Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
Tanzania imeingia katika orodha ya nchi zenye usiri mkubwa kuhusu fedha za viongozi wa serikali na siasa, wafanyakazi na wafanyabiashara wanaoficha fedha nje ya nchi.
Fedha zinazohusika hapa ni zile zinazopatikana kwa njia za rushwa, uporaji wa mali na rasilimali za taifa na kukwepa kodi.
Kimsingi, fedha hizo hufichwa kwenye benki na taasisi za fedha za nchi, majimbo au visiwa ambavyo vina usiri mkubwa wa kutoa taarifa za “wateja” wao.
Tanzania inayoelezwa kukua kwa uchumi kwa haraka zaidi, ukitarajiwa kufikia asilimia 7 kwa mwaka huu, imepata alama 73 kati ya 100 zinazotolewa kwa nchi yenye kiwango kibaya kabisa cha usiri.
Sambamba na kupata alama hizo, Tanzania inashika nafasi ya 75 kati ya nchi 112 zilizohusishwa katika utafiti Mtandao wa Kupigania Haki ya Kodi (Tax Justice Network - TJN) wenye makao yake nchini Uingereza.
TJN hufanya utafiti wake kila mwaka, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Tanzania huenda ikaendelea kuwa na usiri mkubwa katika masuala yanayohusu fedha, uchumi na rasilimali zake kwakuwa imejitoa katika Mfumo wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP).
Mbali na kushindwa kutoa sababu za maana juu ya Tanzania kujitoa katika OGP, pia serikali yetu imeshindwa kuweka saini Mkataba wa Kimataifa Kushiriki kwa Pamoja Masuala ya Kodi (MATM); ambapo mataifa hupeana taarifa na kushirikiana kuhusu namna nzuri ya “kuwabana” wanaokwepa kodi.
Kushindwa kwa Serikali yetu hadi sasa kusaini mkataba huo wa muhimu wa kimataifa, kunatoa mwanya kwa baadhi ya Watanzania kuendelea kutorosha fedha na “kuzificha” nje ya nchi kwa manufaa binafsi.
Ujio wa Rais John Pombe Magufuli ulionekana kuwa neema na mwisho wa mafisadi kutorosha fedha nje, lakini wachunguzi wa mambo wanadai juhudi zake sasa zinatia shaka endapo kweli anasimamia kile anachokieleza kila mara kwamba yeye anaweka uzalendo mbele.
Tusubiri tuone kama mwaka kesho Tanzania itaondoka katika nafasi hiyo na kuwa na usiri zaidi au itaupunguza na kuwa nchi ya uwazi…
Soma hapa chini (PDF imeambatanishwa pia)