Ripoti ya CAG: Ununuzi magari ya Serikali unavyofuja fedha

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,340
Ununuzi magari ya Serikali yanavyofuja fedha
By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz
pic+magari.jpg

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kupambana na matumizi mabovu ya fedha za umma, hali inaonekana ni tofauti katika ununuzi wa magari; ufujaji ni mkubwa, inabainisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

Magari ambayo yalipaswa kununuliwa kwa Sh120 milioni kwa bei ya sokoni, ilinunuliwa na Serikali kwa Sh237 milioni, kiwango ambacho ni takriban mara mbili ya bei, ripoti ya CAG inaeleza.

Ripoti hiyo ni ya ukaguzi uliofanywa na CAG katika ufanisi wa manunuzi makubwa ya magari katika kipindi cha miaka minne.

Serikali hutumia zaidi ya Sh50 bilioni kununua magari ya taasisi zake mbalimbali kila mwaka, lakini Wakala wa manunuzi ya Umma (GPSA) unafuja fedha hizo kutokana na kutokuwa na mpango wa ununuzi, kutoangalia bei ya sokoni, kutotumia ushindani wa bei na kutumia kampuni moja tu na kutokuwa na mpango wa udhibiti wa manunuzi, ripoti ya CAG inaeleza.

Katika ripoti hiyo, CAG anasema kuwa aliamua kufanya ukaguzi huo kutokana na ukweli kwamba Serikali ilitumia Sh219 bilioni kununua magari 1,483 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2017/18 bila ya “GPSA kuwa na kanzidata yake, utafiti wake wa soko, bila ya kuomba ushauri kutoka vyombo vingine, shaka ya umma kuhusu kukuzwa kwa bei.”

CAG anaeleza kuwa kitu kingine kilichomsukuma kufanya ukaguzi ni ucheleweshaji wa magari baada ya kununuliwa, magari yanayoletwa kutofikia kiwango kilichotakiwa, pia kilio kwamba Serikali inauziwa kwa bei ya juu tofauti na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) licha ya magari kufanana na kununuliwa wakati mmoja.

“Nimebaini kuwa hakukuwa na mpango mkakati wa mwaka katika manunuzi ya magari ya Serikali na GPSA haikufanya utafiti wa kujua bei ya soko la magari,’ alisema Profesa Assad.

“Katika kipindi cha mwaka 2014/15 hadi 2017, GPSA ilitumia takribani Sh219 milioni kwa ajili ya kununua magari ya Serikali bila kufanya utafiti wa bei katika soko la magari,” alisema Profesa Assad katika ripoti hiyo.

Profesa Assad alisema katika ukaguzi wao waligundua katika mwaka fedha wa 2014 hadi 2018 hakukuwa na ushindani wa kitaifa wa kumpata mzabuni, hakuwa na ushindani bei na GPSA ilitumia mzabuni mmoja kwa miaka yote hiyo.

“Kwa miaka minne, GPSA imekuwa ikitumia mzabuni mmoja kama njia pekee ya kuchagua kampuni ya kuizuia Serikali magari,” inasema ripoti hiyo.
CAG anaeleza kuwa GPSA iliingia katika makubaliano na wazabuni saba. Hao ni CFAO Motors Tanzania Ltd, CMC Automobiles Limited, Nissan Tanzania Limited, AMC Tanzania Limited, TATA Tanzania Limited, Jaguar Land Roverand M/S na Toyota Tanzania Ltd.
“Licha ya kuwa na kampuni saba za kuagiza magari, mara nyingi GPSA imekuwa ikinunua kutoka Toyota Tanzania Ltd katika kipindi cha miaka minne. Kwa mujibu wa GPSA, maombi ya taasisi (PE) yalikuja yakiwa yametaja mtengenezaji, jambo lililoengua waagizaji wengine,” inasema ripoti hiyo.

“Matokeo yake, Toyota ikawa ndio muagizaji mkuu wa magari ya Serikali. Kutaja mtengenezaji ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma.”
Katika ripoti hiyo Profesa Assad anasema manunuzi hayo hayakuwakilisha bei bora kama sheria inavyotaka, matokeo yake ikanunua magari kwa bei kubwa kuliko ya sokoni au kulinganisha na bei ambayo UNDP ilinunua.

“Ilibainika pia kuwa, bei za magari zinazotolewa na kampuni ya Toyota Tanzania Ltd zilikuwa juu ikilinganishwa na zile zinazotolewa na masoko mengine kwa magari yenye vigezo vinavyofanana na katika mwaka huohuo wa fedha,” alisema.

Ripoti inasema gari aina ya Land Cruiser Hard Top 5 yenye milango 10 ilinunuliwa na UNDP kwa Sh135 milioni wakati Serikali ilinunua kwa Sh158 milioni, huku gari aina ya Toyota Land Cruiser Hard Pick Wagon GXR-High ilinunuliwa na UNDP kwa Sh218 milioni lakini Toyota ikaiuzia Serikali kwa Sh366 milioni.

Vivyo hivyo, gari aina Land Cruiser Hard Pick Up Single Cabin ilinunuliwa kwa Sh109 milioni na UNDP huku lakini wakala huyo wa Serikali akanunua kwa Sh135 milioni na Land Cruiser GXR-manual ilinunuliwa na UNDP kwa Sh120milioni lakini Serikali iliinunua kwa Sh237 milioni, huku Land Cruiser Hard Pick up Double Cabin ilikuwa Sh 114milioni lakini ikanunuliwa kwa Sh146 milioni .

“Hii inaonyesha bei iliyotolewa na Toyota kwa Tanzania ilikuwa kubwa kwa asilimia kati 15 hadi 49 ukilinganisha na bei za UNDP kwa magari ya aina hiyo na yenye sifa zinazofanana,” anasema Profesa Assad.
 
Hawa wahuni, majizi na mafisadi hayajali kabisa kuhusu pesa za walipa kodi. Yanafanya ubadhirifu na ufisadi wa hali juu wa pesa za walipa kodi.
Kamata wote funga ndani wahujumu uchumi Hawa, hakuna cha kesi wala mahakama, ni kupotezeana muda tu. Watu wanaweka "Cha Juu" kisha baadae wanagawana kwa mlango wa nyuma, wezi kabisa hawa.

Mahakama za mafisadi zimejaa tandabui wakati mafisadi wakuu wanapeta tu serikalini na kuzidi kujineemesha. Hii ripoti ni kipimo kwa JPM kama kweli ni mtokomeza rushwa au nae ni "wale wale tu"
 
Inasikitisha sana..... Hivi hakuna namna Serikali ikawa inanunua moja kwa moja kwa Manufacturer? Huu ndio ukwapuaji wa pesa za walala hoi. Halafu mbona tunanunua magari mengi hivi. Ndo kusema kila mwaka yanakufa magari 300 au 400??
Mkuu hii number ya magari tunayonunua isikutishe sana, mengine ni Magari "hewa". Hapa tupo kwenye Uzi wa bei kubwa, ukitafuta uzi mwengine humu wa magari yaliyoagizwa lakini hayajafika bado ndo utaelewa.
 
Warudishe difference yote,na ikiwezekana wafilisiwe kabisa,itangazwe mali zao zisiuzwe wala kubalishwa majina na kwenye akaunti zao,waruhusiwe kuweka tu(deposit)isitoke hata kumi,wametupiga parefu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM ameahidi, mara kadhaa, kwamba wakwapuaji wa fedha za umma atawafanya wazirudishe, na kwamba watazitolea shimo lolote. Haya, yetu macho.

Wezi kumbe ni "wenzetu". Takukuru wanatoka ofisi za serikali kwenda huku na huko kusaka mafisadi na kumbe mafisadi papa wako nao kwenye maofisi hayo hayo ya serikali.

Tumenyonywa vya kutosha, tumeibiwa vya kutosha. Sasa tunataka kufanya mapinduzi. Ila hatutafanikiwa bila kubadilisha watendaji
 
Aiseeee...!! Kama ni sehemu serikali bado haijadhibiti matumizi mabovu ya hela ni kwenye manunuzi ya magari ya serikali..

Tulipiga kelele mno mnoo humu, serikali inunue Land cruiser Prado tu, ( Standard around $40k-$60k) kwa mawaziri wote, wakuu wa mikoa, sectors zote za viongozi, ila Ikulu, Vice President na Waziri Mkuu wao wanaweza nunuliwa Land Cruiser VX V8, custom made..!!

