Ripoti ya Kamati ya Mashirika ya Umma

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

1.0 UTANGULIZI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya kusimamia mahesabu ya Mashirika ya Umma ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Zitto Kabwe,MB (CHADEMA) ilifanya ziara ya ukaguzi wa ufanisi katika miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma, Liganga,Ngaka na Kiwira kuanzia tarehe 6 – 10 Machi,2011.

Kamati ilifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake yaliyoainishwa na kanuni ya 13 (a) – (e) ambayo miongoni mwake ni:

  • kusimamia ufanisi wa mashirika ya umma;
  • kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za mashirika ya umma;
  • kufuatilia sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma.
Ziara ya Kamati ilifanyika katika eneo ambalo Kamati imeliita Eneo Mkakati la uzalishaji wa Megawatt 1500 za Umeme kusini mwa Tanzania (South Tanzania’s 1500MW Strategic Complex) liko katika Wilaya za Ludewa, Mbinga na Ileje/Kyela mkoani Mbeya.

2.0 KATIKA ZIARA HII KAMATI IMEBAINI YAFUATAYO:

1. Eneo hili lina uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawatt 1500 ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo na kuendelea na uzalishaji kwa kipindi cha miaka 150 ijayo kabla ya makaa ya mawe kwisha kabisa.

2. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Mahesabu (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 2009, NDC imewekeza jumla ya Shilingi 1.4 bilioni katika Mradi wa Chuma Liganga , ikiwa ni pamoja na gharama za utafiti zinazofikia Dola za Marekani 36,563.00. Mradi huu ambao bado haujaanza uzalishaji unatarajiwa kuzalisha chuma na kuongeza thamani hapa hapa nchini kabla ya kuuza nje ya nchi. NDC imepewa jukumu la kusimamia rasilimali za Chuma Liganga zinazokadiriwa kuwa Tani 1.2bn, rasilimali ambazo kama zitaendelezwa zitachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi hasa katika uzalishaji wa umeme na hivyo kusukuma mbele maendeleo ya taifa.

3. NDC wanategemea kuingia ubia na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation toka nchini China kuendesha Mradi wa Makaa ya mawe wa Mchuchuma na kuchimba Chuma Liganga, mradi unaotegemewa kugharimu Dola za Kimarekani 3.0 Bilioni. Mkataba wa Ubia bado haujasainiwa na unasubiri maamuzi ya Baraza la Mawaziri. Mradi wa Mchuchuma unategemea kuzalisha 600MW za Umeme. Mradi wa Liganga unatarajiwa kuzalisha Chuma kwa matumizi ya ndani na pia kuuza nje ya nchi kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

4. NDC wameingia ubia na Kampuni ya Atomic Resources ya Australia na kuunda kampuni tanzu ya TANCOAL Energy kwa ajili ya kuchimba Makaa ya Mawe eneo la Ngaka Wilayani Mbinga kwa lengo la kuzalisha Umeme 450MW. Mkataba wa Ubia unaonyesha kuwa NDC watakuwa na Hisa asilimia 70. Uwekezaji katika mradi huu utakuwa takribani Dola za Kimarekani 350m.

5. Kamati imefuatilia mchakato wa kurejesha Serikalini umiliki wa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira na kubaini kuwa mchakato huo bado haujakamilika licha ya miaka miwili kupita tangu Serikali ilipotangaza azma hiyo.

6. Kamati imefuatilia utekelezaji wa agizo lake kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii kuwekweza kwenye miradi ya Umeme na kubaini kuwa mchakato wake bado haujafika mbali. Shirika la NSSF kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Kamati limeomba kumilikishwa mgodi wa Kiwira. NSSF kwa kushirikiana na mwekezaji mwingine (strategic investor) wanatarajia kuwekeza dola za kimarekani 400m na kuzalisha 500MW katika kipindi cha miaka mitano.

7. Kamati imependekeza kwa Shirika la CHC kushirikina na ofisi ya CAG ili kuharakisha zoezi la tathmini na uchunguzi maalum (special audit) wa Mali na Madeni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCPL). Wakati zoezi hili linaendelea Serikali (Wizara ya Fedha) Kamati inapendekeza kwamba Serikali iwape Shirika la NSSF ‘letter of intent’ ili waanze taratibu za zabuni kwa ajili ya kupata ‘strategic investor’ na masuala mengine muhimu kwa ajili ya kufufua mgodi wa Kiwira na kuzalisha umeme.

