Riwaya: Dunia ndani ya dunia mpya

Riwaya: Dunia ndani ya dunia mpya

saul19

Member
Joined
Aug 11, 2015
Posts
35
Reaction score
9
THE WORLD IN THE NEW WORLD
(Dunia ndani ya dunia mpya).

SEHEMU YA…………………………01.
Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
Email: Saulstewarty@gmail.com ******

Tarehe 29-09-2008. Dar es Salaam - Tanzania.
Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda ndani ya jiji la Dar es salaam, ni baada ya mfuatano wa matukio mengi ya kustaajabisha yaliyomfanya kila mmoja kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani ya Tanzania kuwa makini kufuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya jiji hilo.

Ulikuwa ni mwezi mmoja sasa umepita tangu kupotea kwa binti mmoja mrembo kupindukia aliyejipatia umaarufu mkubwa baada ya kulitwaa taji la Miss Tanzania 2008, aliitwa CATHERINE PETER, binti mwenye umri yapata miaka 23.
Ikiwa ni siku mbili tu baada ya Catherine kutwaa taji hilo la miss Tanzania, alipotea ghafula na hakuna mtu aliyejua mahali alipokwenda, ilibidi wazazi wake watoe taarifa kituo cha polisi na hapo msako mkali wa kumtafuta Catherin ulianza mara moja.

Waandishi wa habari pamoja na watu wengine wengi bado walitamani kujua mawili matatu kumuhusu mlimbwende huyo ambaye ama kwa hakika alikuwa na sifa zote za kulitwaa taji hilo la Miss Tanzania 2008, lakini Catherine hakuwepo tena.

Taarifa za kupotea kwa binti huyo mrembo Catherine zilikuwa za ghafula na kushtusha mno, hali hii iliwafanya wapambe na mashabiki wake kuisisitiza serikali kuhakikisha wanampata Catherine mapema akiwa salama salmini.
****

KELVIN JOHNSON kijana mwenye umri wa miaka 25, alikuwa ni mmoja kati ya askari makini wa kitengo cha upelelezi waliopewa jukumu la kuifuatilia kesi ya kupotea kwa Catherine.
Kelvin akiwa ndio kwanza ana miaka miwili tu tangu aanze kazi hii ya upelelezi tayari alikuwa amejipatia sifa na umaarufu mkubwa kutokana na namna alivyokuwa akifanya kazi kwa kujituma na kwa usahihi,
pamoja na umri wake kuwa mdogo lakini Kelvin alikuwa akifanya kazi vizuri mno kuwazidi hata askari wengine waliokuwa na uzoefu.

hali hii ilimfanya Kelvin kuaminika zaidi na wakubwa wake na ndio sababu alikuwa miongoni mwa askari watano waliokabidhiwa jukumu la kuipeleleza kesi hii ya Miss Catherine.

Mara tu baada ya Kelvin kukabidhiwa kesi hii alianza upelelezi mara moja akishirikiana na askari wenzake wanne, lakini Kelvin alikuwa akitumia mda mwingi sana kuifuatilia kesi hii wakati mwingine alilazimika kufanya kazi hadi nyakati za usiku jambo lililomshangaza sana kiongozi wa timu yake waliyependa kumuita Chief Mark.
Ni kweli Chief Mark alielewa kuwa Kelvin ni askari bora anaefanya kazi kwa kujituma sana lakini katika kesi hii ya Catherine, Kelvin alionekana kuvuka mipaka.
alikuwa akiifanya kazi kwa nguvu kubwa sana wakati mwingine alisahau hata kula hali iliyomfanya Chief Mark amtilie shaka.
Waliendelea kufanya kazi kama kawaida lakini safari hii Chief mark alikuwa akifuatilia kila jambo aliloifanya Kelvin kwa siri.
Siku chache baadae Chief Mark alimuita Kelvin ofisini kwake.

“Kelvin unaweza kuniambia wewe na Catherine mnajuana kwa mda gani mpaka sasa hivi?” Aliuliza Chief Mark.
Swali hili lilimfanya Kelvin ashituke kidogo lakini akajitahidi kuficha mshtuko wake.
“Ca..catherine?, catherine yupi?” Kelvin alijibu kwa swali.
“Catherine peter, miss Tanzania 2008 aliyepotea mwezi mmoja uliopita, umejuana nae wapi na ni kwa mda gani mpaka sasa?” Chief Mark aliuliza tena kwa msisitizo zaidi.

