Ripoti ya BOT mbona haitolewi!? Walioiandika wanawekewa shinikizo ili waibadilishe?

Kama waliangalia mwaka mmoja na wizi ni mkubwa kiasi hicho basi imagine kama wangeangalia miaka mingine miwili au mitatu. Nina imani kwamba wizi huu haukuanza 2005, umeanza miaka mingi tu. Wakaguzi wanapogundua makosa mengi katika sample yao basi hutakiwa kuongeza sample hiyo ili kujua ukubwa wa tatizo. Siri kali labda hawakutaka waendelee miaka miwili nyuma 2003/2004 na 2004/2005 kwa kuwa madudu yaliyofanyika hapo BOT yangeongezeka kwa kiasi kikubwa sana.
wizi BoT umeanza miaka mingi kama usemavyo. Jee, hukumbuki mzee nyerere alipong'atuka? BoT iliwashwa moto Mzee mwinyi akarithi majivu ya makaratasi. Unafikiri ule moto ulijiwakia tuu wenyewe? au unafikiri mkuu nyerere alikuwa hajuwi moto ule uliwakaje na ni wa nini na kwa nini? lakini alikaa kimya, kama si ufisadi ni nini? au hamuijuwi system ni nini?
 
wizi BoT umeanza miaka mingi kama usemavyo. Jee, hukumbuki mzee nyerere alipong'atuka? BoT iliwashwa moto Mzee mwinyi akarithi majivu ya makaratasi. Unafikiri ule moto ulijiwakia tuu wenyewe? au unafikiri mkuu nyerere alikuwa hajuwi moto ule uliwakaje na ni wa nini na kwa nini? lakini alikaa kimya, kama si ufisadi ni nini? au hamuijuwi system ni nini?

Ina maana kama wizi ulifanyika wakati wa Nyerere basi inabidi uendelee hata kipindi chetu?
 
...legal action to be taken against all those involved in the theft." Meghji

Do we need more evidence to support our arguments that m/s Meghji needs to be fired!? I don't think so.


Make BoT theft report public, urges Slaa
By Polycarp Machira
THE CITIZEN

An outspoken opposition MP yesterday urged the Government to make public the audit report on the Bank of Tanzania's Sh133 billion scandal, which led to the sacking of its Governor.

Dr Wilbrod Slaa, the MP for Karatu in Arusha region, said the public needed to know the extent of the looting of taxpayers' money in suspect payments through the bank.

The Chadema MP, who has since last year been leading the campaign against massive theft from the Central Bank, called for the release of the comprehensive report by the British audit firm, Ernst & Young, on the External Payments Arrears (EPA).

But contacted for comment, Finance minister Meghji said: "We can't make the report available to the public as the Head of State has ordered legal action to be taken against all those involved in the theft."

Mrs Meghji added: "Doing so would jeopardise the ongoing process to recover the stolen monies as well as take the culprits to court."

Last week, President Jakaya Kikwete sacked the BoT Governor, Dr Daudi Ballali, after an investigation of the EPAs revealed the theft of Sh133 billion in 2005/6.

Speaking to The Citizen in Dar es Salaam yesterday, Dr Slaa said the Government had earlier promised to make public the audit report, but had finally produced only a summary.

He said the report would give Tanzanians the real picture and would prove that the opposition MPs were right when they accused some government officials of "looting" public coffers.

"The Government is cheating the public by not publishing the full report of the audit. In fact, we have the details and only need action," he said.

He accused Finance minister Meghji of failing to make the EPA reports public, despite an earlier pledge.

Dr Slaa also accused the minister of lying to the public that the $30 million paid to Kagoda Agricultural was spent on government issues, something that the audit report had dispelled.

But Mrs Meghji said the Government was still fully committed to seeing that all those responsible for the loss of taxpayers' money face legal action.

In an exclusive interview with The Citizen, Dr Slaa claimed that the 2005 EPA audit had shown that a trillion shillings had been paid out, but nobody could explain the whereabouts of that money.

