SIMULIZI.... BALAA
MWANDISHI...HALFANI SUDY
SEHEMU YA TISA.
Lile anguko la Mwanasheria lilimpeleka moja kwa moja kule kwenye kibonde kidogo lilipoingia gari la Mzee Mpaukha, na kujikuta ameulalia mwili wa mpambe wa Bi harusi,
Hasina Omary.
"Mamaaaaaa"
Mwanasheria alipiga kelele kali sana. Akiwa amemlalia Hasina, macho yake mbele yake alikutana na picha mbaya sana. Picha ya kutisha.
"Ni nini hii, inamaana tumekufa wote" Mwanasheria alijiuliza mwenyewe. Pombe haziongopi kabisa, Mwanasheria alijiona kama na yeye alikuwemo katika ile gari iliyopata ajari, na sasa watu wote wamekufa, akiwemo na yeye. Yalikuwa mambo ya ajabu sana.
Alijiinua taratibu toka katika mwili uliojeruhiwa vibaya sana, mwili wa Hasina, akasimama wima, huku akiwa anayumbayumba, Mwanasheria aliangalia vizuri eneo lote lile la ajari. Japo kwa shida kutokana na giza na kwa macho ya ulevi, lakini alitambua vizuri madhara makubwa yaliyotokea mahali pale.
"Ni nini hii?" Alijiuliza mwenyewe Mwanasheria. Mara akili zake za kilevi zilimtuma kufanya kitu. Alitoa simu yake mkononi na kupiga simu, alipiga simu kwa Robert, alikuwa ni rafiki yake kipenz.
"Hallo Robert" Aliongea kwa sauti ya kilevi.
"Nambie Mwanasheria, mbona usiku sana" Robert aliongea kwa sauti iliyoonesha alikuwa anatoka usingizini.
"Tumepata ajari rafiki yangu"
"Ajari ?"
"Ndio wenzangu wote wamekufa nimebaki mimi peke yangu"
"Ulikuwa na kina nani"
"Siwajui"
Pombe zilimfanya Mwanasheria ajione kama naye alikuwemo katika ile ajari.
"Sehemu gani imetokea hiyo ajari?"
"Mtaroni"
"Come on Mwanasheria be serious"
"Kweli my friend"
"Ulikuwa unatoka wapi mwanasheria?"
"Kilabuni"
Robert alitoa msonyo mrefu na kukata simu. Akihisi Mwanasheria alikuwa katika maruweruwe yake baada ya kunywa pombe za kutosha.
Upande wa Mwanasheria, ulibaki na mshangao, kwanini rafiki yake kipenz Robert kamkatia simu wakati yeye anamueleza jambo muhimu na zito sana.
Mwanasheria alianza kupiga kelele, na maneno ajari na balaa yakisikika mara kwa mara katika kelele zake.
Majirani na lile eneo walisikia walisikia vizuri sana kilio kile cha Mwanasheria, lakini nani katika mji ule alikuwa hamjui Mwanasheria, nani angekithamini kilio cha mlevi yule, kila mtu alipuuzia kilio cha mlevi, Mwanasheria. Lakini Mwanasheria hakupuuza, alizidi kupiga kelele...
Kule hospitali Kivinje hali ya mviziano iliendelea. Baada ya Dokta Yusha kukaa pale kwa muda mrefu, bila simu yake kupigwa, bila kumuona aliyempigia simu, aliamua kuondoka. Huku kichwani alikuwa anawaza, atamwambia nini Nasra na kumuelewa, atawaambia nini wazazi wake. Alitoka nje na kumkuta dereva wa ile pikipiki amesinzia, alimuasha na kupanda.
Wakaondoka.
Wakati wanaondoka walipishana na gari moja lililoingia kwa kasi sana mle hospitali, almanusra liwagonge.
Walipofika Singino, simu ya Dokta Yusha iliita, kuangalia namba ni ya ile sauti ya kizee iliyompigia mwanzo...
ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA.
Maoni/ushauri 0757 633010