Ripoti ya BOT mbona haitolewi!? Walioiandika wanawekewa shinikizo ili waibadilishe?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Posted Date::12/6/2007
Marekani yasubiri kwa hamu ripoti ya BOT
John Stephen na Mwanaid Omary
Mwananchi

SERIKALI ya Marekani imesema inasubiri kwa hamu kubwa ripoti ya tuhuma za ufisadi katika Benki Kuu Ya Tanzania (BoT) ambayo tayari amekabidhiwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza jana na Mwananchi Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jeffery Salaiz, alisema kati ya mambo muhimu ambayo yanasubiriwa na ubalozi wake ni ripoti za tuhuma za rushwa ambazo zinaikabili benki hiyo.

Salaiz alisema kwa ujumla nchi yake haiwezi kutoa maoni yoyote kuhusu ukimya wa Serikali tangu ilipokabidhiwa ripoti hiyo na Kampuni ya Ernst& Young iliyoofanya ukaguzi katika benki hiyo kufuatia tuhuma za ufisadi zinazoikabili.

Msemaji huyo, alisema wanaisubiri ripoti hiyo kwa sababu Marekani inaamini kwa mtu yoyote atakayebainika kuhusika na tuhuma hizo, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Uongozi wa Serikali ya Tanzania tunaukabali na tunaimani kuwa watu watakaotajwa kuhusika katika ufisadi watachukuliwa hatua. Na kusema ukweli hatuwezi kutoa maoni zaidi kwa sababu ripoti hatujapewa,� alisema Salaiz.

Ukaguzi wa tuhuma za ufisadi ambazo zinazoikabili BoT, ulifanywa na Kampuni ya Ernst& Young katika kipindi cha siku 60 kuanzia Septemba, mwaka huu na kuikabidhi ripoti hiyo kwa CAG.

Mapema mwishoni mwa mwezi uliopita, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji alipoulizwa kuhusu ripoti hiyo, alisema bado iko kwa CAG na kwamba hafamu lolote kuhusu kilichomo ndani ya ripoti hiyo kwa sababu hajaiona.

Hadi sasa ripoti iko kwa CAG, sijaipata kama ni suala la maamuzi na nini kilichomo hadi ichambuliwe, nikiipata, nitaipitia, atapewa rais na maamuzi yatatangazwa kwa umma,� alisema waziri huyo.

Mbali na hayo, ripoti hiyo inasubiriwa kwa hamu na Watanzania ili kuona ukweli wa tuhuma za ufisadi ambazo zinadaiwa kufanywa katika Akaunti za Madeni ya Nje (EPA) kwa ajili ya malipo ya vocha mbalimbali.

Kampuni hiyo, awali ilipaswa kuikabidhi ripoti hiyo serikali Novemba 10 baada ya kumalizika kwa siku 60 za kufanya ukaguzi huo lakini haikufanya hivyo na iliiomba serikali wiki tatu kwa ajili ya kuandaa ripoti ambayo ilifanyika London, Uingereza.

Kampuni hiyo, ilipitia mahesabu katika kumbukumbu za vocha za malipo yaliofanywa na BoT katika kipindi cha mwaka 2005/6, kubaini kama kuna ukweli juu ya madai ya ubadhirifu wa fedha katika benki hiyo katika kipindi hicho.

Agizo la kutafuta kampuni ya kukagua vocha hizo na mahesabu ya BoT, lilitolewa na Waziri Meghji Desemba 3, mwaka jana akimtaka CAG kuteua kampuni huru ya wakaguzi wazoefu wenye sifa za kimataifa kupitia baadhi ya kumbukumbu za matumizi ya fedha za benki za mwaka 2005/6 ili kuondoa utata uliopo.

Katika hatua nyingine, Balozi wa Marekani nchini Mark Green amewataka Watanzania kutumia misaada inayotolewa na nchi yake kuzisaidia sekta mbalimbali ipasavyo kwani ni fedha zinazotokana na kodi za wananchi.

Balozi Green aliyasema hayo alipokuwa akikabidhi misaada ya compyuta na vifaa vya maktaba vya thamani ya zaidi ya Sh5 milioni katika shule ya Sekondari ya Kiislam Kionondoni inayomilikiwa na Baraza Kuu La Waislamu(Bakwata).
 
Mkuu Bubu,

Report iliandikwa kabla uchunguzi haujaanza kufanyika. Kinachofanyika hapa ni kuvuta muda ili ionekane jamaa wamechukua muda kweli kuandika. Report ilishaandikwa siku nyingi na ilishavuja.

Unakumbuka Mkjj aliandika parts za hiyo report hapa na namna itakavyokuwa na maneno.... pamoja na hayo... kasoro ndogo... sio kwa makusudi.....kazi vizuri na kwa mafanikio...sio kamili..

Kinasubiriwa tu itoke hiyo nyingine ili ilinganishwe na ile ya kwanza! Wanajua kuwa JF ina hiyo report na sasa wanagwaya!
 
Hivi Bwana Ballali bado hajapona tu?

Nina mashaka kwamba Ripoti hiyo inaweza kuwa na kasheshe na ndiyo maana wanasingizia kwamba bado iko kwa CAG. Ina maana CAG anaangalia namna watakavyoitetea serikali mbele ya IMF na nchi wafadhili?

Kama report ingekuwa iko poa, tangu imekabidhiwa nina uhakika kwamba lazima ingekuwa imeishawekwa hadharani na wangeiweka kwa kishindo kikubwa sana ili kuonyesha kwamba wapinzani ni waongo na hawana hoja. Huo ndiyo ungekuwa msingi/mtaji wa serikali katika kuonyesha kwamba hata ile list of shame is nothing bali majungu tu ya kisiasa.

Kama report ni mbaya, je, hata kama wakikaa nayo kwa mwaka mzima wataweza kui-doctor (kitu ambacho hakiwezekani) ili wafadhili waweze kurudisha imani kwa serikali ya Tanzania? Je, ni nani aliagiza uchunguzi ufanyike? Na kwanini akina Meghji wanasema report bado iko kwa CAG? Kuna umbali gani kutoka ofisi ya CAG mpaka Hazina kwa Mama Meghji? CAG anatumia majuma mangapi kusoma hiyo report kiasi cha kushindwa kuifikisha kwa Meghji aliyemwagiza atafute mtu wa kufanya uchunguzi?

Ukimya wa serikali kwenye kutoa report hiyo kunaleta maswali mengi sana! Sioni mantiki ya CAG kukaa na hiyo report wakati yeye jukumu lake lilikuwa ni u-tarishi tu kwamba alipewa jukumu la kutangaza tenda ya Audit na baada ya kumpata mtu anayefaa na report kuwa tayari alitakiwa akamilishe kazi yake ya utarishi kwa kuipeleka kwa mtu aliyemtuma afanye hiyo kazi. Sasa hapa naona kuna mazingaombwe kwamba CAG amekalia hiyo report wakati haimhusu hata kidogo.
 
Keil heshima kwako mkuu
Inawezekana Balali bado "anaumwa", au nadhani bado yuko chini ya "uangalizi" wa madaktari.
Hii ripoti inaonekana kuwa itakuwa na mengi yanayogusa maslahi ya watu, chama na serikali kwa ujumla. Inawezekana kuwa watu wamekaa kupiga hesabu kuangalia ramification zake, inawezekana ni sababu moja wapo iliyomfanya mkuu wa kaya aache safari ya kwenda Ulaya.
Let us wait and see nini kitapunguzwa!
 
cag sasa ana i-audit report? akishirikiana na Taasisi zingine za Serekali, then ndio mtapewa ikisha kuwa -imepunguzwa makali..
kama si hivyo then ikitoka hapo itaenda kuwa audited again hazina, from hazina Takukuru, then Police nao watai-audit, then Mwisho ikulu nayo ita-audit, kabla ya kutoa tamko.
Tunaogopa kuwahukumu watu bila ushahidi wa kutosha.
 
Ni zaidi ya wiki nne tangu tuambiwe kwamba ripoti ya BOT imekamilika. Je, kulikoni na ripoti hiyo, mbona haitolewi hadharani? :confused:
 
inafanyiwa editing,unataka mkanda bila editing?utapata mikanda yote miwili..
 
Inawezekana kuna mambo magumu ambayo wananchi hawatayaelewa kirahisi.

Wanafanya tafsiri sahii kwa baadhi ya mambo yasije kuleta madhara.
 
Imekwisha toka hiyo hakuna kitu tena. Ndio uzuri wa JK yeye atawaundia tume na matokeo mtayapata akiacha madaraka.
 
