SIMULIZI YA MAPENZI; FARIDA
Imesimuliwa na Halfani Sudy
SIMU; 0674 395733
Sehemu ya Kwanza
Kilwa Masoko...mwaka 2014
Alikuwa ni mwanamke mzuri sana. Mwanamke mrefu, urefu usiochukiza. Alikuwa na sura ya duara. Nywele zake alikuwa amezikata vizuri ndogondogo. Alikuwa na umbo zuri lililotenganeshwa na kiuno chembamba. Kifuani, alibeba maziwa madogo ya duara. Tumbo dogo, yale wayabebayo walimbwende. Chini, alikuwa na mapaja ya haja. Mapaja manene yanayojaa vyema katika suruali. Alikuwa na miguu minene. Miguu iitwayo ya bia. Alikuwa anatembea kwa mwendo wa madaha. Huku akiacha mwili wake unatikisika vizuri sana kwa nyuma.
Hizo ni sifa chache sana za mwanamke niliyokuwa namsubiri. Sikuwa na miadi nae. Nilikuwa namsubiri apite tu ili nimuone.
Hakuwa mpenzi wangu.
Sikuwa namjua kwa jina.
Sikuwa najua anapokaa.
Sikwenda kazini ili nimuone mwanamke ambaye nilitokea kumhusudu sana. Mwanamke aliyetokea kuuteka moyo wangu ghafla. Kuzimeza fikra zangu.
Cha ajabu. Saa saba sasa hakuwa amepita. Alikuwa na kawaida ya kupita kila siku, saa tatu asubuhi, leo hii saa saba alikuwa bado hajatokea.
"Amepatwa na nini? Mbona mpaka sasahivi hapiti? Au anaumwa? Au amesafiri?
Au leo amepita asubuhi sana..
Siku yoyote atakayopita lazima nimueleze jinsi ninavyoumia juu yake. Nimueleze nia yangu ya dhati ya kutaka kuwa nae. Awe wangu. Nimueleze kama ninampenda kuliko mwanamke yeyote yule hapa duniani. Nimueleze kuwa nataka kuishi na yeye milele. Nataka kuwa sehemu ya maisha yake, awe sehemu ya maisha yangu. Nataka anikaribishe katika moyo wake, niweke kambi. Tena kambi ya kudumu..."
Nikiwa katikati ya mawazo mara nilimuona akija. Moyo uliniripuka kwa furaha.
Alikuwa amependeza kuliko siku zote.
Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya pinki. Blauzi nzuri yenye mistari meupe na meusi, rangi iliyofanana na mnyama pundamilia. Mkononi alikuwa amebeba kibegi kidogo cheupe. Alikuwa anatembea kwa madaha kuja pale nilipokuwa nimekaa.
Nilinyanyuka huku nikisema "Samahani dada"
Alisimama huku akiuliza kwa sauti ndogo " Unaniita mimi?"
Nilianza kumsogelea taratibu huku nikijibu "Ndio"
Leo ndio nilipata nafasi ya kuisikia sauti yake. Alikuwa na sauti nzuri mno. Sauti isiyo kera masikioni. Ilikuwa mithili ya sauti ya ndege chiriku.
Alisimama akiwa ananisubiri. Nilimsogelea taratibu. Kichwani mawazo mengi yakishindana kichwani kwangu.
"Samahani tena dada. Kabla sijakwambia sababu ya kukusimamisha hapa, naomba tufahamiane, mimi naitwa Nassib Omary"
Aliniangalia kwa tuo. Alinipandisha chini-juu. Kama alikuwa anathaminisha thamani ya kila kitu nilichovaa. Akabinua mdomo kidogo kwa juu. Akasema " Naitwa Farida.."
Akaanza kuondoka.
Nilimshika mkono. " Sasa mbona unaondoka Farida. Nilisema tutambuane kisha ndo nikueleze sababu ya kukusimamisha. Samahani sana lakini"
Farida alisema huku akifanya harakati wa kutoa mkono wake nilioushika imara "Nimechelewa sana leo. Naomba nitafute muda mwengine"
Niliendelea kumshika " kwani unaenda wapi? Unajua kila siku nakuona unapita hapa, unaenda wapi?"
"Subiri nikupe business card yangu. Nimechelewa sana yaani kaka. Tutawasiliana."
Aliutoa mkono wake niliokuwa nimeushika. Akafungua zipu ya pembeni ya mkoba wake. Akatoa 'business card'. Alinikabidhi.
"Tutawasiliana Nass" alisema kwa lafudhi tamu sana. Sauti itokayo puani. Zaidi, nilifurahia sana kwa jinsi alivyofupisha jina langu.
Alianza kuondoka kwa maringo. Niligeuka kumwangalia jinsi alivyokuwa anaondoka.
Nilikili kimoyomoyo " Farida alikuwa ni bonge la mwanamke"
Nilitabasamu.
Nilirudi kukaa kitini. Nilianza kuisoma 'business card' aliyoniachia Farida.
Kulikuwa na majina yake kamili. Namba yake ya simu. Barua pepe. Jina la sehemu anayofanyia kazi na mambo mengine kadhaa.
Nikaichukua ile namba ya simu na kuinakili katika simu yangu.
Niliiangalia jinsi namba ya Farida ilivyotulia katika simu yangu. Nilitabasamu tena.
Nilienda kazini. Mimi nilikuwa ni daktari katika hospitali binafsi ya Bakwata. Mwaka wa pili sasa tangu nihitimu masomo yangu ya fani ya utabibu katika Chuo kikuu cha Muhimbili.
Nilipomaliza masomo mwaka 2012 niliamua kurudi nyumbani ili kuwasaidia watu wa nyumbani kwetu. Nilifika ofisini na kuegemeza kichwa changu katika meza. Nikimuwaza Farida.
Nikiwa katikati ya mawazo. Ghafla nilistuka baada ya mlango wa ofisi yangu kusukumwa kwa nguvu.
Alikuwa nesi Rehema.
Kwa sauti kubwa alisema " Ajari! Dokta kuna mgonjwa kapata ajari ya bodaboda. Yaani ameumia sana Doktaa"
Sikumjibu. Nilibeba vifaa vyangu vya kazi harakaharaka. Nikaelekea chumba cha mapumziko. Nesi Rehema alikuwa mbele akikimbilia huko. Nami nilikuwa namfuata nyuma kwa kasi.
Tulipofika tu chumba cha mapumziko. Nilimuona. Nilichanganyikiwa sana...
ITAENDELEA... COMMENTS ZENU MUHIMU SANA .