kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,870
- 7,752
Wale watu wa umri mnakumbuka wote Jonas Savimbi. Alitumika na ubeberu kuchelewa ukombozi wa Angola kwa kufanya vita na wale waliyotaka ukombozi wa kweli wa nchi yao.
Alikuwa mpenda madaraka haijatokea. Wenzake wakipigania ukombozi wa nchi yao yeye alipigana hadi umauti kumkuta kwa ajili ya kutaka kuwa Rais wa Angola.
Alitumia itikadi ya ukabila na ueneo kuwagawa waangola na wakagawika kisawasawa. Alikuwa na wafuasi watiifu na wapiganaji waliyojitoa mhanga kwa ajili yake.
Kutokana na kibaraka wa ubeberu Savimbi likatokea janga kubwa Angola hadi walipofika askari wa Cuba kusaidia upande wa wakombozi wa taifa ndio ukombozi wa taifa ukafanikiwa.
Huyu Riek Machar inaonekana kufanana na Jonas Savimbi.Inaelekea Riek Machar ni mpenda urais wa kufa na kupona.
Tuwaombee Mungu hawa jamaa inaelekea hadi watakapoiparura nchi yao vipande vipande ndio akili itawarejea.
Mtu anakwenda Juba kuwa makamu wa rais lakini kila dalili zinaonyesha anakwenda Juba kufanya vita.