The MP told of "some serious forgery" by those involved in the saga. He said the draft management report produced by the CAG on December 21, 2006 cited many irregularities within the BoT on EPA accounts.


"Let the government tell us all the companies paid by the EPA accounts as most of those listed are just very minor partners in the project," Dr Slaa said.

Some of the firms, which had benefited from the payments, he claimed, had not even been mentioned in the report.

He said a government-owned gold mining firm was one of the companies, which received money, but which had not been listed in the audit report.

Dr Slaa also noted that in the 2005 audit report, the CAG had stated that some donors had ceased support to the country, in protest against looted public funds.
The MP claimed the Kiwira Power Project was initially 100 per cent government-owned company, but this had been reduced to 85 per cent ownership.

He alleged that the company had been contracted by Tanesco and was receiving $6 million a month for capacity charges.

"The Government ought to be very clear on this and name these people if it is serious about fighting corruption. We want to know who these people are

He suggested that an independent body be appointed to investigate the culprits and establish how much money they had received. "A parliamentary committee cannot do it as some MPs are involved," he said.

He said a minister was once linked to a shady contract, in which he was paid 12 per cent of the shares in his foreign account, but the government had not taken action against him.

The Kagoda connection

On the allegations that she wrote a letter on September 15th, 2006 to Deloite and Touche explaining where the $30 million paid to Kagoda Agricultural Company went, Finance minister Meghji said: "It is true but I finally established that there were irregularities in the transactions."

She told The Citizen by telephone: "After writing that letter, some two days later, we established that something fishy was going on and I immediately ordered the investigation."

She added: "I took this decision after establishing that the details given by BoT about $30 million transactions lacked grounds. I then rescinded the letter and ordered the Controller and Auditor General to investigate the matter."

The BoT had earlier claimed that the $30 million paid to Kagoda Agricultural Company Ltd was for security expenses by the Government, raising more queries about the legality.

Kagoda Agricultural is among 22 companies that reportedly fraudulently received Sh133 billion from BoT between 2005/6.
 
WOW!

In an exclusive interview with The Citizen, Dr Slaa claimed that the 2005 EPA audit had shown that a trillion shillings had been paid out, but nobody could explain the whereabouts of that money.
 
Yote ni sawa you cannot release it then we are waiting for the action kwa uharaka wake .Sisi ni wavumilivu sana tutangoja ila this time hakuna kusema Watazania ni wasahaulifu hapana .Tupo tu tunangoja .
 
kuna wakuu humu ndani walisema wanayo ripoti.
sasa jee huu ni mtego wa siri-kali kuona kama wapo
jamaa watakaoitoa hiyo ripoti ili nao (siri-kali) walinganishe?
jee wakuu nao watabana kuingojea siri-kali itoe ripoti yao
ili kama imefanyiwa utaalamu basi siri-kali iumbuke?

naona kwa hali hiyo itabidi tungoje hiyo juni 2008.
 
Meghji, Mramba wajiuzulu - Wapinzani

2008-01-15 10:30:25
Na Mashaka Mgeta na Mwandishi PST, Tanga


Ushirikiano wa vyama vinne vya upinzani Wilaya ya Tanga, umemtaka Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji na yule wa Viwanda na Biashara, Bw. Basil Mramba kujiuzulu kutokana na kashfa ya ubadhirifu wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wakati wapinzani Tanga wakitoa tamko hilo, jijini Dar es Salaam, Dk. Wilbroad Salaa naye amemtaka Waziri Meghji kujiuzulu.

Katika mkutano wao wa hadhara mkoani Tanga, vyama vya CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF, vilidai kwamba kwa kuwa ubadhirifu huo umetokea chini za wizara zao, wanatakiwa kujiuzulu ili kumrahisishia kazi Rais Kikwete ya kusafisha nchi.

Tamko hilo lilitolewa jana na makamu mwenyekiti pamoja na katibu wa CHADEMA Wilaya ya Tanga, Bw. Mohamed Waziri na Bw. Rashid Khalid katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mabawa jijini hapa.

