Ripoti ya un: Yaianika serikali, yadai watanzania ni watu wasio na furaha

jobe ayoub

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
203
99
[h=3]RIPOTI YA UN: YAIANIKA
SERIKALI, YADAI WATANZANIA NI WATU WASIO NA FURAHA[/h]
saada_35554.jpg


Naibu waziri wa fedha,
Saada Salum


Wakati Tanzania ikitajwa
kuwa ni miongoni mwa nchi zenye amani na utulivu, imebainika kuwa Watanzania ni
miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa
duniani.


Ripoti inayoonyesha
orodha ya nchi zenye furaha duniani ya mwaka 2013 (World Happiness Report 2013),
imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kati ya nchi
156 zilizofanyiwa utafiti huo.


Ripoti hiyo iliyoandaliwa
na kundi la wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa (UN), kati ya mwaka 2010 na 2012,
inaonyesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya 151 ikiburuta mkia pamoja na nchi za
Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Benin na
Togo.





Upatikanaji wa huduma za
jamii, mtazamo wa watu kuhusu rushwa, umri wa kuishi, ukosefu wa kazi, pato la
taifa na ukarimu wa watu katika nchi husika, ni baadhi ya vigezo vilivyoangaliwa
wakati wa kuandaa taarifa hiyo.


Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudensia Kabaka alieleza kushtushwa na ripoti hiyo kwa maelezo kwamba ni
asilimia 11.7 tu ya Watanzania wasio na ajira na kwamba wale wanaofanya kazi,
wanapata huduma zote za msingi, ikiwa ni pamoja na kwenda likizo na mishahara
inayolingana na taaluma zao.



"Watanzania wana furaha,
kwa upande wa wafanyakazi wanapata haki zao zote wanazostahili, sijui ni vigezo
vipi wametumia...kwa mujibu wa takwimu za 2006 ni asilimia 11.7 ya Watanzania
ndio waliokuwa hawana kazi, lakini wakati huo idadi ya watu ilikuwa ndogo, hivi
sasa imeongezeka," alisema Kabaka na kuongeza:"Usafiri ndiyo tatizo
linalowasumbua wafanyakazi wengi kwa kuwa wanachelewa kwenda
kazini."


Naye, Naibu Waziri wa
Fedha, Saada Salum alisema pamoja na vigezo vingine vilivyotumika kutambua
furaha ya Watanzania, umaskini ndiyo unaoweza kuwa chanzo cha Tanzania kushika
nafasi za mwisho.


"Inategemea na vigezo
vingine walivyovitumia, nakubali kuwa Tanzania ni maskini pengine hali hiyo
imeifanya nchi kushika nafasi ya mwisho," alisema Salum.


Nchi
zilizoongoza


Taarifa hiyo imezitaja
nchi tano; Denmark, Norway, Uswisi, Netherlands na Sweden kuwa ndizo
zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha zaidi duniani, huku Angola ikishika
nafasi ya kwanza Afrika na ya 61 duniani ikifuatiwa na Algeria (73), Libya (78),
Ghana (86), Zambia (91), Lesotho (98), Morocco (99) na Swaziland
(100).


Kwa upande wa Afrika
Mashariki, wananchi wa Uganda ndio walionekana kuwa na furaha zaidi kwani nchi
hiyo imeshika nafasi ya 120 wakifuatiwa na Kenya (123), Tanzania (151), Rwanda
(152) na Burundi (153).


Ripoti hiyo inabainisha
kuwa kati ya mwaka 2005 na 2012, nchi 60 duniani ziliongeza viwango vya furaha
kwa watu wake, kati ya hizo 16 zikiwa barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la
Sahara.


Nchi 29 zilibaki katika
viwango vya awali, huku watu kutoka nchi 41 wakipunguza viwango vyao vya
furaha.


Ikilinganishwa na ripoti
ilifanywa kati ya 2005 – 2007, Tanzania imeshuka kutoka asilimia 40 hadi 37.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa asilimia 10 ya watu duniani wanasumbuliwa na matatizo
ya akili ambayo yamewasababisha kukosa furaha.


Hata hivyo, imebainika
kuwa mtu mmoja anaweza kukosa furaha kutokana na sababu zaidi ya
moja.