Kelvin alitoa macho kwa mshangao, hakutegemea kabisa kama kiongozi wake wa kazi angemuliza swali hilo.

Ni kweli Kelvin anafahamiana vizuri sana Catherine lakini alifanya jambo hilio kuwa siri, hakutamani mtu yoyote wakiwemo polisi wenzake wajue.
Kelvin alibaki ametulia kimya huku akijaribu kumtafakari Chief mark akiwa haelewi ni vipi ameweza kugundua kama yeye na Catherine wanafahamiana.

“Kelvin mbona haunijibu swali langu, okay basi haina shida nakuuliza swali lingine,
Ni kwanini unatumia nguvu kubwa sana ukijaribu kumsaidia Catherine mwanamke ambaye alikuacha na kukutamkia wazi kuwa hakupendi?”
“Heee!! Chief umejuaje haya yote?”.
“Kumbuka mimi ni mpelelezi wa mda mrefu zaidi yako Kelvin na istoshe ni mkubwa wako wa kazi, huna haja ya kuendelea kunificha”.
Yalikuwa ni maneno yaliyomfanya Kelvin akabiki kimya kwa sekunde kadhaa,
“Ni kweli mimi na Catherine tunafahamiana, tulikuwa na mahusiano yaani eeeh! Mmh, tulikuwa tuna…” Kelvin alisita kidogo kueleza
“Kwa nini mlitengana?”
“Aaah! Ni hostoria ndefu sana chief, ila bado nampenda sana Cathe, naamini na yeye pia ananipenda japo ndio ni kweli kwa mara ya mwisho aliniambia kuwa hanipendi lakini……. ” Kelvin aliongea kwa masikitiko mwisho Chief Mark alinyoosha mkono akimtaka asiongee zaidi.

“Okay inatosha, hayo ni mambo yako mwenyewe sitaki kufahamu zaidi kuhusu mahusiano yenu, ila pata muda wa kupumzika na usipende kufanya kazi peke yako, hii kazi ni ya timu nzima haijalishi tunamfahamu au hatumfahamu Catherine.” Alisema Chief Mark kisha akaondoka na kumuacha Kelvin ndani ya ofisi yake hali akiwa na mawazo mengi a akitafakari mambo kadhaa yalyotokea kipindi cha nyuma pindi alipokuwa pamoja na Catherine.
“Am so sorry Catherine, I miss you much”(Samahani sana Catherine, nimekukumbuka mno) Alisema Kelvin huku akisimama kwa unyonge na kuondoka.
*********

Upelelezi uliendelea huku safari hii Kelvin akijitahidi kushirikiana na timu yake kama alivyoelekezwa na Chief mark,
Baada ya upelelezi wa kina hatimae walifanikiwa kumbaini dereva taksi mmoja ambaye ndiye aliyembeba Miss Catherine kwa mara ya mwisho kabla ya kupotea.
Dereva huyu alijulikana kwa jina la Thomas Maziku, picha zake zilisambazwa katika maeneo mbalimbali huku Thomas akihusushwa moja kwa moja na tukio la kumteka Catherine.

Kwa msaada wa raia hatimae polisi walifankiwa kupajua eneo aliloishi Thomas nje kidogo na jiji la Dar es salaam, haraka walifika eneo hilo lakini haikuwa kazi rahisi kumkamata kwani Thomas alikuwa akiishi kama gaidi, alimiliki siraha nyingi za moto.
Baada ya purukushani nzito na ya aina yake hatimae askari walifanikiwa kumkamata bwana Thomas wakafika nae kituo cha polisi kwa ajili ya hamojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kusema mahali alipompeleka Catherine.
********

Baada ya Kelvin kuhakikisha mtuhumiwa ameingizwa ndani ya kituo cha polisi aliondoka taratibu hali alionekana kuchoka sana baada ya purukushani nzito wakati wa kumkamata Bwana Thomas.
Alipiga hatua taratibu huku akijaribu kuwakwepa waandishi wa habari ambao walifika mapema sana baada ya kupata habari kuwa Bwana Thomas amekamatwa.

Wakati Kelvin akizidi kwenda mara ghafula alihisi kunamtu amemshika mkono kwa nyuma, haraka aligeuka kutazama.
Alishangaa kumuona mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka kama saba hivi akiwa ameung’ang’ania mkono wake wa kushoto, mtoto huyo alikuwa amevaa sare ya shule ya msingi akiwa na begi lake mgongoni.