Walisema, mawaziri hao ni viongozi wa juu wa wizara hizo na kwamba wanao wajibu wa kusimamia Benki Kuu ambayo ni sawa na injini ya serikali, kuhakikisha hakutokei ubadhirifu wowote, lakini walishindwa kufanya hivyo hadi Rais Jakaya Kikwete alipoingilia kati.

Kwa mujibu wa viongozi hao, ubadhirifu uliotokea BoT ni kielelezo tosha kwamba mawaziri hao hawana uwezo wa kukemea vitendo viovu katika wizara zao, hali ambayo kimsingi inawatia wasiwasi wananchi kwamba huenda na wao walihusika kwa namna moja ama nyingine katika kadhia hiyo.

Wamemtaja Mramba kwa maelezo kwamba ndiye aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa miaka 10 kabla ya Meghji.

Walishauri kwamba mawaziri hao wakijiuzulu watajenga heshima kwao binafsi na kwa serikali ya awamu ya nne.

Wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimfuta kazi aliyekuwa gavana wa BoT, Dk. Daudi Balali na kumteua Profesa Benno Ndulu kuchuku nafasi yake.

Mbali na kumuondoa gavana, Rais Kikwete pia aliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya BoT kukutana kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zinazopaswa za kinidhamu dhidi ya maofisa waliohusika.

Katika kashfa hiyo, fedha zinazotajwa kupotea ni kiasi cha Sh. bilioni 133 kutoka Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA) ambazo kati ya hizo Sh. bilioni 90.3 zililipwa kwa kampuni 13 hewa ambazo zilitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizobatili na za kughushi.

Naye Dk. Slaa, alisema hatua iliyofikiwa na Rais Jakaya Kikwete, kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk Daudi Balali, na kuviagiza baadhi ya vyombo vya dola, kuchukua hatua za kisheria, haitoshi kwake kumpongeza (Rais).

Alitoa madai hayo jana, alipohojiwa na Nipashe, kuhusu azma yake ya kuendeleza hoja ya utoaji wa taarifa zaidi za ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kuhusu kashfa za BoT.

``Ndio maana hadi leo sijampongeza Rais Kikwete kwa hatua alizofikia kuhusu BoT, kwa sababu hoja iliyojengwa kwa kuangalia fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA), ni kasma ndogo kati ya mabilioni ya fedha zilizohujumiwa,`` alidai.

``Mimi nilitoa tuhuma zilizohusu matrilioni ya fedha, lakini inashangaza kuona wananchi wanaonyesha kuridhishwa na taarifa ya ufisadi wa Sh. bilioni 133 tu, hizo ni fedha nyingi sana, lakini pia ni kiasi kidogo ikilinganishwa na fedha halisi zilizoporwa BoT,`` alizidi kudai.

Kuhusu Bi. Meghji, Dk. Slaa, alitoa mfano kuwa, Waziri huyo, alishiriki kupinga ripoti iliyowahi kutolewa na kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Delloit and Touche, ikielezea malipo hewa kwa kampuni ya Kagoda.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Bi. Meghji, alitoa tamko lenye kueleza kuwa, malipo yaliyofanyika kwa kampuni ya Kagoda, yalikuwa halali na yaliyotokana na shughuli za serikali.

Alidai kuwa, taarifa ya kampuni hiyo, ilipingwa na hatimaye Bi. Meghji, kuwafukuza wataalamu wa nje waliokuwa wanafanya kazi Delloit and Touche.

``Kwa hiyo utaona hapakuwa na sababu ya kutumia fedha nyingine kwa kampuni ya Ernst and Young, wakati taarifa za awali, ikiwamo ya Delloit and Touche, zilishabaini matumizi mabaya katika BoT,`` alidai.

``Kwa kuwa Meghji alishiriki kutoa taarifa ya kulinda uhalali wa malipo haramu kwa kampuni ya Kagoda, sioni sababu ya Rais Kikwete, kumuacha aendelee kuwapo katika wadhifa huo badala ya kumchukulia hatua kama zilizochukuliwa dhidi ya Balali,`` alisema.