8. Kamati imebaini kwamba mipango ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) katika miradi ya Liganga, Mchuchuma na Ngaka iwapo itatekelezwa kwa haraka na kwa umakini, na vile vile maagizo ya kuwapatia Mradi wa Kiwira Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutazalisha 1500 MW za umeme ambazo si tu zitamaliza kabisa tatizo la umeme tulilonalo bali kuwa ni hatua ya nchi hii kuanza kuuza umeme nje ya nchi.

9. Umeme utakaozalishwa katika vyanzo hivi utatakiwa kusafirishwa kwa msongo (Transmission lines) wa 400kv kutoka Mchuchuma mpaka Mufindi (kwa mradi wa Mchuchuma) na kutoka Kyela mpaka Mbeya (kwa mradi wa Ngaka). Hii bado ni changamoto kubwa katika kufikia lengo la Taifa kujitosheleza kwa Nishati ya Umeme.

3.0 MAPENDEKEZO YA KAMATI

1. Kamati inalipongeza Shirika la NDC kwa hatua kubwa waliofikia katika Miradi ya Mchuchuma, Liganga na South Ngaka. Hata hivyo juhudi zaidi zinatakiwa ili kuhakikisha kuwa miradi hii inatekelezwa katika muda mwafaka.

2. Mkataba wa ubia baina ya Shirika la NDC na Kampuni Sichuan Hongda toka China ili kuendeleza Mradi wa Mchuchuma-Liganga ni muhimu usainiwe sasa na haraka na Serikali ishauriwe kutimiza wajibu wake kwa hatua ambayo NDC imefikia ikizingatiwa faida za kiuchumi za Mradi huu. Mazingira ya sasa ya uchumi wa Dunia na mahitaji ya Taifa ni mwafaka kwa miradi ya Makaa na Chuma. Kuchelewa kuanza kwa miradi hii kwaweza sababisha miradi isifanyike kabisa kwani uchumi wa dunia kwenye bidhaa za chuma huwa unayumbayumba sana (fluctuations).

3. Kampuni tanzu itakayoundwa ili kuendesha miradi hii ifuate taratibu zote za uchimbaji ikiwemo kusainiwa kwa Mkataba wa Uendelezaji Migodi (Mineral Development Agreements-MDA) kwa madhumuni ya kulinda maslahi ya Serikali, Watu wa Ludewa na Kampuni yenyewe.

4. Kwa kuwa suala la Ubia bado halijaamuliwa, Kamati inashauri kuwa ubia uzingatie kanuni ya faida (profitability and Pay Back period). Kwa mfano, NDC waweza kuanza kwa kuwa na hisa 20% lakini mara baada ya mradi kulipa (payback period) mgawo wa hisa uwe ni sawa kwa sawa. Pendekezo hili pia lizingatiwe kwa mradi wa Ngaka ambapo NDC wanahisa 30% kwenye Kampuni tanzu ya TANCOAL Energy.

5. Wizara ya Nishati na Madini iharakishe kutoa leseni ya uchimbaji wa Makaa ya Mawe kama ilivyoombwa na kampuni ya TANCOAL ambayo inamilikiwa kwa ubia na NDC ili uchimbaji wa maakaa uanze na hivyo kuanza kuzalisha Umeme. Inapendekezwa kuwa Umeme unaotokana na Makaa ya South Ngaka uzalishwe kutokea Wilaya ya Kyela ili kurahisisha kuunganisha na gridi ya Taifa.

6. Kamati inapendekeza kwa Kamati ya Nishati na Madini kuanza mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini kwa lengo la kutangaza kwamba Rasilimali za Makaa ya Mawe na Chuma kuwa ni Rasilimali za kimkakati (strategic resources) na kwamba leseni za kumiliki vitalu vya madini haya zitamilikiwa na Mahirika ya Umma tu. Pendekezo hili linatokana na ukweli kwamba kuna leseni nyingi sana za kumiliki madini haya ambazo zimemilikishwa kwa watu binafsi (speculators). Inapendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba leseni zote za kumiliki vitalu vya Chuma na Makaa ya Mawe zinazomilikiwa na watu binafsi au makampuni ya nje zifutwe na kumilikishwa kwa ama STAMICO au NDC. Hata hivyo, ifikiriwe kuundwa kwa Shirika la TANZANIA IRON AND COAL CORPORATION itakayomilikiwa kwa ubia na STAMICO na NDC na Shirika lingine lolote la Umma kwa lengo la kuendeleza rasilimali ya Makaa ya Mawe na Chuma hapa nchini.

7. Kamati inalitaka Shirika la Umeme nchini TANESCO kuanza kuwekeza katika msongo wa kusafirisha umeme (TRANSMISSION) kuelekea kwenye miradi hii ili kufanya miradi hii iwe na maana. Kamati imefurahishwa na wazo la wabia wa NDC kujenga msongo wao wa umeme. Hata hivyo, Kamati inaamini kuwa suala la msongo wa umeme liendelee kuwa chini ya Shirika la TANESCO au Serikali iunde Kampuni nyingine ya Umma kwa ajili ya Transmission peke yake. Kwa ajili ya uharaka wa msongo wa sasa Kamati inashauri kuwa wabia wa NDC wajenge msongo huu kama mkopo kwa Shirika la TANESCO.

8. Kamati ya POAC itaandaa mkutano wa wadau kuhusu miradi ya Mchuchuma na Liganga, Nkaga na Kiwira. Lengo la mkutano huu ni kufahamu mipango ya Serikali na Mashirika katika utekelezaji wa miradi hii. Mkutano huu utahusisha Mashirika ya NDC, STAMICO, TANESCO, NSSF na CHC. Pia Makatibu wakuu wa Wizara za Viwanda na Biashara, Nishati na Madini, Kazi na Ajira na Wizara ya Fedha na Uchumi. Wenyeviti wa Kamati za Bunge za Viwanda na Biashara na ile ya Nishati na madini watahudhuria ili kuangalia uwezekano wa kuharakisha miradi ya Mchuchuma, kiwira na liganga kwa lengo la kuzalisha Nishati ya Umeme, kukuza Uchumi kwa kuuza nje Chuma, kutengeneza ajira na kuleta maendeleo kwa Taifa letu. Mkutano huu umepangwa kufanyika siku ya Jumatatu tarehe 21 Machi 2011.

4.0 MGODI WA MAKAA YA MAWE KIWIRA

Kwa mujibu wa Fasili ya 13 (e) ya nyongeza ya nane ya kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la mwaka 2007 inayosomeka” Kufuatilia sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma’’. Kwa kutumia Kanuni hii, Kamati ya POAC imetekeleza Yafuatayo;

NI MUHIMU Serikali ikatambua kwamba ni muhimu maagizo ya Kamati kwa Serikali kwamba Shirika la NSSF lipewe Mgodi wa Kiwira ili kuweza kulikwamua shirika hilo.

HITIMISHO

Kamati inaendelea kutoa tahadhari kwambakuchelewa kusaini mkataba wa NDC na Kampuni ya Sichuan Hongda ya kutoka China na pia kutokamilisha mchakato wa kuumilikisha mgodi wa Kiwira kwa NSSF kunachelewesha maendeleo ya Taifa.

Kamati inategemea kutumia Taarifa yake ya mwaka 2009/2010 ikijikita zaidi kwenye Mashirika ya Umma yanyojihusisha na Miundo mbinu na Nishati kama kichocheo cha Maendeleo ya Taifa.
 
Kuna thread nimeisoma humu leo ikisema tusubiri tutaona jinsi Zitto na Makamba jr. watakavyobeba bango la kuwapa NSSF huu mradi.
Naona mapendekezo tayari yametoka.


HITIMISHO
Kamati inaendelea kutoa tahadhari kwambakuchelewa kusaini mkataba wa NDC na Kampuni ya Sichuan Hongda ya kutoka China na pia kutokamilisha mchakato wa kuumilikisha mgodi wa Kiwira kwa NSSF kunachelewesha maendeleo ya Taifa.
 
Mwenyekit wa kamati ya bunge ya mahesabu za mashirika ya umma, ZITTO ameendelea kung'ang'ania KIWIRA ipewe NSSF, source [ channel ten- habari]
My take, mbona anaforce kama kuna maslahi bnafsi? Wadau kama Mzee Lula wa Ndali MWANANZELA kaongea vizuri Why NSSP wasipewe kiwira? [mwananchi jumapili machi13 uk 16] Great thinker huyu ZITTO vp?
 
Mwenyekit wa kamati ya bunge ya mahesabu za mashirhka ya umma, ZITTO ameendelea kung'ang'ania KIWIRA ipewe NSSF, mbona anaforce kama kuna maslahi bnafsi? Mzee Lula wa Ndali MWANANZELA kaongea vizuri Why NSSP wasipewe kiwira? [mwananchi jumapili machi13 uk 16] Great thinker huyu ZITTO vp?
 
Nimesoma uchambuzi wa M M Mwanakijiji katika gazeti la MWANAHALISI toleo la wiki hii.
Naye amependekeza NSSF wasipewe TENDA hii,naona tahadhari zinazidi kuongezeka
Jamani nafikiri upembuzi yakinifu ungefanyaika ili tujiridhishe ili tusiingie chaka tena
Bado tuna matatizo makubwa katika sekta ya nishati
Tuondokane na mambo ya kufanya haraka haraka tusije kuumiza Tanzania yetu tena
Kama inawezekana na kama itafaa ikiwa itaonekana kwamba NSSF siyo asasi inayoweza kutusaidia basi tupige kelele za kutosha ili wasipewe kiharaka yasije tukuta kama ya IPTL na mengine kama hayo
 
Tujiulize tena tunataka mfumo gani wa uchumi? Sina ugomvi na kumilikisha mashirika ya umma miradi hii mikubwa. Lakini tujiulize, nini kilichotokea wakati uchumi wa Tanzania ulipoendeshwa na sekta umma. Je hili la umilikishaji mashirika ya umma si kurudi kule tuikotoka? Je nafasi ya sekta binafsi iko wapi? Uwezeshaji wa watanzania katika sekta binafsi uko wapi? Je mbona sijasikia lolote kuhusu kampuni kama NICO kuwa partner katika hilo? Tanzania inahitaji kuwawezesha middle class, ili kuwezesha kuumiliki uchumi kitanzania na kuepuka mamluki wa uchumi ambao hutorosha rasilimali mitaji.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

7. Kamati inalitaka Shirika la Umeme nchini TANESCO kuanza kuwekeza katika msongo wa kusafirisha umeme (TRANSMISSION) kuelekea kwenye miradi hii ili kufanya miradi hii iwe na maana. Kamati imefurahishwa na wazo la wabia wa NDC kujenga msongo wao wa umeme. Hata hivyo, Kamati inaamini kuwa suala la msongo wa umeme liendelee kuwa chini ya Shirika la TANESCO au Serikali iunde Kampuni nyingine ya Umma kwa ajili ya Transmission peke yake. Kwa ajili ya uharaka wa msongo wa sasa Kamati inashauri kuwa wabia wa NDC wajenge msongo huu kama mkopo kwa Shirika la TANESCO.



ZITTO BWANA!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa kama hili linawezekana kwanini na NSSF wasifanye hivi pia kwenye KIWIRA?
Mbona ndivyo wanavyofanya kila sehemu hata Ujenzi wa UDOM ni hivyohovyo kwanini KIWIRA wapewe jumla?
Nadhani hili linataka kufanana na ule ujenzi wa UBALOZI NAIROBI ambao jamaa nasikia wanangangania wapewe Jumla pia jengo,
NSSF vipi? Kunani?
 
Naam wakuu, ile tahadhari tuliyotoa jana ndio inaanza Rasmi. Zitto sasa hivi anaact kama LOBBYIST wa NSSF kiasi ambacho Tanesco wamepigwa butwaa. Wenye pesa nchi ya TZ sio NSSF tu, hata NMB, NBC, CRDB lakini hujawahi kusikia bank wakitaka miradi kama ya umeme. Wenye pesa wao ndio wanaitwa investors, wanapartner na makampuni yenye wataalamu wao wanatoa pesa, kwa hiyo NSSF itoe pesa kwa Tanesco.

Zitto anadanganya nchi kwenye ili::

""6. Kamati imefuatilia utekelezaji wa agizo lake kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii kuwekweza kwenye miradi ya Umeme na kubaini kuwa mchakato wake bado haujafika mbali. Shirika la NSSF kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Kamati limeomba kumilikishwa mgodi wa Kiwira. NSSF kwa kushirikiana na mwekezaji mwingine (strategic investor) wanatarajia kuwekeza dola za kimarekani 400m na kuzalisha 500MW katika kipindi cha miaka mitano.

