RIP muasisi wa MOSAD Rafael 'Rafi' Eitan

huwa najaribu kujiuliza kama kuna uhusiana wa nchi ndogo kwa maana ya eneo na idadi ya watu na akili .Yaani nchi ndogo zinakua na watu wenye akili.
UK
Japan
Israel
Cuba
etc
Au inatokea tu kwa bahati nzuri?
 
Wana hatari sana hawa jamaa, sijui kwanini wako hivi.
Wamepewa uwezo huo na Mungu,kuna mahali kwenye Biblia Mungu amewabariki na kuwaambia kuwa wakimtii na kufuata maagizo yake atawapa uwezo askari 10 wa Israeli kuwashinda adui 100,askari 100 wa israel wataweza kuwashinda adui 1000,maneno hayo yaliendelea,andiko lipo.
 
Wana hatari sana hawa jamaa, sijui kwanini wako hivi.
Mungu wa Ibrahim,Isaka,na Yakobo pia akasema,yeyote atakaye mbariki mwanangu Israel nitambariki,na yeyote atakae mlaani nitamlaani.Na kwa maneno hayo ndio maana Marekani akajichukulia fursa ya kulilinda taifa teule la Mungu,Israel ili kujipatia Mibaraka,na wao Wamarekani wanaamini mafanikio yao yanatokana na baraka za kulilinda taifa Teule Israel.
 
Baraka kutoka kwa Mungu wao ,kwani Mungu wao huitwa Mungu wa Israel,kuwa watamiliki mali na utajiri na heshima
 
Lazima uwe brilliant maana bila kuwa brilliant huwezi kufika mbali kwenye jamii kama ile. Kuna kipindi waliwahi kumrekodi Richard Nixon akisema hawaamini sana Wayahudi na wanavuruga Marekani alisema "These Jews are natural born spies"
Na pia walifanikiwa kumrekodi Obama na Sarcozy,wakiwateta wayahudi hawa,ha ha ha ha
 
huwa najaribu kujiuliza kama kuna uhusiana wa nchi ndogo kwa maana ya eneo na idadi ya watu na akili .Yaani nchi ndogo zinakua na watu wenye akili.
UK
Japan
Israel
Cuba
etc
Au inatokea tu kwa bahati nzuri?
Nchi ndogo ni rahisi sana kuzitawala kwasababu ni rahisi mara nyingi huwa zinakuwa na idadi ndogo ya watu hivyo hupelekea mipango ya maendeleo kufanyika kwa ufanisi. Upande mwingine udogo wa nchi huwaunganusha watu kwa urahisi na kufanya sehemu za nje ya makao makuu kuonekana na kufikiwa kirahisi kwasababu miji na vijiji huwa inakuwa jirani sana.

Kama ni huduma za kijamii basi zitatolewa kwa urahisi sana, elimu bora, afya bora na mioundombinu inakuwa bora kwasababu ya udogo wa nchi.

NB: Hata suala zima la ulinzi wa ndani linakuwa ni rahisi sana kwasababu idadi ya watu na udogo inawabeba.
 
Baraka kutoka kwa Mungu wao ,kwani Mungu wao huitwa Mungu wa Israel,kuwa watamiliki mali na utajiri na heshima
Sasa kuna maswali ambayo mimi hapa nataka nieleweshwe kidogo. Kwani kuna jamii ambazo ni bora kuliko nyingine hapa duniani, au kuna jamii ambazo zimebarikiwa kuliko nyingine ???
 

Kuhusu kulaaniwa kwa kuwachukia Wayahudi, binafsi naomba niulize swali dogo la kihistoria. Hivi kwanini mataifa yaliyohusika na kuua Wayahudi wengi kama Ujerumani na Urusi ndiyo mataifa yenye mafanikio makubwa sana hapa duniani, kiuchumi na kijeshi ???

NB: Kwanini Ujarumani haijalaaniwa mpaka leo hii na wanazidi kufanikiwa tu ???
 
Lakini sasa kikosi kidogo cha wanamgambo wa Hezbollah kililisumbua sana jeshi lote la Israeli mwaka 2006-2007. Kwanini mkuu ???
 
Lakini sasa kikosi kidogo cha wanamgambo wa Hezbollah kililisumbua sana jeshi lote la Israeli mwaka 2006-2007. Kwanini mkuu ???
Hah ha haa ,watakua walikiuka maagizo ya Mwenyezi Mungu,hata enzi hizo kuna kipindi walikua wanachukua kisago ile mbaya,wantekwa na kuteswaa,wananyang'anywa ardhi.wakikaa wanajiuliza kwa nini tumepigwa wanagundua kuwa walikiuka maagizo ya Mungu,wanatubu,wakirudi tena wanawaangamiza madui zao.
 
Mkuu swali hili siwezi kulijibu kwani liko juu ya uwezo wangu,pengine walitubu dhambi zao hao GERMAN NA RUSSIA ndio maana Mungu akawasamehe
 
Sasa kuna maswali ambayo mimi hapa nataka nieleweshwe kidogo. Kwani kuna jamii ambazo ni bora kuliko nyingine hapa duniani, au kuna jamii ambazo zimebarikiwa kuliko nyingine ???
Mkuu naomba niseme kwa mara nyingine tena swali hili jingine pia ni kubwa sana kwangu,hata hivyo linahitaji kujipanga na maandalizi ya data na marejeo,hivyo basi nakuomba ulilete kama mada kamili inayojitegemea jukwaa hilihili.wapo akina zitto junior wanaweza kutusaidia kwani wanamaelezo kua mtu mweusi aliistaarabisha dunia kabla ya wazungu,wakati huo tunaona wazungu wako juu kwa kila kitu
 
We jamaa uko vizuri sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…