"Mtu mmoja anaweza kukosa
furaha kutokana na sababu mbalimbali kama umaskini, ukosefu wa kazi, kuvunjika
kwa ndoa na kusumbuliwa na ugonjwa. Lakini sehemu kubwa, matatizo sugu ya akili
yamesababisha kukosekana kwa furaha," inasema sehemu ya ripoti
hiyo.


Alipoulizwa kuhusu ripoti
hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema bado hajaiona
na kwamba atakapoisoma atakuwa tayari kuizungumzia.


"Sijaiona ripoti hiyo kwa
hivyo siwezi kusema chochote hadi niione, wewe si umeiona ndiyo maana ukatupa
maswali?" alihoji Dk Mwinyi.


Wataalamu
wanena


Mwanasaikolojia Modesta
Kimonga, alisema Watanzania wengi wanakuwa na hasira kila wakati kutokana na
kukosa matumaini, baada ya mambo yao kushindwa kufanikiwa.


Alisema hali hiyo
inatokana na watu wengi kushindwa kudhibiti magonjwa na matatizo mengine
yanayowakabili.


"Watanzania wengi
wanasumbuliwa na mood disorder, wanakuwa wakali, wenye hasira kila wakati. Mambo
yao hayaendi wamekosa tumaini. Hali hiyo inawakumbwa hata watoto ambao wanakosa
mahitaji yao ya msingi," alisema Kimonga.


Hata hivyo, ripoti hiyo
inaeleza kuwa zipo sababu mbalimbali zinazowafanya watu kuwa na furaha:
"Wanauchumi wanasema furaha inaletwa na kipato kikubwa, wanasaikolojia wanaamini
furaha inakuja baada ya mtu kuwa na afya njema na viongozi wa dini wanaamini
furaha huletwa na maadili mema," inasema sehemu ya ripoti
hiyo.


Mhadhiri wa Uchumi wa
Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Honest Ngowi alisema kuna uhusiano wa karibu kati ya
umaskini na furaha, kwa kuwa mtu asiye na kipato cha kununua mahitaji yake ya
msingi hawezi kuwa na furaha.


"Gharama za bidhaa zipo
juu, mtu masikini hawezi kuwa na furaha, hata hivyo haimaanishi kuwa nchi tajiri
ndizo zenye furaha. Nchi kama Norway pamoja na kuwa na uchumi mzuri, lakini ina
idadi kubwa ya watu wanaojinyonga," alisema Ngowi.


Akizungumzia ripoti hiyo,
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii, Costantine Akitanda, alisema taarifa hiyo iko
sahihi na kwamba karibu kila Mtanzania analalamika.


"Ukichunguza utagundua
kuwa karibu kila Mtanzania analalamika. Hata sera zilizopo hazina mfumo
unaowawezesha watu kunufaika na maliasili za taifa," alisema
Akitanda.


Pamoja na msukosuko wa
uchumi ulioitikisa dunia kuanzia mwaka 2008, dunia imeshuhudia watu wakiongeza
viwango vyao vya furaha kutokana na sababu mbalimbali kulingana na mahali nchi
ilipo.


Mkazi wa Mabibo,
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Vick Manonge, alisema ripoti hiyo inaonyesha
hali halisi ilivyo hivi sasa hapa nchini, kwa kuwa watu wengi wanaonekana kuwa
na hasira.


"Kama kuna mtu
hakubaliani na hilo (ripoti hiyo) aangalie kwenye daladala watu walivyo na
hasira bila sababu ya msingi, mwingine hataki aulizwe hata nauli, " alisema
Manonge.


Katika siku za hivi
karibuni baadhi ya viongozi wakubwa duniani wamekuwa wakizitaka Serikali kutunga
sera za maendeleo zitakazoendana na hali halisi ya maisha ya watu wa eneo
husika, ili kuweka mazingira yatakayowaletea wananchi
furaha.


Baadhi ya huduma
zinazotolewa na serikali ni afya, kutengeneza ajira, elimu na kuweka mazingira
bora ya kujiwezesha kichumi kwa kila Mtanzania.


Chanzo:mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom