Ripoti ya BOT, Rais Samia aurejesha mzunguko wa pesa nchi

Ripoti ya BOT, Rais Samia aurejesha mzunguko wa pesa nchi

Mtu wa Asali

Senior Member
Joined
May 9, 2022
Posts
149
Reaction score
292
Vijana mmeisoma hii ripoti ya benki kuu ya Tanzania Kuna vitu vya maana sana humu. Kuna fursa na indicators za fursa zimeainishwa.

Kwenye Paragraph ya pili toka mwisho inaongelea fursa iliyoletwa na mabadiliko waliyoyafanya kwenye Foreign Exchange regulations. Kwa Sasa mtanzania unaruhusiwa kuinvest kwenye Government securities katika nchi mbalimbali za SADC. Zamani ilikuwa hadi upewe kibali,kwa mabadiliko haya ni hela yako Hii ina maana Mtanzania anayeishi Malawi, kama Polepole anaweza kununua bondi za serikali ya Malawi bila kuhitaji kibali cha Benki Kuu ya Tanzania.

But pia wakazi wa nchi wanachama wa SADC na EAC wanaruhusiwa sasa kununua bondi za serikali ya Tanzania, tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ni Watanzania tu.

Inakusaidia siyo tu kwa ongezeko la investment avenue Bali pia ku-hedge political risk.

Sehemu nyingine wanaongelea ongezeko la mzunguko wa pesa. Hiki ni kiashiria cha kuboreka fursa za kibiashara (ina maana watu wameanza kutumia pesa). Kazi yako hapa ni kupitia katika analytical documents zao uone ni sector zipi hapa zinaongelewa kukua katika mzunguko,then unajipanga kuwekeza

Mama kaifungua nchi kwakweli.

IMG_4033.jpg
 
Warudishe kwanza zile pesa walizo waibia watu wa maduka ya kubadilishia pesa za kigeni.
Yaani sija wahi kuona benki kuu majambazi kama benki kuu ya Tanzania.
 
Maza anaupiga mwingi balaa, mashuti yake makali mpaka yanatoboa nyavu za magoli.
 
Hadi Leo hamjasema kwa nn mmepunguza asilimia kwenye treasury bonds tokea tumepata Uhuru.
Uzuri ukweli tunaujua
 
Mapolitician wakila kwa urefu wa kamba sasa ni mwendo wa kutoka nduki kwenda kununua hisa south. BOT lazima ijikite ku monitor na aliyeweka zuio ana sababu zake mzitaje na mseme zimeenda wapi kwa sasa
 
Mapolitician wakila kwa urefu wa kamba sasa ni mwendo wa kutoka nduki kwenda kununua hisa south. BOT lazima ijikite ku monitor na aliyeweka zuio ana sababu zake mzitaje na mseme zimeenda wapi kwa sasa

Kwani kununua hisa ni jambo lililokuwa limezuiwa..?
 
Back
Top Bottom