Kuhusu hatua ya Rais Kikwete, kuitaka Bodi ya Wakurugenzi wa BoT kuipitia ripoti ya ukaguzi ya CAG, Dk. Slaa, alieleza wasiwasi kuhusu ufanisi wake.

Alidai kuwa, miongoni mwa mambo yanayosababisha wasiwasi huo, ni kuwapo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, miongoni mwa wajumbe wa Bodi hiyo.

Dk. Slaa, alidai kuwa Bw. Mgonja, alishiriki kusaini ripoti ya mwaka ya BoT ya mwaka 2005/2006, lakini saini yake na nyingine, zilionekana kuwa za mwaka jana.

Alipohojiwa kwa njia ya simu, Bi. Meghji, alikiri kuandika barua iliyopelekwa Delloit and Touche, ikihalalisha matumizi yaliyofanywa na kampuni ya Kagoda.

Alisema alifikia hatua hiyo, baada ya kufuatwa na Dk. Balali, aliyeomba kuandikiwa barua hiyo, kwa madai kuwa fedha zilizolipwa katika kampuni ya Kadoga, zilihusiana na masuala ya usalama wa nchi.

``Balali alinifuata na kuniambia fedha zilizolipwa Kagoda, zilikuwa for national security purposes (usalama wa Taifa), na kwamba Delloit and Touche walitaka barua ya ku-justify hivyo, nilimwambia akaandike na aliniletea, nikaisaini,`` alisema.

Hata hivyo, Bi. Meghji, alisema baada ya kusaini na barua hiyo kupelekwa Delloit and Touche, aliwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Gray Mgonja, aliyepinga hoja ya matumizi ya fedha zilizolipwa Kagoda, kwamba zilihusu usalama wa Taifa.

``Baada ya kupata maelezo hayo na kufanya vikao vya kiserikali, niliandika barua nyingine kwenda Delloit and Touche, kufuta barua yangu ya awali, na hivyo kumwagiza CAG kufanya ukaguzi uliosababisha Rais Jakaya Kikwete, kufikia hatua mnayoiona sasa,`` alisema.

``Kwa hiyo suala hili la ubadhirifu wa fedha za BoT nilianza kulishughulikia hata kabla ya Dk. Slaa, kupata vielelezo kupitia kwenye internet,`` alisema.

Naye Simon Mhina anaripoti kwamba, Naibu Gavana wa zamani wa BoT, Bw. Bob Makani, amesema Bodi ya Benki Kuu (BoT) haitafanikiwa kuwachunguza, kuwabaini na hatimaye kuwachukulia hatua maafisa wote waliohusika na kashfa ya ulipaji wa fedha kwa makampuni hewa kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Akiongea na Nipashe ofisini kwake jana Bw. Makani alisema Bodi hiyo ambayo mwenyekiti wake ni Gavana wa BoT, na wajumbe wengine ambao kimsingi sio watendaji, ndani ya chombo hicho hawataweza kufanya kazi hiyo.

Akifafanua, Bw. Makani ambaye pia ni mwanasheria, alisema ili bodi hiyo, iweze kufanya kazi ya uchunguzi, italazimika kupata taarifa na ushauri kutoka kwa watendaji ambao wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi.

Alisema kimsingi Bodi ya BoT inahusika na kusimamia sera za chombo hicho tu.

Alisema kitakachotokea ni kwamba bodi hiyo inaweza \'kufukia\' baadhi ya mambo.

``Wajumbe wa hii bodi hawawezi kufanikisha kazi hii, hawa kazi yao ni kupelekewa taarifa ya utekelezaji wa masuala yahusuyo Benki Kuu na kisha hutafakari kwamba sera za kifedha hazijakiukwa, hawana jipya,``alisema.

Alisema kinachoshangaza zaidi ni kwamba watendaji wa Benki Kuu watakuwa wanajichunguza wenyewe, hasa ikizingatiwa kwamba Gavana ambaye ndiye bosi na mwajiri wao, ndiye mwenyekiti wa Bodi.

