Ripoti ya ukaguzi ya CAG - 2009-2010

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,437
113,445
Wanabodi,

Hii ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG-Ludovick Utouh.

Niko kwenye chumba cha press conference ya Bunge, ambapo CAG, Ludovock Utouh anaitangaza rasmi ripoti yake kwa waandishi wa habari.

Pamoja na Utouh, ni wale wenyeviti wa oversight commitee, PAC, Mhe.John Cheyo, LGAC -Mhe. Lyatonga Mrema na POAC, Mhe. Zitto Kabwe.

Tuendelee...
 

Attachments

  • RIPOTI YA UKAGUZI WA UFANISI NA UPEMBUZI HADI TAREHE 31 MACHI 2011.pdf
    260.9 KB · Views: 252
  • RIPOTI YA SERIKALI KUU 2009-2010.pdf
    593.8 KB · Views: 252
  • RIPOTI YA SERIKALI ZA MITAA 2009-2010.pdf
    1.7 MB · Views: 403
  • RIPOTI YA MASHIRIKA YA UMMA 2009-2010.pdf
    537 KB · Views: 243
CAG ameripoti kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 2010, serikali imefanya ubadhirifu mkubwa zaidi wa fedha za umma kuliko mwaka uliotangulia.
 
nashukuru kwa taarifa.sasa ametoa sanction gani kwa serikali au ndio hivo kila kitu kinaishia hapo hapo???
 
Wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ya umma, it is wrong!. CAG amesema haiwezekani serikali ikaendelea kufanya wrong things. Kuna mgongano wa kimaslahi. Hakuna nchi yoyote, its not a good practice.

Huku ni kupeana ulaji tuu.
 
nashukuru kwa taarifa.sasa ametoa sanction gani kwa serikali au ndio hivo kila kitu kinaishia hapo hapo???
Ofisi ya CAG ni independent, ila pia serikali yetu hushurutishwi kuwajibika, huishia kushauriwa tuu, hivyo kazi ya CAG ni kushauri tuu.
 
CAG ametetea maroroso ya bodi ya mikopo na kusema mahitaji ni makubwa kuliko fedha zinazotolewa. Ameitaka serikali kuongeza fungu la bodi ya mikopo.
 
CAG ametoa mapendekezo kadhaa kwenye ripo yake. Soma mapendekezo hayo yako kwenye zile nondo hapo juu.
 
CAG amemaliza, sasa anaongea Zitto Kabwe. Ameshitushwa sana na stimulus package!, kumbe wezeiye walijigawiya mahela kupitia mpango huo.
 
haipo independent kaka,na wao ni watumishi wa umma kama wengine tu na fedha zinapitia wizara ya fedha
 
Zitto amesema wamemwandikia Waziri Mkuu, wabunge wote wangolewe kwenye bodi zote.
Zitto amemaliza, sasa anaongea Lyatonga Mrema.
 
Ofisi ya CAG ni independent, ila pia serikali yetu hushurutishwi kuwajibika, huishia kushauriwa tuu, hivyo kazi ya CAG ni kushauri tuu.

Pasco:

Mara zote najiuliza what is the point of doing these Audits? Soma hii extract kutoka "RIPOTI YA SERIKALI KUU: Masuala yasiyoshughulikiwa":-

...Muhtasari uliotolewa hapo juu unaonyesha jumla ya masuala yasiyoshughulikiwa kwa mwaka 2008/09 yaliyohusu
Wizara, Idara, Sekretarieti za Mikoa yalikuwa na thamani ya Sh 1,055,460,602,544, JPY 17,089,499,858 na USD2,100,000.

Katika mwaka 2009/10 jumla ya Wizara, Idara, Idara, na Sekretarieti za Mikoa zenye masuala yasiyoshughulikiwa ilipanda kutoka 37 hadi 46 na kiasi kilichohusika pia kilipanda na kufikia Sh 468,627,883,842, JPY 699,000,000. Aidha, Dola za Kimarekani ziliongezeka hadi kufikia 2,326,580. Kwa hali hiyo, thamani ya masuala yasiyoshughulikiwa iliongezeka katika mwaka 2009/10
ikilinganishwa na mwaka 2008/09
...
 
Lyatonga amesema watumishi wa halmashauri mbalimbali wakiboronga, huamishiwa halmashauri nyingine, ameshangaa serikali kuona uozo mahali, inauhamishia uozo huo mahali pengine, kuanzia sasa, mtumishi wa halmashauri akifanya madudu, atavuna madudu, kwanza alipe fedha aliozoiba, pili afukuzwe kazi na tatu, afikishwe mahakamani.
Mrema amesisitiza mwizi ni mwizi tuu, sio mwizi wa kuku auwawe, mwishi wa mali ya umma aenziwe!, ahamishwe, au aambiwe arudishe alichoiba!.
 
Kimefuata kipindi cha Maswali na majibu, swali la deni la dowans limeibuka, CAG amesema piga ua serikali ndio itawajibika na deni hilo na sio Tanesco.
 
Back
Top Bottom