Frankly speaking, NIPASHE wamethubutu kuandika Habari yenye uchunguzi wa kina, pongezi za dhati kwao, laiti habari kama hii ingewafikia wananchi from the grassroots level na wakapewa deep analysis ya kitu gani kinachosababisha hayo yote, ingekuwa ni turufu njema dhidi ya wanyonyaji hapo 2015. It's very sad kuna watu wanataka kuivua lawama Serikali kwa hoja dhaifu mno mithili ya nyumba ya buibui, hamna huruma nyie na Watanzania wenzenu? Maybe mpo ktk position ya kutoweza kukutwa na masaibu hayo ya Muhimbili, but kumbukeni ipo siku mtakayolipwa kwa kila dhulma mliyoifanya.
Naunga Mkono hoja kwa 100%; what is weird in all this kuna wahusika wakutoa habari hizi ambao ni government agents and independent agents wanaojiita NGO's au hata hospitali yenyewe kuja na ripoti ya self defence kuhusu hali yake kabla gazeti alijanasa na kutoa perspective yake.
Kama gazeti ndio limekuwa la kwanza kutoa extensive report of the problem ni kiashiria tosha tumejaza vimeo kwenye administration ya serikari na usimamizi hafifu kabisa. Inawezekana serikari imeliona kwa kumuondoa katibu wa wizara lakini waziri wake anafanya nini kama na yeye alishiriki kuona hali mpaka inafikia hapo hili ni swala la kufukuza wote sio mtu mmoja tu.
Mimi ndio maana ni mshabiki wa vijana kuwa mstari wa mbele sasa katika kuliongoza taifa letu, maana unakuta haya matatizo hayausiani na chama cha siasa directly lakini kuna wapambe wao watajitokeza kutetea uzembe ambao aujengi bali umekaa kujitia aibu na kuonyesha jinsi gani watu walivyo tayari kutetea hata uovu kwa sababu wazijuazo wao.
Chama tawala kinatakiwa kuwa makini kuhakikisha ilani yake inawafikia wananchi na hili kuweza kufanikisha hilo zoezi lazima iwasimie watendaji wa serikari na taasisi zinazotakiwa kutoa hizo huduma au hizo fursa kwa wananchi. Na huku ndipo katibu mkuu wao Kinana ameonya sana lakini hawa jamaa especially those in the supervisory role and decision makers kama mawaziri au raisi mwenye huwezo wa kuchagua kwa kweli amekuwa very slow to react on this matters. Kwa hivyo unaweza sema tatizo lingine lipo kwa wale wanaomshauri kwa karibu kuhusu maswala ya government administration.
Kiongozi wao mwengine ambae amekuwa sambasamba na Kinana muda wote kuhusu uzembe wa watendaji serikari juzi kwenye hotuba yake kasema ya ukweli kabisa pengine kwakuwa awezi kuyasema chamani kwenye mikutano yao ya CC or whatever the heck they call them. katika hotuba yake aliwasii vijana kuwa chachu yamabadiliko huko CCM maana wanawajibu wa kukiweka chama na wakati hili kukizi mahitaji ya jamii.
Na kwakweli nikisoma idadi za ajali barabarani (na uzembe wa usimamizi au ukaguzi plus regulations), ujambazi uliokithiri au imani za kichawi na social disturbance mara mtu kamfungia mama yake mzazi mara sijui mtoto mchanga katupwa wapi au mtoto wa la saba kaenda kuchunwa ngozi etc to do with people desperation acts (haya maswala ni largely poverty fueled acts), inafikia hatua hata genge la wahuni wanaweza funga mtaa na raia wakajifungia kwa woga polisi wako wapi; kama atuwezi zuia genge wahuni tutaweza zuia matukio ya kijambazi ambayo ni unexpected kweli kama huu uporaji wa fedha unaozidi kua tatizo.
Sasa kwakweli atuwezi kuendelea kuongozwa na watu wasioona changamoto zimezidi na hali ya walio nacho na wasio nacho inazidi kuwa mbaya jumlisha na utendaji mmbovu serikalini kutuletea huduma maana sasa hata huko ni mwenye hela ndio anapata huduma au mwenye kutoa hongo.
Huyu jamaa hapo chini ndio kawaambia ukweli indirectly na wenye masikio wamsikie ni wakati wakufanya overhaul thinking kwenye hiko chama chao especially for those with the role of decision making and the future direction; wabakize wazee tu wenye nguvu za kulinda yale yaliyo muhimu kichama na kwa maslahi ya muungano maana huko hawa vijana bado awa aminiki in my eyes.