7. Kamati imependekeza kwa Shirika la CHC kushirikina na ofisi ya CAG ili kuharakisha zoezi la tathmini na uchunguzi maalum (special audit) wa Mali na Madeni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCPL). Wakati zoezi hili linaendelea Serikali (Wizara ya Fedha) Kamati inapendekeza kwamba Serikali iwape Shirika la NSSF ‘letter of intent' ili waanze taratibu za zabuni kwa ajili ya kupata ‘strategic investor' na masuala mengine muhimu kwa ajili ya kufufua mgodi wa Kiwira na kuzalisha umeme.""


NSSF hawahitaji investor kama plan ambazo DAU anawaambia watu, wanahitaji Partner ambao ni wakandarasi wa kujenga mgodi na kuinstall mashine za kufua umeme. Pesa zote zitatoka NSSF, labda kidogo kwa sababu ya risk kubwa watayashirikisha mabank ya TZ watoe pesa at least 40%.

Sasa zito atueleze, kwa nini TANESCO wasiwe PARTNER WA NSSF na wawe na ownership ya mgodi na Mitambo yote??

Zito anapendekeza NDC na investor wa china wajenge mkongo na kuwapa Tanesco, kwa nini NSSF wasitoe pesa na TANESCO kuown KIWIRA???

Zitto umeshatoa mapendekezo, imetosha, sasa mbona unalobby tena NSSF wapewe Kiwira behind the scenes?? KUNA NINI??
 
Originally Posted by Zitto

Huku ni kuleta propaganda kwenye masuala ya maendeleo ya nchi. Ni upumbavu kila wakati kufikiria kwamba kila uamuzi unalenga uchaguzi wa mwaka 2015. Inaonyesha kuna watu wanaweweseka na uchaguzi wa mwaka 2015 na kudhani kwamba kila mtu akili yake ni huko huko. Ni upumbavu kwa sababu haiwezekani kila mradi wa maendeleo unaofikiriwa basi kuna watu wanataka ulaji. Kuna watu tunaendeshwa na fikra za kutenda na kupata matokeo ya kutenda. Haiwezekani tuwe watu wa kuzungumza tu kila siku.

I have no connection whatsover with RA na EL kwenye Urais au mpango wowote wa kisiasa. I say this loud and clear. I am not supporting anybody. I, myself, am ambitious. Siwezi kuingia kwenye miradi ya watu kutaka Urais kwani wote mnaowataja na kuwaunga mkono au kuwapinga naona hawana uwezo wa kuongoza Taifa hili.

Usinifanyie propaganda za kijinga. Ninafanya kazi yangu kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Sasa kama unataka niwe mwenyekiti posho, kukaa bila kutoa masuluhisho ya maendeleo ya nchi, go and hang yourself. I am not like that. I am action oriented. Call me arrogant or whatever the names, i am different. Mark my words! Acha propaganda kwenye maendeleo ya nchi.

NSSF
Sitafuti support ya mtu yeyote yule. Hoja za NSSF kukabidhiwa Kiwira nimeziweka wazi. Wala sijajificha kama wewe unavyotumia pen name hapa kwa unafiki wako. NSSF wameikopesha sana TANESCO. NSSF wana haki ya kuwekeza kwenye jambo lolote litakaloleta faida kwa mfuko. Hoja zako za kitoto eti why not TANESCO. Mbona Ngaka na Mchuchuma watakaozalisha umeme ni NDC? Nao tuwatoe tuwape TANESCO? Hayo ni mawazo mgando. It is stupidity to stay out there and wait for people to come with solutions and start criticising the solutions. It is even more stupid to link every initiative in Tanzania with Rostam Aziz! Who is Rostam Aziz anyway to be linked to everything. This is cheap propaganda. Yeye amekuwa Pweza anajitandaza kila mahala?

Tuogope kufanya maamuzi kwa kuwa atahusishwa Rostam Aziz? Acha upuuzi.

