…Vernad alitembea taratibu mpaka kwenye kilimakidogo, na alipofika juu yake alitazama chini nakuona mji mkongwe, gofu la mkji uliofunikwa kwamchanga upande wa juu. Bia kuchelewa alitimuambio kulielekea gofu lile, punde tu alikuwa mbeleya mlango mkubwa, bila kusita aliingia ndani,hakupiga hata hatua tano alijihisi kakabwa kwanyuma, alihangaika kujinasua lakini ilikuwa vigumu,aliishika mikono ya kiumbe huyo sawia na kuinamahata kumdondosha kiumbe yule kwa mbele, kitendobila kuchelewa aliuchomoa upanga wake na nakumshindilia kifuani, kiumbe yule alitoa sauti yamaumivu kama sauti ya nguruwe lakini hakutokadamu, Vernad aliuchomoa upanga wake na kumkatavipande vipande kisha akaingia mlango wa pili nakuchukua ngazi kuelekea chini ya gofu hilo, alijikutakwenye ujia mrefu uendao asikokujua, kwa kasi yaajabu alikimbia kuelekea ujia ule uendako akiwa naupanga wake mkononi.

Njiani alikutana mtu mmoja mbele yake ambayealikuwa kafunga njia, Vernad bila kupunguzamwendo alijirusha na miguu yake kutangulia kifuanikwa mtu yule huku upanga ukifuata na kudidimiakatika koromeo la mtu yule ambaye hakupata hatanukta ya kujitetea. Vernad alitua chini na kuuchomoaupanga wake, kabla hajaanza kuondo alipigwangwala moja na kujibwaga chini, wakatianapoanguka alijishika kwenye tofali moja wapolililotokeza katika ukuta huo mara ardhi ikainamanana kufunguka Vernad alitumbukia katika shimo refu, alishuhudia radi kali zilizopiga huku na huku shimonimle. Huku akiwa kajiziba masikio kutokana naupepo mkali uliyoyasumbua, upanga wake ukiwahaupo mikononi mwake, alijikuta akitua chinitaratibu bila maumivu yoyote, alisimama wima nakushangaa eneo lile pana, uwanda mkubwa usiomawaa yoyote. Alijiuliza yuko wapi hakupata jibu,mbele yake aliona majengo mengi sana na watuwakiwa katika kazi nyingi, kazi mbalimbali.

Aliinuamguu kuwafuata watu wale lakini nyuma yake alihisikama anafuatwa alisimama na kugeuka, lo! Umatiwa watu ulikuwa nyuma yake, alijaribu kuwahesabuharakaharaka lakini alishindwa kwa uwingi wao.Watu wengi walionyamaza kimya hakunaaliyetikisika walimtolea macho Vernad mpakaakaogopa, aliporudi nyuma walimfuata alipojaribukuwasemesha sauti haikutoka, walibaki kumtoleamacho tu, watu waliovaa nguo kuukuuzinazoonekana kuoza, macho mekundu kwa meusi,wengine walikuwa na mkono mmoja wenginewalikuwa hawana masikio ilimradi waliogopesha,wafu, lakini mikononi mwao walikuwa na visu,mapanga, miundu na kadhalika.

Vernad alijuwa wazikuwa hapo hakuna msalie mtume, alianza kutimuambio na watu wale wakaanza kumfuata, Vernadaliwaacha mbali kwa mbio zake lakini hakujua niwapi anakoelekea, alipokuwa akiyapita yalemajengo watu wengine walitoka katika yalemajengo na kuanza kumfukuza, Vernad hakuchoka,aliongeza mwendo lakini ghafla alihisi kambaikimfunga shingoni na kuanguka chini, haraka bilakuchelewa alijiinua na alipojaribu kuitoa kamba ileshingoni hakuweza kwani ilimfunga barabara, alihisimiale ya jua ikimchoma machoni kwa kubadilishanaalijikinga kwa mkono wake wa kulia na kujaribukuangalia, aliona kama kiumbe Fulani pale katikatiya mionzi ile.

Mara miale ile ilianza kupunguanguvu,Vernad alishusha mkono wake na kumuona mtualiyevalia joo jeupe, kiunoni akiwa na upangamkubwa, mkono wake wa kushoto kashika ngao nakulia ana kamba ambayo ndiyo hiyo upande wa piliimemfunga Vernad, mgongoni alikuwa na utamkubwa na podo lililojaa mishale.‘Orion’ Vernad alijiwazia, akasimama kwa miguuyake na kuinamisha kichwa kutoa heshima kwakiumbe huyo, aliponamisha kichwa Orion aliufutaupanga wake na kukata shingo ya Vernad. Vernadhakuwa na kichwa tena, alibaki kiwiliwili tu,alianguka chini na roho yake ikauacha mwili.seidon…Hakufanikiwa kwa sababu Orion alimdhibiti nakumuua.

Sasa mimi nilitumwa kuikamilisha kazihiyo iliyoahirishwa vizazi na vizazi” Seidon alimalizakumuelezea kisa hicho Amata ambaye alibakimdomo wazi maana alijaribu kufikiri hatarialiyoikabili Vernad na sasa Seidon.“Wewe umemshinda vipi Orion?” Amata alimuulizaSeidon“Amata! Ni simulizi ndefu sana…” akashusha pumzindefu na kuendelea “Mimi nimepambana na Orionuso kwa uso, sikumshinda kwani yule ni kiumbemwenye akili hata upiganaji wake hauna makosashida yake niliisoma ni moja tu, si mjanja na walasi mwepesi, nilifanikiwa kulipata fuvu alipolificha nahapo ndipo kazi ngumu ilikuwa, Amata!.

Sherhazad alimwangalia Seidon akipotea na farasiwake kwa kasi, akiwa pale katika dirisha lake laajabu alitabasamu na kutikisa kichwa ‘wanaumewajinga sana! Ukilala nao kitandani tu watakupa kilakitu, ngoja alete hilo fuvu hakika kaburi lakelitakuwa hapa hapa Soria’ alijisemea moyoni hukuakitoka katika dirisha lake ambalo kwalo huwezakuona mambo yote yanayoendelea duniani nakusoma mawazo ya kila mtu anayemtaka.HILA ZA SHERHAZAD ZITAFANIKIWA?
 
Sherhazad alimwangalia Seidon akipotea na farasiwake kwa kasi, akiwa pale katika dirisha lake laajabu alitabasamu na kutikisa kichwa ‘wanaumewajinga sana! Ukilala nao kitandani tu watakupa kilakitu, ngoja alete hilo fuvu hakika kaburi lakelitakuwa hapa hapa Soria’ alijisemea moyoni hukuakitoka katika dirisha lake ambalo kwalo huwezakuona mambo yote yanayoendelea duniani nakusoma mawazo ya kila mtu anayemtaka.

CHAPISHO LA 05

Seidoni alipiga mbio bila kuchoka na farasi wakealitii yote aliyoambiwa na bwana wake, punde sipunde alijikuta mbele ya jingo la ajabu, jingo kubwalililoonesha kila dalili ya kutoishi mtu, alijitomandani akiwa na farasi wake huyo, ndani humo alipitakwenye njia ndefu iliyokuwa haionekeni mwishowake, kwa kasi ileile alipita na farsi wake, akiwakatika kukimbia huko akasikia farasi mwinginenyuma yake akipiga kelele alipogeuka alionaakifuatwa kwa kasi na mtu aliyekuwa juu ya farasialiyeoneaka si muda angemfikia.

Seidon aliongezakasi lakini bado alijikuta umbali uleule na farasiyule wa nyuma. Hakuwa na jinsi kwa maanaaligundua kuwa huyu wa nyuma yake angewezakumdhuru muda wowote ukizingatia alikuwa karibusana na yeye, alimkwepesha farasi wake upande nakusimama, yule wa nyuma alipitiliza na tayariupanga wa Seidon ulishapita katika ubavu wa mtuhuyo, kwa kishindo alianguka chini, Seidonaliteremka na kumfuata pale alipo, damu ilikuwaikitoka mdomoni, Seidon akapiga goti moja nakumtazama“Wewe ni nani?” alimuuliza“Mimi kiumbe wa Mashariki ya mbali” alijibu kwataabu“Kwa nini unanifuata?”“Pepo zimenituma nikufuate nihakikishe hufikiuendako, na ukifika usifanikiwe lengo lako, naukifanikiwe usitoke humu na ukitoka usifike mwishowa safari yako…” kabla hajamaliza kuongeaalikoroma na kukata roho. Seidon alipanda farasiwake na kuanza safari yake kwa mbio zilezile, lakinikamba iliyorushwa kwa ustadi iliifunga shingo yaSeidon na kuanguka vibaya, vumbi lilitimka mahalipale na lilipotulia hakukuwa na mtu zaidi ya farasimweupe wa Seidon.

Orion alisimama kuangakli huku na huku hakumuonaSeidon, kazidiwa ujanja. Aliiangalia kamba yakeambayo sasa ilionekana imemfunga farasi waSeidon na sio Seidon mwenyewe. Orion aliterekakutoka katika farasi yule na kutua chini, kishindocvhake cha kutua chini kiliwafanya popo kutimka naardhi kutikisika kwa muda, kwa hatua fupi fupialimuwendea farasi wa Seidon na kumuangalia kwamakini. Orion ambaye daima sura yake haionekanikwa kuwa alikuwa akiifuanika kwa kinyago maalumhuwa hashuki kwenye farasi, yeye hupigana akiwajuu ya farasi wake, lakini akikuona wewe ni mjanjazaidi yake hapo ndipo atashuka ili akukabili vizuri.

Alimtazama yule farasi lakini hakuelewakilichotokea, aliichukua kamba yake na kupandafarasi wake kisha kuondoka kuelekea uelekeo uleule aliokuwa akielekea Seidon.Seidon aliliachia jiwe alilokuwa amelidandia juu yapango lile na kutua chini bila kufanya kishindo,‘amenikosa’, alijiwazia kisha akapanda farasi wakena kuelekea kulekule alikoelekea Orion, baada yamwendo wa kama dakika kumi katika pango lilealijikuta anafika njia panda, nji tatu zilikutana hapo,Seidon alifikiri ni ipi hasa anayopaswa kupita,kwenye njia moja alisikia mvumo wa maji kamamto upitao kasi lakini hakuyaona maji yenyewe, njiaya pili ambayo ilikuwa katikati alisikia mvumo wamoto uwakao mithili ya moto uchomao msitu nanjia ya tatu alisikia kama watu wakinoa mapanga.

Seidon alitulia kimya akitafakari la kufanya, aligeukana farasi wake tayari kwa kurudi akijua kuwa labdakuna njia nyingine lakini sivyo, alipogeuka alikutanana ukuta, hakuiona njia aliyojia, alitafakari na kuonakuwa hana ujanja zaidi ya kuchagua moja,alimgeuza tena farasi katika uelekeo wa kuendeleana safari na moja kwa moja moyo wake ulimtumakupita njia ya moto, hakuwa na muda wa kufikirialijitoma ndani ya ujia huo na kuendelea kupigambio, kadiri alivyouwa akienda alihisi sauti ile yamoto ikizidi kuwa karibu zaidi,kila alipotakakupunguza mwendo alisikia sauti ikimwambiaaendelee kwa kasi.

Seidon aligundua kuwa amepata kampan alipoonakuna farasi wawili na juu yake Malaika wa motowenye upanga makali kuwili wakiwa katika kasiileile, mmoja kushoto na mwingine kulia, Seidonalishindwa kujua afanyeje, akiongeza kasi naowalifanya vivyohivyo, mbele yake alishuhudia motomkubwa sana ambao ulimtisha nafsi yake, afanyenini. Aliamua, kama kufa wacha afe kwani tayari alikuwa kwenye mikono ya mauti, kwa mkono wakewa kulia aliufuta upanga wake na kwa pigo mojaalimchoma yule Malaika wa moto wa upande wakushoto lakini hakuhisi kama kachoma kitualipogeuka kwa yule wa upande wa kulia alikutanauso kwa uso na joka kubwa lililoachama kinywachake, Seidon bila kuogopa wala kufikiri alipigapigo moja kwa upanga wake na kulichoma joka lile,alipouvuta upanga kuuchomoa alihisi kama damuikimrukia usoni alichelewa kujikinga, alijikutaakipoteza uelekeo na kuanguka vibaya, alijiinuaharaka na kusimama kidete, joka lile lilitema ndimiza moto, Seidon alijitupa chini na kujiviringakuelekea kuelekea kule joka lile lilipo, alifanya pigola upanga na kulikata joka lile kipande, kishaaliposimama alijikuta akipaishwa juu kwa ngwalamaridadi iliyopigwa kwa mkia wa joka lile,alijigonga vibaya na lianguka kama mzigo, alijtahidikunyayuka lakini alipoangalia alijikuta chini yaupanga wa moto, Malaika wa moto alisimama juuyake akiwa kamnyoshea upanga.

Seidon alitulia tuli, akijua sasa siku yake imefika,Malaika yule aliushusha upanga wake kwa kasi kwania ya kumkata Seidon, lakini kwa ustadi Seidonalipangua pigo lile kwa upanga wake na kumfanyaMalaika yule apoteze shabaha ile, Seidonalinyanyuka kwa mtindo wa sarakasi na kusimamawima ardhini, alirusha teke kwa kujizungusha nakumtandika Malaika yule kichwani na kumfanyakuyumba kiasi lakini akajiweka sawa na kujibushambulizi, aliuvuta upanga wake na kufanya pigolingine ambalo almanusura liondoe kichwa chaSeidon endapo Seidon asingeinama.

Seidon sasaalikuwa akitazamana na sehemu ya tumbo yaMalaika yule, bila kuchelewa aliuzungusha upangawake na kukata tumbo hilo lakini alichokishuhudiani kurushwa kwa nguvu na kutumbukia katika motomkubwa uliokuwa ukizidi kusogea eneo hilo.***Anna Davis alitazama huku na huku, aliona sandukukubwa kushoto kwake lililomkosakosa kumbondana kumfanya aanguke tu kwa kishindo kile. Akiwaanatweta kwa nguvu alishindwa kujua ni nini hasaanatakiwa kufanya, alipotaka kupiga kelele zamsaada alijikuta hana sauti ya kufanya hivyo,alipojiinua pale chini aligundua kuwa hakuwa pekeyake bali pembeani yake kulikuwa na miiliiliyokauka yaani iliyokufa miaka mingi nyuma, Annaaliogopa sana akaanza kutetemeka, taratibu aliinukaili asisikiwe na miili hiyo.

Alipoketi vizuri alitazamawapi pa kuelekea aliona ngazi ndefu zikishuka chinina pale alipo palikuwa na uwanda mkubwa kiasiuliozungukwa na kuta nene zenye michorombalimbali.Sauti za watu wakisali katika lugha isiyoelewekazilisikika, Anna alitazama vyema na kuona viumbekama watu wapatao kama ishirini hivi wakiwawamezunguka kitu kama kitanda na katikati yakekulikuwa kumelazwa mwili wa binadamu ambaoAnna aliutambua vyema, mwili wa rafiki yake kipeziNesta.

Anna alibaki kakodoa macho akiangaliatukio lile lilivyoendelea kule chini, wale viumbewalipiga magoti wakisali na mmoja aliyeonekanakama kiongozi wao alisimama upande wa miguu waule mwili akiwa na kisu kikubwa mkononi mwake,alikuwa akimwagia unga Fulani juu ya mwili ulekuanzia miguuni kuelekea kichwani huku akisemamaneno kwa kurudiarudia na alipofika kichwanialijaza unga ule usoni mwa mwili ule na kukiinuakisu chake tayari kwa kukata shingo.

Anna alipiga kelele za nguvu mara kuta zote zilianzakutikisika, na wale viumbe walionekana kukatishaibada yao, walisimama na kutawanyikawakipandisha ngazi kuelekea juu alipokuwapo Anna,Anna alipogeuka akimbie alitandikwa kofi moja languvu lililompepesua na kumuangusha chini kwaharaka alinyanyuka na kusimama wima, mbele yakekulikuwa na ukuta na katika ukuta huo kulichorwapicha ya skeleton ya binadamu, hakujua ni nanialiyemchapa kofi lile, aliendelea kushangaa na hapondipo alipoushuhudia mchoro ule ukipata uhai,ukajitikisa na kujibandua pale kwenye ukuta nakukanyaga chini, kwa mwendo wa kustaajabishaulianza kutembea kumuelekea Anna pale alipo.

Hamna la kufanya Anna kwa kujihami aliuchomoamwenge uliokuwa umepachikwa katika moja ya kutazilizopo hapo na kumtishia kiumbe huyoaliyeonekana kusimama kwa kuogopa. Anna alisikiavishindo vya wale viumbe wengine wakipanda ngazizile kwa kasi akaona sasa hapo si pa kukaa tenalakini hakujua ni wapi hasa aelekee. Alitazama hukuna huku akaona viumbe wale wanazidi kukaribiapale alipo, alijaribu kukimbia, lakini alipogeuka tualipigwa kofi lingine la kisogoni lililomfanya ayumbena kujigonga katika ukuta, aligeuka na kukabilianana skeletoni ile ambayo ilikuwa ikitembea kuelekeaalipo msichana huyu, Anna hakuwa na silaha zaidiya mwenge ule uwakao aliurusha kumtupia kiumbeyule ambaye kabla hata hajafikiwa na moto ulealijizungusha na kugeuka mchanga uliotimka nakufanya vumbi jingi ndani mle. Anna aligeukakukimbia lakini mbele yake wale viumbe waliotokakule ibadani walikwishamfikia, walimzunguka.

Kutokana na urefu wa Anna aliweza kuwaona vizurijinsi walivyo wafupi wenye macho ya kutisha namidomo iliyokuwa ikimwagika udenda mweusimzito kila mara, Anna alichota mchanga nakuwamwagia kitendo kilichowafanya watawanyike,Anna aliokota tena ule mwenge uwakao na kuanzakukabiliana nao, aliushika kwa mikono miwili nakuuzungusha kwa kasi kitendo kilichofanyakuwapiga viumbe kama watatu kwa mfululizo nakuviangusha chini lakini bado vilikuwa vikija tena,alifanya tena kama mwanzo na kushuhudiakimojawapo kikilipuka kwa moto ule na kinginekikadaka mlipuko ule, Anna hakuona haja yakuchelewa alipita katikati yao na kutimua mbio, bilakugeuka nyuma akiwa katika kasi hiyo mara mbeleyake aliona ardhi ikifunguka na kwa kuwa alikuwaakikimbia alishindwa kusimama ghafla, alijaribulakini alishindwa alijikuta akimezwa na shimo lile,akitumbukia ndani ya shimo hilo ambalo kwalohakuona mwisho wake.Alijibwaga kwenye lindi la mchanga, mahaliasipopajua, aliketi akiegemea ukuta mkubwa nyumayake, miguu yake aliikutanisha na tumbo lake nakujikunyata akitweta bila kujua la kufanya.

***Seidon alidondoka katika mandhari tulivu, udongolaini ulifanya vumbi sawa na la saruji lililomfanyaseidon kupiga chafya kadhaa, alitazama huku nakule na taratibu kuvuta hatua, mbele yake kulikuwana mlango mkubwa na ndani yake aliona mwangamkubwa uliojaza chumba hicho, Seidon kwamwendo wa tahadhari alinyata na alipoukaribiamlango ule alisikia mlio wa kwato za farasi ukijaupande wake alipogeuka alikutana na kamba neneinayoikaribia shingo yake aliinama na kamba hiyoikamkosa, alipojiinua aliiona ncha ya mkukiikimlenga kifuani akaepa, na mkuki uleukajichomeka mchangani. Orion alikuwa amefikaeneo hilo, Seidon akauwahi mkuki ule lakini kablahajaushika aliona ukiwaka moto, akaamua kuuacha,kabla hajageuka alijikuta akikanyagwa na miguu yambele ya farasi wa Orion ambaye alikuwaamejinyanyua na kusimama kwa miguu miwili.Seidon alidondoka mchangani na kutambaa kamamtoto, alitulia kidogo ili kumvuta Orion, Orionalisogea pale akiwa juu ya farasi wake,alimwangalia Seidon akiwa pale chini, Seidon alituliakimya.

Mara ghafla aligeuka na na kusimama bilakuchelewa aliuvuta upanga wa Orion kutoka kiunonimwake na kuuzungusha kwa ustadi kitendokilichosababisha farasi wa Orion kukatika miguu yambele kwa makali ya upanga ule. Orion aliangukachini na alipojiinua hakumuona Seidon. Seidonaliingia ndani ya chumba kile, mwanga uliojaa humondani ulimfanya kufinyafinya macho maanaalishindwa kuuvumilia, kwa tabu aliliona fuvu laCleopas limewekwa mahali na ndilo hasa lililokuwalikifanya mwanga ule, Seidon alilikimbilia naakajifungua kitamba chake cha kiuno ambachokilikuwa na mfuko na kufunika fuvu lile, mara gizanene likatawala chumba kile.

Seidon alimuona Orion kwa mbali akiwa anaingiakwenye ule mlango, Seidon akajibana kimya kabisa,Orion aliingia mpaka ndani kabisa ya chumba kilelakini alimpita Seidon bila kumuona. Kwa mwendowa taratibu Seidon aliulekea mlango, alihakikishahafanyi kelele yoyote ili asimgutushe Orion,alifanikiwa kutoka nje na akapiga mbinja kali yamtindo wake mara farasi wake akafika eneo lile,bila kuchelewa Seidon akapanda farasi na kuanzakutimua mbio, aliamua kupuuzia maagizo yote yaSherhazad malkia wa Soria, na kuondoka kwakupitia lango la maghalibi.

***Mishumaa mikubwa yapata arobaini na saba ilikuwaimewashwa na kufanya mwanga wenye joto lakipekee ndani ya kasri la Sharhazad, malikia waSoria, akiwa kwenye dirisha lake la ajabu, aliwezakuona ulimwengu wote isipokuwa upande wa nyumayake, aliona kila kitu alichokifanya Seidon na jinsialivyomgeuka, akasikitika na kusema, “Seidonameamua kutugeuka, sasa ntamuonesha mimi ninani,” Sherhazad alitoka kwenye dirisha lake laajabu na kuketi kwenye kiti cha enzi akapiga makofimatatu na mara wazee wane wakaingia navikorokoro vyao vya kichawi.

Walipofika mbele yakewakaanguka kifudifudi na kutoa salamu hiyo yaheshima, Malkia wa Soria akawatazama nakuwaamuru wainuke, wakafanya hivyo, “Niwewaita,kuna kazi ngumu inatukabili mbele yetu, Cleopas,nataka fuvu la Cleopas, yule kijana niliyempa uwezona maagizo ametugeuka, sasa natakamumshughulikie na lile fuvu tulipate hapa haraka,”akasimama kutoka katika kiti chake na kujishikakiuno huku akiziruhusu nywele zake kumwagikasakafuni, akavuta hatua tano mpaka kwa mmoja wawale wazee, akamshika bega na klumwambia,“Nataka kimbunga upande wa Maghalibi,”Vumbi kubwa lilitimka, upepo wa kisulisuliulinyanyua kila kitu, Seidon alipambana na upepohuo ambao ulitaka kumfanya farasi wake ashindwekuendelea, lakini kadiri ya ujasiri wa Seidonalimuendesha farasi yule kwa ustadi kiasi kwambaupepo ule haukumsumbua.Sherhazad akiwa kwenye dirisha lake la ajabu,alikasirika kwa kuona Seidon hapati shida nakimbunga kile, alisonya sonyo refu na kimbunga kilekikakatika ghafla, akageuka kumtazama mzeemwingine, “Mvua ya mawe” aliamuru tena.

Mara anga likatanda wingu nene na mvua kubwa ya maweikaanguka, Seidon akiwa katika mwendo kasi aliionamvua ile ikinyesha kumzunguka lakini alipo yeyehapakuwa na chochote, radi nazo zilijitahidi kupigalakini wapi Seidon aliendelea kupiga mbio.“Inaonekana Seidon kawa jeuri sasa, nampa pigo lamwisho, na hasara iwe kwetu sote. Wape akiliwaamke, Wahamsud na Wakalban”Ndipo Seidon alipohisi anakimbizwa na watu wengiwenye farasi.

****Amata alimtazama Seidon kwa huruma sana,akampa kikoto cha maji ya kunywa, Seidonakayanywa na kidogo akaonekana kupata nguvu.“Seidon” Amata aliita. Seidon aliinua kichwakuashiria itiko. Amata akanyanyuka kutoka palealipokaa na kuelekea kwenye ukingo wa korongokubwa sana, akageuka na kutazama palealipomuacha Seidon, akafungua kinywa chake nakumueleza Seidon,“Ninyi wote hamjui mnachopaswa kutenda, kuliletahilo fuvu la Cleopas kwenye ardhi yako ni kuongezamikosi.”Seidon aligutuka, akamkazia macho Amata,“Amata, we wa wapi? Inaonekana hujui lolote juu yafuvu hilo” Seidon alimueleza Amata huku akimtoleamacho. Amata akacheka kidogo, akaitazama peteyake iliyokuwa iking’aa kwa rangi tofauti tofauti,akaushusha mkono wake.“Seidon, fuvu la Cleopas linatakiwa lirudi kwaCleopas.

Kwa hiyo mwenye kupata baraka zaKlakos ni yule atakayerudisha lile fuvu pale” Amataalimeza mate aliinua kibuyu chake cha maji nakugugumia mafunda kadhaa, akamuendea Seidonna alipomfikia akachuchumaa mbele yake,akamuuliza.“Sikia, Unaijua Klakos ni nini?” Amata alimtupiaswali Seidon, na Seidon alionesha ishara yakwamba hajui.“Vizuri sana, na wote hamjui, wote kabisa hamjuisiri ya fuvu la Cleopas, sasa sikiliza, Cleopas nawenzake sita ndio walikuwa wakiiendesha dunia yachini, dunia ya wafu, dunia ya waliolala, wao daimawamejipanga kwa mtindo huu, kushoto wapo watatuAminus, Petrius na Segidus na kulia wapo watatu Sagitarius, Hesmepitus na Sectogamus, Cleopasyupo mbele katikati yao, ukiwaweka wote hivo ndioule mkao wao unaitwa Klakos sasa waingerezamiaka ile waling’oa fuvu la Cleopas ndiyo wakaletaukame duniani maana chemchem, mito, mimeavyote si vinaota kutoka chini ni baraka za Klakos.Laana aliowapa ndio ile vita ya dunia huko Ulaya namatatizo mengine” Amata alimwangalia Seidonambaye alionekana kukodoa macho tu.“Umenielewa?” alimuuliza Seidon ambaye alibakimidomo wazi, “Sasa unatakiwa uchukue lile fuvuulirudishe kule kwa Cleopas kwenye mji uliopotea,mji wa wafu, Hamunaptra, mji ulio chini ardhini”.

