Ripoti ya UN: Finland yashika namba 1 kwenye orodha ya nchi zenye furaha zaidi duniani; Tanzania ya nne kutoka mwisho

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Wakati Finland ikitajwa kushika namba 1 kwenye orodha ya nchi zenye furaha zaidi duniani, Tanzania ipo kwenye nchi 10 zisizo na furaha na imetajwa namba 153 ikiwa ni namba ileile ya mwaka 2017 kwenye Ripoti hiyo iliyotolewa na UN.

Finland imeipita Norway mwaka huu na kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani, kulingana na Ripoti ya Umoja wa Mataifa(UN).

Ripoti hiyo pia inaonesha kudondoka kwa Marekani katika viwango vya furaha hadi nafasi ya 18 ambayo ni nafasi 5 chini ya ile ya 2016 likiwa ndo taifa kubwa kiuchumi likikabiliwa na kiribatumbo(obesity), matumizi ya mihadarati na sonona.

Nafasi nne za juu zimeshikiliwa na nchi za Nordic; Finland ikifuatiwa na Norway, halafu Denmark na Iceland katika nafasi ya nne.

Burundi imeshika nafasi ya mwisho kabisa (156) ikichangiwa na ugomvi wa kikabila, majaribio ya mapinduzi na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Cha kushangaza, Rwanda, Yemen, Tanzania, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati zimeonesha viwango vya chini vya furaha kuliko hata Syria.

Kwa mara ya kwanza, UN imepima pia viwango vya furaha vya wahamiaji katika kila nchi na Finland imeibuka kinara.

Nchi zilizofanya vizuri zimepata alama za juu katika kipato, hali ya kiafya, msaada/uungwaji mkono wa kijamii, uhuru, uaminifu na ukarimu.

========
Top 10 happiest countries, 2018
(2017 ranking in brackets)

1. Finland (5)

2. Norway (1)

3. Denmark (2)

4. Iceland (3)

5. Switzerland (4)

6. Netherlands (6)

7. Canada (7)

8. New Zealand (8)

9. Sweden (10)

10. Australia (9)

The 10 unhappiest countries, 2018
(2017 ranking in brackets)

147. Malawi (136)

148. Haiti (145)

149. Liberia (148)

150. Syria (152)

151. Rwanda (151)

152. Yemen (146)

153. Tanzania (153)

154. South Sudan (147)

155. Central African Republic (155)

156. Burundi (154)

=====

Finland 'world's happiest place' in 2018

Finland is the happiest country in the world, says UN report
 

Attachments

  • WHR_web.pdf
    2.6 MB · Views: 87
Back
Top Bottom