RIPOTI: Usiri unapelekea Tanzania kuendelea kuibiwa. Nchi inashika kasi katika viwango vya usiri wa fedha

Threads kama hizi huku TZ ni uchochezi kwahiyo usishangae ukatuhumiwa kwa uchochezi na hao majizi wakabaki
 
JK era: Mnaiba na kufisidi na ndani ya mwezi mnajulikana ingawaje hakuna hatua itakayochukuliwa!

JPM era: Mnaiba na kufisidi na hamjulikani ng'o na kwahiyo pia hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa!

CONCLUSION: JK = JPM

Consequences: Enzi za JK tuliijua mijizi ni nani kwahiyo kuwapa madaraka ingekuwa ni matunda tu ya u-shithole wetu!

After JPM, tutayapa madaraka majizi bila sisi wenyewe kufahamu kwamba ni majizi!

NOTE: Hivi kuna mtu anayeweza kunielimisha serikali ilitoa hoja gani hasa ya kujitoa kwenye mpango wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi?

Au waliochotaka ni Kuendesha Serikali kwa Usiri ili wananchi wasijue kinachoendelea?!

Na hilo la kutaka Kuendesha Serikali kwa Usiri ili wananchi wasijue kinachoendelea nadhani wamefanikiwa sana! Yaani kumbe tayari serikali ilishatoa milioni hamsini hamsini kwa kila kijiji halafu wananchi walikuwa wala hawafahamu kwamba kumbe migodi ilishatema.
:D:D:D:D
 
Tanzania imeingia katika orodha ya nchi zenye usiri mkubwa kuhusu fedha za viongozi wa serikali na siasa, wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoficha fedha nje ya nchi.

Fedha zinazohusika hapa ni zile zinazopatikana kwa njia za rushwa, uporaji wa mali na rasilimali za taifa na kukwepa kodi.

Kimsingi, fedha hizo hufichwa kwenye benki na taasisi za fedha za nchi, majimbo au visiwa ambavyo vina usiri mkubwa wa kutoa taarifa za “wateja” wao.

Tanzania inayoelezwa kukua kwa uchumi kwa haraka zaidi, ukitarajiwa kufikia asilimia 7 kwa mwaka huu, imepata alama 73 kati ya 100 zinazotolewa kwa nchi yenye kiwango kibaya kabisa cha usiri.

Sambamba na kupata alama hizo, Tanzania inashika nafasi ya 75 kati ya nchi 112 zilizohusishwa katika utafiti Mtandao wa Kupigania Haki ya Kodi (Tax Justice Network - TJN) wenye makao yake nchini Uingereza.

TJN hufanya utafiti wake kila mwaka, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Tanzania huenda ikaendelea kuwa na usiri mkubwa katika masuala yanayohusu fedha, uchumi na rasilimali zake kwakuwa imejitoa katika Mfumo wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP).

Mbali na kushindwa kutoa sababu za maana juu ya Tanzania kujitoa katika OGP, pia serikali yetu imeshindwa kuweka saini Mkataba wa Kimataifa Kushiriki kwa Pamoja Masuala ya Kodi (MATM); ambapo mataifa hupeana taarifa na kushirikiana kuhusu namna nzuri ya “kuwabana” wanaokwepa kodi.

Kushindwa kwa Serikali yetu hadi sasa kusaini mkataba huo wa muhimu wa kimataifa, kunatoa mwanya kwa baadhi ya Watanzania kuendelea kutorosha fedha na “kuzificha” nje ya nchi kwa manufaa binafsi.

Ujio wa Rais John Pombe Magufuli ulionekana kuwa neema na mwisho wa mafisadi kutorosha fedha nje, lakini wachunguzi wa mambo wanadai juhudi zake sasa zinatia shaka endapo kweli anasimamia kile anachokieleza kila mara kwamba yeye anaweka uzalendo mbele.

Tusubiri tuone kama mwaka kesho Tanzania itaondoka katika nafasi hiyo na kuwa na usiri zaidi au itaupunguza na kuwa nchi ya uwazi…

Soma hapa chini (PDF imeambatanishwa pia)

View attachment 692452[/QU

Tatizo ni ignorance, namna alivyojitengenezea kuogopwa na subordinate atapiga sana, ktk historia ya Tz ataweka record, rejeeni deni la Tf kupanda Mara dufu.
 
DU anachota mapesa kila kukicha in trillions hakuna uangalizi wowote ule wa kuhakikisha pesa hizo haziishii ndani ya mifuko ya majizi na wapiga madili Ikulu na wizara nyingine Serikalini. Kuna wizi wa kutisha awamu hii na kinara wa wizi huyo si mwingine bali lile jizi kubwa kuliko majizi yote nchini.

Tanzania imeingia katika orodha ya nchi zenye usiri mkubwa kuhusu fedha za viongozi wa serikali na siasa, wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoficha fedha nje ya nchi.

Fedha zinazohusika hapa ni zile zinazopatikana kwa njia za rushwa, uporaji wa mali na rasilimali za taifa na kukwepa kodi.

Kimsingi, fedha hizo hufichwa kwenye benki na taasisi za fedha za nchi, majimbo au visiwa ambavyo vina usiri mkubwa wa kutoa taarifa za “wateja” wao.

Tanzania inayoelezwa kukua kwa uchumi kwa haraka zaidi, ukitarajiwa kufikia asilimia 7 kwa mwaka huu, imepata alama 73 kati ya 100 zinazotolewa kwa nchi yenye kiwango kibaya kabisa cha usiri.

Sambamba na kupata alama hizo, Tanzania inashika nafasi ya 75 kati ya nchi 112 zilizohusishwa katika utafiti Mtandao wa Kupigania Haki ya Kodi (Tax Justice Network - TJN) wenye makao yake nchini Uingereza.

TJN hufanya utafiti wake kila mwaka, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Tanzania huenda ikaendelea kuwa na usiri mkubwa katika masuala yanayohusu fedha, uchumi na rasilimali zake kwakuwa imejitoa katika Mfumo wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP).

Mbali na kushindwa kutoa sababu za maana juu ya Tanzania kujitoa katika OGP, pia serikali yetu imeshindwa kuweka saini Mkataba wa Kimataifa Kushiriki kwa Pamoja Masuala ya Kodi (MATM); ambapo mataifa hupeana taarifa na kushirikiana kuhusu namna nzuri ya “kuwabana” wanaokwepa kodi.

Kushindwa kwa Serikali yetu hadi sasa kusaini mkataba huo wa muhimu wa kimataifa, kunatoa mwanya kwa baadhi ya Watanzania kuendelea kutorosha fedha na “kuzificha” nje ya nchi kwa manufaa binafsi.

Ujio wa Rais John Pombe Magufuli ulionekana kuwa neema na mwisho wa mafisadi kutorosha fedha nje, lakini wachunguzi wa mambo wanadai juhudi zake sasa zinatia shaka endapo kweli anasimamia kile anachokieleza kila mara kwamba yeye anaweka uzalendo mbele.

Tusubiri tuone kama mwaka kesho Tanzania itaondoka katika nafasi hiyo na kuwa na usiri zaidi au itaupunguza na kuwa nchi ya uwazi…

Soma hapa chini (PDF imeambatanishwa pia)

View attachment 692452
 
Acha ujuha wewe! Taratibu zimewekwa ili zifuatwe na wote bila ya kuzipindisha. Yeyote anayetaka kupindisha taratibu husika basi anafanya hivyo ili kutimiza adhma yake ya kufanya uovu kwani ni rahisi sana kufanya uovu pale taratibu husika zinapopindishwa tena makusudi.

Na huyu mpindishaji taratibu na history ya kufanya uovu mbali mbali ikiwemo kukwapua nyumba za Serikali, kukwapua bilioni 16 za wahanga wa tetemeko, kuipa mradi kampuni yake ya ujenzi kiwanja cha ndege Chato na uovu mwingine chungu nzima.

Hapa ndio tatizo lilipo. Inawezekana kabisa njia zinazotumika kupata wazabuni ni sahihi na zenye manufaa kuliko kutumia njia za kisheria zenye mapungufu na urasimu na pengine hata mabadiliko yake yanahitaji mjadala mpana na kuchukua muda mrefu.

Kilichotakiwa ni justification ya maamuzi hayo against normal procedures ....sometimes wengine tunajali zaidi values kwenye maeneo muhimu ....issue ni kuweka wazi walau kwa wawakilishi wa wananchi otherwise utakaribisha conspiracy za kila aina na pressure za bure while nia ilikuwa njema ....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom