Ripoti ya CAG ni ya kisiasa ndio sababu inahitimishwa na Bunge, ile ya TAKUKURU ndio ya Kiutendaji!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,026
Mtu anayetenda Wizi au Ubadhirifu hiyo ni Jinai na Wanaohusika nao ni DCI, DPP na Takukuru

Bungeni yanafanyika maamuzi ya kisiasa na kisera, swala la nani ashtakiwe kwa mujibu wa sheria ni la DPP

Panahitajika Elimu ya kuitisha itolewe Watanzania walelewe majukumu ya kikatiba ya Bunge, DPP, Takukuru na CAG

Wengi wanaamini Bunge linaweza kufanya majukumu yasiyo yake kisheria Kitu ambacho hakiwezekani

Kama TRC ilivuruga tenda ya Mabehewa maana yake Takukuru hailisubiri Bunge ili ifundishwe cha kufanya inatakiwa iwe imeshafanya kabla ya November

Kamati maalumu za Bunge ndio hujaga na mambo Mapya siyo hawa akina PAC na LAAC

Eid mubarak!
 
Mkuu vyombo vyote vya serikali havifanyi kazi in isolation. Mwenye mamlaka ya ukaguzi wa kitaalamu wa hesabu za umma ni CAG. Baada ya hapo kama kuna jinai yeyote inapeleka basi inapelekwa kwenye mamlaka husika. Takukuru wanapambana kuzuia au kupambana na jinai zenye rushwa tu. Kama haina rushwa hawahusiki sio mandate yao.

Na hao wote watapeleka majalada kwa DPP ili kufungua kesi. Ukijua mfumo wa utendaji wa hizi taasisi usingeweka hoja yako jinsi ulivyoiweka ni upotoshaji.

Bunge kazi yake ni kusimimia serikali na kuidhinisha mipango yake pamoja na matumizi. Sasa mwangalizi wa Bunge kama serikali imeenda kukingana namipango yake na matumizi sahihi ya fedha ni ofisi ya CAG. Mipango ya serikali imepitishwa Bungeni, bajeti ya serikali imepitishwa bungeni na serikali huleta reporti ya utekelezaji Bungeni sasa kujiridhisha kama imetumika kama ilivyoletwa na serikali ni pamoja reportya CAG na kamati za Bunge.

Sasa unasema report ya CAG ni ya kisiasa wakati imefanywa kwa kutumia vigezo vya proffession husika sielewi unataka kusema nini. Serikali haipemdi kuabishwa imetumia fedha vibaya ni aibu then wewe unasema ni siasa?

Report ya CAG inamapemdekezo nini kifanyike kupotia Bunge inayajadili na kuweka azimio which is binding kwa serikali kwamba ni lazima iyatekeleze. Siasa ipo wapi
 
Back
Top Bottom