Ripoti ya 2008: Maghorofa 100 hatari zaidi Dar

Ripoti ya 2008: Maghorofa 100 hatari zaidi Dar

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Nimeleta post hapa kuna baadhi ya wana JF wamenishambulia. Ama wamesahau, au hawataki kuujua ukweli wa huu mporomoko wa majengo dar. Tungezingatia yaliyoainishwa kwenye Tume ya Lowassa, haya yasingetokea. Tena basi, tutarajie maafa zaidi!! Swali ni je, baada ya Pinda kupata ukweli huu, amechukua hatua gani? Soma hapa:

Ghorofa 100 Dar bomu
Shadrack Sagati, Dodoma
Daily News; Friday,June 27, 2008 @19:01

Zaidi ya maghorofa 100 jijini Dar es Salaam yamebainika kuwa yalijengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge limeelezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi.

Lowassa aliunda tume baada ya jengo la Hoteli ya Chang’ombe Village Inn, Keko, Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibaini kuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku maghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi.

"Can you imagine, mtu kaamua kupandisha ghorofa lake hapo bila kufuata taratibu za mamlaka husika, hii ni hatari kubwa," alisema Pinda wakati anatoa majumuisho ya hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09.

Panda alisema maghorofa mengi yanayojengwa Dar es Salaam yanajengwa holela bila kufuata taratibu za ujenzi, hivyo kuyafanya kuwa hatari kwa maisha ya binadamu. Alisema kama hatua za haraka hazitachukuliwa na serikali, kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kwenye maghorofa hayo ambayo yanachipuka kama uyoga katikati ya Dar es Salaam, likiwamo eneo la Kariakoo.

"Tatizo ni kubwa…kuna hatari ya kupoteza maisha ya Watanzania wengi zaidi kuliko hili lililotokea juzi kama tukiendelea kuwaachia Manispaa suala hilo," alisema Waziri Mkuu. Alisema tukio la kuporomoka kwa ghorofa kulikotokea wiki iliyopita Kisutu, Dar es Salaam, ni uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamo wahandisi wa manispaa husika.

Alisema kutokana na taarifa hiyo ya tume, serikali inaandaa utaratibu mzuri wa utekelezaji wake kuhakikisha maghorofa yanayojengwa yanakuwa bora yanayofuata taratibu zote za ujenzi. Sambamba na suala hilo, alisema serikali pia inaangalia uwezekano wa kuingia katika Jiji la Dar es Salaam, kwani imegundulika kuwa manispaa haziwezi kuachiwa kuendeshwa jiji hilo lenye shughuli nyingi za uchumi.

"Ni lazima serikali tuingilie kati, Dar es Salaam haiwezi kuendeshwa na manispaa, lile ni jiji ambalo ni kioo cha taifa letu," alisema Pinda. Alisema serikali inaangalia mfumo bora wa uendeshaji wa jiji hilo, baada ya kuonyesha mfumo wa sasa wa kuwa na manispaa tatu umeshindwa kupata mafanikio.

Pinda pia ameliambia Bunge kuwa serikali imekubali kutenga Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Itigi kwenda Tabora. Alisema maeneo mengine yataendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu ili miradi iliyopo sasa ikitekelezwa, ujenzi wa barabara hiyo uanze mara moja.
​
 
Mkuu,

Sikio la kufa halisikii dawa...

Hata Nuhu aslisema sana kuhusu gharika watu hawakumsikiliza, alipojenga safina wakaanza kumcheka...

Watanzania tunavuna tulilopanda kwa kuichagua serikali dhaifu...
 
Nadhani ni mwendelezo wa mfumo uleule wa Janga linapotokea inaundwa Tume, then matokeo ya Tume yaweza kutolewa ama la kutegemeana na shinikizo la kijamii. Na inaposomwa uzoefu unaonesha watu wanakuwa wamesahau na vyombo vya habari havilipi uzito au pengine kuna tukio lingine kubwa limetokea katika nyakati hizo nayo Serikali inajisahau au inaacha kufanya utekelezaji. Hii imedhihirisha katika Tume mbalimbali zilizoundwa mfano, Tume ya kuchunguza tukio la kutekwa,kuteswa kwa Dr.Ulimboka Stephen haikutoa majibu, Tume ya Mwangosi ilizua mkanganyiko juu ya nani amehusika kusababisha kifo cha Daudi Mwangosi, na sasa kwa Kibanda naona Jeshi la polisi linapiga danadana. Hapo bado kuna tume ya Mtwara ambayo iliundwa naSpika baadae akaifuta, Kuna tume iliundwa katika mgogoro wa madaktari lakini hakuna majibu. Huu ndio utendaji wa Nchi yetu
 
Nalaumu CITY PLANNERS, ARCHITECTS NA CONSULTANTS wetu uchwara
 
Binafsi namuunga mkono Lukolo hata mimi nipo kwenye list ya kuukana uraia
[URL="https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/424902-kikwete-asipopelekwa-mahakamani-nitaukana-uraia-wa-tanzania.html"]Kikwete asipopelekwa mahakamani nitaukana uraia wa Tanzania
[/URL]
 
Kuna mengine mawili yapo chuo kikuu cha Dar-es-Salaam ambayo ni majanga yanayosubiri kutokea tu.

Ipo siku yata-make headlines.

Halafu wameya-overload.....siombi hii itokee ni hatari...na itakuwa simanzi kubwa labda itokee wakati wa likizo....Hall 5 walitoa bekons zote kulipunguzia uzito!
 
Tatuzo kubwa ni taaluma za mainjinia wetu/ makontracka/Bodi/halmashauri/sheria au wamiliki?
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibaini kuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku maghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi.
................................................................................

Panda alisema maghorofa mengi yanayojengwa Dar es Salaam yanajengwa holela bila kufuata taratibu za ujenzi, hivyo kuyafanya kuwa hatari kwa maisha ya binadamu. Alisema kama hatua za haraka hazitachukuliwa na serikali, kuna hatari ya watu wengi kupoteza maisha kwenye maghorofa hayo ambayo yanachipuka kama uyoga katikati ya Dar es Salaam, likiwamo eneo la Kariakoo.

..................................................................................

Alisema kutokana na taarifa hiyo ya tume, serikali inaandaa utaratibu mzuri wa utekelezaji wake kuhakikisha maghorofa yanayojengwa yanakuwa bora yanayofuata taratibu zote za ujenzi. Sambamba na suala hilo, alisema serikali pia inaangalia uwezekano wa kuingia katika Jiji la Dar es Salaam, kwani imegundulika kuwa manispaa haziwezi kuachiwa kuendeshwa jiji hilo lenye shughuli nyingi za uchumi.

"Ni lazima serikali tuingilie kati, Dar es Salaam haiwezi kuendeshwa na manispaa, lile ni jiji ambalo ni kioo cha taifa letu," alisema Pinda. Alisema serikali inaangalia mfumo bora wa uendeshaji wa jiji hilo, baada ya kuonyesha mfumo wa sasa wa kuwa na manispaa tatu umeshindwa kupata mafanikio.

​

yani wamiliki hawajapatikana kwanini?
kama serikali haijachukua hatua za haraka?
Waziri Mkuu atumie mamlaka yake kupitia Wizara husika na ikilazimu kupeleka miswada bungeni , itasaidia kupata majengo yenye uimara na kupunguza vifo , majeruhi na uharibifu wa mali unaosababishwa na uzembe, tamaa na incompetence.
 
Kuna mengine mawili yapo chuo kikuu cha Dar-es-Salaam ambayo ni majanga yanayosubiri kutokea tu.

Ipo siku yata-make headlines.

:rockon:Jamani tajeni majengo yote ambayo mna uhakika ni mabovu ili watu wayahame mapema kabla hawajafikwa na vifo vya kizembe. Saidia kuokoka maisha.:rockon:
 
Kungekuwa na Serikali makini naamini kabisa kuna watendaji (wakiwemo mawaziri), ambao Pasaka ya mwaka huu ingekuwa chungu kwao kutokana na kujivua wenyewe nyadhifa walizo nazo ama kuvuliwa kwa nguvu na MAMLAKA YA UTEUZI.
 
Kashfa za kila aina na watu wanaendelea na maisha kama vile hakuna jambo lililotokea. Hii nguvu ya ku-react tungekuwa tunaiweka kisayansi ktk utendaji wetu wa siku kwa siku ingetosha na kubaki. Tungekuwa Taifa bora na lenye ustawi na maendeleo makubwa lakini CCM imefanikiwa kutengeneza mfumo na utamaduni wa ovyo sana nchini, wao wanatengeneza matukio na watu wanashabikia kwa reactions.
 
Eti Bw. Manyerere mbona umeishupalia sana hii habari. Nimeshasoma nyuzi zako na michango zaidi ya mia moja juu ya hili.....hii kitu si bure lazima ndani yake iko mneno
 
Ni kweli mkuu panaitwa Yombo nyufa kila sehemu na hayana zaidi ya miaka kumi
 
Unaambiwa hivi , viongozi wetu wapo kwa ajili ya Kusaini Mikataba tu ili tupate Maendeleo , zaidi ya hapo mnataka wafanye nini tena ?
 
Kuna mengine mawili yapo chuo kikuu cha Dar-es-Salaam ambayo ni majanga yanayosubiri kutokea tu.

Ipo siku yata-make headlines.

hall 5 haikosi hapa. Lakini yale yataanguka kwa uchakavu na sio uzembe kwenye ujenzi. Haya hayamalizi hata miaka mitatu yanaporomoka kama tope.
 
Eti Bw. Manyerere mbona umeishupalia sana hii habari. Nimeshasoma nyuzi zako na michango zaidi ya mia moja juu ya hili.....hii kitu si bure lazima ndani yake iko mneno

Hapana maneno ndugu yangu. Naponzwa na spidi tu ya kuandika! Sitafuti herufi!
 
Back
Top Bottom