Alafu mikoani na sehemu korofi za halmashauri ni Land cruiser Hard Top tu basi... Hizi ni ngumu na zinafaa mazingira korofi ya mikoani..

Tatizo liko hapa.. Viongozi karibu wote wajuu, wako kwenye Land Cruiser VX V8.. Na gharama zake za manunuzi ni around $100,000 hadi $ 120,000 gharama za utumiaji mafuta ni kubwa mnoo na maintenance yake ni ghali mno mnoo.. Hili tumepiga keleeee weeee, na hiyo bei CAG anayosema sio kwamba hawajui, hapo kuna 10% za watu lazima..!!
 
Mkuu hii number ya magari tunayonunua isikutishe sana, mengine ni Magari "hewa". Hapa tupo kwenye Uzi wa bei kubwa, ukitafuta uzi mwengine humu wa magari yaliyoagizwa lakini hayajafika bado ndo utaelewa.

Yalinunuliwa 166 yakapokelewa 0
 
Ununuzi magari ya Serikali yanavyofuja fedha
By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz
pic+magari.jpg

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kupambana na matumizi mabovu ya fedha za umma, hali inaonekana ni tofauti katika ununuzi wa magari; ufujaji ni mkubwa, inabainisha ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

Magari ambayo yalipaswa kununuliwa kwa Sh120 milioni kwa bei ya sokoni, ilinunuliwa na Serikali kwa Sh237 milioni, kiwango ambacho ni takriban mara mbili ya bei, ripoti ya CAG inaeleza.

Ripoti hiyo ni ya ukaguzi uliofanywa na CAG katika ufanisi wa manunuzi makubwa ya magari katika kipindi cha miaka minne.

Serikali hutumia zaidi ya Sh50 bilioni kununua magari ya taasisi zake mbalimbali kila mwaka, lakini Wakala wa manunuzi ya Umma (GPSA) unafuja fedha hizo kutokana na kutokuwa na mpango wa ununuzi, kutoangalia bei ya sokoni, kutotumia ushindani wa bei na kutumia kampuni moja tu na kutokuwa na mpango wa udhibiti wa manunuzi, ripoti ya CAG inaeleza.

Katika ripoti hiyo, CAG anasema kuwa aliamua kufanya ukaguzi huo kutokana na ukweli kwamba Serikali ilitumia Sh219 bilioni kununua magari 1,483 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2014/15 hadi 2017/18 bila ya “GPSA kuwa na kanzidata yake, utafiti wake wa soko, bila ya kuomba ushauri kutoka vyombo vingine, shaka ya umma kuhusu kukuzwa kwa bei.”

CAG anaeleza kuwa kitu kingine kilichomsukuma kufanya ukaguzi ni ucheleweshaji wa magari baada ya kununuliwa, magari yanayoletwa kutofikia kiwango kilichotakiwa, pia kilio kwamba Serikali inauziwa kwa bei ya juu tofauti na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) licha ya magari kufanana na kununuliwa wakati mmoja.

“Nimebaini kuwa hakukuwa na mpango mkakati wa mwaka katika manunuzi ya magari ya Serikali na GPSA haikufanya utafiti wa kujua bei ya soko la magari,’ alisema Profesa Assad.

“Katika kipindi cha mwaka 2014/15 hadi 2017, GPSA ilitumia takribani Sh219 milioni kwa ajili ya kununua magari ya Serikali bila kufanya utafiti wa bei katika soko la magari,” alisema Profesa Assad katika ripoti hiyo.

Profesa Assad alisema katika ukaguzi wao waligundua katika mwaka fedha wa 2014 hadi 2018 hakukuwa na ushindani wa kitaifa wa kumpata mzabuni, hakuwa na ushindani bei na GPSA ilitumia mzabuni mmoja kwa miaka yote hiyo.