Seidon alishusha pumzi ndefu na kujiweka vizuribaada ya kusikia habari hiyo mpya.Aligeuka pembeni na kuutazama upanga wake,upanga wa Vernad, akauinua na kuubusu“Sikulijua hilo, na hakuna aliyewahi kuniambia”Seidon alimueleza Amata, aliuinua mkono wake nakuuweka begani kwa Amata “Wewe unatoka wapi?”“Mimi natoka Bara la Giza, nchi isiyo na mwanga,Amata ga imba, shujaa wa msitu wa Solondo,”Amata alijitambulisha kwa ubabe huku akijipigapigakifuani. Seidon alimtazama kwa makini kijana huyumweusi aliyejiamini kuliko vile alivyo.“Amata, nakualika katika hili, ufuatane namitukakamilishe kazi hii, tuondoe laana katika jamii nabaraka za Klakos zitumwagikie kama umande waasubuhi” Seidon alimtupia ombi Amata kwa lughaya kushawishi.

NINI KITAENDELEA?
 
“Mimi natoka Bara la Giza, nchi isiyo na mwanga,Amata ga imba, shujaa wa msitu wa Solondo,”Amata alijitambulisha kwa ubabe huku akijipigapigakifuani. Seidon alimtazama kwa makini kijana huyumweusi aliyejiamini kuliko vile alivyo.“Amata, nakualika katika hili, ufuatane namitukakamilishe kazi hii, tuondoe laana katika jamii nabaraka za Klakos zitumwagikie kama umande waasubuhi” Seidon alimtupia ombi Amata kwa lughaya kushawishi.

SEHEMU YA 06

“Hamna shaka, ombi lako limefika panapostahili,bega kwa bega tutakamilisha hilo, miminitakusindikiza kwa jua na mvua, kwa baridi na joto,kwa shida na raha,” walipeana mikono ya ushindi,kisha Amata akamuacha Seidon aendeleekupumzika.Baada ya majua 14Mazoezi makali yalikuwa yakiendelea kati ya Amatana Seidon katika misitu ya Progos, mazoezi yakutumia panga, mishale yote yalichukua nafasi ilikumuweka fiti Seidon.

Walipokuwa wameketi wakiota moto, Amataakamwambia,“Naona sasa tupo vizuri, twaweza kwenda” Amataalimwambia Seidon“Yah! Kumbuka tunaanzia kwa Wahamsud ambaondiyo sasa wanalo fuvu hilo” Seidon alimkumbushaAmata.“Nakumbuka, Wahamsud tunawavamia usiku wamanane kupitia milima ya Ararat, tukiteremka ulemlima kwa chini utaona kijiji chao pale weweutaenda kuliichukua hilo fuvu na mimi nitakulinda,inabidi tuhakikishe usiku uohuo tuwe tumeikamilishakazi hiyo, maana wakitukamata tutakuwa nyama yambwa” Amata alimueleza Seidon huku wakiwa njianikurudi kijijini.Mchana walijiweka sawa na jioni yake kuondokakijijini kwao kwa dhumuni la kukikabili kijiji chaWahamsud.

Amata aliufutika upanga wake vizuri,aliiweka sawa pete yake ya ajabu aliyoipata kwabibi kizee wa Msitu wa Solondo, kwa ujumla Amataalikamilika. Seidon, mpiga mbio, alikuwa tayari juuya farasi wake, akiwa na upanga wa Vernad kiunonina sasa alidhamilia kuupata upanga wa Orion iweisiwe.Safari ikaanza wawili hawa wakaingia safarini, safariilikuwa ngumu sana, kwa maana ilikuwa ni kupandana kushuka milima yenye mchanga mwingi, marakwa mara walikutana na dhoruba za jangwanizilizowapa taabu lakini walivumilia, safari yote hiyohakuna hata aliyeongea na mwenzake kila mmojaalikuwa akiitafakari safari hiyo ngumu.Jua lilipokuwa maghalibi waliukabiri mlima mkubwauliojaa mawe na miiba, kwa tabu walipanda mlimahuo wakiwa juu ya farasi wao na baada ya muda tuwalifanikiwa kufika kwenye tambarare iliyojazwa nauoto wa mkakati na mimea mingine yenyekustahimili shida, kando ya jiwe kubwa kulikuwa namti wa mtende uliomea vizuri.

“Seidon, tuketi hapa, tusubiri muda ufike ili tuwezekuwashukia Wahamsud,” Amata alimwambiaSeidon.“Kwani haiwezekani kuwavamia sasa?” aliuliza“Hapana, Wahamsud wanategemea nguvu ya nyotainayoitwa LEO, inabidi tusubiri hapa kwa masaakama mawili, nyota ile ikifika maghalibi tayarihawana nguvu, tutafanya kazi yetu kwa urahisiambao hautautegemea, na tukishalipata fuvu nisafari ya moja kwa moja Hamunaptra kupitiaupande wa kusini kandokando ya bahari nyekundumapaka kaskazini mwa Kushi, tusipite kwa yulemchawi Sherhazad atatusumbua sana kwa kuwabado ana chuki na wewe.”

Waliketi chini ya mtende huku Amata ga Imbaakiendele kuburudika na kibuyu chake cha pombe.“Amata, huoni kwamba pombe unayokunywainaweza kuharibu mipango yetu?” Seidon aliulizabaada ya kuchoka kuvumilia kwa kuwa wao kwaopombe ni mwiko kabisa kwani wamelelewa nafalsafa inayosema pombe hulowesha roho.“Hapana, hii inasaidia sana kwa kuwa kuna baadhiya nguvu za kishetani ambao hazitaki pombe, sasamimi na wewe hatujui tukienda huko tunaendakukutana na nini,” lilikuwa jibu la Amata ga Imba.Ilipotimu usiku wa manane, sauti ya Mbweha wajangwani ikasikika, Amatagaimba aliinuka kutokapale chini ya mtende, mbala mwezi ilikuwa iking’aasana, Amata alisimama na kuangaza macho yakehuku na kule, akamwamsha Seidon.“Kijana, amka, saa imefika inapaswa tutende liletulilolikusudia,” Amatagaimba alimuamsha Seidon.

Seidon alisimama na kujinyoosha, akachukuagudulia lake la maji na kugugumia mafunda kadhaa,kisha akalitua na kulirudisha kiunoni.“Na hii mbalamwezi huoni kama itatuharibia?”Seidon aliuliza.“Usiwe na shaka, Seidon, nitaifunika kwa nguvu zaajabu, na wingu litasimama juu yake mpakatutakapomaliza kazi yetu,” Amatagaimba,alimtazama farasi wake na kumshikashika kichwani,“Seidon, tunaingia katika mji bila farasi, kwamwendo wa miguu yetu,” Amata alizungumza hukuakiweka podo lake mgongoni na kuukamata vyemauta wake, kwa mwendo wa taratibu walianzakuushuka mlima ule huku Seidon akishuhudia winguzito likianza kuifunika ile mbalamwezi taratibu nakutengeneza kivuli kizito.

Haikuwachukua mudawalifika katika kilima kingine kidogo tu, walipokweampaka juu waliweza kuona mji wa Wahamsud ukiwakimya ni mioto tu ya hapa na pale iliyokuwaikiendelea kuwaka. Amata ga Imba alituliaakiangalia kwenye zile nyumba za Wahamsud,Seidon hakuthubutu kumuuliza anaangalia nini balialiendelea kumtazama.“Seidon, hapa kazi ni ndogo tu, unaiona nyumbaileeeeeeee,” Amata alimuonesha Seidon nyumbailiyopo katikati ya zingine, iliyokuwa ikiwaka taahafifu, “Pale ndipo penye fuvu la Cleopas, ulinziuliopo pale ni mkali sana usione pametulia, sasajiweke tayari tunaenda na lolote linaweza kutokea,mimi nitalinda nje wakati wewe utaingia ndanikulichukua hilo fuvu,” Amata alitoa maelekezo nakisha akauchukiua uta wake na kuuweka sawa,akachomoa mshale na kuutunga vyema kishaakauvuta kwa nguvu sote, “Seidon, washa motohapo mbele, nataka niwapelekee kizaizai,”

Seidon akawasha moto kwenye ncha yam shale wa Amatagaimba iliyokuwa imefungwa kwa kitambaakizito chenye mafuta mazito ya mimea, kiliposhikamoto sawia, Amata aliutazma mshale wake ulikuwatayari kwa shambulizi, “Nakuagiza, katika jina laAmatagaimba, shujaa wa msitu wa Solondo,alieukonga moyo wa Baghoza na kuushusha utawalawa Kerume kwa mshale huu, mshale wa urithi wamzee Nkhunulaindo, uende ukaanzishe kiletunachokikusudia,” akaunuia mshale wake aliokuwaamekwishauvuta kwa nguvu zote, akauachia naoukaondoka kwa kasi ya ajabu, mvumo wake ulitikisamiti michache iliyo jirani na mle ulimopita,wakasimama juu ya kilima kile wakiuangali ukiendaulikotumwa.

Juu ya paa la nyumba ya mtawala wa Hamsud,mshale wa ule ulitua na kuwasha moto paa lilelililojengwa kwa aina Fulani ya mimea iliyoshikamoto ule kwa kasi.“Twende sasa!” Amatagaimba akamwambia Seidonkisha wote wawili wakashuka wakikimbia upandeule kuliko na ile nyumba lilikohifadhiwa lile fuvu,Seidon, mpiga mbio alikuwa mbele na upanga wakemkononi, upanga wa Vernad mwana wa Velvesh.Watu walitoka kwenye nyumba zao na kujilinda hukuwengine wakienda kusaidia kwa mfalme.“Tumevamiwa!!!” sauti ilitoka kwa mtu mmojamwenye tambo kubwa aliyekuwa juu ya paa lanyumba mojawapo lililoonekana lilijengwa kamangome ya kuweza kuwaona adui wanapokujakutokea pande za milima Ararat.

“Tumevamiwaaaaaa!” Yule mtu aliendelea kutoahamasa kwa wengine, milio ya panga zilizofutwakutoka katika ala zake ilisikika kila upande, Yulemtu kule juu alichukua baragumu na kupuliza, ikiwani ishara ya kuruhusu mapigano ya damu, kablahajatua lile baragumu lake, mshale mmoja wa Amatagaimba ulipenya kifuani na kumdondoshakutoka juu mpaka chini, Amatagaimba alitua ardhinikutoka juu ya nyumba moja wapo na kuufuta upangawake, hakujali ni wangapi wamemzunguka na silahagani lakini ustadi wake wa kuuzungusha ule upangauliweza kuwapunguza nguvu adui kwa kuwakatavibaya, ijapokuwa walionekana ni wengi lakiniwalionekana kana kwamba hawana nguvu za kufanyamapigano hayo ya kushtukiza.

Seidon, alipambana na upinzani mkali kuwezakulifikia lango la ile nyumba, huku nje tayari akiwaameshaua askari kadhaa, aliupiga teke mlango naukafunguka bila kipingamizi, aliingia ndani nakutazama huku na huku, mara akasikia sauti yakicheko nyumma yake, alipogeuka aligonganamacho na mfalme wa Hamsud aliyevalia guo lakejeusi, mkononi akiwa na upanga wa makali kuwili,Seidon alisimama kimapigano na upanga wakemkononi.“Umekuja mwenyewe sio, sasa kama siku ilenilikuacha hai leo lazima nikikate kichwa chako kwaupanga huu, upanga wa Hamsud, wenye mapigo yaajabu,” Yule mfalme aliongea kwa jazba hukuakimfuata Seidon kwa kasi.

“Hakika, nimekuja kuitaka roho yako na kulichukuafuvu la Cleopas ambalo si mali yako, aminnakuambia upanga huo mkononi mwako leo hiiutakuwa mikononi mwangu,” kabla Seidonahajamaliza kusema, ilisikika kelele ya panga mbilizilizogongana na kutoa cheche, ilikuwa ni pigo lakifo lililotoka katika mikoni ya Yule mfalme, lilikuwalikikielekea kichwa cha Seidon ambaye tayari nayeye Alisha inua upanga wake na kuuzuia ule wa Yulemfalme, kisha wote wawili wakashusha mikono yaochini na zile panga bado zikawa zimesigana katakatiyao, wakisukumana na kutazamana kwa gadhabu.Seidon alijisogeza pembeni kwa ghafla na kumpigapigo la kiwiko Yule mfalme, lakini kabla hajafanyalolote, upanga wa mfalme ulipita katika tumbo laSeidon na kuchana upande wa vazi lake, Seidonaakaruka sarakasia kutua upande wa pili alijishikatumbo kwa maumivu, lakini bado alikuwa katikamapambano, mapigo kadhaa ya mapangayaliifunikiza nyumba ile huku Seidon akionekanakuzidiwa maarifa na Yule mfalme, hakuna mtualiyeingia katika pambano hilo.

Amata ga Imba alikuwa nje akiimarisha ulinzi kwakupambana na askari wale ambao walijiziuka nayewakisahau kuwa ndani ya hekalu lao kuna mwingineanayepambana na mfalme wao. Amata ga Imbaaliangusha wengi awezavyo huku akiwakwepa kwaustadi wa hali ya juu, akijaribu kuvuta muda iliSeidoni afanikishe lile alilotumwa.Amata ga Imba alipoona Seidon hana dalili zakutoka alifanya kila hila za kimapigano nakukimbilia upande, mwingine ambao alikuwa jiranikabisa na lile hekalu la Wahamsud, mara akajikutaamezingirwa na askari wenye uchu wa kuitoa rohoyake, aliishika pete yake na kuifanya anachojuayeye, mwanga mkali ukatoka kwenye pete ile nakuwaumiza mcho wale askari hata wasiweze kuonatena.

Amata aliukaribia mlango wa hekalu na kuonajinsi pambano lile lilivyokuwa likiendelea lakiniSeidon hakuonekana na upanga mkononi,“Seidoooooonnnnn!” Amata aliita na kumrushiaupanga wake, Seidon alijrusha kwa ustadi nakuudaka ule upanga, alijiviringisha kwa ufundikumuelekea Yule mfalme ambaye alishidwa kujuaamshambulie nani.Mfalme wa Wahamsud akiwa katika kutahamakiSeido alikuwa ameshafika miguuni pake nakumshindilia upanga wa tumbo uliompelekeakutokwa na uhai.

Seidon akampisha adondokeepembeni kisha akanyanyuka kwa haraka na kumkatakichwa, aliurudisha upanga wa Amata kwa kuurushana kisha akauokota ule wa kwake, akaurudisha alanina kuingia kwenye kijichumba kimojawapo, maragiza likatawala ndani ya hekelu lile. Amata ga Imbaalipoona giza hilo akajua kumekucha, akapigambinja kali na muda mfupi tu, farasi wale wawiliwalikuwa tayari wamefika, Seidon akarukia juu yammoja wapo na Amata vilevile kisha wakapigambio kuelekea upande wa kusini. Nyuma yao jeshililikuwa likija kwa kasi na farasi.“Amatagaimba! Wanatufuata….” Seidon alipigakelele huku akiwa katika kasi ya ajabu.“Usijali Seidon, piga mbioooo,” Amata alijibu,akainua mkono wake na kuibusu pete yake, “Shushadhoruba ya jangwani ee pete ya ajabu,” Amataalisema maneno hayo huku pete ile ikiwaq jiranikabisa na kinywa chake. Mara radi moja kali ilipigana mchanga uliochanganyika na vumbi ulitimkanyuma yao na kuwatenganisha kati yao.

Seidon naAmata walisimama mbele na kugeuka nyumaambako walishuhudia vumbi zito likiwazuia adui zaowasiweze kuwafikia.Amata ga Imba na Seidon, wakagonganisha viganjavyao na kupeana ishara ya mafanikio, kishawakaendelea na safari kuelekea mji wa Hamunaptra,tayari kwa kazi ya kurudisha fuvu lile la Cleopas.“Seidon,” Amata amuita swahiba wake, “Sasatunakabili mji wa Kush, hauna tabu kuuvuka, lakinisharti lake hutakiwi kuongea na mtu yeyote, na mjiule ni vizuri kuuvuka majira ya saa tano wakati jualinapokuwa linauendea utosi, lakini kuna kijiji kidogoambacho lazima tukipite kijiji hiki ni jicho kubwa lamalkia wa Soari, Sharhazad, pale patakuwa naugumu wa kupita kwa vyovyote vile, kwa hiyotujiimarishe kiroho na kiakili,” Amata alimaliza risalayake na kumuacha Seidon akiwa midomo wazikwani yote haya hakuwa akiyaelewa tangu awali.Waliendelea mwendo mrefu kidogo na kufikasehemu moja tulivu yenye dimbwi la maji safi,dimbwi lililozungukwa na mitende na maua mazuri.

“Tupumzike hapa Amata, nimechoka sana,” Seidonaliomba, Amata alisimama na kumtazama Seidonambaye tayari alikuwa amekwishaikanyaga ardhi nakuyakimbilia maji yale.“Seidon!” Amata aliita, Seidon akageuka, “Subirikwanza, unajua tupo wapi?” Amata aliuliza,“Jangwani, kwani vipi?” Seidon alijibu na kutupaswali, “Sasa wewe umeshawahi kuona jangwanikuna maji? Seidon hayo si maji,” Amataalimwambia Seidon huku akimvuta kumrudishanyuma.

NINI KITATOKEA?
 
“Tupumzike hapa Amata, nimechoka sana,” Seidonaliomba, Amata alisimama na kumtazama Seidonambaye tayari alikuwa amekwishaikanyaga ardhi nakuyakimbilia maji yale.“Seidon!” Amata aliita, Seidon akageuka, “Subirikwanza, unajua tupo wapi?” Amata aliuliza,“Jangwani, kwani vipi?” Seidon alijibu na kutupaswali, “Sasa wewe umeshawahi kuona jangwanikuna maji? Seidon hayo si maji,” Amataalimwambia Seidon huku akimvuta kumrudishanyuma.

CHAPISHO LA 07

Seidon hakulipinga hilo, alirudi nyuma na molja kwamoja akapanda farasi wake, akamtazama Amata,Amata alikuwa akiyaangali yale maji kwa makinisana.

“Huo ni mji wa watu, tusiwaamshe twendetuendelee mbele,” baada ya kusema hayo Amata naSeidon waliendelea mbele zaidi na zaidi, wakipandavilima na milima ya jangwani. Jua la asubuhi lilianzakuchomoza upande wa Mashariki na kuanzakuliangaza anga lote, Amata alimuongoza Seidonmpaka kwenye mji Fulani ulioonekana kukaliwa nawatu wachache sana, wake kwa waume,hapakuonekana mtoto, waliusogelea mji huo nawalipoufikia walipokelewa na wasichana warembo.Seidon aliwatazama wasichana hawa, walikuwawarembo wa kuvutia, kisura hata kiumbo.“Usiogope Seidon, hapa ni mahali salama sana,kula, kunywa, lakini usilale na mwanamke, ukifanyahivyo utakuwa umeharibu kila kitu,” Amataalimwambia Seidoni wakati akiingia ndani yanyumba moja iliyoonekana kupambwa na mauamengi mazuri lakini bado ilhali iko jangwani.

Ndani kulikaa mzee mmoja wa makamo aliyevaliavazi la ngozi ya ngamia, na kichwani mwake akiwana kofia ya manyoya ya mbuni.“Unakaribishwa sana ewe shujaa wa msitu,” Yulemzee alitamka maneno hayo huku akiinamishakichwa chake.“Nimekaribia, ee mfalme wa Kushi, nimekuja kwakomimi na mwenzangu, tunapita njia tunaenda hukowaliko wafu, utujalie yale tunayohitaji pamoja namema yako,” Amata akasema hayo hukuakiinamisha kichwa chake kwa namna ile ilealiyofanya Yule mzee pale mwanzo.“Shaka ondoa, siku zote, mwema hupata mema nambaya hubaki na mabaya yake, kwa nini nikupedhoruba ilhali shwari ninayo? Seidon kitukuu chaVernad, mwana wa Velvesh, bahati yako sanahukumrudia Sherhazad, lakini roho ya babu yakoVernad iko ndani yako, usimuache huyu shujaa waMsitu hata utakapotimiza lile ulilotumwa,” Yulemzee aliongea kwa utulivu sana, Seidon alishangaakukuta Yule mzee akilijua jina lake vyema, kalijuajeyeye hakuwa na jibu.

Amata ga Imba na Seidon,walikaribishwa kwenye zuria safi la ngozi yangamia, kisha wasichana warembo waliingia nakuwapa huduma zote wazitakazo, huku Seidonakipewa matibabu ya jeraha lake hukuakikandwakandwa viungo vyake.Amata ga Imba na mwenzake Seidon walipewaukarimu wa hali ya juu sana, huduma zotealizostahili kupata mwana wa Suiltan basi waowaliziopata pia. Seidon alihisi nguvu zimemrudia namwili wote ulikuwa umekuwa katika hali yake yakawaida.

“Unajisikiaje sasa?” mwanadada\mrembo aliyepigamagoti mbele ya Seidon alimtupia swali lile, Seidonalijikuta anashindwa kujibu, alibabaika kwa swalihilo hasa alipomwangalia msichana yule mbichiambaye alivaa nguo ndefu lakini iliyoanzia kiunonikurudi chini huku juu alibaki hivohivo, chuchuzilizochongoka na kusimama zilimfanya Seidonapagawe, midomo ilimchezacheza, kabla hajasemakitu alikabidhiwa ua zuri la manukato safi,akalipokea na kulinusa, ua la yugiyugi, Seidonakaongea maneno yasiyoeleweka katika lugha yakwao na lile ua likachanua mkononi mwake,akatikisa kichwa kuashiria kuwa kuna kituamegundua. Katika mila za Wavelvesh, ua layugiyugi lilimaanisha bahati, hivyo msichana huyukumletea ua hilo Seidon ilikuwa ni kama bahati.“Unaitwa nani?” Seidon akamuuliza“Teboria,” akajibiwa.“Teboria, Teboria, Teboria!” Seidon alirudia kutamkajina hilo kwa mara kada kwa sauti ya chini, alihisiameshawahi kulisikia sehemu lakini hakumbuki niwapi.

Teboria akaketi jirani na Seidon, Seidon akahisiharufu nzuri ya manukato kutoka kwa binti yule,akasogeza kinywa chake jirani na yule binti, yulebinti naye akafanya hivyo, ndimi zo zikapishana kwaufundi mkubwa sana, Seidon alihisi raha ya ajabuambayo hakuwahi kuipata katika maisha yake, sautiza mahaba zikaanza kukijaza chumba kile. Seidonakachanganyikiwa, akaweka upanga wake pembenina kutaka kumsaula yule binti, yule binti akajitoakifuani mwa Seidon, Seidon alipomtazama usonihakuwa Teboria, balisura ya msichana mwinginekabisa ambayo pia haikuwa ngeni usoni mwake.

“Ni nani wewe?” Seidon alimuuliza yule msichanahuku akiwa kajirushia upande wa pili wa kichumbahicho.“Ulinikimbia ee? Sasa nimekupata tena, nasintokuacha mpaka uitimize ile ahadi yangu, mimini Sherhazad, Malkia wa Soria, nimekuona tanguukiwa Hamsud na nikafurahi kwa kuwa ulifanikiwakuchukua lile fuvu, haya nikabidhi au la naitoa rohoyako na fuvu nalichukua,” Sherhazad, sasa alichukuasura na umbo lake la kawaida. Chumba kikajaamanukato maradufu, Seidon akabaki anatetemekamkononi akiwa ameshika ule mfuko mweusi ambaondani yake kulikuwa na lile fuvu. Sherhazadalimfuata huku mikono yake ikiota kucha ndefukupita kawaida, ilikuwa ni hali ya kuogofya, ulimiwake uligawanyika mara mbili, mara kichwa chakekikageuka na kuwa cha nyoka, Seidon alisimama nakuutwaa upanga wake, sasa Sherhazad akawa nyokakamili, nyoka mkubwa, tuseme joka.

Lile joka likaruka kumfata seidon pale aliposimama, Seidonakaepa na kuvurumisha ule upanga lakini akalikosa.Kishindo kile kikubwa cha lile joka kuangukia chinikiliwashtua wengi.Amata ga Imba akiwa amejilaza chini ya mtende,alisikia kishindo hicho na mara akasimama nakukimbilia kwenye kile kinyumba alimokuwa Seidon,alipofika hakuamini macho yake, Seidon alikuwaamevirigwa na lile joka, Amata ga Imba akaufutaupanga wake na kukata sehemu ya mkia wa lilejoka, mara akasikia sauti ya mwanamke ikichekakwa kebehi, Amata ga Imba alitazama huku na kulehakuona kitu wala mtu ila sauti hiyo iliendeleakumcheka kwa kebehi.

Amata ga Imba akatulia palealipo huku upanga wake ukiwa juu hewaniameushika mpini kwa mikono yake miwili,alipoushusha alikata katikati mwa lile joka, lile jokalikapiga ukelele wa ajabu na kumuachia Seidon,kisha likajizungusha pale chini na badala yakeakasimama msichana mrembo, Teboria.“Amatagaimba, majini haya, tuondoke,” Seidon,alikurupuka na kutoka nje, Amata akamfuata,Seidona alikuwa tayari juu ya farasi wake, “Seidon,”Amata aliita na kumuamuru ateremke kwenye farasi.“Nilikwambia nini Seidon?” Amata ga Imbaalimuuliza kwa ukali, “Nilikwambia nini?” aliulizakwa kelele, “Sikiliza Seidon nilishakwambia epukanasana na wanawake, hawa wataharibu mpangomzima, sio binadamu wale ni majini, sasa usirudietena, Sherhazad keshajua unakoelekea naameshakuona ukiwa na hilo fuvu sasa kazi ni nzitokufika Hamunaptra, na hii ni kwa sababu tuumekiuka masharti.

Wewe mwenyewe ulinambiakuwa babu yako amekuonya hivyo hivyo juu yawanawake, sasa kwa nini utaki kusikia? Kuwamwangalifu,” alimaliza Amata ga Imba kishaakarudi na Seidon mpaka pale chini ya mtende.Wakiwa katika kuketi pale mara akaja mmoja wamasuria wa yule mzee aliyewakaribisha akawapaishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo,wakaingia ndani na kuketi mbele yake.“Sikilizeni vijana, hapa pameshaingia matatizo,inabidi muondoke mara moja, tayari pepo zinatakahilo fuvu kwa nguvu zote, pepo la Soria, mwanamkehatari tayari limeshakuja hapa kwa nguvu zotekabisa.

