wapendwa,
hayo ya lecturer/assistant lecturer/tutorial assistant etc ni masuala yanayohusu schemes of service zilizoko vyuoni. tatizo lililokuwepo huko nyuma kidogo ni kuwa hizo schemes hazikuwa harmonized na kila chuo kiliachwa kujiandikia scheme kinayoona inakifaa kwa mazingira yake. ndo utakuta mtu ana masters lakini anapata promotion hadi lecturer au hata senior lecturer position na in some institutions kulikuwa na mpaka principal lecturer na hata chief lecturer!
kwa sasa kuna utaratibu wa harmonized scheme of service wa taasisi za elimu ya juu zilizoko chini ya NACTE na TCU respectivelly. ili kuwa recturer kwa sasa chini ya taratibu za NACTE kwa mfano, lazima uwe PhD holder regardless una uzoefu wa miaka miaka mingapi au umepublish kiasi gani. PhD ni basic qualification kuwa recturer na further promotion will be based on publications and experience!
kwa hiyo inawezekana kabisa marehemu mwalimu celestine alikwa lecturer kihalali kwa wakati huo na hadi mauti yanamkuta akawa alishashushwa chini kuwa assistant lecturer (kama hakuwahi kupata PhD) kwa mujibu wa scheme of service ya sasa!
pia imekuwa kama utamaduni kuwa mwalimu wa chuo kikuu anajulikana kama lecturer na ndio maana utakuta hata tutorial assistant anaitwa lecturer huko vyuoni. si wote wanaojua kuwa lecturer ni cheo anachokifikia (kwa promotion) mwalimu mwenye PhD na sio common status ya kila mwalimu wa chuo cha elimu ya juu. kwa hiyo kuwaita hata ma-tutorial assistant lecturers ni suala la mazoea/utamaduni tu na mi sioni ubaya wake kwa kweli na huenda kwa kufanya hivyo tunawa-inspire (indirectly) kusoma zaidi waweze kufikia hicho cheo.
nadhani sasa tuko pamoja kwa hilo.
kuhusu hoja ya kuondoka na wengi, si vibaya kuizungumza kama inafaa kwa kuwaonya wengine, muhimu lugha ya staha izingatiwe, isijekuwa tunamdhihaki marehemu.
RIP mwalimu celestine,
mbarikiwe wote na Bwana