“Kwa miaka minne, GPSA imekuwa ikitumia mzabuni mmoja kama njia pekee ya kuchagua kampuni ya kuizuia Serikali magari,” inasema ripoti hiyo.
CAG anaeleza kuwa GPSA iliingia katika makubaliano na wazabuni saba. Hao ni CFAO Motors Tanzania Ltd, CMC Automobiles Limited, Nissan Tanzania Limited, AMC Tanzania Limited, TATA Tanzania Limited, Jaguar Land Roverand M/S na Toyota Tanzania Ltd.
“Licha ya kuwa na kampuni saba za kuagiza magari, mara nyingi GPSA imekuwa ikinunua kutoka Toyota Tanzania Ltd katika kipindi cha miaka minne. Kwa mujibu wa GPSA, maombi ya taasisi (PE) yalikuja yakiwa yametaja mtengenezaji, jambo lililoengua waagizaji wengine,” inasema ripoti hiyo.

“Matokeo yake, Toyota ikawa ndio muagizaji mkuu wa magari ya Serikali. Kutaja mtengenezaji ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma.”
Katika ripoti hiyo Profesa Assad anasema manunuzi hayo hayakuwakilisha bei bora kama sheria inavyotaka, matokeo yake ikanunua magari kwa bei kubwa kuliko ya sokoni au kulinganisha na bei ambayo UNDP ilinunua.

“Ilibainika pia kuwa, bei za magari zinazotolewa na kampuni ya Toyota Tanzania Ltd zilikuwa juu ikilinganishwa na zile zinazotolewa na masoko mengine kwa magari yenye vigezo vinavyofanana na katika mwaka huohuo wa fedha,” alisema.

Ripoti inasema gari aina ya Land Cruiser Hard Top 5 yenye milango 10 ilinunuliwa na UNDP kwa Sh135 milioni wakati Serikali ilinunua kwa Sh158 milioni, huku gari aina ya Toyota Land Cruiser Hard Pick Wagon GXR-High ilinunuliwa na UNDP kwa Sh218 milioni lakini Toyota ikaiuzia Serikali kwa Sh366 milioni.

Vivyo hivyo, gari aina Land Cruiser Hard Pick Up Single Cabin ilinunuliwa kwa Sh109 milioni na UNDP huku lakini wakala huyo wa Serikali akanunua kwa Sh135 milioni na Land Cruiser GXR-manual ilinunuliwa na UNDP kwa Sh120milioni lakini Serikali iliinunua kwa Sh237 milioni, huku Land Cruiser Hard Pick up Double Cabin ilikuwa Sh 114milioni lakini ikanunuliwa kwa Sh146 milioni .

“Hii inaonyesha bei iliyotolewa na Toyota kwa Tanzania ilikuwa kubwa kwa asilimia kati 15 hadi 49 ukilinganisha na bei za UNDP kwa magari ya aina hiyo na yenye sifa zinazofanana,” anasema Profesa Assad.
Ujumbe huu,umfikie General Mabeyo,
Kwamba hawa wanaofanya ufisadi huu,ndio wanohatarisha usalama wa nchi hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Warudishe difference yote,na ikiwezekana wafilisiwe kabisa,itangazwe mali zao zisiuzwe wala kubalishwa majina na kwenye akaunti zao,waruhusiwe kuweka tu(deposit)isitoke hata kumi,wametupiga parefu mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii excess washagawana wajanja wachache, pengine GPSA walipewa Proforma Invoice (Quotation) yenye bei ya cha juu wakasaini kuiridhia. Hapa ni kukamata maafisa wa GPSA weka ndani miaka ya kutosha tu wajifunze uzalendo.
 
Walizogawana watakuwa wamejengea,wamenunua magari na mali mbalimbali,ni kufilisi na kusukuma jela mpaka wasahaulike,na hapa ndipo ilipaswa kubadili sheria kwa hati ya dharula,unaweka kifungo cha maisha na kutaifisha haya majizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamata wote funga ndani wahujumu uchumi Hawa, hakuna cha kesi wala mahakama, ni kupotezeana muda tu. Watu wanaweka "Cha Juu" kisha baadae wanagawana kwa mlango wa nyuma, wezi kabisa hawa.

Mahakama za mafisadi zimejaa tandabui wakati mafisadi wakuu wanapeta tu serikalini na kuzidi kujineemesha. Hii ripoti ni kipimo kwa JPM kama kweli ni mtokomeza rushwa au nae ni "wale wale tu"
Jpm anapaswa kutiwa ndani akawajibike kwa kuzalisha ufisadi mwingi katika utawala wake.
 
Back
Top Bottom