Nadhani sasa ni muda muafaka kwa vyama mbadala kutukusanya tujimwage jangwani kudai hii ripoti tuione!!, kwani hao wakaguzi wametumia hela zetu pia achilia mbali kwamba ni haki yetu ya msingi kujua mabilioni yetu yalienda wapi? na wahusika ni wepi tuwakabe koo warudishe kilicho chetu!
 
Inawezekana kuna mambo magumu ambayo wananchi hawatayaelewa kirahisi.

Wanafanya tafsiri sahii kwa baadhi ya mambo yasije kuleta madhara.

I really hope that you are being sarcastic maana hakuna kitu kinachonikera kama mawazo potofu ya wanasisiem wanaodhani kwamba they are the best thing after sliced bread na wananchi wote ni bumbubumbu! Never underestimate the mass, maana wanaelewa mengi sana!
Wizi ni wizi tu hata ukiremba vipi!
 
Ninadhani kuwa wizi uliionekana na mkubwa sana na kuna vigogo wakubwa sana serikalini wamekuwa implicated. Kwa kuwa watanzania tunajulikana sana kwa kusahau, basi wazee wana buy time kusudi tusahahu na hiyo ripoti iishie kapuni.
 
duhhh aliyesema husahau tuu kaniua kinyama comments kama hizo ningeweza ngekua nazipeleka kwenye jokes na udaku!!
abt the ripoti...nadhani zitakuaj jumlishwa zoote then zitolewe mwisho wa kipindi chake then wa tz wapate ripoti kamili ya uongozi wake!!kwani ripoti za kawaida za wanafunzi si hutolewaga mwisho wa muhula?

ila lets be serious wajimini ni another wastage of resources hiyoo kamati zaundwa kwa mkwara mzitooo ila nothing is done after kamati hiyo wala even kuongelewa basi hiyo ripoti
 
besides kama ile ya malima na mengi ilicost zaidi ya milioni ngapi sijui kujadili abt kashfa za watu je hii kamati imecost kiasi gani kujadili abt wizi wa mabilionii??nalo tujumlishiwe kwenye hiyo report na tukipata un edited ones ndo zawa nzuri sio zikiwa edited zishajazwa umbeya kibao
 
Aisee, hapa bandugu inabidi kushikamana, yaani na hili tusahau??? kwanza nawaomba waandishi mnao pita humu anzeni kutoa makala motomoto za kuchokonoa walete ripoti yetu kwani si yao peke yao!

Kwa kuanzia kuchokonoa andika makala za maoni ya wananchi jinsi tulivo na wasi wasi na dukuduku kwamba kimya hicho wapo wanaibadilisha!

Kwa uapande mwingine wakulu walioko jikoni juhudi ziongezeke za kutafuta ripoti original ikiwezekana mziki murua umwagwe humu JF, kwani huu naamini utakuwa malidhawa haswa!
 
Nadhani wako "kuipika vizuri", ili baadaye waje waseme kuna "kasoro ndogo ndogo" za kiutendaji BOT ili watu wasiadhibiwe na chama kisikose kura, upumbavu ulioje!
Nadhani Field Marshall atatuletea ripoti hii kwa muda mwafaka, maana namuaminia.
 
Nadhani wako "kuipika vizuri", ili baadaye waje waseme kuna "kasoro ndogo ndogo" za kiutendaji BOT ili watu wasiadhibiwe na chama kisikose kura, upumbavu ulioje!
Nadhani Field Marshall atatuletea ripoti hii kwa muda mwafaka, maana namuaminia.

kuhusiana na hiyo report kupikwa huko jikoni...kama kawaida yetu WaTanzania vyovyote vile ikitolewa na mpishi huko jikoni kwa smile lake lile hata iwe mbichi au imeungua sie tutaikubali tuu!!
namaanisha hata tuambiwe kulikua hamna kitu wrong na kashfa ilee sie tutasema hewala baba Tawileeeee!yaani kama tumelogwaaaa
 
kuhusiana na hiyo report kupikwa huko jikoni...kama kawaida yetu WaTanzania vyovyote vile ikitolewa na mpishi huko jikoni kwa smile lake lile hata iwe mbichi au imeungua sie tutaikubali tuu!!
namaanisha hata tuambiwe kulikua hamna kitu wrong na kashfa ilee sie tutasema hewala baba Tawileeeee!yaani kama tumelogwaaaa

Sitashangaa sana!
"Kigumu Chama Cha Mapinduzi"
 
Back
Top Bottom