``Hapa lazima kutatokea mgongano wa kimaslahi, hapakuwa na sababu ya Bodi kupewa jukumu hilo,`` alisema.

Bw. Makani alisema kimsingi dhamira ya Rais Jakaya Kikwete kutaka uchunguzi ufanyike na watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua, ni njema, lakini angeweza kuteua chombo kingine kufanya kazi hiyo.

Alikumbusha kwamba sakata la wizi na kughushi BoT zilianza zamani mno, hivyo hana imani kwamba kuna wajumbe hawahusiki moja kwa moja au kwa kupitia njia nyingine katika kashfa hiyo.

Alisema kwa uzoefu wake wa miaka mingi ndani ya Banki Kuu, hana imani na Bodi hiyo kufanya kazi iliyoagizwa na Rais.

Bw. Makani alisema kinachomfanya asiwe na imani na bodi ni kwamba miaka ya nyuma ililetwa kampuni moja toka Afrika Kusini kwa ajili ya kukagua vitabu vya BoT, lakini ikawekewa mizengwe na kisha ikatimuliwa.

Alisema anazo taarifa kwamba kampuni hiyo na mwakilishi wake walitimuliwa baada ya kubaini mchezo mchafu katika ulipaji wa makampuni hewa kupitia akaunti ya EPA.

Alisema kampuni iliyotiliwa shaka na wakaguzi hao, imo kwenye orodha ya makampuni hewa yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni uliofuatiwa na Rais Kikwete kutoa maelekezo kadhaa ikiwemo kumfukuza kazi Gavana wa BoT, Bw. Daudi Balali.

Bw. Makani alisema haamini hata kidogo kwamba wakaguzi hao waliondolewa bila baraka za bodi hiyo.

``Hili ndilo linanifanya nisiwe na imani na Bodi ya BoT kwa sababu imeshindwa kufuatilia mambo mengi sana, na siamini kwamba walishindwa kwa bahati mbaya, bali walifanya hivi kwa makusudi ya kimaslahi,`` alisema.

Alipoulizwa anashauri nini kifanyike, Bw. Makani alisema suala hilo linapaswa kushughulikiwa na vyombo vya dola.

Alisema kama ambavyo Rais alitoa agizo kwa Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Polisi na Mkurugenzi wa TUKUKURU, kuchunguza makampuni hewa yaliyolipwa, pia wangepewa jukumu la kuwasaka maofisa waliohusika.

``Kwa ushauri wangu hawa viongozi wa vyombo hivi vya dola, wangepewa majukumu yote kwa vile haya makosa ya makusudi yanaonekana yanakwenda pamoja,`` alisema.

SOURCE: Nipashe
 
Habari za kuaminika lakini ambazo hazijathibitishwa zinadai kwamba katika wiki 10 tangu CAG akabidhiwe ripoti na wakaguzi toka Ernst & Young na kuifanyia 'mchakato' kwa muda wote huo kulikuwa na majadiliano makali kati ya management ya Ernst & Young na viongozi wa juu wa siri kali.

Katika majadiliano hayo, viongozi wa siri kali walidai kwamba ripoti hiyo ikionekana na nchi wafadhili wanaweza kusimamisha misaada na mikopo ambayo inasaidia sana katika bajeti ya siri kali na hivyo kuuweka 'uchumi wa Tanzania' na 'usalama wa taifa' katika hali ngumu.

Viongozi wa Ernst & Young walidai kwamba professional ethics za wakaguzi zimewafunga mikono kubadili ama kufuta yaliyomo katika ripoti hiyo. Na pia watajiharibia reputation ya kampuni yao pindi ikijulikana walibadilisha ripoti hiyo baada ya shinikizo kali.

