Mtanzania Safi
Member
- Oct 9, 2014
- 95
- 13
Jambo Leo j/mosi desemba, 6 2014
Na, Peter Ambilikile.
RIPOTI ESCROW YATUA KWA JK, IKULU WADAI KINA NGELEJA WANAONEWA.
Sakata la Akaunti ya Escrow limetua ofisi ya raisi kwa hatua nyingine za uamuzi kuhusiana na viongozi wanaotuhumiwa kuchota zaidi ya sh. bilioni 306 kutoka benki kuu ya Tanzania (BoT).
Hatua hiyo imekuja baada ya bunge kuazimia kuwa, viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo wachukuliwe hatua na mamlaka ya uteuzi kwa kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili tangu ripoti hiyo itolewe bungeni umebaini kuwa,mamlaka ya uteuzi haitachukua hatua za kumwajibisha kiongozi yoyote kwa shinikizo au hila hadi itakapojiridhisha na tuhuma zinazowakabili .
Hata hivyo; gazeti limedokezwa kuwa, mamlaka ya uteuzi inafanya kazi zake kwa kuzingatia msingi wa utawala bora na wa sheria na si vinginevyo, kwani taasisi ya uraisi ni nyeti, hivyo haiwezi kufanya kazi zake kwa mfumo wa bendera kufuata upepo.
"Kitu kikubwa kinachomuumiza Raisi ni kutokana na uteuzi wake makini alioufanya unaohusisha watendaji wa kimataifa kama Proffesa Sospeter Muhongo na Proffesa Anna Tibaijuka ambao aliwaomba waje wamsaidie kwenye Ardhi na Nishati na kuonekana wanafaa" alisema mtoa habari wetu.
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, ndani ya kipindi kifupi Muhongo amefanikisha upatikanaji wa umeme kuanzia mjini hadi vijijini akiwa anaendeleza mambo ya msingi aliyoyafanya kijana mtafiti na anayeumiza kichwa kutwa kucha apewapo jukumu mh. Willium Mganga Ngeleja.
Mtoa habari huyo alisema kwamba, Rais hatakubali kupuuza bunge kama mhimili wa kusimamia serikali juu ya mapendekezo yao kuhusiana na suala la akaunti ya escrow.
Mkurugenzi wa mawasiliano ikulualipoulizwa na gazeti hili kama taarifa hiyo imefika ofisi ya Rais, alisema watanzania wawe watulivu kwani suala linahitaji umakini na endapo litakuwa tayari wananchi watajulishwa. "Rais hafanyi kazi kwa kumwekea 'deadline'," alisema.
Hata hivyo, aliomba vyombo vya habari visiwe sehemu ya upotoshaji kwani kufanya hivyo ni kuwachanganya wananchi.
Awali katibu mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliliambia gazeti moja la kila siku chini kuwa,hadi sasa ofisi yake haijapokea maazimio rasmi kutoka bungeni na kubainisha kuwa, ni muda gani utatumika kuyafanyia kazi ni vigumu kwake kusema ni lini.
"Nasema hivi, kwanza hatujayapokea, lakini nikiyaona Rais atayatafakar na kuyashughulikia, watu wasihisi kwamba ni leo,kesho au lini", alisema Balozi Ombeni. Alisema alivyosikia ni kwamba, wametoa ushauri, hivyo aliyeshauriwe ndiye atajua afanye nini na kwa wakati gani.
"Ushauri ni ushauri, lakini ushauri wa bunge lazima uchukuliwe kwa uzito unaostahili kwa uzito unaostahili, ndicho ninachoweza kusema, hauwezi kuchukuliwa slightly (kiwepesi), lazima utachukuliwa kwa uzito unaostahili, siwezi kukwambia kwamba, Rais ataamua vipi, ninachokwambia ni kwamba hawezi kuuchukulia slightly, ataupa uzito unaostahili," alisema.
Kuna watu wametajwa kuingiziwa fedha na Rugemalira James na taarifa zinazotoka uko juu ni kwamba watu hawa hawatachukuliwa hatua yoyote kwani kamati ilishindwa kuzingatia "the principle of natural justice", wangehojiwa ingekuwa vyema sana lakini kamati haikuwahoji kitu ambacho kinatoa utata katika kuyafanyia maamuzi maaazimio yanayowahusu watu hawa, na kwa hili tuwashangae kamati kwanini walishindwa kutaja majina ya waliochukua fedha stanbic bank, kamati inaonesha kuwadanganya watanzania na hili halitovumiliwa,..