RIPOTI: Gaddafi aliuawa kimakosa

Ni matatizo gani unayoyakusudia na ni nchi gani hizo ambazo hazina matatizo kwa sababu ya kubadili uongozi?
Na kwanini waafrika matatizo yetu yawe viongozi tu miaka nenda rudi kwani hao viongozi tunawapata wapi?
Ni maisha gani walikuwa nayo walibya yenye kuhitaji ukombozi wenye gharama za kuvumilia hichi wanachopitia? Ni humo kukaa kwenye vibanda ndio kuliko hitaji ukombozi wenye gharama ya vita?
 
Mzee unalalamika nashindwa kuelewa point hasa ni ipi?
 
Shida ni kujifanya tunayajua sana maisha ya Walibya, tunawaelezea kama watu ambao walikuwa na maisha ya raha sanaaaaaaa, wengine wenu mkaenda mbele kiasi cha kusema walisomeshwa bure hadi chuo kikuu.

Swali la msingi: hawa watu waliosomeshwa hadi chuo kikuu, ndio hao hao waliodanganywa kijinga na 'mabeberu' kiasi cha kumuua mgawa riziki wao?

Shida yako huamini katika uhuru. Mtu mwenye nafsi yenye utumwa haamini katika uhuru. Hudhani kuwa watu wana hiari ya kuamua waongozwe na nani. Kwa maoni yako, Gadaffi ni lazima apendwe (japo wewe si Mlibya). Benin, Gabon, Jamhuri ya Africa ya Kati na Gambia zimekuwa na viongozi wamekaa muda mrefu madarakani, kwa mtazamo wako ile ndio AMANI? Kwa kuwa wanakula na kulala basi wasithubutu kubadili uongozi sababu aliyepo hataki kutoka kwa hiyo vita itakuja?

Umeuliza nchi gani ambazo hazina matatizo kwa kuwa zinabadili uongozi...sijui swali la aina gani hili. Umeshasikia Ghana, Cape Verde, Namibia, Botswana, Zambia au Mauritius kuna mtu anamkaba mwenzake na vifaru aachie madaraka?

Kuna aina fulani ya UNYAMAPORI inatuathiri sana. Hatuna succession plan. Kila anayeingia madarakani anataka atawale badala ya kuongoza, anaamini yeye ana akili kuliko taifa zima, akili za kimugabe. Akili za kisultani ni akili za hovyo.
 
Kwa nini asingeanza kwa kuruhusu waafrica wote waingine Libya kirahisi rahisi
Are you serious kuuliza Hili swali? Seems mkuu hufahamu lolote kuhusu Libya. Kwa taarifa yako tu.

Gadaffi karibia alimaliza tatizo la Ajira Libya na nafasi zilikuwa nyingi zaidi akafungua mipaka nchi kibao za jirani zikawa zinaenda kuajiriwa. Libya walikuwa na tatizo la Skilled labour, nchi Kama Nigeria, Niger, Chad, Sudan na nchi za karibu walineemeka Sana


Baada ya Gadaffi kupinduliwa Sasa Hivi kila mtu amekimbia Sasa Hivi Libya imebaki tu sehemu ya watu kukimbilia ulaya.
 
Loh mkuu unaruka hoja Kama chura, ulikuwa unazungumzia idadi ya walibya waliokuwa wanampenda/kutompenda Ghadafi hayo mengine ya marekani, sijui nchi za kiaAfrica sijui hata yameingiaje. Bdw marekani hajashiriki Vita Hivyo mainly alikuwa Ni Mfaransa na muingereza kidogo.
 
Huwezi kuelewa ninachozungumzia kuhusu Afrika na Marekani huenda shule imekupita kushoto. Unajua AU ilianzishwa kwa madhumuni gani? Ufaransa tangu lini akawa na uadui na Libya? Aliyeratibu mipango yote ya vita ni Marekani, ufaransa na Uingereza walishiriki ili kuwapoteza maboya. Hapa JF hakuna lolote litakalosaidia zaidi ya kupiga kelele tu. Ghadafi ameshauwawa tayari. Wewe vimba upasuke, sijui walimpenda lakini ameshakufa hivyo. Na wakimtaka mwingine wanaua tena halafu watu wanakuja tena hapa JF kupiga kelele. Walimtaka Sadam Hussein wakamkata wakamnyonga, watu wakapiga kelele weweee. Wakamkamata Osama naye wakamnyonga, watu wakapiga kelele na uchungu mwingi, wakamkamata Ghadafi naye wakaua, watu wakapiga kelele wewe. Marekani, uingereza na washirika wake wanamaliza mmoja mmoja ambaye anajifanya mbabe. Huyo Ghadafi aliingia kwa mabavu baada ya kumpindua kiongozi aliyeoko madarakani ili akae yeye na akapinduliwa. Wewe unakaa madarakani miaka 36 na zaidi kwani hakuna watu watakaongoza Libya? Wafrika wanaonea huruma LIbya wakati wao ndiyo masikini mpaka basi. Watu kama nyinyi ndiyo mnaharibu nchi. Wewe na wenzako mnataka muandamane ili Magu akae madarakani mpaka atakapochoka na mnadai uchaguzi usifanye sababu atapita na hela itapotea. Unajua maana ya kuwepo kwa katiba na sheria za nchi? Huyo Ghadafi alitaka ajimilikishe Libya ambapo ni kosa kubwa sana ambalo lilipelkea mpaka kuwawa. NI SAWA NA KWENU ULIPOZALIWA MPO WATOTO 5 HALAFU MALI ZA NYUMBANI UNATAKA KUZIMILIKI WEWE PEKE YAKO. LAZIMA UTAUWAWA. NDICHO ALICHOKIFANYA GHADAFI. NAKUSHANGAA UNASEMA WALIKUWA WANAPEWA MAHITAJI YOTE KWAHIYO WATU WALIBYA WALIKUWA HAWAFANYI KAZI? JE, USHAWAHI KUFIKA LIBYA UKATHIBITISHA WALIKUWA WANAHUDUMIWA KILA KITU NA GHADAFI AU UMESOMA MITANDAONI TU? VIONGOZI WA AFRIKA WAPUUZI SANA WEWE UNAKAA MADARAKANI MIAKA ZAIDI YA 10 HALAFU UKIUWAWA WAMEKUONEA.
 
Mzee unalalamika nashindwa kuelewa point hasa ni ipi?
Wewe endelea kujiliwaza JF wala haibadilishi ukweli. Unayempenda ameshakufa tayari. Walimtaka Sadam Hussein wakamkata wakamnyonga, wakamkamata Osama wakanyonga na wakamkamata Ghadafi wakamuua kama kibaka wa mtaani. Angekuwa anapendwa na watu IRAN anayejigamba ana silaha kali sana na North Korea wangemsaidia. Kiufupi alikuwa hapendwi na wanalibya walikuwa wamemchoka. Hata Mugabe alitolewa na jeshi kwa sababu walimchoka ila kwa vile alijiongeza hakutaka vita na mtu.
 
Kutimia ama kutotimia kwamlengo yao hilo sio swali swali ni nani alomuua ghaddafi

Unahisi bila msaada wa mabebru gaddafi angekufa ?!

LIBYA Ingekua hv ilivyo leo

Mabeberu wauaji sanaaa washenzi
 
sikuwa informed sawasawa mkuu. Now I am.
 
HAPo umenena! Ili nchi iwe na maendeleo endelevu inahitaji taasisi imara na sio kumtegemea binadamu.

Hizo taasi zinajemgwa na watu wenye tabia mbalimbali sio namna yoyote yakujenga taasis immara bila kuwa na watu waadilifu , na imaera
 
Kutimia ama kutotimia kwamlengo yao hilo sio swali swali ni nani alomuua ghaddafi
Unahisi bila msaada wa mabebru gaddafi angekufa ?!
LIBYA Ingekua hv ilivyo leo
Mabeberu wauaji sanaaa washenzi
Asingeuwawa ila angejiimarisha kama Kuruzinza au mwenzake wa Uganda. Maraisi wa Afrika waroho sana wa madaraka. Wanaona kama nchi za kwao. Nchi ya wanalibya halafu wewe unataka ujimilikishe. Wewe ni nani? Angekubali tu kama mwenzake Mugabe angepungukiwa nini?
 
Kati yahao ulo wataja kuna alojiimarisha kwa kipi[emoji23][emoji23]

Labda kuwatia dhiki na njaa raia wamataifa yao
 
Ttzo la watu wamejawa na chuki na kusikiliza zaidi propaganda juu ya jamaa ila jamaa alikua maana halisi kabisa ya kiongozi

Hakuna nchi ambazo hazina demokrasia kama za wazungu kama hawa wa UK hawa Wana Jiita Kabisa United Kingdom Ila wanajifanya kusambaratisha nchi za wenzao kwa kiaingizio cha demokrasia


Wajamaa wauaji sana wamemtanguliza ghaddaf wa wa2 bureee ila sio mbaya nawao watamfuata 2
 
Tatizo la msingi kwenye kulaumiana kwa mabeberu sio kumtoa Gaddafi per se.

Bali ni kutokuwa na plan what happens next wakishamtoa kwa stability ya nchi, hayo makundi waliyokuwa wanayasaidia walikuwa hawayajui kwa undani.

In short kukurupuka kwao Libya kumtoa mtu aliekuwa anaweka stability ndio kumeleta madhara yanayoendelea leo.

Hila Gaddafi mwenyewe walikuwa wanamlia timing tu, bila ya msaada wake Irish Republican Army (IRA) wasingekuwa na financial wala military resources za kuisumbua UK.

Kupitia Gaddafi kuanzia early 70’s mpaka miaka ya 90’s ndiye aliyewapa jeuri ya kusumbua jeshi na uwezo wa kutengeneza mabomu yaliouwa watu wengi sana North Ireland na mainland UK.

Kwa hivyo Gaddafi was always on their wish list, tatizo ni kutoondolewa responsibly hapo ndio wanapolaumiana.
 
That was obvious.
No need to research on obvious.
 
Unajua wewe hujanielewa mie sipo hapa kumtetea Gadaffi bali nacholaumu mimi ni walibya kuingiza nchi yao kwenye vita na sasa kuwa wakimbizi kwa sababu tu et Gadafi alikuwa hatoki madarakani huo ndio ujinga ninaoupinga na kuona kutoka kwa walibya,mimi sizungumzii hayo sijui ya sijui walibya waliishi maisha ya raha wala shida hoja yangu ni hicho kitendo cha kuharibu nchi sasa kama wewe mkuu uliwahi kuishi Libya na ukaona walibya maisha yao waliyokuwa wanaishi kwamba walikuwa wanastahiri kufanya hichi walichofanya basi sawa ila kama sababu yenyewe ya walibya kuingia vitani huku wakijua watapitia haya wanayopitia kisa tu Gadafi kung'ang'ania madaraka basi hiyo sababu tambua ni ujinga.
Hata hapa Tz Ccm inang'ang'ania madaraka je ndio ukipewa mtutu uanzishe vita kama nfio njia ya kuiondoa ccm utakubali?

Halafu waafrika inaonesha hatujui ni nini tunataka,yani mkianza kuzungumzia habari za kubadili viongozi mtu anaweza kusema afrika hawana matatizo zaidi ya viongozi wao tu kung'ang'ania madaraka lakini kumbe hata hizo nchi zinazobadili viongozi na kusifiwa kwa demokrasia bado tunaona nchi zao zina matatizo kibao na wakati mwengine hupelekea fujo mbambali.
 
Sasa mbona ametoka ,wapo wenyewe Nchi haitawaliki,pale angesema naondoka ,kundi linalomtaka na wasio Mtaka wangevurugana sasa hakukua na msingi mzuri
 
Hoja yako ni ipi mkuu bado hujaeleweka naona unabwabwaja tu? Kuna sehemu nimesema nilikuwa nampenda Gadafi humu?
 
Sheria ,kuhoji na democrasia hivi madikteta wanaviogopaga sana.pamoja nagaddafi kutoa huduma zotehizo kwaraia,olewako uthubutu kufanya vitu vitatu tajwa hapo juu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…