Naomba watu wangu wasidhurike,muondoke, muende na safari yenu, lakini kwakuwasaidi ili mfike salama, sikilizeni, msipandefarasi kwani hana uwezo wa kuvumili shida nadhoruba za jangwani, maana sasa mtakatishajangwa kubwa lenye vikwazo vingi lakini hamnabudi kuvuka ili mfike haraka huko muendako na hiyondiyo njia fupi, piteni katikati, usiku, miifuata nyotaya kilimia itawaongoza mpaka katika bonde laSham, ambapo amtalivuka na kutokea karibu namto Frati kutoka hapo nafikiri mnaijua njia,” yulemzee mwnyeji wao aliwaekeza na kisha kuwapatiangamia, masurufu ya njiani na kuwaruhusu waendezao, mara tu Maghalibi ikifika ili waondoa nuksikatika kijiji chao.Safari ilianza jioni hiyo, Amata ga Imba akiwa mbelena Seidon akiwa nyuma yake, walilikata jangwa kwataabu ya upepo na ghasia za vumbi lakiniwalivumilia ili lengo lao lipate kutimia.

Usiku wamanane walijikuta wamefika mbali sana na mbeleyao palionekana kitu kama korongo kubwa sana,mbala mwezi ilikuwa ikiwaongoza kwa mwangawake mwanana, wakasimama kwa muda nakutazama mandari ile yakutisha kama si ya kuvutia,‘Bonde la mauti’ Amata ga Imba alihisi sautiikimnong’oneza, akageuka nyuma asione mtu,akaendelea kutazama kutazama lile korongo kubwasana, kitu kama moshi kilikuwa kikifuka na kulijazalile korongo, waliweza kuona vitu kama mawe simawe ilimradi tu vilikuwepo vipo. “Seidon, hapakuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon,akageuka kumtazama akamuona ametulia kimyakama mtu anayetafakari kitu fulani.

“Seidon,unawaza nini?” akamuuliza.“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maananaona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukatatamaa,” Seidon alijibu.“Usikate tamaa, hakikisha unafika mwisho naunarudisha hilo fuvu kwa Kleopas uwaokoe watuwako,” Amata ga Imba alimueleza kwa upole.“Hapa ni wapi au niulize hiki ni nini?” Seidon aliulizahuku akioneshea mkono kwenye lile bonde, Amataga Imba kwa kutumia upanga wake akaukandamizachini mkono wa Seidon, “Usipanyoshee kidolemahali hapo, hapo ni bonde la mauti, mji wa wafu,”alimjibu. Seidon alionekana wazi kushikwa na wogawa hali ya juu sana katika hilo.

Akajiinamia kichwakwenye nundu ya ngamia, akatazama ule mfukomweusi wenye fuvu la cleopas, akarudisha machoyake tena kwenye lile korongo, akamuuliza Amataga Imba, “Tunavuka?”“Ndiyo hatuna budi kuvuka,” Amata ga Imbaakaibusu pete yake na kuitazama kwa makini, kishaakshusha mkono, “Sikia, inabidi tufike paleeeeeekwenye ule mlima unaong’aa sana, tykifika paletayari Klakos itaanza kuvuta harufu ya hilo fuvu,najua nguvu kutoka kwao zitatujia ilitukamilishesafari na wakati huohuo upinzani utaongezeka, hayatwende,” Amata ga Imba alisema hayo nakumuamuru Seidoni kuendelea na safari.Amata ga Imba na mwenzake Seidon walipewaukarimu wa hali ya juu sana, huduma zotealizostahili kupata mwana wa Suiltan basi waowaliziopata pia.

Seidon alihisi nguvu zimemrudia namwili wote ulikuwa umekuwa katika hali yake yakawaida.“Unajisikiaje sasa?” mwanadada\mrembo aliyepigamagoti mbele ya Seidon alimtupia swali lile, Seidonalijikuta anashindwa kujibu, alibabaika kwa swalihilo hasa alipomwangalia msichana yule mbichiambaye alivaa nguo ndefu lakini iliyoanzia kiunonikurudi chini huku juu alibaki hivohivo, chuchuzilizochongoka na kusimama zilimfanya Seidonapagawe, midomo ilimchezacheza, kabla hajasemakitu alikabidhiwa ua zuri la manukato safi,akalipokea na kulinusa, ua la yugiyugi, Seidonakaongea maneno yasiyoeleweka katika lugha yakwao na lile ua likachanua mkononi mwake,akatikisa kichwa kuashiria kuwa kuna kituamegundua. Katika mila za Wavelvesh, ua layugiyugi lilimaanisha bahati, hivyo msichana huyukumletea ua hilo Seidon ilikuwa ni kama bahati.“Unaitwa nani?” Seidon akamuuliza“Teboria,” akajibiwa.“Teboria, Teboria, Teboria!” Seidon alirudia kutamkajina hilo kwa mara kada kwa sauti ya chini, alihisiameshawahi kulisikia sehemu lakini hakumbuki niwapi.

Teboria akaketi jirani na Seidon, Seidon akahisiharufu nzuri ya manukato kutoka kwa binti yule,akasogeza kinywa chake jirani na yule binti, yulebinti naye akafanya hivyo, ndimi zo zikapishana kwaufundi mkubwa sana, Seidon alihisi raha ya ajabuambayo hakuwahi kuipata katika maisha yake, sautiza mahaba zikaanza kukijaza chumba kile.

Seidonakachanganyikiwa, akaweka upanga wake pembenina kutaka kumsaula yule binti, yule binti akajitoakifuani mwa Seidon, Seidon alipomtazama usonihakuwa Teboria, balisura ya msichana mwinginekabisa ambayo pia haikuwa ngeni usoni mwake.“Ni nani wewe?” Seidon alimuuliza yule msichanahuku akiwa kajirushia upande wa pili wa kichumbahicho.“Ulinikimbia ee? Sasa nimekupata tena, nasintokuacha mpaka uitimize ile ahadi yangu, mimini Sherhazad, Malkia wa Soria, nimekuona tanguukiwa Hamsud na nikafurahi kwa kuwa ulifanikiwakuchukua lile fuvu, haya nikabidhi au la naitoa rohoyako na fuvu nalichukua,” Sherhazad, sasa alichukuasura na umbo lake la kawaida. Chumba kikajaamanukato maradufu, Seidon akabaki anatetemekamkononi akiwa ameshika ule mfuko mweusi ambaondani yake kulikuwa na lile fuvu.

Sherhazadalimfuata huku mikono yake ikiota kucha ndefukupita kawaida, ilikuwa ni hali ya kuogofya, ulimiwake uligawanyika mara mbili, mara kichwa chakekikageuka na kuwa cha nyoka, Seidon alisimama nakuutwaa upanga wake, sasa Sherhazad akawa nyokakamili, nyoka mkubwa, tuseme joka.

Lile jokalikaruka kumfata seidon pale aliposimama, Seidonakaepa na kuvurumisha ule upanga lakini akalikosa.Kishindo kile kikubwa cha lile joka kuangukia chinikiliwashtua wengi.Amata ga Imba akiwa amejilaza chini ya mtende,alisikia kishindo hicho na mara akasimama nakukimbilia kwenye kile kinyumba alimokuwa Seidon,alipofika hakuamini macho yake, Seidon alikuwaamevirigwa na lile joka, Amata ga Imba akaufutaupanga wake na kukata sehemu ya mkia wa lilejoka, mara akasikia sauti ya mwanamke ikichekakwa kebehi, Amata ga Imba alitazama huku na kulehakuona kitu wala mtu ila sauti hiyo iliendeleakumcheka kwa kebehi.

Amata ga Imba akatulia palealipo huku upanga wake ukiwa juu hewaniameushika mpini kwa mikono yake miwili,alipoushusha alikata katikati mwa lile joka, lile jokalikapiga ukelele wa ajabu na kumuachia Seidon,kisha likajizungusha pale chini na badala yakeakasimama msichana mrembo, Teboria.“Amata ga imba, majini haya, tuondoke,” Seidon,alikurupuka na kutoka nje, Amata akamfuata,Seidona alikuwa tayari juu ya farasi wake, “Seidon,”Amata aliita na kumuamuru ateremke kwenye farasi.“Nilikwambia nini Seidon?” Amata ga Imbaalimuuliza kwa ukali, “Nilikwambia nini?” aliulizakwa kelele

NINI KITAENDELEA?ONE LOVE....
 
lile joka likapiga ukelele wa ajabu na kumuachia
Seidon, kisha likajizungusha pale chini na badala
yake akasimama msichana mrembo, Teboria.
“Amata ga imba, majini haya, tuondoke,” Seidon,
alikurupuka na kutoka nje, Amata akamfuata,
Seidona alikuwa tayari juu ya farasi wake, “Seidon,”
Amata aliita na kumuamuru ateremke kwenye farasi.
“Nilikwambia nini Seidon?” Amata ga Imba
alimuuliza kwa ukali, “Nilikwambia nini?” aliuliza
kwa kelele,
CHAPISHO LA 08
“Sikiliza Seidon nilishakwambia epukana sana na
wanawake, hawa wataharibu mpango mzima, sio
binadamu wale ni majini, sasa usirudie tena,
Sherhazad keshajua unakoelekea na ameshakuona
ukiwa na hilo fuvu sasa kazi ni nzito kufika
Hamunaptra, na hii ni kwa sababu tu umekiuka
masharti. Wewe mwenyewe ulinambia kuwa babu
yako amekuonya hivyo hivyo juu ya wanawake, sasa
kwa nini utaki kusikia? Kuwa mwangalifu,” alimaliza
Amata ga Imba kisha akarudi na Seidon mpaka
pale chini ya mtende.
Wakiwa katika kuketi pale mara akaja mmoja wa
masuria wa yule mzee aliyewakaribisha akawapa
ishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo,
wakaingia ndani na kuketi mbele yake.
“Sikilizeni vijana, hapa pameshaingia matatizo,
inabidi muondoke mara moja, tayari pepo zinataka
hilo fuvu kwa nguvu zote, pepo la Soria, mwanamke
hatari tayari limeshakuja hapa kwa nguvu zote
kabisa. Naomba watu wangu wasidhurike,
muondoke, muende na safari yenu, lakini kwa
kuwasaidi ili mfike salama, sikilizeni, msipande
farasi kwani hana uwezo wa kuvumili shida na
dhoruba za jangwani, maana sasa mtakatisha
jangwa kubwa lenye vikwazo vingi lakini hamna
budi kuvuka ili mfike haraka huko muendako na hiyo
ndiyo njia fupi, piteni katikati, usiku, miifuata nyota
ya kilimia itawaongoza mpaka katika bonde la
Sham, ambapo amtalivuka na kutokea karibu na
mto Frati kutoka hapo nafikiri mnaijua njia,” yule
mzee mwnyeji wao aliwaekeza na kisha kuwapatia
ngamia, masurufu ya njiani na kuwaruhusu waende
zao, mara tu Maghalibi ikifika ili waondoa nuksi
katika kijiji chao.
Safari ilianza jioni hiyo, Amata ga Imba akiwa mbele
na Seidon akiwa nyuma yake, walilikata jangwa kwa
taabu ya upepo na ghasia za vumbi lakini
walivumilia ili lengo lao lipate kutimia. Usiku wa
manane walijikuta wamefika mbali sana na mbele
yao palionekana kitu kama korongo kubwa sana,
mbala mwezi ilikuwa ikiwaongoza kwa mwanga
wake mwanana, wakasimama kwa muda na
kutazama mandari ile yakutisha kama si ya kuvutia,
‘Bonde la mauti’ Amata ga Imba alihisi sauti
ikimnong’oneza, akageuka nyuma asione mtu,
akaendelea kutazama kutazama lile korongo kubwa
sana, kitu kama moshi kilikuwa kikifuka na kulijaza
lile korongo, waliweza kuona vitu kama mawe si
mawe ilimradi tu vilikuwepo vipo. “Seidon, hapa
kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon,
akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya
kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon,
unawaza nini?” akamuuliza.
“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana
naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata
tamaa,” Seidon alijibu.
“Usikate tamaa, hakikisha unafika mwisho na
unarudisha hilo fuvu kwa Kleopas uwaokoe watu
wako,” Amata ga Imba alimueleza kwa upole.
“Hapa ni wapi au niulize hiki ni nini?” Seidon aliuliza
huku akioneshea mkono kwenye lile bonde, Amata
ga Imba kwa kutumia upanga wake akaukandamiza
chini mkono wa Seidon, “Usipanyoshee kidole
mahali hapo, hapo ni bonde la mauti, mji wa wafu,”
alimjibu. Seidon alionekana wazi kushikwa na woga
wa hali ya juu sana katika hilo. Akajiinamia kichwa
kwenye nundu ya ngamia, akatazama ule mfuko
mweusi wenye fuvu la cleopas, akarudisha macho
yake tena kwenye lile korongo, akamuuliza Amata
ga Imba, “Tunavuka?”
“Ndiyo hatuna budi kuvuka,” Amata ga Imba
akaibusu pete yake na kuitazama kwa makini, kisha
akshusha mkono, “Sikia, inabidi tufike paleeeeee
kwenye ule mlima unaong’aa sana, tykifika pale
tayari Klakos itaanza kuvuta harufu ya hilo fuvu,
najua nguvu kutoka kwao zitatujia ilitukamilishe
safari na wakati huohuo upinzani utaongezeka, haya
twende,” Amata ga Imba alisema hayo na
kumuamuru Seidoni kuendelea na safari.
Walishuka katika bonde lile wakiwa na wale ngamia
taratibu, ukimya ulitawala kila kona giza likazidi
kuwa kubwa, wakazidi kutokonmea gizani mpaka
wakafika mahali hawaonani. Amata ga Imba
akasimama, akapapasa na kumgusa Seidon,
akamshika mkono, kisha taratibu akazidi kwenda
nae ndani zaidi ya korongo lile. Kelele za watu
waliokuwa sokoni zilisikika kwa mbali, mwanga
hafifu ukaanza kujitokeza kwenye lile giza, Seidon
alikuwa akiogopa sana, “Usioneshe unaogopa,
jikaze, huu ni mji wa wafu, hawa wote utakaowaona
ni wafu, waliokufa zamani huko duniani,”
Amatagaimba akamwambia Seidon, wakaendelea
kwenda, Seidon alianza kuona watu wengi kwa
mbali na baada ya mwendo mrefu kidogo walifika
kwa watu wale na kuwapita taratibu lakini baadae
wakajikuta wamezingirwa na watu kama kumi na
tano hivi, wao wakiwa katikati, Seidon na
Amatagaimba wakapeana migongo na kuwatazama
watu wale kwa zamu.
“Mnakwenda wapi?” mmoja wa wale watu ambaye
alionekana ana rangi ya kijivu aliuliza, si
Amatagaimba wala Seidon aliyejibu swali hilo, akaja
mwingine wa kijani mwili wote mpaka mavazi
aliyevaa, “Hamusikii? Au hamuelewi? Mbona
hamjibu?” kabla hajamaliza kuuliza mwingine
akapita katikati yao na kusimama uso kwa uso na
Sedon, “Lete huo mzigo hapa haraka!”
Amatagaimba alisikia sauti hiyo, akajua kuwa jamaa
hao wamegundua kuwa wao wamebeba nini,
akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari
upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha
Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na
akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka,
kila walipowakata kata na panga zao wale watu
walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa
yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.
Amatagaimba na Seidon walipopata upenyo
wakatimua mbio maana waliona wazi kuwadhibiti
watu wale isingekuwa rahisi, nyuma yao bado kundi
kubwa la watu lilikuwa likiwafuata kwa kasi wakiwa
na silaha mbalimbali. Seidon na Amata walikaza
mwendo kwa kukimbia wakifuata ujia mwembamba
uliokuwa ukiongoza wasikokujua, baada yam bio za
muda mrefu bila ya kusimama, wakafika eneo
ambalo lilikuwa na miamba mingi sana
wakasimama na kujificha, walikuwa wakihema sana,
Seidon alijilaza chali chini katika vumbi,
Amatagaimba akabaki kuchungulia kama hao jamaa
wanakuja, hakuwaona. Akatoka katika lile jiwe na
kujisjika kiuno, “Seidon! Hawapo,” akamwambia
Seidon ambaye muda huo alikuwa amejilaza pale
chini, akajinyanyua na kuketi, atulia kidogo na
kuweka sawa ule mfuko wake ambao ndani yake
kuna lile fuvu, alipoliufungua alibaki akishangaa,
Amatagaimba akamtazama Seidon, “Vipi mbona
umeduwaa?” akamuuliza Seidon.
“Amatagaimba, njoo uone maajabu haya!” Seidon
akamwambia Amatagaimba, akajongea karibu na
ule mfuko, alipotazama ndani alishangaa kuona lile
fuvu liking’aa katika yale matundu ya macho,
“Seidon,” Amatagaimba akaita kwa kunong’ona,
Seidon akamtazama Amatagaimba usoni, “Klakos
wameshapata harufu ya fuvu la Cleopas, sasa wao
ndio watatuongoza katika hisia kulifikisha mahali
pake, lakini bado mitihani mingi inatukabili, hatuna
budi kuivuka, hasa hasa Serhazad, inabidi
tumzunguke” Amatagaimba aliongea. Seidon
akaufunga vyema ule mfuko na wote wawili
wakaanza kutembea polepole kuendelea na safari
yao, wakafika njia panda, sehemu hiyo ilikuwa ni
njia nne zilizotoka kwenye njia moja, wakasimama.
Amatagaimba akaziangalia kwa makini zile njia,
Seidon alibaki amesimama akiwa hajui la kufanya.
Kati ya zile nne, walipoiangalia njia ya kwanza
mbele kabisa wakaona kuna msitu mkubwa ukali
mbali, njia ya pili kulikuwa na maji mengi sana
kama bahari kubwa ing’azwavyo kwa jua la
adhuhuri, njia ya tatu kulikuwa na jangwa kubwa
ambalo ukiangalia tu utaona kitu kama mvuke wa
moto unaowaka juu ya mchanga ule, upepo nao
uliuyumbisha huku na kule, njia ya nne ilikuwa na
milima mikali ya mawe yabisi ambayo ilikuwa ni
ngumu kwa mwanadamu wa kawaida kuyakwea.
“Tunafanyaje?” Seidon akamuuliza Amatagaimba.
Amatagaimba hakuwa na la kujibu kwa wakati ule,
alilitazama jua linalochomoza kwa mbali
likipendezeshwa kwa miale yake murua,
akamtazama Seidon alieonekana kukata tama katika
hali hiyo.
“Lete hilo fuvu ndilo litakalotuongoza njia,”
akamwambia Seidon, akafanya hivyo, akatoa katika
ule mfuko mweusi fuvu la Cleopas akamkabidhi
Amatagaimba. Hatua chache katikati ya zile njia,
Amatagaimba akalishika lile fuvu na kulitazamisha
katika njia moja baada ya nyingine, njia ya tatu, njia
ya jangwa, macho ya lile fuvu yakang’aa, wote
wawili wakatazamana na kutabasamu. Seidon
akalirudisha lile fuvu mfukoni, kisha wakaanza
kutembea kuelekea ile njia ya tatu.
Jua lilizidi kupanda juu, mwendo ukazidi kuwa
mgumu, mchanga ukaishika miguu yao na kuifanya
mizito kama iliyofungwa mawe. Wakiwa katikati ya
jangwa lile, Seidon aligeuka nyuma na kuwaona
watu wane wakija kwa kasi farasi, wakielekea ule
upande ambao wao walikuwepo. Amatagaimba
aliwatazama watu wale akiwa amesimama bila
kufanya lolote, nao wakizidi kukaribi pale
walipokuwepo.
Amatagaimba alisikia mlio wa upanga ukifutwa
kutoka katika ala yake, akamgeukia Seidon,
akamuona ameushika upanga wa makali kuwili
mkononi mwake. “Seidoni, yumkini watu hawa si
wa shari, rudisha upanga wako mahali pake, tusije
tukakosa Baraka za Klakos,” Amatagaimba
alimwambia Seidon. Upanga ukarudishwa mahali
pake na wote wawili wakasimama kwa heri. Wale
watu wane wakawafikia Amatagaimba na Seidon,
watu wale walikuwa wamevaa mavazi tofauti kwa
rangi. Mmoja wao akashuka kutoka katika farasi,
yeye alikuwa amevaa nguo nyeupe zinazometameta,
sura yake haikuonekana sawasawa kutokana na
kinyago alichovaa ambacho mbele badala ya sura
kulionekana kama tundu kubwa jeusi. Akasogea na
kumwasogelea Amatagaimba na Seidon, “Seidon,
Amatagaimba,” aliwaita kwa kuwatazama kwa zamu
kila mmoja kwa wakati wake, “Safari mnayokwenda
ni ndefu sana ijapokuwa mmekaribia pale
muendapo, sikilizeni kwa makini, sisi mnaotuona,
tumetafuta hilo fuvu kwa karne na karne na
hatukulipata ndio maana mwaona mvua hakuna, jua
ni kali na kadhalika, ninyi wanadamu mnatutegemea
sisi daima. Mimi ni Malaika wa Jua, huyo mwenye
vazi la kijani ni Malaika wa Mvua, huyo mwenye vazi
jekundu ni Malaika wa Vita na huyo mwingine
mwenye vazi la kijivu ni Malaika wa ukame na
shida, kila mmoja ana uwezo wa kuleta kile
alichonacho na kukizuia.
Tulipata maono kuwa ninyi mnalo hilo fuvu na mko
mbioni kulirudisha kwa Cleopas, maamuzi mazuri
sana, sasa twaomba tuwasindikize mpaka katika
mlango wa piramidi ambalo Klakos ipo ndani yake
hapo sisi tutasubiri nje na kuwatakia heri kwa hilo
lililo jema kwa wanadamu.”
Amatagaimba akamtazama Seidon na kumpa ishara
ya kuwafuata, kufumba na kufumbua waliona farasi
wao wakija pale walipo, wakashangaa kwa hilo,
walipowafikia, wakawapanda na safari ikaanza,
Amatagaimba na Seidon wakawa katikati na wale
watu wakawa mbele wawili na nyuma wawili, safari
ikaanza.
Baada ya mwendo mrefu juani walifika eneo pana
lenye uwazi mkubwa mno, hakuna kilichoonekana
zaidi ya mchanga na upepo unaovuma ambao
unafanya vumbi la kutisha, “Sisi ni pepo nne za
dunia, hapa tulipo sasa ni katikati ya dunia, nguvu
ya uvutano inatawala eneo hili tulilosimama,”
alisema Yule wa kijani.
“Nasikia vurugu kubwa huko katika dunia ya chini,
ulimwengu unavutana na kuzimu, mbingu zimetulia,”
akasema Yule mwenye guo jekundu. “Basi na
tusisonge mbele, maana hapa tulipo ni mji wa
wafu,” akamalizia Yule mwenye vazi la kijivu.
Wakateremka kutoka juu ya farasi wao na
kusimama chini, juu ya mchanga, wakakutanisha
mikono yao pamoja na kufanya kitu kama mraba.
Amatagaimba na Seidon hawakuelewa
kinachofanyika, wale watu wakatulia kimywa wakiwa
wameinamisha nyuso zao chini, mavazi yao
yalikuwa yakipepezwa kwa upepo mkali uliofanya
vumbi jingi. Mara tai mkubwa alipita kwa kasi
katikati ya Seidon na Amatagaimba, kufumba na
kufumbua Yule tai alikuwa amenyakuwa ule mfuko
mweusi wa Seidon wenye fuvu, Amatagaimba bila
kuchelea alichomoa mshale katika podo lake na
kuuweka kwenye uta wake, akavuta huku akibana
jicho moja na kumlenga Yule tai aliyekuwa akienda
kasi sana, Amatagaimba alijuwa wazi kuwa kama
tai Yule alitoka upande wa kusini basi lazima
atarudi kusini aliufyatua uta wake na ule mshale
ulichomoka kwa kasi ya ajabu, kila aliyeangalia kwa
macho aliona mshale ule kuwa umepigwa upande
tofauti.
“Usimuuuueeeeee!!!!!!” Yule Malaika wa jua alipiga
ukulele na mara ule upepo ukakatika ghafla na
vumbi lote likatulia ardhini kama mwanzo. Wote
nyuso zao zikuwa zikitazama kule juu kwa Yule tai,
mshale ule kama ulivyotumwa, wakati Yule tai
akijigeuza kurudi upande wa kusini alikutana nao na
ukampiga shingoni, miguu yake ikaliachia lile fuvu
likawa likidondoka kwa kasi kurudi ardhini, Seidon
alikwea farasi na kupiga mbio kuelekea kule fuvu
linakodondokea, Amatagaimba alimtazama Yule tai
na badala yake hakumuona tai bali aliona taswira ya
mwanamke ikija kasi kutoka juu kuja kwake, mbele
ya mikono yake kulikuwa na donge kubwa la moto.
“Tufaaaaaaannnnnnnnn” Yule Malaika wa rangi
nyekundu, Malaika wa vita alipiga kelele na wengine
wote wakalala chini katika mchanga, Amatagaimba
aliuchomoa upanga wake na kuuweka barabara,
Yule mwanamke akauzungusha ule moto na
kuuwacha utangulie kabla ya yeye hajafika,
Amatagaimba aliuepa kiufundi na kupiga upnga
wake pigo la kifo lakini Yule mwanamke alipita na
kutua akasimama chini. “Ni nani wewe mwanamke
muovu?” Yule Malaika akauliza, “Sherhazad Malkia
wa Soria,” Yule mwanamke alijtambulisha, kabla
hajamaliza Yule Malaika wa vita akaizungusha
mikono yake kwa namna ya ajabu na kutengeneza
kitu kama moto uliokuwa ukiwaka mbele ya mkono
yake na kuutuma kwa Sharhazad,
lakini kwa nguvu ya kichawi, Sharhazad nae aliuzuia
moto huo katikati, ukawa ukiwaka hewani,
Amatagaimba aliona ile vita haiwezi alisimama
kando, alipowatazama wale wengine aliona bado
wamelala kifudifudi huku vumbi kubwa likitimka
upya eneo hilo, mapigano yalikuwa makali mpaka
ardhi ya eneo lile ilikuwa ikitetemeka, Seidon
alisimama kando ya Amatagaimba akiwa na ule
mfuko mkononi baada ya kuudaka salama, wakati
mapigano hayo yakiendelea asrdhi ilizidi
kutetemeka, radi kali zikapiga na kuchora michoro
ya kutisha angani, mara kipande cha ardhi
kikamegeka na kudidimia, pakabaki uwazi mkubwa
sana, Yule mwenye vazi la kijivu akawatazama na
kuwaamuru kuingia kwa ishara ya mkono. Hakuna
aliyesita, Seidon na Amatagaimba waliingia kwa
kasi kwenye lile shimo wakiacha vumbi likitimka
huko nje kwa jinsi ardhi ile ilivyokuwa ikizidi
kutetemeka, hofu iliwajaa mara giza nene likatawala
mbele yao,
Seidon alipogeuka nyuma hakuona mwanga wan je,
ardhi imejifunga. Amatagaimba akapapasa ukutanai
na kushika kitu kama mti kilichopachikwa katika
kiango, akauchomo na kugundua kilikuwa ni kienge
ambacho kingewasaidia kuona humo ndani,
Amatagaimba akachukua kitu mfano wa kijiti katika
pindo la vazi lake, akakisugua katika nywele zake
kile kijiti kikashika moto, akawasha kile kienge na
mwanga wakutosha ukatokea. Seidon alisikika
akishusha pumzi ndefu, kisha wote wawili
wakaongoza kwenye ujia mrefu ulioonekana
ukielekea mbele zaidi. Huku wakisaidiwa na ule
mwanga kutoka katika kile kienge walitembea kwa
tahadhari kubwa, Seidon alikuwa mbele wakati
Aamatagaimba alikuwa akifuata kwa nyuma.
HAYA MAPAMBANO YANAZIDI.... JE WATAFIKA
SALAMA?
 
