Sina hakika kama Wabongo tuna haki ya kudhihaki mtu mwenye hata basic certificate ya taaluma yoyote ile na kumwita kuwa hajasoma. Embu mtu atuletee takwimu za Watanzania na viwango vyao vya elimu, kama mimi na wewe sio tu tutakuwa kwenye kundi dogo sana la Watanzania na wengi wao watakuwa hao tunaowacheka ambao kwa kiasi kikubwa kutopata bahati hii ambayo mimi na wewe tumeipata kumesababishwa na wao bali na wabinafsi wachache wasiokuwa hata na dhima katika jamii yetu.