Ripoti hii ilifichwa: Chanzo cha kuporomoka Elimu Tanzania!

OFISI ya waziri mkuu imekaa serious,kutafuta suluhisho serious la taifa...kwa nini usi appreciate serikali yako inapokuwa bold?
 
Maslahi duni ya walimu mbona cjaiona kwenye ripoti jamani ........au...
 
Ninapoyaona haya mpaka leo nashindwa kuelewa hivi hawa wanaoendelea kuisapoti hii serikali wana akili ya aina gani??, matatizo ya kushuka elimu yako wazi kabisa, na tume ilishaundwa watu wakala pesa, muda, na malighafi mbalimbali zikatumika, then kwa makusudi pinda akakataa ripoti hii isitolewe hadharani 2011 leo miaka 2 baadae anaunda tena tume ya kuchunguza tattizo lilelile kwa kutumia gharama zaidi... Na hii ripoti ya hiyo kamati haitasolve lolote wala kusomwa popote tena..

adui wa maendeleo ya watanzania ni watanzania wenyewe...
Bahati mbaya watanzania mnafanya kila kitu siasaMnapaswa mjue kuwa Elimu yetu haijashuka isipokuwa kilichoshuka ni kiwango cha Ufaulu ambacho kinasababishwa na wanaotakiwa kufaulu kutotaka kufaulu. Siasa zimewapotosha watu kiasi kwamba Wazazi, Jamii inayowazunguka wanafunzi na Wakati Mwingine Walimu kutotimiza wajibu wao kwa vile kila mmoja amekariri usemi wa Mwana -------- ni mzigo wa mamaye.
Kama Watanzania hatutabadilika na kukiri kwamba usimamizi wa wanafunzi wetu ili wafaulu ni jukumu la kila mmoja tutaendelea kupiga kelele tu hata kama nchi hii itatawaliwa na Mitume au Malaika kwani uzinzi,starehe na Elimu havitangamani kamwe. Habari ndiyo hiyo pompompo watupu
 
Walimu wamewekwa nyuma hawawez kuzungumziwa,siunajua kuwa wao ni daraja la kupitia kwenda Ikulu na Bungeeniii?


Bomoa daraja, alafu tuone watapitia wapi. Walioshindwa kidata cha IV ndio wanaofundisha watoto wa shule ya Msingi. Kwa maana hiyo mwanafunzi anayefaulu darasa la saba anaongozwa tu kujipeleka sekondari.
 
Wao wanalinda ajira, kazi hawafanyi. kama wewe unaendelea kuuliza maslahi kwenye ripoti, kalagha bao. Maslahi yao ni kuuza ubuyu na vitenge vya kukopeshana. kama kweli wanafundisha watoto wangekuwa wanafaulu mitihani. Kwa vile wanalinda ajira... wanafika kazini kusaini daftari la mahudhurio. Maandalio ya somo ni miongoni mwa vitendea kazi ambavyo havitumwi mashuleni. Sasa mwl afanyeje....?
 
Dr. Slaa anaambiwa kutubu... je toba ya walionunua rada ya magumashi ilisikilizwa na nani? Chenji ya radi iko wapi? Nasikia imenunua vitabu vyenye makosa kimantiki. Ama kweli Fungu la kukosa .... ni la kukosa.
 
Back
Top Bottom