Inasemekana kwamba ripoti imechezwa, ila haijulikani kama ilibadilishwa kwa idhini ya Ernst & Young au bila idhini yao. Wakaguzi waliotayarisha ripoti walijua hili la kutaka kubadilisha ripoti lazima litatokea ili kulinda 'heshima' ya waliopo madarakani hivyo wakachukua ripoti ambayo haijabadilishwa ili kama kukitokea lolote basi wawajulishe umma wa Watanzania yaliyojiri katika ripoti hiyo.

Inasemekana pia baadhi ya mambo mazito yaliyomo katika ripoti hiyo kuna baadhi wanayo tayari na kama siri kali itaendelea kuwa na kigugumizi cha kuiweka ripoti hiyo hadharani basi wao hawatasita kuyaanika yote kwa Watanzania.

Inadaiwa pia sirikali inafikiria mara mbili mbili kuhusu kutoa ripoti iliyochezwa ndio maana wanafanya kila njia kuendelea kuificha ripoti hiyo kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu.
 
.. This guy ni mkoloni na mbaguzi mkubwa kabisa. Alitumia magazeti yake ya habari corp wakati wa kampeni ya ccm ya 2005 kumchafua kabisa Salim Ahmed Salim kwa kumuita majina ya ajabu ya kibaguzi.

Amekuwa anatumia biashara zake na pesa zake kuwanunua waandishi wa habari ili kuchafua wapinzani wa Kikwete. Amesikika mara kwa mara akimtukana Jenerari majina ya kibaguzi kutokana na msimamo wa Ulimwengu wa kutonunuliwa kwa pesa za wizi.

My sister are you talking about Jenerali Ulimwengu au mtu mwingine, huyu aliyenda kwa Rostam akimpigia magoti amwokoe na akamuuzia Habari Corp bei ya jioni! Are you sure about his hypocrisy na kujifanya hajanunuliwa na JK ? Kesi ya nyani dada yangu usiipeleke kwa tumbili! Lakini kwa JK ni mshikaji haswa, ukifika Dar ulizia wazee wa pale club next to nyumba ya sanaa, ndo utagwaya dada yangu!

Labda Jerenerali mwingine lakini kama ni Ulimwengu, labda uniambie kuwa hawakai chumba kimoja na BWMaliyeplekea majambazi waliompiga na kuiba passport tu, na alipoenda kuomba nyingine akaambiwa yeye Banyamulenge kumbe mwenzake naye Mmakua!
 
Mh! Ripoti haiwezi kuwekwa wazi ndugu! Watu si watauwana? Wabongo ni watu wa ajabu sana, amesoma ripoti ya EPA na kumfukuza Balali watu wakataka kuandamana. Yaani wanaona kafanya kitu kikubwa sana!!!!!! Na hilo ndilo alilohitaji, basi. Wewe ukimwambia atoe ripoti wakati hata vyama vya upinzani vimerithika na hatua hiyo .... Mh! Mungu isaidie TZ
 
Vyombo vya dola vilipewa miezi sita kufanya uchunguzi na hatimaye kuwachukulia hatua wahusika wote wa ufisadi wa shilingi 133 milioni. Je, kuna dalili ya kufanikisha azma ya JK au itakuwa ni usanii mwingine? maana miezi sita tangu ripoti hiyo itolewe inakaribia kukamilika.
 
Vyombo vya dola vilipewa miezi sita kufanya uchunguzi na hatimaye kuwachukulia hatua wahusika wote wa ufisadi wa shilingi 133 milioni. Je, kuna dalili ya kufanikisha azma ya JK au itakuwa ni usanii mwingine? maana miezi sita tangu ripoti hiyo itolewe inakaribia kukamilika.

Ni vigumu kujua kama kunadalili au hazipo kwani 'watu' wenyewe wamekuwa si wawazi. Wakati Kamati hiyo inaundwa ilielezwa kwamba watakuwa wanatoa taarifa kila mara 'wapi bana! zaidi ya hilo CCM ilitoa tamko kwamba Kamati hiyo ifanye kazi kwa uwazi, hamna uwazi kabisa.

Ila katika hili sisi hatutanyamaza ni vema wakatekeleza kiuungwana vinginevyo tutapiga kilele mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom