Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,695
- 784
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imemtaka Meya Adam Kimbisa kukutana na mjumbe wa baraza hilo, Rita Mlaki kumshauri ahudhurie mikutano ya halmashauri hiyo kabla ya kuchukuliwa hatua za nidhamu.
Taarifa hiyo iliwasilishwa jana na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa, mbele ya Naibu Meya wa Jiji hilo, Ahmed Mwilima, wakati baraza hilo lilipokutana kwa ajili ya kupitia na kupitisha taarifa za kamati za robo tatu ya mwaka 2007/2008.
Londa alisema hadi kufikia Februari 26, mwaka huu, Mlaki ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, hakuhudhuria mikutano 17 ya baraza hilo na mikutano 25 ya Kamati ya Fedha na Uongozi, hali ambayo kwa mujibu wa kanuni, alipaswa kusimamishwa udiwani wa halmashauri ya jiji.
Mheshimiwa Mlaki alikuwa akipelekewa taarifa ya wito wa vikao vya baraza hili tangu Februari mwaka 2006 pasipo kuhudhuria, alisema Londa. Londa alisema katika taarifa hiyo kuwa kamati hiyo imeazimia kwamba Kimbisa akutane na mjumbe huyo ili kumshauri ahudhurie mikutano ya halmashauri kwa mujibu wa kanuni kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Mlaki alipopigiwa simu na gazeti hili kujua ni sababu zipi zilizomzuia kuhudhuria vikao hivyo kwa kipindi chote hicho, alikuwa mkali na kushutumu vikali gazeti hili kwa kuandika habari hiyo na kudai kuwa hawezi kujibu chochote kuhusiana na suala hilo.
Nasema hivi mimi ndio Rita Mlaki, andika chochote unachotaka na sikujibu, ninyi gazeti la Serikali badala ya kuwaachia akina (alitaja jina la gazeti) waandike mambo kama haya, nyie ndio mnaandika, sasa sisemi kitu na ukaandike, alisema mbunge huyo kwa hasira.
Halima Mlacha
Daily News; Thursday,July 03, 2008 @00:03
Pia Londa katika taarifa yake hiyo, alisema kamati hiyo imeazimia kuwa kesi ya Halmashauri ya Jiji dhidi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa), juu ya umiliki wa jengo lililopo Mwananyamala, isifutwe kama ilivyoamriwa na uongozi wa ngazi za juu.
Alisema jengo hilo ambalo awali lilikuwa mali ya iliyokuwa Tume ya Jiji, lilipewa kwa Jiji na kupangishwa na Dawasa waliolitumia kama ofisi yao na kukubaliana kulipa kodi ya pango, jambo ambalo baadaye walikiuka kulipa kodi hiyo na kuifanya Jiji iishtaki Dawasa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Mvumbo Dollah, akiwasilisha taarifa ya kamati yake, alisema mpaka sasa majengo ya biashara 6,191 yamekaguliwa katika manispaa zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni ambako zilitolewa ilani 2,153 na kutekelezwa ilani 1,231 hivyo kuwafikisha mahakamani wamiliki 243 kwa kukaidi ilani hizo.
Source: Habari leo