Kelvin alimtazama yule mtoto kwa sekunde kazaa, yule mtoto nae alimtazama Kelvin huku akiachia tabasamu pana kisha akaingiza mkono kwenye mfuko wa sketi yake akatoa kitu fulani na kumpatia Kelvin.

“Unaitwa nani mtoto mzuri” Kelvin alipokea kile kitu alichopewa huku akimtupia swali yule mtoto, kisha akatazama ni kitu gani amepewa, ilikuwa ni saa nzuri ya kike yenye umbo la kopa.
Kelvin alishtuka kidogo baada ya kuiona ile saa, haraka aliigeuza upande wa nyuma na kuitazama kwa makini hapo alijikuta anashtuka zaidi
Kelvin aliikumbuka vizuri saa hiyo, ilikuwa ni zawadi pekee aliyompatia Catherine miaka mingi iliyopita baada ya Catherine kumaliza darasa la saba, nyuma ya saa hiyo kulikuwa na picha dogo iliyoonyesha sura Catherine
Ni saa ambayo Catherine allikuwa akiithamini kuliko kitu kingine chochote.
“umepata wapi hii saa?” Aliuliza Kelvin huku akigeuka kumuangalia yule mtoto lakini hakumuona tena, tayari alisha ondoka .
Aliangaza macho huku na huku kwa mbali alimuona yule mtoto anakimbia na kutokomea kwenye msongamano mkubwa wa watu.
Haraka Kelvin nae alianza kupiga hatua ndefu ndefu kumfuata, hakutaka kabisa kumuacha aende kwani alikuwa na maswali mengi sana ya kumuliza.

Yule mtoto alizidi kukimbia huku Kelvin nae akizidi kumfuata nyuma hali akimuangalia kwa makini asije kumpotea.
Ilikuwa hivyo kwa zaidi ya dakika 15, Mwisho Kelvin alimuona yule mtoto anaingia ndani ya jengo moja kubwa lenye ghorofa kadhaa.
Haraka Kelvin nae pasipo kuwa na wasiwasi wowote elienda moja kwa moja na kuingia ndani ya lile jengo,
Baada tu ya Kelvin kuingia ndani mara milango miwili ya jengo hilo akajifunga lakini Kelvin hakuona hilo.
**********

Ndani kulikuwa kimya kabisa, ilionekana ni eneo ambalo hutumiaka kama ukumbi wa starehe lakini hakukuwa na mtu hata mmoja wakati huo.
Kelvin aliendelea kuangaza macho huku na huku akijaribu kumtafuta yule mtoto kwani alikuwa na asilimia mia moja kwamba yupo mle ndani.
ni kweli baada ya muda alifanikiwa kumuona yule mtoto akiwa amepanda ngazi na kufika eneo la juu kabisa.
Baada ya yule mtoto kukutanisha macho na Kelvin alitabasamu na kumpungia mkono kisha akakimbia tena, hali hii ilimshangaza kidogo Kelvin lakini hakusita kuendelea kumfuata.

Alipandisha ngazi upesi upesi na hatimae alifika juu kabisa eneo alilomuona yule mtoto kwa mara ya mwisho, akafuata uelekeo ule alikokimbilia.

Kelvin aliendelea kupenya na kuingia ndani zaidi ya jengo hilo lilokuwa na utulivu wa ajabu, alionekana kuwa na ujasiri wa ajabu kutokana na kazi yake aliyokuwa akiifanya, tayari alishakutana na matukio mengi ya kutisha hivyo mazingira ya jengo hilo kwake aliyaona kawaida tu.
Alianza kunyata akifuata uelekeo wa korido moja ndefu.

Wakati anazidi kwenda mara ghafula taa zilizima na kuwaka, zikazima na kuwaka tena kisha kikazima tena jumla, kukawa na giza zito eneo lile.
Wakati Kelvin akizidi kutahamaki mara ghafula ukatokea mkikisiko mkubwa, kufumba na kufumbua eneo alilokuwa amesimama likaanza kushuka chini kwa kasi.

Hali hii ilimtisha sana Kelvin akatamani kupiga kelele za kuomba msada lakini akasita akalala chini na kujishikilia vizuri kwenye kile kitu kilichokuwa kikimpeleka chini kwa kasi.

Dakika tatu baadaen Kelvin alilushwa na kujikuta anadondoka chini kwenye ene.o lingine tofauti, mara hiyo taa zilianza kuwaka moja baada ya nyingine kukawa na mwanga tena.

Kelvin alijikuta yupo ndani ya chumba kimoja kikubwa sana, kwa mtazamo wa haraka haraka Kelvin aliweza kulifananisha eneo hilo kama eneo la bunge, lakini viti na meza vilikuwa wazi hakukuwa na mtu hata mmoja.
Akiwa katika hali ya kushangaa mara ghafula alisikia vyishindo mbele yake, haraka aliina macho yake kutazama.
kwa mbali aliwaona wanaume watano wanakuja upande wake taratibu. Wanne walikuwa wamevaa suti nadhifu zenye rangi nyekundu, mmoja alivaa suti nyeupe mkononi akiwa ameshikilia mkongojo wenye rangi nyeupe pia.

Kelvin alibaki amekaa palepale chini, hakuweza kurudi nyuma wala kusogea mbele.
Mwisho wale watu walifika na kusimama mbele yake.
Kelvin aliwatazama kwa zamu mmoja baada ya mwingine. Zilikuwa ni sura ngeni kabisa kwake.

“Kelvin Johnson, bila shaka upo hapa kwa ajili ya kumtafuta mtu humihu sana kwako, Catherine peter” Alisema yule mzee aliyevaa suti nyeupe hali akiachia tabasamu mwanana.

JE NINI KITAFUATA?
=>Kelvin yupo eneo salama?
=>Catherine je, yuko wapi?
Nini maana ya Dunia ndani ya Dunia mpya.
Huu ni mwanzo tu,
FB_IMG_1648366415571.jpg

ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA.
 
View attachment 2165733

ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA.
naamini kuna burudani ya kutosha hapa na hatutojutia na pia utaheshimu kiu ya mashabiki
 
THE WORLD IN THE NEW WORLD
(Dunia ndani ya dunia mpya).
SEHEMU YA…………………02.
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Email: Saulstewarty@gmail.com

⭐⭐⭐

ILIPOISHIA….
Kelvin alibaki amekaa palepale chini, hakuweza kurudi nyuma wala kusogea mbele.
Mwisho wale watu watano walifika na kusimama mbele yake.
Kelvin aliwatazama kwa zamu mmoja baada ya mwingine. Zilikuwa ni sura ngeni kabisa kwake.

“Kelvin Johnson, bila shaka upo hapa kwa ajili ya kumtafuta mtu humihu sana kwako, miss Catherine peter” Alisema yule mzee aliyevaa suti nyeupe hali akiachia tabasamu mwanana.

JE NINI KITAFUATA?

SASA ENDELEA….

Kauli hii ilimfanya Kelvin ashituke na kumtazame zaidi mzee huyo, hakuelewe ni vipi amelifahamu jina lake pia anamfahamu vipi Catherine.

“Mshukuru mungu kwa kuwa hadi sasa hivi ninavyoongea Catherine yupo hai, ila ukifanya uzembe atakufa”
Yule mzee aliendelea kutoa kauli zenye utata.

“Yuko wapi Catherine?” hatimae Kelvin alifungua kinywa na kuuliza swali

“Hayuko hapa, Catherine yupo mbali sana sehemu ambayo binadamu yeyote hawezi kufika”
“Una maana gani?”
“Hebu inuka ukae kwanza” Aliongea yule mzee huku akika kwenye kiti kisha akamuonyesha ishara Kelvin nae akae.
Kelvin alizunguuka upande wa pili wa meza hali akiwa makini na wale watu wenye suti nyekundu waliokuwa wamezikunja sura zao ngumu, hawakuonyesha hata chembe ya masihara.
Akakaa kwenye kiti huku akizitafakari kauli za mzee huyo ambaye baadae alijitambulisha kwa jina la Alex Chapanga.
“Umesema Catherine yuko wapi?” Kelvin alirudia swali lake.
“Yuko mbali, mbali na dunia” Mzee chapanga alijibu kwa ufupi.
“Una maana gani?, mbali na dunia ndio wapi, kwanza hapa ni wapi?” Kelvin aliendelea kuuliza maswali ya udadisi akionekana hamwamini kabisa Mzee Chapanga na watu wake.

“namaanisha Catherine hayupo dunia hii, hebu tazama kwanza hizi picha” Alisema Mzee chapanga, akafungua droo ya meza, akatoa picha kadhaa na kuzitupa mezani mbele ya Kelvin.

Kelvin alizipokea na kuanza kuzitazama moja baada ya nyingine.
Mara ghafula alishtuka na kusimama, mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio isivyo kawaida, jasho jembamba likaanza kumtoka taratibu, mambo aliyoyaona kwenye picha zile yalimshtua na kumtisha mno.
Ni picha zilizomuonyesha Catherine akiwa kwenye mazingira ya ajabu sana, hakuwa peke yake, alionekana kuwa pamoja wa wanawake wengine ambao walivaa kitamaduni(kizamani) mavazi yaliyoziba sehemu ya kifua na kijisketi kifupi, wengine wakiwa juu ya farasi wengine wakiwa wameshika siraha za jadi upinde mishare na mikuki, wengine waliwa wamejichora tatoo za ajabu kwenye miili yao. Yalikuwa ni mazingira ya ajabu sana ambayo Kelvin alizoea kuyaona kwenye tamthilia za zamani za kikorea alizopendelea kuangalia.
Kelvin alijikuta anatetemeka mikono na miguu, akashindwa kustahimili kusimama, akakaa tena kwenye kiti.
Hakika alionyesha kumpenda sana Catherine, zile picha alizoziona zilikuwa ni ishara tosha kuwa Catherine hayupo salama hata kidogo.

“Huku ni wapi, yuko wapi Catherine wewe mzee” Kelvin aliongea kwa sauti kubwa hali akimsogelea Mzee chapanga kwa hasira lakini kabla hajafika alizuiliwa na wale watu waliovaa suti nyeukundu, akarudishwa tena kwenye kiti.

“Hizo picha ni mfano mdogo tu wa sehemu aliyopo mpenzi wako lakini kuna mambo makubwa na mazito zaidi ya hayo, jitahidi kuwa mpole hukuingia humu ndani kwa ajili ya kuleta ugomvi, na endapo ukiruhusu hasira zako zikutawale utasababisha Catherine apotee moja kwa moja na wewe utakufa pia” maneno haya ya Mzee chapanga yalifanya hasira za Kelvin kuanza kuyeyeka taratibu.

“Hebu tazama tena hii picha, unamfahamu huyu mtu?” Aliuliza Mzee Chapanga.
Kelvin aliipokea ile picha na kuitazama, akatikisa kichwa akiashiria kutomfahamu kabisa mtu aliyemuona kwenye picha hiyo.

“Anaitwa Deus P. Zollanda, hili jina nalo ni geni kwako?”
“Nimewahi lisikia zamani, ila sikumbuki vizuri”
"Umaweza kukumbuka angalau unielezee huyu mtu ni nani"
"Nimesema sikumbuki, mzee mbona maswali ni mengi kwa nini usiniambie tu ni wapi Catherine alipo"

"Kwa hiyo hutaki maswali yani, hivi kwa unavyoona kati ya mimi na wewe hapa ni nani mwenye shida?"

"Aah sawa basi nitakujibu, umeuliza kuhusu Zollanda si ndio, niliwahi kusoma habari zake tu wakati nipochuo kwenye mafunzo ya askari mpelelezi, niliambiwa Zollanda ee, yani ee.. ni mtu tu sifa zake ni kama Osama bin laden lakini yeye tofauti yake alikuwa anahusika na mambo ya sayansi na teknolojia kama sijakosea" Kelvin alijaribu kueleza yale anayoyajua kumuhusu Zollanda.

“Sawa uko sahihi ila nisikikilize kwa makini huyu bwana unaemuona kwenye picha ni mjukuu wa Deus P. Zollanda huyo unaemsema wewe, anatumia jina la babu yake ambaye miaka mingi iliyopita alikuwa akitafutwa kwa nguvu sana na serikali ya marekani baada ya kuhatarisha usalama wa dunia nzima, ZOLLANDA ni mwanasayansi mkubwa sana wa zamani aliyekuwa na wazo ambalo lilihatarisha usalama wa Dunia nzima.
Yeye na baadhi ya wanasayansi wakubwa duniani walikuja na wazo lenye utata wazo la kutaka kuunda dunia mpya, dunia ambayo itakuwa sawa kabisa na hii dunia yetu, lakini lilikuwa ni wazo ambalo lilipingwa vikali na nchi zote ulimwenguni hasa serikali ya China kwani kufanya hivyo kulihatarisha usalama wa dunia hii tuliyopo, mbaya zaidi Zollanda ambae ndiye alikuwa kinara wa mpango huu alikuwa ni mtu mweusi, kama unavyojua ubaguzi wa rangi haujaanza leo. Mpango wake ulipingwa katakata lakini Zollanda hakutaka kushindwa aliendeleza jambo hili kwa siri ” Mzee Chapanga alitulia kwa muda akanywa glasi moja ya maji kisha akaendelea kuzungumza huku Kelvin akimsikiliza kwa makini.
“Baadae Zollanda alikamatwa akawekwa gerezani lakini aliweza kutoroka na hakuna aliyejua alipokwenda, kwa kuwa alikuwa na mpango hatari serikali ya marekani ililazimika kusambaza wapelelezi katika nchi zote duniani hapa kwetu alikuja dada mmoja aliyejulikana kwa jina la Alexander, ni jasusi mkubwa ambae yupo hadi leo na serikali ya Tanzania inamtumia katika kesi mbalimbali ngumu. kwa zaidi ya miaka 10 bado hawakufanikiwa kumpata Zollanda mwisho waliamini kwamba amekufa na habari zake zikaishia hapo.
Hili likawa kosa kubwa Zollanda hakuwa amekufaa, alikuwa hai, tena akiendeleza mpango wake kwa siri kubwa yeye na wanasayansi wengine wakubwa.
mpango wake umekuja kukamilishwa na mjukuu wake miaka miwili iliyopita, hivi sasa tunavyoongea kuna Dunia nyingine mpya inayomilikiwa na Deus P. Zollanda, na huko ndipo yupo mtu unayemtafuta yaani Catherine na wengine wengi waliopetea kama yeye” mzee Chapanga alimaliza maelezo yake.

Kelvin alibaki ameduwaa kwa dakika kadhaa hali akiyatafakari maelezo ya Mzee chapanga, mwisho kelvin alitabasamu tu.

"Ila wewe mzee bana"
"Kijana unacheka, huo mda wa kucheka unatoa wapi"
"Hivi mzee unanionaje kwanza, yaani hii stori uliyonipa kwa akili yako unaona mimi naweza kuiamini ki urahisi tu yani?" kelvin aliuliza,
"Najua ni ngumu kuamini, hakuna aliyehawi kuamini kwa kuelezwa tu kama hivi wewe, hadi pale utakaposhuhudia mwenyewe kwa macho yako, Usijali ni suala la muda" alisema Mzee Chapanga akionekana kumaanisha kile alichokisema.
Hapo kidogo Kelvin alionekana kuanza kumuelewa japo kwa kiwango kidogo sana.

“kwa hiyo nitawezaje kumpata Catherine?”
“Wewe unamfikiria tu Catherine, vipi hukusu watu wengine ambao nimekwambia wapo huko wanaishi kama mateka, unafikiri wao hawahitaji msaada?”
“Mmmh! Sawa namaanisha tutawezaje kuwasaidia?”.

“Hahahahah, unaongea kirahisi sana Kelvin, ikiwa taifa kubwa kama marekani wameshindwa kuzuia mpango huu wewe ambae hata hujulikani utawezaje, hawa watu wamejipanga ni ngumu sana tena sana"

“Mzee kwa hiyo unamaanisha siwezi kumpata Catherine?” Aliuliza Kelvin hali akionyesha hofu yake waziwazi.
“Ooh! Come on, bado unarudia kosa lilelile nimekwambia kule hayupo Catherine peke yake”
Alisema Mzee Chapanga hali akionyesha kukelwa na namna Kelvin alivyokuwa akimzungumzia Catherine kila wakati.
"Sawa samahani basi, niambie tunafanyaje?"
"Hilo ndilo swali la msingi, nimekuleta hapa kwa makusudi kwa sababu lengo letu ni moja kuwatoa wapendwa wetu kutoka kwenye Dunia ya Zollanda" aliongea mzee Chapanga kisha akasimama na kumtazama Kelvin usoni.
"Nifuate"

JE, NINI KITAENDELEA...?
=> Mzee Chapanga atasema nini?
=>Miss Catherine yupo salama?
=>Ni kweli kuna dunia nyingine au kuna siri gani hapa?
ITAENDELEA...
 
  • Thanks
Reactions: ADK
Back
Top Bottom