Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
WIKI iliyopita Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Assad ametoa ripoti ambayo imeonyesha matatizo yaliyopo kwenye usimamizi na hata ufuatiliaji wa fedha za umma.
Ripoti hiyo ambayo imezua mjadala kwa wanasiasa, wanataaluma na umma kwa ujumla, licha ya kutuhimiza kumuunga mkono Rais John Magufuli na serikali yake, pia inafanya tusubiri kujua ni hatua gani zitachukuliwa na serikali kuondooa udhaifu uliopo.
Hatua zilizotangazwa mwanzoni na serikali ya awamu ya tano, kama vile kupiga marufuku idara za serikali kufanya warsha na semina kwenye hoteli za kifahari, kupunguza gharama za uzinduzi wa Bunge kutoka Dola 100,000 hadi Dola 7,000, kukomesha posho ya vikao, kufuta matumizi ya fedha kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru, kuzuia safari za maofisa wa serikali nje ya nchi bila idhini kutoka kwa rais au katibu mkuu kiongozi, zimeokoa fedha nyingi.
Kwa habari zaidi, soma hapa => Ripoti ya CAG inatutaka tumuunge mkono Rais Magufuli katika usimamizi wa fedha za umma | Fikra Pevu