Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,489
- 40,997
Ukweli ni kwamba tunasubiria embe chini ya mkaratusi.
Tunaushangaa wizi na ubadhirifu wa pesa ya umma ulioibuliwa na CAG, kwani sisi tulikuwa na mategemeo gani? Hivi mwizi anaweza kuacha asili yake? Mwizi wa shati hawezi kuacha kuiba suruali ikikaa kwenye mapito yake. Wala mwizi wa maboga hawezi kuacha kuiba pesa kama ikimfikia. Halikadhalika mwizi wa kura, mwizi wa madaraka, hawezi kuacha kuiba pesa kama ikimkaribia.
Katiba inasema Waziri mkuu atateuliwa miongoni mwa wabunge wa kuchaguliwa. Majaliwa, alichaguliwa na wapiga kura wa wapi? Alipata kura ngapi? Kwa uhakika ni kwamba hakuchaguliwa na mpiga kura yeyote. Hana hata kura moja ya mpiga kura.
Badala yake alianda mipango ya kishetani ya kumteka na kumtesa mpinzani wake kwa kipigo cha kuelekea kumwua. Halafu akatangazwa eti amepita bila kupingwa.
Hatujui aliwalipa nini majambazi aliyoyakodi kumteka na kumpiga mpinzani wake.
Hatujui alimlipa nini OCD ili akatae kuchukua hatua zozote dhidi ya majambazi aliowatuma
Hatujui alimpa nini Msimamizi wa uchaguzi ili amtangaze kuwa amepita bila kupingwa.
Halafu mtu mwovu wa kiwango hicho utarajie atakuwa mwadilifu kwenye kwenye utumishi wake?
2) Hawa wanaoitwa Mawaziri, wote katika kuupata ubunge walifanya mambo aliyoyafanya huyu kiongozi wao au yanayokaribiana nayo.
Hii ni wakeup call kwa wananchi kuwa kiongozi aliyeupata uongozi kwa uovu, mbele ya safari hawezi kuondoka kwenye asili yake ya uovu.
Pia PM atolee ufafanuzi wa ghorofa lake la Dodoma linalojengwa kwa gharama ya mfanyabiashara. Ni urafiki tu au ni kwa gharama ya umma.
Wananchi tunatakiwa kufahamu kuwa tupo kwenye nyakati ngumu sana. Tunaongozwa na waovu lakini tunasubiria mema. Waziri mkuu mwovu wa uchaguzi, mawaziri waovu wa uchaguzi, wabunge waovu wa uchaguzi. Hawa watu ni waovu dhidi ya umma. Hawastahili hata kuitwa viongozi.
Rais Samia kama una dhamira njema, harakisha mchakato wa katiba mpya ili tuweke mazingira yatakayozuia siku za mbeleni watu waovu kupata madaraka kwa njia ya uovu wao.
Na iwekwe sheria kuwa yeyote ambaye amewahi kutumia uovu kwenye uchaguzi kwa nia ya kudhulumu mamlaka ya wananchi au haki ya mshindani wake, ni marufuku kuomba upngozi kwenye ngazi yoyote ile maisha yao yote.