....Amatagaimba akachukua kitu mfano wa kijiti
katika pindo la vazi lake, akakisugua katika nywele
zake kile kijiti kikashika moto, akawasha kile kienge
na mwanga wakutosha ukatokea. Seidon alisikika
akishusha pumzi ndefu, kisha wote wawili
wakaongoza kwenye ujia mrefu ulioonekana
ukielekea mbele zaidi. Huku wakisaidiwa na ule
mwanga kutoka katika kile kienge walitembea kwa
tahadhari kubwa, Seidon alikuwa mbele wakati
Aamatagaimba alikuwa akifuata kwa nyuma.
CHAPISHO LA 09
Mchakato wa miguu ya farasi anayekimbia kwa kasi
ilisikika, kwa jinsi ilivyosikika hakuna aliyejua ni
upande gani ilitokea, mbele au nyuma. Mara ghafla
upande wa nyuma waliona moto mkubwa ukija,
wakaanza kutimua mbio kuelekea mbele, walikimbia
na kukimbia lakini bado farasi Yule wa moto
alikuwa akija kasi na akizidi kuwakaribia, “Orion,”
Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia.
Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku
tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon
alizidi kukimbia bila kutazama nyuma.
Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla
hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi
alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.
Baada ya kikumbo hicho kilichomfanya ajibamize
vibaya ukutani, alijikuta anaishiwa na nguvu na
upanga wake asiuone mkononi mwake, haraka
akautoa uta wake na kuchukua mshale ambao
aliupachika na kuuvuta kwa kulenga shabaha kwa
Yule farasi wa moto, alipouachia mshale ule
ulikwenda moja kwa moja ukimuelekea Yule farasi
wa moto ambaye sasa alikuwa sambasamba na
Seidon. Seidon alimshuhudia aliyekuwa juu ya farasi
huyo, akianguka udongoni kwa kishindo na
kusababisha mlipuko mkubwa uliotetemesha pango
lote hilo, mara vumbi na mchanga vilionekana
kutokea katika nafasi zilizomo kati ya jiwe na jiwe.
Amatagaimba aijinyanyua haraka na kukimbilia kule
ambako Seidon naye al;ikuwa ameanguka baada ya
mlipuko ule kumsukuma. Akamshika mkono na
kumvutia kando.
Mchanga ulizidi kumwagika kutoka katika ile
mipenyo na pango zima likawa linatetemeka,
“Amatagaimba, tuondoke hapa si salama,” Seidon
alimwambia Amatagaimba wakati huo yeye akiwa
tayari ameanza kuondoka eneo lile, Amatagaimba
naye akaanza kutimua mbio kumfuata Seidon, ule
moto uliendelea kuwa mkubwa na ukaanza tena
kuwafuata huku mbele yake ukitanguliwa na upepo
mkali sana. Katika kimbia hiyo Seidon aliona katika
ukuta kuna kitu kama kichwa cha farasi lakini
kilichochongwa kawa kutumia jiwe kikiwa
kimejitokeza katika moja ya mawe yale
yaliyopangwa kwa ustadi kufanya lile pango
kuonekana katika hali ile. Seidon alilishika kwa
mikono miwili lile jiwe lenye umbo la kichwa cha
farasi, akafanya kama anabembea, akitumia mikono
yake na kuinyanyua miguu yake, uzito wake ulifanya
lile jiwe kuinama na mara baadhi yam awe yakaaza
kurudi kwa ndani na kutengenea uwazi
mdogomdogo katika kuta hizo. Amatagaimba aliona
mawe ya mbele yake yakifunguka na kufanya kitu
kama mlango,
hakuuliza aliingia na kusimama ghafla kisha
akageuka nyuma na kumchungulia Seidon ambae
alikuwa tayari ameliachia lile jiwe na kukimbili kule
aliko Amatagaimba wakati ule moto nao ulikuwa
umemkaribia sana, kabla hajaufikia ule mlango
tayari moto ulikuwa umemfikia, “Amataaaaaaaaaa
aaaa!!!!!!” alipiga ukulele na kabla Amatagaimba
hajafanya lolote mara ilipiga radi kali sana iliyofanya
mistari ya mwanga wa kutisha ndani ya pango lile,
na ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha, ajabu.
Amatagaimba aliishuhudia mvua ile ikinyesha bila
simile ikitoka tu juu ya pango lile ambalo lilikuwa
limeezekwa kwa mawe kwa ufundi wa hali ya juu,
akanyosha mkono wake na kuushika ule wa Seidon
kisha akamvuta kule alikokuwa yeye, mara ile mvua
ikaacha kunyesha ghafla, na ule moto ulikuwa
umezimika wote, Amatagaimba alitazama na
hakuona farasi wala mtu aliyekuwa na farasi,
‘Orion?!’ alijiuliza huku amejishika kifua, moyo
ukimwenda mbio, akamtazama Seidon aliyekuwa
kajilaza chini akitweta.
“Tuondoke,” Seidon alimwambia Amatagaimba huku
akinyanyuka na kifuata njia hiyo inayopita chini kwa
chini, sasa hawakuwa na kile kienge cha moto kwa
ajili ya kuwaangazia, giaza liliwafunika kama
kawaida, Amatagaimba akakumbuka kitu,
akaufungua ule mfuko uliofungwa mgongoni mwa
Seidon, mfuko wenye fuvu, akalitoa na kukuta
liking’aa katika macho yake na kufanya mwanga
mkali na mweupe kama wa jua la mchana. Mara
baada ya kulito na kupata mwanga huo alianza
kusikia kama kelele za vikaragosi vikishangilia na
kukimbia huku na huko, “Nini hicho?” Seidon
aliuliza. Amatagaimba akatega sikio kusikiliza
akainua mkono wake na kuitazama pete yake ya
ajabu, ndani ya pete hiyo aliona viumbe vya ajabu
vikikimbia huku na huko, vingine havikuwa na
vichwa, vungine vina mguu mmoja, vingine vilikuwa
na shepu isiyoelezeka kimaandishi labda kimichoro.
Amatagaimba akashusha mkono wake chini,
akamtazama Seidon, “Tupo kwenye roho chafu,”
Amatagaimba alimwambia Seidon huku akimzuia
kwa mkono wake maana Seidon alitaka kupita
mbele yake, akamtazama Seidon na kumwambia,
“Hapa lazima tupite kinyumenyume ili hizi roho
chafu zisituone,” wakafanya hivyo, wakapita eneo
lile kinyumenyume, bado waliendelea kusikia
vishindo vya roho hizo zikimbia huku na huku huku
zikipiga kelele kama za panya walionaswa katika
mtego. Baada ya kuvuka eneo hilo wakajikuta
wametokea eneo la wazi kisha kuna ngazi ndefu
inayoshuka chini na huko chini kunafuko moshi kana
kwamba kuna moto uliozimwa muda huohuo,
wakasimama na kuangaza macho yao kule,
“Hamunaptra,” Seidon aliongea kwa kunong’ona. Ni
Amatagaimba tu aliyemsikia, kisha wote wawili
wakaanza kutelemka zile ngazi kwenda kule chini,
walipofika katikati ya waliikuta ile ngazi imeishia
hapo na ule mji waliouona ukali mbali bado,
wakasimama na kushangaa jambo hilo.
Walipokuwa kule juu waliiona ile ngazi imejichoma
katika ule moshi, kumbe ilikuwa imeshia pale.
Amatagaimba akabaki kuduwaa hajui afanye nini,
alipogeuka nyuma alikuta hakuna ile ngazi ila yeye
kasimama juu ya nguzo ndefu ambayo juu yake
kulikuwa na eneo dogo sana la nusu mita ya mraba,
alishindwa afanya nini, alipomtazama Seidon naye
alikuwa katika nguzo nyingine kama hiyo.
Amatagaimba aliangali chini ilikoanzia nguzo ile
hakuona kutokana na kitu kama moshi kutanda
eneo hilo, alichokiona ni urefu mfupi wa nguzo
kama mita moja hivi zaidi ya hapo ni moshi
uliokuwa ukipita kutoka sehemu moja kwenda
nyingine ambao haukuwqaruhusu kuona chini kabisa
zilikoanzia nguzo zile. Sauti za farasi na watu
zilisikika mbali sana kutoka chini.
§§§§§§
“Aaaaaaaaaa ha ha ha ha ha ha ha ha …” ilikuwa
sauti kali ya Sherhazad iliyosikika akiangua kicheko
kikali ambacho kiliwatoa ndege kwenye matundu
yao. Alivuta hatua chache kutoka kiti chake cha enzi
kilichotengenezwa kwa dhahabu safi, akateremka
vijingazi hivyo huku akifuatiwa na vazi lake refu
lililokuwa likimetameta kwa jinsi lilivyoundwa, kwa
maana halikushonwa.
Chini katika sakafu ya jumba hilo la kifahari
kulikuwa na wazee wanne waliolala kifudifudi
kuonesha heshima kwa Malkia huyo wa Soria.
“Inukeni enyi wazee wangu,” aliwaamsha nao
wakaamka. Akawatazama mmoja mmoja kisha
akaangalia kule kwenye dirisha lake la kichawi na
kuwaona Amatagaimba na Seido wakiwa bado
katika zile nguzo, akacheka tena cheko lake la
ajabu.
“Asanteni sana kwa kazi mliyoifanya ya kuwatega
wale wajinga pale, sasa tunakwenda kuwamalizia
palepale kwani hawana uwezo wa kukimbia,”
aliposema hayo akatoa vazi lake alilojifunga
shingoni na kuonesha jeraha lake kubwa, “Hapa ni
upanga wa Amatagaimba umepita, lazima moyo
wake niutafune nyama, twendeni,” Sharhazad
akaamuru. “Sikiliza ee jirani sana na mwezi kwa
sasa, hivyo mpaka yapite majua mawili,” alisema
mmoja wa wale wazee, kisha mwingine naye
akafungua kinywa chake akasema, “Tazama ee
Malkia, Amatagaimba, shujaa wa msitu wa Solondo
ana pete ya ajabu aliyopewa na Malkia Baghoza wa
msitu wakati alipoweza kuurudisha utawala wake
kwa kumuangamiza Kelume, akiwa na pete ile
kamwe hatutaweza kumshinda, isipokuwa tunaweza
kupotea sisi wote, na utwala wako ukaanguka
vibaya,”
Yule mzee aliposema hayo Malikia Sherhazad
alikunja sura yake na alionekana wazi hasira kumjaa
kichwani mwake, radi kali zilipiga na kupasua anga,
wale wazee wakaanguka kifudifudi, “Si hivyo ee
Malkia, bali tahadhari ni muhimu kuliko hatari,”
walisema wote kwa sauti moja. “Ninyi mnajua wazi
kuwa tukilipata lile fuvu, sisi ndiyo tutakuwa na sauti
juu ya ulimwengu wote wa majini, wale pale
wameshafika Hamunaptra na tukiwakosa wakiingia
katika pyramid kubwa, chini ya ardhi basi
hatutawaweza tena,” Sherhazad aliwaeleza wale
wazee, “Na sasa nataka niiteketeze hiyo pete ya
Baghoza kwa moto wa ajabu kabla hatujaenda
pale,” akaongeza kusema huku mikono yake ikiwa
imeshikishwa kiunoni. Akautoa mkono wa ke wa
kushoto na kuongea lugha ya ajabu lugha
isiyoeleweka, macho yake yakageuka na kuwa
mekundu kama makaa ya moto, ulimi wake ulikuwa
kama muale wa moto unaowaka kwa nguvu,
Sherhazad alipandisha sauti na kuwa makelele
mengi ndani ya jumba lile kisha akatema donge
kubwa la moto lililopita katika lile dirisha la ajabu
na kupotelea milimani. Wale wazee waliinuka na
kutazama pambano hilo litakalotokea huko katika
mji wa Hamunaptra.
§§§§§
AMATAGAIMBA akiwa pale juu ya nguzo bado
alikuwa hajui la kufanya kwa kuwa hakuwa anajua
urefu kwenda chini, kila alipoangalia bado ni
mawingu au ukungu ulimnyima uhuru wa kuona
chini. Akiwa katika kutazama hilo alisikia sauti ya
Seidon ikimpa tahadhari kuwa kuna kitu kama jiwe
kikimjia kwa kasi, Amatagaimba aligeuka na kuona
ile dhahama inayokuja, akashindwa afanye nini,
alishangaa badala ya jiwe sasa liligeuka kuwa
donge la moto, Amatagaimba akafikiri haraka na
kujiweka tayari kuukinga moto ule, ulipofika akaepa
ukapita pembeni lakini alishangaa moto ule ulikuwa
ukija mkononi mwake, akagundua baadae kuwa ni
pete inayotafutwa, akainua mkono akaibusu na
kisha akanyoosha ule mkono wenye pete na
kuusukuma kwa kasi ule moto kurudi ulikotoka,
kitendo kile kilimfanya kuyumba na kudondoka
kutoka pale aliposimama, alijitahidi asidondoke
lakini haikuwa hivyo, alidondoka ila katika kujikinga
akatanguliza mguu mmoja cha kushangaza
hakudondoka badala yake mguu ule ulikanyaga
ardhi umbali wa nusu mita tu kutoka pale
aliposimama.
“Shiiit,” alitoa sauti hiyo na kumwambia Seidon
ashuke kutoka pale alipo kuwa hakuna shimo eneo
lile, Seidon akaruka na kutua chini kisha wakatimua
mbio kushuka poromoko lile kuelekea chini,
wakaingia kwenye pango kubwa. Amatagaimba
alipogeuka nyuma hakuona ule moto, wakendelea
kusonga mbele na walipoibuka upande wa pili,
waliona mapyramid mengi sana yaliyojipanga katika
mtindo mzuri.
“Sasa tupo Hamunaptra, inabidi tutafute pyramid la
kale kuliko yote, humo ndimo tutapata Clakos,”
Amatagaimba alisema hayo huku akiwa kasimama
akiangalia yale mapiramidi, Seidon alikuwa nyuma
yake tu nae akiuangalia mji huo. Akikumbuka jinsi
alivyofika kwa mara ya kwanza kwa shida kuchukua
fuvu lile. Wote wawili wakaendelea kutembea kwa
kupita njia zinazowaficha ili watu wenye nia mbaya
wasiwaone na kuwadhuru, lakini bado watu
walikuwa wakiwakodolea macho kila hatua
wanayopiga. Baada ya mwendo kidogo walikutana
na mzee mmoja wa makamo, aliyevaa guo refu na
kufunika kichwa chake, alionekana uso tu, uso wake
ulikuwa ni kama wa kijivu hivi.
“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa
hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na
nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia,
Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha
wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja
naye. Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi
moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka
vipande, lilionekana ni la kale kuliko yote.
Wakaingia ndani, chumba kilikuwa na giza lakini
mishumaa ilijitahidi kulishinda giza hilo, Seidon
akiwa na mfuko wake barabara mkononi mwake na
upanga wa Vernadi kiunoni mwake, alikuwa akifuata
kwa makini kila apitapo mzee Yule, Amatagaimba
naye vivyo hivyo, yeye alikuwa nyuma kabisa
akiwaacha Seidon katikati na Yule mzee mbele yao.
Joto kali lilitawala katika piramidi lile, joto
lililotokana na wingi wa mishumaa iliyojazwa katika
vitu kama ngazi nyingi zilizozunguka katika piramidi
hilo. Baada ya mwendo kidogo, Yule mzee
akawanyooshea mkono kuwapa ishara ya
kusimama, nao wakatii na kusimama. Hakuna
kilichoendelea kati yao isipokuwa joto lililowafanya
kulowa kama wamepita kwenye mvua.
“Joto kali, kwa nini msizime mishumaa hii?” Seidon
akauliza. Yule mzee akatulia bila kujibu kisha
akageuka kumtazama.
“Dunia yenu haiwezi kuwapa uhai ninyi bila
mishumaa hii, endapo itazimika piramidi hili
litajifunga nikimaanisha pande nne za piramidi hili
ndizo pepo nne za dunia, hapa ndipo penye majira
ya mwaka, panapogawa miezi, siku na miaka, ndipo
panapofanya jua liwake, mvua inyeshe, hapa ndipo
penye kila kitu, ukitaka kwenda mwaka 2000
unaweza, ukitaka kuona yatakayotokea kesho na
miaka mia nne ijayo hapa ndio mahali pake, kwa
kifupi niwaambie kuwa hapa ndipo katikati ya dunia,
kitu chochote chenye madini ya chuma hakiwezi
kuanguka chini wala kutoka mahali kilipo,”
Yule mzee akamjibu Seidon, kwa Seidon na
Amatagaimbailikuwa kama simulizi ya kusadikika
hakuna aliyeamini ukweli wa maneno hayo,
wakatazamana kwa mara nyingine tena na kisha kila
mmoja akacheka peke yake moyoni. Amatagaimba
akaushika upanga wake na kujaribu kuuchomoa
kutoka katika ala yake lakini upanga ule
uling’ang’ania katika ala, haukutoka, Amatagaimba
alijaribu tena na tena lakini hali ilikuwa ileile,
akamwambia Seidon ajaribu naye kuutoa wa kwake
lakini hakuna aliyeweza.
“Ina maana hamuniamini ninachowaambia?” Yule
mzee aliuliza, “Sikieni ninyi wanadamu, katika dunia
ya sasa huu sio mwaka mnaouishi, sasa mnaishi
katika dunia ya kale, kama hamtakuwa na imani
basi mjue safari yenu hamtofika kwa maana ili
mfike Hamunaptra, mji wa wafu, mji uliopotea
ambao upo chini kabisa ya ardhi lazima mvuke
daraja la pepo, daraja ambalo lazima ufunge
milango yako yote ya fahamu ndipo uweze kuvuka
ukishindwa utatumbukia katika shimo kubwa
ambalo kwenu duniani mnaliita kuzimu huku linaitwa
bonde la uvuli wa mauti,” maneno hayo ya Yule
mzee yaliwafanya Amatagaimba na Seidon kuingiwa
na hofu kuu.
“Mbona hatuendelei mbele?” Amatagaimba
akauliza.
“Ha ha ha ha haaaa!!!!” sauti ya kicheko cha kutisha
kutoka kwa Yule mzee ikatawala mle ndani na
kufanya mwangwi wa kutisha, “Hatuwezi kupita
hapa sasa kwa sababu dunia hivi sasa inapishana
na sayari ya Venus kwa upande huu wa Mashariki,
hivyo kuna tetemeko kubwa la ardhi hatuwezi
kuvuka,” Yule mzee aliwaeleza. Baada ya dakika
chache waliona kitu kama vumbi kikipukutika
kutoka katika kona za piramidi hilo, Amatagaimba
akataka kufumba macho ili kuepuka vumbi hilo
lakini alikatazwa na Yule mzee, akaambiwa kuwa
ndani ya piramidi hilo hutakiwi kufumba macho hata
mara moja. Ikabidi wote watulie hivyohivyo mpaka
dhoruba ya tetemeko na vumbi ilipopita.
“Sasa tunaweza kwenda, kulikabili daraja la pepo,
tukifika eneo linaloitwa milima mitano itabidi
kufanya ibada ya kufunga milango ya fahamu ili
kuvuka daraja hilo, hapo hapahitaji utani hata
kidogo,” Yule mzee aliwaasa kisha wakaendelea na
safari.
WATAVUKA? TUONANE KESHO
 
Baada ya dakika chache waliona kitu kama vumbi
kikipukutika kutoka katika kona za piramidi hilo,
Amatagaimba akataka kufumba macho ili kuepuka
vumbi hilo lakini alikatazwa na Yule mzee,
akaambiwa kuwa ndani ya piramidi hilo hutakiwi
kufumba macho hata mara moja. Ikabidi wote
watulie hivyohivyo mpaka dhoruba ya tetemeko na
vumbi ilipopita.
“Sasa tunaweza kwenda, kulikabili daraja la pepo,
tukifika eneo linaloitwa milima mitano itabidi
kufanya ibada ya kufunga milango ya fahamu ili
kuvuka daraja hilo, hapo hapahitaji utani hata
kidogo,” Yule mzee aliwaasa kisha wakaendelea na
safari.
CHAPISHO LA 10
Giza lilikuwa nene, kati yao kulikuwa na wadudu
wengi wa vimulimuli ambao walifanya nuru ya
kupendeza, walitembea polepole wakimfuata Yule
mzee aliyekuwa akiwaongoza njia. Mbele kidogo
wakasikia sauti kama ya maji yanayopita mbali
katika maporomoko makubwa. Amatagaimba
akasimama na kugeuka huku na kule, ndani ya mlio
huo wa maji alikuwa akisikia mlio wa farasi na
mvumo kama upepo mkali. Yule mzee nae
akasimama, akaonesha ishara tena ya mkono kisha
wote wakasimama.
“Orion!” Yule mzee akasema kwa sauti ya taratibu,
Amatagaimba akaushika upanga wake tayari kwa
pambano lakini hali ilikuwa ni ileile, upanga
haukutoka katika ala yake. Amatagaimba hakuwa na
ujanja, Seidon naye alijaribu lakini haikuwezekana,
“Tupo katikati ya usumaku wa dunia, hakuna kitu
cha chuma kinachoweza kufanya lolote hapa,” Yule
mzee aliwaambia. Kisha akawapa ishara ya
kuondoka na kuongeza mwendo.
§§§§§
ORION alijua wazi kuwa hapo katika daraja la pepo
ndipo pa kuweza kutimiza azma yake kwani
alielewa wazi kuwa hakuna silaha ya chuma
itakayotumika. Orion alipiga mbio na farasi wake
kulikabili lile daraja.
“Ongeza mwendo Orion anatukaribia,” Yule mzee
aliwahimiza akina Seidon ambao walikuwa
wakitembea kwa tahadhari kwani giza lilikuwa nene
mno. Amatagaimba akajipapasa na kujikuta akiwa
na kamba kiunoni mwake, akafikiri jinsi ambavyo
ataitumia kamba hiyo kuwa silaha dhidi ya Orion
mwindaji mashuhuri wa enzi na enzi mwenye
shabaha isiyokosa hata mara moja.
Seidon na Amatagaimba walikuwa wakionekana
wazi kwa macho ya ajabu ya mwindaji huyo
aliyepewa kazi maalum na wachawi wa Misri
kuhakikisha analipata fuvu la Cleopas. Akainua uta
wake mkubwa wenye nguvu alioamini kuwa kwa
kasi ambayo mshale huo utachomoka katika uta
wake lazima utapasua nguvu za usumaku na
kumfikia Seidon ambaye alikuwa nyuma tu ya Yule
mzee.
Akauvuta kwa nguvu zake zote huku misuli ya
mikono yake mikakamavu ikiwa imedinda na
kufanya nyama ya mikono hiyo kuwa ngumu ajabu.
Ilikuwa bado hatua chache sana Amatagaimba na
Seidon kumaliza ule ukanda wa usumaku wa dunia,
ila Yule mzee tayari alikuwa amepita eneo lile.
Mshale wa Orion ukaja kwa kasi ya ajabu mvumo
wake ukawastua wote, ulikuwa ni kama mruzi
upigwao. Kutahamaki Yule mzee alipigwa kichwani
na ule mshale wa Orion, mshale wa kichawi,
ukamtawanya kichwa chote na kisha kiwiliwili chake
kubaki kimesimama vilevile. Seidon aliuona mshale
ule ukimjia usoni, akatamani kupiga kelele lakini
akajikuta akishindwa, akashangaa mshale ule
ukisimama sentimeta chache kutoka usoni kwake,
ukaganda kama igandavyo barafu ndanin ya jokofu,
Seidon akashusha pumzi ndefu na kujaribu kuushika
ule mshale.
“Acha!,” Amatagaimba akamwambia Seidon,
“Mshale huo umenasa katika nguvu za usumaku,”
Seidon akaelewa kwa nini, akakumbuka Yule mzee
alivyowaambia kuwa hakuna kitu cha chuma
kinachoweza kufanya lolote katika eneo lile.
Wakavuka na kufika eneo la pili eneo la milima
mitano. Mbalamwezi ya kung’aa iling’aza eneo hilo
lote na vilima vile vilionekana wazi umbali mfupi tu
mbele yao, lakini hawakujua ni wapi watapita, Yule
mzee tayari alikuwa hana kichwa na aliganda
palepale kama nguzo. Mbele ya milima ile kulikuwa
na giza linguine nene lisilo hata na vimulimuli,
katikati ya giza hilo kulikuwa na kitu kama ujia
mdogo uliokuwa uking’aa sana, daraja la pepo.
Wawili hao wakatulia kwanza na kutafakari, wakiwa
kimya kabisa, mara wakasikia mvuma mkali wa
mbawa za ndege mkubwa.
“Pelargonis,” Amatagaimba akaongea taratibu.
“Umesemaje?” Seidon akauliza, kabla Amatagaiba
hajajibu alijikuta kapigwa na ubawa mkubwa wenye
nguvu wa ndege huyo na kuanguka mbali, Yule
ndege akataka kunyakuwa ule mfuko wa Seidon,
lakini Seidon naye hakukubali, mara hii alipoufuta
upanga wake ukatoka ndani ya ala, akaushika kwa
mikono yake miwili na kuanza kupambana na ndege
huyo mkubwa.
Amatagaimba alijaribu kuinuka, na alipofanikiwa
tayari idadi ya ndege wale iliongezeka na kumfanya
Seidon kuelemea nao. Amatagaimba akautoa uta
wake mgongoni na kuchukua mshale katika podo
lake, shabaha yake haikuwa haba, kila mshale
mmoja ulikuwa ukiangusha ndege mmoja. Yule
ndege aliyeonekana kama ndio mama yao akaona
wenzake wanavyopukutika, akamuacha Seidon
akipambana na wengine yeye akamjia
Amatagaimba, shabaha yam shale wa Amatagaima
ilikielekea kichwa cha ndege Yule, lakini hakuamini
kilichotokea, Yule ndege akaudaka mshale ule kwa
midomo yake mirefu na kuuvunja. Amatagaimba
akatoa kamba iliyokuwa kiunoni mwake na kuanza
kumkabili ndege huyo wa kutisha. Aliizungusha ile
kamba kwa ustadi mkubwa na alipoiachia Yule
ndege alishuka chini zaidi na ile kamba ikapita juu,
Amatagaimba alijirusha upande mwingine na
shambulizi la ndege huyo likakosa lengo.
Seidon kwa kutumia upanga wake aliweza kukata
ndege wengi sana lakini alikuwa amechoka sana
nab ado pambano lilikuwa likiendelea.
Amatagaimba akiwa chini alikuwa hana ujanja
mwingine Yule ndege alikuwa akija tena huku
kapanua domo lake tayari kumdonyoa, akili ilikuja
mara moja, kulikuwa na jiwe pembeni akaliinua na
kulirusha, likatua sawia ndani ya domo la ndege
huyo, likamkwama kooni, akaanguka na
kujirusharusha huku nakule, Amatagaimba
akachukua nafasi hiyo akauchomoa upanga wake na
kumkata kichwa. Alipohakikisha kiumbe huyo
amekwisha, ndipo alipomtazama Seidoni aliyekuwa
bado akipambana na ndege hao. Kwa kutumia
upinde na mshale wake aliweza kuwapiga ndege
wote na kumkamata mmoja kwa kutumia ile
kamba. Walimfunga barabara, alikuwa ndege
mkubwa sana na wa kutisha ambaye hakuwahi
kuishi wakati wetu huu, wote wawili walitweta
wakiwa na kiu cha ajabu lakini hawakuwa na hata
tone la maji.
“Amatagaimba, tutavukaje daraja la pepo ilhali
aliyekuwa akituongoza amekufa?” Seidon akauliza.
“Swali gumu Seidon, tazama daraja lilivyo refu, na
halina ukingo katika pande zake,” Amatagaimba
alionesha mashaka katika hilo.
“Na hapa si salama kwetu, itakuwaje kama Orion
atatukuta hapa?” Seidon akauliza. Amatagaimba
hakujibu neno, akainua mkono wake na na kuigonga
kwa kwenzi mara tatu ile pete yake. Mara mbele
yake pakatokea moshi mikubwa mno, Amatagaimba
akatulia akiutazama na katikati yake alionekana
Bagoza, bibi jinni wa Solondo, akiwa kazungukwa na
upepo mkali uliochanganyika na ndimi za moto.
“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini
jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba,
nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana,
nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo
nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa
kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya
kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la
Hamunaptra, ukishafika katika mlango huo, ingia
bila woga, ijapokuwa Hamunaptra ni mji wa wafu,
usiogope ndani yake kuna mji mkubwa sana ambao
katikati ya mji huo kuna Clakos chini ya ardhi. Sasa
shikeni njia mpita Mashariki kuzunguka milima
mitano, baada ya majua mawili tu mtakuwa
mmefika Hamunaptra, yeyote mtakayekutana naye
njiani msiongee naye wala msimpa mkono, katikati
ya njia mtapata shida kwa maana lazima mpitie mji
mmoja katikati yake lakini mtavuka tu,” Baghoza
alimueleza Amatagaimba.
“Ewe baghoza malkia wa majinni, tunamhofia Orion
na Sharhazad, je tutafika?” Amatagaimba aliuliza
kwa mashaka huku akiwa ameinamisha kichwa
chake chini.
Baghoza akaizungusha fimbo yake katika pepo zote
nne, kisha akamgeukia Amatagaimba.
“Orion haonekani, Sharhazad haweze kuwashambulia
hapa kwani nayeye hawezi kuvuka daraja la pepo,
nendeni msichelewe, jua la tatu litapatwa na mwezi,
huo ni wakati mbaya sana kwetu, je vipi kuhusu
ninyi?” mara ule upepo ukaongezeka, vumbi
likatimka na baghoza akatoweka mbele ya
Amatagaimba. Aamatagaimba akaitazama pete
yake, kisha akainuka kutoka pale alipokuwa
amepiga magoti.
“Amatagaimba umekiona kimbunga cha ajabu?”
Seidon akauliza.
“Je wewe uliniona wakati wa kimbunga hicho?”
Amatagaimba akamwuliza Sedon.
“Hapana,” Seidon akijibu kwa woga.
“Hakikuwa kimbunga, ila mimi nilikuwa ndani yake,
Seidon, sasa twende hatua ya mwisho ya safari
yetu,” Amatagaimba alipokuwa akisema hayo, mara
matone ya mvua yakaanza kuwatonesha, Seidon
aliachama kinywa chake na kuruhusu matone
kadhaa yaingie ndani yake, kiu yake ikakatika na
nguvu zikamrejea tena. Kisha wote wawili
wakashika njia kuielekea milima mitano, Seidon
alikuwa mbele na mfuko wake mweusi wenye fuvu
ndani yake, Amatagaimba alikuwa nyuma yake,
hakuna aliyeongea kila mmoja alikuwa akifikiri juu
ya safari hiyo ya hatari.
Jua lilipokuwa likizama Amatagaimba alikuwa
amechoka bila kificho.
“Tupumzike hapa na tupate chakula,” Amatagaimba
akamwambia Seidon, wakaingia katika moja ya
mapango yam awe yaliyokuwa eneo hilo na kuketi
wakiangazwa kwa mbala mwezi. Seidon akafanya
moto wa kuota maana baridi ilikuwa kali,
wakatafuna masurufu waliyokuwa wamebeba, na
wote wakapata usingizi.
§§§§§
Usiku wa manane, Amatagaimba na Seidon wakiwa
wamelala katika pango hilo. Orion akiwa juu ya
farasi wake mkubwa alivuta harufu na kuhisi kuna
wageni pande hizo. Akamuongoza farasi wake
kuelekea milima mitano ambako alipata hisia juu ya
watu hao.
Upepo uliendelea kuvuma na kuufanya ule moto
waliokuwa amekoka Seidon kuongezeka na kufanya
joto kali ndani ya pango lile. Orion alifika na
kusimama mbali, kila alipojaribu kuvuta harufu ile
aliyoisikia mwanzo hakuipata badala yake joto kali
la moto lilipenya pua zake na kumuumiza mapafu
yake, akarudi nyuma zaidi na kusimama, hakuna
ujanja.
KATIKA MJI WA SORIA
NDANI ya kasri kubwa la Shrhazad, kulikuwa na
watu walewale, wazee wa kichawi waliojaribu
kuisitisha safari ya Amatagaimba na Seidon
wakashindwa. Sasa walikuwa wakisubiri muda ufike
ili kupambana upya.
“Sikilizeni enyi wachawi wa Soria, Seidon na
mwenzake wapo katika mapango ya Oregon, jirani
kabisa na mji mtukufu wa Hamunaptra, lazima
watavuka nchi ya Sharidan katika kijito cha Usoil,
sasa na tuwasubiri pale kijitoni, mara hii tusikubali
kabisa kulikosa lile fuvu maana ile ni neema ya
Clakos, tukilipata tutaitawala dunia yote na itakuwa
chini ya neno letu,” Sharhazad aliwaambia wachawi
wake huku akitoka katika dirisha lake la ajabu.
Akakiendea kiti chake cha enzi, kiti kilichotengenez
wa kwa dhahabu safi na kung’azwa kwa moto mkali
wa kuyeyushia chuma, vazi lake refu jeupe lenye
mkia mrefu lilimfanya Malkia huyu kuonekana
mkubwa kupita kiasi lakini alikuwa na mwili mdogo
isipokuwa alikuwa na nguvu sana dhidi ya maadui
wake, kila tawala iloimuogopa Sharhazad kwani
alikuwa na uwezo wa kukugeuza chochote
anachokitaka na usimzuie. Akakei juu ya kiti chake,
na wale wazee wachawi wakainama mpaka chini
kumpa heshima yake, kisha wakainuka na kuketi
kwa kutumia magoti yao ilhali miguu yuao
wameikunja kwa nyuma.
“Tufanyeje tuwaangamize wale watu?” akauliza
Sherhazad.
“Mtukufu malkia, pete ya Amatagaimba ndiyo pekee
inayotukwamisha kukamilisha ulilotutuma, ni lazima
kwanza tuikamate pete ile kisha kazi inayobaki ni
ndogo sana, kumbuka wakifika tu kwenye mstari wa
Ikweta kamwe hatutawaweza tena kwani pale tayari
Clakos itaona fuvu lake na nguvu za ajabu zitakuwa
juu yao, tutafanya nini ee Malkia?” mchawi mmoja
kati ya wale waliokuwepo pale akajibu huku
akitetemeka kwa woga.
“Kwa nini u muoga sana wewe? Kwa nini unaonesha
kukata tama wakati tama yenyewe imeijaza mioyo
yetu sote, nitakupeleka kwenye ulimwengu wa
wadudu watambaao kwa jinsi zao mara moja
endapo utaonesha udhaifu wako tena,” maneno
makali ya Sharhazad yaliyokuwa yakimtoka kinywani
huku yakisindikizwa kwa radi kali yaliwafanya wazee
wote wainame tena kumpa heshima Malikia.
NINI KITAENDELEA?
 
“Kwa nini u muoga sana wewe? Kwa nini unaonesha
kukata tama wakati tama yenyewe imeijaza mioyo
yetu sote, nitakupeleka kwenye ulimwengu wa
wadudu watambaao kwa jinsi zao mara moja
endapo utaonesha udhaifu wako tena,” maneno
makali ya Sharhazad yaliyokuwa yakimtoka kinywani
huku yakisindikizwa kwa radi kali yaliwafanya wazee
wote wainame tena kumpa heshima Malikia.
CHAPISHO LA 11
“Ee malkia wa Soari uishi milele!!!” wote walisema
maneno hayo.
“Fusha mafusho, ili majinni yote yakusanyike,”
Sharhazad akatamka. Mchawi mmoja wapo
akachuku kitu kama kibuyu kikubwa, akatia ubani
mwingi na vitu vingine kama amdalasini, akasema
maneno ya ajabu katika lugha ya kicawai lugha yao
wanayoielewa wao wenyewe, mara moshi mzito
ukaanza kutoka kwenye kile kibuyu, harufu izuri ya
udi, ubani na manukato ya ajabu yalilijaza lila kasri
zima. Sauti za watu wengi zikaanza kusikika kama
watu wanaobadilishana mawazo ya jambo Fulani.
Kishindo cha kofi kali kikasikika, ukimya mkuu
ukatawala, Sherhazad sasa likuwa kabadilika sura
yake na kuwa Joka kubwa lenye vichwa vitatu,
likiwa pale juu ya kiti, likanyoosha shingo yake huku
na kule. Kisha likafungua kinywa chake na kuanza
kuanza kunena kwa lugha yao.
“Umefika wakati wa kuitawala dunia na pepo zake
zote nne, viumbe yabisi na viumbe hewa vyote view
chini ya mamlaka ya Soria, nyote mnajua kwa karne
nyingi tumekuwa tukilitafuta fuvu la Cleopas ili
kupata neema za Clakos zenye wingi wa mamlaka
juu na chini ya mbingu, viumbe wawili wanalirudisha
fuvu hilo kwa Cleopas, na wamebakisha jua moja tu
kufikia lango la Hamunaptra, nimewaita ili sasa sisi
sote tuweze kufanya kila hila tulipate fuvu hilo kabla
hawajaingia nalo ndani ya Hamunaptra, mimi na
wengine wachache tutawasubiri katika kijito cha
Usoil, lakini nataka ninyi mutangulie mbele kufanya
hila ya kuwazubaisha,” Sharhazad aliongea na
viumbe wake kwa sauti ambayo wewe mwanadamu
wa kawaida ungesiki milio ya ajabu ajabu tu
ikimtoka nyoka huyo.
“Ewe malkia mtukufu, sote tuko hapa kulinda na
kuhakikisha utawala wako wenye nguvu hauanguki,
yumkini hawa ni nani? Viumbe dhaifu vya dunia ya
kesho hata vituzuie sisi ambao tuna nguvu,
mamlaka na enzi kuikamilisha kazi yetu?
Tunakuahidi kutekeleza na kuitawala dunia, kwa
kuwa wale ni nyama na mifupa tutawapiga kwa
magonjwa nao hawatakuwa na uwezo tena,” mmoja
wale waliokuja pale aliongea.
“Aaaaaah! Wewe bado ni mchanga sana kati ya
wachanga, kumbuka katika mbingu hii magonjwa
hayana nafasi, sisi tunaweza kuwapiga kwa
magonjwa wakiwa kwao duniani, lakini katika
ulimwengu huu wa jinni ya jinnu hakuna hewa
inayotembea hivyo magonjwa hayawezi, lakini
tumieni sura na maumbo yenu ya kuazima ili
kuwatia udhaifu wale,” Sharhazad akatoa maelekezo
kwa viumbe wake, kisha kwa kupitia dirisha lake la
ajabu akawaonesha Amatagaimba na Seidon mahali
walipo. Lakini jambo moja liliwashtua wote waliomo
katika kasri lile. Walimuona Orion akiwa kasimama
juu ya farasi wake mweupe, farasi anayeweza
kuchomoa mbawa na kuruka kama ndege wa
kawaida ‘pegasus’. Sherhazad alijawa na hofu.
“Na huyu ni kikwazo kingine,” akawaambia.
“Ewe Malikia mtukufu wa Soria, Orion ametumwa na
wachawi wa Misri ili apate fuvu lile na kuwapeleka
kisha wao watampa maji ya uzima ambayo kwayo
kamwe hatoweza kufika katika miisho ya maisha
yake,” mwingine akasema na kumwambia
Sharhazad, akahamaki kwa jibu hilo.
“Na tumuweke katika jalada la maangamizi kabla ya
jua la mashariki ijayo,” Sharhazad akawaagiza na
kisha moshi ule wa mafusho ukakatika ghafla, kasri
likabaki tupu, kitini alikuwa yuleyule mwanamke
mrembo, Sharhazadi, sasa katika umbo lake zuri la
kibinadamu lakini alikuwa amelowa jasho mwili
mzima.
§§§§§
“Seidon,” Amatagaimba alimwamsha Seidon, kisha
wakajiandaa kwa safari, mbalamwezi ilikuwa ikitoa
mwanga wake murua na kufanya vilele vya milima
ile mitano kuonekana kama mtu aliyevaa kanzu
nyeupe. Walipohakikisha kila kitu kipo salama
wakaanza safari ya kumaliza ngwe hiyo. Wakiwa
njiani, nyuma yao walisikia kwato za farasi
akimbiaye, kabl;a hajatahamaki mfuko wa seidon
ambao ndani yake kulikuwa na lile fuvu,
ukanyakuliwa na Orion kisha Yule farasi akafungua
mbawa zake na kuanza kuiacha ardhi, Amatagaimba
alimshuhudia Seidon naye akinyanyuliwa kwani
mfuko huo ulifungwa barabara kiunoni mwake.
Amatagaimba akauchomoa uta wake na kuuweka
mshale wake utani, akavuta huku akibana meno kwa
hasira na uchungu, akauachia uta huo nao ukasafiri
kwa kasi. Amatagaimba akashuhudia farasi Yule
akidondoka tena ardhini pamoja na Orion aliyekuwa
juu yake. Vumbi kubwa likatimka, lile fuvu
ilikachomoka kutoka kwenye ule mfuko,
Amatagaimba na upanga mkononi akafika eneo lile,
alipiga upanga lakini Orion akaupangua kwa wake,
akauvuta na kupiga pigo linguine, Orion akaupangua
kwa ustadi zaidi. Mara pigo la upanga la Orion
liliikosa shingo ya Amatagaimba padogo sana,
akaepa na kudondoka chale katika mchanga. Oriona
akawa anakuja kwa kasi na upanga wake wa
makalikuwili uliokuwa uking’aa sana mkononi
mwake, akaruka kwa nguvu zake na kuelekea kutua
juu ya Amatagaimba. Kwa haraka akauvhomoa
upanga wake na kuukinga ncha yake ikatazama juu.
Amatagaimba aliliona jitu la kutisha lililoachama
domo lake ambalo lilikuwa likitoka joka kubwa,
Amatagaimba akajawa na woga lakini hakuondoka,
alifumba macho na kutulia. Upanga wa
Amatagaimba ukapita katikati ya kifua kikavu
kisicho na damu cha Orion, akalitupia pembeni jitu
hilo, kisha akasimama na kuuchomoa upanga wa
Orion mikononi mwake akakata shingo yake, Orion
akaanza kuyeyuka na kupukutika kama kuwa vumbi.
Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile
lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla
hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia
mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha
lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe
jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya
vumbi. Seidon aliinama na kuokota fuvu hilo kisha
akalitia katika mfuko ule na kujifunga tena vizuri
kabisa. akamsaidia na Amatagaimba kutembea kwa
maana misuli ya mguu wake ilishtuka katika anguko
lile. Orion hakuonekana tena, lakini hakuna
aliyeamini kuwa kiumbe huyo kaisha waliona ni
muujiza au kiini macho tu.
Wakiwa njiani kwa mwendo wa taratibu, mara
kimbunga kikali kiwatokea mbele yao, vumbi na
upepo wa kisulisuli ukawatenganisha wawili hawa,
Seidon alikuwa mbele na Amatagaimba alikuwa
nyuma, katikati yao palikuwa na vumbu jingi na
upepo mkali.
“Tupatie hilo fuvu, haraka!” sauti kali ya kike
ilimwambia Seidon.
“Hilo haliwezekani,” Seidon alikataa huku akiufuta
upanga wake na kuukamata kwa nguvu kwa mikono
yake miwili. Sauti kali ya muungurumo kama wa
radi ikatawala pande zote. Seidon akiwa tayari
kajiandaa kwa lolote, mara kwa mbali aliona vumbi
jingine likitimka lakini hili lilikuwa dogo tu, kutoka
katika vumbi lile alimuona mtu aliyepanda farasi
akija kwa kasi sana upande wake. Mara utulivu
mkubwa ukatawala eneo lile, akageuka nyuma.
“Amatagaimbaaaaa!!!!!” aliita bna kuita, lakini
hakumuona Amatagaimba wala hakusikia sauti ya
kuitika kwake. Walikuwa wametenganishwa katika
njia ya kutatanisha. Seidon aliushusha upanga wake
na kuupachika alani mwake. Msichana mrembo
mwenye nywele ndefu kichwani mwake alisimama
mbele ya Seidon akiwa juu ya farasi. Akamtazama
Seidon kisha akateremka juu ya farasi huyo, alipotua
chini katika ardhi, Seidon alihisi kama ardhi
ikitikisika hivi, kisha ikatulia. Yule msichana
akatabasamu, alijua kosa alilolifanya ambalo
lingemgharimu baadae.
“Ewe kiumbe wa dunia? Ni wapi uendako hata
udiriki kuvuka katika nchi hii isiyo yako?” Yule
msichana akmuuliza.
“Ni nani wewe, hata kuniuliza swali kama hilo?”
Seidon akajibu kwa swali.
“Sikiliza, hapa ulipo si sehemu salama kwako,
nakuhurumia kwani hatari inayokukabili ni kubwa,
panda kwenye farasi nikuvushe kisha nikuache
uende zako,” yule msichana akamwambia Seidon
bila kumjibu swali lake. Seidon akatulia kimya,
akainama chini kisha akainua uso wake.
“Hapana, nitakwenda mwenyewe ninakotaka kwenda
ama la jitambulishe kwangu kwanza hapo nitatimiza
matakwa yako,” Seidon alimwambia Yule msichana.
“Mimi ni Zamaradi, kutoka mlima wa tatu kati ya
mitano uionayo, nchi inayoishiwa na wasichana tu
ambao wote ni bikra kwa kuwa hakuna mwanaume
kwetu, napenda nikukaribishe kwetu ili uishi nasi
japo kwa kipindi kifupi kisha nitakuonesha njia fupi
ya kufika utakako,” Yule msichana alijitambulisha
kwa Seidon kuwa yeye ni Zamaradi. Yule msichana
akamsogelea Seidon jirani kabisa, harufu ya
manukato aliyojipulizia yaliziburudisha pua za
Seidon hata kuanza kujisahau.
“Kwani wewe unajua ninakokwenda?” Seidon
akmuuliza.
“Sisi, ndiyo tunaotawala mawazo yote ya binadamu,
naliiona nafsi yako tangu ikianza safari ya kuja huku,
yuko wapi mwenzi wako? Tazama upepo mbaya
umemchukua na hutomuona tena, yuko wapi Orion?
Adui aliyewazuia njia, usikifikiri ni ninyi
mliyempoteza bali ni jeshi kubwa lililokuzunguka
nyuma yako, ambalo ndilo limemchukua rafiki yako
wa safari, hapa limetulia kwa kuwa linaniogopa
mimi, nikikuacha tu nawe utakuwa katika hali
mbaya,” Zamaradi alimwambia Seidon, akageuka
nyuma hakuona mtu.
“Mbona sioni chochote?” Seidon akamuuliza
Zamaradi.
“Macho yenye damu hayawezi kuona kilichopo
katika giza nene,” Zamaradi akajibu akamshika
mkono Seidon na kukitazama kiganja chake,
“Ooooh Hamunaptra, una safari ngumu sana kufika
hamunaptra, nitakuonesha njia fupi zaidi,” akasema
na kumuachia mkono wake.
Seidon alihisi kama anapigwa kwa shoti ya umeme,
aliona vimulimuli vya radi kali vikipita mbele yake
pale aliposhikwa mkono na Zamaradi.
‘…mshikane mkono na kiumbe chochote…’
Seidon alirudiwa na maneno hayo, na hapohapo
akaona kosa alilolifanya. Zamaradi akamchukua na
kumpandisha katika farasi wake kisha kupiga mbio
pamoja nae.
Walipokuwa njiani Zamaradi akaingiwa na kitu
kingine, yeye aliagizwa na Sherhazad akafanye hila
ya kumpata Seidon baada ya kusaidiwa
kutengenishwa watu hao, Zamaradi katika uwepo
wake hakuwahi kuona mwanaume wa kibinaadamu,
na sehemu anayoishi ni wanawake tupu, ulimwengu
wa chini, akatamani kuonja mapenzi ya binadamu,
akapiga mbio na kupita karibu na kabisa na
miamba mikubwa sana ambayo haikuwa mbali na
lango la Hamunaptra, pembezoni tu mwa Ikweta.
Akasimamisha farasi wake.
“Na tupumzike hapa!” akamwambia Seidon huku
akitangulia kwa hatua zake za ajabu mpaka ndani ya
jiwe kubwa akaketi, “Keti hapa karibu nami,”
akamwambia Seidon. Zamaradi alimtazama Seidon
kwa jicho la uchu, akaanza kumshikashika shingoni,
Seidon akaanza kuhisi raha ya ajabu ambayo
hajawahi kuihisi maishani mwake, akatulia
akiiruhusu mikono ya Zamaradi ifanye inachotaka
 
“Na tupumzike hapa!” akamwambia Seidon huku
akitangulia kwa hatua zake za ajabu mpaka ndani ya
jiwe kubwa akaketi, “Keti hapa karibu nami,”
akamwambia Seidon. Zamaradi alimtazama Seidon
kwa jicho la uchu, akaanza kumshikashika shingoni,
Seidon akaanza kuhisi raha ya ajabu ambayo
hajawahi kuihisi maishani mwake, akatulia
akiiruhusu mikono ya Zamaradi ifanye inachotaka.
CHAPISHO LA 12
Sheria au utaratibu wan chi ya Soria iliyopo katika
ulimwengu wa chini, kunakoishi wanawake wengi ni
kuwa hutakiwi kufanya mapenzi na mwanadamu
ijpokuwa kwao ilikuwa ni kitu cha kifahari sana
kama ukifanikiwa hilo. Wengi wao walipokujwa
kwenye matembezi yao ya kificho walikuja duniani
na kuwakwaza wanaume wengi kwa kuwapa utajiri
mwingi lakini kwa sharti moja tu la kufanya nae
mapenzi, na walikuwa na mapenzi mazito nay a
dhati kuliko wanawake wa dunia hii, walikuwa na
utamu usioelezeka katika kufanya mapezni walijua
kumridhisha mwanaume kwa kila hali, watakufanya
ukojoe kadiri unavyotaka na usijisikie kuchoka,
sharti lao kwako ni moja tu, usimwambie mtu kama
wao si binadamu na wala usiwe tena na mapenzi na
binadamu wa kike, ukitimiza hayo watakupa kila
kitu, wivu kwao ulikuwa ni ugonjwa. Lakini
hawakutakiwa kufanya mapenzi na mwanadamu
katika ardhi yao, hilo ndilo lilikuwa baya zaidi na
hata hivyo hakuna mwanadamu aliyekanyaga ardhi
yao bila idhini.
Zamaradi alitamani kuonja kile alichokisikia kwa
wengine waliowahi kufanya hivyo, kutokana na umri
wake na ubikira wake alisahau kabisa sharti moja la
kutofanya mapenzi katika ardhi ile kwani unaitia
najisi.
Akamfanyia maandalizi Seidon, maandalizi ya nguvu,
Seidon alishangaa kwa raha inayoufunika mwili
wake, sasa nay eye akatamani ale tunda hilo la
ajabu, akamkumbatia kwa nguvu Zamaradi, lakini
akashangaa vazi lake likitoweka na kubaki kama
alivyo, Seidon akiwa katika shughuli nzito alihisi
kama anapaa kwa jinsi alivyokolezwa na Zamaradi,
naye Zamaradi hakuamini anachokipata kwani aliona
raha isiyo kifani. Miguno na milio vya mahaba
ikatawala, sauti ya Zamaradi ikazidi ile ya Seidoni,
ikaanza kuwa sauti ya kutisha sana, sauti kama ya
mnyama mkali mwenye uchu wa nyama, Seidon
alipomtazama lo, alikuwa amekumbatia mnyama
mbaya wa kutisha, mwenye meno makali na marefu,
ulimi kama nyika uliogawanyika vipande viwili,
miguu ya ng’ombe yenye manyonya yaliyosimama
kama miba ya nungunungu, pembe mb I zenye ncha
kali. Seidon aliogopa lakini alijikuta hawezi
kubanduka kwa Yule mnyama, aliendelea kufanya
mapenzi, raha ya penzi hakupotea, iliongezeka mara
dufu.
Mara tetemeko la ardhi likaanza kuitikisa ardhi ile,
likazidi na kuzidi, vipande vya mawe vikaanza
kuwaangukia Seidon na mnyama Zamaradi, mara
donge la moto likaja kutoka kusikojulikana,
likavamia ndani ya pango lile, Zamaradi akatoa
yowe kali la kutisha lililozidisha lile tetemeko,
Seidon akaanguka kutoka kwa Yule mnyama na
kutua chini kwa nguvu, fahamu zikamjia akatafuta
huku na kule fuvu hakuliona lilikoelekea, akahisi
kuchanganyikiwa, mara kwenye ule moto akatokea
farasi mkubwa wa moto na juu yake kulikuwa na
malaika wa moto, mwili wake ulitangenezwa kwa
ndimi za moto, mikononi mwake alishika upanga
wa moto. Sauti ya Zamaradi bado ilikuwa ikisikika
kwa nguvu na ilikuwa ya kutisha kuliko mwanzo.
§§§§§
“Zamaradi umeniuzi, umekiuka masharti ya kazi
niliyokutuma, adhabu yako unaijua, nitaiteketeza
roho yako na kuitupa katika dimbwi la tope la
ukaidi, huko utaishi milele kwa mateso na dhiki,”
ilikuwa sauti ya Sherhazad ikimwambia Zamarad.
Zamarad alimtazama Sherhazad kwa woga,
akamwangukia na kumuomba msamaha lakini
hakukuwa na kitu kama hicho, Zamaradi
alikwishajua mwisho wake umefika, kwa kuwa alijua
pia ambacho Seidon atafanyiwa na wenzake pindi
akichukuliwa na malaika wa moto, akajaribu kuona
cha kumsaidi kabla hajatupwa katika dimbwi hilo
ambalo hukiingia hutoki tena kwani roho yako
inageuka kama uji na kukutana na roho zingine za
kale katika shida na dhiki kuu.
Wakati hayo yakiendelea, Zamarad alimuona kiumbe
mwingine akimkabidhi fuvu lile Sherhazad
alilolichukua kwa Seidon.
§§§§§
Mwaka 2010
Katika mapiramidi
Amatagaimba alianguka vibaya katika shimo kubwa
lenye giza nene, akabwagika mchangani. Ilikuwa
ngumu kwake hata kusimama baada ya shambulizi
hilo alilolipata kwa ghafla kutoka kwa kiumbe
ambacho hakukiona kwa macho, ila alikuwa akihisi
tu mara anabebwa na mara anabwagwa chini,
akatumbikizwa kwenye shimo refu na kujikuta huko.
Alijaribu kujinyanyua lakini ilishindikana.
Alibaki pale chini akihema kwa nguvu na mhemo
wake ulikuwa ukisafiri ndani ya shimo hilo kubwa,
hakuwa na jinsi, macho yake yalipotulia akaona
muali mwembamba wa nuru ya mwanga, akatambaa
kama mtoto kuuelekea mwanga huo, Amatagaimba
hakujua ni wapi alipo, aliendelea kutambaa huku
akihema kwa nguvu, kiu nayo ilikuwa ni sehemu
nyingine ya mateso yake.
Amatagaimba akafika katika ule muali wa mwanga,
mara tu alipoufikia mkono wake ulikutana na ule
mwanga ile pete yake ikang’aa na kufanya nuru
katika shimo zima. Amatagiamba akasimama kwa
miguu yake, akatzama huku na kule asipajue alipo.
“Niko wapi?” aliongea kwa sauti ya chini lakini
ilionekana kusikika kila mahali, michoro iliyokuwa
katika kuta za shimo lile ilianza kufungua vinywa
vyao na kucheka kwa sauti kali iliyosababisha kuta
zile kutikisika. Amatagaimba katika kona moja ya
kuta za shimo lile aliona kama kitu kilichojikunja au
mtu, hakujua hasa ni nini anachoiona. Akaufuta
upanga wake na kujikongoka taratibu mpaka
kwenye ile kona, macho yake hayakumuongopea,
alikuwa mtu, mwanamke, akamshtua, na Yule mtu
akageuka kumtazama ijapokuwa alikuwa na woga
machoni pake. Amatagaimba akarudisha upanga
wake na kumpa mkono, akamwinua.
“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.
“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha
kwa sauti ya kukwamakwama.
“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena
mara hii kwa mshangao zaidi.
“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata
kufanya nini, mimi nika, nika, ah, sikumbuki, kwani
wewe ni nani?” Anna alijibu lakini alionekana
kupoteza kumbukumbu. Amatagaimba alimtazama
binti huyu aliyekuwa kachafuka mwili mzima kwa
vumbi, nywele zote zilikuwa hazitamaniki jinsi
zilivyo timtim. Alimuona wazi kuwa hawezi hata
kusimama sawasaw kwa jinsi alivyochoka.
Amatagaimba akamsaidia kunyanyuka.
“Nina kiu,” akamwambia Amatagaimba. Eneo hilo
lote hakukuwa na maji Amatagaimba akapapasa
kibuyu chake na kugundua kuwa hanacho,
akajishika kiunoi lakini hakukata tama, kw akutumia
pete yake ya ajabu aliiomba imletee maji, mara
wakasikia radi kubwa ikipiga na sauti kama sauti ya
maji ilisikika upande wa chini. Amatagaimba
akamshika mkono Anna na kuondoka nae eneo lile,
walielekea upande wa kaskazini nahuko wakakuta
ngazi ndefu zikielekea chini, wakateremka nazo na
huko walikuta maji yaliyokuwa yakitembea, maji
yam to ambayo hayakuonekana yatokako wala
yaendako. Anna aliyavamia na kunywa kwa pupa
mpaka akapaliwa, mara akataka aoge kabisa, lakini
Amatagaimba akamzuia kuwa hapo si mahala pake.
Kila mtu aliporidhika wakapita kandokando yam to
ule na kutokea upande mwingine ambako kulikuwa
na ngazi nyingi zikipanda kuelekea juu, wakazikwea
taratibu, Anna akiwa mbele na Amatagaimba akiwa
nyuma. Baada ya kupanda ngazi kadhaa
hawakusikia tena ule mto wa maji kama mwanzo.
Ila walianza kusikia kelele za popo wengi waliokuwa
ndani humo. Amatagaimba akamwambia Anna
asimame, naye akasimama kisha yeye akaenda
mbele na kutazama popo wale kwa makini sana,
hawakuwa wakitikisika lakini walikuwa wakipiga
kelele kama wanaoongea jambo Fulani.
Amatagaimba akamgeukia Anna akamtazama
kifuani, alikuwa amevaa kidani cha jiwe Tanzanite na
hereni zake.
“Vua kidani, na hizo hereni pia,” Amatagaimba
akamwambia Anna, naye akafanya hivyo bila kujua
kwa nini anaambiwa hivyo.
Kisha wakaendelea kwenda mbele wakivuka lile
eneo lenye popo wengi. Anna alijitahidi kumfuata
Amatagaimba kila anakonkwenda, wakapita ndani ya
mapango mengi mengine ya kutisha sana,
walikutana na viumbe vya ajabu ajabu kila wapitapo,
kwingine waligeuza njia, kwingine walijitahidi kupita
hivyo. Ilikuwa ni kazi ngumu kuona njia ya kutokea
nje.
“Tutatokaje humu Amatagaimba?” Anna akauliza
huku akihema sana.
“Humu ndani hatutoki kwa kutumia njia za kawaida
kama huko duniani…” Amatagaimba alianza kueleza.
“Sijakuelewa unasemaje?” Anna akauliza kwa
mshangao.
“Nimesema, humu ndani hatutoki kama huko
duniani, unajua sasa hivi upo miaka mingi nyuma!
Mimi nilikotoka ni miaka 1200 iliyopita, na nilipotea
kimiujiza kama wewe, hivi wewe sasa kama ulitoka
duniani mwa elfu mbili na kitu basi sasa upo
mwaka elfu moja na kitu, hivyo kutoka humu ni
kupata miaka iliyobaki,” Amatagaimba alieleza
lakini Anna hakuelewa kabisa somo hilo, “Ili kutoka
humu inabidi ukumbuke mwaka uliotoka duniani
halafu tupate dira ya kutuonesha uelekeo, na dira
hiyo ipo kwenye mnyama hatari, mnyama ambaye
ndiye anayeshika pande nne za dunia,”
Amatagaimba alimuelea Anna vitu vya ajabu
ambavyo kwake vilionekana kama havina maana.
“Kwani wewe umetoka wapi?” Anna akauliza.
“Mimi nimetoka duniani miaka mingi sana, nikaingia
ulimwengu huu wa chini ya dunia tangu nikiwa
katika msitu wa Solondo nilipotoka sikuweza kurudi
kwani njia yangu ya kurudi imekuwa ngumu mno,”
Amatagaimba akaeleza.
“Msitu wa Solondo!!!” Anna akashangaa kwa kusikia
jina hilo.
“Ndiyo vipi unaufahamu?” Amatagaimba akauliza
huku akimtazama binti huyu usoni.
“Siufahamu, na wala sijawahi kuuona kwa macho,
ila nimeusoma kwenye kitabu cha riwaya kikibebwa
kwa jina hilo, simulizi ya zamani sana hata mimi
sikuwa nimezaliwa,” Anna akaeleza. Amatagaimba
alimtazama mwanamke huyu mrefu, mwenye umbo
shupavu.
“Ni nini kitabu hicho kimeeleza?” Amatagaimba
akauliza huku akiwa amemshika mabegani Anna,
wakitazamana uso kwa uso.
“Sasa ndiyo naelewa,” Anna akajibu na kuitoa
mikono ya Amata kwa ghafla mabegani mwake,
‘Mzimu?!’ akajiuliza, Anna akaanza kutimua mbio.
“Anna!” Amatagaimba akaita, mara kuta zikaanza
kutikisika, Amatagaimba akaanza kutimua mbio
kumfuata Anna, akamfikia, kila alipojaribu kumshika
mkono, Anna alijitoa katika mikono ya
Amatagaimba na kutimua tena mbio, Amatagaimba
hakumuacha, naye alimkimbiza, wakiwa katika
kukimbizana kwenye ngazi hizo, mara lile jengo
likaanza kutetemeka kana kwamba kuna kitu kizito
kikipita juu yake. Amatagaimba akasimama na
kutazama huku na kule wakati Anna aliingia kwenye
mlango mmoja ulioonekana wazi. Alipoingia tu
mlango ukajifunga, Anna akabaki ndani, hana ujanja,
aliuendea mlango na kuanza kuupigapiga huku akilia
na kuita.
“Amatagaimbaaaaaaaa!!!!! Nisaidie,” aliita kwa
nguvu zote.
AMATAGAIMBA ANAKUTANA NA ANNA ... NINI
KITAENDELEA ?
 
“Anna!” Amatagaimba akaita, mara kuta zikaanza
kutikisika, Amatagaimba akaanza kutimua mbio
kumfuata Anna, akamfikia, kila alipojaribu kumshika
mkono, Anna alijitoa katika mikono ya
Amatagaimba na kutimua tena mbio, Amatagaimba
hakumuacha, naye alimkimbiza, wakiwa katika
kukimbizana kwenye ngazi hizo, mara lile jengo
likaanza kutetemeka kana kwamba kuna kitu kizito
kikipita juu yake. Amatagaimba akasimama na
kutazama huku na kule wakati Anna aliingia kwenye
mlango mmoja ulioonekana wazi. Alipoingia tu
mlango ukajifunga, Anna akabaki ndani, hana ujanja,
aliuendea mlango na kuanza kuupigapiga huku akilia
na kuita.
“Amatagaimbaaaaaaaa!!!!! Nisaidie,” aliita kwa
nguvu zote.
CHAPISHO LA 13
Haikuwa rahisi kwa Amatagaimba kuingia, mlango
mkubwa wa jiwe ulikuwa umejikita, Amatagaimba,
akajisjika kiuno hakujua la kufanya, akatazama huku
na kule bado hakuweza kujua la kufanya. Mtikisiko
ulikuwa ukiendelea, Amatagaimba ikambidi atoke
eneo lile na kwenda upande mwingine, mbele
kidogo tu dude la ajabu likatua mbele yake, shetani
si shetani, jinni si jinni, lilikuwa ni kiumbe kikubwa
kilichosimama kwa miguu miwili yenye kwato,
mikono miwili yenye vidole vitatu kila mmoja,
alikuwa mkubwa mara tano ya binadamu, na
alionekana kuwa na uzito mkubwa, midomo yake
ilikuwa kama ya bata na macho yenye kung’aa sana,
katika tumbo lake kulikuwa na kitu kama goroli
kubwa lililokuwa likitoa mionzi mbalimbali.
Amatagaimba akarudi nyuma taratibu, akiweka
nafasi kati yake na mnyama yule, huku akiangalia
kile kitu mfano wa goroli.
Mara moja aligundua kuwa kitu kile ndicho hasa
anachokitafuta ili kuweza kutoka nje ya shimo lile
kubwa, kwani kinaweza kukuelekeza njia ya kutokea
kutokana na nguvu yake iliyoshika pande nne za
dunia. Lile limnyama likawa linamfuata polepole,
lakini alichoshangaa halikuwa na nia ya kumdhuru.
Amatagaimba akajikuta akiugonga ukuta nyuma
yake, ikambidi kusimama, lile limnyama likamfuata
mpaka pale, na kumuinamia, nyuso zao zikakutana,
lile limyama likamtazama Amatagaimba,
halikumfanya chochote. Mara kelele za Anna zikawa
zina sikika kwa mbali, lile limnyama likageuka
kuangalia kule zinakotokea kelele, kisha
likamwangalia Amatagaimba, akatoa ukelele mkali
ambao uloifanya vumbi litimke mle ndani,
Amatagaimba akaanguka chini kwa woga. Lile
limnyama likaanza kuvuta hatua kuelekea kule aliko
Anna, Amatagaimba hakujua nini cha kufanya
akatulia kusubiri aone. Kwenye ule ukuta kulikuwa
na masanamu ya ya vichwa vya samba kuzunguka
kote, lile limnyama likashika kichwa kimojawapo na
kukikandamiza chini, mala lile lango la jiwe pale
kwenye tundu alipoingia Anna likafunguka, Anna
akatoka kwa kasi na kumkumbatia Amatagaimba
aliyekuwa tayari amesimama wima akiangalia tukio
lile.
“Anna,” Amatagaimba alipiga kelele huku akiwa
amemdaka. Kisha wote wakageuka na kumtazama
yule mnyama. Yule mnyama akaanza kuwasogelea
tena tarataibu mpaka pale waliposimama,
likawainamia na kunyanyua mkono wake mpka
kwenye shingo ya Anna na kuushika mkufu wake
wenye kito safi cha Tanzanite ya buluu, akaukata na
kukitazama kwa makini kile kito, akatikisa kichwa,
akatenganisha kito na mkufu, akachukua kito tu,
kisha akamtazama Anna ambaye alikuwa ametulia
tuli, kabla hajafanya lolote, Amatagaimba akamvua
Anna heleni zake nazo zilikuwa na kito hichohicho
akampa yule mnyama, yule mnyama akanguruma na
kutikisa kichwa chake kisha akageuka kuondoka
kwa hatua zake nzitonzito za kutisha. Amatagaimba
na Anna walikuwa wamesimama, baada ya hatua
kama tano hivi alikuwa amefikia ukuta ule mkubwa,
akasimama na kugeuka nyuma akawaona Anna na
Amatagaimba wakiwa palepale, akaunguruma na
kuwapa ishara wamfuate, wakafanya hivyo.
Wakasimama palepale aliposimama, radi moja
kubwa ikapiga kwa nguvu ndani mwote mkajaa
mwanga, akamuonesha Amatagaimba jiwe kubwa
lililojitokeza kama pande la tofari, Anna akapanda
kisha yule mnyama akatikisa sanamu linguine na
mawe ya mtindo ule yakatokeza mengi na kuyfanya
ngazi kwenda upande wa juu, Anna na Amata
wakazukwea kuelekekea juu ya shimo lile, akawapa
ishara ya kuwa waondoke wakati yeye
amekandamiza lile sanamu kwa mkono wake.
Amatagaimba na Anna wakakwea kwa kukimbia
kuelekea juu, zilikuwa ngazi nyingi ambazo
unatakiwa uzipande kwa uangalifu sana. Muda si
mrefu walijikuta wanatoikea mahala pendine kabisa.
Anna alipotoka kwenye zile ngazi akaangukia
kwenye mchanga mwororo ambao ulikuwa kama
mchanga wa jangwani.
“Tumepona Amatagaimba,” Anna akamwambia
Amatagaimba ambaye alikuwa akijvuta pale
mchanagani nae akiwa hoi.
“Uhhhh!!!! Bado, kazi sijamaliza,” Amatagaimba
akamwambia Anna, “Rafiki yangu sijui yuko wapi,”
akajisemea.
“Rafiki?! Rafiki gani?” Anna akauliza.
“Ha, we unafikiri huku nimekuja peke yangu? Niko
na mwenzangu, na tuko na kazi maalumu nab ado
hatujaimaliza, sasa yapata nimtafute popote alipo ili
tukamilishe misheni hiyo,” Amatagaimba alisema.
“Nyanyuka twende zetu hatutakiwi kulala hapa, tuko
hatarini sana,” Amatagaimba akamwambia Anna na
kisha wote wakaanza safari ya kutembea kwenye
mchanga kuelekea wasikokujua.
§§§§§
Zamarad aliendelea kumtazama huyo kiumbe
akimkabidhi fuvu lile Sherhazad, naye akawa
akilipokea huku akitabasamu.
“Humsaing tuuunggg, seiduss seiduss” Zamaradi
alitamka maneno hayo ambayo kwa kiwango chao
katika ulimmwengu huo, ungeweza kujigeuza na
kuwa kiumbe yoyote yule.. Mara upepo mkali
ukaanza kuvuma ndani ya jengo lile. Zamaradi
akageuka mwewe, akachomoka pale alipo na
kulinyakuwa lile fuvu na kutoka nalo dirishani kwa
kasi.
Sherhazad alitamani kulia kwa kuona Zamarad
amemzidi ujanja katika hilo, akanyoosha mkono
wake na kupewa uta wake wa kichawi, akaweka
mshale juu yake na kuuvuta kwa nguvu, akautuma
kwa maneno yasiyoeleka kwa lugha yake ya kijini,
ule mshale ukaondoka kwa kasi kumfuata yule
mwewe.
Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni
kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la
kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni
wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi
zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto
akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga
hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea
mlio ule. Malaika wa moto anayetegemewa na
Sherhazad katika shughuli ngumu kama hizi huwa
hatakiwi kuguswa na maji hasa mvua kwani mwili
wake umeumbwa kwa moto hivyo akiguswa na maji
ndiyo mwisho wa uhai wake. Mara moja bila
kuuliza, akamgeuza farasi wake na kuondoka, na
kweli mvua kubwa ikanyesha eneo lile na kukatika
kwa muda mfupi. Mbele ya Seidon akatua mwewe
mkubwa aliyeshika fuvu la Cleopas miguuni mwake,
akatua na alipoliacha lile fuvu na kuondoka hakufika
hata mita 10 mshale wa kichawi uliotumwa na
Sherhazad ukampiga yule mwewe na kisha
ukageuka nyoka aliyekuwa akijiviringa mwilini kwa
yule mwewe. Yule mwewe akaanguka chini na
vumbi likatimka eneo lile.
Seidon akalichukua lile fuvu na kuondoka mahala
pale haraka, alikumbuka maneno ya yule mzee
ambaye alikufa kwenye bonde la mauti, kuwa akifika
katika mstari wa Ikweta basi nguvu zote za majini
haziwezi kufanya kazi, hakuwa mbali na eneo hilo.
Seidon akiwa na upanga wa Vernad mkono wake wa
kulia na ule wa kushoto amelishikilia lile fuvu, sasa
halikuwa kwenye mfuko lilikuwa wazi mkononi
mwake, akaanza kutimua mbio kuielekea Ikweta.
Nyuma yake alisikia sauti za watu wanaomkimbiza
lakini kila alipogeuka hakuwaonaa, aliendele
kukimbia lakini bado aliona hafiki wakati mahali
penyewe palikuwa karibu. Mara hii alipogeuka
nyuma aliona kundi kubwa la watu waliokuwa
wakimfukuza kwa miguu na farasi. Seidon alikimbia
kwa nguvu zake zote, akakaribia kabisa Ikweta,
ndipo alipoanza kuona maajabu ya lile fuvu
alilolibeba, akajikuta amekuwa mwepesi, anakimbia
akikanyaga hewani na si ardhini kama ilivyokuwa
mwanzo, wakati huo vishindo na kelele za radi
zilikuwa zikisikika na anga lote lilikuwa likikatwa
kwa miali mikali ya radi. Seidon aliendelea
kukimbia na alipoingia Ikweta alijikuta akikimbia
zaidi kuliko mwanzoni, mwisho wake akaingia ndani
ya pango na kujificha, lile fuvu likatengeneza
mwanga wa kutosha uliopitia katika matundu ya
macho yake.
Seidon akawa anashangaa kila analoliona likifanyika
sasa kutoka katika fuvu lile.
“Amatagaimba, uko wapi?” akanong’ona Seidon.
Mara akasikia sauti za watu wawili wakiongea, sauti
zao zilikuwa zikisikika kutoka chini. Seidon
akasimama na kuangalia huku na huko lakini
hakuweza kuona mtu yeyote isipokuwa aliendelea
kusikia sauti zile mbili, ya kike nay a kiume.
Seidon akashtuka kidogo, kwani alikuwa akizisikia
sauti zile kutoka chini ya ardhi, akapiga magoti na
kutega sikio lake ardhini, akaisikia kwa uwazi kabisa
sauti ya Amatagaimba.
“Inatupasa tutoke humu, namtafuta rafiki yangu
Seidon,” ile sauti ikasikika.
“Amata gaimba!” Seidon akaita kwa sauti ya
taratibu.
§§§§§
Amatagaimba akamzuia Anna kwa mkono wake wa
kuume.
“Vipi?” Anna akauliza.
“Kuna mtu ananitafuta,” akamjibu. Baada ya kutulia
kama dakika tatu hivi, akatazama kidole cha mkono
wake, akaitazama pete ya ajabu aliyokuwa nayo
kidoleni, akaongea maneno Fulani na mara upepo
mkali ukavuma na kutimua vumbi jingi. Anna Davis
kwa woga akajificha nyuma ya Amatagaimba
akitetemeka kwa hofu.
Amatagaimba akanyosha mikono yake na lile vumbi
likatulia, katikati ya vumbi lile kukabakia farasi
mkubwa aliyesimama kimya akimtazama
Amatagaimba. Akamshika mkono Anna na
kumwelekea yule farasi.
“Mi naogopa kupanda farasi,” Anaa alikataa.
“Endelea kuogopa, utabaki hapo hapo ulipo maisha
yako yote!” Amatagaimba akamjibu huku
akimtazama, “Twende! Tena wewe una kazi ngumu
sana ya kufika huko ulikotoka”. Amatagaimba
akakwea farasi, akamtazama tena Anna bado akiwa
amesimama palepale.
“Tazama nyuma yako!” akamwambia. Anna
akageuka nyuma na kushuhudia moto mkubwa
ukiwaka huku ukielekea kule walikosimama wao.
“Mamaaaaaaaa…. Amatagaimba nisaidie!” Anna
alipiga kelele za woga, akakimbilia pale kwenye
farasi, mkono wake ukashikwa na ule wa
Amatagaimba na farasi akaanza kuondoka kwa kasi
huku Anna akijiweka vizuri mgongoni mwake.
“Wanakuja Amatagaimba, watatuua wale kimbia!”
Anna alikuwa akipiga kelele mgongoni mwa
Amatagaimba. Farasi alikuwa akipiga mbio za
ajabu, lakini Amata gaimba kila alipogeuka nyuma
aliona jeshi lile linakuja kwa kasi kuliko yake.
Vumbi lilikuwa likitimuliwa na miguu ya yule farasi,
hakujali mchanga mwingi wa jangwani alizipiga
mbio kwelikweli. Kwa mbali kidogo, Amatagaimba
aliona kitu kama nyumba au mlima hivi hakuweza
kujua haraka ni kitu gani kiuhakika.
“Huyo atakuwa Dherhazad na swahiba zake!”
Amatagaimba aliendelea kuongea.
“Sherhazad?” Anna akauliza akiwa bado
kamng’ang’ania Amatagaimba kiunoni.
“Ndiyo ni Malkia wa majini katika milki ya Soria,”
akamjibu. Baada ya mwendo wa muda kidogo
wakakaribia kabisa ule mlima, mara zikaanza
kusikika kelele za watu, watu wengi kana kwamba
kuna kitu wanakifukuza. Kelele zao zilikuwa
zinaumiza masikio, mara nyingi Anna alikuwa
akijiachia na kuziba masikio na kuataka kuanguka,
kelele zilizidi sana, Amatagaimba hakujali.
JE SHERHAZAD ATAFANIKIWA KULITWAA FUVU
HILO?
YUKO WAPI SEIDON?
 
“Sherhazad?” Anna akauliza akiwa bado
kamng’ang’ania Amatagaimba kiunoni.
“Ndiyo ni Malkia wa majini katika milki ya Soria,”
akamjibu. Baada ya mwendo wa muda kidogo
wakakaribia kabisa ule mlima, mara zikaanza
kusikika kelele za watu, watu wengi kana kwamba
kuna kitu wanakifukuza. Kelele zao zilikuwa
zinaumiza masikio, mara nyingi Anna alikuwa
akijiachia na kuziba masikio na kuataka kuanguka,
kelele zilizidi sana, Amatagaimba hakujali.
CHAPISHO LA 14
“Anna!!! Jishike vizuri, tunaingia Ikweta!”
Amatagaimba alipiga kelele huku akimwimiza farasi
kupiga mbio, zile kelele sasa zilikuwa kali zaidi
kiasi kwamba zilikuwa zikisumbua masikio ya wote.
Alipogeuka nyuma aliona wale majeshi wanakuja na
farasi wao tena hawakuwa mbali.
“Amatagaimba., wanatufikia, hawa hapa!” Anna
alipiga kelele za woga.
“Tulia Anna, tukifika Ikweta tutakuwa
tumekwishapona,” akajibu.
Mara ghafla yule farasi akawakama amejipiga
kwenye ukuta au jiwe, wakaanguka chini wote
wawili na farasi wao, tayari walikuwa wameingia
Ikweta, lakini farasi yule aliishia pale ambapo
Ikweta inaanzia kwa kuwa hakuwa farasi wa kweli
bali wa kutengenezwa. Amatagaimba aliinuka
nharaka na kumshika mkono Anna aliyekuwa
amechafuka kwa vumbi la janagwani kisha akaanza
kukimbia naye mpaka kwenye kitu kama mlango,
akaupiga teke ukafunguka wakaingia wote wawili na
kuufunga mlango nyuma yao, kisha wakasimama
kwa kujibanza kwenye pango hilo lenye kiza kinene.
“Hamunaptra!” Amatagaimba alijisemea kwa sauti
ndogo, kisha akaanza kufuatilia ngazi ndefu
zilizokuwa zikiteremka chini.
“Amatagaimba” Anna akaita kwa kunong’ona.
“Shhhhhh!!!!! Usiamshe roho zimelala” Amatagaimba
alaimwambia Anna. Amatagaimba akatazama zile
ngazi zilizokuwa zikielekea shimoni, giza lilitanda,
sauti ya vitu kama wadudu ndiyo iliyokuwa
imetawala ndani humo, alikuwa akikanyaga kwa
hatua za polepole ambazo hazikuwa zikitoa hata
kelele, huku upanga wake ukiwa mikononi mwake
barabara kabisa kwa hatari yoyote, mbele zile ngazi
zikaisha pakabaki uwanda mkubwa lakini uliojazwa
na giza totoro.
Mara sauti za milango ikifunguliwa zilisikika,
Amatagaimba akasimama ilhali upanga wake
ulikuwa mikononi mwake, mara kitu kama jiwe
kilimpitia jirani na kugondokea upande wa pili. Mara
kelele kama za watu waliokuwa wakija
kumshambulia zikaanza kusikika, aliutwaa upanga
wake na kuanza mapambano, ilikuwa ni kazi ngumu
sana kwani alikuwa havioni viumbe anavyopigana
navyo kutokana na giza lililokuwa mahala hapo.
Alijitahidi kuutembeza upanga wake wa nguvu zote
alihisi kupiga vitu Fulani lakini hakuweza kuviona.
Anna alibaki nyuma ya Amatagaimba akijikinga
kupitia mgongo wake.
“Amatagaimba, nisaidie!!!” Anna alipiga kelele
alipohisi mguu wake kama unafungwa minyororo,
amatagaimba aligeuka kwa wepesi na kuona japo
kwa taabu, mwiliwa Anna ukivutwa, akaruka
sarakasi na kukata ule mnyororo. Kelele zilizodo
kuongezeka na viumbe hivyo vya ajabu vilizidi
kumiminika ikawa taabu.
Mara ardhi ya mule ndani ikaanza kuzunguka,
taratibu na kueongeza kasi.
“Aiyaaaaaaa!!!!!” Amatagaimba alipiga kelele
alipomuona Anna akitumbukia katika ufa mkubwa
wa uliojitokeza ukutani na kufanya mwanga wa
upande wa pili uking’aa, kwa haraka akawahi na
kupenya katika ule ufa lakini kabla hajamaliza
kuingia nguo yake ilibanwa na ule ufa.
Sasa kelele za radi zikaanza kusikika, mvua kubwa
ikaanza kunyesha.
“Hapo sasa hauna ujanja, kama nilivyomkamata
mwenzako sasa ni zamu yako,” sauti ya kike
iliyoksikika kwa mwangwi ilikuwa inaongea sana,
“Ingia, ingia wewe huko!” amatagaimba alianguka
chini baada ya Anaa kukata ile nguo iliyonasa
kwenye mwamba. Mara moshi mzito ukaanza kujaa
mahala hapo.
“Aaaaaaa ha ha ha ha ha, Aaaaaa hahahaha, zama
zenu zimekwisha nipeni hilo fuvu, niutawale
ulimwengu wote wa juu na wachini,” sauti kali ya
Sherhazad ilisikika na kufanya kile chumba kiwe na
vitu kama radi katika kuta zake, ilikuwa ni hali ya
kuogofya sana, Anna alikuwa akipiga kelele huku
akiziba masikio yake.
Kwa mbali Amatagaimba akawa anasikia kana
kwamba kuna ibada ilokuwa ikiendelea, kwani sauti
za watu wengi zilikuwa zikisikika nkama watu
wanaosali katika lugha isiyoeleweka.
“Krusum krusum, sontum sontum …” ile sauti ilizidi
kukaribi akana kwamba waliokuwa wakisali
walikuwa wakitembea. Kwa sekunde kadhaa
hawakusikia sauti ya Sherhazad. Amatagaimba
alizidiwa na moshi ule wakati huo Anna alikuwa
chini kaishiwa nguvu, mara radi kali na mngurumo
ikasikika mara moja.
“Amatagaimba… nifuate!” ilikuwa sauti ya Seidon.
“Seidonnnnn!” Amata naye aliita huku akimtazama
Anna aliyekuwa hajiwezi kwa moshi ule, akamvuta
kwa mkono wake na kumburuza mpaka pale
alipomkuta Seidoni ambaye alisimama katikati ya
ufa mkubwa wa ukuta ule wa jiwe akiwa juu ya
farasi wa ajabu.
“Amatagaimba, pita!” akamwamuru, Amatagaimba
akafanya hivyo, akapita na kutokea upande wa pili,
nje ya lile shimo la mtego, Seidon akamwamuru
farasi kurudi nyuma, naye alipoumaliza ule ukuta tu,
ukajifunga kwa nguvu na kufanya mawe kutoka juu
kuanza kudondoka huku na kule. Seidon akashuka
juu ya yule farasi.
“Huyu ni nani shujaa wangu? Si unakumbuka huku
hatutakiwi kufanya lolote na mwanamke” Seidon
akafoka huku akipiga magoti kumwangalia Anna.
“Seidon, huyu ni mwnadamu sio jinni kama
unavyofikiria, nimemkuta amenasa huko chini
nikamsaidia kutoka, ni hadithi ndefu, tutaongea
zaidi,” akamwangalia Seidon juu mpaka chini, “Fuvu
liko wapi?” akamwuliza.
“Amatagaimba bora nimekuona nalikuwa nakutafuta
kila upande wan chi hii, fuvu limenidondoka katika
shimo refu sana hata sikuwa na uwezo wa
kulichukua, twende twende mara moja,” Seidon
akamwambia Amatagaimba.
Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji
kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa
fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna
akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua
nyuma yake, safari ikaanza.
Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima
vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na
Wafuasi wake wamezingira eneo lote!”
akamwambia.
“Sasa tunafanyeje, inatubidi kutoka nje?”
Amatagaimba akauliza.
“Hapana, hatutoki nje kwani fuvu limedondokea
humu ndani na tukilipata tu mlango wa kuifikia
Klakos uko hukohuko chini,” akamjibu huku
akimchochea farasi yule kusonga mbele, mote
walimopita mlikuwa giza tupu, mara ghafla yule
farasi akapiga ukelele na kupoteza muelekeo,
akajipigiza katika jiwe na wote watatu wakaanguka
chini. Yule farsi alilala chini kimya, Amatagaimba
akachomoa nyoka kutoka usawa wa kifua cha farasi,
akamshika mkononi, yule nyoka alikuwa
ametumbukia kichwa ndani ya mwili wa huyo farasi.
Akamsika mkia na kichwa akamvutaq kwa nguvu
yule nyoka akakamaa kama mshale, Amatagaimba
akautoa uta wake na kumpachika yule nyoka kisha
akauvuta na kuufyatua gizani. Kitendo kile
kilimuudhi sana Sherhazad ambaye alikuwa
akitazama kila tukio kupitia dirisha lake la ajabu.
§§§§§
“Ni nani huyu anayeniuzi? Ana nguvu gani za
kunifanya mimi mjinga, nilishamdhibiti sasa katoka
vipi? Enyi Wachawi wa Soria, wazuieni njia, nataka
sasa niende mwenyewe kwani fuvu lkile liko jirani
kabisa na Klakosi, sasa hivi wanaweza kulirudisha,
name sintokubali walirudishe,” Sherhazad alipiga
kelele, akatoka dirishani na kuliendea joho lake
kubwa la kung’aa, akakwea farasi wake wa kijini
mwenye uwezo wa kupita angani, “Sasa sintotuma
kivuli changu tena ila nakuja mwenyewe, naona
mlipofika ni pabaya,”
Sherhazad aliondoka kwa kasi kuelekea
Hamunaptra, ilimchukua nukta kadhaa tu kufika
katika mji huo, mji wa kale, mji ambao kwa macho
ya kibinaadamu hauonekani kwa kuwa umepotea.
Hasira zilimtawala Sherhazad, alikuwa akipiga mbio
zisizo za kawaida na farasi wake, akitaka kuwahi
kabla Seidon na Amatagaimba hawajaingia mle
shimoni ambako huko ndiko kwenye njia ya kuifikia
Klakos. Kwa kuwa hakuweza kuipita Ikweta, ilimbidi
azunguke njia ndefu ambayo ingemtolea upande wa
pili wa mji huo, huko angeweza kuingia kiurahisi
zaidi.
“Angusha tufani kubwa ya mvua yam awe ndani ya
shimo hilo,” akasema huku akiwa mwendo wa kasi
juu ya farasi wake. Wale wachawi wake walisikia
ombi lake na kuanza kufanya linalowezekana.
Sherhazad alikasirishwa na jibu la wale wachawi
kuwa imeshindikana kuteremsha tufani katika shimo
ile.
“Nini, nini kimewashinda enyi wachawi
Wapumbavu?” akawauliza kwa kuongea nao kwa
hisia tu mawazoni mwao.
Akajibiwa kuwa ndani ya shimo hilo kuna nguvu
kubwa ambayo ipo kinyume na wao, ndiyo
inayokinga yote hayo.
“Shiit! Nikimpata huyu kijana namla nyama,”
akajisemea huku akiendela na safari yake. Mbele
yake alikabiriwa na bonde kubwa, kwa akili yake ya
haraka akakumbuka kuwa bonde lile ni mto
mkubwa wa maji ambao umekauka miaka mingi,
karne na karne. Na alijua wazi kuwa mto ule ulikuwa
ukiingia moja kwa moja chini ya mapiramid na
kutokea kwenye kiti cha Klakos.
Nitapita hapa, nitatokea moja kwa moja kwa
Klakos, alijisemea na kumwamuru farasi wake
aliyekuwa angani kulipita bonde hilo abadili njia na
kurudi chini.
§§§§§
Wakati wale wachawi walipokuwa wakijaribu
kuumba mvua yam awe ili kuwanyima njia Seidon
na Amatagaimba, ndani ya shimo lile kubwa nako
kulikuwa na jambo lingine, Amatagaimba akiwa na
ile pete yake ya ajabu alikuwa akiomba iwafikishe
salama waendako kwani ni kitambo kidogo tu
kilichobakia wao kufika chini katika lile shimo.
Kishindo kikubwa kikasikika na vumbi la wastani
likatimka. Amatagaimba, Seidon na Anna Davis
walidondoka katika udongo laini, chini ya shimo hilo
lenye giza. Seidon aliamka haraka bila kujali
maumivu aliyoyapata akaamua kuliwahi fuvu ambalo
lilikuwa mahala hapo, alipoweka mkono tu
kulinyanyua, akaona kitu kama upanga kinatua
karibu na kiganja chake cha mkono, akawahi
kuutoa, akatazama juu akamwona mwanamke mrefu
mweupe mwenye nywele nyingi, nguo yake
iliyofunikwa na joho kubwa ilikuiwa ikimetameta na
kuyafanya macho ya Seidon yashindwe kuona
sawasawa.
“Amatagaimbaaaa!!!!” Seidon akaitwa kwa nguvu
huku mikono yake ikiziba macho yake.
Amatagaimba akashtuka na kumtazama Seidon
aliyekuwa kajiinami ilhali lile fuvu limesogea mbali
kidogo.
“Seidon, Seidon!” akaitwa na kunyanyuka haraka
kisha akamwendea Seidon lakini kabla hajamfiki,
alihisi kama jiwe zito limempiga kifuani akatupwa
upande wa pili na kujibamiza ukutani. Mara tu
baada ya kujibamiza ukutani kishindo cha ajabu
kikasikika, na ule ukuta ukapasuka katikati, radi kali
iliyokata ule ukuta ilitisha na mwanga mkali kutoka
ndani ya ule ukuta ilipenya na kung’aza lile shimo
lote. Hakuna aliyeweza kutazama mwanga ule lakini
Amatagaimba alihisi kua upande wa pili kulikuwa na
kitu kama chumba kikubwa, kilichong’aa kwa
dhahabu safi kutokana na miali ya kitu kama jua
iliyokuwa ikipenya kupitia matundu Fulani.
Hakuelewa sawasawa lakini aliona vitu kama
viumbe Fulani vilivyojiinamia katika mtindo wa nusu
duara na mbele yao akiwapo mwingine, lakini kwa
jinsi miali ile ya mwanga ilivyopishanapishana mle
ndani hakupata uhalisia wa kile anachokiona.
“Klakos!” akatamka Seidon, na mara ileile ukatokea
mngurumo mkubwa wa kutisha uliofuatana na ardhi
kutetemeka. Seidon akajirusha kulichukua lile fuvu,
lakini akapambana na upanga mkali wa Sherhazad.
“Tulia Mpiga mbio, huna uwezo wa kulichukua hilo
fuvu na wala huwezi kuingia pale kwenye kiti cha
enzi cha Cleopas, kabla sijakuua, ulinifanya mimi
mjinga ukanihadaa sio?” Sharhazad aliongea huku
akimzunguka Seidon aliyekuwa bado pale chini
kajiinamia.
“Ewe mwanamke jinni dhalimu, kwa nini hupendi
neema za wanadamu ilhali wanadamu hao hao
unawatumia katika mambo yako mengi?”
Amatagaimba akauliza huku akijiweka sawa, upanga
wake ukiwa mkononi.
“Kelele! Ewe kiumbe wa dunia, kwanza umeingilia
vita isiyo yako na kwa hilo utaijutia nafsi yako,”
Sharahazad akamwambia Amatagaimba na wakati
huo akijibizana na Amatagaimba, Seudon
alijinyanyua kwa haraka na kujirusha sarakasi
akalikamata lile fuvu na kutaka kumpiga chenga
Sherhazad, lakini lo, jinni ni jinni tu, Seidon aliona
taswira nyingi za Sherhazad ndani ya lile shimo
akashindwa kujua hasa yupi ni yupi.
Amatagaimba akavuta hatu na kujirusha kumkabili
Sherhazad, panga zao zikakutana hewani, wote
wawili wakashuka chini na kutua kwa miguu yao.
Sherhazad alitumia nguvu zote kumsukuma
Amatagaimba ili apate nafasi ya kufanya shambulizi,
lakini Amatagaimba alitulia palepale hakusogea hata
milimita moja. Nguvu mbili zilizshindana, sherhazad
akaingalia pete ya Amatagaimba, pete inayompa
jeuri, akautoa upanga wake ghafla na kujizungusha
kwa umahiri mkubwa. Amatagaimba akaitambua
hila yake, akainama na Sherhazad akapita juu yake,
alaipotua tu, upanga wa Amatagaimba ukapenya
mbavu za Sherhazad.
“Aaaaaaaaiiiiiggghhhhh!!!!!” kelele za Sherhazad
zikapasua anga, mara kilicho kwenye kuta, paa, nje ,
ndani ya kaburi kikarudiwa na uhai.
“Aisatuuum, Aisatuuum,” akaongea lugha
isiyoeleweka, pale ulipochoma upanga pakawa
panatoka moshi wa buluu, Amatagaimba alikuwa
bado kashikilia upanga wake palepale na kumfanya
Sherhazad asisogee popote, kwani alipochoma
ndipo hasa penye uhai wa kiumbe huyo.
Kelele za watu wa kutisha zikaanza kuzikika ndani
ya shimo lile. Amatagaimba akaona hapo mambo
yataharika wakati tayari wameshafika mwisho.
Akauchomoa upanga wake haraka kutoka katika
mwili wa Sherhazad.
“Seidoooonnnn!” akaita huku akinyoosha upanga
wake kule kwenye ule mlango uliojitokeza katika
ukuta, Seidon akaruka na kujitupa upande wa pili
kwenye ule mlango lakini hewani alikutana na kifua
cha Sherhazad, Seidon akaanguka na kukohoa.
Anna Davis, akarudiwa na fahamu akasimama
haraka haraka akiwa anathema kama aliyekimbizwa
na mbwa.
Seidon alitambaa huku akiwa na maumivu, na fuvu
likiwa mkononi mwake, Sherhazad alijitahidi
kumshambulia lakini alijikuta anaishiwa na nguvu,
anashindwa, viumbe wake aliowaita kijini nao
walijikuta wanakosa nguvu ya kufanya lolote.
Amatagaimba akamshika mkono Seidon na Anna,
Seidon akajitahidi kunyanyuka na kuvuta hatua
taratibu kuuelekea ule mlango.
Sauti za watu waliokuwa kwenye ibada zikaanza
kusikika kwa mbali zikitoka ndani ya kile chumba
cha Klakos.
Sherhazad akajitahidi kuruka ili amkamate Seidon
haikuwezekana, alijikuta anashindwa kufanya lolote.
Kila walipozidi kuufikia mlango walijikuta wakipata
nguvu na kuanza kukimbiua kuelekea ndani, kelele
za watu waliokuwa kama wakishangilia zilisikika.
Kufumba na kufumbia, tena waligundua kuwa
wanapita hewani nyanyo zao hazigusi ardhi. Punde
si punde wakajikuta ndani ya chumba kile tulivu,
mvumo wa kitu kama upepo ulikuwa ukisikika
taratibu. Jinsi walivyokitazama kile chumba,
kilionekana kama mji mkubwa sana, wenye magofu
mengi nay a kutisha, masnamu ya wanyama
mbalimbali mengine bado yamesimama kwenye
nguzo zake na mengine tayari yamekwishaanguka.
Hakukuwa na mmea wenye uhai, yote ilikuwa
imekauka kwa ukame uliokithiri. Kwa ujumla
ulikuwa mji uliopotea, ukungu ulijaa kila mahali,
mvumo wa upepo uliendelea kufanya sauti tamu.
“Hamunaptra!” Amatagaimba akatamka.
Seidon na Anna wakageuka kumtazama,
“Hamunaptra?” Anna akauliza.
“Ndiyo, Hamunaptra,” Seidon akaongezea kumjibu
Anna kwa ni alionekana kuwa na dukuduku juu ya
hilo. Mara baada ya kutaja jina hilo wakasikia sauti
hafifu ya kitu kama bembea inayobembea huku na
kule na minyororo yake kufanya hiyo sauti kuashiria
kuwa ni minyororo mikavu isiyo na kilainishi. Sauti
hiyo ilisikika umbali mdogo tu kutoka pale
waliposimama. Ukungu mzito uliwafanya wasiweze
kuona hata mbele yao kuna nini, kwani hata wao
wenyewe walikuwa wakionana kuanzia viunoni kuja
juu. Ile sauti ya watu waliokuwa wakifanya ibada
iliendelea. Dakika chache baadae walisikia kama
mlango ukifunguliwa sehemu Fulani, kisha ukimya
ukawakabili.
SAFARI INAFIKA UKINGONI.....
NINI KITATOKEA?
 
Sauti hiyo ilisikika umbali mdogo tu kutoka pale
waliposimama. Ukungu mzito uliwafanya wasiweze
kuona hata mbele yao kuna nini, kwani hata wao
wenyewe walikuwa wakionana kuanzia viunoni kuja
juu. Ile sauti ya watu waliokuwa wakifanya ibada
iliendelea. Dakika chache baadae walisikia kama
mlango ukifunguliwa sehemu Fulani, kisha ukimya
ukawakabili.
CHAPISHO LA 15 MWISHO
Ule ukungu uliowazunguka ukaanza kupungua
taratibu na wote wakaweza kuona ardhi iliyopo eneo
lile, vito vya thamani vya dhahabu, almasi, yaspi,
quartz, coral na vingienvingi vilikuwa viking’azwa na
mwanga wa jua husio na joto la kuchoma bali la
kuburudisha lakini kila walipoangali hawakuliona jua
lenyewe isipokuwa mwanga tu.
Mbele yao kulikuwa na kidaraja kidogo sana chini
ya kidaraja hicho kulikuwa na mto lakini mto huo
uliwashangaza kwani ulionekana kupitisha kitu kama
uji wa buluu uliochanganyika na wekundu na weusi,
uji huo ulikuwa ukichemka. Nyuma yao wakasikia
kishindo cha ajabu, Amatagaimba akageuka na
kumwona Sherhazad akija kwa kasi, mkononi
mwake amekamata upinde wa ki-jini.
“Tuondokeni haraka!” Amatagaimba aliwaambia
Seidon na Anna.
“Tuelekee wapi?” Seidon akauliza huku mkono
mmoja ukiwa umemshika Anna na mwingine
umekamata lile fuvu.
“Vuka hilo daraja,” Amatagaimba akawaambia.
Seidon akaanza kuliendea lile daraja, lakini kabla
hajaanza kulivuka Anna akaponyoka mkononi
mwake na kubaki nyuma.
“Anna!” Seidon akaita.
“Naogopa kuvuka, daraja hilo minyororo yake
imeoza, tutatumbukia,” kabla hajamaliza kujibu
Anna, akajikuta akipigwa kikumbo kikali ambacho
kilimsukuma mpaka darajani. Seidon akiwa tayari
katikati ya daraja ambalo lilikuwa likinesa vibaya, na
minyororo iliyoshika daraja hilo kuanza kushindwa
kuhimili uzito, inayoanza kuachia mmoja baada ya
mwingine, akamdaka Anna na kukimbia nae kuvuka.
Walipokaribia mwisho mnyororo mmoja ukakatika
na lile daraja likainama upande mmoja.
“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza
vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi
kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari
ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya
daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa
mwisho wake sasa umefika.
“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon
alipiga kelele hukumkono wake mmoja tu ukiwa
umemshika Anna, “Shika kwenye daraja kisha jivute
juu,” Seidon akatoa maelekezo.
“Seidon siweziiii !” Anna alilia.
Wakati huo maopambano makali katika ya
Amatagaimba na Sherhazad yalikuwa yakiendelea,
Amatagaimba alikuwa akimzuia Malkia wa majini
kulifikia hilo daraja, pia alitaka Seidon amalize kazi
hiyo kwani baada tu ya daraja lile kulikuwa na ngazi
ambayo juu yake kulikuwa na sakafu kubwa na
Klakos ilikuwa hapo.
Seidon akashindwa afanye nini, amuachie Anna na
kwenda kurudisha lile fuvu au amshike Anna na
achelewe kufikisha lile fuvu wakati huohuo hajui nini
kitatokea.
§§§§§
Upande wa juu baada ya lile daraja kulikuwa na kitu
kama jukwaa lenye ngazi zisizopungu ishirini na
nne, na juu kabisa kulikuwa na kitu kama viti saba,
vitatu upande wa kushoto na vitatu upande wa kulia,
kisha kimoja kilikuwa mbele kabisa. juu ya hivi viti
sita kulikuwa na viumbe sita vilivyokaa katika
mtindo unaofanana, vyote vikiwa vimeweka viganja
vyao magotini na sura zao zilikuwa zimenama na
kuangalia chini. Kiti cha mbele kabisa kulikaa
kiumbe kingine, hiki kilikuwa kikubwa zaidi ya hivi
sita, hakikuwa na kichwa.
Viumbe vyote vilionekana havina uhai,ngozi zao
zilisinyaa kabisa vikaonekana kama vimepakwa
vumbi.
Sherhazad aliendelea kutembeza kichapo kikali kwa
Amatagaimba ambaye alijitahidi kupigana kadiri ya
uwezo wake. Sherhazad alionekana kuwa na nguvu
sana ili kutimiza lengo lake. Amatagaimba aliona
wazi kuwa wakileta mchezo hapo ndio mwisho wao
kwani Sherhazad alikuwa anatumia mbinu kali za
kichawi ambazo zilimfanya Amatagaimba kusahau
kila kitu na kupumbazika.
“Seidon, Seidon!” aliita kwa taabu, Seidon
akamtazama Amatagaimba aliyekuwa akitambaa
chini.
“Muachie Anna, nenda kapachike hilo fuvu kwa kile
kumbe kisicho na fuvu,” Amatagaimba alijitahidi
kupiga kelele.
Seidon alimtazama Anna akiwa bado ananing’inia na
huku amemshika kwa mkono wake mmoja ambao
ulikuwa unavuja jasho na ukitetemeka kuonesha
kuwa umefikia mwisho wa kustahamili, macho ya
Anna yalijaa machozi nay a Seidon yaliakisi hali ile.
“Niache Seidon, niache uende, asante kwa yote,”
Anna akafumba macho. Seidon hakuwa na lingine
zaidi ya kumwachia Anna ili yeye amalize kazi
iliyompasa kuifanya, hakupenda kumpoteza
mwanadada huyo lakini ilimbidi.
“Seidooooonnnn!!!!” Amatagaimba aliita, sauti ile
ilimgutusha Seidon asliyekuwa akimtazama Anna
kwa huzuni, akamwachia ili atumbukie kwenye ule
mto wa ajabu. Seidon hakubaki mahala pale, alivuta
hatu na kulimaliza lile daraja akaanza kupanda ngazi
kuelekea juu ambako Klakos ilikuwapo. Mara ghafla
upepo mkali ukaanza kuvuma na kumfanya Seidon
kushindwa hata kunyanyua mguu wake. Ule upepo
haukukoma uliendelea kumpa shida Seidon, nay eye
hakukubali alijilaza chini na kupanda zile ngazi huku
akitambaa kama nyoka.
Wakati huo Amatagaimba alikuwa amesitisha
mapambanao na Sharhazad ghafla baada ya
kutoweka kwake, Sherhazad na Ujini wake lakini
hakuwa na nguvu ya kupanda pale ilipo Klakos nah
ii ilitokana na uovu mwingi uliomzunguka, hivyo
alimwacha Amatagaimba na kuzunguka nyuma
kisha kuanza kutengeneza upepo mkali kutoka
katika kinywa chake kwa minajili ya kumpa
kipingamizi, Seidon.
Ilikuwa bado ngazi chache sana Seidon afike kwa
viumbe vya kwanza vile ambavyop kimoja kipo
kushoto kinaitwa Aminus na kile cha kulia kinaitwa
Sagitarius. Bado viumbe vile vilikuwa vimetulia
kimya hata havikutikisika; ni utando wa buibui tu
uliokuwa umewazunguka hapa na pale.
§§§§§
Anna alipoanguka baada ya kuachiwa mkono na
Seidon, alijigonga vibaya kwenye moja ya nguzo za
lile daraja, ivyo mwelekeo wa mdondoko wake
ukabadilika badala ya kwenda chini akasukumiwa
kushoto na kudondokas jirani na jiwe kubwa lenye
kung’aa sana, alifumbua macho aliyokuwa
kayafumba muda wote huo na kujikuta kama umbali
wa meta moja kutoka kwenye ule mto ambao maji
yake mazito yalikuwa kama uji mzito wenye rangi
mchanganyiko.
Kizunguzungu kikamshika akajivuta pembeni na
akulala kimya akipulizwa na ule upepo ambao
hakujua hatima yake nini, maumivu makali yalikuwa
katika eneo la mbavu zake ambapo alijgonga vibaya
katika ile nguzo.
§§§§§
Amatagaimba akajibiringisha pale alipo na kujificha
nyuma ya kitu kama ukuta mfupi, akachomoa uta
wake mgongoni akautia mshale na kuuvuta kwa
nguvu zake zote kuelekea kule ambako Cleopas
alikuwa amekaa, alipouachia, ule mshale ukakata
upepo kwa kasi na kuipita shingo ya Cleopas kwa
nukta chache sana kambla haujapiga hewa na ule
upepo ukakatika ghafla.
Seidon akanyanyuka haraka na kupanda kazi
iliyobaki akakanyaga eneo lile la Klakos, mara
alimwona Sherhazad akiwa na mshale uliochoma
kinywani mwake akija hewani kwa kasi na papo
hapo, lile fuvu likamtoka mikononi. Vile viumbe sita
bikawa kama vimepata uhai baada ya Seidon
kukanyaga Klakos. Macho ya vile viumbe Aminus,
Petrius, Segidus, Sagitarius, Hesmspitus na
Sectogamus yakaanza kung’aa na vichwa vyao
vikageuka kwa Seidon kisha vikageuka kwa ghafla
kuelekea kwa Cleopas na ndipo lile fuvu lilipotoka
mikononi mwa seidon na kwenda kunasa moja kwa
moja kwenye shingo ya Cleopas.
Viumbe sita vikainamisha vichwa vyao kama
vinavyotoa heshima. Nukta hiyohiyo. Sherhazad
alijikuta akipigwa na dharuba kali isiyoonekana,
akapaisha juu na kujibamiza kwenye ukuta kisha
akaanguka chini akihema, hakuweza hata kuvuta
hatua.
Vitu kama milipuko vikaanza kutokea kona
mbalimbali za lile shimo au pango, vitu anuai
vilivyotengenezwa kwa dhahabu safi vikaanza
kung’aa na kupendezsesha mle ndani. Seidon
aslipiga magoti, Amatagaimba palepale alipo naye
alifanya hivyo. Mara Sherhazad kutoka pale alipo
aliinuliwa juu na kitu kisichoonekana akashushwa
mbele ya Klakos kwa kishindo, alipotua tu, vazi lake
alilovaa likaanza kugandamana na ngozi yake.
“Jostrutus, Jostrutus, loctus loctus, abilante
sekretus …” yalikuwa maneno yaliyosikika kutoka
kila kona lakini hakuna aliyeonekana kufungua
kinywa chake. Sherhazad akatulia kimya sasa akiwa
kiumbe wa ajabu kabisa, Seidon ambayew hakua
mbali naye alikuwa akitetemeka kwa hofu.
“Jostrutus, ulikuwa una nia gani na viumbe hawa?”
Aminus na Sagitarius walimuuliza Sherhazad
ambaye jina lake katika ulimwengu wao alijulikana
kama Jostrutus.
Hakujibu akabaki anathema, vile viumbe vikageuka
kwa Cleopas ambaye sasa shingo yake ilikuwa
ikinesanesa baada ya kupata uhai kwa lile fuvu.
“Miaka 500 umekuwa ukisumbua viumbe hawa,
umekuwa ukiwapumbaza wasijue nini maana ya
Klakos, ulikuwa na nia gani?” Petrius na Hesmepitus
nao wakauliza kwa pamoja. Siri kubwa ya viumbe
hawa walikuwa wakitumia roho moja kila viumbe
viuwili vilivyotazamana. Upepo ukaanza kuvuma
tena lakini mara hii ulikuwa ni upepo mtulivu, wale
vioumbe wakainama vichwa vyao kumwelekea
Cleopas.
“Cambialus Serpentus, Cmbialus Serpentus…”
viumbe wale sita walianza kutamka kwa kurudia
rudia maneno hayo.
Macho ya Cleopas yakang’aa sana na kufanya kama
mwali wa moto uliotua moja kwa moja mwilini mwa
Sherhazad ambao wao walimtambua kama
Jostrutus. Ukelele wa ajabu ukamtoka Sharhazad na
mara mwili wake ukaanza kugeuka na kuwa chatu
mkubwa wa kutisha, na rangi ya vasi lake ndiyo
ikawa rangi ya ngozi yake.
Seidon alihisi kuzimia lakini alijikaza akitetemeka,
ule ukelele uliotoka katika joka lile sasa ulikuwa
ukisikika hewani lakini haikujulikana ulitoka wapi,
mara lile joka likatoka taratibu na kuingia katika ule
mto wenye maji mazito, likaishia humo na yale maji
yalionekana kama uji unaochemka kwa hasira.
Mwisho wa Sherhazad ukawa ndani ya mto huo.
§§§§§
“Mmetoka wapi?” sauti ilitoka kwa Cleopas na
kufanya mwangwi mkubwa ndani ya pango lile.
“Hamjui mlikotoka, lakini sisi tunajua mlikotoka, na
kila mmoja atarudishwa salama kule alikotoka,
lakini kila aliyefika mwisho wa mbio hana budi
kupata zawadi,” ile sauti iliendelea. Mara vile viu,be
vyote vikainama tena na mikono ta Cleopas ikatoka
magotini na kuwekwa kifuani mwake.
“Neema zote za ardhi na mbingu nakurudishieni kila
mmoja na alikotoka, mvua zitanyesha, mito yenu
itajaa maji, mazao na mashamba yenu vitarutubika
na njaa itaondoka katika uso wa nchi, vita na
matatizo vitakoma, lakini na alaaniwe kila aliyejaribu
kuvuruga mpango wa kuirudishia Klakos uhai. Sisi
ni viumbe tunaowapa uhai wa mimea na ninyi pia,”
mwangwi wa ile sauti uliendelea na mara hii radi
kali ilipasua anga kuashiria mvua kubwa iliyokuwa
ikinyesha huko duniani.
Kisha Cleopas akaonesha ishara ya kuwaita pale juu
wote watatu, Anna alihisi ghafla kutowekewa
maumivu yake, akainuka na kufuatana pamoja na
Amatagaimba na Seidon wakapiga magoti mbele ya
Cleopas, katikati ya Klakosi.
“Wewe ni shujaa wa Hamunaptra, na Msindikizaji
wako pia, safari hii ya hatari imewagharimu na
kuwapunguzia sehemu ya maisha yenu, Mnataka
niwape nini?” Cleopas akauliza kwa sauti yake
yenye mwangwi ambayo ilisikika pande zote lakini
yeye mwenyewe hakuonekana kufungua kinywa.
“Tunahitaji kurudi tulikotoka,” Seidon, Amatagaimba
na Anna walijibu kwa pamoja.
“Fumbeni macho, msiwaze lolote vichwani mwenu,”
Cleopas akawaambia nao wakatii,
Upepo Mwanana ulianza kuvuma, kila mmoja wao
alijiona kama anapaa angani, hali ya utulivu ilitawala
kwenye vichwa vyao.
Hospitali ya Dar El Shefa – Cairo, Misri
WAHUDUMU wa Hospitali walimshusha Anna Davis
kutoka katika kitabda maalumu na kumlaza kwenye
kitanda cha wosini, alikuwa hajitambui, fahamu zote
zilimtoka kutikana na lile janga la kule kwenye
mapiramidi. Wanafunzi wenzake walikuwa tayari
wamekata tamaa ukizingatia mmoja wao alikuwa
amepoteza maisha.
“Ataamka muda wowote huyu!” sauti hio ilipenya
kwa mbali sana ngoma za masikio ya Anna,
hakuelewa nini kinatokea, akili yake ilikuwa ikirudi
taratibu kutoka katika safari ya mbali, kutoka katika
ulimwengu wa chini kabisa.
Mara akakurupuka na kuanza kuhema kwa nguvu
kama aliyekuwa anakimbizwa.
“Ameamka, ameamka!” sauti ya muuguzi ilimshtua
mawazo Anna.
“Niko wapi hapa? Niko wapi? Amatagaimba, Seidon
wako wapi? Wako wapi?” alikuwa akiongea kama
mtu anayeweweseka.
“Anna, Anna tulia Anna, unanifahamu mimi?”
Anna akatulia kiasi na kumtazama mtu aliyekuwa
mbele yake, “Ndiyo nakufahamu,” akajibu.
“Mimi ni nani?” yule mtu akauliza.
“Profesa Masati,” Akajibu, kisha akaanza
kuwatazama mmoja baada ya mwingine,
akamtambua na mwanafunzi mwingine aliyekuwa
hapo.
“Inaonekana alikuwa kwenye maono mazito sana
katika mzimio wake, labda baadae tutamuuliza kwa
tuo ili tujue nini alikiona,” Daktari bingwa wa
magonjwa ya akili ambaye aliwaambia tangu
mwanzo kuwa kutoka na vipimo, Ubongo wake
umepata shida kidogo hivyo anweza kuamka akiwa
hana kumbukumbu au nusu kichaa.
Anna alilala kitandani, lakini mara alikuwa anacheka
mwenyewe na mara alikuwa ananuna au kutajka
majina ya vitu visivyoeleweka.
“Akae hapa kwa wiki zaidi ili nimwangalie namna ya
kumsaidia” yule daktari akamwambia Profesa
Masati na wakakubaliana hilo.
Jangwa la Uajemi
JUA kali lilikuwa likiwaka, vumbi lilitimka kama
limetumwa. Watu wawili waliokuwa juu ya ngamia
walitazamana bila kuongea, lakini baadae mmoja
alivunja ukimya.
“Amatagaimba, Shujaa wa Msitu wa Solondo,
Asante sana kwa kazi hii, Baraka za Klakos ziwe
nawe,” Seidon akamwambia Amatagaimba.
“Nawe pia, Mpiga mbio, Shujaa wa Hamunaptra,
kama zilivyo mbali Mashariki na Magaribi nasi nafsi
zetu hazitaonana tena,” Amatagaimba akashuka
katika Ngamia na Seidon akafanya hivyo,
wakakumbatiana na kuagana kisha kila mmoja
akaenda upande wake.
≈ MWISHO ≈
0766974865 .... 0672160016
 
Sauti hiyo ilisikika umbali mdogo tu kutoka pale
waliposimama. Ukungu mzito uliwafanya wasiweze
kuona hata mbele yao kuna nini, kwani hata wao
wenyewe walikuwa wakionana kuanzia viunoni kuja
juu. Ile sauti ya watu waliokuwa wakifanya ibada
iliendelea. Dakika chache baadae walisikia kama
mlango ukifunguliwa sehemu Fulani, kisha ukimya
ukawakabili.
CHAPISHO LA 15 MWISHO
Ule ukungu uliowazunguka ukaanza kupungua
taratibu na wote wakaweza kuona ardhi iliyopo eneo
lile, vito vya thamani vya dhahabu, almasi, yaspi,
quartz, coral na vingienvingi vilikuwa viking’azwa na
mwanga wa jua husio na joto la kuchoma bali la
kuburudisha lakini kila walipoangali hawakuliona jua
lenyewe isipokuwa mwanga tu.
Mbele yao kulikuwa na kidaraja kidogo sana chini
ya kidaraja hicho kulikuwa na mto lakini mto huo
uliwashangaza kwani ulionekana kupitisha kitu kama
uji wa buluu uliochanganyika na wekundu na weusi,
uji huo ulikuwa ukichemka. Nyuma yao wakasikia
kishindo cha ajabu, Amatagaimba akageuka na
kumwona Sherhazad akija kwa kasi, mkononi
mwake amekamata upinde wa ki-jini.
“Tuondokeni haraka!” Amatagaimba aliwaambia
Seidon na Anna.
“Tuelekee wapi?” Seidon akauliza huku mkono
mmoja ukiwa umemshika Anna na mwingine
umekamata lile fuvu.
“Vuka hilo daraja,” Amatagaimba akawaambia.
Seidon akaanza kuliendea lile daraja, lakini kabla
hajaanza kulivuka Anna akaponyoka mkononi
mwake na kubaki nyuma.
“Anna!” Seidon akaita.
“Naogopa kuvuka, daraja hilo minyororo yake
imeoza, tutatumbukia,” kabla hajamaliza kujibu
Anna, akajikuta akipigwa kikumbo kikali ambacho
kilimsukuma mpaka darajani. Seidon akiwa tayari
katikati ya daraja ambalo lilikuwa likinesa vibaya, na
minyororo iliyoshika daraja hilo kuanza kushindwa
kuhimili uzito, inayoanza kuachia mmoja baada ya
mwingine, akamdaka Anna na kukimbia nae kuvuka.
Walipokaribia mwisho mnyororo mmoja ukakatika
na lile daraja likainama upande mmoja.
“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza
vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi
kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari
ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya
daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa
mwisho wake sasa umefika.
“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon
alipiga kelele hukumkono wake mmoja tu ukiwa
umemshika Anna, “Shika kwenye daraja kisha jivute
juu,” Seidon akatoa maelekezo.
“Seidon siweziiii !” Anna alilia.
Wakati huo maopambano makali katika ya
Amatagaimba na Sherhazad yalikuwa yakiendelea,
Amatagaimba alikuwa akimzuia Malkia wa majini
kulifikia hilo daraja, pia alitaka Seidon amalize kazi
hiyo kwani baada tu ya daraja lile kulikuwa na ngazi
ambayo juu yake kulikuwa na sakafu kubwa na
Klakos ilikuwa hapo.
Seidon akashindwa afanye nini, amuachie Anna na
kwenda kurudisha lile fuvu au amshike Anna na
achelewe kufikisha lile fuvu wakati huohuo hajui nini
kitatokea.
§§§§§
Upande wa juu baada ya lile daraja kulikuwa na kitu
kama jukwaa lenye ngazi zisizopungu ishirini na
nne, na juu kabisa kulikuwa na kitu kama viti saba,
vitatu upande wa kushoto na vitatu upande wa kulia,
kisha kimoja kilikuwa mbele kabisa. juu ya hivi viti
sita kulikuwa na viumbe sita vilivyokaa katika
mtindo unaofanana, vyote vikiwa vimeweka viganja
vyao magotini na sura zao zilikuwa zimenama na
kuangalia chini. Kiti cha mbele kabisa kulikaa
kiumbe kingine, hiki kilikuwa kikubwa zaidi ya hivi
sita, hakikuwa na kichwa.
Viumbe vyote vilionekana havina uhai,ngozi zao
zilisinyaa kabisa vikaonekana kama vimepakwa
vumbi.
Sherhazad aliendelea kutembeza kichapo kikali kwa
Amatagaimba ambaye alijitahidi kupigana kadiri ya
uwezo wake. Sherhazad alionekana kuwa na nguvu
sana ili kutimiza lengo lake. Amatagaimba aliona
wazi kuwa wakileta mchezo hapo ndio mwisho wao
kwani Sherhazad alikuwa anatumia mbinu kali za
kichawi ambazo zilimfanya Amatagaimba kusahau
kila kitu na kupumbazika.
“Seidon, Seidon!” aliita kwa taabu, Seidon
akamtazama Amatagaimba aliyekuwa akitambaa
chini.
“Muachie Anna, nenda kapachike hilo fuvu kwa kile
kumbe kisicho na fuvu,” Amatagaimba alijitahidi
kupiga kelele.
Seidon alimtazama Anna akiwa bado ananing’inia na
huku amemshika kwa mkono wake mmoja ambao
ulikuwa unavuja jasho na ukitetemeka kuonesha
kuwa umefikia mwisho wa kustahamili, macho ya
Anna yalijaa machozi nay a Seidon yaliakisi hali ile.
“Niache Seidon, niache uende, asante kwa yote,”
Anna akafumba macho. Seidon hakuwa na lingine
zaidi ya kumwachia Anna ili yeye amalize kazi
iliyompasa kuifanya, hakupenda kumpoteza
mwanadada huyo lakini ilimbidi.
“Seidooooonnnn!!!!” Amatagaimba aliita, sauti ile
ilimgutusha Seidon asliyekuwa akimtazama Anna
kwa huzuni, akamwachia ili atumbukie kwenye ule
mto wa ajabu. Seidon hakubaki mahala pale, alivuta
hatu na kulimaliza lile daraja akaanza kupanda ngazi
kuelekea juu ambako Klakos ilikuwapo. Mara ghafla
upepo mkali ukaanza kuvuma na kumfanya Seidon
kushindwa hata kunyanyua mguu wake. Ule upepo
haukukoma uliendelea kumpa shida Seidon, nay eye
hakukubali alijilaza chini na kupanda zile ngazi huku
akitambaa kama nyoka.
Wakati huo Amatagaimba alikuwa amesitisha
mapambanao na Sharhazad ghafla baada ya
kutoweka kwake, Sherhazad na Ujini wake lakini
hakuwa na nguvu ya kupanda pale ilipo Klakos nah
ii ilitokana na uovu mwingi uliomzunguka, hivyo
alimwacha Amatagaimba na kuzunguka nyuma
kisha kuanza kutengeneza upepo mkali kutoka
katika kinywa chake kwa minajili ya kumpa
kipingamizi, Seidon.
Ilikuwa bado ngazi chache sana Seidon afike kwa
viumbe vya kwanza vile ambavyop kimoja kipo
kushoto kinaitwa Aminus na kile cha kulia kinaitwa
Sagitarius. Bado viumbe vile vilikuwa vimetulia
kimya hata havikutikisika; ni utando wa buibui tu
uliokuwa umewazunguka hapa na pale.
§§§§§
Anna alipoanguka baada ya kuachiwa mkono na
Seidon, alijigonga vibaya kwenye moja ya nguzo za
lile daraja, ivyo mwelekeo wa mdondoko wake
ukabadilika badala ya kwenda chini akasukumiwa
kushoto na kudondokas jirani na jiwe kubwa lenye
kung’aa sana, alifumbua macho aliyokuwa
kayafumba muda wote huo na kujikuta kama umbali
wa meta moja kutoka kwenye ule mto ambao maji
yake mazito yalikuwa kama uji mzito wenye rangi
mchanganyiko.
Kizunguzungu kikamshika akajivuta pembeni na
akulala kimya akipulizwa na ule upepo ambao
hakujua hatima yake nini, maumivu makali yalikuwa
katika eneo la mbavu zake ambapo alijgonga vibaya
katika ile nguzo.
§§§§§
Amatagaimba akajibiringisha pale alipo na kujificha
nyuma ya kitu kama ukuta mfupi, akachomoa uta
wake mgongoni akautia mshale na kuuvuta kwa
nguvu zake zote kuelekea kule ambako Cleopas
alikuwa amekaa, alipouachia, ule mshale ukakata
upepo kwa kasi na kuipita shingo ya Cleopas kwa
nukta chache sana kambla haujapiga hewa na ule
upepo ukakatika ghafla.
Seidon akanyanyuka haraka na kupanda kazi
iliyobaki akakanyaga eneo lile la Klakos, mara
alimwona Sherhazad akiwa na mshale uliochoma
kinywani mwake akija hewani kwa kasi na papo
hapo, lile fuvu likamtoka mikononi. Vile viumbe sita
bikawa kama vimepata uhai baada ya Seidon
kukanyaga Klakos. Macho ya vile viumbe Aminus,
Petrius, Segidus, Sagitarius, Hesmspitus na
Sectogamus yakaanza kung’aa na vichwa vyao
vikageuka kwa Seidon kisha vikageuka kwa ghafla
kuelekea kwa Cleopas na ndipo lile fuvu lilipotoka
mikononi mwa seidon na kwenda kunasa moja kwa
moja kwenye shingo ya Cleopas.
Viumbe sita vikainamisha vichwa vyao kama
vinavyotoa heshima. Nukta hiyohiyo. Sherhazad
alijikuta akipigwa na dharuba kali isiyoonekana,
akapaisha juu na kujibamiza kwenye ukuta kisha
akaanguka chini akihema, hakuweza hata kuvuta
hatua.
Vitu kama milipuko vikaanza kutokea kona
mbalimbali za lile shimo au pango, vitu anuai
vilivyotengenezwa kwa dhahabu safi vikaanza
kung’aa na kupendezsesha mle ndani. Seidon
aslipiga magoti, Amatagaimba palepale alipo naye
alifanya hivyo. Mara Sherhazad kutoka pale alipo
aliinuliwa juu na kitu kisichoonekana akashushwa
mbele ya Klakos kwa kishindo, alipotua tu, vazi lake
alilovaa likaanza kugandamana na ngozi yake.
“Jostrutus, Jostrutus, loctus loctus, abilante
sekretus …” yalikuwa maneno yaliyosikika kutoka
kila kona lakini hakuna aliyeonekana kufungua
kinywa chake. Sherhazad akatulia kimya sasa akiwa
kiumbe wa ajabu kabisa, Seidon ambayew hakua
mbali naye alikuwa akitetemeka kwa hofu.
“Jostrutus, ulikuwa una nia gani na viumbe hawa?”
Aminus na Sagitarius walimuuliza Sherhazad
ambaye jina lake katika ulimwengu wao alijulikana
kama Jostrutus.
Hakujibu akabaki anathema, vile viumbe vikageuka
kwa Cleopas ambaye sasa shingo yake ilikuwa
ikinesanesa baada ya kupata uhai kwa lile fuvu.
“Miaka 500 umekuwa ukisumbua viumbe hawa,
umekuwa ukiwapumbaza wasijue nini maana ya
Klakos, ulikuwa na nia gani?” Petrius na Hesmepitus
nao wakauliza kwa pamoja. Siri kubwa ya viumbe
hawa walikuwa wakitumia roho moja kila viumbe
viuwili vilivyotazamana. Upepo ukaanza kuvuma
tena lakini mara hii ulikuwa ni upepo mtulivu, wale
vioumbe wakainama vichwa vyao kumwelekea
Cleopas.
“Cambialus Serpentus, Cmbialus Serpentus…”
viumbe wale sita walianza kutamka kwa kurudia
rudia maneno hayo.
Macho ya Cleopas yakang’aa sana na kufanya kama
mwali wa moto uliotua moja kwa moja mwilini mwa
Sherhazad ambao wao walimtambua kama
Jostrutus. Ukelele wa ajabu ukamtoka Sharhazad na
mara mwili wake ukaanza kugeuka na kuwa chatu
mkubwa wa kutisha, na rangi ya vasi lake ndiyo
ikawa rangi ya ngozi yake.
Seidon alihisi kuzimia lakini alijikaza akitetemeka,
ule ukelele uliotoka katika joka lile sasa ulikuwa
ukisikika hewani lakini haikujulikana ulitoka wapi,
mara lile joka likatoka taratibu na kuingia katika ule
mto wenye maji mazito, likaishia humo na yale maji
yalionekana kama uji unaochemka kwa hasira.
Mwisho wa Sherhazad ukawa ndani ya mto huo.
§§§§§
“Mmetoka wapi?” sauti ilitoka kwa Cleopas na
kufanya mwangwi mkubwa ndani ya pango lile.
“Hamjui mlikotoka, lakini sisi tunajua mlikotoka, na
kila mmoja atarudishwa salama kule alikotoka,
lakini kila aliyefika mwisho wa mbio hana budi
kupata zawadi,” ile sauti iliendelea. Mara vile viu,be
vyote vikainama tena na mikono ta Cleopas ikatoka
magotini na kuwekwa kifuani mwake.
“Neema zote za ardhi na mbingu nakurudishieni kila
mmoja na alikotoka, mvua zitanyesha, mito yenu
itajaa maji, mazao na mashamba yenu vitarutubika
na njaa itaondoka katika uso wa nchi, vita na
matatizo vitakoma, lakini na alaaniwe kila aliyejaribu
kuvuruga mpango wa kuirudishia Klakos uhai. Sisi
ni viumbe tunaowapa uhai wa mimea na ninyi pia,”
mwangwi wa ile sauti uliendelea na mara hii radi
kali ilipasua anga kuashiria mvua kubwa iliyokuwa
ikinyesha huko duniani.
Kisha Cleopas akaonesha ishara ya kuwaita pale juu
wote watatu, Anna alihisi ghafla kutowekewa
maumivu yake, akainuka na kufuatana pamoja na
Amatagaimba na Seidon wakapiga magoti mbele ya
Cleopas, katikati ya Klakosi.
“Wewe ni shujaa wa Hamunaptra, na Msindikizaji
wako pia, safari hii ya hatari imewagharimu na
kuwapunguzia sehemu ya maisha yenu, Mnataka
niwape nini?” Cleopas akauliza kwa sauti yake
yenye mwangwi ambayo ilisikika pande zote lakini
yeye mwenyewe hakuonekana kufungua kinywa.
“Tunahitaji kurudi tulikotoka,” Seidon, Amatagaimba
na Anna walijibu kwa pamoja.
“Fumbeni macho, msiwaze lolote vichwani mwenu,”
Cleopas akawaambia nao wakatii,
Upepo Mwanana ulianza kuvuma, kila mmoja wao
alijiona kama anapaa angani, hali ya utulivu ilitawala
kwenye vichwa vyao.
Hospitali ya Dar El Shefa – Cairo, Misri
WAHUDUMU wa Hospitali walimshusha Anna Davis
kutoka katika kitabda maalumu na kumlaza kwenye
kitanda cha wosini, alikuwa hajitambui, fahamu zote
zilimtoka kutikana na lile janga la kule kwenye
mapiramidi. Wanafunzi wenzake walikuwa tayari
wamekata tamaa ukizingatia mmoja wao alikuwa
amepoteza maisha.
“Ataamka muda wowote huyu!” sauti hio ilipenya
kwa mbali sana ngoma za masikio ya Anna,
hakuelewa nini kinatokea, akili yake ilikuwa ikirudi
taratibu kutoka katika safari ya mbali, kutoka katika
ulimwengu wa chini kabisa.
Mara akakurupuka na kuanza kuhema kwa nguvu
kama aliyekuwa anakimbizwa.
“Ameamka, ameamka!” sauti ya muuguzi ilimshtua
mawazo Anna.
“Niko wapi hapa? Niko wapi? Amatagaimba, Seidon
wako wapi? Wako wapi?” alikuwa akiongea kama
mtu anayeweweseka.
“Anna, Anna tulia Anna, unanifahamu mimi?”
Anna akatulia kiasi na kumtazama mtu aliyekuwa
mbele yake, “Ndiyo nakufahamu,” akajibu.
“Mimi ni nani?” yule mtu akauliza.
“Profesa Masati,” Akajibu, kisha akaanza
kuwatazama mmoja baada ya mwingine,
akamtambua na mwanafunzi mwingine aliyekuwa
hapo.
“Inaonekana alikuwa kwenye maono mazito sana
katika mzimio wake, labda baadae tutamuuliza kwa
tuo ili tujue nini alikiona,” Daktari bingwa wa
magonjwa ya akili ambaye aliwaambia tangu
mwanzo kuwa kutoka na vipimo, Ubongo wake
umepata shida kidogo hivyo anweza kuamka akiwa
hana kumbukumbu au nusu kichaa.
Anna alilala kitandani, lakini mara alikuwa anacheka
mwenyewe na mara alikuwa ananuna au kutajka
majina ya vitu visivyoeleweka.
“Akae hapa kwa wiki zaidi ili nimwangalie namna ya
kumsaidia” yule daktari akamwambia Profesa
Masati na wakakubaliana hilo.
Jangwa la Uajemi
JUA kali lilikuwa likiwaka, vumbi lilitimka kama
limetumwa. Watu wawili waliokuwa juu ya ngamia
walitazamana bila kuongea, lakini baadae mmoja
alivunja ukimya.
“Amatagaimba, Shujaa wa Msitu wa Solondo,
Asante sana kwa kazi hii, Baraka za Klakos ziwe
nawe,” Seidon akamwambia Amatagaimba.
“Nawe pia, Mpiga mbio, Shujaa wa Hamunaptra,
kama zilivyo mbali Mashariki na Magaribi nasi nafsi
zetu hazitaonana tena,” Amatagaimba akashuka
katika Ngamia na Seidon akafanya hivyo,
wakakumbatiana na kuagana kisha kila mmoja
akaenda upande wake.
≈ MWISHO ≈
0766974865 .... 0672160016

Safi sana... Story nzuri sana..

Chapter closed



Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom