RIPOTI: Gaddafi aliuawa kimakosa

Walibya walikuwa na option ya kuepuka haya madhara hakukuwa na ulazima wa kutumia nguvu zaidi ili tu kumuondoa Gaddafi,sasa hebu jiulize kipi hasa kilichowalazimu kuingiza nchi kwenye machafuko ni kumkomoa Gaddafi au kuna sababu ya msingi ambayo inaweza kufanya tusiwalaumu walibya kwa haya madhara yaliyopo kutokana na uamuzi wao wa waliyoufanya? Ulevi wa madaraka unajulikana hivyo walibya wangetafuta njia nzuri ya kudeal na hilo lakini walichofanya haukuwa uamuzi sahihi,unafikiri hata Gaddafi angejiondoa mwenyewe ni kipi wangefaidika walibya kwa kujiondoa kwake Gaddafi? Ndio maana nasema wametumia nguvu kubwa na kuingiza kwenye vita hali ya kuwa hakukuwa na ulazima huo. Kuishia kumtupia lawama tu Gadaffi katika uchu wake wa madaraka kwamba yeye ndio wa kulaumiwa ni sawa na kumlaumu mwanamke aliyeuliwa na mumewe kwa sababu ya usaliti.
 


Waliokuwa hawamkubali ni wachache sana, pengine hawafiki hata milioni moja...mabeberu wajanja sana, wakishaona nchi za kiafrika zimekuwa kiuchumi basi ujuwe watakufanyia kila njia uporomoke, hata wakifa wananchi wako sawa tu ilimradi lengo lao litimie.
 

Tatizo ni pale wachache wanapokukataa lakini wengi wanakukubali sana.

Halafu hao wachache wabebe silaha waanzishe uasi kisha wasaidiwe na NATO, kiufupi inabidi usimame kidete ulinde haki ya wengi, huo ndiyo uongozi ulivyo, hakuna kiongozi anayependwa 100%
 
Thread closed.
 
Kuna mambo ya kijinga sana yametujaa vichwani waafrika kiasi huwa nashangaa tunawezaje kujenga nyumba isianguke ikiwe hatujui umuhimu wa MSINGI.

1. Ili tuendelee, tunahitaji TAASISI IMARA na sio KIONGOZI IMARA. Gaddaffi hakuwa TAASISI, alikuwa KIONGOZI MBINAFSI asiyekumbuka kuwa siku moja angekufa. Kwa mfano asingeuliwa na aliowaudhi akafa kwa kugongwa na gari la farasi kwa bahati mbaya, Walibya wangelazimika kumfufua?

2. Si kweli kuwa Walibya wote walikuwa wakineemeka na utawala wake. Hakuna mtawala kwa mabavu asiye na wafuasi. Kinachotofautiana na idadi ya hao wafuasi na mirengo yao, maana ndani yao kuna WANAFIKI na WAKWELI. Wanafiki hawanaga ushirika wa kudumu, siku ukianguka wanageuka na kuwa washirika wa aliyekuangusha. Wa kweli hupigana pembeni yako hadi mwisho...Je, kuna dalili ya kundi kubwa kumpigania Gadaffi hadi mwisho?

Ukisoma kitabu cha Things Fall Apart cha Chinua Achebe, utajifunza kitu kuhusu HAKI na USAWA unavyotukwamisha. Lilikuwapo tabaka la watu waliotengwa ndani ya jamii ya Ibo ambalo lenyewe lilikuwa la kwanza kushawishika kujiunga na Wamisionari sababu hawakukubalika na jamii yao. Hawa wanafanana na Walibya walioishi kwenye vile vibanda vilivyochoka kule Benghazi, hawa hata kama ungelikuwa ni wewe...ungeitikia wito wa kumng'oa Gadaffi.

Waafrika tujifunze kuheshimu zile fundamental human rights. Hata ujenge bahari kila mkoa, ukiutweza utu wa mwanadamu, hautaungwa mkono kwa moyo, utaungwa kwa woga na hila.

3. Jambo la tatu lenye kunifikirisha nisipate majibu ni hili la kuwa ukioa sijui na kufanyaje basi utapata pesa bure kutoka kwa Gadaffi. Ikiwa haya ni kweli, ina maana Walibya hawafanyi kazi, maana kazi tunafanya ili tuweze kujikimu. Kuna serikali yenye kuweza kuadvocate maisha ya namna hiyo kwa wananchi wake? Walibya si sehemu ya manusura ya wahamiaji haramu wanaookotwa pwani ya Italia pamoja na Waafrika wengine wa Kaskazini? Je kuna watu wanaokimbilia Libya kutafuta kazi kama ilivyo USA, South Africa na Saudia Arabia?

Kwangu mimi Gadaffi ni FAILURE. Kiongozi asiye na plan ya kuwaandaa wengine kuchukua majukumu yake ni mbinafsi na wa hovyo kabisa. Badala ya kutengeneza uongozi endelevu kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi, akajitengeneza kuwa mungu, na sasa ni marehemu.
 
waache Walibya wale jeuri yao!
 
Kama Gaddafi angefanikiwa kuifanya sarafu moja ya umoja wa Africa, nchi ya USA na Umoja wa Ulaya zingekuja kununua madini kwa thamni ya pesa ya Africa.
 
WHAT HAPPENED IN LIBYA .., WHAT IS HAPPENING IN LIBYA NOW ,, AND WHAT WILL HAPPEN IN LIBYA IN FUTURE TIMES.,,, IS LIKE THE TEARS OF THE SUN .,,THAT NEVER DRIED.......
 
Yaani kweli sisi wote hapa tulikuwa tunasubiri report ya kamati ya Bunge ya Uingereza kutambua makosa yaliyofanywa ktk mauaji ya gadhafi?
 
Ukiwa kiongozi lazima utumie busara, hekima, akili nyingi na nguvu kidogo. Na hapa mabeberu ndiyo wanapotushinda na mwisho wa siku tunabaki kuwalaumu huku majanga yameshatokea. Alipoamua kupambana na watu wachache aliweza kuwashinda? Unapoingia na adui vitani hata kama ni watu 20 lazima ujiulize hawa wanajiamini nini? nani walioko nyuma ya adui yako. Adui anasilaha kali kuliko wewe halafu unasema upigane naye. Lazima ujiulize hawa silaha wametoa wapi? Hiyo vita Ghadafi alishinda? Wewe unafikiri kwanini Marekani haijaivamia Irani au north korea? Kwasababu wanatumia akili nyingi na nguvu kidogo. amepiga hesabu hasara ni nyingi kuliko faida. Watu wanakaa mezani wanajadili faida na hasara zitakazotokea. Wakiona hasara ni nyingi kuliko faida wanapiga chini mpango wa vita. Ni sawa na mtu A anataka apigane na wewe halafu kuna mtu B hakupendi anakuchukia. Huyu mtu B lazima ashirikiane na mtu A kukupiga wewe. Mabeberu wanashinda siku zote kwasababu wanatumia akili nyingi na nguvu kidogo. Shida ya viongozi wa Afrika wanatumia nguvu nyingi akili kidogo ndiyo matokeo yake hayo. Watu wakiandamana kidogo utawaona FFU wanakuja na bunduki, mabomu na magari ya kuwashawasha wakati waandamaji hawana hata fimbo mkononi.
 
Hawana lolote wapuuzi tu hawa
 
Africa tumezidi ujinga,ni sawa na wale elections observer,huwa European Union wakitoa comments zao hasa zikiwa + unakuta watu wanashangilia
Yaani kweli sisi wote hapa tulikuwa tunasubiri report ya kamati ya Bunge ya Uingereza kutambua makosa yaliyofanywa ktk mauaji ya gadhafi?
 
Mjanja siku zote ndiyo anashinda. Wewe unapigana na watu wachache hata hujiulizi hawa wachache wamewezaje kuivimbia serikali iliyoko madarakani? Shida ya viongozi wa Afrika wanatumia nguvu nyingi na akili kidogo wakati mabeberu wanatumia akili nyingi na nguvu kidogo. Ushajiuliza kwanini Marekani haikuivamia North Korea? Wamekiri wamemuua Ghadafi kimakosa. Ni nani aliyemuua Ghadafi? je, nani atashitakiwa kwa kumuua Ghadafi? Watu wameshachukua mafuta na wameacha lawama. Hao ndiyo mabeberu. Kasome Capitalism na Neo-colonialism ndiyo utajua hawa watu wanaakili nyingi sana ili uweze kuwashinda lazima na wewe utumie akili nyingi.
 
HAPo umenena! Ili nchi iwe na maendeleo endelevu inahitaji taasisi imara na sio kumtegemea binadamu.
 
Ume elezea mengi sana mkuu ila point inarejelea pale pale asee yakwamba maamuzi yao hayakua sahihi na kwa nnnwalifanya waloyafanya uonevu na kutetea maslahi yao kwanjia zakishenzi
 
Leo hii tuona Marekani ambayo inawezeka kuipiga Iran ila inashindwa kukurupuka kufanya hivyo kwa sababu ya wanajua kutakuwa na madhara makubwa endapo wataamua kufanya hivyo kwa maana hiyo lazima watafute njia ambayo haitaweza kuleta majanga, Mkuu yaani huko juu koote na chini yake nimekubaliana na ww ila hcho kipengele chako nlokikopi hapa ndio sijakubaliana na ww mkuu

Kama Kweli US anakhofia hicho pale IRAN Angefanya juu chini akamaliza mgogoro wa SYRIA

Angefanya juu chini Akaumaliza Mgogoro Wa YEMEN

Angefanya juu chini akaumaliza huu mgogoro unaoendelea pale LIBYA Badala yake anajua kuna serikali inayotambulika kimataifa ila jamaa anaenda kumuunga mkono KHAFTAR


Nikwambie 2 US Anacho Ogopa IRAN nihasara zitakazo tokana na ile vita Halina Ubishi kwamba IRAN Anaweza akapigwa tena vibaya na sana ila IRAN Nae atalipiza majibu kwa ukali sanaaaa

Hvyo ss US Anajiuliza ana anzaje kuingia vitani na MUAJEMI Hizo zakusema cjui anakhof nn cjui nn ni habari 2 vijiweni vyakahawa ila ukweli Ndio Huu MKUU
 
Ume elezea mengi sana mkuu ila point inarejelea pale pale asee yakwamba maamuzi yao hayakua sahihi na kwa nnnwalifanya waloyafanya uonevu na kutetea maslahi yao kwanjia zakishenzi
Ghadafi ameuwawa. Je, aliyemuua Ghadafi ni nani? Na nani atashitakiwa kwa mauaji ya Ghadafi?
 
Gaddafi kauliwa kimkakati...

He was a very strong leader, a leader with missions and visions not only to libya but to whole of Africa...


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…