Kwamba Caspian watapewa tender ya kuchimba makaa. Huu ni upuuzi tu ili kujenga chuki na fikra hasi za initiative ya kuhakikisha Kiwira inafufuliwa. I dont care nani atachimba makaa pale. What i care ni kuona Kiwira inafufuka, makaa yanachimbwa na umeme unazalishwa. Hizi mbinu za kuhusisha makampuni yanayomilikiwa na watu wenye mawaa ya ufisadi na miradi ili ikwame ni mbinu za kitoto, za kijinga na za kipuuzi.

Hizi ni propaganda za kishenzi kabisa!

On my agenda - moja mchuchuma na Liganga miradi ianze. Mbili, Ngaka coal fields mradi uanze. Tatu, Kiwira ifufuliwe. Nitahakikisha kwa kupitia kamati yangu tunawezesha NDC na NSSF wanatekeleza miradi hii na kuliondoa taifa kwenye tatizo la umeme katika muda wa kati.

I dont care about the next election. I do about the next generation.

Endelea kumwaga sumu zako. Sibabaiki. I do the right thing and inshaallaah i will succeed for the benefit of my country!

*********************************************************************************
*****************************************************************************************


Mh. Zitto nashukuru kwa majibu ingawaje umejibu kwa jazba.

Let us go in Facts on this SAGA in few lines.

1) I agree with U that Kiwira should be developed quickly to add power to the National Grid and also to sell excess coal overseas.

2)The issue then comes, NSSF is neither a power company nor has any expertise in this field of power generation. Whichever way U cut it, NSSF will need a PARTNER to generate Power and also to mine coal.

Hapo sasa ndio mchezo mchafu unapotaka kuchezwa. Tanesco ni shirika la umma na lina matatizo makubwa sana ya Cash flow sasa kama wakiwezeshwa kwenye KIWIRA faida kubwa itapatikana na hiyo faida Tanesco watatumia kwenye POWER DISTRIBUTION ambako kunahitaji massive investments.

So issue here ni PARTNER WA NSSF awe TANESCO au ?????????.............

Kwa kuwa kamati yako inasimamia both Mashirika, tulitazamia uwe mbele kutaka hii win win SOLUTION, yaani NSSF wanafinance wanapata interest yao say 10% per yr ( WITH GOVT GUARANTEE) na Tanesco wanapata faida kwa kugenerate power na kutumia pesa kuimarisha miundombinu ya kusambaza umeme.

IS THERE ANYTHING WRONG WITH THE ABOVE SUGGESTION Mh. (MB)??????

May God Bless Tanzania.
 
Napenda nianze kwa kukupongeza wewe binafsi mh. Zitto na kamati yako kwa kazi nzuri iliyofanyika. pamoja na pongezi hizo, nataka niungane na Moelex23 kukutahadharisha kuhusu hii hoja yako ya kutaka NSSF ikabidhiwe mgodi wa Kiwira mara moja. Kamati yako kama msimamizi wa hesabu za mashirika ya umma inalazimika kuhakikisha mashirika hayo hayachezei kamali fedha za umma yaliyokabidhiwa. Hivyo kuitaka NSSF kukabidhiwa mradi huo kabla haijaufanyia uchambuzi yakinifu ni sawa na kuchezea kamali fedha za wanachama wake. Ikumbukwe NSSF kuanzia henzi za NPF haijawahi kuonyesha umakini unaostahili katika uwekezaji wake. Taarifu ya tume ya rais ya kurekebisha mashirika ya fedha iliweka wazi suala hilo. Hivyo kamati yako inawajibika kuliongoza shirika hilo kufanya uamuzi wa kuwekeza baada ya kupata hali halisi ya mradi huo badala ya kuimiza lijitumbukize kwenye mradi ambalo halina taarifa kamili.
 
Wakuu hongereni nyote kwa michango kwenye post hii, mimi nadhani si sahihi kwa kamati ya bunge ya mshirika ya umma inayoongozwa na zito kuipangia nssf ifanye uwekezaji katika maeneo yapi, kamati imepaswa kukumbuka kuwa nssf ina wanaoifanya iwe na fedha (wanaochangia mfuko huo), kamati ingeshauri michango ya wanachama ipewe thamani (ziwe hisa) na wanachama wawe na sauti na haki ya kupata gawiwo ikiwa watakubaliana kuingia kwenye biashara, tukiwapa sauti wenye hisa tutaongeza udhibiti wa investiment yoyote tunayofikiria kuifanya. Nadhani wakati unakuja tutagundua hizi kamati za bunge zitatumika kutuingiza mkenge. Kuweni macho watanzania
 
Wadau,
Hivi karibuni kuna report ambayo kamati ya Zitto imeitoa kuhusu jinsi ya kuondoa tatizo la umeme. Sasa sijui kama ni yeye anajichanganya au ni waandishi wamemquote vibaya.

Ila article ya kwanza inayopatikana hapa (An Eye Opener Week-long Visit to South Tanzania 1500MW Electricity Complex « Zitto na Demokrasia) inasema hivi kwenye kisehemu kimoja:

Sichuan Hongda Corporation Limited and China Africa Development Fund plan to invest about USD $ 3 Billion Dollars in both the Mchuchuma Coal and Liganga Iron ore project. They expect to make about USD $ 1.2 Billion dollars a year. Somebody informed me that this Chinese company is experienced in Zinc mining and has no experience in Power generation….Due diligence?

Halafu kwenye article nyingine inayopatikana hapa (Home) inasema hivi:

Zitto cited the joint venture contract between the National Development Corporation (NDC) and a Chinese company - Sichuan Hongda Corporation - to run Mchuchuma and Liganga projects, which he said awaited cabinet approval.
“It is important for the contract to be signed now and the government should be advised to fulfill its responsibility basing on the stage reached by the NDC as well as social and economic benefits,” stressed Zitto.


SWALI LANGU:
Sasa mbona kwenye hiyo article ya kwanza Zitto anasema kuwa hiyo kampuni ya kichina haina uzoefu wa kutengeneza umeme, halafu kwenye hiyo article ya pili Zitto huyo huyo anasema serikali iharakishe kwenye kusign mkataba nao?

Naomba kuwasilisha
 
Yale yale ya Rex Attorneys. Huku haifai ukegeuka nyuma inafaa! Ufisadi mtupu hapo
 
Zitto hata ukipaza Sauti kwa Jaziba haitasaidia.
Kazi ya kamati ya Bunge sio Management ya Masharika ya UMA, sana sana labda mfanane na Mauditor, hakuna mtu aliyesema kwamba your idea is stupid, tatizo ni approach yako, kwa nini wewe unang'ang'ania, unasukuma, na sasa hautaki hata kusikiliza ushauri wowote ule, kwanza wewe mwenyewe sio professional kwenye Power and Energy industry, kwa nini unataka kutumia popularity yako kusukuma hili swala liende fasta fasta.

Usitake kutuchanga bwana, experience tuliyopata kwa namna Lowasa aliyolazimisha, akasukuma saaana, kwenye deal ya Richimond/Dowans inatutosha. Kabla ya Pale Lowasa hakuonekana na kosa mpaka alipotughafirisha, as a brother and a friend nakushauri achana na style hii.

Unasema we ni mtu wa actions, kumbuka kamati yako haijawa entrusted with power unayolazimisha kuiexercisize, sio majukumu ya kamati yako kufanya analysis na kutoa maelekezo katika level unayolazimisha. Huu mradi ukienda kama unavyotaka wewe alafu ukaja kufail unataka nani awajibishwe, unafahamu vizuri sana kwamba hautakuwa wewe. My point ni kwamba, you have a good point, stop there acha wahusika waendelee, Kama ni NSSF wana investment depertment yao, wanaplans zao tayari, let them buy your idea ila sio kiivyo unavyofanya sababu ya nafasi yako.By the way NSSF hawajawhi kusema they have an idol fund na wanakaribisha maoni ya investment, wewe umejuaje kwamba NSSF wanamuscles na wako tayari kuinunua Kiwira, ni Mashirika gani mengine umeyareview and you are confised kwamba there is non other than NSSF. By the way NSSF wenyewe wako Kimyaa tukusema una kiherehere utalalamika?

Ni kweli una access ya information zaidi yetu, lakini si kweli kwamba you more right than us all.
Nenda kareview na Mashirika mengine, nenda NECTA, nenda Bandari na kwingine and am seating here
waiting to hear your powered, good recomendations like this one from those ends too.
 
megawat 1500 kwa miaka mia? shame on us.... wangenambia mg 10000 hv sawa makaa ya mawe yote hayo na je ce tutakuwa tunapungua na matumiz ya umeme yanapungua tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom