mapengo junior
JF-Expert Member
- Jun 28, 2011
- 1,135
- 276
SIMULIZI........BALAA SIMU-0757633010
MWANDISHI..HALFANI SUDY
SEHEMU YA KWANZA
KILWA KIVINJE, mwaka 1989.
Ilikuwa tarehe kumi na tano, mwezi wa nne, mwaka elfu moja mia tisa themanini na tisa. Ilikuwa usiku wa manane, usiku wenye kiza kinene, usiku ulioandamana na mvua kubwa sana, na radi iliyotoa sauti kali na za kutisha sana pamoja na miale yenye mwanga wa kuogopesha.
Usiku huo ulikuwa ni usiku muhimu sana, kwa Don Genge pamoja na kundi lake hatari sana. Usiku huo wa tarehe 15 mwezi wa 4 mwaka 1989 katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika hospitali ya wilaya ya Kilwa, maarufu kama Kinyonga, iliyopo katika mji wa Kilwa Kivinje, mkoa wa Lindi, kulikuwa na mkutano wa siri.
Don Genge akishirikiana na madaktari mahiri wa hospitali ya Kinyonga, pamoja na manesi wenye roho nyeusi, roho mbaya kabisa, roho zisizokuwa na chembe ya huruma hata kidogo, roho zinazojari pesa na kusahau utu, walikuwa wanaendelea na kikao chao cha Siri, kilichofanyika katika chumba cha siri, kikiwahusisha watu wanaojua kutunza siri.
Katika kikao hiko cha Siri. alikuwepo Don Genge mwenyewe ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao, Dokta Zaidi Kilumba, mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dokta Sharifa Juma, daktari bingwa wa upasuaji wilayani Kilwa, Dokta Tamaa Karimu, daktari aliyekuwa ndiye mkuu wa chumba hiko cha kuhifadhia maiti, kulikuwepo pia na watu sita, walinzi wa Don Genge, walikuwa walinzi mahiri, walinzi makini, wenye kujua kupigana aina zote za mapigano. Walinzi waliopitia vyuo mbali mbali duniani, waliojifunza aina mbali mbali za kuuwa na kufuzu kwa kiwango cha juu sana, waliopitia mateso makubwa sana katika mafunzo hayo, mateso ambayo si rahisi kuvumilika kwa binadamu wa kawaida, ndio, walipitia mateso katika mafunzo, mateso ambayo yamewafanya wawe imara sana leo hii, kutokana na mateso hayo sasa wana uwezo mkubwa sana wa kutesa, kumtesa mtu yeyote yule na kusema chochote watakachomuuliza, hata kama aliapa kiapo cha damu kutosema, vijana hao sita walikuwa wanajulikana kama SIX KILLERS, na majina yao walipewa kwa namba, kulikuwa na one, two mpaka six, namba zilizotolewa kutokana na ubora wao katika mapigano, ubora wao katika kujua mambo.
Katika kikao hiko cha siri walikuwepo pia manesi watano, manesi ambao walikuwa na umuhimu mkubwa sana katika mpango huu wa siri, manesi walioapa kuzitunza siri, kuzitunza siri vifuani mwao zikatulia tuli katika mioyo yao mibaya.
Ulikuwa mkutano muhimu sana kwao, labda ungeweza kufanyika sehemu nyingine tofauti na chumba hiki cha kuhifadhia maiti. Lakini sehemu zingine zote waliona siyo sahihi kwao, wakihofia siri zao kuwa hadharani. Waliamua kufanya kikao chao hiki katika chumba hiki, wakiamini ni sehemu salama sana, chumba ambacho kingekuwa ndio ofisi yao ya muda katika kutekeleza mambo yao hayo ya kinyama, mambo ya siri sana, yaliyohitaji sehemu ya siri na kuhusisha watu wenye kujua kutunza siri kama hawa.....
ITAENDELEA