Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,179
Reaction score
829,142
Hii ni kaliba iliyojaa upweke na mateso japo kuna watu eti wanatamani wanatamani kuwa wachawi.

Mojawapo ya advertise ya kuwa mchawi ni uwezo wa kujigeuza umbo la kibinadamu na kuwa mnyama... Na binadamu wengine wasikujue kabisa kama wewe sio mnyama halisi.. Japo wanyama huwa wana hisia na maranyingi watajitenga na wewe ama kukufukuza...

Unapokutana na kundi la wanyama lakini kuna mmoja kajitenga na wenzake... Tambua tu kwamba huyo si mnyama halisi kwa asilimia kubwa.

Kwenye mikusanyiko ya watu ukifanikiwa kuwa na jicho la tatu utaona mengi sana.. Pale kariakoo pale Ilala sokoni, buguruni nknk kuna wanyama wengi sana katikati ya makundi ya watu..

Kujigeuza umbo la kibinadamu kuwa mnyama ni uthubutu wa hali ya juu japo ni sifa kwa mtendaji ila anapaswa kuwa na msingi mzuri kwenye taaluma yake kwakuwa akikutana na nguvu kubwa kuliko yeye atapigwa dafrau na kupoteza maisha..

Kuna wanga hupenda kujigeuza paka na kuingia kwenye majumba ya watu, sometimes panya au hata nyoka nk.. Sasa hawa ukiwavizia ukawalia timing ukawapa mkong'oto... Asubuhi yake utapata tu habari..

Utasikia mzee fulani kaumia bega au kichwa au mkono nknk.. Na ukija kurudisha kumbukumbu nyuma unakuta pale ulipompiga yule mnyama ndio hapo hapo anapoumwa huyo mzee.. Na haendi hospital ataugulia nyumbani mpaka apone..

Risk kubwa ni pale wanapopata kipigo mpaka kupoteza maisha. Siku ya pili mtaani utaona turubai!
 
Kuna paka mmoja ilikuwa jioni tumekaa kibarazani wakati anakuja kudoea doea bi mkubwa alikuwa anapika pika ,akajikuta kamwagia maji ya moto kwnye kiuno...kesho yake asbh akaja mjukuu wake katoto kadogo kakatuambia kunabibiake anumwa kababuka makalio
 
mshana jr
Nilikuwa siamini binadamu aweza kuwa mnyama,

Pale kibo kushuka kule bonde la gide,kuna siku nimeshinda nje akatokea mama mmoja anafoka anadai paka amemfuata alipokuwa anachota maji,na amempa kichapo hivyo tusubiri msiba,

Kama masikhara tukawa tunacheka tukajua ni utani,

Hayakupita masaa tukasikia yowe za msiba mzee mmoja mitaa ile akafariki na aliondoka na mpangaji wake pia.
 
Hahahahahaha kuna mzee mmoja hapa mtaani alikuwa anakuja kuniwangia anajigeuza paka siku nikamtegeshea akapigwa dafrau akaugulia kwake akawa ananiulizia mbona siend kumuona ajab siku nimeenda kumuona asubuh jion akapona hakukoma akaja tena akachezea vitasa sasa anaugulia ndani pamoja na kuniulizia sijaenda kumuona
 
Mkuu kuna hizo dawa za kua na jicho la tatu nataka nione hayo ambayo wataalam wanayaona.Huwa natembelea sana hayo maneo uliyoyataja.
Simple, chukua mwiko uliosongewa ugali halafu haujaoshwa, lala nao kitandani ukiwa umeukumbatia kichwani. Ila baada ya hapo utakumbuka kila ulichokiona lakini hautaweza kusimulia kamwe wala hata kuandika ulichokiona
 
Kuna paka mmoja ilikuwa jioni tumekaa kibarazani wakati anakuja kudoea doea bi mkubwa alikuwa anapika pika ,akajikuta kamwagia maji ya moto kwnye kiuno...kesho yake asbh akaja mjukuu wake katoto kadogo kakatuambia kunabibiake anumwa kababuka makalio
Hahahahha nimecheka sana
 
Back
Top Bottom